UKINIPA SISEMI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 31
Upande wa Matonya yeye alikuwa kimya ametulia wala hakuongea kitu chochote. Baada tu ya Hukumu kutolewa tulifungwa Pingu tena tukabakiwa kwenye Defender safari ya kupelekwa Magerezani Uyui kuwa wafungwa Rasmi ilianza
Ndani ya Gari kipindi tunapelekwa Gerezani tulikuwa tumekalishwa chini huku ukimia ukiwa umetawala. Kila mmoja alikuwa kimya akifikilia kitu cha kufanya. Moyo kwa kweli ulikuwa unauma sana. Kijana ambaye nilikuwa na maono ya kuishi vizuri na bado nilikuwa na mchango mkubwa kwenye taifa nimejikuta nafungwa kifungo cha Maisha jela kisa kuwa na Uhusiano wa kimapenzi na Mtoto wa Masanja. Nilifikilia Maisha yangu nilipotoka hadi nilijikuta na Mwaga machozi maana ni mengi sana nilikuwa nimepitia na mengi sana yalinisubilia kufanya. Nilisoma Shule ya Seminary na kupoteza miaka kibao ili baadae niwe Padri ila katikakati ya Masomo yangu niliharibiwa na Magreth ambaye alikuwa anafanya kwa lengo la kulipiza kisasi. Nikaachana na Seminary ili kumfanya Magreth kutimiza kile anachotaka na Mimi nikaangukia kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Klinita lakini nako nikaambulia kifo cha Mama yangu kwa kuchinjwa vibaya kisha kichwa nikatumiwa kama zawadi. Katika vitu ambavyo viliniuma maishani kwangu na yananipa nguvu za kutaka kufanya mambo mabaya kwa Mchungaji masanja bila kujali ukatili wake ilikuwa kifo cha mama yangu pamoja na kile ambacho alimfanyia mama yake na Magreth mwajuma nyamilambo pamoja na ukoo wake kwa Ujumla. Simulizi ya maisha ya Magreth ambaye alinipa ilikuwa inatisha na inatia Huruma hivyo nilipaswa kumuonyesha Masanja kuwa kile ambacho anafanya siyo kizuri. Safari iliendelea hatimae tulifikishwa Gerezani tukaandiskishwa kisha tulipewa Mavazi tukapelekwa kwenye chumba ambacho tungekuwa tunaishi. Kiukweli chumba kilikuwa kichafu sana huku sehemu ya kulala kulikuwa na vipande
vya Godoro ambavyo vilikuwa na Rangi ya kama kunguni wanaishi mle. Mazingira ya kile chumba pamoja na Vigorodo ndio vilinipa mzuka wa kutoroka na nilikubali kabsa bora kitu chochote kibaya kinitokee lakini kutoroka kupo pale pale. Muda ule ule baada ya kuonyeshwa sehemu ambayo tungekuwa tunaangusha tulikuja kuchukuliwa kwa Ulinzi mkali na kupelekwa sehemu kufanya kazi. Kazi ambayo tulipelekwa kwa kweli ilikuwa na Ugumu wake maana ilikuwa kufyatua tofali za block ukifikilia na mimi nilikuwa Mlaini kwa kazi Ngumu kama zile nilikuwa sijazizoea. Hata pale Magerezani kitu kingine ambacho kilikuwa kinaniumiza tangia nikamatwe sikuwahi kumuona ndugu yangu hata Mmoja anakuja kunisalimia. Hii nilihisi baada ya kusikia kuwa mimi ndio nimemuua mama yangu ili kupata utajiri nahisi ndio walichukia. Maisha yaliendelea Gerezani hatimae tulimaliza miezi mitatu bado tulikuwa hatujatoroka kabsa maana ulizi kwetu ulikuwa siyo wa mchezo mchezo. Kila sehemu ambayo tulikuwa tunapelekwa kufanya kazi kulikuwa na ulinzi imara sana kitu ambacho kilikuwa kinatupa Ugumu wa sisi kufanya kazi. Hali ya afya zetu kwa kweli nazo zilipungua kwa kiasi kikubwa hii ilitokana na kazi ngumu ambayo tulikuwa tunafanya alafu unakula chakula hakieleweki na bado unakuwa na mawazo. Kwa maisha ambayo nilikuwa naishi kwa Muda ule Gerezani nilitamani kutoroka hivyo hivyo hata nikiwa kwenye ulinzi mkali. Nakumbuka ilikuwa siku ya Juma mosi tulichukuliwa kwenda kulima shamba la Mkuu wa Gereza kutokana na Udogo wa lile Shamba tulichukuliwa watu watatu tu ambao tulikuwa tunakaa chumba kimoja. Ilikuwa mimi Matonya pamoja na Mzee wa makamo Mzee Juma. Ingawa tulikuwa watatu lakini askari magereza ambao walikuwa wametupeleka hadi shambani na walikuwa na Jukumu la kulinda walikuwa zaidi ya wanne. Ile hali mimi nilishaizoea na nilijua lazima kuna mtu anasisitiza sisi kulindwa vile ili tusitoroke na alikuwa anajua tukitoroka maisha yake yatakuwa magumu sana. Tukiwa tunaendelea kulima matonya alinisogelea kama alikuwa anataka kuongea neno hivi. Maana mkiwa mnalima afande hawakai karibu sana na nyinyi wanakuwa mbali hata kama mtapiga stori kwa sauti ya chini hawawezi kusikia. “Sam nilikuwa kimya miezi hii kaza na ulikuwa unaniuliza lini hasa tunatoroka na sikukupa jibu maana nilikuwa kwenye uchunguzi. Naomba jiandae kesho saa mbili kamili wakati wafungwa wanaenda kanisani ndio muda wa sisi kusepa. Tulikuja Gerezani wawili lakini tutatoka watatu pamoja na Mzee juma nimeshaongea naye na atashirikiana na yeye kutoka Gerezani”Yalikuwa ni Maneno ambayo aliongea Matonya kwa Sauti ya chini ambayo yalinishitua kidogo. Swala la kutoroka Gerezani kwangu ndio nilikuwa nalisubilia kwa hamu kubwa sana. Hivyo niliposikia neno kutoroka kwanza nilifarijika maana. “Najua siku zote ulinzi huwa mkali sana ispokuwa siku ya juma pili ambao Askari wengi huwa wapo mapumziko na wengine huwa wapo kanisani. Leo Jioni kuna afande ataniletea bastora mmoja ambaye ndio itatusaidia kutoka Gerezani kirahisi maana walinzi watakuwa wachache. Najua Gerezani tutatoka lakini tutakuwa tunatafutwa Sana hivyo Tukishatoka Gerezani Sehemu ya kwenda kujificha itakuwa kwa adui yetu mzee Masanja na Mpenzi wako klinita ndio atatakiwa kufanya hivyo Ingawa hatujamuambia. Tukijificha kwa Masanja Vigumu sana Kugundulika na baada ya mambo kuwa shwali Tutatoroka tena kuelekea Brazil kwenda kujipanga ili kuja kupambana na Masanja”Aliongea Matonya.
