JICHO LA TATU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 9
***ilipoishia***
Mtemi alionekana akutafuta sehemu nzuri ya kujificha ili aweze kuufyatua mshale huo kutoka kunako upinde huku akiwa ametulia…….na kulenga shabaha kwa umakini mkubwa ili mshale huo uingie katikati ya kifua cha..Joshi.
akafanikiwa kupata sehemu ya kujificha vyema…akachukua ule upinde akaweka mshale na kuuvuta vyema…akawa tayari kwa kuufyatua….lakini alikuwa akisubiri Joshi ageuke ili afyatue mshale huo kifuani mwake…
Ghafla Joshi akageuka ili kutazama nani kabaki ili amuangamize………
Mtemi akavuta upinde huo kwa nguvu zake zote akauachia mshale huo…………
***Endelea***
Joshi akauona mshale huo..akaukwepa na kutimua mbio akatokomea Mstuni…
aliweza kuuona mshale huo kwa haraka kutokana na lile jicho la chui alilolipachika kwenye sehemu ya jicho lake….aligundua kuwa mshale huo ni hatari kwa uhai wake,,ndio sababu iliyomfanya atimue mbio…
Mtemi alikasirika sana…kwa sababu ile dawa aliyoipaka kwenye mshale…haipatikani kwa urahisi..inaweza kumchukua miaka arobaini(40) kuitengeneza dawa hiyo…na inatumika mara moja tu..bila kurudia…vinginevyo itamlazimu utengeneze dawa nyingine…..kwa miaka arobaini(40).
Akaangaza angaza macho yake huku na kule..akasikitika sana kuona viwiliwili vingi vya maiti zisizokuwa na idadi….huku vichwa vimekatwa na kudondoka aridhini..damu nyingi ilitapakaa katika kijiji hicho cha jamii ya Wakololo.
Baada ya lisaa limoja kupita walionekana baadhi ya wakololo waliokimbia kwenda kujificha kwa ajili ya kuokoa maisha yao,,,wakitokea mafichoni kurudi kule kwenye kijiji chao….
*****************
Upande mwingine alionekana Michael bado akiwa amejificha ndani ya kichaka,,akiendelea kusubiri mawindo yake…ule mtego umnase mnyama ili aweze kujipatia kitoweo….alisubiri kwa muda mrefu bila kuona dalili yoyote ya mnyama kuja upande huo! akakata tamaa akaamua kusonga mbele kuwatafuta wenzake…
wakati huo huo walionekana wale maaskari watano wakizipiga hatua za tahadhari huku macho yao yakitaza kwa umakini mkubwa……ghafla wakasikia vishindo vizito vya miguu ikikimbia…..wakaanza kushambulia kwa kufyatua Risasi mfululizo kwenye ule upande ambao vishindo hivyo vilisikika….
waliendendelea kushambulia kwa muda wa dakika tano mfululizo….
kisha wakaacha na kutulia kimya,,,,, hawakusikia vishindo hivyo tena…wakajipa imani kuwa tayari wamemuuwa Joshi….wakaamua kuzipiga hatua za kunyatia kulekea ule upande waliokuwa wakifyatua risasi…wakastahajabu kumuona Kifaru mkubwa sana akiwa amedondoka chini huku akitokwa na damu nyingi kwenye matundu baada ya kupigwa risasi nyingi……
wale maaskari wakajiona wamefanya jambo la kijinga kwa kupoteza Risasi nyingi kwa lengo ambalo silo….wakaamua kusonga mbele wakaendelea kuitafuta njia ya kutoka mstuni humo……wakatokezea lile eneo ambalo kamanda mkuu wa kikosi (Michael) alikuwa hapo muda mchache uliopita…….ghafla maaskari wili wakakanyaga ule mtego alioutega Michael kwa ajili ya kumnasa mnyama ili ajipatie kitoweo….
Mtego huo ulifyatuka na kuwatoboa tumboni maaskari hao wawili…wakapoteza maisha papohapo….
wale maaskari watatu waliobaki,,wakaanza kutimua mbio,,,walikimbia bila kujua ni wapi wanaelekea……kwa mbali wakaona mto,,wakaamua kuufuata ili wavuke na kutokuzea upande wa pili….
***************
upande mwingine alionekana Joshi akizipiga hatua za kikakamavu huku akiwa na hasira za hali ya juu…..kwa mbali akaona mto…akaamua kuufuata mto huo anywe maji…kwa sababu alihisi kiu kikali.
wakati huohuo alionekana Makala akiendelea kutimua mbio akiwa uchi wa mnyama..huku akidondoka mara kwa mara…..akatokezea kando ya mto akaufuata mto huo ili apoze njaa angalau kwa kunywa maji…ghafla akakutana uso kwa uso na Joshi….Makala akastuka! hofu kubwa ikatanda juu yake….akatimua mbio…..
kutokana na mwili wake kuwa mnene pamoja na kitambi akajikuta hawezi kukimbia kwa kasi..ghafla akakanyaga sehemu iliyokuwa na udongo tifutifu akatereza na kudondoka akatumbukia ndani ya mto…
Joshi akamfuata Makala ndani ya Mto huo…
wale maaskari watatu wakomuona Joshi…wakaanza kumfyatulia Risasi mfululizo.. Joshi akaacha kumfuata makala akawafuata wale maaskari….
kumbe kamanda Michael hakuwa mbali na eneo hilo akasikia milio ya Risasi akaamua kuja upande huo..akakawaona wenzake wakiendelea kumfyatulia risasi Joshi lakinj Joshi aliendelea kuzipiga hatua kuwafuata….!!
