KENGELE YA KIFO
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 4
alipomaliza alichukua toroli dogo akaliingiza kwenye mlango wa njia ya chini kwa chini…akachukua nyama na kuiweka kwenue toroli,,akaianza safari ya kuelekea kwenye mgahawa wake kwa kupitia njia hiyo ya siri..
upande mwingine alionekana mtu mmoja akiwa mstuni…….ndani ya gari lake..mtu huyo alifahamika kwa jina la MUKI…anajishuggurisha na fundi seremala..
siku ya lei alikwenda kwenye msitu huo kwa lengo la kukata miti iliyokomaa kwa ajili ya kuchana mbao..ili zimsaidie katika kazi zake za useremala.
akashuka kutoka ndani ya gari akachukua(CheanSaw) msumeno wa kutumia umeme..ndani yake kuna betri inayochajiwa katika umeme na kuhifadhi umeme kwa muda wa masaa sita(6) mfululizo huku ukiwa unafanya kazi ya kukata magogo makubwa…. kabla hahaanza kukata miti ghafla likatanda wingu kubwa na upepo mkali mvua ikaanza kunyesha….ilinyesha mvua kubwa sana akaamua kuingia ndani ya gari lake akaliwasha na kuondoka zake ili akapange siku nyingine aje kuchana mbao ……akiwa njiani ndani ya msitu huo gari lake lilikwama kwenye udongo ulietifutifu,,,akakanyaga mafuta kwa nguvu magurudumu yakazunguka kwa kasi huku yakichimba aridhi..mpaka gari ikatitia…..Muki akakasirika sana…akawaza jinsi ya kufanya ili aweze kulitoa gari lake….akazima gari kutokana na mvua kubwa na maji kuwa mengi pamoja na uzito wa gari likaanza kutitia kuelekea chini ya aridhi .
kumbe hiyo sehemu lilipokua limekwama gari la Muki na kutitia ,,ndio sehemu ambapo ile njia ya siri inayopita chini kwa chini aliyoitengeneza mzee sule kwa ajili ya kupitisha nyama za biadamu kwa ajili ya kuzipeleka kwenye mgahawa wake.
mvua iliendelea kunyesha na maji yakawa mengi zaidi udongo ulilainika kutokana na maji hayo ukameguka na gari la Muki likatumbukia chini ya aridhi na kudondoka ndani kabisa kwenye ile njia ya chini kwa chini ya aridhi, mzee Sule alisikia kishindo cha gari hilo kudondoka, akastuka aliogopa sana akalitelekeza toroli lililokua na nyama za binadamu akatimua mbio ili kuokoa maisha yake…..alihisi ni kifusi kimedondoka,,akapata hofu ya kufunikwa na kifusi…..alikimbia bila kugeuka mpaka akatokezea kwenye mlango wa kuingilia ndani ya nyumba yake…mlango huo ulikuwa kwenye sakafu ya chumbani kwake……
Muki alionekana kustahajabu sana..baada ya gari lake kutumbukia chini ya aridhi ba yeye akiwemo ndani yake…..akashangaa sana kuona kunanjia inayopita chini ya aridhi….akaamua kufungua mlango akachukua tochi,,na kisu akatoka ndani ya gari…akaanza kuifatilia njia hiyo ili aone inatokezea wapi……akatembea kwa mwendo dakika kumi..Muki alizipiga huku macho yake yakitazama kwa tahadhari kubwa sana…
huku akimulikamulika pande zote kwa kutumia tochi yake…..kwa mbali kama hatua kumi hivi akaona kuna kitu..alipomulika na kutazama kwa umakini akagundua kuwa ni toroli….akazipiga hatua kulisogelea toroli hilo..akamulika ili aone toroli hilo limebeba nini ndani yake…..akaona kuna nyama..akastuka..akatazama kwa makini akaona makalio ya vinadamu yamekatwakatwa vipande vipande…akaona maini na moyo pamoja na utumbo..akagundua kuwa ni binadamu waliouwawa na kukatwakatwa vipande vipande…akajiuliza,,”mbona hakuna viungo vingine kama miguu mikono na kichwa…inamaana kuna watu wanakula nyama za binadamu!!!! ni nani huyu aliyefanya mauwaji haya??
Muki alikuwa jasiri sana, aliwahi kuwa mwanajeshi akaacha kazi hiyo ya uwanajeshi kutokana aliugua ugonjwa wa akili……..mkuu wa jeshi akaamuru Muki asimamishwe kazi akatibiwe,,Baada ya kutibiwa Muki alipona kabisa akili zake zikarudi katika hali ya kawaida(TIMAMU) akaamua kuachana na kazi ya jeshi akawa mjasiliamali wa kutengeneza vitanda,,makabati,,meza na vitu vingine vinavyotengenezwa kwa mbao..Muki hakuogopa akaendelea kuifuata njia ile…
*****************
Upande mwingine kule kwenye mgahawa..walionekana watu wakiingia na kutoka…walipishana utadhani sokoni..Mgahawa wa mzee Sule ulizidi kupata umaarufu……kutokana watu wengi waliowahi kula kwenye mgahawa huo waliusifia sana…
kwa mbali alionekana mwanamke mmoja akitembea hatua za kikakamavu…mwanamke huyo alikuwa kavaa miwani yenye kioo cheusi huku nywele zake zimeanguka mgongoni…akaingia ndani ya mgahawa wa Mzee Sule.
kutokana na watu kuwa wengi kuliko viti vya kukalia…Mwanamke hiyo alisimama….
kwa mbali akaonekana yule kijana mkubwa wa mzee Sule akimfuata mwanamke huyo..ili kumuuliza anahitaji huduma gani? alipomkaribia akamuuliza…yule mwanamke akasema,,”niletee sambusa tatu na supu…weka nyama yenye mafutamafuta…..yule kijana akazipiga hatua za haraka haraka akaingia jikoni…akaandaa supu pamoja na sambusa tatu…akapeleka kwa mwanamke yule…..akaweka kwenye meza iliyokuwa imejaa vyakula juu yake…
yule mwanamke akachukua sambusa moja akaitafuna,,,akachota supu kwa kijiko akasita kuipeleka mdomoni…alipoitazama kwa makini..aliona kucha ya binadamu ikielea kwenye mchuzi…akaacha kula..akamuita yule kijana akatoa noti ya shilingi elfu kumi..yule kijana aliipokea pesa hiyo akarudi jikoni kuchukua chenji ili amrudishie mwanamke yule……
alipokuwa anarudi akamuona yule mwanamke akizipiga hatua kuelekea upande wa nje…..akamuita lakini hakugeuka..akaamua kumfuata kwa nyuma….alipotoka nje hakumuona mwanamke yule…akaangaza angaza macho lakini hakufanikiwa kumuona,,akabaki na mshangao…akajiuliza inamaana kayayuka au!!!? mbona hakuna hata kichochoro,,,atakuwa kapitia wapi….
hakujali akaamua kurudi ndani ya mgahawa akapitiliza moja kwa moja mpaka jikoni….akaendelea kuwahudumia wateja wengine waliokuwa wanaingia….
