π‘π ππππππ πππππ‘π π π π π π
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 11
Clara alimuangalia Mishi kisha akaachia tabasamu.
” Niambie basi.
” Mishi sikufichi Masu ni kichaa lakini mmmh….
” Mmmmh nini sasa?
” Shuhuri yake sio ya kitoto. Anayajua mapenzi, anayeweza utafikiri yeye ndio mkufunzi wa mahaba.
” ππππ Mishi alijikuta anacheka sana na kuona kama rafiki yake kuchanganyikiwa.
” Clara wewe ni kichaa eeee…
” Wewe niite hivyo wala sipingi sababu kile alichonipa Masu mimi ni kichaa mazina .
” Wewe Clara wewe , yani huoni hata aibu.
” Aibu ya nini shoga yangu wakati mwenzio nilikuwa kupata raha.
” Makubwa haya.
” Ndio hivyo , lakini siri yako kipenzi usije ukanianika .
” Mmmh mimi na wewe tena , haitakaa itokee. Siri yako ni yangu kipenzi.
Wiki mbili zilipita tangu Clara na Mishi waanze kumtafuta na kumuulizia Masu. Walienda kila kona waliyoamini Masu angeweza kuwa , mitaa na kuulizia kwa watu wachache waliokuwa wakimfahamu , Lakini kila walipouliza, walipata jibu moja.
βHuyo mtu tuna muda hatujamuona.
Clara alianza kupoteza matumaini ya kumuona Masu .
” Mishi hii ni ya mwisho sasa siwezi tena kumuona Masu.
” Isikatwe tamaa labda atakuwa kapatwa Chimbo jipya acha tuendelee kumtafuta kwenye majalala.
” Siamini kama tutampata hata hivyo nachoka sana .
” Basi twende tukapumzike. Hata hivyo Ibra yupo .
” Hawezi kumfikia Masu.
Siku zilizidi kwenda na Mwili wa clara ulianza kuwa dhaifu, akawa anachoka bila hata ya kufanya kazi ngumu na mara nyingi alihisi kichefuchefu bila sababu.
Lakini mara kadhaa alijipa moyo kwa kusema.
βLabda ni msongo wa mawazo tu.
Lakini dadri siku zilivyozudi kwenda hali ilizidi kuwa mbaya mara anashindwa kula, kuna siku akiwa kazini alianguka akapoteza fahamu .
Ilikuwa ni hela heka watu walimpa huduma ya kwanza akapata fahamu .
” Clara inabidi twende hospitali. Alisema Mishi.
” Sipendi , nipo sawa.
” Acha ujinga, unajua ilipoteza fahamu muda mfupi uliopita.
” Ni uchovu tu.
” Uchovu gani mpaka uzimie? Au bado unakuwa za hiyo kichaa Masu?
” Hebu achana na hayo mambo , nenda kaendelee na kazi zako.
” Alafu niliendekea na kazi na wewe inakuwaje?
” Nimemwambia nipo sawa.
Clara alifika kabisa kupelekwa hospital ikabidi Mishi amuachie na kwenda kuendelea na kazi zake.
Siku moja Ibra alienda nyumbani kwa Clara , alipomkuta Clara akijiegemeza kwenye ukuta akiwa anazunguka kichwa, alishtuka sana.
βClara! Wewe una nini? Kwani siku hizi unashifmda gani wewe?
Clara alimuangalia kisha akasema.
“Nipo sawa sina tatizo lolote.
” Angalia mwili wako unazidi kudhoofika.
Clara hakujibu, alibaki akimwangalia tu .
βKesho lazima tuende hospitali, sitaki ubishi. Ibra aliongeza kwa msisitizo.
Ibra alimshika mkono wakaenda ndani , anamuweka kwenye kiti .
” Utakula nini?
” Sijisiki kula chochote.
” Utaishi vipi bila kula?
Ibra hakutaka kubishana nae alienda jikoni kuandaa supu ya kuku wa kienyeji.