Kamanda Michael akajumuika na wenzake akaanza kufyatua Risasi mfululizo
Risasi ziliingia kwenye mwili wa Joshi lakini akazitema kupitia mdomo wake….
Michael akachukua ile silaha maalumu kwa kutungulia ndege angani…iliyokuwa mgongini mwake…akaweka shabaha kumlenga Joshi…..akabofya kitufe cha kufyatulia…likatoka kombora likaenda moja kwa moja mpaka kifuani mwa Joshi….likatoa mripuko mkubwa ukiambatana na moto pamoja na moshi mkubwa,,,punde si punde ukaonekana ule mzimu ulioingia kwenye kiwiliwili cha Joshi ukitoka na kupotelea hewani,,,kitendo hicho wale maaskari hawakukiona kwa sababu walikuwa wakipongezana kwa ushindi ….baada ya dakika mbili moshi pamoja na moto ukatoweka… lakini wakamuina Joshi akiwa anaelea juu ya maji huku kafumba macho…wakafurahi sana…wakaamini kuwa wamemuangamiza Joshi….
******************
upande mwingine alionekana Makala akitimua mbio..akakutana uso kwa uso na kundi la watu wengi wa jamii ya Wakololo wakitimua mbio kuja upande wake….akastuka..akageuza na kukimbia kurudi alipotoka..akajikwaa na kudondoka chini…alipotaka kunyanyuka akaona tayari amechelewa!! kwani wakololo walikuwa wamemkaribia hatua tano kutoka hapo alipo..akakata tamaa akajua ndio mwisho wa uhai wake..akafumba macho na kufunika uso kwa kutumia viganja vyake….lakini akastahajabu kusikia tu vishindo vya miguu…. akafumbua macho yake..akashangaa kuona wakololo wanatimua mbio wakimpitiliza bila kumgusa….akajiuliza,,”watu hawa wanamaanisha nini? mbona hawanikamati!!?
kumbe ule mzimu ulitoka kwa Joshi na kwenda kuingia kwenye kiwiliwili cha Mtemi…akili ya Mtemi ikabadilika,,akaingiwa na Roho ya kikatiri..akaanza kuwafyeka shingo Wakololo wenzake…..kwa kuanza kuangamiza familia yake,,alimchinja Vida(binti yake) pamoja na Subi(mkewe)
wale wakololo waliobaki walishuhudia Mtemi akifanya mauwaji hayo…wakajisemea moyoni ,,” kama Mtemi kaweza kumchinja binti yake kipenzi, pamoja na mkewe,,,sisi hatoweza kutuacha tukiwa hai wakaamua kutimua mbio ili kuokoa uhai wao…..
Makala aliendelea kuwashangaa wakololo wakizidi kumpitiliza na kutokomea mstuni…..wakati anastahajabu na kujiuliza maswali ghafla…akasikia kitu kimedondoka kando yake..alipogeuza shingo yake kutazama…akaogopa sana baada ya kuona kichwa cha mkololo mmoja aliyechinjwa…….
Makala akanyanyuka haraka,,akatimua mbio kusonga mbele zaidi angalau atafute sehemu ya kujificha…….
Sehemu Ya 10
upande mwingine kule makao makuu,,
yule kuu wa kitengo cha utafiti,,akaanza kuipatwa na wasiwasi,,,lei ni siku ya tatu hajapata taarifa yoyote!!! pia hata kile kikosi cha maaskari saba(7) wakiongozwa na Kamanda Michael hawajawasili kazini,,,kutoka kwenye msitu UNGEBO…..akateuwa kikosi kingine cha watu kumi(10) waende kule mstuni kuchunguza nini kinaendelea… huenda kamanfa Michael na maaskari wenzake wamepatwa tatizo….
amri ikatekelezwa mara moja..na safari ya kwenda msitu UNGEBO ikaanza…
*****************
upande mwingine kule mstuni..alionekana Michael pamoja na maaskari wenzake watatu….wakiwa bado wamesimama kandi ya mto…Michael akauliza,,”wenzenu watatu mmewaacha wapi??
wale maaskari wakashindwa kujibu….huku nyuso zao zikionesha kuwa na huzuni ya ghafla baada ya kuulizwa swali hilo……
askari mmoja akasema,,”jana usiku mvua ilipokuwa inanyesha askari mmoja alipatwa na maradhi ya kifua….yaliyosababishwa na baridi kali..mpaka akapatwa na Mauti…
Michael alisikitika sana kusikia taarifa hiyo…akauliza tena,,” na wenzenu wawili wapo wapi??
kabla hajamalizia sentensi,,yule askari akadakia na kusema,,”wameuwawa kwa mitego hatari iliyotegwa mstuni….
Michael akauliza kwa mshangao,,” Mitego??? upande upi??
yule askari akasema huku aikisonta kwa kidole chake,,”upende ule kwenye ile miti mirefu….
Michael akastuka!! akasema,,”MUNGU WANG inamaana ile mitego imeuwa askari wangu mwenyewe??
wale maaskari wakatazamana wakauliza kwa pamoja,,”unamaanisha nini Kamanda??
Michael akajibu,,”Mimi ndiye niliyetega mitego hiyo kwa lengo la kuwinda mnyama kwa ajili ya kitoweo….
wakajikuta wapo katika hali ya majonzi….ghafla wakamuona Joshi anakurupuka baada ya kupata fahamu,,sasa hivi alikuwa katika hali ya kawaida alikuwa ni binadamu kabisa,,baada ya ule mzimu kutoka ndani ya kiwiliwili chake,,,lakini Uso wajoshi ulikuwa vilevile unatisha,,,kwa sababu uso wake haukuwa na gozi ya juu hivyo ilionekana nyama ya ndani kama kilivyo kidonda…..
