UJI MZITO
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 7
“Nilipokuja kushtuka sikumwona tena, masikini hata jina sikumjua, lakini huku kati kwangu nikahisi kama nimebandikwa kitu, ile kuangalia kilikuwa ni kikaratasi, nikakitoa na kukifungua, kiliandikwa namba za simu na jina Hassan. Nilibaki nikitabasamu tu mwenzangu, basi nikanyanyuka na kwenda kuoga tena…
SONGA NAYO…….
Mama Fei alimaliza kumsimulia Mrs Lomo tukio hilo lililomsisimua na kumfanya atamani msumari. Mama fei aliendelea kumpa ushauri Mrs lomo kuwa asije kujaribu kuchepuka maana atahamia huko moja kwa moja. Mrs lomo akawa anacheka tu, wakapiga stori nyingi sana lakini mwishoni mama fei alikumbuka kuwa kuna birthday ya rafiki yake hivyo aliona sio mbaya Mrs lomo pia aende.
“Sidhani kama nitaweza,” Mrs Lomo alijibu hivyo
“Yaani ukikosa tutakosana, nimemualika Hassan, kwahiyo nitaenda naye,”
“Wewe! Mbona haraka hivyo?”
“Alinionjesha kazi nzuri sana, inabidi nimtafutie siku tutoane uvivu hasa,”
“Haya bwana, mimi nitakujulisha,”
“Saa moja mwisho saa mbili na nusu,”
“Sawa nitakuja.” Mrs Lomo alipokubali, mama Fei alifurahi kisha akaondoka zake.
Mrs Lomo alichukua simu yake ya mkononi na kuangalia ‘missed call’ maana alijibipu muda ule kwa kutumia simu ya Mbosoni. Akaihifadhi namba hiyo kwa jina la Mbo, baada ya kufanya hivyo alitabasamu kisha akafuta na kuandika Mbosoni. Akamtumia ujumbe mfupi,
“Hello Mbo!” hata sekunde haikupita, akajibiwa
“Naam mama yangu mzuri kuliko wakinamama wote,” Mrs Lomo alicheka aliposoma kisha anamuuliza,
“Utakuwa na nafasi unisindikize mahali?” ujumbe huo Mbosoni hakuujibu bali alipiga simu kabisa na kumwambia mama huyo kuwa nafasi kwa ajili yake haiwezi kukosekana muda wowote ule. Wakakubaliana kituo atakachompitia kisha Mrs lomo akaomba ushauri ni nguo gani avae, Mbosoni akageuka kuwa ‘dizaina’ alimchagulia gauni refu, ndani yake avae kaba shingo, alipotaka kumchagulia nguo ya ndani Mrs Lomo alimkatisha kwa kumwita kifupi cha jina lake ambapo Mbo alisisimka kweli.
Kwenye tafrija hiyo waliwasili, uchokozi ulianzia kwenye gari, ni kama kila mmoja alimtamani mwenzake japokuwa tamaa ya mbosoni ndio haikujificha. Mbosoni alivalia suti yake nzito kama mbunge Fulani, ukichanganya na kwenda saluni, lile timba alilokuwa nalo alipendeza kweli. Katika maisha yake hakuwahi kuwa na suti, ila kitu cha kuelewa ni kwamba mwanaume hashindwi kitu akikivalia njuga.
Mama Fei alipowaona wawili hao wanaingia kama mtu na mumewe, alishtuka maana haikuwa kawaida ya Mrs Lomo kuonekana na mwanaume mwingine zaidi ya mumewe. Kitu kingine ambacho kilimtambulisha mama fei ni ushakunaku wenye udakudaku ndani yake, aliwafuata,
“Habari hendisam,” aliita hivyo huku akimtazama Mrs Lomo kwa makusudi
“Nzuri, za kwako,” alijibu Mbosoni
“Zangu ziko kama sura ya Latifa,” alipojibiwa hivyo Mbosoni hakuelewa, alibaki akishangaa tu, akamvuta Mrs lomo pembeni utadhani alikuwa akimdai,
“Shoga usiniambie kama lango la kati limeshambuliwa!” Mama fei huyo alisema hivyo
“Hamna, mbona ni kijana tu,”
“Unafikiri shoo ya huyu kijana na ya mzee Lomo zinafanana! Yaani kama magari huyu kijana ni Kruza, halafu Mzee lomo ni Spacio, upo?” wote wakacheka
“Hassan yuko wapi?”
