BAO TATU ZA MGENI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu ya 32
Mzee Mtata hakuwa yule katili wa kuogopwa tena,alikuwa mdogo kama pilitoni,aliposikia jina la Lukas,hasira ilipanda na presha ikawa juu!
Machozi yalibisha hodi na hata kabla hajayaruhusu yalitoka kwa wingi,Mzee Jomo alimshangaa sana Mzee mwenzie,amemzoea ni mtu mwenye kiburi na majivuno,hakuwahi kufikiria kwamba kuna siku atatokwa na machozi mbele yake!
“Mzee mwenzangu nini tatizo!”
“Acha tu mzee mwenzangu!”
Bila kuficha kitu japo alijihisi aibu lakini aliamua kumueleza kila kitu mzee Jomo,jinsi alivyomkamata na kumleta kwake!Alieleza mengi sana kuhusu Lukas!
“Mzee Mtata kwa hiyo unamaanisha Lukas kawapa mimba wake zako wote?”
“Ndiyo!”
“Dah!hiki kitoto kumbe kishetani hivi!”
“Nakushauri mzee mwenzangu kaipime familia yako yote,yule kijana sidhani kama ametembea na binti zako wawili tu mpime hadi mkeo!”
“Mkewanguuu hapana hapo nakataaa!”
Mzee Mtata alimueleza jinsi mke wake alikuwa anakuja kwake akisema Lukas ni mdogo wake,kwahiyo ana wasiwasi pia na mkewe!
“Kama kamgusa mkewangu namuua namuua mende yule!”
“Humuwezi!”
“Unasema?”,aliuliza Mzee Joma kwa mshangao!
“Nasema humuwezi na hicho ndicho kinachoniuma mimi,yule kijana nilimuamini sana,kwa upendo niliokuwa nao kwake nilimpa kinga kali sana ambayo hata mimi nikitaka kumfanyia ubaya siwezi,muache tu!”
“Haiwezekeni nasema haiwezekani!”,aliondoka kwa hasira mzee Jomo na kumuacha Mtata anamuita bila mafanikio!
Alirudi kwake akachukua ndimu tatu akazikata kisha akachanaganya na madawa aliyoyajua yeye,alipomaliza aliita familia yake yote!
“Huyo mpuuzi kawatia mimba wake wa mzee Mtata wote,navyoongea na nyinyi hapa Mzee Mtata yuko hoi kitandani!”
“Siyo kweli baba siyo kweli Lukas wanamsi…!”
“Kimyaaa!mwanaizaya wewe!”
Zubeda alijaribu kumtetea Lukas lakini baba yake alimnyamazisha!
“Sasa nisikilizeni hapa,ninawapima mimba!”
Mama Zubeda alishtuka sana,kauli ya mume wake ilimfanya apate hofu kubwa sana,aliamua kujitetea mbele ya mume wake!
“Sasa baba Zubeda kwanini usiwapime watoto mimi mambo yao yananihusu nini?”
“Tena unyamaze Mtata kaniambia kila kitu!naomba mchukue ndimu hizo kila mtu alambe!”
Alisema lakini hakuna aliyeshika ndimu kila mtu alibaki kukodoa macho,mzee Jomo akasimama!
“Msinitanie kila mtu achukue ndimu hapo!”
Kwa hofu wote walichukua ndimu wakiwa wanatetemeka baada ya kulamba wakakaa kusubiri,ile ni dawa ambayo imechanganywa ili kama mtu ana mimba akilamba atahisi kichefuchefu na kutapika!
Johari ndiye alikuwa wa kwanza kutapika wote wakamshangaa,mzee Jomo alijiuliza ina maana na Johari ametembea na Lukas!
Wakati anajiuliza swali lile Suzy naye ngoma ikatiki akarudisha chenji wote wakashangaa ,maana yeye anasema aliwafumania Lukas na Selina!
“Wewe si ulisema umewafumania?”
Kabla hajajibu kitu alishangaa kumuona mkewe anarudisha chenji kumaanisha na yeye naye kitu kimetiki!
“Mamaaaaaaaaaaaaaaa!na wewe!”,binti zake waliuliza kwa mshangao!
Mzee Mtata aliingia ndani akatokana panga akasimama akiwaangalia,wote walikuwa wanatetemeka!
Ajabu Zubeda hakuwa na mimba alisubiliwa lakini hakukuwa na matokeo yoyote,jambo lile llimuuma sana akabaki kulia tu!
Mzee Jomo aliwauliza na wote walikiri kuwa mimba ni za Lukas,alitetemeka kwa hasira alihisi kujutia sana!
“LUKASIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII!!!!”
Alipiga kelele kubwa akiwa haamini kama Lukas ndiye kanmfanyia unyama ule,akiwa katika sintofahamu ghafla alikuja mgeni akiwa ameongozana na binti yake!
