WAKATI MWINGINE MICHEPUKO HUIMARISHA NDOA
Wapendwa Asalam Alaikum/Bwana Yesu asifiwe.
Leo sijaja na mambo mengi kama ambavyo huwa nakuja siku zote.
Leo naongea kwa uchache sana wapenzi.
Jina hili nadhani si zuri sana kulitumia kwa muktadha wake, ‘Mchepuko’ ila itabidi nilitumie hivohivo.
Wakati mwingine michepuko husaidia sana katika kudumisha ndoa za watu wengi na laiti kama wanawake wenzangu wangejua thamani na nguvu ya michepuko, wala wasingeleta fujo.
Mke umetoka kujifungua tuseme na operation na hutakiwi kukutana kimwili na mwenza wako kwa mujibu wa daktari hapa lazima mchepuko uhusike.
Kuna wale wanawake wanaopata hitilafu ya kupata damu kwa muda mrefu huenda miezi na miezi, hapa lazima mchepuko uingie kazini ili kunusuru ndoa yako.
Pia kuna wale wanawake wanaopata safari za kikazi za muda mrefu, hapa lazima michepuko iingie kazini ili kunusuru ndoa yako.
Kuna wanawake wenye visirani na viburi, mume hatakuonesha kama unamkera au lah! ila ujue atatoka nje kwa mchepuko ili kupooza akili yake na kusahau kero za nyumbani kwa muda.
Huwa tunawabeza sana michepuko ila kwa kiasi fulani wanasaidia sana katika kuimarisha ndoa nyingi.
Kuna wale wanaume ambao si waongeaji na hata ukimtukana na kumuonesha jeuri, basi wala hatajibizana na wewe ila ataenda kwa mchepuko wake kupoza hasira za mke.
Na pia wakati mwingine mke uliye ndoani ndie anayesababisha mumewe kutafuta michepuko.
Hongera zao sana wale wanawake wanaowaheshimu waume zao na kuwatii.
Kwa leo naishia hapa ila jambo langu ni moja tu,
Wanawake tulieni na ndoa zenu. Nasi tunataka kuingia ndoani hukohuko.
Mpende na kumuheshimu mumeo.
Akilia lia nae
Akicheka cheka nae.
Usimpangie muda wa kupata penzi lako.
Jifunze vitu vipya sio kila siku style moja tuuu, akipata style tofauti nje utalia na mito kitandani.
Wanawake mlio ndoani mnajisahau sana.
Zile kashikashi ulizokuwa unampa kabla hajakuoa huwa mnaacha kuzifanya mkishaingia ndoani, kwanini?
Mpe penzi na usim-banie.
Jifunze vitu vipya kila siku.
Na wewe mwanaume usibweteke, mpe penzi la kushiba mkeo.
Chanzo: Jamii Forums