********************************************************************************************* Maneno ambayo aliniambia Mzungu kuwa tunatoroka yalinifurahisha Sana na Muda Mwingi nilikuwa nasubilia Kitu Kama Hicho. Pia kituo ambacho alisema tutaenda kujificha kabla ya kuondoka hicho nacho nilikifurahia maana ningepata Muda wa kumuaga Klinita na kuondoka huku nikiwa na mpango wa Kuja kumuoa nikirudi kama Magreth alivyoniambia na kama mimi tulivyoahidiana na Klinita kipindi nimefukuzwa shule na yeye alikubali kuondoka na mimi na kuacha shule lengo nimuoe. Kitu ambacho kilinishitua na kunitia Wasiwasi ni Kwa nini Mzungu Alimshirikisha na Mzee Juma kutoroka Gerezani wakati ile ishu ilikuwa ya kwetu wawili na kitendo cha kumshirikisha mzee Kama yule mimi nilihisi kwa Upande Mwingine ishu itakuwa Ngumu sasa. “Bado sijakupata Ndugu matonya swala la kutoroka watatu ila nimekupata kuwa kesho ndio siku ya kutoroka hapa Gerezani. Kwa nini tusitoroke wawili tu unataka kumshirikisha na Mzee Juma hujui kama hii kazi itakuwa Ngumu”Nilimuuliza Matonya ili nijue zaidi. “Sam hujui mengi kuhusu huyu mzee ila jibu ni Fupi Huyu mzee kakaa sana Gerezani huku akiwa na mbinu ya kutoroka Gerezani. Njia nyingi anajua ambayo ukipita utakutana na ulinzi sawa lakini hautakuwa Mkali kama wa njia nyingine. Ila kama unataka kujua zaidi kwa nini mimi nataka na huyu Mzee tutoke naye Tukirudi Gerezani muulizie vizuri
“Alinijubu Matonya. Yale Majibu ya Matonya niliyaelewa na kujua kuwa Pamoja na Mzee Kuwa anajua njia ya kutokea Kwenye Hili Gereza Kiurahisi pia lazima kuna Jambo jingine ambalo lilimfanya mzee kuwa Humu na limemshawishi Matonya kutaka kutoka naye. Maana hata Gerezani matonya alikuwa anapenda Sana kuongea na yule mzee. Ambacho nilipanga nikienda Gerezani nilitaka kuongea kwa kina na yule mzee kwa nini Mzee kama yule alikuwa anataka kutoroka Gerezani wakati alitakiwa kusubilia tu kifungo chake kiishe awe huru. Maana nilishawahi kumuuliza bado miaka mingapi imebaki kuwa huru akanijibu miwili ambae ni sawa na Mwaka Mmoja tu kwani Gerezani usiku na mchana huwa zinahesabiwa siku Mbili. Niliendelea kufanya Kazi ya Kulima ambayo tulifanya Mpaka Muda wa saa tano tulirudi kwenda kunywa uji. Baada ya kunywa Uji tulirudi tena Shambani maana haikuwa mbali sana na kuendelea kulima. Wakati nikiwa nalima nilikuwa nawaza sana mambo ambayo nitayafanya kwa haraka kama nitafanyikiwa kutoroka Gerezani. Pia muda wote nilikuwa namuomba Mungu kuwa wakati tunatoroka tufanikiwe maana kuna kuwa na hali ya hatari sana. Tulilima kwenye lile shamba hadi Muda wa saa saba ndipo tuliondoka kurudi tena Gerezani. Tulipofika Gerezani tayari Muda wa kula ulishafika hivyo tulienda kuchukua chakula. Nilipochukua mimi niliongoza hadi kwa Mzee Juma ili kwenda kumuuliza kwa nini Matonya anataka tutoroke wote. Kweli kujua njia za Gerezani tu ndio sababu ya Matonya kutaka kutoroka na Mzee Juma au kuna kitu kingine kama alivyosema matonya kuwa sijui vitu vingi kuhusu mzee Juma. Mzee Juma tulikuwa tunalala chumba kimoja na yeye ndio alikuwa mwenyeji wetu lakini kamwe sikuwahi kumuuliza kitu gani kilimfanya kuja jela zaidi nilimuulizaga anakuwa huru lini na akanijibu bado miaka miwili. Nilipofika kwa Mzee Juma nilimtania kidogo kama kawaida yangu kisha nilikaa na kuanza kula. “Mzee Najua unafahamu fika kuwa kesho tunampango wa kutoroka Gerezani na nimepewa taarifa na Matonya kuwa na wewe utakuwa Moja ya watu ambae tutatoroka gerezani. Mzee mimi nakushauri kwa nini huo mpango wa kutoroka wewe uache maana bado mwaka mmoja tu uwe huru ukitoroka na Ukakamatwa hujui kama utajiongezea adhabu bure. Pia wewe saizi ni Mzee kitu gani unakikimbilia Uraiani kwenda kukifanya mzee wangu. Maana unapotoroka Gerezani huwa kuna mambo mawili kukamatwa na kunafanikiwa ingawa asilimia kubwa wanakamatwa. Na kama unavyojua mtu akikamatwa Wakati anatoroka adhabu huwa kubwa zaidi. Mimi nakushauri mzee wangu kama hakuna Sababu kubwa ya wewe kutoroka tulia malizia kifungo chako na sisi