Michael na maaskari wenzake wakaweka bunduki zao tayari kwa kumshambulia Joshi….wakabofya vitufe vya kufyatulia risasi…hazikutoka…walipotazama bunduki zai wakagundua Risasi zimekwisha….wakahisi kuchanganyikiwa….
Joshi aliona wale maaskari wameshikilia bunduki zao kuzielekezea upande wake..akanyoosha mikono yake juu,,kisha akapaza sauti,,”jamani msiniuwe!! mimi ni raia mwema..
Kitendo kile kilimshangaza Michael..naye akapaza sauti,,”hivyohivyo ulivyo njoo huku ukiwa umenyoosha mikona yako juu…
Joshi alifanya kama alivyoambiwa akazunguka na kupita kwenye mawe yaliyokuwa yamepangana kwa mstari akavuka na kutokezea upande wa pili….Kamanda Michael akasema,,”lala chini
Joshi akalala chini haraka…Michael akamfuata na kumfunga kamba kwenye mikono na miguu….
kisha akamnyanyua na kumkalisha kitako..
akaanza kumuhoji,,kwa nini alikuwa anafanya mauwaji!! Joshi alishangazwa na swali la Michael..akauliza kwa mshangao,,”MAUWAJI?? mbina mimi sijafanya mauwaji!! kwani hapa nimefikaje??
Michael akastuka akachomoa kisu akakiweka kwenye shingo ua Joshi akasema,,wewe umeuwa askari wangu mmoja kwa kurusha upanga ukamchoma….alafu unajifanya haujui kilichokuwa kinaendelea???? sasa nasema hivi! usiponiambia ukweli nakuchinja bila huruma…Joshi akaingiwa na hofu akasema kwa sauti ya unyenyekevu…Utaniuwa bure…lakini ukweli ni kwamba mimi sijui chochote…na sijui nimefikaje huku mstuni…….
maneno hayo yalimfanya michael akasirike…kwa kuona Joshi anadanganya hajafanya mauwaji..wakati yeye alimshuhudia kwa macho yake….akakandamiza kisu ili amchinje Joshi….ghafla wakaona askari mmoja anadondoka chini…Michael akastuka…pia wale maaskari wawili wakaingiwa na hofu kubwa…kumuona mwenzao kadondoka chini huku kisu kikiwa kimeingia upande wa ndani ya koo..kikining’inia…Michael akamtazama Joshi kwa macho ya chuki na hasira za hali ya Juu akamdunga kisu cha paja kisha akasema kwa sauti ya ukali,,”NIAMBIE NINI KINAENDELEA…akabla hajamaliza kuongea wakasikia vishindo vikubwa….mpaka aridhi ikawa inatetemeka…alipotazama uoande wa pili wa mto..akamuona Mtemi akiwa ametapakaa damu mwili mzima..Michael akamuacha Joshi…
huku akisema tukimbieni…wakaanza kutimua mbio huku wamemuacha Joshi pale chini…..
Joshi akaingiwa na hofu kubwa……huki akihisi maumivu makali sana kwenye lile jeraha alilochomwa kisu na kamanda Michael kwenye paja…alipotazama ule upande aliokuwepo Mtemi…hakumuona tena….Joshi akazidi kuchanganyikiwa alishindwa kunyanyuka kutoka pale chini kwa sababu alikuwa kafungwa mikono na miguu…mapigo yake ya moyo yakazidi kupiga kwa kasi.. akajikuta vinamtoka vijampo mfululizo.(bhu bhu) kutokana na uwoga wa hali ya ju..
********************
Upande mwingine…alionekana Michael na maaskari wenzake wakitimua mbio..lakini Michael akaingiwa na roho ya huruma!! akajisemea moyoni,,”sio vyema kumuacha pale yule mtu…wakati kunahatari…akaamua kurudi kumfuata Joshi amfungulie kamba….
wale maaskari wawili wakashangazwa na kitendo cha kanda Michael…kurudi kule kwenye hatari!! lakini Michael hakujali alitimua mbio mpaka kule alipomuacha Joshi..akamfungulia kamba kisha akasema,,”tuondoke haraka..
Joshi alimshukuru Michael..alimuona kama Mwokozi wake……..
*********************
upande mwingine…walionekana wale maaskari kumi(10) waliotumwa kutoka makao makuu kuja msitu UNGEBO..maaskari hao walianza kukaribia kufika msitu Ungebo na baada ya dakika tano wakafika…wakashuka kutoka ndani ya gari na kuanza kusonga ndani zaidi ya msitu huo kwa kutembea kwa miguu….ghafla wakakutana uso kwa uso na wakololo wakitimua mbio kuja upande wao huku wameshikilia mikuki na mishale….
wale maaskari wakasema mpo chini ua ulinzi….
wakololo hawakusikia wala kutii amri ya maaskari hao…wakololo walizidi kutimua mbio kuja ule upande walipo maaskari hao….
maaskari wakaingiwa na hofu wakajihami kwa kufyatua risasi angani…..lakini wakololo hawakusimama waliendelea kukimbia wakapitiza kuelekea upande ambao maaskari walitokea bila kuwagusa maaskari hao…
mpaka wakatokomea na kutokuonekana kabisa..
maaskari wakashangazwa na kitendo hicho…lakini hawakujali wakazidi kusonga mbele kuingia ndani ya msitu huo…
wakati huohuo alionekana Mtemi akiendelea kuzipiga hatua kusonga mbele zaidi….ghafla akakutana uso kwa uso na wale maaskari kumi…
akasimama na kuwatazama….. askari mmoja akauliza,,”wewe ni nani? mbona umevaa ngozi ya mnyama(Simba)? ulipata wapi kibali cha kuuwa mnyama wa mstuni na kumchuna ngozi??