********************
upande mwingine alionekana Muki akiwa chini ya aridhi,,kwenye ile njia inayopita chini kwa chini..
akaona kunamlango wakutokea ndani ya njia hiyo ya siri…akausogelea,,,alipojaribu kuusukuma,,haukufunguka ulikuwa umefungwa kwa ndani…akaanza kuupiga kwa mateke ili uvunjike..lakini akashindwa….mzee Sule aliutengeneza mlango huo kwa mbao za mti wa MPINGO..akaweka komeo kubwa la chuma…. mlango huo ulikuwa umezungukwa na zege iliyochanganywa kwa simenti kali…haikuwa rahisi kuuvunja…..Muki akaamua kurudi kule lilipokuwepo gari lake
Mzee Sule alisikia kama kuna mtu anagonga ule mlango wake wa siri…akastuka akafunua chini ya kitanda,,akatoa upanga…akatoka nje haraka ili aende akatazame ni wapi mtu huyo ameingilia, amuuwe kabla hajatoa siri…
*****************
upande mwingine kule kwenye mgahawa Nyama ikaanza kupungua huku wateja wakizidi kuingia..hatimae supu ikaisha….Mke wa mzee sule akachanganyikiwa…akajiuliza mpaka muda huu mumewe Mzee Sule hajaleta nyama kulikoni??
akaamua kumtuma kijana wake mkubwa apitie kwenye mlango wa njia ya siri..awahi nyumbani angalau akalete nyama ndoo moja,,,na utumbo,maini,bandama pamoja na ubongo aweke kwenye ndoo nyingine…..
Yuele kijana akachukua tochi akafungua mlango na kuianza safari ya kwenda nyumbani.kwa kupitia njia hiyo ya siri….kwa mbali aliona kama kuna kitu kimeziba njia..akasita kuendelea kukimbia..akaanza kutembea kwa hatua za tahadhari….alipokaribia akagundua kuwa ni gari limetumbukia..na limeziba njia..hivyo hawezi kutokezea upande wa pili…yule kijana akaamua kuvuta mlango wa gari ukafunguka,,akaingia ndani ya gari akafungua mlango wa upande wa pili ili atoke aendelee na safari yake ya kufata nyama kule nyumbani kwao…kabla hajatoka ndani ya gari..aliona kuna mwanga wa tochi ukilifuata gari..yule kijana hakujali alijua ni Mzee Sule…akatoka ndani ya gari na kuanza kuzipiga hatua…pia Muki aliona mwanfa wa tochi ukitokea kule lilipokuwa gari lake,,akastuka akaamua kuizima tochi yake…
akalete nyama ndoo moja,,,na utumbo,maini,bandama pamoja na ubongo aweke kwenye ndoo nyingine…..
Yuele kijana akachukua tochi akafungua mlango na kuianza safari ya kwenda nyumbani.kwa kupitia njia hiyo ya siri….kwa mbali aliona kama kuna kitu kimeziba njia..akasita kuendelea kukimbia..akaanza kutembea kwa hatua za tahadhari….alipokaribia akagundua kuwa ni gari limetumbukia..na limeziba njia..hivyo hawezi kutokezea upande wa pili…yule kijana akaamua kuvuta mlango wa gari ukafunguka,,akaingia ndani ya gari akafungua mlango wa upande wa pili ili atoke aendelee na safari yake ya kufata nyama kule nyumbani kwao…kabla hajatoka ndani ya gari..aliona kuna mwanga wa tochi ukilifuata gari..yule kijana hakujali alijua ni Mzee Sule…akatoka ndani ya gari na kuanza kuzipiga hatua…pia Muki aliona mwanfa wa tochi ukitokea kule lilipokuwa gari lake,,akastuka akaamua kuizima tochi yake..
Yule kijana wa mzee Sule alipo ona ule mwanga wa tochi hauonekani tena…akaingiwa na hofu..akapaza sauti kumuita baba yake,,”BABA..
Muki akauliza kwa sauti ya ukakamavu,”WEWE NI NANI??
yule kijana aligundua hiyo sio sauti ya baba yake..akaamua kutimua mbio akaingia ndani ya gari akafungua mlango wa upande wa pili akatoka na kuendelea kutimua mbio kurudi kwenye mgahawa..
******************
Upande mwingine alionekana mzee Sule akizipiga hatua za haraka haraka..kuifuata ile njia ya siri akiwa upande wa juu ya aridhi…alitembea mwendo wa dakika kumi..huku macho yake yakitazama kwa umakini akastuka,,kwa mbali akaona kuna gari limetumbukia chini ya aridhi huku likionekana kiasi kutokeza upande wa juu ya aridhi..amzee Sule akatimua mbio kuelekea kwenye gari hilo…
wakati huohuo..kule chini ya aridhi alionekana Muki akizipiga hatua za tahadhari huku kashikilia kisu chake,,tayari kwa lolote litakalotokea,,alipolikaribia gari lake akawasha tochi akamulika huku akitazama kwa umakini…akagundua kuwa hakuna mtu ndani ya gari lake…akaingia ndani ya gari..alipomulika kwenye kioo cha dirisha akaona bado njia hiyo inaendelea..akafungua upande wa pili akatoka na kuanza kuifuata njia hiyo….
**************
kule juu ya aridhi,alionekana mzee Sule akilisogelea gari la Muki akavunja kioo cha nyuma akaingia ndani ya gari. …akafungua mlango akatoka ndani ya gari…nia na lengo lake amuwahi yule mtu kule aliposikia mlango unagongwa…akawasha tochi akaanza kukimbia kuelekea kwenye mlango wa kutokezea ndani ya nyumba yake.
upande mwingine alionekana Muki akiendelea kusonga mbele zaidi..kuelekea ule upande ambao ulikuwepi mlango wa kutokezea kwenye mgahawa…
Macho ya muki yalikuwa makini kutazama..alizipiga hatua kwa tahadhari kubwa…
huku akimulika kwa tochi…kwa mbali akaona kama kunamlango…akazipiga hatua za haraka haraka…alipoukaribia…akazima tochi..akachungulia kwenye upenyo wa mlango huo uliotengenezwa kwa mbao…alipotazama kwa makini,, akaona kunawatu wanapika…akaangaza angaza macho..akaona kiganja kimoja cha binadamu kikiwa kimekatwa….akastuka..akaona kunanyama imetundikwa….nyama hiyo ilikuwa imekatwa kwenye sehemu ya paja la binadamu….Muki akasikitika sana akajisemea moyoni..”inamaana…humo ndani wanakula nyama za watu….hakujua kuwa nyama hizo za binadamu zilikuwa zikipikwa kwenye mgahawa….akaamua kurudi kule lilipokuwepo gari lake…
*******************
ule upande mwingine alionekana mzee Sule akirudi baada ya kutokumkuta yule mtu aliyekuwa anagonga mlango wake wa siri…akazipiga hatua kuelekea kwenye lile gari lililokuwa limetumbukia kwenye hiyo njia yake ya siri..inayopita chini kwa chini….
