YENYE KIRUNGU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 16
Tulipoishia……….
Nilichungulia kwa dirishani
“Wewe uliyeko ndani ni nani?” Niliuliza. Ghafla nikaona yule kijana amekuja dirishani na kunitazama. Aliponiona tu hivi alianza kutokwa na machozi ikabidi nimuite Jerry
Jerry alikuja haraka na kuingia ndani, alipofika ndani yule kijana alidondoka na kupoteza fahamu akawa anatoa mapovu mdomoni
Songa nayo
Jerry alianza kucheka kwa furaha na kufunga mlango wakajifungia ndani
“Nini kimetokea?” Nilimuuliza
“Wewe subiri huko nje” Aliniambia Jerry halafu akafunga mapazia na kunifanya nisione chochote kinachoendelea ndani
Nilikaa kwa wasiwasi, huwezi amini nilianza kumkumbuka Mungu, nilijutia, nilijihisi nilikosea hatua kuingia katika familia ile ambayo ilionekana kukolea ushirikina
Ghafla nikiwa nawaza na kusali kimoyo moyo, nilisikia kelele mume wangu akipiga kelele ndani ya nyumba nilishtuka sana
“Wewe……Jerry!!!” niliita kwa sauti na kusogea mlangoni nikagonga kwa nguvu “Wewe mume wangu…..Jerry!!” nilisema kwa uoga maana nilikuwa nina wasiwasi na yule kijana mara baada tyu ya kuniambia kwamba yeye anafanya kazi ya kupeleka damu za watu kuzimu pamoja na nyama
“Uwiiiiiii…….uwiiiiiiii…….uwiiiiii majirani…” nilipiga yowe huku nikiruka ruka kwa wasiwasi “Nisaidienii….” Nilizidi kupiga yowe
Dakika moja tu watu walianza kujaa pale nyumbani
“Vipi kuna nini jirani?” Mzee mmoja aliuliza
“Mi sielewi kuna kitu kama mzimu kimemtokea mume wangu ndani….” mara nikasikia puuuh ndani, na kimya kikatawala, nilishindwa kuendelea kumueleza yule mzee nikawa natetemeka nawaza yaliyomkuta Jerry ndani
“Kitu kama mzimu yaani kivipi mbona sikuelewi?” aliniuliza yule mzee…. Halafu akanitazama mkononi ile pete ambayo haionekani na watu wengine nilishangaa yeye kaiona akanishika mkono na kuitazama kwa mshangao
“Anithaa……!” yule mzee aliniita na kunishika mkono ule akautazama “ina maana una mkataba? Umeshajitoa sadaka?” Aliniuliza lakini mi sikuwa na uelewa mpana, yule mzee kwanza amejuaje na kwanini aione pete akati watu wengine hawaioni
“Ahahahaahaaaaaa……” alianza kucheka kwa nguvu “ahahaha”
“Vipi mzee Marwa??” niliuliza kwa mshangao
Watu wanazidi kujaa. Mara ghafla nikaona mlango umefunguliwa wa nyumba.
Wote tulikodolea ndani tuone kilichotokea lakini alitoka yule pacha wa mume wangu akasimama na kututazama, alikuwa kifua wazi.
Watu walikuwa sasa wana uwezo wa kumuona kwa macho ya nyama niliogopa sana
“Jerry!” Mama Mima alimuita akijua ni mume wangu maana walifanana kabisa
“Jerry……Jerrry. ….Jirani kuna nini?” Waliuliza kwa mshangao
Kijana yule hakujibu alirudi ndani
“Mume wangu yuko wapi?” Niliuliza kwa masikitiko makubwa maana nilihisi ameshapata majanga huko ndani…
SEHEMU YA 17
Ilinibidi kuwahi mlangoni haraka kabla hajafunga, sijui nilipata wapi ujasiri, niliingia ndani bila kujali yupo humo ndani mzimu kama ule. Niliona kama mume wangu ameuawa basi heri na mimi pia niuawe.
Watu walikuwa wananishangaa maana walikuwa hawajui kinachoendelea, wao walifikiri yule ni mume wangu maana walifanana.
