𝗡𝗜 𝗞𝗜𝗖𝗛𝗔𝗔 𝗟𝗔𝗞𝗜𝗡𝗜 𝗠𝗠𝗠𝗠𝗛
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadith
SEHEMU YA 1
Ilikuwa majira ya saa sita mchana Clara alikuwa akitembea kando ya barabara akielekea sokoni kwaajili ya kwenda kununua vitu kwaajili ya matumizi ya nyumbani kwake. Akiwa anataka kuvuka barabara kwaajili ya kwenda kuingia kwenye lango kuu la soko aliona watu wakikimbia huku wakisema .
Leo kichaa cha Masu kimeamka anachapwa watu hivyo.
Clara aligeuka wanaotokea wale watu ndipo akamuona kichaa anakuja mbio huku akiwa kashika fimbo mkononi , kafungs kamba kichwani na Makopo aliyafunga na kamba na kuning’iniza kifuani kwake.
” Mmmh kikiendelea kukaa hapa huyu kichaa atamaliza fimbo yake mwilini kwangu.
Kwa haraka Clara alivuka barabara na kuingia sokoni, alifanA manunuzi ya vitu alivyokuwa anahitaji, alipomaliza alitoka huku akiwa kabeba mifuko.
Mara ghafla akakutana uso kwa uso na yule mwanaume kichaa.
Ajabu yule kichaa alimuangalia Clara huku akiwa anacheka. Clara alipata uwoga kidogo na kupita pembeni , yule kichaa aligeuka kumuangalia na kuanza kumfuata, Clara alitembea haraka haraka huku akigeuka nyuma. Yule kichaa bado alikuwa akimfuata.
” Mungu wangu niepushe na huyu kichaa asije kunifanyia kitu kibaya. Clara aliomba Mungu huku alikazana kutembea.
Ilikuwa kitendo cha ghafla sana yule kichaa alimfikia na kusimama mbele yake huku akiwa anahema, Clara alisimama huku akitetemeka na kumuangalia usoni, kichaa alicheka na kuanza kuimba nyimbo.
” Nipo salama , salama , sijui wewe huko…. Aliishia hapo na kuanza kucheka sana, baada ya muda aliacha kucheka ghafla na kumkazia macho .
‘”Ila wewe ni mzuri, wewe ni mzuri sana , utakubali niwe mpenzi wako?
Hapo Clara alihisi kuchanganyikiwa aliangalia kila upande kwaajili ya msaada lakini watu hawakuonyesha kutaka kumsaidia kutoka kwa yule kichaa na wengine walikuwa wanacheza .
Ilikuwa kama bahati alitokea kaka mmoja na kumsaidia Clara.
” Wewe masumbuko wewe toka hapo unataka kumfanya nini dada wa watu.
” Sitaki huyu mrembo ni wangu huwezi kumpata.
” Toa uchizi wako hebu muache. Alisema yule mwanaume huku akimtishia
“unataka tugombane , njoo sasa. Masu alijibu huku alinyanyua fimbo yake.
Yule kijana aliokota fimbo , masumbuko alipita pembeni ya Clara na kumpiga kibao kidogo kwenye makalio.
Clara alishituka na watu waliokuwa karibu walicheka.
” Masu muhuni huyo .
” Nae anataka demu jamani muoneeni huruma warembo.
” Inaonekana alirogwa kwa kuchukua wake za watu.
Ilikuwa gumzo kila mtu aliongea lake.
Clara alimshukuru yule kaka kisha akaondoka . Lakini bado hakuwa sawa alikuwa anatetemeka sana.
Masumbuko alikuwa kichaa mpya kwenye yale maeneo ya sokoni, watu hawakujua ametokea wapi lakini kila siku asubuhi na mapema alikuwa sokoni tena akiwa amevalia nguo nyingi mwilini mwake.
Kuna muda alikuwa sawa na kucheka na kila mtu, kuna muda alitulia pia kuna muda alikuwa mkali na kukimbiza watu.
Watu wengi walikuwa wakimuuliza
” Masu mbona umevaa nguo nyingi ?
” Dawa ya mwizi ni nini? Masu aliwauliza na hakuna alijibu swali lake ikambidi ajibu mwenyewe.