wakati huo huo,, alionekana Muki akiingia ndani ya gari akapanda kwenye viti akatoka upande wa nje.kwa kupitia kwenye kile kioo kilichovunjwa na mzee Sule….akazipiga hatua za harakaharaka..kuifua njia hiyo inayopita chini kwa chini ya aridhi..yeye akiwa upande wa juu ya aridhi…..alitembea umbali mrefu kidogo kwa muda wa dakika kumi natano…akaona kuna nyumba imejitenga porini….akaamua kuifuata nyumba hiyo..alipofika..akapiga hodi kwenye mlango..lakini hakuona dalili yoyote ya mtu kufungua mlango…akajaribu kusukuma mlango ukafunguka..akaingia ndani ya nyumba hiyo…akakuta kuna radio ndogo ikipiga mziki…akapaza sauti..”HIDI HUMU NDANI!!….
hakusikia mtu akimjibu..akajisemea moyoni….inaonekana mwenye nyumba hayupo mbali,,kwa sabavu radio ilikuwa ikipiga mziki..akaamua kuzipiga hatua kutoka nje..ghafla akaona kuna damu kwenye sakafu,,damu hiyo ilikuwa ikitokea ndani ya chumba ikitiririka kupitia chini ya mlango…akastuka.akazipiga hatua kadhaa akafungua mlango wa chumba hicho….
akastuka kukuta miguu sita na mikono sita ya binadamu ikiwa imekatwa…imekusanywa sehemu moja..alipotazama juu ya meza aliona kuna vichwa vitatu vikiwa vimepasuliwa katikati..na kutolewa ubongo…kumbukumbu ikamjia akakumbuka..lile toroli aliloliona kule kwenye njia inayopita chini kwa chini ya aridhi…lilikuwa na nyama ya binadamu ikiwa imekatwakatwa….akagundua kuwa mtu anayeishi ndani ya nyumba hiyo ndiye aliyeweka toroli lile..lililojaa nyama za binadamu. ..
**************
upande mwingine..kule chini ya aridhi..alionekana mzee Sule akifungua mlango wa gari la muki akaingia ndani akafungua mlango wa upande wa pili..akatoka na kuelekea kule ulipokuwepo mgahawa…alipoukaribia mlango hakuona mtu yoyote…akajisemea moyoni,”lazima nimnase mtu huyu..Lah! si hivyo.. titakuwa matatani…kwa sababu mtu huyu ameona lile toroli..na ameshajua kuhusu hii njia yangu siri….ngoja nirudi nyumbani nikachukue gari nimtafute..nina imani bado hajatoka nje ya msitu huu.
mzee Sule akakasirika sana..akarudi kule lilipokuwepo gari la Muki.akaingia ndani ya gari akafanda juu ya viti..akatoka nje kwa kupitia kwenye kioo alicho kivuja……akazipiga hatua za haraka haraka kuelekea nyumbani kwake……
*************
wakati huohuo alionekana Muki bado yumo ndani ya nyumba ya mzee Sule…akiendelea kuchunguza,,vyumba vyote vilivyomo ndani ya nyumba hiyo….akainfia kwenye chumba kingine..akakuta kuna pesa nyingi sana….pesa hizi alizihifadhi mzee Sule ndani ya chumba hicho…kutokana na mauzo ya kila siku kule kwenye mgahawa wake…..Muki alistahajabu sana alijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu…..akatoka nje ya chumba hicho..akaingia kwenye chumba kingine….akakuta kuna mashine…ya kusagia nyama……pia kuna diaba kubwa likiwa limejaa nyama iliyosagwa…Muki akazidi kustahajabu…..akajiuliza nyama hiyo iliyosagwa bila shaka pia itakuwa ni ya binadamu.
akaisogelea mashine hiyo akawasha swichi..lakini haikuwaka akaamua kutoka ndani ya chumba hicho bila kuizima ile swichi……akaanza kuutafuta ule mlango unaitokezea kwenye ile njia ya chini kwa chini ya aridhi….
********************
upande mwingine alionekana yule mwanamke aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha kule kwenye mgahawa wa mzee Sule… akiingia ndani ya Taxii…kisha akamwambia Dereva ampeleke….KIBAHA..dereva akawasha gari na safari ya kwenda Kibaha ikaanza…
****************
upande mwingine alionekana mzee Sule akizidi kusonga..alipoikaribia nyumba yake..akasikia mashine yake ya kusagia nyama ikiwaka na kuanza kunguruma….akastuka akaanza kutimua mbio kuufuata mlango wa kuingilia ndani ya nyumba ili amuwahi huyo mtu aliyewasha mashine yake kabla hajatoka nje…..kumbe mashine hiyo ikiwashwa inachukuwa muda kuanza kuzungusha injini na kuanza kufanya kazi.
tangu ule muda ambao Muki aliiwasha ile swichi,,sasa hivi ndio mashine imewaka..
wakati huohuo alionekana Muki akiwa ndani ya nyumba ya mzee Sule…akastuka kusikia mngurumo wa mashine hiyo,!!akahisi kuna mtu huenda kaingia na kuiwasha mashine hiyo…
Muki akachomoa kisu akajificha chini ya uvungu wa kitanda kwenye chumba cha mzee Sule..
kule nje ya nyumba hiyo akaonekana mzee Sule akiingia ndani ya nyumba huku kashikilia upanga..tayari kwa kumuangamiza mtu aliyeingia ndani ya nyumba yake.
Akafunga mlango akaanza kuzipiga hatua kuelekea kwenye kile chumba kilichokuwa na mashine ya kusagia nyama…akaangaza angaza macho pande zote lakini hakuina mtu…akatoka akaingia chumbani kwake…….akasita kutafuta akatoka nje haraka akaingia ndani ya gari lake…..akamtafute huyo mtu aliyejaribu kucheza kwenye Himaya yake….akajisemea moyoni hatakuwa hajafika mbali….
kumbe kamuacha Muki kule ndani…chini ya uvungu wa kitanda, kwenye chumba chake cha kulala……
Sehemu Ya 5
kule ndani ya nyumba ya mzee Sule,, alionekana Muki akiwa bado yumo chini ya uvungu wa kitanda..akatoka uvunguni haraka…akachungulia upande wa nje kwa kupitia dirishani….akaona gari la Mzee Sule likitokomea mstuni….akazipiga hatua kutoka nje…..akaparamia sanduku dogo la mbao..likadondoka na kufunguka….alipolitazama akaona kuna picha Tatu…pamoja na nyaraka za siri za Mzee Sule.. akazichukua zile picha…akazitazama….picha hizo zilionekana za kizamani…akazirudisha..akachukua zile nyaraka akazisoma…..macho yakamtoka…
nyaraka hizo zilieleza hivi,,,
Miaka hamsini iliyopita…..wakati huo mzee Sule alikuwa na umri wa miaka kumi na moja… alianza kupata na hali ya kutamani kula nyama mbichi tena alipendelea zaidi nyama ya binadamu….hali hiyo iligundulika baada ya mzee Sule kudondoka wakati anaendesha baiskeli…akapata jeraha la mchubuko kwenye mkoni wake wa kushoto…..baada ta wiki mbili kupita,,wazazi wake wakaanza kuingiwa na wasiwasi kwa nini kidonda cha Sule hakiponi,,wala hakuna dalili yoyote ya kidonda hicho kukauka…..kila kukicha kinaonekana kuwa vilevile kibichi,,alafu kinazidi kuongezeka uchimbika kwenda ndani zaidi……..
