𝗡𝗜 𝗞𝗜𝗖𝗛𝗔𝗔 𝗟𝗔𝗞𝗜𝗡𝗜 𝗠𝗠𝗠𝗠𝗛
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 16
Baada ya kumaliza kupeana mahaba mazito Clara alipitiwa usingizi mzito ni wazi alikuwa amechoka. Masu akamfunika shuka vizuri kisha akaenda bafuni kuoga.
Alipomaliza alitoka na kurudi chumbani akachukua taulo na kuanza kujifuta maji mwilini kwake. Mara simu ya Clara ilianza kuita. Masu aliacha kujifuta akapiga hatua akaichukua na kuangalia mtu aliekuwa anapiga.
Aliguna baada ya kusoma jina lililo savewa KING OF MY HEART.
moja kwa moja alijua ni Ibra. Alisubiri simu iitwe mpaka ilipokata lazima na kuiweka pembeni.
Clara alikuja kuamka muda ulikuwa umeenda sana na Masu alikuwa pembeni yake .
” Vipi mpenzi umeamua?
Clara alijinyoosha.
” Mbona zaa zimewashwa kwani saizi saa ngapi?
” Ni usiku.
Clara valikinja sura huku akinyanyuka taratibu pale kitandani, aliangalia pembeni hakuona simu yake.
” Simu yangu iko wapi?
Masu alinyoosha mkono juu ya stoo akachukua simu na kumpatia.
” Mbona simu yangu imezima?
” Nadhani tulikuwa hazihitaji usumbufu ndio maana nikaamua kuizima.
” Umetuma bila ruhusa yangu?
” Mimi ndio mumeo hapa , sitaki mtu yoyote akusumbue ukiwa na mimi.
Clara hakumjibu akihangaika kuwasha simu yake.
” Clara kumbuka hiyo mimba iliyobeba mimi ndio muhusika Na sio yule mwanaume wako mjinga.
” Masu hili swala halihitaji hasira .
” Halihitaji hasira unamaana unataka nitilie tu nikiona unampa damu yangu yake mwanaume ambae hawezi kumpa mwanamke mimba.
” Kwani wewe una uhakika gani kama hii mimba ni yako?
Masu alimgeukia huku akiwa kakunja sura.
” Unataka kusema nini? Unataka kuniambia hiyo mimba niya yule Ibra?
“Masu naomba usinichanganye akili yangu ujio wako unanipa hofu nilishamwambia Ibra huu ni ujauzito wake.
Masu alicheka sana alafu akasema.
” Unampenda sana?
Clara alitulia kimnya.
” Nijibu Clara, kati yangu na Ibra nani ana nafasi kwenye moyo wako?
Bado Clara alinyamaza kimnya.
” Mimi najua , naelewa mimi ndio kipaombele chako, unanipenda sana ila kwa Ibra upo kimazoea tu.
Machozi yalimtoka Clara, Masu alisogea na kumfuta.
” Usilie mpenzi wangu hili ni swala la muda tu kila kitu kitakuwa sawa.
” Haitakuwa rahisi kiivyo namjua Ibra anaweza kukifanyia kitu kibaya.
” Namjua kuliko unavyofikiria na mbio zake zinaenda ukingoni . Sitamani Ibra aje amguse mtoto wangu akidhani ni wake .
Clara nataka kukuthibitishia kuwa Ibra hawezi kuzalisha, hawezi kumpa mwanamke mimba.
” Kwanini unasema hivyo kwa kujiamini , umejuaje?
” Namjua Ibra kuliko inavyofahamika wewe.
” Unaniacha njia panda Masu.
Masu alimsogelea akambusu kwenye paji la uso na kumkumbatia .
” Ni swala la muda kila kitu kitakaa sawa.
” Hivi ni kweli unanipenda?
” Nakupenda mno, nakupenda sana Clara na roho yangu inakiuka sana kuona na share penzi na mwanaume mwingine na sio mwanaume wa kawaida bali ni adui yangu.
Masu alizidi kumchanganya Clara.
” Adui yako kivipi?
Masu aliachia tabasamu.
Mtu anayecheza na mpenzi wangu ni adui yangu.
” Nataka kuondoka.
” Uende wapi muda huu?