” Ni kuvaa nguo zote mwilini. Baada nguo zote ili kuwakomesha wezi.
Basi msemo wake huo ulikuwa kwa kasi na watu walikuwa wakimuuliza mara kwa mara.
Siku nyingine Clara alikuwa akitoka kwenye nyumba moja akiwa ameongozana na rafiki yake Mishi, wakitembea taratibu huku wakiongea mambo yao mara Ghafla mbele yao walimuona Masu.
” Hee! huyu kichaa anafika mpaka huku? Aliuliza Clara huku akiwa kasimama.
” Mmmh huyo Masu ni matembezi hatari , hii ndio mitaa yake ya kujidai.
” Kumbe una mfahamu?
” Ndio lakini sio kiivyo ila ni kichaa mmoja mchangamfu sana . Siku akiwa na furaha basi yeye ni kuimba tu na amejaaliwa sauti.
” Mbona na nikimuona sokoni akiwa anakinbiza watu na kuwapiga?
” Labda walimchokoza.
” Mimi namuogopa bwana zibadilishwe njia.
” Tubadili njia tunaenda wapi sasa wakazi njia ndio hii?
Masu alipowaina aliwakimbilia huku aliwaita shangazi.
” Nyie mashangazi, hebu subirini hapo nakuja sasa hivi.
” Mungu wangu anatufuata? Mishi mimi siwezi …..
” Usiwe na hofu sio mkorofi hawezi kufanya chochote mbele yangu.
” Mishi unajua mimi mwenzio nina areji na vichaa.
Mara Masu alifika na kusimama mbele yao.
” Shangazi …
” Masu mimi sio shangazi yako mimi ni dada. Alisema Mishi.
” Huyu hapa nani?
” Rafiki yangu.
” Nataka kumuowa. Mishi aliangua kicheko na Clara akaishia kuguna.
” Shoga bahati yako hiyo mchumba ndio huyo.
” Mishi sitaki.
” Sasa hutaki mimi ndio nimesema.
” Hebu nimpeleke kituoni mimi niwahi nyumbani.
Waliendelea kutembea huku Masu akiwafuata nyumba na kuimba nyimbo za mapenzi. Aliimba kiswahili badae akaimba kihindi na kuwafanya Clara na Mishi wacheke.
” Umeona mambo hayo , yani Tanzania to bollywood.
” Kweli huyu kiboko.
Siku zilienda mara kwa mara Clara alikuwa akikutana na Masu na Masu alikuwa akimfuata nyuma .Clara alikuwa na hofu sababu hakuwahi kuamini kichaa yoyote. Kuna wakati alimfokea Masu asimfuate. Watu walimcheka na kumtania mchumba wa Masu.
Clara alikuwa anachukiwa sana ila nguo hakuweza kumzuia aache kumfuata.
Siku moja majira ya jioni Clara alikuwa amekaa kwenye bar moja akiwa na mpenzi wake Ibra wakawa wanaongea lakini kwenye maongezi yao walipishana kauli kidogo na kumfanya ibra aondoke kwa hasira bila hata kulipa bili.
” Wewe Ibra yani jambo dogo unanikasirikia na kutishia kuondoka.
” Wewe unajifanya una misimamo sana mara ngapi nimekubembeleza ubebe mimba lakini unanikatalia?
” Ibra mbona mimi najitahidi sana sema sijafanikiwa tu kubeba hiyo mimba.
” Haujawa tayari, siku utakayokuwa tayari utanitafuta.
” Jamani Ibra….
Ibra alinyanyuka akaondoka bila kulipa bili ikabidi Clara alipe bili.
Alitoka nje ya bar akakuta Ibra ameshaondoka. Alienda pembeni kidogo na kusimama kwenye nguzo huku machozi yakimtoka . Ghafla alihisi mtu kasimama pembeni yake aliponyanyua uso kuangalia alimuona masumbuko.
” Wewe kichaa unafanya nini hapa?
Masumbuko alikuwa anacheka cheka tu alafu badae akasema.
” Mimi nitakupa mimba.
SEHEMU YA 2
Clara alijikuta akimuangalia kwa mshangao.
” Wewe unajielewa kweli?
” Ndio mimi nakupenda nitakupa na hiyo mimba ambayo ameshindwa kukupa yule boya.