Kesho yake mapema sana waliamka na Ibra akijiandaa kisha wakaenda hospitali. Waliona na daktari kisha wakaandikiwa vipimo.
Walienda maabara kupima , alichukuliwa vingi vingi ikiwelo kipimo cha damu, mkojo, na ultrasound. Baada ya muda, daktari alirudi akiwa na tabasamu.
βHongera mama, una ujauzito wa karibu wiki sita.
Clara alimuangalia uso wa daktari moja kwa moja. yale maneno hayakumuingia vizuri kichwani mwake.
Ibra, aliyekuwa pembeni, alicheka kwa furaha.
βHatimaye Mungu ametusikia! Clara hatimaye tutakuwa wazazi.
Alimkumbatia kwa nguvu, lakini Clara alibaki kimya. Moyo wake haukuwa na furaha ulikuwa mzito wenye woga, na mashaka.
Waliondoka pale hospitali Ibra akiwa na furaha mno lakini Clara hakuwa sawa kichwani kwake ila alikuwa akimlazimisha tabasamu
Kesho Clara alikutana na Mishi kwenye mgahawa . Alikaa kimya kwa muda kabla ya kusema,
βMishiβ¦ nina ujauzito.
Mishi alishangilia kwa furaha.
βAh! Hongera rafiki yangu! Hii ni baraka uliyoisubiri kwa muda mrefu. Angalia sasa Mungu amekukumbuka . Hongera sana kipenzi nimefurahi sana.
Wakati Mishi anafurahia huku maneno yakimtoka Clara alikuwa anamuangalia .
Na taratibu machozi yalitiririka usoni mwake.
Mishi alishtuka.
βClara mbona unalia sasa? Hii sio habari njema kwako?
Clara alitikisa kichwa kisha akaongea kwa sauti ya kutetemeka,
βMish, hii mimba sio ya Ibra.
Mishi alinyamaza na kumuangalia kwa mshangao
βUnamaanisha nini?
Clara alifuta machozi, akavuta pumzi ndefu na kusema kwa sauti ya chini .
βKwa asilimia mia moja, mimba hii ni ya Masu.
Mishi alishika mdomo wake kwa mshangao.
βMasu? Yule kichaa imembeba na mimba ?
Clara alitikisa kichwa kama ishara ya kukubali. alishusha pumzi ndefu.
βNdiyo, Nilihisi tangu mwanzo, na sasa nina uhakika.
Kimya kizito kilitanda.
Mishi alishindwa kuongea. Alimuangalia rafiki yake, mwanamke aliyekuwa ameangukia kwenye upendo wa mtu ambae hakuna atakaemuelewa lakini wake ulikuwa kweli kabisa.
Clara aliweka kiganja chake tumboni kwake , alimuandalia Mishi usonijinsi na wote wakatazamana
βMishi, sijui yuko wapi, sijui kama yuko hai au vipi , lakini ukweli ni kwamba sehemu yake ipo ndani yangu.
” Kwahiyo hiyo hiyo mimba utampa Ibra na mtoto alizaliwa atatambua Ibra ndio baba yake mzazi?
SEHEMU YA 12
Swali la Clara lilizua ukimya wa muda .
” Itabidi Ibra aendelee kujua kuwa huyu ni ujauzito wake.
βClara, usijidanganye unafikiri utaweza kuishi na siri kama hii?
Clara alipumua kwa nguvu huku machozi yakimtiririka
βSijui, Mishi. Najua nikimwambia Ibra ukweli atanichukia, ataniona mwasherati, na ataniacha nihangaike na hili tumbo.
βLakini kumdanganya haitasaidia. Mishi aliongea kwa sauti ya upole.
” unataka nimwambie ukweli ?
” Sijui , sijui atalipikeaje. Mishi naomba unifichie siri yangu mpaka nitakapokuwa sawa.
” Kuficha siri sio shida cha kuomba mtoto asije kukuumbua maana anaweza kuja na sura kama ya Masu au mambo ya utamaduni yanaleta shida.
” Siamini mambo hayo na Mungu aepushie mbali.
Clara aliweka kiganja tumboni, akafumba macho.