Mtemi alibaki kimya bila kujibu chochote…..Maaskari hao waliendelea kumshangaa,, yule askari mmoja akasema,,”upo chini ya ulinzi,nyoosha mikono yako juu…
Mtemi aliendelea kumtazama yule askari,,kisha akazipiga hatua kuosogelea….alipomkaribia akarushakofi kali sana,,likampiga yule askari usoni…kofi hilo lilimrusha mbali askari huyo….
wale maaskari tisa wakastuka wakaanza kumshambulia Mtemi kwa risasi……walifyatua risasi mfululizo lakini Mtemi hakudhurika na risasi hizo…zilindunda kwenye mwili wake na kudondoka chini… wale maaskari wakaingiwa na hofu..wakaanza kutimua mbio..kurudi nyuma walipotoka…
Yule askari aliyepigwa kofi,alionekana kalala chini akiwa amekufa….
Mtemi akazipiga hatua na kusonga mbele zaidi….
*****************
Upande mwingine alionekana kamanda Michael akiwa na Joshi,pamoja na wale maaskari wawili..
wakikimbia na kuingia ndani ya pango kubwa kiasi…wakajificha…..Kamanda Michael akaanza kumuhoji Joshi,,alimuuliza juu ya mauwaji aliyokuwa akiyafanya….Joshi akajibu,,”kiukweli mimi sifahamu chochote,,kama nilivyokueleza mwanzo,,hata sifahamu nimefikaje ndani ya msitu huu!!!! lakini kwa kumbukumbu zangu,,mara ya mwisho nilimzika muuwaji…
Kamanda Michaeli akauliza kwa mshangao,,”MUUWAJI?? ni yupi huyo??
Josgi akasita kuongea… akashusha pumzi,kisha akasema,,”ndio,,namaanisha Muuwaji aliyeuwa wazazi wangu..
Michael bado alibaki mdomo wazi,,hakuelewa maneno aliyokuwa anayaongea Joshi…..
akauliza,,”ulimzija wapi huyo muuwaji? inamaana kuwa huyu anayefanya mauwaji ndiye yule muuwaji uliyemzika??
Joshi akajibu,,”mimi sijui chochote!!
Michael alizidi kuchanganyikiwa,,,hakumuelewa joshi anachokiongea….
********************
Upande mwingine walionekana wakololo wakiendelea kutimua mbio….walikimbia umbali mrefu,,wakaliona lile hema lililokuwa kama kambi ndogo yakupumzika maaskari wanaokuwa kwenye zamu ya kulinda wanyama pori…
wakololo wakasimama na kulitazama hema hilo…wakaamua kuelekea kwenye hema hilo….walipolikaribia,,yule mkuu wa vijana wa kikololo akaingia upande wa dani,,akaangaza angaza macho yake kila kona ya hema hilo….kisha akatika nje na kuongea kwa lugha yao akimaanisha,,”Tutapumzika hapa panaonekana kunausalama..
***************
upande mwingine alionekana Mtemi akizidi kusonga mbele zaidi….alitembea umbali mrefu,,hatimae akatokezea jirani kabisa na lile hema..
wakati huo huo walionekana wale maaskari tisa wakimbia kuelekea ule upande lilipokuwepo hema…
********************
Upande mwingine kule ndani ya pango Joshi alionekana kama kuna jambo atataka kumueleza Kamanda Michael…..ghafla simu ya mawasiliano kutoka makao makuu ikaita…. Michael akaipokea..
akamsikia mkuu wa kitengo cha hifadhi ya wanyama pori akisema,,”mbina tunajaribu kuwatafuta lakini mtandao haukamati mawasiliano yenu? kunatatizo gani? Michael akajibu,,”kunaatatizo makubwa sana ndani ya msitu huu..na sidhani kama kuna mtu atafanikiwa kutoka akiwa hai..kabla hajamaliza kuingea….simu(Radio call) ikamponyoka na kudondoka kwenye jiwe ikapasuka na kusambaratika….
kule kwenye hema walionwkana wakololo wakitengeneza silaha za jadi kwa kutumia…miti kuchonga mishale mingi sana!! mkuu wa vijana hao wa kikololo akatengeneza mshale moja.na kuupaka dawa maalumu….dawa hiyo ni ile dawa ya kumuangamiza mzimu aliyeingia kwenye kiwiliwili cha binadamu…..mkuu wa vijana wa kikololo alipewa dawa hiyo na babu yake…alimkabidhi dawa hiyo,,usiku kabla ya kifo chake….mkuu wa vijana wa kikololo akaitunza dawa hiyo kwa kuihifadhi kwenye kipande cha ngozi ua nyani aliyokuwa akitembea nayo kila sehemu aendako….
akachukua ule mshale alioutengeneza,,maalumu kwa kazi hiyo akapaka dawa ile kwenye ncha ya mshale huo…….
wakati wakololo wakiendelea kutengeneza mishale ya kutosha…wakamuina mtemi anakuja upande wao kule hema lilipo…
TAHARUKI….