” Wewe kichaa hebu toka , kaa mbali na mimi?
” Mimi kichaa naweza kukaa mbali na wewe ila huu moyo wangu umeshindwa .
Clara alimuangalia bila kummaliza kisha akashusha pumzi . Masu aliendelea kucheka huku akisema.
” 😀😀😀 Muineni mkubwa mzima analia , eti machozi yanammwagika iloooo…. Tumzomeeni huyooooo.
” Wewe laana zina kusumbua .
Clara aliona kama masumbuko anazidi kumvuruga akili yake aliamua kuondoka lakini Masu hakumuachia aliendelea kumfuata nyuma.
” Shangazi unaenda wapi, unaenda wapi sasa ?
Clara alisimama na kumuangalia Masu kwa hasira.
” Wewe kichaa naomba usinifuate tena ukome nuksi wewe.
Ukali wa Clara ilimfanya Masu tulie. Clara aliondoka kwa hasira na kumuacha Masu akiwa kasimama anamuangalia Mpaka Clara alipotea kwenye upeo wa macho yake ndipo nae akageuka na kurudi alikotoka.
Kesho yake Clara akiwa kazini kwake alikuwa ni mtu mwenye mawazo sana.
” Unawaza nini wewe? Mishi alimuuliza huku akiwa kasimama pembeni yake.
“Mmmh Mishi bado nipo matatani sijui kwanini sipati mimba ili mambo yangu na Ibra yawe sawa.
” Kwani bado ameshikilia swala la wewe kubeba mimba?
“Ndio .
” kwani hajui kila kitu kinapanga na Mungu?
” Amechoka kusubiri.
” Siwezi kushauri ila nataka kusikia uamuzi wako kwake.
” Sina cha kuamua . Jana aliondoka kwa hasira hakulipa bili alimuachia nikupe mwenyewe.
” Clara yule mwanaume atakukondesha chukua maamuzi mapema.
” Achukue maamuzi gani?
Ilisikika sauti ya Ibra aliingia ofisini na wote wanageuka kumuangalia
” Vipi mbona upo hapa muda huu? Clara aliuliza kwa hofu akijua atakuwa kadikia walichoongea.
” Nimekuja kukupitia twende tukale pamoja chakula cha mchana.
” Sawa, lakini naomba dakika chache .
” Nawatakia mlo mwema . Alisema Mishi kisha akaondoka huku Ibra akimsindikiza kwa macho.
” Hivi huyu rafiki yako kisiwani anashinda gani na mimi?
” Kwani akifanya nini baby?
” Huoni dharau zake , ananiangalia kwa kunipatia kuanzia juu mpaka chini.
” Achana nae .
” Nini sipendi dharau. Mwambie kama damu yake haipatani na yangu akae mbali na mimi nizmtakuja kumpiga tukio la ajabu.
” Nimeshakwambia achana nae mpenzi.
” Sawa nakusubiri nje.
Ibra alitoka nje kwenda kumsubiri , Clara alichukua pochi yake na kwenda chooni , alisimama mbele ya kioo ,akafungua pochi yake na kutoa vipodozi na kuuweka uso wake sawa na kupaka rangi nyekundu ya mdomo kisha akatoka na kumfuata Ibra.
Waliondoka pamoja na kwenda kwenye mgahawa mmoja maarufu pale mjini. Waliagiza chakula na kuanza kula.
” Umefikiria vipi kuhusu kile nilichokwambia jana?
Hilk swala lilikuwa kama kisu kilichopita kwenye moyo wa Clara maana alijua Ibra akianzisha maongezi hayo lazima wamalize vibaya.
” Ibra mpenzi wangu , hili swala ni letu sote alafu swala la kupata mtoto ni mpango wa Mungu.
” Ni kweli mpango wa Mungu lakini jitihada zako ziko wapi? Au utakaa tuna kusema mpango wa Mungu bila hata kujipambania?
” Kujipambania vipi?
” Sikiliza Clara mimi sitakuwa na muda wa kupoteza kama mwaka huu hautabeba mimba basi mimi nitatafuta mwanamke mwingine.
Clara hakuwa na la kusema alishusha pumzi na kumuangalia Ibra , alishindwa kabisa kula chakula alikiona kichungu. wakati huo Ibra hakuwa anajali alikuwa anakula hakujali chochote.