ikafika kipindi Sule akaanza kuwa na tatizo la kupungukiwa damu…akawa anapelekwa hospitali mara kwa mara,,kwa ajili ya kuongezewa damu…madaktari walistahajabu sana…kwa sababu sio jambo la kawaida kwa binadamu kuongezewa damu kila baada ya wiki moja…….kila wakikifunga kindo cha Sule kwa bandeji…haichukui muda..wanakuta Sule kaitoa bandeji hiyo…na kidonda kuonekana kuwa kibichi…ikabidi wazazi wake watafute njia mbadala,,ya kumsaidia mtoto wao Sule……
kumbe Sule alikuwa anaifyonza damu yake kwa kupitia kidonda hicho….wazazi wake hawakulitambua hilo…kwa sababu Sule alikuwa hafanyi kitendo hicho mbele yao…..
hali ya kidonda cha Sule ilizidi kutisha kadri wiki zilivyozidi kusonga…..
siku moja baba Sule..alishauriwa na rafiki yake kuwa ampeleke Sule NIGERIA kwa mganga matata aitwae OBINA…baba Sule aliandaa hati mbili za kusafiria….yake pamoja na Sule…akaongozana na Rafiki yake…huyo aliyempa ushauri huo…..
baada ya siku kadhaa safari ikawadia…wakapanda ndege kuelekea NIGERIA.
wakafika salama…wakaelekea mpaka kwenye msitu ISAKABA alipokuwa anapatikana Mganga matata OBINA…walipofika baba Sule akaeleza tatizo la Sule kupungukiwa damu kila wiki…na kidonda hakiponi..kadri siku zilivyozidi kusongo..ndivyo kiliongezeka ukubwa utadhani kaumia muda huohuo……hata madaktari walipomfanyia vipimo haikugundulika tatizo ni nini…linalosababisha Sule kupungukiwa damu kila wiki….
OBINA akasema “tiba ya Sule ni kubwa sana,,,kuna masharti ya kuyafuata…na Tiba hiyo itachukua muda wa wiki tatu…Sule atapona…..Mganga OBINA aliongea maneno hayo huku akipiga TUNGURI zake za kichawi….akasita akabaki kimya kwa sekende kadhaa,,kisha akasema…”mtoto wako anasumbuliwa na mzimu wa JIGO..mzimu huo unanyonya damu ya mwanao kwa kupitia,,Sule mwenyewe….baba sule akastuka..kwa sababu JIGO ni jina la UKOO wake…jina hilo ni la muazilishi wa ukoo ambaye ni babu wa mababu katika ukoo wa baba Sule…..
mganga OBINA akasema,,”ili mzimu huu usiendelee kumsumbua mtoto wako…inabidi Sule amuuwe binti wa umri kama wake..ndani ya siku tatu………..na baada ya wiki tatu kupita,,,,, mzimu huo utaacha kumuandama Sule…pia baada ya miaka hamsini(50) kupita…binti huyo atafufuka akiwa katika umbile la mwanamke mwingine…huko kwenye nchi yenu….na atakuwa mtumwa wa Sule…..sharti sule asithubutu kumkasirisha binti huyo……..Mganga OBINA akamnywesha dawa Sule…..dawa hiyo ni maalumu ya kumpa Sule ujasiri wa kufanya mauwaji ya binti wa umri kama wake….
*************************
Rafiki yake baba sule akawaongiza mpaka kwa kaka yake aliyekuwa anaishi hukohuko NIGERIA
wakaishi hapo mpaka Sule atakapo maliza kutibiwa….ilipofika majira ya usiku…Sule aliamka bila yeye kujitambua akafungua mlango na kutoka nje..akazipiga hatua za kikakamavu mpaka kwenye nyumba ya jirani…..akabofya kengere…..iliyokuwa ukutani kando ya mlango
ndani ya nyumba hiyo alikuwema…mama moja mgonjwa aliyekuwa akiishi na binti yake aitwae TINA…
Tina alisikia mlio wa kengere..akastahajabu…ni nani anayebofya kengere hiyo usiku kama huo…akanyanyuka kitandani..akaenda sebuleni..alipofungua mlango….Sule akamkamata na kumkaba shingo….Tina akakosa pumzi…akatapatapa mpaka akafa….Sule akazipiga hatua na kurudi ndani ya nyumba akalala……
Baada ya siku tatu kupita….Ile hali ya Sule kunyonya damu yake ikatoweka…akaanza kuhisi maumivu kwenye kile kidonda….
na baada ya mwezi mmoja kupita….tiba ya Sule ilikamilika mganga Obina akasema,,”sasa mnaweza kurudi nchini kwenu…..
*****************
Muki akastuka baada ya kuisoma stori ya mzee Sule iliyokuwa imeandikwa kwenye nyaraka hizo za siri..kwa mkono wa mzee Sule mwenyewe…. Muki akarudisha haraka nyaraka hizo…
akazipiga hatua za harakaharaka kutoka upande wa nje…kabla hajatoka akasikia mngurumo wa gari likija kwenye nyumba hiyo……alipochungulia akaona ni gari la mzee Sule………akiliendesha kwa kasi..
akatoka haraka ndani ya chumba hicho akakimbia sebuleni…na kujificha ndani ya kabati kubwa lililo na vitu vichache ndani yake….
*********************
upande mwingine alionekana yule mwanamke aliyekwenda Kibaha…mwanamke huyo alikuwa akimtafuta mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la
MBEGA………mzee huyo ndiye yule aliyemshauri baba sule miaka hamsini (50)iliyopita..ampeleke Sule kwa mganga OBINA kutibiwa huko Nigerea….
