
za Mapenzi, Maisha na Uchawi Mautundu Kitandani
PISI YA KIJIJI
EPISODE 13
Tunaanzia pale pale tulipoishia ambapo Gabriel aliona kelvin na mariamu wakipeana mabusu aliita kelvin kwa hasira kelvin
Kelvin aligeuka na kuita “Gabriel” huku akimtazama Gabriel hakujiuliza
alimsogelea na kumpiga ngumi kelvin
ya uso paaah kelvin alianguka chini na kushika taya yake huku akiyema kisusio ….
Aliinuka na kumwambia ” Gabriel mbona sielewi ngumi ni za nini sasa ” anataka ampige ngumi nyingine mariamu aliingilia na kusema “inatosha Gabriel”
Kelvin alishangaa “kumbe mnajuana “
Gabriel hakuongea zaidi ya kuondoka kwa hasira sana ……
Ndipo akamwambia kila kilichotokea na mambo yote kuwa Gabriel alikuwa
akimtaka na alimtongoza lakini
alimkataaa na mwishowe kuja kuniona na wewe ndo akafanya hivyo kelvin aligundua kosa lake ni kutokumuweka wazi mapema rafiki yake kuwa kuna mwanamke anampenda bila hata kumwambia hiyo ingesaidia Gabriel kujua mapema na kujitoa kwenye kinyanganyiro hicho …….
Baada ya tukio hilo Gabriel alianza kujilaumu njiani akitembea na mwishowe anakutana na Olesta naye akiwa ana mawazo kelvin hamtaki alipomuona alianza kumwambia kwa sauti kubwa
” nampenda sana rafiki yako na
hanitaki nifanyaje “
Alishangaaa sana huyu kelvin wadichana wanampendea nini mpaka kila mtu anamtaka . Alichokiona sasa ni bora hata amfariji kwa kimkumbatia tu ……..
***************
Mapema asubuhi siku iliyofuata
…………
katika cafteria ya hospitali, kulikuwa na hali ya utulivu sana . Wafanyakazi wachache walikuwa wameanza
kuingia, wengine wakihitaji kahawa
angalau watulize akili , lakini kwa Isabella hii haikuwa siku ya kawaida. Moyoni alikuwa na mchanganyiko wa furaha na hofu baada ya tukio la jana usiku na Samweli.
Na alikuwa anatamani aweze angalau kumuona maana kashammisi jamani mapenzi bhana anyway tuendelee
Alifika mezani akiwa amevaa mavazi ya wahudumu , macho yake yakitafuta tu kiti cha kukalia lakini pia kwa ndani alitamani tu kumuona… Samweli
mtoto kapenda sana muombeeni na
samweli naye ampende pia ………
Na hapo sauti za hatua zilisikika zikipita na samweli alikuwa akitembea kuingia cafteria ……..
Samweli akiwa amevaa koti jeupe la udaktari, uso wake uking’aa kwa utulivu wa ndani, macho yake yakionyesha furaha yake kwa siku mpya Alipoingia cafteria, macho yake yalilenga moja kwa moja kwa Isabella, kana kwamba moyo wake ulimwita alitabasamu .
Lakini kwa isabela uchizi ndo
unampanda mpaka Tinna akamshtukia lakini macho yake kwa samweli ………
Waliangaliana kwa sekunde chache macho yao yakizungumza kuwa kuna kitu kitu wahindi wanasema ” KUCHI KUCHI HOTAE” , kama lugha ya wapenzi waliochelewa kukiri na kutubu hisia zao.
“Habari ya asubuhi, daktari,” alisema Isabella kwa sauti nyororo lakini yenye heshima ya ndani.huku akimtazama kwa tabasamu
Samweli alitabasamu, “Nzuri sana, lakini ingetimia zaidi kama ningeanza siku kwa kukaa na mtu spesho… kama wewe.”aliongea kwa utani ….
Isabella akacheka kwa aibu, macho yake yakishuka chini. Kisha akamuonyesha kiti kwa mkono wake.
“Wanaagiza nini wageni spesho hapa cafteria?” aliuliza Samweli huku akiketi.
“Leo tuna kahawa na maandazi,
chapati, supu ya ngombe na ya samaki na wali pia ,” alijibu Isabella, lakini moyo wake ulikuwa ukienda kasi .
Alikuwa akihema polepole, akihisi joto linalopanda mwilinii mwake.
Baada ya muda mfupi, Samweli akasogea kidogo karibu naye. “Isabella,” alisema kwa sauti ya upole lakini ya kina, “naweza nikawa nasoma mabandiko ya maumivu kwa wagonjwa, lakini macho yako yamenifundisha lugha nyingine… ile ya moyo.”