Baada ya kumaliza kula waliongozana pamoja wakiwa wanakaribia lililo gari ya Ibra , masumbuko alitokea na kuanza kumuita Clara.
” Shangazi, shangazi…. Clara alijikausha kama vile hajamsikia.
Masu aliwasigelea karibu na kusimama karibu yao.
” Huyu kichaa anataka nini? Ibra alimuuliza
” Amenizoea tu.
” Nini? Umeanza kuwa na mazoea na vichaa? Ibra aliongea kwa ukali kisha akaanza kumfukuza.
” Wewe kichaa toka hapa.
Masu alikimbia , Ibra akamfungulia mlango na Clara akaingia kwenye gari. Ibra nae alienda kupanda na kuendesha gari.
” Hivi huoni kama inajitoa nuksi kuzoeana na vichaa?
” Lakini nae ni mtu na hajapenda kuwa vile.
” Wacha wewe kwahiyo unataka kujilinganisha na yule chizi? Clara nasema sitaki kuishusha hadhi yangu , sitaki kuambiwa na watu kuwa mwanamke wangu anazoeana na vichaa. Hii ninayosema ni amri sitaki kuona wala kusikia unakuwa karibu na watu wa ajabu.
SEHEMU YA 3
Siku moja Mida ya saa mbili usiku Clara alikuwa amekaa ndani kwake akiangalia tamthilia lakini bado alikuwa ameroreka.
” Sasa nifanye nini kuondoka na na huu upweke? Alisema Clara baada ya kufikiria aliachia tabasamu”
” Acha niende kwa Ibrahim tena namfanyia surprise.
Alinyanyuka pale kwenye kochi akaenda chumbani kwake , alifungua kabati na kutoa nguo yake nzuri akaweka kitandani baada ya hapo aliingia bafuni akaoga haraka kisha akatoka na kujiandaa haraka , alivaa gauni lake la zambarau , viatu vyeupe na pochi nyeupe. Alifunga mlango wake kisha akaondoka kuelekea barabarani. Huko alichukua usafiri na kuelekea nyumbani kwa Ibra.
Alipofika alifungua geti akaingia . Alipiga hatua kuelekea kwenye mlango wa kuingilia sebleni lakini kabla hajafika mlangoni aliona vimvuli vya watu wawili kupitia dirishani .
Moyo wake ulishituka kidogo.
” Ibra atakuwa yupo na nani humo ndani? Hali ya wivu ilianza kutawala kwenye moyo wake.
Alipiga hatua haraka kuelekea mlangoni. Alishika kurasa mpango ulikuwa wazi, alifungua na kuingia ndani. Akiwa amesimama mlangoni alimuona Ibra akiwa anatoka jikoni huku akiwa kashika sahani ya kuku wa kuoka. Ibra alipomuona alishituka sana.
” Wewe umefika saa ngapi hapa?
Kabla Clara hajajibu ilisikika sauti ya mwanamke.
“Baby njoo maramoja.
” Ibra ni nani uyo? Clara aliuliza huku akipiga hatua kuelekea jikoni, Ibra aliweka sahani mezani na kumzuia.
” Unaenda wapi sasa?
” Naenda kumuangalia huyo anaekuita baby.
“Hebu tutoke nje.
“Sitaki , niache…
Katika purukushani yule mwanaume akatoka jikoni.
” Ibra kuna nini? Huyu mwanamke ni nani?
” Na wewe tulia huko…
” Unataka kujua mimi ni nani? Hawezi kukwambia ila mimi nitakwambia. Mimi ni mwanamke wake , mpenzi wake tuna miaka saba kwenye uhusiano wetu.
” Mmmh makubwa. Yule mwanamke alishangaa. Lakini Ibra alijitahidi sana kumtoa clara nje. Alimbeba na kumtoa nje.
” Ibra wewe ni wakunifanyia haya yote?
” Unakujaje bila taarifa?
” Sikujua kama hii ndio michezo yako. Aliongea Clara huku akilia, lbra hakuweza kujitetea .
” Asante Ibra , nimeelewa huyo mwanamke ni bora kuliko mimi ndio maana umemuacha ndani mimi unaishia kujitupa nje. Asante sana , nashukuru kwa haya unayonilipa.