mwanamke huyo akazipiga hatua mpaka kwenye duka lililokuwa linauza vinywaji baridi..akanunua maji ya chupa..akaketi kando ya duka hilo…akiwa ameketi…kunatukio akawa analiona katika fikra zake likizunguka ndani ya ubongo wake….akamuona mzee Mbega,,kwenye frikra hizo,,pia akamuona Sule ambae kwa sasa anaumri wa miaka sitini na moja(61)…..akakumbuka siku ile Sule alipobofya kengere ya mlango wa nyumba yao na kumkaba shingo mpaka akafa,,,akakumbuka lile tukio aliloliina hivi karibuni la mume wake Domy akiwa amelala nyuma ya gari la Mzee Sule, huku ametapakaa damu mwili mzima baada ya kugongwa na gari la mzee Sule…..pia katika fikra hizo hizo akaona mtaa na nyumba anayoishi..mzee mbega…
kumbe mwanamke huyo ni Tina,,kwa sasa yupo katika umbile lingine la mwanamke tofauti na muonekano wa Tina wa mwanzo…..alibadirika pasipo yeye kujijua,,baada ya kupata mstuko,,alipomuona mumewe kafa na kuingizwa ndani ya gari la mzee Sule….likasirika sana…akatoweka kimiujiza….akarudi kivingine katika umbile la mwanamke mwingine…sasa hivi hii ndio sura na umbile halisi la Tina yule aliyeuwawa miaka hamsini(50) iliyopita,,,
Tina akanyanyuka kutoka pale alipokuwa ameketi,,akazipiga hatua kuelekea ule mtaa anaoishi mzee Mbega bila kujitambua….alipofika kwenye nyumba ya Mzee mbega akastuka,,,akajiuliza,,”hii nyumba kama nimeshawahi kuiona mahala fulani,,lakini sikumbuki ni wapi…akawa anashangaa pasipo kujielewa….akamua kuufuata mlango wa nyumba hiyo akagonga hodi….ikasikika sauti ya kizee ikisema,,”karibu,, ingia mlango upo wazi….Tina akafungua mlango na kuingia ndani….Mzee Mbega akastuka sana,,kumuona mwanamke huyo,,,akajaribu kuvuta akamkumbuka,,,kuwa huyo ni yule binti,,aliyeuwawa miaka hamsini iliyopita….kwa sababu sura ndio ile ile,,,ya yule binti aliyekutwa kauwawa kwa kunyongwa shingo…jirani na nyumba ya kaka yake aliyekuwa anaishi kule Nigeria,ambaye kwa sasa pia ni marehemu….
Tina akaketi kwenye kiti…..akauliza,”Samahani wewe ni nani??
yule mzee akabaki kimya kwa sekunde kadhaa akajibu mimi naitwa Mbega…nikusaidie nini binti??
Tina akabaki kimya kisha akasema,,”kho Aaam….ee..hata sijui nataka nini,,pia sijui hapa nimefikajefikaje??? mzee Mbega akastuka akajisemea moyoni,”bila shaka binti huyu bado hajajitambua yeye ni nani…..akasema,,”Tina…
Tina akastuka..akakumbuka alishawahi kuitwa jina hilo…..lakini hakumbuki ni wapi….akauliza,,”wewe umejuaje jina hilo? mzee Mbega akazidi kustahajabu,,akajisemea moyoni….inamaana Sule bado yupo hai?? na atakuwa wapi kwa muda huu….kwa sababu yule mganga Obina alisema baada ya miaka hamsini kupita huyo binti atafufuka huko nchini kwenu….mzee Mbega akastuka akasema,,”nisubiri nakuja,,akazipiga hatua za kizee akaingia chumbani kwake…..alipofika chumbani kwakeaka,,akajiuliza,,”kama amefufuka basi itakuwa balaa,,,akakumbuka maneno ya mganga Obina kuwa…mwanamke huyo akifufuka atakuwa mtumwa wa sule….pia akakumbuka….jinsi ya kumdhibiti Mzimu aliyeingia katika kiwiliwili na kuonekana ni binadamu wa kawaida…ni kumchoma na kipande cha mbao ya mti wa MKARATUSI….akaamua kuchukua kipande hicho cha mbao akakiweka kwenye mfuko wa suruali yake,,ili Tina asikione,,,,mzee Mbega aliamua kufanya hivyo ili kuikoa maisha ya wengine…kwa sababu mwanamke huyo hakufufuliwa kwa nia nziri akaona ni vyema akamuuwe ili arudi kwenye kifo…..mzee Mbega akazipiga hatua kurudi sebuleni..kule alipokuwepo Tina.
************************
upande mwingine kule nyumbani kwa mzee Sule alionekana,,akishuka kutoka ndani ya gari,,akaweka mitego,,ya miti iliyochongoka,,ili kama kunamtu atakanyaga eneo la nyumbani kwake kuanzia sasa hivi..basi atauwawa kwa kuchomwa na mitego hiyo hatari..alipomaliza kutega mitego hiyo,akazipiga hatua,,kikakamavu
na kuingia ndani ya nyumba yake,,,akapitiliza mpaka chumbani kwake huku ameshikilia upanga….
akauweka chini akachukua shoka kubwa.
akatoka chumbani….akaanza kukagua vyumba vyote….ili ahakikishe kama vitu vyake vipo sawa…
akatoka upande wa vyumbani akaelekea sebuleni..
**********************
upande mwingine kule nyumbani kwa mzee Sule alionekana,,akishuka kutoka ndani ya gari,,akaweka mitego,,ya miti iliyochongoka,,ili kama kunamtu atakanyaga eneo la nyumbani kwake kuanzia sasa hivi..basi atauwawa kwa kuchomwa na mitego hiyo hatari..alipomaliza kutega mitego hiyo,akazipiga hatua,,kikakamavu
na kuingia ndani ya nyumba yake,,,akapitiliza mpaka chumbani kwake huku ameshikilia upanga….
akauweka chini akachukua shoka kubwa.
akatoka chumbani….akaanza kukagua vyumba vyote….ili ahakikishe kama vitu vyake vipo sawa…
akatoka upande wa vyumbani akaelekea sebuleni..
Upande mwingine kule kwenye mgahawa watu walizidi kuingia….kwa ajili ya kujipatia chakula na supu matata…wakaanza kulalamika kuwa huduma inacheleweshwa……
mke wa mzee Sule hakuwa na namna..kwa sababu nyama ilikuwa imekwisha…hata supu ilikuwa imekwisha……
kwenye sufulia la kupikia Supu….ilibaki kwa ajili ya familia ya mzee Sule…masikio,,pua,na viganja vya mikono ya binadamu…..ghafla yule kijana mkubwa,,ambaye ni mtoto wa mzee Sule akasema.,,”mama ninawasiwasi,,kunamtu ameingia kwenye njia ya siri..anayoitumia baba kuleta nyama huku jikoni…tunaweza kukamatwa muda wowote…ni vyema tukakimbia kwa usalama wa maisha yetu…kabla hajamaliza kuongea….
mke wa mzee Sule akadungua mlango wa nyuma wa kutokea nje kabisa…wakatimua mbio kuelekea kule mstuni,,ilipokuwepo nyumba yao….baada ya dakika arobaini(40)kupita walianza kuikaribia nyumba yao…walipoanza kukanya ardi ya mazingira ya nyumba hiyo..ghafla yule kijana mkubwa,,,pasipokujua akakanyaga ule mtego uliotegwa na mzee Sule ambaye ni baba yake
mara ghafla ile miti iliyochongoka na kutengeneza ncha kali ikafyatuka na kuruka upande wao pasipo wao kujua…wakatahamaki kusikia sauti kama ya vitu vilivyorushwa kwa kasi mara ghafla..
miti hiyo iliruka na kuwachoma….
miti miwili ilikwenda moja kwa moja mpaka tumboni mwa mke wa sule ikatokezea mgongoni akadodoka chini na kupoteza uhai papohapo..
miti mingine mitatu ikaruka kuelekea kwa kijana mkubwa wa mzee Sule…mmoja ukaingia kwenye jicho na kutokeza kisogoni….mti mwingine ukamchoma kwenye ubavu,,,na ule mti wa tatu ukatoboa shingo yake na kutokeza upande wa nyuma…akadondoka na kupoteza uhai papohapo..
pia alionekana yule mtoto wa mwisho wa mzee sule,,,akidondoka chini,,akapoteza uhai baada ya kuchowa na miti miwili ikaingia tumboni na kutokezea mgongoni..