Hakuwa mwingine alikuwa ni mama Zahara na Zahara,alipofika tu hakuuliza moja kwa moja akauliza!
“Yuko wapi huyo klidume aliyemtia mimba binti yangui?”
“Kuna nini?”,aliuliza Mzee Jomo!
“Kuna kijana anaishi hapa anaitwa Lukas kamtia mimba binti yangu!”
Kauli ile ilimfanya Zubeda aanguke na kupoteza fahamu,shughuli ikawa imeishia pale!Mzee Jomo hakuwa na namna japo moyoni alisema atamfanya kitu kibaya Lukas!
Siku ile ilipita lakini kesho yake asubuhi walipoamka hawakumkuta Zubeda ,alikuwa ameacha ujumbe kuwa anaenda mjini kumtafuta Lukas!
“Lukas!Lukas!Lukas!”,alilia Mzee Jomo familia yake iligawanyika,mpaka hapo kapoteza binti zake wawili!
Kijiji kiliingia gharika,ule mzimu uliokamatwa na Mzee Mtata na kuwahakikishia kuwa hautorudi,ulirudi kwa kasi sasa ukawa unabaka watu mpaka mchana!
Mzimu ule ulikuja na nguvu kubwa sana,safari hii hii ulikuwa unabaka na kupotea,wanakijiji waliogopa hata kutembea hasa mabinti na wanawake!
Siyo ivyo tu misukule nayo ilionekana mara kwa mara ikikatiza mitaani,walionekana hata watu waliosadikika kufa zamani ambo kumbe walikuwa wamechukuliwa na mzee Mtata!
Kucha zao zilikuwa ndefu na nywele zao pia,kiufupi walikuwa wanatisha sana,hawakuwa wakiongea wengine walikuwa wamekatwa ulimi na wengine walikuwa wana ndimi ila zilikuwa nzito kuongea!
Viongozi walifunga safari mpaka kwa mzee Mtata hili wakamuulize imekuwaje mzimu umerudi na kingine ile misukule imetokea wapi?
Walipofika walishangaa kukuta mazingira ya nyumba yakiwa yamebadilika kila kitu kilikuwa ovyo ovyo tu,ng’ombe walikuwa wamekufa na mbuzi pia,wake wa mzee Mtata hawakuonekana!
Inasemekana walikimbia baada ya kuona misukule imetoka na inaanza kufanya fujo,ule mzimu pia ulianza kuwabaka hata wao!
Mazingira ya nyumba yaliwatisha viongozi lakini walijikaza wakaingia kilingeni ambako hawakuamini walimkuta mzee Mtata kafariki siku nyingi mpaka kaoza,pembeni yake ulikuwaa umekaa ule mzimu ila ulipowaona ukapotea!
Viongozi walitoka mbio baada ya kuona tukio lile,hawakuwa na namna mdaiwa wao alikuwa amekufa!
Hata ng’ombe walizompa walizikuta zimekufa zote na mbuzi,ilibidi wakakae upya kutafakari hatima ya kijiji chao ambacho sasa kila kona ni misukule na ule mzimu ulishika kasi!
Baada ya kutafakari sana walimtafuta mganga nguli kutoka kijiji cha jirani ili aje awasaidie kufanya ile kazi arudishe amani kijijini!
Alikuja nguli kutoka kijiji cha jirani ambaye alipofika tu aliitisha kikao cha wanakijiji wote wakakusanyika!
Alifanya manyanga yake mwisho akaamrisha aitwe mtu anayeitwa mzee Jomo,watu walishangaa sana!
Mzee Jomo alikuwa nyumbani na mawazo yake akafuatwa na sungusungu wa kijiji na kupelekwa mpaka kwenye ule umati!
Hakuwa anajua chochote kuhusu wito ule alibaki kushangaa,Mganga alipomuona tu alisema!
“Matatizo yote yameanzia kwa huyu mzee!”
Wanakijiji walishangaa sana na kubaki kuulizana imekuwaje mzee Jomo anahusikaje na mzimu ule,hata mzee Jomo alibaki kushangaa tu!
“Najua mnashangaa ila huyu mzee kuna mgeni alimkaribisha kwake,mzee uongo kweli?”
Kidogo sasa mzee Jomo akaanza kuelewa alitingisha kichwa kuashiria ni kweli alimkaribisha mgeni ,japo mpaka hapo hajui mgeni yule anahusikaje na ule mzimu!
Alipewa nafasi aelezee kilichotokea mpaka akamakaribisha mgeni nyumbani kwake,alisimama kwa masikitiko makubwa sana!
Kwanza aliwataka radhi wanakijiji kisha akahadithia jinsi alivyokutana na mgeni yule na kumpa hifadhi nyumbani kwake!