Clara aliondoka na Ibra hakusema chochote zaidi ya kumuangalia mpaka alipotoka nje ya geti .
Clara alitembea barabarani akiwa hajielewi huku machozi yakimtililika mashavuni kwake.
Alifika sehemu akamuona Masu.
” Shangazi unaenda wapi?unataka nikusindikize?
Clara alimuangalia kisha akafuta machozi na kuangalia mbele lakini ghafla aligeuka kumuangalia tena , siku hiyo Masu alikuwa amevalia shati safi la right blue na suruali nyeusi alikuwa msafi tofauti na siku zote.
” Wewe Masu hizo nguo umepata wapi?
Clara akajikuta anamuuliza
Masu alijiangalia na kujiweka sawa huku akitabasamu na kusema
” Kanipa mjomba. Nguo zangu nzuri.
Clara aliamua kuachana nae alipoangalia pembeni ya barabara aliona kuna benchi akaenda kukaa na Masu akamfuata na kukaa karibu nae.
” Unalia kama mtoto. Alisema Masu huku akiangalia barabarani magari yanakopita.
” Niache nilie huenda hali yangu ikawa sawa.
” Umefanya nini? Nani kakupiga?
” Nimepigwa na mapenzi. Clara alijikuta akiongea tu ili kujiridhisha aliamini Masu hawezi kumsaidia wala kumfariji kwa chochote ila kwakuwa alikuwa ndio mtu akiwa karibu nae alijikuta akiongea kila kitu huku machozi yakimtililika mashavuni kwake, Masu alimuangalia kwa huruma , aliyoahidi maumivu yake taratibu alinyanyua mkono wake na kushika kichwa cha Clara na kujilaza kifuani kwake. Clara alijilaza kifuani huku akilia kwa sauti.
” Lia, mpaka hasira zako ziishe. Masu aliongea kwa sauti ya upole huku akipapasa nywele za Clara.
Clara alilia mpaka machozi yakaachwa kutoka akanyamaza, huku akiwa anaendelea kusikiliza mapigo ya moyo ya Masu . Alijihisi mwenye amani alisahau kabisa kama yupo kwenye kifua cha kichaa.
Baada ya muda kusogea ndipo akashituka na kujitoa kifuani kwa Masu. Waliangaliana usoni, Masu alimuangalia kwa utulivu na kumfanya Clara ashangae.
” Hii imekuwaje, kwanini hivi? Clara aliuliza kisha akanyanyuka haraka akachukua pochi yake na kuondoka huku akiwa anafuata barabara. Masu alikuwa akimsindikiza kwa macho kuku akiwa na hisia tofauti.
Clara alitembea barabarani akiwa kama vile hajitambui akitetemeka na kuishikilia pochi yake kwa nguvu.
” Wewe dada saizi ni usiku usitembee kwa kujiamini . Alisema kaka mmoja ambae alikuwa kwenye bajaji , hapo ndipo alishituka akasimama na kusubiria usafiri. Ikipita tax alisimamisha na kuingia kumbe wakati huo Masu alikuwa akimfuatilia kwa siri .
Clara alifika nyumbani kwake akajitupa kwenye kochi la watu wawili na kuanza kukumbuka matukio yaliyotokea hasa tukio la mpenzi wake kumsaliti na mwanamke mwingine alafu akamfukuza. Clara alijikuta analia kwa uchungu .
” Siku zote amekuwa akiniambia ananipenda kumbe alikuwa ananidandanya yupo na mwanamke mwingine , au ananifanyia hivyo kwasababu sijafa ikiwa kubeba mimba yake? Sasa mimi nitafanya nini jamani sina uwezo wa kulazimisha nipate mimba.
Alilia na hatimae akajikuta amevutiwa na usingizi pale pale kwenye kochi.
Kesho kulipokucha Clara aliamka na kukaa kwenye kochi akawa anafikiria jinsi Masu alivyokuwa alimbembeleza na kumlaza kifuani kwake.
” Masu alinikata kifuani kwake na nikajihisi nina amani sana , kwanini nilikuwa vile , kwanini nimeanza kupata hisia flani juu yake?
Mmmmh Masu ni kichaa tu sipaswi kumfikiria hivi .