” Nyumbani kwangu.
” Leo utalala hapa na mimi.
” Lakini…..
” Hakuna cha lakini . Clara unatakiwa kumsahau huyo Ibra na nafasi yake unipe mimi.
Ndio kwanza Masu alipanda kitandani na kumlaza Clara kifuani kwake na kumkumbatia.
SEHEMU YA 17 – 18
Clara hakuwa na jinsi alitulia na usingizi ulimpitia.
Kulipokucha asubuhi Clara aliamka na kujikuta yupo kitandani mwenyewe.
Alinyanyuka na kuingia bafuni akaanza kuoga , mara mlango ulifunguliwa na Masu akaingia bafuni na kumkumbatia kwa nyuma huku maji yakiwamwagikia mabegani mwao.
” Nakupenda Clara nataka uwe wangu pekee yangu.
” Mimi ni wako baba unanikosha , unaniweza kwako sina pingamizi kila kitu kwangu ni ndio.
Waliendelea kuoga huku wakipeana maneno matamu na vitendo.
Walipomaliza walirudi chumbani na kuvaa nguo zao kisha wakaenda kupata kifungua kinywa .
” Vipi baby nikupeleke kazini?
” Yule kichaa anaweza akawepo kazini ili kuepusha ugomvi bora niende mwenyewe.
” Basi sawa nitakukuchukulia usafiri.
Masu alichukua simu yake na kupiga sehemu baada ya dakika kadhaa gari ilifika.
Masu akimsindikiza mpaka getini. Kabla Clara hajatoka Masu alimshika kiuno na kumkumbatia huku alimmiminia mabusu.
” Uende salama mpenzi, na kama itatokea huyo Ibra akakusumbua basi nipigie simu mara moja.
” Sawa.
Masu alichukua pochi ya Clara kisha akaongoza mkono mfukoni na kutoa kiasi cha pesa na kuweka ndani ya pochi.
” Kwanini Masu?
” Kwasababu ni jukumu langu kufanya hivi.
Bado nina mengi ya kukulipa. Alimpatia Clara pachi yake kisha Clara akaondoka .
Alipanda kwenye gari na moja kwa moja alielekea kazini kwake.
Aliposhika tu kwenye gari aliona gari ya Ibra imesimama nje ya ofisi yao.
” Hapa moto lazima uwake.
Alisimama kidogo kisha akatoa simu yake na kuificha kwenye mauwa .
Baada ya hapo aliingia ofisini, alimkuta Ibra na Mishi wakiwa wamesimama.
Walipomuona Ibra alimfuata na kuuliza kwa ukali.
” Wewe ulikuwa wapi usiku kucha?
” Acha kunifokea ongea na mimi taratibu hujui nini kimenipata.
” Umepatwa na nini malaya wewe , umeamua kuona na simu.
” Sina simu jana nilivamiwa na vibaka ,sijui majambazi wakaishia kuchukua simu yangu.
” Majambazi alafu urudi hivyo? Huna michubuko wala ngeu.
” Hawakuwa na nia na mimi ila ni wewe Ibra ndio maana wamebaki na simu yangu .
Ibra alianza kupata wasiwasi.
“Hata hivyo wameniachia nije kukuba ujumbe kuwa ujiandae.
” Itakuwa ni Ilphan au Alphan.
Clara aliposikia jina la Ilphan alianza kupata pichabouwa hawa watu wawili wanafahamiana vizuri sana.
” Vipi upo salama , hawajakufanyia kitu kibaya?
” Hawajanifanyia kiti chochote kibaya.
” Okey. Kuwa makini hii ni hatari sana kwako.
Ibra alisema hivyo kisha akaondoka.
Mishi alikuwa haelewi na Clara bado alikuwa anatafakari kitu.
” Wewe Mishi ni kweli ulitekwa?
” Hapana nilikuwa kwa Masu.
” Wewe mbona una mambo ya hatari sana?
” Sina mambo ya hatari kama hawa watu wawili wenye siri nzito iliyojifika katikati yao.
” Watu gani?
” Ibra pamoja na huyu Ilphan.
” Ilphan ndio nani?
” Masu , jina lake halisi ni Ilphan.
Mishi alimuangalia kisha akasema.