Sehemu Ya 11
wakati huo huo walionekana wale maaskari tisa kati ya wale maaskari kumi..ambao mmojawapo aliuwawa na Mtemi. walitimua mbio kulifuata hema…walipolikaribia hema hilo wakastuka kuwakuta wale wakololo…pia wakamuona Mtemi…
walipojaribu kushambulia kwa Risasi..wakakumbuka bumduki zao hazina hata risasi moja..wakaamua kutimua mbio kurudi kule mstuni…
***********************
upande meingine alionekana Makala akiwa anakimbia akaingia ndani ya kichaka kwa lengo la kujificha….akastuka kukuta joka kubwa ndani ya kichaka hicho,, akaingiwa na hofu kubwa..akakurupuka na kutimua mbio….alikimbia mwendo mrefu kiasi…akakutana na maaskari wawili wameuwawa kwe mtego uliokuea umetegwa mstuni humo…
kumbe ndio wale maaskari walionaswa na ule mtego uliotegwa na Machael….
Macho yakamtoka Makala!! akaingiwa na wazo,kuwa achukue nguo zilizokuwa juu ya mwili wa askari…ili ajistili kwa sababu alikuwa uchi wa mnyama…..akazipiga hatua akainasua kutoka kwenye mtego maiti moja ya askari.ili achukue zile nguo avae…..alipomaliza akaanza kuzipiga hatua kwa tahadhali huku macho yake yakitazama
kwa umakini wa hali ya juu…alitembea umbali mrefu kiasi akiifuata ile njia iliyokuwa ikielekea kwenye hema pasipo yeye kujua…..Makala aliamua kuifuata njia hiyo akihisi huenda itamsaidia kutoka nje ya msitu huo
*****************
wakati huohuo alionekana kamanda Michael akiwa na Joshi pamoja na wale maaskali wawili…wakizipiga hatua kutafuta njia ya kuelekea kule kwenye Hema angalau wapumzike pia waangalie namna ya kufanya mawasiliano na makao makuu.. ili iletwe ndenge waweze kupata msaada…..walipokaribia wakaona wakololo wakimshambulia Mtemi kwa mishale mingi mfululizo…mishale hiyo iliingia kwenye mwili wa Mtemi lakini haikumdhuri…
wakololo waliendelea kumshambulia Mtemi wao kwa mishale….
akaonekana yule mkuu wa vijana wa kikololo akiuchukua ule mshale alioupaka dawa maalumu ya kuangamiza mzimu ulioingia kwenye kiwiliwili cha binadamu….akauweka mshale huo kwenye upinde na kupiga hatua mbili kulifuata dirisha la hema hilo……akaweka shabaha kumlenga Mtemi katikati ya kifua…
wakati huo huo akaonekana makala akitokeza kwenye eneo lilipokuwepo hema hilo…akastuka kuwaona wakololo wakimshambulia Mtemi kwa mishale…akajificha nyuma ya mti mkubwa kiasi huku akiendelea kushuhudia vita ya Wakololo na Mtemi wao….kumbe kamanda Michael,,,Joshi pamoja na wale maaskari wawili walikuwa eneo hilohilo..wakatokea nyuma ya makala,, Kamanda Michael akasema,,”nyoosha mikono yako juu..Makala aliposikia hivyo akakurupuka na kutimua mbio bila kugeuka nyuma..akakimbia na kutokeza sehemu iliyokuwa wazi hakuna miti…jirani kabisa na lile hema…
kule mdani ya hema alionekana yule mkuu wa vijana wa kikololo akiuvuta upinde kwa nguvu zake zote..mpaka misuli ya mikononi,,svhingoni pamoja na kichwani ikachomoza…..akauachia mshale..kuelekea kwenye kifua cha Mtemi,,punde si punde Mtemi akageuka kumtazama makala akikimbia bila muelekeo huku akidondoka chini mara kwa mara kutokana na ukubwa wa kitambi,
mshalee ule ukawa umempiga Mtemi kwenye bega lake la kushoto…ghafla ule mzimu ukatoka ndani ya kiwiliwili cha Mtemi na kuelekea angani…
kumbe mshale ule ungeingia katikati ya kifua cha Mtemi basi ndio ungekuwa mwisho wa mzimu huo……
ule mzimu ulionekana ukielea hewani kuelekea ule upande alipokuwepo kanda michael…..Joshi pamoja na wale maaskari wawili,,
Wakati huo Makala alikuwa kadondoka chini…wakati ananyanyuka ule mzimu ukaingia kwenye kiwiliwili cha Makala…….akili ya Makala ikabadilika..akaingiwa na Roho ya kikatiri kuliko Mtemi na Joshi..walipoingiliwa nazimu huo.
Makala akawa ni mtu katiri wa kutisha..akazipiga hatua kulifuata hema….
kitendo cha Makala kuingiwa na mzimu,,,, hakuna mtu yeyote aliyeweza kuona jambo hilo…..
Wakololo walionekana kufurahia kuutoa Mzimu uliokuwa umeingia kwenye kiwiliwili cha Mtemi wao….walimpongeza sana mkuu wa vijana wa Wakololo…huku wakipiga kelele za shangwe kifurahia ushindi…..Mtemi alizinduka akanyanyuka pale chini..baada ya kupata fahamu!! akainekana kustahajabu kujikuta yupo eneo hilo…wakololo wakamsogelea Mtemi wao….huku wakimpa pole kwa kuongea lugha yao…..ghafla wakamuona Yule mtu aliyetakiwa kuuwawa kwa kunyongwa(Makala)..baada ya kukutwa na Vida(binti wa mtemi)
wakastuka kumuona kavaa nguo za kiaskari zilizofanana na wale maaskari waliowapita kulestuni….wakabaki wakimtazama Makala…
Makala alizipiga hatua mpaka pale walipokuwa wamekusanyika wakololo kumzunguka Mtemi wao…alipofika akasimama na kutazama nyuso zao…ghafla akamvuta kijana mmoja wa kikololo na kumnyang’anya mkuki..akamdunga kwenye koo!!
wakololo wakastuka wakaingiwa na hofu..
wakati wanatahamaki..Makala akamchoma mkuki wa tumboni kijana mwingine wa kikololo..