βMasu sijui yuko wapi. Lakini kila nikikaa napata hisia kuwa yupo na ipo siku tutaonana , atakuja kuonana na mtoto wake.
” Acha kujipa moyo kwa mambo ambayo hayana maana cha kushukuru ni kwamba Masu kakutoa kimasomaso , kakuachia zawadi ya mimba . Maisha yako na Ibra yanaenda vizuri mtaenda kufunga ndoa.
Wakiwa bado wanaendelea kuongea mara simu ya Clara ikaita. Clara alitoa kwenye pochi na kuangalia.
” Ibra anapiga.
” Pokea.
Clara alipokea ile simu.
” Uko wapi?
” Nipo sehemu na Mishi.
” Clara unajua hali yako hairuhusu wewe kuzurula unatakiwa kupumzika.
” Narudi sasa hivi.
” Niambie uko wapi nije kukuchukua.
” Nipo millenium restaurant.
Nitakuwa hapo baada ya muda mchache.
Baada ya maongezi alikata simu.
” Ibra anakuja kunichukua.
” Anaonyesha mapenzi ya hali ya juu.
Clara hakujibu .
Baada ya dakika kadhaa Ibra alikuwa fika na kumchukua wakarudi nyumbani.
Ibra alikuwa alimuhudumia na kumjali kwa kila kitu huku akiwa na furaha , matarajio ya kuwa baba.
Siku zilienda na Clara alianza kusahau kuhusu Masu na kuishi maisha ya raha na kudekezwa bila bughdha lakini aliishi na siri nzito sana moyoni mwake.
Baada ya miezi miwili kupita .
Siku moja majira ya saa moja jioni Clara alikuwa amesimama kwenye kituo cha daladala akisubiri usafiri. Siku hiyo usafiri ulikuwa wa shida sana kila daladala na bajaji zilizokuwa zinapita zilikuwa zimejaa.
Alitembea kwa mwendo mdogo mdogo akiwekea kituo cha pili .
Alipofika kituo cha pili alikutana na dada mmoja ambae walikuwa hawafahamiani.
” Leo usafiri wa shida sana.
” Nahisi tunalala hapa leo.
” Usiwaze tutatoka hapo.
Alisema yule dada.
” Kwani mwenzangu unaelekea wapi?
” Magogoni.
” Magogoni pale pale au kwa mbele?
” Pale pale.
” Kumbe tunaenda njia moja mimi naishia kwa sande kituo cha nyuma kabla haujafika Magogoni.
Clara aliendelea kusimama huku yule msichana akiwa anatembea na kurudi akipunga mkono kusimamisha magari.
Waliendelea kusimama kwa muda bila mafanikio.
Baada ya muda kidogo ikipita gari nyeusi ya kifahari na kwenda kusimama mbele kidogo. Ile gari ilisimama kwa muda kisha ilirudi nyuma na kusimama walipokuwa wamesimama wakina Clara.
Kioo cha dirisha la gari kilifunguliwa akaonekana kaka mmoja mtanashati.
” Habari .
” Salama kaka. Aliitikia yule msichana kwa sauti ya kuchangamka.
” Kaka tunaomba lift tusigeze mpaka hapo mbele.
” Sawa pandeni.
Yule msichana alitaka kufungua mlango wa gari lakini alipogeuka nyuma kuangalia akamkuta Clara bado kasimama.
” Dada twende.
Clara alikuwa na wasiwasi.
” Twende bwana utakaa sana hapo .
Clara alikubali kupanda kwenye gari lakini alikuwa na hofu sana kupanda kwenye usafiri wa mtu ambae hamfahamu.
Yule msichana hakuwa na wasiwasi ndio kwanza akafungua mlango wa mbele akapanda na Clara alipanda nyuma na safari ikaanza.
SEHEMU YA 13
Safari iliendelea kukawa na ukimya kwa muda, kila mtu akiwa kimya kwamba kila mmoja alikuwa na mawazo yake.
Ghafla yule msichana aliyeomba lift alianza mazungumzo na yule dereva.