tuonyeshe Njia tu ya kutoka hapa gerezani” Nilimwambia Mzee yule. Nilipomwambia yale maneno yule mzee kwanza Mzee aliacha kula na kuniangalia kwa jicho la Huruma sana kwa muda kama wa dakika mbili bila kuangalia sehemu nyingine. Dakika mbili zilipoisha mzee aliangalia chini kisha akaniangalia tena. Aliponiangalia tena kwa kweli nilishituka nilipomuona Mzee Akiwa anatokwa na Machozi. “Sam wewe hujui vitu vingi sana kuhusu mimi. Ila mwenzako Matonya anajua ndio maana ananishirikisha na mimi nitoroke Gerezani. Labda nikwambie kitu kimoja kazi ambayo nyinyi mnaenda kuifanya ndio hiyo hiyo mimi natakiwa kuitimiza. Sam mimi nimefungwa jela kifungo cha maisha na siyo nimebakiza miaka miwili kama nilivyokwambia wewe. Toka nimefungwa ninampango wa Kutoroka Gerezani na huu ni mwaka wa ishirini nipo humu Gerezani. Nilishajaribu kutoroka lakini askari wananikata. Huyo Matonya ambae mnataka kuroka naye alishawahi kufungwa humu na tulikuwa tunaishi chumba kimoja na siku ya kutoroka tulitoroka wote yeye alifanikiwa na mimi nilikamatwa” Aliongea Mzee Juma kisha alipeleka Mkono wake hadi usoni akafuta machozi yaliyokuwa yanamlenga kisha alipeleka mkono kwenye shingo yake akafungua cheni mmoja ambaye alikuwa amevaa. Kwenye ile cheni kulikuwa kitu kama kimkebe kidogo hivi alifungua tena nikaona picha ya mtoto hivi alikuwa ameifadhi humo. “Huyu ni Mwanangu na Ameshakufaga siku nyingi na ndio ananipa Nguvu mimi za kutoroka kwenye hili Gereza. Sam kama Najua kuna Stori ulipewa na sister Magreth kuhusu Mama yake Mwajuma Nyamilambo ambaye alikuwa anasomea Usister na baadae alipata mimba ambaye alipewa na padri Masanja. Ile mimba Mwajuma Nyamilambo aliambiwa anitaje mimi ili siri ya padri isivuje mimi nifukuzwe Shule na yeye atakuja kuolewa.
Sasa mimi ndio nilifukuzwa shule siku ile na licha ya kufukuzwa shule kuna vitu ambavyo vinaniogopesha hata kukwambia”Aliongea Mzee Juma na machozi yalianza kumtoka tena.
Sehemu Ya 32
Kwa kweli kilio cha yule Mzee kilianza kunitia Wasiwasi na kuhisi huenda yaliyomkuta na yeye yalikuwa makubwa sana. Mpaka pale alipoongea tayari nilibaini kuwa alikuwa na Mtoto tayari ameshakufa ila sikujua muhusika wa yale mambo alikuwa nani. Nilichofanya kwa Muda ule ni kuongea maneno ya Busara na Mzee Juma ya Kumsihi asilie anisimulie kile ambacho kilimtokea. “Sam kuna mambo yamenitokea Makubwa sana nataka kwenda kuyafanya hata nikifa haitakuwa mbaya. Ila kabla sijafa natakiwa nishuhudie kifo cha watu wawili ndio nife. Nataka kushuhudia kifo cha Masanja na kifo cha Mzee Jonasi. Hawa watu wawili nikiona Wamekufa hata mimi nitafurahi sana. Hawa watu ndio wamenifanya mimi kuwa kwenye hili Jela Bila hatia. Yani huwezi Amini pamoja na kutendewa unyama Mkubwa bado mimi nae nililetwa Jela. Unajua Sama Mimi nilikuwa Nasoma Upadri shule Mmoja na mama yake na magreth ambaye baadae jina lake alianza kujiita Mwajuma Nyamilambo. Nikiwa nasoma Pale chuoni mimi nilikuwa tishio kwa akili mbaya na nilikuwa mpenzi wa kila mtu pale Shuleni. Kwenye Mitihani mtu ambaye alikuwa ananisumbua alikuwa Mwajuma Nyamirambo tu ambaye alikuwa mama yake na Magreth. Siku moja nikiwa nasoma Darasani nilifuatwa na Kijana Flani na kuniambia naitwa Ofisini. Nilienda Hadi Ofisini kwenda kusikiliza naitiwa nini. Kwa kweli nilipofika Ofisini na kusikiliza kile ambacho niliambiwa nilijikuta nachanganyikiwa mbaya. Maana niliambiwa mimi nimempa mimba Mwajuma Nyamilambo. Waliendelea kusema kwa kuwa walikuwa wananipenda sana pale shuleni wanataka walimalize lile jambo kisiri wakiwa na maana hawataki kuona mimi nafungwa. Walisema kuwa mimi nikubali kuwa nimempa mimba yule mwanafunzi mwenzangu alafu niondoke pale shuleni maana bila kufanya vile walikuwa wanasema nitafungwa kifungo cha maisha. Kwa kuwa Hata yule binti Ambaye ndio Mama Yake na Magreth alikuwa amesema mimi ndio nilimpa mimba tena mbele ya Padrid mazasanja na Mzee jonasi na Sister wengine mbalimbali sikuwa na jinsi niliamua kukubaliana. Ilibidi niende hadi Bwenini kwangu nikakusanya changu