CHUMBANI KWETU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Episode 8
Mimi naogopa🥺no usiogope hakuna kibaya kitakukuta mmh wakati umesema mauzauza sijui hamna bhana usijali mke wangu, umesikia?
sawa lakini nikakosa amani kuanzia hapo😭basi ikapita kama wiki tukasikia juu ya bati kama mtu anatembea😳
mume wangu unasikia uko juu kuna nini bhana yaan naweza nikafa wewe upo umu umu usikii vishindo juu ya bati?🙄 mmmh Sasa huyo ni paka au nani?
paka awe na kishindo hivyo🙄ngoja nikaangalie ni nini kilichopo hapana uende uko upate matatizo usiku wote huu uenda ni mtu atokee akujeruhi usiende plz sawa mke wangu ila usiogope mimi nipo sawa🥺basi tukalala lakini naogopaje🙄🙄
siku moja nkawasikia wanaongea na mama ake eti anaogopa mimi nisije patwa na yaliyotokea kwa najma nikawaza au niende jifungulia kwetu mimi nisije nikafa hapa😭
ikabidi nimshirikishe betty akasema nisiogope atakuwa bega kwa bega na mimi hakuna kitachontokea kwanza akasema kuanzia hiyo siku atakuwa anaamka sa nane usiku kuniombea yaani mpaka siku nijifungue,
nikasema kweli rafiki angu ana imani na upendo mana nikawaza ata niende kijijini wachaw kwan uko hawafiki🤣🤣
hapa ni kubaki tu na mimi akanambia Kila nikitaka kulala niombe🥰 tukaenda tu na mume wangu kusalimia wazazi afu tukarudi,siku moja akarudi kiunyonge akanambia kuwa anasafiri siku mbili yaani nilale mwenyewe mi naogopa mume wangu😭 vumilia Kesho kutwa tu ntakuwepo…..
sitaki mimi😭ntaenda kulala na wifi zuu ni sawa lakin kuna leo na kesho zuu akiolewa utalala na nani vitu vingne unapaswa uvumilie tu hakuna kibaya kitakukuta ni vitisho tu hivyo vinavyotokea hivyo hivyo vitisho siwezi kuvivumilia mimi sawa mke wangu ,
basi usiku huo nikasema ngoja nilale mwenyewe😆naogopa hatari nikakaa kaa mwisho nikapitiwa na usingizi nikaja kushtuka saa 7 usiku nikakuta michanga kitandan🙄🙌
niliogopa nikampigia betty apokei🥺 mume wangu pia apokei nikasema cha kufia nini?😂 nikaenda mgongea wifi zuu🥺 akafungua wifi mimi naogopa asee imagine kitandan nmekuta michanga usiku huu hahaha ila wifi una fix jaman🤣🤣
hebu acha kunidanganya michanga kabisa ata kama kuna mauzauza hawawez kufikia hivyo wifi twende ukaone mwenyewe nikamshika mkono🤝 makubwa haya jaman sasa michanga wanakuwekea yaniniiii🥺🥺
mimi ata sielewi 😔 mimi ata silali tena naomba nikalale chumbani kwako hamna shida twende tu tukaenda kulala kabla usingizi haujanipitia..
bety akapiga simu nimekuta missed call shoga angu usingizi ulikuwa mzito ata sjasikia mama ndo naamka nianze kusali nikamuhadithia akasema usijali shogangu hivyo ni kitisho vya shetani tu kuanzia sasa hivi usiogope chochote maana hofu ndo silaha ya shetan kukunyong’onyesha utavuka hiki kipindi salama Mungu awezi kataa maomb yetu kiasi hiki,
tukalala sikuona mauzauza tena kwanza usingizi ulikuwa mtamu tu😴 hata kesho yake pia nililala uko raha mstarehe mpaka nikawa namwambia mume wangu alivyorud kuwa ntaendelea kulala kwa wifi 🤔😘😹ebu acha ujinga bhana mke wangu mimi nimekumiss
bas mimba ikafikisha miezi nane,siku moja nimeamka asubuhi nakuta nimeingia period😭😭😭 jamani nina mimba period naingia ya nini…!!!😔
narudi vipenzi❤
Episode 9
basi nikamwambia mume wangu akasema twende hospital nikafanyiwa uchunguzi ikaonyesha ujauzito uko sawa,yaan sikuwa na tatizo sasa bleeding ya nini?