“Hajafika bado, ila atakuja.” Basi waliishia hapo maongezi yao, tafrija hiyo ilikuwa ikifanyikia nyumbani kwa huyo mhusika na alipaandaa vizuri, viti vilikuwepo vya kutosha, vinywaji na aina nyingi za vyakula.
Mbosoni na Mrs Lomo walikwenda kukaa kwenye meza yao. Na hapo ndipo alipojua kuwa Mrs Lomo anaitwa Latifa, kwahiyo mama Fei alipojibu “Zangu ziko kama sura ya Latifa” alimaanisha ni nzuri kwa maana sura ya Latifa ambaye ni Mrs Lomo ni nzuri. Mrs Lomo alikubali kuitwa Latifa na Mbosoni. Hapo kwenye meza waliangaliana kwa macho Fulani, ukiangalia mwanamke amejiremba vya kutosha, mekapu za kitajiri sio kama mekapu zetu wakinadada wa mtaa wa nonino, ukitoka jasho sura inageuka kuwa mahali ambapo watoto walikuwa wakichezea rangi mbalimbali za ukutani.
Mbosoni alianza kummwagia sifa Latifa kuanzia unyweleni mpaka kwenye visigino, Latifa alibaki akitabasamu tu,
“Damu zetu zimeendana,” alisema Latifa
“Kwanini?”
“Sijawahi kuruhusu mwanaume mwingine anipe furaha,”
“Kwahiyo nina bahati?”
“Ndiyo, tena kubwa tu!”
“Napenda unavyoyafanya hivyo macho yako, na hivyo vishavu vyako unapoanza kutabasamu,”
“Toka huko!” Latifa alitabasamu huku akiongea hivyo, ni kweli alikuwa mzuri usoni usipime, kila kitu alijaaliwa huyu mwanamke kasoro mtoto tu…
SEHEMU YA 8
Mama fei sasa! Kitu cha kwanza alikuwa kama mhudumu wa Mbosoni na Latifa, alihakikisha wamekunywa vya kutosha na kula pia. Aliwachangamsha kwenye meza yao mpaka kuna muda walimfukuza, ilionekana amezidiwa na vinywaji.
Majira ya saa tatu ndio waliamua kuondoka Mbosoni na Latifa. Hakukuwa na aliyelewa, njiani ndani ya gari hawakukaa kama mabubu,
“Vipi umefurahia usiku wa leo?”
“Furaha yako, kwangu mara mbili yake, vipi, wewe umefurahia?”
“Ndio, una maneno wewe!”
“Mbele ya mwanamke mzuri aliyebarikiwa kila kitu nitakosaje maneno, ni kama kuna mwandishi mmoja maarufu alishawahi kuandika, katika mguso wa mapenzi, kila mtu ni mwanamashahiri,”
“Kweli?”
“Ndiyo, kwahiyo ukiwa na mtu kwenye mahusiano halafu akawa ana mtindo wa ‘kukufowadia’ jumbe za mapenzi, jua huyo hana mguso wa mapenzi,”
“Haya Dokta love.” Alivyomwita hivyo, wote wakacheka huku Mbosoni akilikataa jina hilo.
Gari iliendeshwa mpaka ilipofika yale maeneo alikochukuliwa Mbosoni. Kwenye akili yake Mbosoni alijua alichotakiwa kufanya ni kumuaga na kushuka nje ya gari,
“Nataka nipajue kwako,” Latifa alisema hivyo kwa sauti ya kichovu sana
“Kwangu?”
“Hapana, sio kwako, kwa Mr Mbo!” hilo jina Mr Mbo alilitaja kama kwa sekunde tano hivi, alivuta hasa maneno,
“Kwahiyo unataka upajue kwangu na kwa Mbo?”
“Ndiyo! Ni watu wawili tofauti eh?” swali hilo jibu lake lilikuwa ni Kicheko tu.