Sehemu Ya 6
Upande wa ndani ya nyumba hiyo,,alionekana mzee Sule akiendelea kutazama na kuvikagua vitu vyake kama vipo sawa…..akazipiga hatua kuifuata kabati aliyokuwa amejificha Muki…..akashika mlango ili aufungue mlango wa kabati hiyo…ghafla akahisi kama ile mitego aliyoitega nje.. imefyatuka….akatabasamu,,….akiamini kuwa,, mitego hiyo imemnasa mtu aliyekuwa ameingia kwenye eneo la nyumba yake na kujaribu kuchunguza vitu vyake……..akaacha kufungua mlango wa kabati akazipiga hatua kuelekea nje,,ili akamtazame mtu huyo..
***********************
Upande mwingine,, kule kwenye mgahawa, walionekana wateja wakiendelea kusubiri huduma,,,wengine walihitaji supu,na wengine walihitaji ugali nyamachoma,,kuna mteja mmoja alikuwa kaagiza Supu,,akaambiwa asubirie supu inaletwa lakini akastahajabu,,,inakaribia kupita lisaa limoja haoni dalili yoyote ya muhudumu kuleta supu aliyomuagiza….akaamua kunyanyuka na kuelekea kule jikoni ili akaulize kama kuna tatizo!!! kwa sababu supu imecheleweshwa,,alipoukaribia mlango wa jikoni,,akasema,,”jamani mbona nimeagiza supu,,lakini hamjaleta mpaka sasa hivi ni lisaa limoja limepita….
hakuna mtu aliyemjibu…akaamua kufungua mlango, akaingia upande wa ndani ya jiko..hakuona mtu!!! akaangaza angaza macho,,ghafla akaina sufuria kubwa likiwa jikoni,,ndani yake kulikuwa na supu panoja na viganja vya mikono ya binadamu!! akastuka…akazipiga hatua za tahadhari kulisogelea sufuria hilo…akaona pia kuna masikio ya binadamu pamoja na pua ya binadamu!…..macho yakamtoka,,ghafla akahisi kichefuchefu akatapika,,,akasema,,”MUNGU WANGU!!! INAMAANA SIKUZOTE NAKUNYWA SUPU KWENYE MGAHAWA HUU KUMBE NAKULA NYA YA BINADAMU MWENZANGU…akatoka haraka na kurudi kule kwenye viti walipokuwa wameketi wateja wengine..akatapika tena kwa mara nyingine!!!wale wateja waliokuwemo ndani ya mgahawa huo wakamshangaa mtu huyo…..mteja mmoja akamfuata na kumuuliza ,,”Unaumwa??
mtu huyo hakujibu kitu chochote akanyoosha kidole kukielekezea kule jikoni…wale wateja wakajiuliza ,,mtu yuho anamaanisha nini?? mteja mmoja akaamua kwenda kule jikoni akafungua mlango na kuingia upande wa ndani,,akaangaza angaza macho akaona sufuria kubwa,,ndani yake kuna supu pamoja na viungo vya binadamu,,viganja,,masikio na pua…akastuka akatoka haraka huku akitimua mbio…wale wateja wengine walipo ona mtu huyo anatimua mbio,,wakaamua kwenda kushuhudia…kuna nini huko jikoni..kwa sababu ni kama huduma ya supu na chakula imesitishwa kwa muda wa lisaa limoja sasa…wakafungua mlango wa jikoni,,,,baadhi ya wateja wakaingia upande wa ndani…wakastuka kukuta kunasufuria lina supu ndani yake…pia kuna viungo vya binadamu!!! wakakasirika sana……..ikasikika sauti ya mchaga mmoja miongoni mwa wateja hao,,walioingia humo jikoni akaropoka,,,”YELEUUUWI..YESU NA MARIA,,AISEE MEKU…huyu mama anatulisha nyama ya BINADAMU….
wale wateja wakaamua kuchoma moto mgahawa huo..kisha wakatoka nje kwa pamoja na kuingia mitaani kumtafuta MAMA MUUZA SUPU wamuangamize..kwa kitendi hicho cha kuwalisha nyama za binadamu kwa miaka mingi…pasipo wao kujua..
***********************
Upande mwingine kule kwa mzee Mbega alioneka
alionekana,,,Tina akiwa bado ameketi kwenye kiti,,sebuleni,,akaonekana mzee Mbega akitokea chumbani kwake,,Tina akamtazama Mzee mbega wakakutanisha macho,,Tina akastuka,,, akahisi hali ya hatari,,,ghafla kuna fikra ikamuingia kwenye mawazo yake….akukumbuka matukio ya mauwaji yaliyofanywa na mwanamke akinyonga watu kwa kutumia kamba…mawazi hayo yalizunguka ndani ya ubongo wake,,ghafla akamuona mzee Mbega ndani ya fikra hizo zilizokuwa zikizunguka kwenye ubongo wake,,kuwa mzee mbega katoa kipande cha mbao ya mti wa MKARATUSI anamuangamiza yule mwanamke aliyekuwa anafanya mauwaji akinyonga watu kwa kutumia kamba….
TINA akastuka!! akarudi katika fikra zake za kawaida….wakati huo mzee Mbega alikuwa tayari kamkaribia Tina…..
Tina akaona mzee Mbega anaingiza mkono wake ndani ya mfuko wake wa suruali.. ghafla akatoa kipande cha mbao ya mti wa MKARATUSI….
akastuka akauliza kwa mshangao,,”Unataka kufanya nini???kabla hajamaliza kuongea Mzee mbega alipeleka mkono wake uliokuwa umeshikilia kile kipande cha mbao,,moja kwa moja mpaka kwenye kifua cha Tina..