na Kurudi nyumbani. Ilikuwa Kazi ngumu Sana kuwaeleza wazazi wangu nakunielewa lakini nilijitaidi kuwaambia kuwa sikufanya kitu kama kile. Huko kitaani maisha yaliendelea huku na mimi nikijitaidi kupeleleza ni nani hasa ambaye alihusika na kumpa Mwajuma nyamilambo mimba pia kwa nini yule binti alinitaja mimi wakati anajua kabsa hata salamu tu kumpa ilikuwa ni shida. Nilikaa kama Muda wa miezi miwili nilisikia wazazi wa Mwajuma wameuawa kinyama sana na baadaa ya wiki mbili tena nilipata barua kutoka kwa Mwajuma Nyamilambo ambayo ilikuwa inaniomba Msamaha kwa kile ambacho alinifanyia na kuniambia kabsa kuwa aliyesababisha kunitaja mimi ni Mchungaji masanja na ndio amempa mimba Mwajuma pia ndio amehusika na kifo cha wazazi wake na Mwajuma. Ile baruakwa kweli ilinishitua sana na sikuamini kama Padri Masanja angefanya kitu kama kile. Niliposoma ile Barua kwa kweli sikuweza kuvumilia. Nilitamani kumuulizia padri Masanja nikweli amefanya kile kitu au binti yule anataka kumchafua tu. Pia nilijua kama nitamwambia vile Masanja nakumpa kile kimeo cha barua huenda angenipa nafasi hata ya kurudi shuleni. Nilichofanya nilitafuta namba Ya padri Masanja na Kumpigia tukaongea naye. Nilipoongea naye Padri Masanja aliongea Vizuri sana na kuniambia yule binti anataka kumchafua tu. Aliendelea kusema kuwa hata wao wamegundua kuwa Mimi sijahusika kumpa mimba Mwajuma hivyo watanirudisha shuleni. Ile hali ilinifanya kufurahi sana maana niliona naenda kutimiza lengo langu. Masanja aliendelea kusema kesho atakuja nyumbani kuja kuwaomba na wazazi wangu Msamaha na anataka wote wawepo. Baada ya kuelewana Masanja nilikata simu na kuwaelezea wazazi wangu mambo yote. Wazazi wangu kwa kweli walifurahishwa na ile taarifa.
Kesho yake Masanja alikuja hadi nyumbani huku akiwa na watu ambae walionekana watumishi wazuri wa mungu maana wote walivaa Majoha. Walipofika walikaa na kuongea mambo mengi na wazazi wangu. Tukiwa Mwisho mwa maongezi namanisha wakiwa wanakula ndipo
Sehemu Ya 33
Masanja alibadilisha kibao kwa kutoa bundi yake na kuwaambia wazazi wangu wamejua siri yake wanatakiwa kufa. Kama mchezo mchezo masanja aliwauwa wazazi wangu. Alipowauwa wazazi wangu walimteka Mdogo wangu ambaye ndio huyu kwenye haka kamkebe na wewe nimekwambia mwanangu. Nilikuwa nampenda Sana Mdogo wangu ndio maana huwa nasema ni mwanangu. Walipomteka Mdogo wangu waliniambia ili wasimuue nifanye jambo moja. Jambo ambalo nitafanya ni kuwapigia simu na kuwatarifu askari kuwa nimewauwa wazazi wangu bahati mbaya nilikuwa napambana na majambazi walituvamia. Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana mdogo wangu niliamua kukubali na kupiga simu polisi nakuwaelezea sehemu ambayo nilikuwepo na tukio ambalo nilifanya. Nilipomaliza kupiga simu Masanja aliniambia wanaondoka na mdogo wangu hadi watakaposikia nimefungwa ndio watamuacha huru. Kweli Masanja aliondoka na Mdogo wangu huku wakinihaidi kama sitafungwa lazima wamuue na Mdogo wangu. Ile hali mimi ilizidi kunichanganya kwa kweli maana hakuna mtu ambaye nilikuwa nampenda kama mdogo wangu. Nilichokifanya ni kuwasubilia Polisi wanikamate na chochote ambacho wangeniuliza ningekubali kuwa mimi nimehusika ili tu nisimpoteze mdogo wangu. Kweli polisi walifika wakanikamata na waliponiuliza nilikubali kuwa mimi ndio nimewauwa wazazi wangu nikiwa kwenye pilikishani za kupambana na Majambazi. wiki mbili mbele mimi nilihukiwa kifungo cha maisha jela kitu ambacho kiliniumiza sana maana sikutegemea kama ningehukumiwa vile. Sikuwa na jinsi nilifungwa huku nikiwa nashukuru mungu mdogo wangu atakuwa Salama. Baada ya wiki moja kupita ndio sasa nilipatwa na pigo baada ya kupata taarifa kuwa mdogo wangu naye kakutwa amekufa ndani kwa kujipiga Bunduki. Ila baadae Masanja mwenyewe alikuja kuniambia kuwa na yule alikuwa anajua siri wameamua kumuua. Sasa Sam utaniambiaje Mimi niendelee kuwepo humu Gerezani. Nasema lazima nitoroke jela na nikamle nyama kabsa Masanja”Alinielezea Mzee Juma Huku Machozi yakiwa yanamtoka.