” Kwahiyo Masu ndio kakwambia uje useme ulitekwa?
” Hapana nimejikuta nimeongea na nimeanza kupata mwanga.
Mishi siwezi kutulia mpaka nizmtakapijua ukweli.
Clara alienda kuomba ruhusa kisha akatoka pale ofisini na kwenda kuchukua simu yake. Aliwasha na kumpigia Masu.
” Vipi mpenzi mambo yanaenda je huko?
” Vibaya.
” Akifanya nini huyo mwana haramu?
” Masu nataka tuonane muda huu.
” Unataka tuonane wapi?
” Popote hata hotelini.
” Tukutane white house hotel.
” Sawa.
Clara alichukua usafiri na kuelekea hotelini.
Baada ya dakika kama 20 alifika na kumkuta Masu akiwa kafika.
Walienda kuchukua chumba na kwenda kuongelea huko bila mtu yoyote kuwaona wala kusikia maongezi yao.
” Niambie mpenzi.
” Nilimdanganya Ibra kuwa nilivamiwa na majambazi wakanipiga simu.
Alikuwa na wasiwasi sana pia alitaja majina mawili jina lako Ilphan na Alphan.
Masu aliachia tabasamu dogo.
” Masu nataka kujua nini kinaendelea kati yako na Ibra.
SEHEMU YA 19 – 20
” Kwakuwa una wasiwasi mwingi nitakwambia ila unatakiwa kutulia na unihakikishie hautamwambia mtu mpaka mpango wangu ukamilike.
” Mpango gani?
” Hivi unajua Ibra ni mafia .
Clara alimtolea macho .
” Unaishi na muuwaji ambae hana uwoga anaweza kukatisha maisha ya mtu yoyote kisa mali na pesa.
Ilphan na Alphan ni mapacha . Ni kaka yangu ambae tumefana sana na tulikuwa tunashirikiana.
Alpha alichagua kusimamia kampuni za mzee na mimi niliamua kuunda kusomea kazi ya upelelezi.
Nikimaliza masoma yangu nikapata ajira lakini ilikuwa nje ya nchi.
Baada ya mwaka nilipokuwa simu na mzee akaniambia mwenendo wa Alpha hauewi ameanza kujiingiza kwenye makundi na kufanya biashara haramu.
Nilimpigia simu rafiki yangu mmoja ambae tunafanya kazi pamoja nikamuomba achunguze mwenendo wa Alpha.
Mussa alianza kumfuatilia Alpha akagundua ni kweli wananya biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Nilimpigia simu alpha nikaongea nae sana kuhusu tabia yake lakini aliishia kunijibu.
” Ilphan Kil mtu ana njia zake za kufikia malengo kwenye haya maisha naomba uniache na haya maisha yangu na wewe fanya yako.
Niliamua kufunga safari nikarudi. Nilikaa na mzee tukaongea sana. Nilikuahidi mzee kusimamia hilo.
Nilianza kumfuatilia Alphan. Alikuwa na wenzake wanne ambae ni Ibrahim na wenzao wawili.
Siku moja katika harakati zao walianza kuzungukana. Ibrahim na wenzie walimgeuka Alphan na kutaka kuchukua mgao wake ambayo ilikuwa ni pesa nyingi sana.
Wakati Alphan anatoka kwenye lile jengo alipigwa risasi bahati ilimpitia mkononi.
Ibra na wenzie walishuka na kumpiga sana mpaka akapoteza fahamu.
Tulipata taarifa hali ya Alphan alikuwa na hali mbaya sana.
Tukimiwahisha hospitali akadnza matibabu . Lakini bado Ibra na wenzie waliendelea kumfuatilia ndipo mzee akaamua kumuhamisha nchi za nje.
Baada ya siku mbili tukasikia mtu mwingine kwenye kundi lao amefariki kwa kupigwa risasi.
Kwa uchunguzi ikaonekana Ibra ndio uhusika wa hayo mauwaji.
Japokuwa nae alijeruhiwa sana sehemu za tumbo kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
Baada ya kufanyiwa matibabu ilionekana kwa asilimia 98 hana uwezo walimpa mwanamke mimba .