Kijana yule alisimama sebuleni nikasita
“Niambie mume wangu yuko wapi? Usikute umemuua, nitakuua nakuambia” Nilisema kwa hasira na kumpita nikaelekea chumbani
Ile nimefika chumbani hivi nilimkuta mume wangu anapaki vitu vyake na yuko mzima kabisa
“Jerry!” Nilisema huku nikihema sana
“Nini?” aliniuliza huku akiinua kichwa anitazame
“Uko salama?” Aliniuliza
“Ndio, nimemaliza kazi yangu” Alisema na kufunga zipu ya begi kisha akainuka na kulishika akaanza kuliendesha maana lilikuwa na vitairi
“Unaenda wapi?” Nilimuuliza lakini alizidi kutoka mlangoni bila kunijibu “Mume wangu unaenda wapi?” Nilimuuliza tena halafu nikawahi na kumzuia asizidi kutoka
“Niachie nipite…..” Alisema, nilishangaa sana machozi yalikuwa yameshaanza kumtiririka kijana yule “Please niache niondoke” alisema
“Unalia Jerry?”
“Nimechoka Anita, nimechoka acha nikaishi maisha yangu” alisema huku akijifuta machozi
“Umechoka nini, mbona unalia sasa mi sikuelewi”
“Hapana, hujui tu mapenzi yanavyouma, acha niondoke”
“Jerry nimef…..”
“niacheee!” alinifokea halafu akanisukuma nikapepesuka, nilirudi nyuma kidogo “Usinishike mimi sio wa aina yako, endelea na huyu” aliniambia
“Jerry nisamehe….” Nilimuambia lakini alizidi kutoka huku machozi yakimtoka machoni
Nilijiona mwenye hatia hata kuamua kumuacha aondoke, niliona aibu maana majirani walikuwa pale nje. Yule pacha yake ambaye alikuwa ndani, alinifuata chumbani na kusimama mbele yangu akanitazama kwa jicho lenye shauku ya kutaka kitu fulani.
“Toka kwangu, toka, umeshaniharibia ndoa” Nilimuambia kijana yule kwa hasira “Ondoka…..Shindwa katika jina la Yesu” niliongea lakini wapi, alizidi kunitazama.
Kijana yule alinisogelea anataka anikumbatie lakini mimi nikamsukuma akapepesuka kule, Ghafla alianza kulia, sijui alikuwa analia nini, alilia mpaka akaketi chini kwa sababu alionekana mwenye maumivu makali.
“Ondoka, nenda zako nakuambia” Nilizidi kumkomalia.
Taratiibu kijana yule aliinuka na kunitazama kwa mara ya mwisho, anajaribu kuniongelesha ila hawezi kuongea
Niliona amegeuka taratibu huku akinitazama na kuanza kupiga hatua kuelekea katika mlango wa sebule.
Nilimtazama, muda huo nilikuwa na hasira kali sana maana ni kama ameshaniharibia maisha, kilichoniuma zaidi ni kwamba nilihisi ametumwa kuja kuivuruga ndoa yangu.
Alichukua tisheti iliyokuwa chini imelowa, akavaa na kutoka nje.
Nilisogea mlangoni ili nifunge mlango, majirani wote wananishangaa,
“Vipi? Huyu nani? Mumeo ana pacha? Wewe!” maswali yalikuwa mengi ila sikusikuliza, nilifunga mlango na kuketi ndani huku nikilia kwa uchungu.
Siku ilizidi kusogea
*
Ilipofika jioni saa 12, nilipitiwa na usingizi mzito sana kiasi kwamba nililala kama vile nakufa, halafu nililala chini kwenye zulia na wala sio kitandani.
Baada ya muda nilisikia sauti za ajabu ajabu zikiniita. Zilichanganyika sauti kama 6, zote zilikuwa zinatisha. Hii ilinifanya nikashtuka usingizini na kutazama. Ile nimefungua macho hivi niliogopa sana maana nilikuta nimezungukwa na watu 7 , wamesimama kando kando ya kitanda wamevaa mavazi meusi na nyuso zao wamezifunika hivyo sura hazionekani
“Mamaa….!” Nilipiga kelele kwa nguvu sana huku nikijaribu kusogea ukutani ili kujikomboa
“Anita Anita” Sauti nzito ililitaja jina langu mimi nikatulia huku nikitetemeka sijui la kufanya “Anitaaaa…..tumekuja kukuchukua” alisema mtu mmoja kati yao
“Hapana….shindwaaa” Nilisema kwa wasiwasi
“Hahaha…..tunakuhitaji wewe kama mshirika wetu” alisema
“Mimi sio mshirika wenu”
“Una mkataba wa kututumikia miaka yako yote ya uhai, la sivyo tutakuua….”