Kwa kweli maelezo ya Mzee Juma yaliniumiza sana na kuamini kweli anahaki ya kutoroka gerezani. Stori ambayo nilipewa na Magreth kuwa mama yake alimtajaga mtu mwingine kuwa amempa mimba kumbe Muhusika alikuwa ni Mzee Juma. Pia nilishindwa kuelewa Masanja alikuwa mtu wa Namna Gani maana alionekana kachukua roho za watu wengi sana Duniani. “Hiki ndio kinanifanya nitoroke kesho Gerezani sam. Nilishawahi kutoroka na Huyu huyu Matonya lakini nikakamatwa na nilipata adhabu kali sana ila kesho tena natoroka wala siogopi kufa. Maana bora nife kuliko kuendelea kumuona adui yangu yupo. Unajua Sam baada ya Mdogo wangu kuuawa nilitokea hadi kubadilisha Jina na dini kutoka Yohana hadi nilianza kujiita Mzee Juma. “Aliongea Tena Mzee Juma. Kwa maelezo ambayo alitoa Mzee Juma sikuwa kabsa na neno la kuongezea zaidi nilimwambia ajiandae tu ili kesho tuchomoke. Siku hiyo tulijiandaa sana kwa safari na Jioni ilipofika Matonya alikutana na yule Afande kisha alipewa Bunduki ambaye ingetusaidia kutoroka Gerezani na kibegi kidogo kukabiliana na askari yeyote ambaye angeshitukia Dili. kesho yake saa mbili tayari mpango wa kutoroka Gerezan ulishakamilika na tulipanga Kutoroka asubuh kabsa Muda wa saa nne. Tulisubilia tu muda wa uji ambae ilikuwa saa nne ifike wakati wafungwa wanakunywa uji sisi tungekuwa tuna escape kutoka Gerezani. Saa nne ambayo tulikuwa tunaisubilia ilifika na wafungwa waliatoka kwenda kunywa uji. Wafungwa walipoenda kunywa Uji huku na sisi tulijipanga Safari ya kutoroka ilianza. Haikuwa kazi Rais kuweza kutoroka Gerezani ila kwa milango ambayo tulikuwa tunapitia kutokana na Ramani ambayo Mzee Juma alikuwa ameisomea kitambo tulifanikiwa kwa kiasi kikubwa. Baadhi ya milango tulikutana na mlinzi mmoja na wao tulimshambulia kwa kumzimisha kisha tunapita. Dakika kama tano hivi Tayari tulikuwa nje ya Gereza. Tulipotoka nje ya Gereza matonya alifungua Begi yake ndogo ambayo alikuwa naye tangia jana na alipewa na yule afande. Alipofungua alitoa nguo akatugawia nakubadilisha. Tulipo vua Nguo za wafungwa sasa tulionekana tupo huru kabsa. Tulitembea kwa kasi sana kutoka maeneo ya Gerezani huku tukipita sehemu ambazo hazikuwa na watu wengi. Tulipohakikisha sasa tupo mbali na Gerezani tulimtafuta mtu ambaye alitusaidia simu kisha nilimpigia Klinita maana namba yake ilikuwa kichwani. Klinita alipopokea simu nakumwambia kuwa mimi ni Sam nataka aje sehemu flani kunichukua alifurahi sana. Baada ya robo saa klinita alishafika sehemu ambayo tulikuwepo na kuja kutuchukua. Alipotuchukua nilimpa maelekezo kabsa kuwa tunatakiwa kwenda kujificha kwao muda wa siku kazaa kabla ya sisi kuondoka kuelekea Brazil kwenda kujipanga kwa ajili ya kuja kupambana na Masanja. Nilipomwambia vile Klinita wala hakubisha zaidi alifurahia. Tulienda hadi kwenye Nyumba ya adui yetu kisha tuliingia hadi ndani.
Nje tulikutana na walinzi ila hakuna hata mmoja ambae alitushitukia maana ile nyumba ilikuwa ni kubwa na watu walikuwa wanaingia mara kw mara. Tulipoingia ndani Klinita alitupeleka hadi chumbani kwake ambako alikuwa analala na huko ndiko tulikuwa tunatakiwa kupumzika kwa siku kazaa kusoma upepo then tunaondoka. Tulikaa mle hadi muda wa saa saba ndio taarifa ya Wafungwa watatu kutoroka Gerezani ilitangazwa kwenye taarifa ya habari ikiambatana na picha zetu. Tena serikali ilihaidi donge Nono kwa wale ambao wangefanikisha sisi kukamatwa . “Nilijua kitu kama hiki kitatokea ndio maana niliwaambia tuje tupumzike kwanza huku. Waache wahangaike kwa siku kama kumi hivi hali ikiwa shwali sisi tutatoroka bila shida”Aliongea Matonya na sisi tulimuunga mkono. Tulikaa pale ndani chumbani kwa Magreth kama muda wa saa tano hivi tukipiga Stori na Magreth mara ghafla mlango ulianza kugongwa. Kwa haraka magreth alituingiza chooni maama chumba chake kilikuwa na Self cointener. Tulipoingia chooni magreth alienda kumfungulia yule mtu aliyekuwa anagonga mlango. “Mwanangu na wewe punguza kulala wewe muda wote wa kulala tu. Hivi umesikia taarifa kama sam na yule mzungu wametoroka Gerezani. Tena wametoroka wakiwa na mzee Flani. Sasa mwanangu tuwe makini maana hawa wataka kulipiza kisasi cha Magreth hivyo kuwa makini”Yalikuwa ni maneno ya Masanja ambaye alikuwa anaongea na mwanae magreth bila kujua wale watu waliotoroka walikuwa ndani kwake tena chumba kile kile ambacho alikuwa yupo. “Naenda kumuua sasa