Akiwa bado anafikiria mara mlango wake uligongwa. Alinyanyuka kivivu kutoka pale kwenye kochi na kwenda kufungua mlango. Alikunja sura yake baada ya kukutana na na sura ya Ibrahim.
” Mambo. Ibrahim alisalimia
” Unataka nini kwangu?
” Clara nataka tuongee.
” Kwani kuna cha kuongea mimi na wewe?
” Ndio mpenzi.
” Usinitie mpenzi, mpenzi wako ni yule uliobaki nae jana nyumbani kwako.
” Acha kuwa na hasira , nipo hapa kwaajili ya kukuelezea kila kitu.
Ibra aliingia ndani walikaa sebleni na kuanza kuongea.
” Clara ni kweli nimekosea ila nataka kujihakikishia kuwa yule mwanamke sina mapenzi nae kama ilivyo kwako ila ninachotaka kutoka kwake ni mtoto tu maana ndugu zangu wananisumbua sana kuhusu hilo swala ukizingatia umri wangu unaenda.
” Kwahiyo tupo wawili na nilikuwa sijui?
” Ila nafasi yako ni kubwa sana.
” Vipi kama nilibeba mimba mimi kabla yake?
” Itakuwa bora zaidi.
” Ibra kama unanipenda achana na huyo mwanamke mimi nitabeba hiyo mimba.
” Kama ni hivyo hata sasa hivi naachana nae ila kabla sijafanya hivyo nataka tukakutana na daktari kwaajili ya kukifanyia vipimo pamoja na ushauri.
SEHEMU YA 4
Clara alikubali kwenda kufanyiwa vipimo na wakakubaliana kesho yake waende hospitali.
Baada ya Clara kumaliza kuongea na Ibra alienda kuonana na Mishi kwenye fukwe ya bahari na kumsimulia kilichomtokea jana usiku.
” Clara shoga yangu njaa zitakuuwa au kukufanya mtumwa wa mapenzi.
” Usiseme hivyo Mishi.
” Acha nikwambie ukweli , Ibra anacheza na akili yako akiwa anajua unampenda kupita kiasi. Sasa kosa kubwa kama hili nae kaka kukiri kuwa ni mwanamke wake wewe unakubali je kumsamehe kirahisi?
” Nampenda.
” Basi endelea kuwa mtumwa.
” Mishi rafiki yangu unajua kabisa kwa kiasi kikubwa nategemea Ibra, kwenye kazi yangu nalipwa mshahara kidogo ambao haukizi mahitaji yangu yote. Alafu Ibra nachukulia kama ndugu na mtu wa karibu sababu unajua kabisa sina ndugu wa kunizingatia.
” Clara bwana tuachane na hayo ila nakuomba kwa Mungu usiku na mchana akipitishwa kwenye njia iliyo bora.
” Ameen , kipenzi.
Walikaa kimnya kwa muda wakiangalia mawimbi ya bahari yalivyokuwa kakipiga.
” Mishi kuna kitu kingine.
” Kitu gani?
” Masu.
” Bado ana kusumbua?
” Nilikutana nae jana usiku wakati natoka kwa Ibra, unajua yule kichaa kanistaajabisha sana.
” Kafanyaje tena?
” Nilikuwa nakuja, nikaenda kukaa sehemu , si akaja madu na kuanza kunibembeleza na kujilaza kifuani kwake.
” 😀😀😀 Na wewe ukalala kabisa.
” Tena nilikuwa na amani kupita maelezo.
” Jamani Clara na ile minguo nyingi alikuwa hanuki?
” Yani huwezi amini sikusikia hata harufu ya jasho zaidi ya kupata hisia.
Mishi alimuangalia kwa mshangao na kuanza kucheka.
” Sasa shoga yangu unaanza kuchanganyikiwa hisia na kichaa zinatoka wapi?
” Mwenyewe najishangaa mpaka muda huu.
” Hilo ni pepo chafu linakunyemelea.
Waliongea na kuendelea kutaniiana na kucheka .
Mishi alichukuliwa kama utani lakini kwenye moyo wa Clara na akili yake ilianza kumchukulia kadi kwa aina nyingine.