Macho yakamtoka Tina,,huku mdomo wake ukiwa wazi,,akabaki kasimama kama sanamu….ngozi ya Tina ikaanza kubadilika na kuwa ngozi ya mzee,,nywele zake zikaanza kubadirika rangi,,zikawa mvi…uso wake ukakunjamana,,akadondoka chini….akaanza kupukutika kama vumbi linalopulizwa na upepo…hatimae akatoweka kimiujiza…akarudi katika hali ya umauti…..ukawa ndio mwisho wa Tina……wakati huo macho ya mzee Mbega yalikuwa yakitazama ile sehemu alipodondoka Tina na kutoweka….akajisemea moyoni,,”ni bora umerudi mavumbini kuliko ulivyokuwa unaishi duniani bila kujitambua kuwa wewe ni mfu uliyefufuliwa..aliyasema maneno hayo kwa sauti yake ya kizee….akazipiga hatua kurudi chumbani kwake…akakirudisha kile kipande cha mbao,,ghafla ukavuma upepo mkali sana!!! upepo huo ukaezua bati la nyumba yake ukaendelea kuvuma kwa kasi kubwa….Mzee mbega akaingiwa na hofu kubwa…akaamua kutoka nje ya nyumba..kwa kuhofia huenda nyumba ikabomoka akafunikwa na kifusi cha matofali akafa……
alipotoka nje bado aliona upepo ukivuma kwa kasi,,pia vumbi lilikusanywa na upepo huo likawa linapepea hewani…upepo ulikuwa mkali sana ulinyanyua hata vitu vizito..vikawa vinapelekea na angani….huku vikirusha huku na kule…
wakati mzee mbega anatahamaki..kuna kipande cha chuma kilichokuwa kimechongoka,,kilirushwa na upepo huo kikaenda moja kwa moja mpaka kwenye paji la uso la mze Mbega akapoteza maisha papohapo…
*****************
Upande mwingine,, kule nchini Nigeria…kule kwenye kaburi alilozikwa Tina…likatikisika na kutoa nyufa za mpasuko kutoka chini ya aridhi…likatokea tetemeko kubwa la aridhi,,tete meko hilo lilisababisha makaburi mengine yakapasuka na kuzama chini ya aridhi…pia baadhi ya nyumba zilizokuwa jirani na maeneo ya makaburini….zilibomoka kwa mtikisiko huo……
watu wakaanza kutimua mbio,,huku wakipiga mayowe kwa hofu…..ndani ya dakikaka chache mji mzima ulikuwa kimya..haikusikika hata sauti ya ndege warukao…..
wakati huo huo..kule kwenye himaya ya mganga matata OBINA….akaanza kupata misukosuko…….kilitokea kimbunga kikiambatana na upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu!!!!upepo huo ulitoa mngurumo mkubwa wa kutisha….
Macho yakamtoka Obina…akaamua kuuzuia upepo huo kwa kutumia nguvu zake za kichawi lakini akashindwa….akachukua Tunguri zake na baadhi ya vitu vyake vya muhimu vinavyompa nguvu za kichawi,, ili atimue mbio baada ya kuona mambo yamekuwa magumu….kabla hajafika mbali…ule upepo ukamfuata ukamvuta!! akawa katikati ndani ya kimbunga hicho akizunguka hewani….kisha ukamrusha kule kwenye kaburi la Tina,,Mganga Obina akatumbukia ndani ya kaburi hilo,,,likajifunga na kurudi katika hali yake ya kawaida,,ukawa ndio mwisho wa mganga Obina…..,, kimbuga hicho pamoja na upepo uliokuwa unavuma kwa kasi..ukatoweka,hali ikawa shwari na ukimya ukatawala……
****************
upande mwingine kule mitaani,,walionekana wale wateja waliokuwa wakinywa kila siku supu,, pamoja na nyama choma katika mgahawa wa mzee Sule…wakiwa wameshikilia mapanga na marungu..wengine wamebeba mawe na madumu yaliyokuwa na petroli ndani yake….waliizungukia mitaa yote lakini hawakufanikiwa kumpata Mama muuza supu,,ambaye ndiye mke wa mzee sule..
wakakata tamaa!! wakaanza kutawanyika kila mmoja akipitia njia yake kwenda kuendelea na shughuri zake…..hatimae mkusanyiko huo wa watu ukaisha kabisa……
************************
Upande mwingine kule nyumbani kwa mzee Sule..alionekana akitoka nje ya nyumba yake..akazipiga hatua za tahadhari huku kashikilia shoka kubwa..kuelekea kule alipokuwa ametega mitego ya kumnasa mtu atakayeingia kwenye himaya yake….hakuwa na wasiwasi na familia yake..kwa sababu…huwa wanarudi nyumbani kwa kupitia ile nja ya chini kwa chini ya aridhi…hivyo hakuwa na shaka kabisa….alipokaribia lile eneo alilotega mitego,macho yakamtoka,,,hakuamini kile alichokiona!!! alikuta mkewe kalala chini amekufa kwa kunaswa na ile mitego aliyokuwa kaitega yeye mwenyewe!! alipoangaza angaza macho yake akawaona watoto wake wa pekee nao wakiwa wamekufa kwa mitego hiyo!!! akapiga kelele zaaumivu ya moyo kwa kuiangamiza familia yake yeye mwenyewe pasipo kutarajia……akapaza sauti kwa kusema,,”WEWE ULIYEINGIA KWENYE NJIA YANGU YA SIRI INAYOPITA CHINI YA ARIDHI,,NDIO CHANZA CHA KUONDOKEWA FAMILIA YANGU…..HAKIKA SITOKUACHA UKIWA HAI….
wakati huo huo alionekana Muki akiwa bado kajificha ndani ya kabati la mzee Sule lililokuwela sebuleni,,akitafakari namna ya kufanya ili ajiokoe..kutoka mikononi mwa mzee sule….
kule nje alionekana mzee Sule kazipiga hatua kuelekea mstuni….ghafla akasita akasimama kwa sekunde kadhaa….akaamua arudi ndani kwake akachukue mashine ya kukatia miti(chain sow) iliyokuwa ndani kabati lake kule sebuleni….akaingia ndani,,Uso wa mzee Sule ulionekana kuwa na hasira kali….mpaka mwili wake ulikuwa unatetemeka…macho yake yalikuwa mekundu huku machozi yakimlenga…..akaikaribia kabati akanyanya mkono wake kuushika mlango wa kabati hilo…
Ndani ya kabati alionekana Muki..akitetemeka kwa uwoga..hofu kubwa ilitanda juu yake….akakishikilia kisu chake sanjari..tayari kwa lolote litakalotokea..
Mzee Sule lipotaka kuufungua mlango huo…ghafla akasikia sauti ya mngurumo wa upepo ukivuma kwa kasi!! akasita kufungua kabati hilo..akazipiga hatua kutoka nje ili ashuhudie ni nini kimetokea…
akastahajabu kuona Kimbunga kikubwa angani kimeambatana na vumbi kali….ndani ya kimbunga hicho kulionekana vitu vingi vilivyobebwa na upepo mkali….macho yakamtoka mzee Sule baada ya kuona kimbunga hicho kikija upande wa nyumba yake!!! kutokana na upepo mkali..miti iling’oka na kupeperuka kuelekea angani katikati ya kimbunga hicho….upepo uliendelea kuvuma kwa kasi ya ajabu huku ukizunguka kama gurudumu!!! Mzee Sule akalitupa shoka alilokuwa amelishikia akaamua kutimua mbio akatokomea mstuni….
mule ndani ya kabati alionekana Muki,,akiendelea kusubiri mzee Sule adungue kabati..amchome kisu cha kwenye koo…ghafla akasikia sauti ya mngurumo…akajiuliza,,”mngurumo huo ni wa kitu gani!!? wakati bado anajiuliza..akasikia sauti ya kitu kungo’ka kwenye nyumba hiyo..kumbe kile kimbunga kiliezua batu la nyumba ya mzee Sule..
vitu vilivyokuwa ndani ya nyumba hiyo vikaanza kusombwa na upepo,,, kuvitwa kuelekea angani..ghafla lile kabati likavutwa na kimbunga hicho kuelekea angani……Muki akaingiwa na Hofu kubwa..akahisi anaelea hewani…alipojaribu kufungua mlango wa kabati akashindwa..