hivi huyu Mwanaharamu kamwe siwezi kumchelewesha. Huu ndio Muda wa kuondoka na hii Roho ya Mwanaharamu hakuna muda wa kusubilia mara kwenda Brazil. Naitaji kumuua ili hata mimi nikifa haina shida ila siwezi kuvumilia kumuacha huyu Mbwa”Yalikuwa ni Maneno ambayo aliongea Mzee Juma kwa hasira tena kwa sauti bila hata kuogopa. Wakati tukiwa tunashangaa kitu Gani kile alikuwa anakifanya mwenzetu tayari alishafungua Mlango wa choo kwa kasi na kwenda hadi chumbani. Ilibidi tu na sisi tutoke kwa haraka maana tulijua yule Mzee hawezi kupambana na Masanja. Tulipotoka Chooni tayari Mzee juma walishazoana na Masanja na wote walianguka hadi chini. Magreth muda ule naye hakujua afanye nini alikuwa anashangaa tu. Kwa kasi ya ajabu nilikimbia kwenda pale ambao walikuwa wameanguka masanja na mzee Juma ili nataka kumsadia mzee Juma nilisikia mlio wa Paa hali iliyonifanya nisite. Wakati natafakali kitu gani kimetokea masanja aliibuka kwa kasi ya ajabu kwa kumtupa mzee Juma pembeni kisha aliniweka chini ya ulinzi. “Hamuwezi kuniua kirahisi hivyo kama nyinyi mnavyohisi. Mimi kufa bado sana hivyo njia ambayo walipitia wenzenu ndio na nyinyi mnaifata. Haya Sam Msalimie Mwanangu Magreth mwambie na wewe nimekuwahi nimekuua kabla hata hujalipiza kisasi: “Aliongea Masanja lakini hata kabla hajamalizia kuongea Maneno yake nilishangaa kikombe ambacho kilikuwa na maji kikitua usoni mwake. Nilipoona kikombe cha maji kimetua usoni mwake nilimuwahi nakwenda kumzoa kisha wote tulianguka chini. Matonya naye aliwahi na kuja kumpiga teke la mkononi masanja hadi aliachia bastora yake na huo ndio ulikuwa masaada wangu. Kumbe wakati mimi natoka chooni kumsaidia mzee Juma matonya alibaki na huo ndio ukawa msaada wangu. Kwa haraka tulimshika vizuri masanja kisha tulimuagiza klinita kamba na kujakumfunga kisha tulimziba mdomo kwa kusokomeza tambala mdomoni na kwenda kumuweka bafuni. “Masanja hadi hapa ninao muda wa kukua ila siwezi kukuua kabsa kwa sasa maana hutakiwi kufa kwa hara. Nikikuua Ghafla kwa kweli sitakuwa nimekufanyia kitu kizuri nakuacha uendelee kuishi ngoja nikajifunze Ugaidi kwanza nitarudi”Aliongea Matonya kisha alifunga mlango wa chooni tukarudi hadi kwa mzee juma ambaye alikuwa amepigwa risasi na kumbeba ili kumkimbiza Hospitalini kwenda kutibiwa.
Tulimbeba mzee juma huku damu zikiwa zinamtoka lengo ilikuwa kumpeleka hospitalini kwenda kuokoa maisha yake. Kwa Jinsi ambavyo nilikuwa nimechanganyikiwa nilishasahau kuwa tulitoroka Gerezani na tulikuwa tunatafutwa. “Klinita tukitoka hivi huku tukiwa tumembeba Mzee Juma lazima kutakuwa na Maswali Mengi kwa walinzi wenu. Pia hizi Sura walinzi wanaweza kuzishitukia. Ambacho nakuomba kawatoe Walinzi kijanja kisha sisi tuje kumpakia Mzee Juma kwenye Gari tumkimbize Hospitalini”Aliongea Matonya wazo ambalo hata mimi niliona bora zaidi. “Sawa mimi nitafanya Hivyo ila hata hivyo Hospitalini niachieni mimi nimpeleke huyu Mzee Juma maana kumbukeni nyinyi mnatafutwa. Hivyo Bora akamatwe Mzee Juma nyinyi mbaki mtajua Namna ya kuweza kukabiliana na kumsaidia kuliko wote tena kukamatwa”Aliongea Klinita Maneno ambayo yalinikumbusha Mimi kuwa tulikuwa tumetoroka Gerezani. “Hapana Klinita tukianza kukushirikisha wewe kwenye vitu kama hivi tutakuwa tunakutengenezea kifo kwa baba yako. Hata hapa unatakiwa kurudi kwa baba yako ukajifanye kama tulikuteka ili asigundue kama tunashirikiana na wewe.
Ukifanya Msaada kama wewe unavyotaka na sisi tunampango wa kuondoka hapa Tanzania unafikili nani atakusadia zaidi ya baba yako kukuona Msaliti na Kukuua”Aliongea tena Matonya. Alipoongea yale maneno matonya hapakuwa na
Sehemu Ya 34
Mjadala tena maana lengo ilikuwa kuokoa maisha ya Mzee juma. Alichofanya klinita ni kutangulia nje kwa lengo la kwenda kuwarubuni walinzi ili tumtoe mzee Juma na kwenda kumpakia kwenye Gari kumpeleka hospitalini kwenda kumsaidia. Klinita alipotoka nje kuna kitu kilinijia kwenye fikra zangu. Niliwaza na kubaini sipaswi kumwacha masanja hivi hivi bila kumuwekea hata alama ya kumbukumbu. Kwa kupambana na mtu hatari kama Masanja ilikuwa kuhatarisha maisha yetu maana wengi walikuwa wanapambana na masanja wamekufa na wameacha kazi kwa wengine wamalizie. Hata mimi nilihisi huenda nikafa bila kufanikisha kile ambacho nilikuwa nataka. Kitu ambacho kilinijia akilini kwa muda ule ni kwenda kuondoka na kiungo kimoja cha