Nikisikitishwa na maneno yale, niliposikia masuala ya mkataba niligundua fika ni ile pete niliyovishwa usingizini wiki kadhaa zilizopita ndo inayoonyesha mkataba.
Niliishiwa pozi nikabaki nalia tu…
SEHEMU YA 18
Nilinyanyua mkono nikatazama pete iko kidoleni mwangu, nilijaribu kuitoa lakini nilijikuta nalegea na kupoteza fahamu.
Nilikuja kushtuka baada ya muda, nilijikuta niko katikati ya mafuvu mengi ya watu, huku kukizungukwa na mioto.
“Mamaa…..” Nilipiga kelele kwa nguvu huku nikiinuka
Natazama ni maeneo ya katikati mwitu, niko peke yangu hakuna kiumbe kingine kilichonizunguka,
Kulikuwa na miili ya watu waliofariki muda mrefu yaani mifupa na mafuvu, hata hivyo pia kulikuwa na watu wachache walilazwa kando walionekana kufariki muda usiokuwa wa siku nyingi.
Aidha walikiwa miili yao imeoza, inanuna kiasi cha kunipa kichefu chefu, ukijumlisha mimba niliyokuwa nayo nilipata shida sana
Machozi yakinitiririka nilianza kutembea kutafuta njia, lilikuwa eneo pekee lililo wazi, pande zote kukizungukwa na msitu mkubwa uliotandwa na giza totoro.
“Mungu baba nisaidie” Nilisema huku nikiangalia kule na huku. Nilizidi kutembea
Nilifika mwisho wa mafuvu yale nikawa nakaribia msitu lakini ule msitu ulitisha zaidi, maana viumbe vyenye kufanana na binadamu sijui ni binadamu au majini, vilivalia nguo nyeupe na vilipaa kuzunguka eneo, mara nyingi vilitokea na kupotea.
Nilizidi kuogopa nilijiuliza ni wapi kule nilipopelekwa, nilijutia maamuzi yangu katika penzi.
Nilijaribu kuivua pete lakini nilishindwa bado. Nikiwa naangalia gizani kwa uoga, mara kwa mbaaali niliona vimulimuli, yaani wale wadudu shaya ambao wanawaka waka muda wa usiku.
Nilikumbuka jinsi walivyokuwa wakimzunguka pacha wa mume wangu kipindi alipolala kwangu, nafsi ikaniambia labda huenda ikawa yuko pale.
Nilianza kukatiza msituni peke yangu, usiku wa kutisha usiku mnene kwenye giza, nachomwa na miba na sijui ninakoelekea kama kuna usalama
Nilitembea nafuata wale wadudu, hadi nilipokaribia ene lile. Kweli bwana, nilichokuwa nimekidhania kilikuwepo. Nilimuona Jerry (Pacha wa mume wangu) akiwa juu ya mti ametulia anazungukwa na wale wadudu taratibu.
Aliponiona alishuka mtini na kunifuata akanikumbatia.
“Jerry…..Huku wapi?” Nilimuuliza lakini hakunijibu maana hakuwa na uwezo wa kuzungumza. Alichofanya Alinishika mkono na kunivuta.
Tulipofika mbele alinikumbatia na kulia kwa kwikwi halafu akapiga magoti na kunishika kile kidole chenye pete yangu akafumba macho na kutafakari kwa muda mrefu sana.
Baada ya kufikiria kwa muda mrefu niliona pete ile ya kichawi ikinitoka taratibu na kunivua, alipohakikisha imevuka, aliitupa katikati ya msitu halafu akanishika macho yangu kuyafunga.
Ile nafungua hivi, tuko chumbani kwangu, nilishtuka sana lakini pia niliogopa, nilishukuru ameniokoa
“Hapa wapi?” Nilimuuliza,
Jerry alipoona nimeduwaa aliwasha taa. Kuwasha taa hivi.