Kuna siku nilikuwa nafuatilia wakaingia kwenye nyumba moja na mimi nilitaka ukuta na kutaka kuingia ndani hapo ndipo waliniotea na kunipiga na kitu kizito kichwani . Walimpiga sana wakiahidi wamenimaliza.
Lakini kwa uwezo wa Mungu nilipona .
Niliamua kubadilisha muonekano wangu
na kuanza kufuatilia ili nipate ushahidi wa kumfunga.
Hapo ndipo nilipogundua uhusiano wenu .
Nilichofanya kichaa na kugundua mambo mengi sana ambayo anafanya na nimefanikiwa kuniharibia mipango yake mingi sana bila yeye kujua.
Pia niliona jinsi ilivyokuwa unateseka na mapenzi nikajikuta nakuomba huruma lakini mambo yakageuka tukajikuta zimezama kwenye mapenzi.
” Clara Ibra sio mtu sahihi kwako.
“Kwahiyo siku ile nilipokuta damu pia ulikuwa kwenye mapambano?
” Mapambano yake hayahusiani na Ibra ila ni moja kati ya kazi zangu.
Clara alichoshwa na maneno ya Masu.
” Sasa nitafanyaje, nimeanza kumuogopa. Kama akijua hii mimba sio yake si ataniuwa mimi.
” Anaweza kufanya hivyo lakini sitampa nafasi kwakuwa umeshajua na ushahidi wote tunao bado ibra atakanatwa na kwenda kujibu mashtaka.
Baada ya maongezi marefu sana na yaliyompa hofu Clara waliamua kuondoka . Clara alirudi nyumbani akiwa muoga na mwenye hofu aliogopa hata kumsogelea Ibra na wakati huo Ibra hakuwa sawa ni kama kuna vitu vilichanganya akili yake.
Baada ya siku mbili kupita majira ya saa moja Ibra na Clara wakiwa wamekaa sebleni . Mlango uligongwa . Clara alinyanyuka kutaka kwenda kufungua.
” Unatarajia kupata mgeni muda huu?
” Hapana.
” Subiri niende mimi.
Ibra alinyanyuka na kwenda kufungua mlango. Ile anafungua tu akakutana na sura ya Ilphan .
Ibra alishituka na kurudi nyuma.
” Hatimae nimekutana tena mr. Ibrahim.
Ibra alitaka kukimbia Ilphan aksmnyooshe bastola.
” Kukimbia nafyatua risasi. Tii sheria bila shuruti. Ibra alisimama na polisi walimvamia na kumfunga pingu.
Clara alisimama na kumsogelea.
” Usiogope Clara nitarudi , nitarudi mke wangu nitadhuhudia mtoto wetu akija duniani.
” Hapana Ibra, huyu sio mtoto wako. Ibra alimuangalia huku akiwa kakunja uso.
” Unasemaje?
” Hiyo ni mimba yangu Ibra. Alisema Masu huku alisogea karibu na Clara na kukipapasa tumbo lake. Ibra alitamani kuwavamia lakini ndio alikuwa na pingu mkononi kwake.
” Ni kweli hii mimba niya Masu kichaa yeye ndio alikuwa faraja yangu.
” Huna kinyaa wala aibu wewe mwanamke nasema nilitoka huku nakuuuwa.
” Hizo ni ndoto. Askari prlekeni huko huyo mtuhumiwa.
Ibra alichukuliwa na kupelekwa kituoni.
Alitafuta wanasheria kwaajili ya kusimamia kesi yake na mwisho wa siku alipandishwa mahakamani na ushahidi wote. Ibra hakuwa na la kujitetea alihukumiwa kifungo cha miaka kumi.
Clara na Masu waliishi maisha yao kwa uhuru. Ilphan alimtambulisha kwa wazazi ndugu na jamaa .
Kwakuwa Clara alikuwa yatima wazazi wa Ilphan alimchukua kama binti yao wa kumzaa.
Baada ya miezi kusogea Clara alijifungua mtoto wa kike mwenye afya nzuri.
Ilikuwa ni familia yenye mapenzi makubwa na furaha. Ilphan alimchukua Clara na mtoto wake wakaenda kuishi nje ya nchi ambako alikuwa anafanyia kazi mwanzo.
MWISHO