masanja kumuonyesha kama mimi nilikuwa na hasira na yeye kuliko mtu yeyote duniani. Nilichofanya nilimwambia Matonya anisubilie kuna kitu muhimu sana nimesahau chumbani ambapo tulikuwepo. Sikutaka kabisa kumwambia kuwa naenda kuondoka na kiungo cha masanja hata kidogo. Nilipomwambia Vile matonya aliniruhusu na kuniambia nifanye haraka. Kwa kasi ya ajabu nilirudi mbio hadi chumbani kwa Klinita ambako kule ndio masanja alikuwepo. “Yani nyie wanaharamu wajinga kweli. Hivi ni kweli mmepata bahati ya kuniua mmeniacha mnajifanya wataalamu. Kumbuka wengi wamekufa kwa kujifanya wanataka kulipiza kisasi kitaalamu. Tena wewe mjinga yukwapi mama yako na baba yako. Yukwapi sister yako magretha ambaye alikuwa na hasira na mimi kuliko hata wewe. Tena mama yako nimemuua kinyama hadi sasa nimetenganisha kichwa chake na mwili wake. Sasa huko kaburni kama wanaenda mbinguni mama yako atakuwa kichekesho na kituko kikubwa kwani ataenda bila kichwa” Yalikuwa ni maneno ya Masanja ambaye alikuwa anaongea kwa kashifa sana huku akiwa anacheka. Yale Maneno ya masanja yalinipa hasira hadi machozi yalianza kunitoka. Niliona ambacho anakiongea huyu mjinga ni ukweli mtupu hatukupaswa kumsamehe kwa muda ule. Masanja hata alipoongea yale maneno mimi sikusema kitu chochote. Nilienda hadi kwenye meza na kutafuta haraka kitu sahihi cha kuondoka na kiungo cha Masanja hapo ndipo angeona kuwa nina hasira mbaya. Kwenye ile meza nilipata kiwembe na kuchukua kisha nilimsogelea Masanja. Nilipomfikia nilikata sikio lake bila huruma hali iliyomfanya masanja kulia kwa sauti ya juu. “Hasira ambazo ninazo siku ya kuja kukuua nitatoa kiungo kimoja kimoja. Leo nimeanza na hili sikio kama kumbukumbu yangu kwako. Masanja mimi ninahasira hadi nashindwa kuelezea ili kukuonyesha kama wewe hupaswi kuzikwa kaburini mwili wako unatakiwa kutafunwa kama nyama na kupitishiwa na maji kisha nikutolee mkunduni kama mavi naanza na hili sikio”Nilimwambia Masanja maneno machache kisha kiujasiri kabsa sikujua huo ujasiri nimeutoa wapi nilipeleka sikio la matonya mdomoni na kuanza kulitafuna. Kiukweli hiyo Siku hata mimi sikujua Nilikuwa nimefanya nini ila nilijua kufanya vile hasira zingepungua na ningemuonyesha Masanja kuwa hata mimi nilikuwa na hasira mbaya. Nilipopeleka sikio la masanja mdomoni nilitafuna mbele yake na Kulimeza huku machozi yakiwa yananitoka kwa hasira hali iliyomfanya masanja kubaki akiwa anashangaa. Nilipomeza ile sikio sikuongea kitu chochote nilienda bafuni nikaosha damu damu ili matonya asishituke na kutoka. Nilipotoka tulimbeba Mzee Juma na kwenda kumpakia kwenye Gari na Safari ya kuelekea hospitalini ilianza. Kutoka kwa Masanja hadi hosiptalini ya Wilaya kitete ilikuwa kuna umbali sana. Tukiwa Njiani Mzee Juma alifumbua Macho yake na kuonyesha hali iliyonifanya kufarijika kidogo na kuhisi kifo kwa mzee juma kilikuwa bado. “Sam kunipeleke mimi Hospitalini ni sawa na kunirudisha Gerezani tu kitu ambacho sipendi kitokee. Tena hamnirudishi mimi tu Gerezani bara hata nyie Mnaweza kurudishwa Gerezani. Ninachowaomba Niacheni mimi nife na nyinyi katafuteni maisha nchi nyingine hapa tanzania mtaishia jela tu. Ila kabla ya Kufa mimi nataka nione Masanja akifa kwanza tena nataka mnichomee Nyama ya Masanja nile ninywe na Maji ndio nife. Watu wengi sana walitaka kuona Masanja anakufa lakini wao ndio wanatangulizwa kwangu mimi sitaki itokee hivyo. Ndugu zangu nikifa mimi Kabla Masanja ajafa mimi nitaenda kumueleza nini mdogo wangu na wazazi wangu kule Kaburini. Tafadhalini sana Masanja siyo mtu wa kupewa Msamaha pindi unapopata nafasi ya kumuua. Ukimsamehe Masanja uje wewe utakufa na kumuacha. Tafadhalini Msinipeleke Hospitalini kamchukueni Masanja nije nilipe kisasi kisha mnichomee nyama yake nile ili nife nikiwa na amani. Masanja hata mkisema muende kisheria hamtamuweza hukumu yake ni kuliwa nyama tu. Au wewe Sam nambia unataka mimi nife bila kulipiza kisas. Hata Rafiki yenu Klinita kule mlikomuacha kama Masanja atafunguliwa kamba lazima atauawa maana ni msaliti aliwaingiza kwenye chumba chake na yeye ndio alileta kamba mkamfunga masanja”
Aliongea Mzee Juma Maneno ambayo yalikuwa na ukweli mtu. Matonya naye alimuelewa mzee juma na kukubaliana na kile ambacho alikuwa anakitaka. Tulichofanya tuligeuza Gari letu kwa kasi ya ajabu na kurudi tena nyumbani kwa Masanja kwenda Kumaliza kazi.