Ilipofika usiku Clara alichukua nguo zake akanyoosha , alipomaliza alipanda kitandani kwaajili ya kulala ili kesho awahi hospitali.
Usiku huo Clara alipata ndoto .
Aliita yupo kwenye chumba kimoja kizuri sana amejilaza kitandani mara akaingia mwanaume mmoja mtanashati aliekuwa amenyoa vizuri , nywele zake zilikuwa zenye urefu wa wastani maeneo ya kazi na pembeni zilikuwa ndogo zaidi alikuwa kifua wazi, kifua na mikono kilichojaa kwa mazoezi na alikuwa kavalia suruali nyeusi . Yule mwanaume alikuwa na mvuto sana na kumfanya Clara tabasamu ukiwa usingizini, alipiga hatua kuelekea kitandani . Alienda kukaa karibu na Clara huku wakiangaliana kwa macho yaliyo jaa mahaba. Mara Clara akaanza kuwewesekavhuku aliita jina la Masu.
Alikurupuka kutoka usingizini.
” Masu, yule mwanaume niliemuota ni Masu . Hapana huyu ni shetani .
Clara alijikuta akiwa na wasiwasi na ile ndoto akianza kuamini ni pepo mchafu anaanza kumfuata.
Kesho yake mapema Ibra alienda kumchukua Clara wakaelekea hospitali, walienda kuonana na daktari wa mambo ya wanawake na uzazi. Clara alifanyiwa uchunguzi alionekana yupo sawa .
” Bwana Ibra naona Clara yupo sawa hana tatizo lolote kuhusu uzazi.
” Doctor sasa shida ni nini?
” Labda tungeangakia na upande wako pia.
” Mimi? Ibra aliuliza huku akiwa katia jicho.
” Ndio huenda shida ipo kwako mbegu…..
Kabla doctor hajamaliza kuongea Ibra alimkazia.
” Kwa upande wangu sina tatizo kabisa.
” Ilishawahi kufanya vipimo?
” Ndio. Ndio maana nikamleta na mwenzangu. Ibra hakuwa mkweli alidanganya ili yaishe.
” Basi tutampa Clara dawa za virutubisho.
” Sawa doctor fanya hivyo.
Clara alifungashiwa dawa wakaondoka huku Ibra akiwa anasisitiza kutumia dawa.
Siku moja Clara alikuwa akitoka kwenye mizunguko yake mara akakutana uso kwa uso na Masu. Clara alishituka na kutaka kugeuza ili aondoke Masu aliushika mkono na Clara akageuka kumuangalia usoni.
” Unamuogopa au unanipenda aibu? Masu aliuliza , Clara alikunja uso huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio alipokumbuka na ile ndoto aliyoota.
” Wewe kichaa hebu niache.
” Sawa nitakuacha lakini vipi hali yako wewe kichaa wa mapenzi?
Maneno ya Masu yalimuacha Clara mdomo wazi.
” Hivi wewe ni kichaa kweli ?
Masu alicheka na kuanza kukimbia akamuacha Clara akiwa namamuangalia.
SEHEMU YA 5
Masu aliendelea kukimbia huku akiruka ruka kama mtoto na kuzunguka .
” Aaaah , hivi huyu mtu ni kichaa kweli au anaigiza? Clara alijiuliza bila kupata jibu maana kuna muda alihisi ana igiza na kuna muda akiangalia mambo anayofanya aliamini ni kichaa kweli.
Akiwa bado anamfikiria Masu mara simu yake ikaita. Ibra ndio alikuwa anapiga.
” Clara uko wapi?
” Ipo..
” Ipo wapi? Nimepita ofisini kwako hii ni mara ya pili na sijakukuta.
” Nimetoka kidogo kuna kazi nafanya nje na hapo ofisini.
” Sawa nataka jioni tuonane.
” Sawa, nitakupigia simu nikimaliza mizunguko yangu .
Swala la Masu lilizidi kumchanganya Clara mpaka ilimbidi aende kumshirikisha rafiki yake Mishi.
” Kuna jambo moja lina shuhurisha sana akili yangu.
” Jambo gani ?
” Mishi nina wasiwasi na yule kichaa Masu.
” Wasiwasi wa nini?
” Kuna muda nahisi Masu sio kichaa, ni mtu ambae anaigiza tu.