Basi Mbosoni akawa anatoa maelekezo ya jinsi ya kufika kwake. Kwa bahati nzuri, palikuwa panafikika na mahali pa kuegesha gari palipatikana japo hapakuwa salama sana. Kabla hajaingia ndani, alimsimamisha kwanza Latifa, kidume kilijua tu huko alivyopaacha, ni kama palichezewa disko. Kabla hata hajamaliza sekunde tatu Latifa aliingia, alikuta vitu viko shagalabagala, alicheka kwa sauti kubwa mpaka akadondokea kwenye kochi,
“Ndio maana ukanisubirisha nje, naondoka zangu,” kauli ya Latifa ilimshtua Mbosoni ambaye utadhani aliambiwa atakufa kesho, kijasho kilimtoka, alipiga magoti akimuomba Latifa asiondoke, huwezi amini kidume machozi yalianza kumtoka, Latifa alishtuka kuona machozi ya Mbosoni kwasababu hakuwa siriazi, alimjaribu tu,
“Mbosoni Jamani nilikuwa nakutania tu!”
“Kwahiyo hautaondoka?”
“Ndiyo,”
“Naomba unipe dakika chache nifanye usafi, ukae kwangu hata kwa nusu saa tu na roho yangu itapona,”
“Usijali, kuhusu usafi niachie mimi,”
“Hapana bwana,”
“Unataka niondoke! Kama hutaki basi niachie nifanye usafi.”
Latifa akaanza kufanya usafi, alideki, aliosha vyomba, alitandika kitanda, makochi aliyapanga vizuri. Ndani kwa mwanaume kukang’aa, mpaka Mbosoni mwenyewe akapasifia.
“Fumba macho,”
“Ili?”
“Unanibishia?”
“Hapana Malkia.”
Latifa alimuamrisha Mbosoni lengo lake lilikuwa ni kubadilisha nguo. Alivalia shuka jepesi lililomkaa kweli,
“Nataka kwenda kuoga,”
“Kweli?”
“Ndio,”
“Au wewe huendi?” hilo swali ni kama lilikuja ghafla kwa Mbosoni na kumsababishia kigugumizi cha ghafla. Basi Mbosoni alimwekea maji kisha Latifa akaenda kuoga. Alipotoka tu kuoga, alimtaka Mbosoni aende akaoge haraka,
“Mimi nina mida yangu, usijali,” alijibu hivyo Mbosoni
“Mida gani? Ebu nenda kaoge usinitanie,” Latifa aliongea akiwa siriazi, Mbosoni hakuelewa,
“Siwezi kulala na mtu ambaye hajaoga.” Kauli hiyo ndiyo iliyomwinua mbosoni kutoka pale kwenye kochi kama umeme, hiyo haraka yake usingeweza kuifananisha na kitu chochote, malapa yenyewe aliyakata kwa haraka, hilo taulo alivyojifunga sasa! Alikimbilia bafuni bila maji, sekunde kadhaa alirudi,
“Nilikuwa nakushangaa tu, unaenda kuoga na mate!” Mbosoni ni kama alijiziba masikio, alichanganyikiwa kusikia mama huyo atalala naye kwa usiku huo.
Dakika tatu mtu alishamaliza kuoga. Alirejea ndani na kumkuta Latifa akiwa amejilaza kitandani akiangalia runinga. Sasa ile khanga aliyoivaa Jamani, ilimwishia juu kidogo ya magoti yake yaliyokuwa na weupe Fulani wa maji ya kunde, au rangi ya mtume….
SEHEMU YA 9
Msumari ndani ya taulo haukutulia, ilibidi avae bukta lake pana la kulalia na vesti. Alitamani kwenda kukaa kitandani lakini roho yake ilisita, ikabidi aende kuketi kwenye kochi,
“Unaniogopa eeh?” Latifa alimwambia Mbosoni
“Hapana, kwanini unasema hivyo?”
“Unamwacha mgeni Mwanza, wewe unakaa Mtwara,”
“Tatizo amechagua kukaa kwenye mji wenye utata hapo Mwanza,”
“Mji gani?”
“Nyegezi.” Aliposema hivyo Latifa alicheka huku akiendelea kumkubali Mbosoni kuwa ana maneno sana
“Njoo kitandani, kuna kitu nataka nikwambie.” Latifa aliongea kwa sauti Fulani ya umakini sana, Mbosoni akamfuata, wakaketi wakiwa wameegemea kingo ya kitanda iliyoko kichwani.
Latifa aliuchukua mkono wa Mbosoni na kuushika kwa mikono yake miwili iliyoegemea kwenye mapaja yake, yaani kitendo hiko ndio kiliongeza hasira ya msumari wa Mbosoni uliotaka kutoboa kufuri lake.