Wale wachawi wenye mavazi meupe walikuwa wamekizunguka chumba changu bado.
“Eeeh mama” nilipiga kelele huku nikijaribu kuwahi mlangoni nitoke.
Ghafla walimnasa Jeri na kumuweka katikati yao. Kumbe walikuwa wamemuweka katika mtego kijana yule masikini…
SEHEMU YA 19
“hahahaaaaa……..” Wachawi wale walipiga kelele kwa furaha baada ya kumpata mtu wao. Halafu walipotea naye moja kwa moja
Nilibaki nimeduwaa naogopa, nashindwa kuelewa nini kinachoendelea. Nilitoka nje haraka na kwenda kwa mwenyekiti wa mtaa kuomba nilale pale maana niliona kwamba nitauawa na mizimu na mashetani.
Asubuhi ilipofika nilienda kwa padri kanisani
“Padri nina tatizo”
“Tatizo gani mwanangu?” Aliniuliza
“Kuna mizimu inatokea ndani ya nyumba yangu kila mara, naomba uniombee”
“Imetokea tangu lini?”
“Mwezi sasa”
“Haya, pole sana, unasali lakini?” aliniuliza
“Kila mara baba”
“Sawa nitakuombea na nitakupa maji ya baraka utaenda kumwaga ndani ya nyumba yako, na kwa jina la Yesu aliye hai kamwe haitoona majini tena wala chochote cha nguvu za giza”
“Amen”
Padri na masister kadhaa waliniombea kisha nikapewa maji ya baraka nikaenda nayo nyumbani.
Ile nimefika hivi bila kumimina maji niliwasha simu maana ilizimika tangu jana yake usiku. Nilikutana na ujumbe mrefu sana kutoka kwa yule pacha wa mume wangu ambaye alikuwa amekombolewa kutoka katika nguvu za giza jana yake.
Ujumbe ulinisikitisha sana…
SEHEMU YA 20
Ujumbe wenyewe ulikuwa kama ifuatavyo
“Anita, wewe ni binadamu ambaye nimetokea kukupenda sana. Najua nia yenu ilikuwa kunikomboa niwe kama nyinyi, na kweli mlijitahidi lakini kwa bahati mbaya uchawi ni kama sayansi ambayo ipo kichwani mwangu, hata ukinikomboa kama nikiwa nakumbuka yale maneno ya kichawi basi nazidi kuwa mtumishi wa kuzimu.
Tazama, mliponitoa katika nguvu hizi nilitoka lakini walikuchukua wakiamini nitakufuata kuuokoa. Kumbe katika kukuokoa waliniwekea mtego ili wanikamate nisijetoboa siri zao
Hakika nimefanikiwa kurudishwa kuzimu kwa sababu yako, na hii ni kwa sababu ninakupenda, na najua una picha ya watoto wangu wawili naomba uitunze na unizalie ili iwe kumbukumbu. Mimi sitaweza kuja kuwaona tena maana nimefungwa kifungo cha milele huku nikichomwa moto wa adhabu kuzimu. Kwa heri” niliisoma ile message nikasikitika sana.
Nikiw natafakari ujumbe ule, simu yangu iliita na ni yeye ananipigia nikaipokea, na kuweka loud
Masikini nilisikia sauti za kelele za maumivu akionekana anaumia sana
“aaaaaaaaaa……….aaaaaaaaah……..aiiiiiaaaaah” ilikuwa ni sauti iliyoonyesha maumivu makali, nilijikuta naogopa na kukemea nikachukua maji ya baraka na kumwagia ndani kwa haraka haraka.
Nilipomaliza nilizima simu na kuvunja laini sikutaka usumbufu tena.
*
Maisha yaliendelea ila ni miezi minane sasa mume wangu hajarudi tena kwangu, nilipoona maisha yamekuwa magumu nilianza kuuza mama lishe ili kujikimu na hata mpaka sasa nina mimba kubwa tu nailea. Sijui nitapata watoto wa aina gani. Nashindwa kuelewa naombeni mniombee maombi na dua zenu.
MWISHO