Alielezea yote kila kitu mpaka alivyotoroka na mwanaye na kuacha amewatia mimba binti zake wawili,ila hakumtaja mkewe!
Bila kuficha alieleza pia kuwa mgeni aliwatia mimba wake wote wa mzee Mtata hadi kupelekea akapata presha iliyomlaza kitandani na kuuchukua uhai wake!
Wanakijiji walishika kichwa walitamani sana kumjua huyo mgeni shujaa aliyeingia kwa mzee Mtata na kuwajaza mimba wake zake wote!
Waliona ni mtu wa ajabu sana,baada ya kumaliza kuongea aliomba radhi tena huku analia machozi,aliumia kuona kumbe mgeni ndiye amesababisha mambo ya mizimu kuja kijijini!
Mganga alisimama na kuanza kuelezea chanzo sasa rasmi kilichopelekea mzee Mtata autoe mzimu kaburini!
Wanakijiji walishangaa kusikia kuwa mgeni alilala kaburini siku tatu ili aweze kurudi mjini,ila mganga alisema pia mzee Mtata alipoteza nguvu nyingi kumpatia kinga mgeni yule ambayo amekufa akijutia mapa leo!
Kila kilichoongewa kilikuwa kama ndoto au filamu fulani iliyoigizwa na waigizaji mahiri sana duniani!
Baada ya hapo yule mganga alifanya manyanga yake na kuutoa hadharani ule mzimu,wanakijiji walitaka kuushambulia lakini akawazuia!
Baada ya hapo akaongozana na wanakijiji mpaka makaburini huko akafika mpaka kaburini ulipotoka!
Walishangaa kukuta kaburi liko wazi na jeneza liko wazi juu likiwa limechakaa sababu ni la zamani sana!
Mganga alifanya yake mzimu ukakubali kuingia kwenye jeneza na kisha akaurudisha kaburini,kanuri likafukiwa,wanakijiji ili kuhakikisha hautokuja tena kutokea waliufukia kwa mawe na kokoto nyingi sana!
Amani ikarejea kijijini tena mganga yule aliiondoa misukule haikuonekana kabisa amani ilirejea kama zamani!
Ndipo hapo likatolewa tamko kubwa kuhusu wageni kuingia ndani ya kijiji hiko,na hapo ndipo chuki dhidi ya wageni ilianzishwa rasmi!
Wageni hawakukaribishwa tena vizuri katika kijiji kile,ukipata mgeni unaenda kumtambulisha kwa mjumbe kwanza na unaulizwa anakaa siku ngapi?
Sehemu ya 33
Mzee Jomo alianza kuhangaika huku na kule akitafuta dawa ya kumfanyia ubaya Lukas,lakini kila alipoenda aliambiwa haiwezekani na wengine wakamtapeli tu!
Aliuza mpaka ng;ombe zake akasafiri mpaka Nigeria lakini hakuambulia kitu,kinga aliyoweka mzee Mtata ilikuwa kiboko!
Hatimaye mkewe alijifungua na binti zake wakajifungua pia,watoto ambao ukiwaona unasema huyu ni Lukas mtupu!
Hali ile ilimchefua zaidi mzee yule ambaye aliongeza juhudi za kutaka kumfanyia ubaya Lukas ambaye zote ziligonga mwamba!
Mzee Jomo hakula kwa amani,alikonda kwa mawazo na huzuni,miaka ikakatika watoto wakawa wanakuwa na kibaya walichukua sura ya baba yao mtupu!
Mawazo hayakumuacha salama Mzee Mtata alifariki miaka mitano baadae, na kumuacha mkewe akiwa analea familia!
Wake wa mzee Mtata waliondoka na kwenda kuishi kijiji cha jirani,ambako wengine walishaolewa huku kila mtu akiwa na chata ya Lukas!
Miaka kumi sasa imepita siyo Lukas,Selina wala Zubeda walioonekana kijijini,hakuna aliyewaona wala kupata tetesi za wapi walipo!
Historia ya mgeni ikawa imeishia hapo,mgeni alikuja mwenyewe kaondoka na watu wawili,hakuja na mtoto lakini kaacha watoto!
Mgeni kamuua shujaa wa kijiji hiki aliyeogopwa mpaka na sisimizi,mgeni kamuua mzee Jomo kabla hata ya siku zake!
Mgeni kafufua mizimu,mgeni kaleta mizimu mgeni kaleta taharuki,ni nani atampenda mgeni tena katika kijiji hiki?Nani atamkaribisha mtu hasiyemjua tena katika kijiji hiki?nani?nani atamuamini tena mgeni katika kijiji hiki!Hakuna hakuna hakuna!
MGENI ALISHUSHA THAMANI YA WAGENI KATIKA KIJIJI CHETU,VIJIJI VINGINE WANAFURAHI WAKIPATA WAGENI LAKINI HAPA MGENI ANATOA KUMBUKUMBU MBOVU SANA ILIYOWAHI KUTOKEA!