😔 nikawa na waswas sana mimba yangu itaharibika hapana hamna tatizo mke wangu tukarud nyumbani tuone kama itaendelea ✍🏻 ikapita wiki bleeding haikati😫🤔
mpaka siku kumi na mbili😭😭😭bado tu siku hiyo betty akaja aliomba ruhusa akaja nitembelea tukashinda wote bado akawa ananitia moyo maana mimi nilishaanza kuwa na waswas akanambia usiogope rafiki angu huu ujauzito hautoharibika utazaa salama kabisa na hiyo bleeding itakata akanishika na tumbo akaniombea nkamshukuru kwel kidogo nikapata moyo bas akaaga nikamwambia ngoja nikaoge tukusindikize mimi na wifi maana ilikua jion wif anantembezaga kufanya mazoezi🙏
nikaoga zangu nikabadili pad tukatoka tukamsindikiza betty akarudi kwake mimi na wif tukatembea tembea then tukarud nyumbani ,sasa nkawa kujikagua bleeding nikakuta imekata😳 nkampigia betty wee betty eti ulivyoniombea pale nmekuta bleeding imekata pad haijachafuka masaa matatu sahivi😳 kweli? ndiwo dah..!
ni jambo la kushukuru sana🙏 kwa hili betty sikati tamaa kumbe maombi yanajibiwa eeh? kabisa mimi nashangaa tu wewee mwenyewe waogopa💃
kuanzia leo siogopi chochote wallah vile ata kitokee kitisho gani👌👌 kuanzia apo bleeding haikurudi tena mimba ikafika miezi tisa,siku hiyo nikakaa na wifi nikamuuliza mbona sijawah muona Shem wangu wifi unanbania😹😹
aiii jaman yupo Shem wako ila bado tu hujapata nafas ya kumwona ndo unanibania sasa sio vizuri hvyo wif angu hahah ntakutambulisha……..
bas maana mpaka umemuuliza sio mchezo kabisa usijali ila mimi nilitaka nmtambulishe akikaribia taratibu za kunioa kwahyo hata hawa watu wa nyumbani hawamjui ndio hawamjui ila wewe nitakutambulisha wif angu umjue ntafrah sana …
usijali ila leo mwenzio kiuno na mgongo vinauma itakua unakaribia kujifungua hauna siku nyingi uchungu utakuja weee wif tunaanza kutishana jaman sikutishi ila nasikiaga hivyo sasa unaogopa nini jamani😹😹😹 acha tu naogopa hatar ndo ukubwa huo mama yaan nawaza mno 😿 usiogope mamy
sasa usiku sindo uchungu ukaanza😿nyieee kumbe unauma hivyo😾nikakimbizwa hospital kufika tukapokelewa vizuri ila ghafla uchungu ukakata🥺 mume wangu akaomba likizo ya siku tatu lakini zilipita zote sijajifungua bado😭nilikasirika mimi yaani uchungu unauma unakata😏
nikabaki kulala na wifi zuu mume wangu tukamwambia awe anarudi kulala nyumbani tu,
betty akanambia tumefika fainali lazima tushinde shoga angu 🤸🏻♀️ nkamwambia inashindikana kujifungua naona ntafanyiwa operation😭😭
hapana utajifungua kawaida tu kesho narudi dar nije nikuone shogangu maana alikuwa ameenda kijijini kwetu kumtambulisha mchumba ake,basi kesho yake wakaja na mama angu mzazi kwakuwa walifika usiku wakasema tutakuja asubuhi kukuona,
asubuhi kweli wakaja na mume wangu pia akapitia pale hospital kuniona afu akaenda kazini ,
basi wifi zuu akasema ngoja mimi nirudi nyumban mara moja maana hapo hakurud nyumban hyo ilikuwa siku ya sita alikuwa na mimi tu hospital ,
nkamwambia sawa kwakuwa mama na betty wapo hamna shida akaondoka, basi bhana uchungu ukanishika tena 😭😭😭nkasema najua tu sijifungui wiki nzima hivi hivi nateseka usiseme hivyo bas rafiki angu mimi naamini leo utajifungua tu usipoteze matumaini mama pia akasema utajifungua mwanangu tena salama tunakuombea sana🙏 uchungu ukachachamaa nyie nyieee😭
betty na mama wakasema tunakuombea utajifungua ,basi nikaingizwa labour sasa kila nikipush zinatoka tu damu mtoto kagoma🥺 yaani nilipush mpaka nahisi nakufa leo mara wakawa wanasema amekunywa midawa ya kienyeji nini huyu😏
nikasema hapa nina hati hati ya kufa mimi au mtoto😭😭😭 wakasema nikimbizwe theater kufanyiwa operation wakakamilisha taratibu nfanyiwe operation mume wangu na mama mkwe walikuwa wamefika,
basi wakawa wananipeleka theater kufanyiwa operation yaan nimefika mlango wa theater sijui nguvu za kupush yaan nilijifungulia mlangoni na hapo hapo nikapoteza fahamu🥺
nkaja kushtuka saa mbili usiku nikakuta nipo na mama,mama mkwe na betty wakanipa pole na hongera nimejifungua mtoto wa kike……!
INAENDELEA