βAfadhali umesimama, leo kweli usafiri ni mateso.aliongea huku akicheka.
βNi kweli, lakini usiku huu wanawake mnapaswa kuwa waangalifu, haipendezi kuwa barabarani tena kwenye makundi maana vibaya huwa hawakosekani .
” Ni kweli kabisa ndio maana mimi nilikuwa napambania niondoke pale.
Clara alikuwa kunyamaza kimnya huku Macho yake yalikuwa yakiangaoia nje barabara kupitia kioo cha dirisha.
lakini ndani ya moyo wake kulikuwa na hofu ya usalama wake.
Baada ya muda mfupi gari likaingia barabara kwenye barabara ya vumbi.
βExcuse me kaka,β Clara alisema na yule kaka akageuka kumuangalia.
” Vipi dada Kuna tatizo? Yule mwanaume aliuliza kwa sauti yake nzito.
βmbona unaingia njia hii? Hii siyo njia ya Magogoni.
Yule dereva alitabasamu kisha akasema.
βNajua, ninajaribu kupitia njia ya mkato.
Clara moyo ulichungulia dirishani akiangalia nje barabara ilikuwa kimya, miti mirefu iliyokuwa pande zote za barabara.
” Hii njia sikfahamu. Alisema Clara na
Yule msichana aliyekuwa amekaa mbele alianza kuonyesha wasiwasi.
βKaka, turudishe barabara kuu tafadhali, mimi naogopa njia hii ina giza sana na wala sijawahi kupita.
βMsijali mpo sehemu salama. Haitachukua muda tutafika huko muendako.
” Usije ukatuwahisha ahera . Alisema yule msichana na yule mwanaume akacheka.
Dakika chache baadaye, gari liingia tena kwenye barabara juu na kuelekea Magogoni .
Walipofika kwenye kituo anachoshika yule dada gari ilisimama nae akashuka.
” Asante sana kaka ubarikiwe mno.
” Sawa.
” Kaka hata mimi mashuka hapa. Alisema Clara.
” Magogoni ni hapo mbele.
” Lakini sio mbali acha kishuke na wewe uwahi kenda kupumzika bila shaka familia yako itakuwa ina kusubiri.
” Usijali , usalama wako kwanza.
Aliwasha gari na safari ya kuelekea magogoni iliendelea.
Walifika mbele ya nyumba ya Clara na gari ikafunga breki .
Clara alishika tumbo lake kwa hofu.
βTatizo nini kaka?β
Mwanaume akageuka polepole namacho yake makali lilikutana na macho ya Clara.
” Vipi Clara unaendeleaje?
Clara alishituka.
” Wewe unanifahamu ?
” Kwa i wewe hunifahamu?
Clara alimuangalia kwa sekunde chache akijaribu kuvuta hisia lakini bado.
” Tafadhali nataka kuondoka.
” Muangalie vizuri bila uwoga. Aliongea kwa sauti ya upole ila ilikuwa mzito yenye haina ya kiume
Moyo wa Clara ulianza kuruka.
” tafadhali niruhusi niondoke mimi sikufahamu alafu mimi ni mjamzito hapa nilipo usije ukadhurumu maisha ya huyu kiumbe asiyekuwa na hatia acha azaliwe kwa amani.
” Najua una mtoto tumboni kwako. Na huyo mtoto ni muhimu sana kwako na kwangu pia sababu mimi ndio baba . Baba niliempandikiza kwenye lile jumba bovu .
Clara alishituka na kumtolea macho, alimuangalia kwa makini huku akimmulika kwa tochi ya simu yake
βMasu? aliita kwa sauti ya juu na mikono yake ikianza kutetemeka.
Yule mwanaume alitabasamu kisha akasema
βHatimaye umenikumbuka.
Clara hakuamini macho yake.
βMasu… wewe ni … yule …. Nilidhani umepatwa na tatizo kubwa na hata kupoteza maisha yako
βNilihitaji kupotea , Lakini nilijua ipo siku nitakuona tena.
