ALIZAA NA MUME WANGU KWA MBWEMBWE SASA, ANATAKA HURUMA ZANGU
Alianza kubadilika taratibu, mwanzo kila akiwa kazini alikua ni mtu wa kunipigia simu, tunaongea hata nusu saa labda akiwa na kazi falani ataniambia, kikitokea kitu mimi ndiyo nilikua mtu wake wa kwanza kuongea naye, kwakifupi ndoa yangu ilikua vizuri sana.
Lakini wakati nina uajuzito wa mtoto wangu wa pili mambo yalianza kuabdilika, nyumbani hatulii, kila wakati kazi, kuna namba moja alikua anaongea nayo sana, nikaichukua nankuangalia,a likua ni mdada kufuatilia ni mfanyakazi mwenzake, tena mke wa mtu, nilifuatilia zaidi nikagundua kuwa alikua kagombana na mume wake mwanaume kamuachia nyumba kaondoka.
Kumuuliza mume wangu akaniambia anamshauri tu lakini hawana kitu chochote. Lakini siku zilivyoenda ukaribu wao ulizidi, akawa mpaka anampost mume wangu namuona status, anaweka vijembe na mambo kibao, kila nikimuambia mume wangu sitaki mazoea na huyo dada ananiambia nitaacha lakini dada anzidisha vituko.
Tulikua tunagombana sana na mume wangu kiasi kwamba kwenye kujifungua alinilazimisha nirudi kwetu, ingawa tulishapanga kuwa mdogo wangu atakuja lakini alikataa, kuondoka ndiyo nikasikia wana ukaribu na yule dada mpaka anakuja kwangu, nikimuuliza mwanaume ananinunia ananiblock hata wiki nzima.
Yule dada alianza kupost tumbo, hata nilipojifungua mume wangu aligoma mimi kurudi, aliniambia nikae nyumbani mpaka anifuate, kila msiku nilikua mtu wa kulia, ilifikia kipindi hata maziwa hayatoki, mume wangu hakutaka hata kumuona mtoto, hakuniomba picha n ahata nikimtumia alikua hajibu chochote, si kusifia mtoto wala nini?
Mama alikua ananiuliza shida nini najifanya mimi ndiyo sitaki kwenda kwangu lakini ukweli nilikua naujua mimi. Mtoto alifikisha miezi sita mume hataki kuja kunichukua, nikajua kabsia kuwa yule dada ana mimba ya mume wangu, nikimuuliza anaishia kunijibu vibaya naishia kulia.
Hakuna mtu aliyakua anajua Mambo yangu zaiadi ya Mama, lakini kuna siku Kaka aliniamia tu hauko sawa, msome huyu mtu utakua na amani, asikusumbue hivyo huyo mtu. Alinielekeza katika ukurasa wako na kuninunulia kitabu chako. Sikua na mood ya kusoma lakini kwakua sikua na kazi ya kufanya nilikua sina namna, nilisoma Kitabu chako nikagundua kitu kimoja.
Kwamba kama siwezi kuwa na furaha mimi mwenyewe basi ni ngumu sana mume wangu kunirudia, hataki nirudi si kwakaua hanipendi bali kwakau aanjua sina pakwenda, nipo nyumbani nipo salamaa hivyo hana shdia. Kitu cha kwanza nilichokifanya ni kaucha kulalamika.
Nilikua nikimpigia simu tukaongea nusu saa dakika 25 nitamzungumzia huyo mwanamke tunabishana mpaka anakata simu. Nikaacha, nikaamua tu kuwa hata kama nitaongea dakika moja na mume wangu absi itakua ni kuhusu mimi na wanangu, namuambia mambo ya watoto absi, silalamiki tena.
Kitu cha pili nilichoamua kukifanya ni kuomba kazi, nina elimu ya chuo lakini nilikua sijishughulishi na chochote, nikawa natuma barua za amombi, namuambia mume wangu,a ananiambia nisubiri watotow akue lakini namuambia hapana, mbona wengi tu wanafanya kazi.
Baada ya kama mwezi hivi alianza kulalamika, akaniambia nina mwanaume mwingine ananipa kiburi, kwanza nilicheka. Hivi unafikiri na hawa watoto nanyonyesha nina akili gani mpaka kutafuta mwanaume mwingine? Akaw kama kanielewa kidogo ila abdo anawasiwasi, akaniuliza mbona sizungumziia kurudi kwangu, nikamuambia nasubiri akiweka mambo sawa kama alivyoniambia ataniita sina hataka kwani niko nyumbani.
Sikulalamika tena na hakunitafuta tena baada ya wiki nilishanga mtu huyu hapa, alikuja nyumbani mwenyewe na kunichukua. Tukarudi, kufika sikumzunguzmia tena yule mwanamke, mambo ya mimba wala kumuuliza kama wameshaaachana au la? Niliamua kuishi maisha yangu, hata nilipowasikia kwenye simu wanaongea, kutukanana mwanamke akimtumia meseji kibao za kumuambia kamharibia maisha yake na mambo kibao sikutia neno.
Niliamua kuhangaika na ndoa yangu, yule dada alijifungua, mume wangu alirudi, akaniomba sana msamaha akiniambia kuwa ni shetani, hajui ni kwa namna gani aliingia kwenye mahusiano na huyo dada kwani ukaribu wa kushauriana ndiyo uliwepelekea. Nilimsamehe yakaisha, akawa ananiambia mambo ya huyo mwanamke sijui anamsumbua lakini nilimuambia sitaki kujua. Kuna siku huyo dada akanitafuta kua mume wangu kamtelekeza hahudumii mtoto lakini sikumpa nafasi, nikamuambia pambana na hali yako.

