Nimegundua Mke wangu alikua anafanya Mapenzi kinyume na Maumbile
Mke wangu ana rafiki yake alishindwana na mume wako huko kaja kamleta hapa anaishi kwangu. Huu ni mwaka wa pili. Kila nikikuambia kuhusu kuondoka ananiambia hajakaa sawa. Ni rafiki yake alimsaidia tangu zamani na mambo kibao.
Kusema kweli, mwanzo nilikuwa namchukia, lakini baadaye nikaanza kumpuuzia. Ila kuna tabia alianza za ajabu, kuniamia mambo ya mke wangu ya zamani. Unaweza kumkuta anakaumbia hivi: “Unajua shemeji, mke wako zamani alikuwa anatembea na Mbunge fulani.” Mwanzo nilikuwa napuuzia, lakini nikajikuta naanza kufuatilia, najua ni kweli.
Nakua na hasira, nagombana na mke wangu. Nikimuambia kumuondoa rafiki yake, anakua mkali, na huyo rafiki anajifanya kama bado anamaumivu ili abaki. Nakaa, utasikia: “Hivi unajua shemu, mke wako alishawahi kulala na wanaume wawili wakati mmoja?” Hujakaa sawa, anakutumia picha za zamani za mke wangu na wapenzi wake wa zamani si zauchi ila anajifanya kama kakosea flani halafu anakuelezea!
Utasikia: “Shemu, unamjua huyu? Hii picha nimeiona kwenye simu yangu ya zamani sana.” Basi nakua na hasira. Najizuia lakini nashindwa. Imefikia hatua sasa, kila nikitaka kufanya mapenzi na mke wangu, nahisi kinyaa. Nimejua mambo mengi sana ya zamani ya mke wangu mpaka namchukia.
Najua rafiki yake alikuwa ananimbia kwakua ananitaka. Lakini hata kama angebaki pekee yake duniani, siwezi kutembea naye. Najua mambo anayoniambia ni ya zamani, na sipaswi kumkasirikia mke wangu, kwani mimi nina yangu. Lakini najikuta nakua na hasira sana.
Kuna kitu kaniambia juzi ambacho kimenifanya nikutafute. Aliniambia kuwa mke wangu alishawahi kufanya mapenzi kinyume na maumbile. Kweli nimechoka. Nina hasira na baada ya kuniambia hivyo, nilimuambia mke wangu kama haondoki, basi mimi nitaondoka.
Kweli, alimuondoa na kumpeleka kwa rafiki yao mwingine naye ana ndoa. Shida ni kwamba, namchukia mke wangu. Nina hasira naye na sitamani kabisa kuwa naye. Nikifikiria suala la kinyume na maumbile, nachanganyikiwa. Nakua namkagua mke wangu, sioni chochote. Ila sitaki kuwa naye.
Nisaidie, nifanye nini kuondokana na hii hali? Kama kweli alifanya mambo hayo ya kinyume na maumbile, je, aliacha kabisa, au mimi niko naye ila kuna wengine wanamfaidi?