Clara alianza kulia, hakuwa na nguvu za kuendelea kuongea
Masu alitamani kumbembeleza lakini hakuweza hata kumkumbatia, alimshika mkono .
” Usilie , sasa nitakuwa karibu na wewe.
” Kwani ulikuwa wapi?
” Clara najua una maswali mengi ambayo unahitaji majibu yake .
” Ndio nina mengi ya kuongea na wewe Masu.
” Lakini sio sasa. Nenda kapumzike mimi nitakutafutia wakati mwingine.
Masu alimbusu kwenye paji la uso kisha akamruhusu ashuke kwenye gari kisha akawasha gari na kuondoka.
Clara alibaki amesimama hakuamini kwa asilimia zote kama kweli yule mwanaume mtanashati , mwenye kunukia marashi ya bei ghari , mwenye kuendesha gari ya kifahari ndio yule mwanaume kichaa ambae alikuwa akikutana nae kwenye jumba bovu.
” Hapana , au nipo usingizini Naota? Kuna kitu gani kinaendelea , alikuwa anafunga nini kwa kujifanya kichaa? Hayo maswali yote
Alijiuliza Clara huku akiangalia upande gari ya Masu iliopelekea mara akashituka baada ya kuguswa begani .
” Uuuuh Ibra itakuja ouniuwa kwanini unanishitua hivyo mwenzio na unalijua hali yangu?
” Umesimama muda inaangalia nini?
” Nimejisikia tu kusimama hapa.
” Kwahiyo unajisikia raha kuwa hapa?
” Nimechoka nataka kupumzika.
Clara alipiga hatua mpaka getini akatoa funguo na kufungua kisha wakaingia ndani.
” Unapenda nikuandalie chakula gani mpenzi?
” Sijisiki kula chochote naenda kuoga alafu nataka kupumzika.
Clara alienda chumbani kwake , akaenda bafuni kuoga lakini akili yake ilikuwa kwa Masu , alikumbuka kila kitu kilichokuwa kikitokea kati yao.
” Nilihisi huyu kichaa hakuwa kichaa wa kawaida. Na amejua je kama nina mimba yake?
Akiwa katikati ya mawazo mara mlango ulifunguliwa na Ibra akaingia akiwa na bakuli la matunda.
” Huwezi kulala tumbo likiwa tupu mpenzi wangu kula kwaajili ya afya yako na mtoto wetu alie tumboni .
Clara alimuangalia Ibra jinsi alivyokuwa akikitumia na kukuthamini ule ujauzito ,akajikuta anajiuliza.
” Kwa hekaheka zote hizi , vipi siku akijua kuwa hii mimba sio yake niya Masu ?
SEHEMU YA 14
Clara alijikuta anazubaa na kumshangaa Ibra usoni.
” Clara mbona unaniangalia hivyo? Swali la Ibra ilimfanya Clara arudi kwenye hali ya kawaida.
“Ahh, hapana , kuna kitu nilikuwa nawaza. Alijibu Clara kisha akatoa tabasamu.
” Unawaza nini tena mpenzi wangu?
” Nina wazo ya kawaida tu.
” Pasi punguza sipendi kukuona unawaza nipo hapa kwaajili yako.
Ibra alichukua kipande cha tikiti na kumpatia.
” Kula mama alafu upumzike. Mimi nakupenda sana wewe nataka mtoto wetu azaliwe akiwa salama.
” Ibra….
” Naam…
” Kwahiyo maneno yote na huu upendo iliyoongezeka ni kwasababu ya hii mimba?
” Clara bwana sasa unaniuliza maswali gani hayo?
Clara hakutaka waendelee kuongea maana wangekutana mpaka kukuche. Alijitahidi akala matunda baada ya hapo alipanda kitandani akalala.
Lakini usiku ule ulikuwa mgumu sana kwake alijikuta kumbukumbu zote za matukio waliyofanya na Masu zinajirudia kichwani mwake kuanzia matukio waliyokuwa wanafanya kwenye lile jumba bovu mpaka usiku ule walipoona na tena.
