NILIPOTEZA KIZAZI BAADA YA KUTOA MIMBA KADHAA
Mwanamke ambaye alifanya umalaya ili kujipatia riziki,alijua kuwa hakuna mwanaume ambaye atamkubali kuwa mke, hivyo alienda hospitali na kumwambia daktari avuruge mfumo mzima wa uzazi ili asiendelee kutoa mimba tena.
Baada ya miaka kadhaa ya umalaya na kujiuza, mtu mmoja alimwambia kuhusu Neno la Mungu na Upendo wa Kristo kwa ulimwengu,mara moja, aliokoka na kuanza kufanya kazi kanisani na kumtumikia Mungu.
Kadiri muda ulivyosogea, Mchungaji mmoja alimuita na kumwambia
‘Dada yangu, Bwana ameniambia kuwa wewe ni mke wangu, nataka kukuoa.’
Yule mwanamke akatabasamu na kusema,
‘Mchungaji, Bwana hakukuambia chochote kuhusu maisha yangu? au labda hukumsikia vizuri, rudi uzungumze nae tena kwa sababu hata sina mpango wa kuolewa na mwanaume yeyote”
Mchungaji alirudi na kumwambia tena
‘Bwana amesema kuwa wewe ni mke wangu’.
Mwanamke huyo alitabasamu na kumsimulia hadithi ya maisha yake.
Mchungaji bado aling’ang’ania kumuoa na akamwambia..,
‘Mimi sina kizazi, nilikitoa baada ya kutoa mimba kadhaa’,
Lakini bado mchungaji akasisitiza,
‘Bwana ameniambia kuwa,wewe ni mke wangu’ hivyo wakafunga ndoa. .
Muda si mrefu baada ya miezi kadhaa kupita akapata mimba. Walienda hospitali ambayo aliitumia kutoa kizazi, daktari alidhani ameenda kufanya biashara nyingine … lakini yule mwanamke akamwambia daktari kuwa..
‘Mimi ni mjamzito na nimekuja hospitalini kwako kujiandikisha na kuanza kliniki’.
Daktari alishtuka, huku akicheka kwa dharau..
“Uliniambia nitoe kizazi chako,huwezi kupata watoto tena’.
Lakini yule mwanamke akamwambia ni
“NEEMA na REHEMA za MUNGU nimepata mimba”
Daktari alimfanyia vipimo ambavyo vilionyesha kuwa kweli alikuwa na ujauzito wa mwezi mmoja.
Kwa kutoamini na machozi yakimtoka, daktari alisema,
‘Tafadhali, nionyeshe Mungu wako, nataka kumwabudu’.
Miezi kadhaa baadae yule mwanamke akajifungua mtoto wa kiume.
ILIKUWA NEEMA, KIBALI NA REHEMA ZA MUNGU, yule kahaba aliolewa na kupata mtoto.
Kwa hiyo, ninaomba juu ya maisha yako kwamba chochote ambacho kinaweza au kingeweza kuharibu na kuleta maumivu na majuto maishani mwako, katika mwili wako, katika ujuzi wako, kazi yako, elimu yako, biashara yako, NEEMA, REHEMA, NA MUUJIZA WA MUNGU UKUPATE… AMEN