” Mmmmmh unataka kuniambia ni mpelelezi kama watu wanavyozusha?
” Sitaki kusema hivyo lakini naweza kuhisi hivyo sababu ya mambo yake anayofanya kwangu.
” Mambo gani bwana.
” Tangia siku ile usiku niliyokutana nae kule bar nimekuwa nikimkwepa sana kutokana na hisia zangu kwake lakini leo nimekutana nae uso kwa uso kwa jinsi alivyokuwa ananiangalia na maneno aliyoongea yule sio kichaa bwana.
” Kasemaje? Na kakuangaliaje?
” Kwanza kaniangalia usoni kwa macho ya umakini sana alafu akasema unaniogopa au unanionea aibu ? Alafu baada ya hapo alicheka sana na kukimbia kama chizi vile.
” Sio kama chizi ni chizi na jaribu kuzuia hiyo mihemko yako. Masu ni chizi , kichaa full.
Mtu gani mwenye akili timamu anakula vitu vichafu, anakuwa ovyooo .
” Mmmh basi huo Masu ni 50 kwa 50.
Mishi akicheka
” Acha achachekesha Clara yani akili yako ndio inaona hivyo ?
” Kabisa yani , yani kama dishi limeyumba kuna muda mawimbi ya nanasa.
Kuanzia siku hiyo Clara alikuwa akimfikiria sana Masu kutokana na maneno yake na mambo yake ya kichokozi.
” Jamani, jamani huyu kichaa kanitoga au na mimi nataka kuwa kichaa.
Uuuuh Mungu wangu nipe uvumilivu wa hii nafsi.
Siku moja Mida ya saa kumi na mbili Clara alimuona Masu akitembea kwa mwendo wa haraka huku akiwa kamshikilia suruali yake alivyovaa. Huyo suruali ilikuwa na kiuno kikubwa.
” Sasa leo ndio siku ya kumfuatilia.
Clara alianza kumfuata nyuma huku Masu aliendelea kukata mitaa.
Masu akifika sehemu akasimama kwa sekunde kadhaa kisha akageuka nyuma, ilikuwa bahati Clara alikuwa kajibanza sehemu . Masumbuko alipoona hauna mtu anayemfuatia alitembea taratibu tena huku akiwa na wasiwasi.
Clara nae alitembea huku akijificha , walifika sehemu aligeuka na Clara nae akampa mgongo.
“Mbona kama ana wasiwasi? Alijiuliza Clara au kashitukia kama namfuatilia?
Baada ya kutembea hatimae Masu alifika kwenye jumba moja bovu akaingia ndani.
Clara alifika mpaka karibu na ile nyumba .
” Sasa hapa sijui niingie?
Kwakuwa nina nia ya kutaka kujua acha niingie.
Alipiga hatua ndogo na kuingia ndani ya kile jumba kwa tahadhali .
Aliingia ndani ya chumba kimoja akakuta nguo na matambara pia vikopo.
“Itakuwa hapa ndipo anapoishi. Huyu ni kichaa kweli.
Kumbe wakati huo Masu alimzunguka na kuja kusimama nyuma yake na kumshitua.
Clara alishituka sanapaka kudondosha mkoba wake na simu na Masu akaanza kucheka.
Mapigo ya moyo ya Clara yalidunda kwa kasi na mkono wake aliweka kifuani huku akiwa kafumba macho, mwili mzima ulitetemeka.
Masu aliokota vitu vya Clara na kusogea karibu. Yake zaidi.
” Shika vitu vyako.
Clara alitaka kuchukua lakini mikono ilikuwa ina tetemeko sana.
Masu aliweka pochi na simu juu ya bosi kisha akaenda kumkumbatia Clara.
Clara alijikuta ametulia na Masu akaanza kupapasa mgongoni .
Taratibu hisia zao zilianza kuhama clara wala hakuweza kufikiria kama yule mwanaume aliekuwa pale ni kichaa.
Hisia zilipanda Masu akimsogezea ukutani na kuanza kumbusu .
Hali ilizidi kuwa mbaya kwa wote wawili ilionekana Masu alikuwa mtaalamu sana kwenye mambo ya mahaba maana Clara alikuwa kulegea kama mlenda
INAENDELEA