” Aaaah , kwanini Masu, kwanini ulioitwa na umerudi tena wakati mambo yangu na Ibra yameanza kuwa mazuri?
Baada ya kuwaza sana usingizi ulimpitia . Lakini hata kwenye Njozi zake aliota na kuweweseka huku akitaja jina la Masu.alilitaja kwa sauti mpaka Ibra aliekuwa Kalala pembeni yake akasikia .
Ibra aliamka na kukaa, aliwasha taa na kumuangalia jinsi anavyoweweseka mpaka jasho linamtoka.
“Masu? Hili sio kuna hebu masikioni kwangu . Huyu Masu ni nani?
Ibra alijiuliza huku akijaribu kukumbuka badae akawa anakumbuka.
” kichaa. Kwanini anamuota hivi?
Ibra alijaribu kumuamsha lakini Clara alionekana kuwa na usingizi mzito , alifumbua macho kidogo kisha akageuka upande wa pili na kuendelea kulala.
Kulipokucha asubuhi wakati wanajiandaa kwaajili ya kwenda kazini Ibra akauliza.
” Ulikuwa unatoa ndoto gani kuhusu Masu?
Clara aliposikia jina la Masu alishituka.
” Unasema ?
” Ulikuwa unaweweseka na kuita jina la Masu mara kadhaa.
Clara alipata jibu la haraka.
” Nilikuwa naota ndoto mbaya , mbaya sana.
” Umeotaje?
” Yule kichaa Masu alikuwa ananikimbiza huku akiwa kashika fimbo kuombwa mkononi.
” Pole , lakini nilikwambia kaa mbali na vichaa.
” Lakini ni ndoto tu.
” Ohoooo, unatakiwa kuwa makini na vichaa kumbuka hawana akili ikitokea kaliuwa ndio basi tena hana kesi yule na ukumbuke utaniavlcha kwenye wakati mgumu sana ….
” Mmmm Ibra inatosha bwana , maliza kuvaa tuondoke.
Wakiwa kwenye gari wakielekea kazini mara simu ya Clara iliita ,alipoangalia aliona namba mpya . Alikuwa na wasiwasi kidogo kupokea.
” Mbona hupokei simu? Ibra alimuuliza huku akiendesha gari na macho yake yakiangalia mbele .
Clara aliamua kupokea ile simu na sauti nzito ya kiume ilisikika.
” Habari mama kijacho wangu.
Clara alishituka kwani alikuwa kashagundua aliyepiga simu alikuwa ni Masu.
” Salama.
” Vipi umeamkaje wewe pamoja na mtoto huko tumboni?
” Sasa mimi kipo njiani nakuja hapo kazini nikifika hapo zitaelekezwa vizuri. Alijibu Clara kisha akakata simu. Ibra hakuwa amepewa chochote alijua ni mambo ya kazi.
Ilipofika majira ya saa sita na nusu Clara alikuwa akijiandaa kutoka kwaajili ya kwenda kula mara mlango wa ofisini kwake ulifunguliwa.
” Clara kuna mgeni wako.
” Mgeni gani?
” Kaka mmoja hivi.
Clara alishituka , moja kwa moja alijua ni Masu kumfuata kazini.
” Yuko wapi?
” Yupo hapo nje.
Clara alinyanyuka haraka huku akiwa na shauku ya kutaka kumuona.
Alipotoka nje akakutana na sura tofauti ambayo hajawahi kukutana nayo.
” Habari madam Clara.
” Salama.
” Nina mizigo yako hapa.
” Imetoka wapi?
” Utakutana na maelezo ndani .
Yule kijana alimkabidhi uwa kubwa pamoja na mfuko.
“Kwaheri madam.
” Asante.
Clara aliingia ndani ofisini kwake na kuweka vile vitu mezani , kabla hata akafungua Mishi alifika.
” Nimeona kwa mbali nikasema hata mambo haya hayawezi kunipiga ngoja nije kushuhudia kwa karibu.
Alichukua uwa na kulinisa.
” Mmmmm linanukia vizuri. Naona sasa mahaba yanazidi kuchanua.