Mtemi akapaza sauti kwa lugha yao..akimaanisha,,”shamvulia mtu huyu…
vijana wa kikololo wakaanza kumshambulia Makala kwa mishale…lakini mishale hiyo haikumdhuru Makala..
Makala aliendelea kufanya mauwaji ya kikatiri…
kwa mbali alionekana kijana wa kikololo akimfuata Makala kwa nyuma ili amchome mkuki…Makala akageuka na kumchoma mkuki wa Jicho ukatokezea kisogoni..kisha akauinua mkuki huo na kumrusha mkololo huyo mbali zaidi…
wakololo wakamchukua Mtemi na kutimua mbio kuelekea mstuni….baada ya dakika kadhaa hakuonekana hata mkololo mmoja…wote walitokomea mstuni…wakabaki baadhi ya wakololo waliouwawa wakiwa chini…..
kamanda Michael,,, Joshi pamoja na wale maaskari wawili wakatimua mbio kurudi stuni.. baada ya kuona mambo yamekuwa magumu…..
****************
Upande mwingine walionekana Wakololo wakiendelea kutimua mbio wakajikuta wametokezea kwenye kijiji chao…Mtemi alikasirika sana kukuta binti yake(Vida)kauwawa pamoja na mke wake(Subi) akawachukia sana wale maaskari kwa kuhisi,,maaskari ndio wameleta mzimu huo ndani ya Msitu….
kwa sababu..Mtemi alipozinduka na kulata fahamu baada ya mzimu kutoka kwenye kiwiliwili chake…..alimuona Makala akiuwa wakololo,,,na kwa sababu makala alikuwa kavaa nguo za kiaskari…basi Mtemi akajua maaskari watakuwa wanajua kuhusu mzimu huo….
Mtemi akatoa amri kwa vijana wa kikololo waende kuangamiza maaskari wote waliokuwemo ndani ya msitu huo…..vijana wa kikololo wakaandaa zana za kazi…ikiwemo mishale,,,mikuki,,pamoja na silaha nyinginezo za jadi…wakaingia mstuni kuwatafuta maaskari……
VITA KABAMBE…
Wakati huo huo alionekana Kamanda Michael,Joshi pamoja na wale maaskari wawili…
Michael akasema,,”itabidi tufanye jambo ili tuweze kutoka nje ya msitu huu tukiwa hai..
Joshi na wale maaskari wawili walimsikiliza Kamanda Michael kwa makini,,huku wakimtazama usoni….askari mmoja akauliza,,”kamanda sasa tufanye jambo gani? na bunduki zetu hazina risasi hata moja…
Michael akasita kuongea,,akafungua bunduki yake akatazama upande wa risasi..akaona kabakiwa na risasi moja tu….akasema,,”tafuteni miti mirefu migumu..,,muichonge zitengeneze ncha kali,,angalau mpate silaha kwa ajili ya kujihami….wale maaskari wawili wakakubali kutekeleza wazo la kamanda Michael..wakazipiga hatua na kuingia ndani zaidi ya msitu huo kutafuta miti mirefu migumu…..
Sehemu Ya 12
Upande mwingine walionekana wale maaskari tisa wakiwa bado wamejificha kwenye kichaka kikubwa kiasi…walikaa hapo kwa masaa mengi..walipo ona ukimya umetawala wakaamua kutika ndani ya kichaka hicho..wakasonga mbele kutafuta njia ya kutoka ndani ya msitu huo… walipotembea mwendo wa dakika arobaini mfululizo…wakakutana uso kwa uso na Wakololo! kijana mmoja wa jamii hiyo ya wakololo akaweka mshale kwenye upinde akauvuta,,,kabla hajaachia mshale huo vikasikika vishindo vizito!! punde si punde wakamuona Makala anakuja upande wao huku mikono yake ikiwa imetapakaa damu…
wale maaskari tisa wakatimua mbio….na kutokomea mstuni..walikimbia kila mmoja alipita njia yake…..
Wakabaki wakololo wakipambana na Makala walimpiga mishale mingi isiyokuwa na idadi….lakini mishale hiyo haikumdhuru makala..akamkamata kijana mmoja wa kikololo akamnyofoa kichwa na kukirusha mbali….wakololo wakaamua kutimua mbio,baada ya kuona mabo yamekuwa magumu….
*************************
Upande mwingine kule makao makuu alionekana mkuu wa kitengo cha wanyama pori akiamuru ndege tatu za kivita zielekee msitu Ungebo..kisha akatoa amri kuwa wahakikishe wanaangamiza kila kitu kitakachoonekana ndani ya msitu huo…
mkuu wa kitengo hicho..aliamini maaskari wote wamekufa ndani ya msitu huo…kwa sababu leo ni siku ya nne hajapata taarifa wala mawasiliano yoyote kutika kwa maaskari waliokwenda ndani ya msitu huo………ndege gizo za kivita aina ya (chopper) zikaruka angani kuelekea msitu Ungebo..
********************
kule mstuni walionekana wale maaskari wawili wakiwa wanachonga fito ndefu ngumu….ghafla wakololo wakaonekana wakikimbia kuja upande huo…walipowaona maaskari wakawashambulia kwa kuwachoma mikuki mpaka wakafa….
upande mwingine alionekana kamanda Michael akimwambia Joshi..aende kuwatazama wale maaskari wawili waliokwenda kutafuta fito kwa ajili ya kutengeeza silaha mbadala…..Joshi akazipiga hatua kuelekea ule upande walioelekea wale maaskari wawili akastuka kukuta wakiwa chini wameuwawa huku damu nyingi zikiwatoka mwilini!! joshi akatimua mbio kurudi kwa kamanda Michael…akatoa taarifa…kuwa amekuta wale maaskari wameuwawa. Michael akastuka macho yakamtoka baada ya kupokea taaeifa hiyo kutoka kwa Joshi…..