Sehemu Ya 35
Muda ule tulipanga kwenda kumalizana na Masanja kabisa na tulikuwa tunaomba Mungu Klinita awe bado hajamfungua baba yake. Muda ule ningekuwa na simu ningempigia klinita kumjulisha asimfungue masanja ila hatukuwa na Simu. Kusimama na kutafuta simu ndio tungejichelewesha zaidi. “Nashangaa mlikuwa mnataka kunipeleka Hospitalini kwanza mngeambiwa mtafute kibari kutoka polisi cha mimi kutibiwa sijui mgenikitoa wapi. Matonya ongeza Mwenda bhana kabla sijafa nile nyama ya masanja maana nahisi kifua changu kinawaka moto sijui nakaribiakufa”Aliongea Mzee Juma huku akiwa anatabasamu hali iliyonifanya kubaini kuwa mzee Juma alikuwa anapenda sana kumuona Masanja akifa. Matonya alicheza na usukani vilivyo hata dakika tano hazikwisha tayari tulishafika kwa Masanja Gheti lilifunguliwa na tuliingiza Gari hadi ndani. Yulipofika pale tulishuka na kumuacha mzee Juma kwenye Gari. Mlinzi mmoja ambaye alikuwepo pale alitukaribisha ndani sijui yeye alikuwa bado hajausoma mchezo. Kupitia Bastora moja ambaye Matonya alikuwa nayo ambaye alipewa kituoni alijiweka vizuri na kuanza kuusogelea mlango wa chumba cha Klinita. Tulipofika Mlangoni nilishitulia na Mlio wa Risasi kutoka kwenye kile chumba ingawa mlio haukusikika sana Kutokana na kile chumba kuwa gymsang bord. Ule mlio wa Risasi kwa kweli ulinilegeza na Muhusika pale Nilijua lazima alikuwa ni Klinita huenda alimfungua baba yake. Mlio wa Risasi ulitufanya kujiandaa vizuri na kusimama pembeni ya mlango ili akitoka tu analo. Ni kweli baada ya dakika moja tangu mlio usikike mlango wa chumba ulifunguliwa na Masanja alitoka. Alipotoka tu matonya alimuweka chini ya ulinzi. “Tumebadilisha Ratiba bana tumeona bora tuje kuchukua roho yako mapema maana tumeona utamaliza watu wengi. Pia Mzee juma anahamu na Nyama yako ale kabla ya kufa ili akawasimulie wazazi wake”Yalikuwa maneno machache sana aliyongea Matonya. Alipoongea vile matonya masanja alitaka kutoa bastora kiunoni kwa ajili ya kujitetea lakini Mzungu alikuwa mwepesi alimtwanga mtama ambao ulimpeleka hadi chini. Matonya hakutaka kufyatua risasi maana angewashitua walinzi ambao wengi wanakuwa ndani ya vyumba ya ile nyumba. Nilipoona Matonya amemuweza masanja mimi nilikimbia hadi ndani ya kile chumba kwenda kuangalia nani yule alikuwa amepigwa risasi. Nilipoingia kwenye kile chumba nilibaki nikiwa nimedua kwa kile ambacho nilikiona. Kwa kweli sikuamini macho yangu kama Masanja alikuwa amemuua Klinita. “Nenda salama mpenzi wangu Klinita hakika hatujafikia kile ambacho tulikuwa tunakipanga. Pia Asante kwa Kuhatarisha maisha yako ili kunitetea mimi nakupenda kuliko maelezo na Pumzika mahali pema na mimi nakuja”Niliongea Maneno machache sana kwa klinita na kutoka chumbani. Sikutaka kufikilia sana maana kwa jinsi ambavyo nilikuwa nampenda klinita ningeshindwa kufanya kazi. Nilipotoka chumbani nilimwambia Matonya kuwa klinita kafa. Tulimchukua Masanja huku akiwa chini ya ulinzi. Mlinzi naye ilibidi tumuweke chini ya ulinzi ili kuchelewesha taarifa kufika polisi. Tulienda tukawapakia hadi kwenye Gari na safari ya kuelekea Porini ambako tungeenda kula nyama ya Masanja ilianza. Tulikimbiza Gari kama muda wa Nusu saa tayari tulishaingia porini. Tulipolianza tu pori tulisimamisha gari tukamshusha yule Mlinzi na kumueleza kuwa masanja ndio amemuua mwanae na kumwambia kuwa atoe taarifa polisi kuwa wafungwa wale ndio wanaenda kumla nyama masanja kutokana unyama wa kuwauwa watu mbalimbali na kesi wakatupiwa wale wafungwa ambao sisi. Baada ya kumpa yale maelezo tuliendelea na safari. Tulitembea tena kama dakika tano ndani ya pori gari tulienda kusimamisha tukamshusha masanja na mzee juma na kuingia naye porini. Huko porini tulimfikisha masanja tukamfunga Kamba kisha tulikata Paja lake na kumchomea Haraka Mzee Juma ili ale kwani Hali yake ilikuwa mbaya. Tulikuwa tunapeleka vitu haraka ili kuwahi Mzee Juma aone wakati tunamuua masanja kama yeye alivyosema. Nyama ya masanja tuliichoma kisha tukakata vipande vidogo vidogo tukampa mzee juma na kuanza kula kwa shida maana hali yake ilikuwa mbaya sana. Wakati mzee Juma akiwa anakula nyama Huku Masanja alikuwa analia kwa uchungu kuomba msamaha kitu ambacho kilikuwa kinaniboa sana. Mzee juma alikula kama finyango tano ya nyama ya masanja huku akitabasamu kisha tulimpa maji akanywa. Alipokunywa maji tulimfungua masanja kamba na kumsogeza karibu na Mzee Juma kisha tulimpa mzee juma kisu ili alipe kisasi. Ingawa mzee Juma alikuwa amepigwa Risasi kwenye mbavu lakini alijikaza kwa nguvu zote huku machozi yakimtoka na kukipeleka kisu kwenye kifua cha Masanja. Alipopeleka kile kisu mzee juma alicheka sana hali ilimyomfanya hadi kuanguka chini na kutulia kimya. Nilipoenda kumgeuza nilikuta tayari kafa huku akiwa anacheka. Ile hali ilinisikitisha sana ila sikuwa na jinsi .
Sisi kisasi kwa masanja tulikifanya haraka kwa kumuwekea miti akiwa vile vile bado anahema na kisu kikiwa kifuani na kuchoma moto. Baada ya kuchoma moto tulimuacha na mzee Juma pale huku tukiwa tumeandika ujumbe wa maelezo yote ya Unyama aliyofanya masanja hadi kufikia kumpa adhabu ile na kuondoka. Tulitembea Mguuu kwa mguu tena Hadi kwenye kijiji kimoja ambacho hata jina sikijui.
Tulipofika kwenye kile kijiji tulinunua ijabu za kike na kuvaa lengo tusafiri kama wanawake hadi namanga Arusha huko tungevuka Mpaka wa Tanzania na kuingia kenya na kwenda kutafuta Usafiri wa kwenda brazil maana Tanzania tulikuwa tunatafutwa. Mungu siyo Athumani tulisafiri salama hadi sasa hivi Tupo Brazil naendelea na Maisha mazuri ninawatoto wawili na nimeoa binti wa kibrazil. Watoto wangu wote wakike wakwanza nimemuita klinita na wapili Magreth. One day nitarudi Tanzania tayari mmenisahau.
***MWISHOOO***