kumbe mlango huo ukiufunga haufunguki bila kuzungusha kitasa….na kitasa hicho kipo nje ya mlango!! Muki akahisi kuchanganyikiwa…..
kutokana na upepo kuvuma huku ukizunguka….
vitu vilivyokuwa vimevutwa na kuwekwa katikati ya kimbunga hicho pia vilizunguka….hata lile kabati ambalo alikuwemo Muki ndani yake lilizunguka kwa kasi!!!,, kitendo hicho cha kabati kuzunguka kwa kasi….ule msumeno wa kukatia miti mikubwa(hain sow)ulimgonga Muki sehemu ya kichwani akahisi kizunguzungu akapoteza fahamu akiwa huko angani,,ndani ya kabati hilo!!!
watu walistahajabu…wakaingiwa na hofu wakidhani ni MWISHO WA DUNIA….mji mzima ulichafuka…watu walikimbia mbio kila mtu akipita njia yake..ili kutetea nafsi yake…..
ghafla vikaanza kudondoka vitu kutoka angani.kuja kwenye ardhi!!!.ikiwemo miti mingi mikubwa isiyokuwa na idadi….pamoja na vitu vingi vizito……
***********************
upande mwingine alionekana mzee Sule akitimua mbio,,,macho yalimtoka! alikimbia bila kujua ni wapi anaelekea..ghafla akaanza kukutana na maiti nyingi zisizokuwa na idadi zikiwa katika hali ya nafsi,,,maiti hizo zilionekana kuwa na huzuni kwenye nyuso zao…zilimtazama mzee Sule kwa macho ya msisitizo….Mzee Sule akapagawa…akaanza kukimbia ovyo..akawa anajikwaa na kudondoka chini mara kwa mara…kila alipokua ana kimbilia bado umati wa maiti hizo zilimfuara kwa nyuma zikitembea….Mzee Sule akazidi kuchanganyikiwa..alikimbia mpaka akachoka..alipokuwa akisimama na ule umati wa maiti ukisimama pia…Mzee Sule akaanza kupiga mayowe ya kuomba msaada lakini hakuna hata mtu mmoja aliyesikia sauri yake..kutokana alikuwa katikati ya pori…..alikimbia mpaka nguvu zikamuishia akasimama…akakata tamaa….alipotazama kushoto kwake…akamuona mkewe pamoja na watoto wake wakiwa wanazipiga hatua muja pale alipokuwa amesimama…..akaanza kuingiwa na amani…alijua familia yake imekuja kumpa msaada…..ghafla familia yake ikatoweka…ikajitikeza tena….
kumbe…hayo yalikuwa ni mawazo ya mzee Sule…akakumbuka kuwa familia yake haipo tena duniani….akaingiwa na hofu,,,akaanza kulia kwa uchungu,,ghafla akaona ule umati wa maiti…ambao ni wale watu aliokuwa akiwauwa kikatiri kwa kumtumikisha Tina kichawi pasipokujijua……na kuwanyonga watu hao……ule umati wa maiti hizo ukaanza kumzunguka mzee Sule na kumuweka katikati…akawa hana sehemu ya kukimbilia…….Akainekana Domy akiwa katika hali ya umauti…akizipiga hatua kumfuata mzee Sule….alipomkaribia akamkamta mzee Sule akamnyofoa macho kwa kumtoboa na vidole vyake..akavuta macho hayo na kuzipiga hatua akasimama kando….Mzee Sule alipiga mayowe….alihisi maumivu makali,yaliyosababisha haja ndogo kumtoka mfululizo…damu nyingi zilimtoka…ikaonekana maiti nyingine..ammbaye alikuwa mmoja kati ya wale walevi wawili akizipiga hatua kumsogelea mzee Sule…alipomkaribia..akamnyofoa mkono kwa kuuvuta mpaka ukang’oka kwenye bega….mzee Sule akapiga mayowe ya kuomba msaada,,lakini hakuna aliyemsaidia……
maiti nyingine ikamfuata na kumnyofoa mkono mwingine…mzee Sule akahisi maumivu ya hali ya juu…alipiga kelele mpaka saiti ikakauka…ikaonekana maiti ya yule jirani yake Domy ikizipiga hatua kufuata mzee Sule na kumnyofoa mguu…Mzee Sule akadondoka chini…alihisi maumivu makali..mpaka mwili ukawa na ganzi,,,akawa ahisi maumivu tena….
ikainekana maiti ya yule fundi aliyekuwa anatengeneza kengere kwenye nyumba ya jirani yake Domy..akizipiga hatua kumfuata mzee Sule kamnyofoa mguu wa pili…..ikaonekana maiti ya Tina ikimfuata mzee Sule kumtoboa kifuani na kuunyofoa moyo wake…Mzee Sule akatulia tuli.. mati zilizobaki zikawa zinanyofoa baadhi ya viungo vya mwili wa mzee Sule mpaka akaisha kabasa..pale alipokuwa amelala pakabaki tupu…..umati huo wa maiti ukatoweka kimiujiza..ukawa ndio mwisho wa mzee Sule….
************************
upande mwingine kule angani…kilipokuwepo kimbunga …..kikatoweka ghafla…ni baada ya mzee Sule kufa… .likaonekana kabati likishuka kutoka angani likatumbukia kwenye bahari…..likawa linaea juu ya maji!!!! kwa mbali walionekana wavuvi wawili wakiwa kwenye mtumbwi
(Wood boat) wakapiga kasia kuifuata kabati hiyo..wakafungua kitasa cha mlango huo..wakastahajabu kukuta binadamu…wakasikiliza mapigo yake ya moyo kifua…wakasikia bado uanapiga….mvuvi mmoja akasema,,”mtu huyu kapoteza fahamu..wakamchukua na kumuingiza ndani ya mtumbwi…..wakaanza kupiga kasia..kuelekea nchi kavu…..kabla hawajafika Muki akazinduka,,alipoangaza macho yake..akastahajabu kujikuta yumo baharini ndani ya mtumbwi…mvuvi mmoja akasema,,”pole ndugu..tumekukuta ndani ya kabati lililokuwa likielea juu ya maji….Muki akashusha pumzi baada ya kugundua kuwa yupo katika mikono salama….baada ya dakika kadhaa Muki alijisikia nafuu kabisa…akaanza kuwasimulia wale wavuvi kilichomtokea……walimuonea huruma ……mvuvi mmoja akasema,,”MUNGU NI MWEMA,HAKUNA LINALOSHINDIKANA MBELE YAKE…POLE SANA NDUGU…KWA MISUKOSUKO ILIYOKUPATA..
Muki akasema,,”Asante sana nashukuru kwa msaada wenu MUNGU AWABARIKI..
Muki alifika nyumbani kwake akiwa salama kabisa…akaamua kuacha kuendelea kuifanya kazi ya ufundi seremala…akawa mfanya biashara…aliishi kwa amani na furaha…
***MWISHO***