**************************
upande mwingine walionekana maaska wanne waliokimbia njia moja kati ya wale maaskari tisa…walikimbia wakajikuta wamerudi kulekule kwa Makala…..walipomuo makala wakatimua mbio Makala akang’oa mti mkubwa..akaurusha kwa wale maaskari wanne waliokuwa wanaharibu kumkimbia…mti ule uliwaponda na kuwakandamiza,maaskari watatu wakafa papo hapo…na askari mmoja aliyekuwa amekandamizwa mguu na mti huo..alipiga kelele kwa maumivu makali aliyoyapata baada ya kuvunjika miguu yote miwili huku ikiwa bado imekandamizwa na mti huo…..Makala akazioiga hatua kumfuata askari huyo alipomkaribia akampiga teke kali la uso,,kichwa cha askari huyo kikang’oka na kuruka kando!! akafa papohapo…
Makala akazipiga hatua kusonga mbele zaidi…kuelekea ule upande aliokuwepo Kamanda Michael na Joshi……wakati huo huo alionekana Michael na Joshi wakitoka eneo hilo kuelekea ule upande aliokuwepo Makala….ghafla wakakutana uso kwa uso na Makala…..Michael na Joshi wakashtuka!!!
wakati wanatafakari wafanye nini! ikasikika milio ya ndege za kivita zikiwa tayari zimeingia kwenye anga la msitu huo……..
Ndege hizo zikaanza kurusha makombora mfululizo…Ghafla rubani mmoja akahisi kama kaona watu ndani ya msitu huo..akamwambia mwenzake aliyekuwa ameketi kwenye kiti cha pembeni yake,,”nahisi kama nimeona maaskari wenzetu….ebu chukua darubini(Binocolus)tazama kwa makini upande wa chini,,tusije tukawaangamiza maaskari wenzetu,,yawezekana bado wapo hai! yule askari akachukua darubini..akatazama upande wa chini kwa kutumia Darubini hiyo…akastuka kumuona Kamanda Michael akipambana na Makala….wakaamua kufanya mawasiliano na makao makuu…ili watoe taarifa kuwa baadhi ya maaskari wapo hai ndani ya msitu huo!! hivyo zoezi la kufanya mashambulizi kwa kurusha makombora lisitishe..
*************************
Upande mwingine walionekana wakololo wakiendelea kuwawinda maaskari waliokuwemo ndani ya msitu huo…..wakakutana na maaskari watatu..kati ya wale maaskari tisa….wakawauwa kwa kuwalenga na mishale..wakafa papo hapo.
kisha wakololo wakazidi kusonga mbele kutafuta maaskari waliobakia wawaangamize…
**************************
upande mwingine alioneka Kamanda Michael akiendelea kupambana na Makala….
Makala akastahajabu sana kwa nini kamanda Michael anamsumbua mpaka Muda huu hajaweza kumkamata Mikononi mwake!!
wakati huo Joshi alikuwa kando kajificha kwenye kichaka akishuhudia vita kabambe,,baina ya Kamanda Michael na Makala…..Jishi akaingiwa na wazo akajisemea moyoni,,”yanipasa nikimbie. huyu ,,kamanda Michael hawezi kupambana na huyo Mtu!! na bila kutumia akili ya ziada hatuwezi kutoka tukiwa hai ndani ya msitu huu.
Joshi akakurupuka kutoka ndani ya kichaka hicho akatimua mbio…baada ya kukimbia mwendo wa dakika tatu akakutata uso kwa uso na wakololo…
akaingiwa na hofu kubwa..punde si punde ikasikika miripuko ya mabomu ndani ya msitu huo…mabomu hayo yalitoa mlio mkali sana kwa mfululizo..Wakololo wakaingiwa na hofu…tangu wamezaliwa ndani ya msitu huo,,hawajawahi kusikia mlio wa namna hiyo..
wakaamua kutimua mbio wakamuacha Joshi..kumbe ule upande ambao Wakololo wanaelekea,,ndio ule upande ambao yupo Makala anapambana na Kamanda Michael…
**********************
Ulande mwingine kule makao makuu alionekana Mkuu wa kitengo akipokea mawasiliano kutoka kwa rubani mmoja kati ya maruban watatu waliokwenda msitu Ungebo..na ndege tatu za kivita aina ya (chopper)
akaamuru wasitishe kurusha makombora kwenye msitu Ungebo….amri ikatekelezwa wale marubani..wakasitisha kuendelea na mashambulizi…..
******************
kule ndani ya msitu,,Kamanda michael alionekana kuzidiwa nguvu na Makala…..