“Mbosoni,” aliita kwa hisia huku akimtazama usoni
“Naam, mrembo Latifa,”
“Napenda jinsi mapigo yako ya moyo yanavyokwenda haraka,”
“Umejuaje?”
“Kupitia jinsi unavyoongea, na uso wako pia unaonyesha,”
“Kweli?”
“Ndio,”
“Utabiri wako umekwenda vizuri,”
“Kwanini mapigo ya moyo yanakwenda mbio hivyo?”
“Aaah..”
“Aaah nini Jamani Mbo,”
“Naomba nikwambie tu ukweli wa moyo wangu Latifa…”
“Ishia hapo hapo, nisikilize kwanza mimi,”
“Sawa..”
“Ni muda mrefu sana mume wangu kutoshiriki kula chakula nyumbani nilichokipika, siku ile ulipokuja na kushiriki nami nilijisikia amani sana, hasa pale ulipokuwa umekisifia chakula changu ni kitamu, nilifurahi kupita maelezo. Wapo vijana wengi waliotamani kuwa na mimi, wengi mno, wengine wakiniahidi watanioa, wapo waliodiriki kuacha wachumba zao ili wanipate katika ukubwa wangu huu huu. Nilimpenda sana mume wangu, na sikuwa tayari kumsaliti japokuwa yeye alifanya hivyo zaidi ya mara moja.
Kukosa kwangu mtoto kulimfanya ashindwe kunivumilia na kuniona kama mzigo nyumbani. Nikakosa mtu wa kuongea naye kama rafiki, upweke ukanisonga. Nimevumilia kwa muda mrefu sana. Hali ilizidi kuwa mbaya pale ambapo uwanjani alikuwa hafanyi majukumu yake inavyotakiwa, kila rafiki yangu alikuwa na mchepuko, tulibaki mimi na mama Fei ambaye naye juzi juzi hapa amepata.
Mr Lomo alinioa kwasababu moja tu, nilikuwa mzuri kupita maelezo, nilijijua. Nyumbani kwetu maisha hayakuwa mazuri sana, ila kuolewa naye kuliinua familia yangu, nilihitaji kuwa shujaa kwa familia yangu, niliolewa nikiwa na miaka ishirini, Mr Lomo alikuwa mkubwa kwangu, alinizidi miaka kama kumi tano. Na yeye ndiye aliyekuwa mwanaume wangu wa kwanza, nilimpenda lakini ndio hivyo kukosa watoto kukapunguza upendo wake kwangu, kuna muda niliona ni sahihi anisaliti ilia pate watoto nafsi yake itulie, mpaka sasahivi najua ana watoto nje japo hajaniweka wazi,” Latifa alimaliza kusimulia kisa chake kilichobeba historia yake kwa ufupi na Mr Lomo, machozi yalimtoka,
“Pole sana, uko mikono salama,” alisema Mbosoni akimfuta machozi Latifa huku akimkumbusha thamanai ya machozi yake, kwahiyo hatakiwi kuyaruhusu yatoke.
Latifa alijilaza kwenye mapaja ya Mbosoni, mahali ambapo msumari pia ulijilaza ila katika ya ukakamavu kweli maana ulishajiandaa kugongelea.
“Mbosoni,”
“Naam mrembo wangu,”
“Leo nachepuka,”
“Hapana, unafanya kitu sahihi,”
“Namsaliti mume wangu wa ndoa,”
“Ambaye ameshakuzalia watoto nje! Kwanza usimkumbuke tena,”
“Sawa, leo mimi ni wako, usiku mzima, nifanye vile unavyotaka,” kauli hiyo ilimsisimua Mbosoni na kusababisha msumari wake upige pushapu ya nguvu iliyomgusa Latifa
“Kweli umeamua kutoka moyoni?”
“Ndiyo, nilijua unanipenda tangu kipindi kile tukiwa mazoezi, nilivutiwa na wewe jinsi ulivyo lakini sikutaka kuziamini sana hisia zangu,”
“Kumbe ulikuwa unajua tangu kipindi kile?”
“Ndiyo, mwenyewe ulikuwa unaniangalia sana, nikikuangalia unaangalia pembeni,”
“Basi tangu kipindi kile mwenzako nilikuwa nakuwaza tu, nakupenda sana Latifa, nakupenda kuliko kitu chochote,”
“Kweli?” Mbosoni alipouliza hivyo alishindwa kujibu kwani Latifa alimbana hasa…
MWISHO