**************
“EFUUUUUUUUUUUUHHHHHHH!”
Nilishusha pumzi ndefu sana,hakika ilikuwa ni simulizi yenye kusisimua na kusikitisha sana,hata mimi nilikubali kwa namna ile ni haki wageni tuchukiwe!
“Ndiyo hivyo kaka!”
“Aiseeh poleni sana!”
“Tulishapoa ila ndo ivyo hatupendi wageni!”
“Kwahiyo na mimi unanichukia?”
“Kidogo maana umeonyesha utofauti!”
“lakini hujaniambia mwanzo kabisa ulisema ulimpoteza dada yako kisa mgeni!”
“Zahara alikuwa dada yangu,alifariki akijifungua yeye pamoja na mtoto!”
“Dah pole sana!”
Wakati tukiwa pale tunajadili walipita watoto watatu wanacheza ndipo Regina akanishtua!
“Eeeh unamuona yule mtoto?”
“Ndiyo!”
“Sasa yule mtoto wa Johari yule aliyekuwa anamchukia mgeni basi unaambiwa ndo kaizaa kopi yake yani ukimuona huyo wanasema ni sawa na Lukas kabisa kwa wanaomjua!”
“Ebhu muite!”
“Unataka ufanyeje?”
“We muite tu!”
Regina alimuita yule mtoto alipofika akatusalimia kisha nikachukua simu yangu nikampiga picha kama tatu hivi!
“Sasa mbona umempiga picha?”
“Aaah nimependa tu!”
Kiukweli nilikuwa sina sababu ya kubaki kijijini sababu nilikuwa nimemaliza utafiti wangu kwa asilimia zote,mbali na utafiti wangu lakini pia mbali na utafiti nilipata story nzuri ambayo nina uhakika itapendwa sana na wengi!
Niliomba nipelekwe kwa mama Zubeda wakafanya ivyo,haikuwa rahisi lakini kutokana na kwamba niliwaambia nataka niwasaidie kuwatafuta binti zao yaani Selina na Zubeda walikubali nikaongea nao kisha nikawapiga picha ya pamoja na picha moja moja!
Niliaga nikaondoka kijijini huku Regina akionekana kuhuzunika sana,hata mzee wake aliumia akinisihi nibaki lakini sikukubali!
Niliondoka nikiwaahidi kuwa nitarudi na Selina,Zubeda na pia nitamleta Lukas aje aombe msamaha kwa kijiji ili wageni tupokelewe tena kijijini!
Nilipanda gari asubuhi na mapema na kuanza safari ya kurejea Dar,safari yangu ilitawaliwa na tabasamu pana kwa kupata simulizi nzuri!
Lakini kichwani nilitamani kuyajua maisha ya Lukas baada ya kurudi mjini,je ni kweli wabaya wake walimsamehe au mzee Mtata alimuingiza choo cha kike!
Nilifika nikapumzika wiki nzima kisha nikachukua ile picha ya yule mtoto wa Lukas nikaitoa kisha nikamtafuta mchoraji hodari na maarufu sana kwa jina la Masoud Kipanya!
“Mdogo wangu mambo vipi?”
“Safi kaka shikamoo!”
“Ahh unaniona mzee,nilishakukataza kunizeesha nambie vipi hatuonani?”
“Kaka Masoud nina shida!”
“Ipi tena!”
“Nina picha hapa”,nilimpa ile picha akaiangalia kisha nikamuambia!”
“Kaka nataka iyo picha unichoree lakini huyo mtoto akiwa mtu mzima,yani uvute taswira huyo dogo akiwa mtu mzima atafananaje najua unaelewa cha kufanya we mzoefu!’
Nilimuelezea Masoud kwanini naitaka ile picha akakubali kunifanyia,baada ya wiki moja aliniita na kunikabidhi picha tatu zikiwa tofauti nyingine zina ndevu nyingine hazina!
Nilizichukua zile picha nikarudi nyumbani nikazihifadhi,nilitamani sana kumpata Lukas ili anipe stori yake na Selina mjini!
Bado namtafuta na hakika nikimpata nawaahidi nitawaletea simulizi nyingine ya Lukas kama season ya pili ya hadithi hii!
Bado nina shauku ya kumjua Lukas kiundani,nataka nimjue aliishije baada ya kutoka kijijini?
Nawashukuru sana kwa kuwa pamoja unaweza kutoa maoni yako kuhusu simulizi hii,mwisho wa hadithi hii ni mwanzo wa hadithi nyingine!
TUTEGEMEE SEASON TWO KAMA NIKIMPATA NDUGU YETU LUKAS!
MWISHOOOO*****


1 Comment
Bao tatu za mgeni season 2 tunaitaka