Michael akaanza kuchoka..kwa sababu alikuwa akimkwepa Makala kwa kutumia akili na nguvu nyingi… ..ghafla Michael akadomdoka chini..huku akionekana kuregea kupita kiasi,,jasho lilikuwa linamtoka mfululizo,,,Makala akazipiga hatua kumfuata michael pale chini alipokuwa amedondoka…..alipomkaribia akanyanyua mguu wake ili ampige teke la uso ang’oe kichwa cha Michael…ghafla wakalolo wakatokezea sehemu hiyo..wakaanza kurusha mishale kumshambulia Makala..Makala akamuacha Michael na kuwafuata Wakololo…
Wakololo walirudi nyuma huku wakiendelea kumshambulia Makala kwa mishale…
*********************
Upande mwingine alionekana Joshi akiendelea kutimua mbio baada ya kunusurika kifo kutoka kwa Wakololo…wakati anakimbia..akaingiwa na roho ya huruma,,akajisemea moyoni,,”kamanda Michael aliokoa maisha yangu…sio vyema kumtelekeza ndani ya msitu huu,,Joshi akaamua kurudi kule alipomtelekeza kamanda Michael!!
alipofika akakuta wakololo wakimshambulia Makala kwa mishale mfulilizo..Wakololo wakaanza kupungukiwa mishale..hatimae wakajikuta kila kijana wa kikololo kashikilia upinde tu ba hata kuwa na mshale mmoja!! walipo ina mambo yamekuwa magumu wakaamua kutimua mbio..na kutokomea mstuni…
wakati huo kamanda Michael alikuwa hoi!! bado kalala pale chini alipodondoka……akanyanyuka kutoka pale chini……….
wakati huo huo Makala akamuona Joshi amejificha nyuma ya mti..
akamfuata,,alipomkaribia akanyanyua akanyanyua mguu ili amkanyage kifuani…Ghafla ikasikika sauti ikisema,,”Muache mtu huyo..kama unauwezo wa kupambana njoo upambane na mimi…
Makala akamtazama Michael kwa hasira kisha akamtazama Joshi…
Makala akainua mguu wake…kabla hajaushusha kifuani mwa Joshi…Michal akachomoa kisu chake kilichotengenezwa kwa madini ya shaba…alichozawadiwa na mkuu wa kitengo…kama pongezi ya askari mtiifu,,,akakirusha kisu hicho,kikaenda moja kwa moja mpaka kwenye mgongoni wa Makala..Punde si punde!!,, ukaonekana moshi ukitokea kwenye ile
sehemu alipodungwa kisu hicho cha shaba..
kumbe ule mzimu haupatani na madini ya shaba..ni mwiko kwa mzimu huo…Makala akaanza kupiga kelele..ghafla moshi ukazidi kuongezeka…kumbe moshi huo ndio mzimu ulikuwa unajitoa kwenye miwiliwili cha Makala..ghafla moshi huo ukatoweka kimiujiza na ikawa ndio mwisho wa mzimu huo…Makala akaonekana kujishangaa!!! huku akiutazama mwili wake….akaangaza angaza macho yake..akamuona Michael akauliza,,”kwani wewe ni nani??
Michael akashangaa kumsikia makala akimuuliza swali hilo!! Joshi akadakia na kusema,,”huyu aliingiliwa na mzimu ule ulioniingilia mimi…
hata mimi pia niliushangaa mwili wangu baafa ya mzimu huo kutoka ndani ya mwili wangu…lakini hawezi kukumbuka chochote….kwa sababu mawazo na akili haikuwa yake…alikuwa anaongozwa na mzimu huo……punde si punde wakaonekana wale maaskari watano waliobaki hai kati ya wale maaskari kumi…waliokuja mstuni humo kwa awamu ya pili..Walifurahi kumuona kamanda Michael…
Michael akasema tusipoteze muda..tuondokeni…wakaanza safari ya kutoka ndani ya msitu huo….walitembea mwendo wa masaa matatu mfululizo…
kwa mbali wakasikia mngurumo wa gari….wakatimua mbio kuufuata mngurumi huo..wakafanikiwa kuliona gari la jeshi lao…wakapiga mayowe ili wale maaskari waliokuwemo ndani ya gari hilo wasikie pia waweze kuwaona…..
kwa sababu walikuwa wameanza kutoka nje ya msitu huo…waliweza kuonekana kwa urahisi..kutokana miti ya eneo hilo haikuwa mingi sana…gari hilo likawafuata na kuwachukua…Wale maaskari watano,,kamanda Michael pamoja na Joshi…..wakaianza safari ya kutoka nje kavisa ya msitu huo na kuelekea makao makuu..
*************************
Baada ya mwendo wa masaa kadhaa…wakaanza kuingia mjini…Joshi na Makala wakaomba washushwe hapo mjini…wakawashusha….kisha kamanda Michael pamoja na wale maaskari wengine wakaendelea na safari ya kuelekea makao makuu..
Makala akaamua kukodi pikipiki impeleke nyumbani kwake….na baada ya nusu saa alifika nyumbani salama…NOREGA(mke wa Makala) alifurahi kumuona mumewe….kisha makala akaingia chumbani akafungua kabati akatoa noti ya shilingi elfu kumi..akasema,,”kaampe dereva bodabida pesa hii…Norega akatoja nje akamlipa dereva bodaboda..na kueudi ndani huku akitabasamu akauliza,,”nguo zako ziko wapi?? mbona umevaa nguo za kiaskari??
Makala akamsimulia yaliowapata huko mstuni..Norega akasikitika sana..lakini akamshukuru Mungu kwa kumrudisha mumewe nyumbani akiwa hai…tangu siku hiyo makala akaacha kazi ya utafiti akawa mfanya biashara….
*******************
Asubuhi palipokucha,,,alionekana Joshi akiwa kule nyumbani kwake aliamua kuhama mji…akachukua vitu vyake vya thamani na kuviweka ndani ya begi…alipomaliza akatoka nje ya nyumba yake akafunga mlango…akaondoka kuelekea ubungo…akapanda basi kuelekea Mbeya….akaishi huko pia akaamua kuwa mkulima wa mazao ya chakula..
******************
kule makao makuu kamanda Michael akapandishwa cheo….kutokana na kufanya kazi kubwa kwa umakini na ushupavu…..
___MWISHO ___