” Sio huyo unaemzungumzia.
” Unamaana kuwa sio Ibra ambae Karuma hivi?
” Ndio.
” Umepata mdhamini mwingine ?
“Mishi , Masu amerudi tena amerudi kivingine kabisa. Sio kichaa wa kuvaa nguo zote mwilini ni mwanaume mtanashati tena mwenye kutembelea gari za bei ghari. Akili yaje imetulia .
” Unasemaje? Aliuliza Mishi huku alichukua ile kadi iliyokuwa mkononi kwa Clara na kusoma maneno mazuri ya kimahaba na mwisho kulikuwa na kina la masumbuko . Aka Masu kama walivyozoea kumuita.
” Clara hii inawezekana vipi?
” Sijui nikwambiaje ila jana kama zali nikakutana nae . Unajua mpaka sasa akili yangu haijakaa sawa . Nahisi nitakuwa sawa baada ya mimi kuonana nae tutaongea kuhusu kila kitu kinachoendelea.
SEHEMU YA 15
Ndani ya siku mbili Masu alikuwa akimpigia simu na kumjulia hali. Clara ombi lake lilikuwa ni kuonana nae tu .
” Masu shauku yangu kubwa ni kuonana na wewe.
” Najua ila tulia kwanza bado hali si shwari ila naahidi hivi karibuni nitakutana na wewe.
Clara alishika na jibu la Masu alitulia na kusubiri hiyo siku ambayo watakutana .
Baada ya siku kadhaa mbele Masu alifika karibu na ofisi anayofanya kazi Clara, alisimamisha gari yake pembeni huku wakiendelea kuwasiliana.
Baada ya dakika kadhaa Clara alitoka na kwenda moja kwa moja kwenye gari, alifungua mlango na kupanda.
” Mambo.
” Safi. Aliitikia masu huku akitabasamu . Alivua miwani yake ya jua na kuiweka pembeni kisha akaanza kuendesha gari.
Muda wote aliokuwa akiendesha gari Clara alikuwa akimuangalia sana .
” Masu….
Aliita na Masu akageuka kumuangalia.
” Niambie mrembo wangu.
Clara alihisi damu kukimbia kwenye mwili wake.
” Hivi kweli ni wewe?
” Huamini kama ni mimi?
” Kuna muda naamini lakini kuna muda naona kama unaniigizia tu.
” Nitakufanyia uamini kipenzi.
Walifika kwenye jumba moja la kifahari , geti likifunguliwa wakaingia ndani. Masu alienda kuegesha gari kwenye sehemu maalum ya maegesho kisha akashuka na kwenda kumfungulia mlango Clara.
” Karibu. Kuwa na amani.
Clara alimuangalia usoni , Masu alimshika mkono na kuingia kwenye ile nyumba nzuri ambayo ilikuwa umepambwa kwa vitu vya thamani na kuifanya ivutie sana.
Walienda kukaa kwenye makocha ya thamani huku Clara akitangaza macho kila kona ya ile nyumba.
” Utatumia kinywaji gani? Masu aliuliza.
” Chochote kisichokuwa na kilevi.
Masu alienda kuchukua vikao la juice na grass kisha akaenda na kumimina .
” Karibu.
” Asante. Clara alipokea na kuweka kwenye studio ya kioo.
“Najua sasa hivi.
Alisema basi kisha akanyanyuka na kupanda ngazi akaelekea juu.
Clara alinyanyua grass ya Juice akanywa fundi moja huku akiendelea kuangaza macho.
Baada ya muda Masu alishuka akiwa kavalia zile nguo zake alizokuwa amevaa siku ile walipokutana sokoni. Shati jeupe lililochanika.
Alifika na kusimama mbele ya Clara .
” Sasa unaweza kuamini?
Clara alitingisha kichwa akimaanisha ndio.
Masu alisogea na kwenda kukaa pembeni yake. Kisha akaongea kwa sauti ya chini lakini nzito ambayo ilipenya vizuri kwenye masikio ya Clara.
” Au unataka nikukumbushe zile nyakati nzuri tulipokuwa pamoja kwenye lile jumba bovu?
Clara alihisi pumzi zake zinataka kukata, mapigo ya moyo wake yalikuwa yalidunda kwa kasi.
Masu alizidi kusogea karibu yake zaidi mpaka joto la pumzi zake ilifika kwenye shavu la Clara.
” Masuuuu….
” Niambie mpenzi.
Clara alinyamaza na kushindwa kuongea kile alichotaka kusema.
” Mbona umenyamaza?
” Huwezi kuelewa kile ninachohisi muda huu yani kila kitu nahisi ni ndoto.
” Hakuna ndoto kila unachokiona ni halisi.
Clara alihisi kuna mambo mengine yanaweza kutokea pale alisogea pembeni kidogo .
” Vipi mbona unanikimbia?
” Masu nataka kujua nini kinaendelea kwenye maisha yako?
” Ila sio sasa.
” Ila saa ngapi?
” Haya mambo hayataki haraka mpenzi.
” Unajua ukiniita hivyo unazidi changanya .
Masu akitabasamu.
Sitaki kujichanganya mpenzi wangu niambie unataka nini?
” Nataka kujua kila kitu kuhusu wewe.
Masu aliachia tabasamu kidogo kisha akasema.
” Unataka kumjua Masu wa sasa na Masu wa zamani yani yule kichaa si ndio?
” Haswaa.
” Uuuuh…… Masu alishusha pumzi ndefu kisha akavuta lile shati lilichanika na kubaki na vest yake nyeupe na kufanya misuli ya mwili wake na michoro ya kifua chake ionekane.
” Kwanza siitwi Masumbuko naitwa Ilphan Hasani.
Kuja kwenye maisha yako nimekuja kwa makusudi flani .
Clara alishituka na kumkazia macho na Masu alimuangalia bila kupepesa macho.
“Unamaana gani kuniambia hivyo na nimakusudio gani hayo?
Masu alimuangalia usoni na kuiona hofu yake .
Akajisemea moyoni.
” Huyu ni mwanamke hawezi kuvumilia hiki ninachotaka kumwambia sasa natakiwa kumzungusha mpaka mipango yangu itakapotimia .
Mara ghafla Masu akaanza kucheka , Clara clara kazidi kuwa na hofu.
” Unacheka , au bado kichwa chako hakijakaa sawa?
” Umeogopa eee.
” Usije ukanifanya mimi ndio nikawa chizi wa kweli Masu , sijui Ilphan niambie ukweli wa kile anachokijua.
” Shhhh tulia basi . Hakuna kitu kibaya nilikuwa na kutisha nione hofu yako.
” Uuuuh , lakini upoje wewe?
Alisema Clara na kuanza kumpiga kifuani lakini Masu alikuwa anacheka na mwisho akimvuta na kumkumbatia kifuani kwake. Clara alitulia huku akitoa tabasamu.
” Masu…
” Niambie mpenzi.
” Kwanini uliondoka?
” Niliondoka kwa sababu ila niliamini nitarudi tena kwaajili yako.
” Nilikuja nikakuta damu kwenye lile jumba nilikuwa na hofu sana nilijua umepata matatizo.
” Ni kweli nilipata matatizo ambayo yananifanya niwe imara.
Clara alijinyanyua kwenye kifua cha Masu akamuangalia usoni na kuuliza.
” Matatizo gani?
” Kwa leo tusiwape nafasi hayo maongezi.
Masu alinyanyuka na kumnyanyua juu kama mtoto mdogo kisha akapandishwa ngazi kuelekea chumbani.
” Masu unanipeleka wapi?
” Tunaenda kumtoboa masikio huyo mtoto wetu.
Clara akitabasamu kwa aibu huku akiangalia pembeni.
Walifika chumbani Masu akampata kitandani kisha akajilaza juu ya Clara na kuanza kukiss.
Utamu ulikolea katika purukushani Clara akawa juu na Masu akawa chini.
INAENDELEA