Isabella akatazama moja kwa moja ndani ya macho yake. Kisha akacheka kwa sauti sana mpka wahudumu na watu wengine wakageuka akaanza kuona aibu na kuziba mdomo . Kisha aliondoka na kukaaa akanywa chai ila macho yake kwa isabella … Mpaka isabella anashindwa kufocus anashindwa kufanya kazi ……
************
Mariamu naye alikuwa akiendelea na matibabu hospitalini hapo mara ghafla akaambiwa kuna mgonjwa anaumwa sana na ni mtu anayemjua
sana.Mariamu alitoka mbio mbio
kuwahi chumba maalamu alipofika mule alitahamaki sana baada ya kumuona yule mtu
Allkuwa akicheka na kusema kumbe wewe ni muoga lakini alichokifanya mariamu ni kumkumbatia tu ……
Nakusema “umeniogopesha sana ,my love nimeogopa jamani”
“nilikuwa nakusuprise mpenzi , nipo hapa mama yangu mgonjwa”
” kiss me baby” “nikukiss wapi jamani” “hapa mdomoni “
Kelvin alimshika shingo mariam
nakuanza kumpa alichoomba walipigana makisss sana kila mtu akionyesha hisia mpaka pale waliposikia kuna hatua za mtu zikipiga kuelekea kwao ……….
Waliachana kelvin alipita mlango mwingine na kweli aliyekuja alikuwa ni mganga mkuu..alipoingia alimwangalia mariamu kama kuna kitu amekiona hivi
Je amekiona nini usikose sehemu ya kumi na nne ya moto huu mkali wa mapenzi …….,
EPISODE 14
Dakika kadhaa baada ya mganga mkuu kuingia kwenye chumba maalum, Mariamu alijikuta akitetemeka kwa hofu. Hakuwa na uhakika kama amesikia au ameona kile kilichokuwa kikitendeka dakika chache zilizopita kati yake na Kelvin.
“Uko sawa Mariamu?” mganga mkuu aliuliza kwa sauti tulivu lakini yenye mashaka.
Mariamu alikuna kichwa huku
akijifanya anashughulikia kumbukumbu. “Ndio, nimeshtushwa
tu na hali ya mgonjwa… nilihisi kama ni mtu wa karibu sana,” alisema huku akihema.
Mganga mkuu alimtazama kwa muda, kisha akaandika kitu kwenye karatasi na kuondoka. Mariamu alipumua kwa nguvu. Sekunde chache baadaye, Kelvin alirudi kupitia mlango wa nyuma, na wote wakacheka kwa utulivu.
“Kama si wewe ni mwepesi,
tungeshikwa,” Mariamu aliongea huku akimkumbatia Kelvin tena kwa upole.
“Sio mimi tu… bali ni moyo wangu unajua pa kutorokea penzi lako,” Kelvin alijibu kwa kicheko.
Wakawa wanashikana wanakumbatiana yaani mapenzi moto moto wanatazamana wanabembelezana yaani penzi jipya kama hujalipitia pole nakupa pole sana … Tuendeleee na utamu wa kigongo. Mwishowe ilibidi kelvin
aondoke angalau mariamu afanye kazi
sasa……
Lakini kila mtu hataki kumuacha mwenzake jamani mkipendana hata muda wa mapenzi hautoshi kabisa …
**************
Upande wa Gabriel…
Baada ya kutoka hospitalini akiwa amechanganyikiwa, aliamua kwenda kwa Olesta. Mvua ndogo ilikuwa ikiendelea kunyesha, lakini mioyo yao ilikuwa na mawingu mazito zaidi.
Alipomwona Olesta, moyo wake
ulipata faraja. “Olesta… siwezi tena. Kila ninayempenda anampenda Kelvin. Mbona mimi ni wa kukataliwa tu?”
Olesta alimshika mkono na kusema, “Gabriel… si wote duniani wanampenda Kelvin. Kuna mmoja anayekupenda ni mimi na bora tupendane tu mi na wewe maana sasa hakuna namna kabisa kelvin nimemkosa nawewe mariamu umemkosa bora unipende mimi .”
Walitazamana kwa sekunde kadhaa,
na kimya kilizidi kusema zaidi ya maneno. Walikumbatiana kwa muda mrefu, na kwa mara ya kwanza Gabriel alihisi pumziko la kweli. Na aliona hamna namna zaidi ya kuianza safari na Olesta j
Unaweza ukashangaaa kwanini watu waliyokuwa hawapendani kabisa wamekubaliana na kuwa pamoja jibu ni rahisi sana ni kwa sababu mapenzi ya kweli yanatengenezwa hayapatikana na hayauzwi kama maembe vitunguu mtu mnaweza msipendane lakini mwisho wa siku
kwa kadri mnavyoishi mtajikuta
mnaanza kupendama na kudumu mwanzo ndio shida inayofanya watu waamini watu wanaanza kujuana ndiyo kupendana jamani tusikalili…….
Basi hapa ndio safari ya olesta na Gabriel ikaanza rasmi na ndio mapenzi yameshaanza kati yao…..
*************
Kwa upande wa Isabella…
Baada ya tukio na Samweli kwenye cafeteria, moyo wake haukutulia.
Hakuweza kufanya kazi kwa utulivu,
kila mteja akimuuliza alikosa majibu
sahihi. Rafiki yake Tinna alimuuliza, “Mbona leo hauko sawa, Isabela?
Moyo wako uko wapi?”
Alijibu kwa sauti ya chini, “Kwa Samweli…”
Tinna alicheka, “Sema basi kama umeanguka kichwa kichwa. Lakini kuwa makini naye. Mapenzi ya hospitali huwa hayaponi haraka yakiumia.”
Isabella alimkumbuka Samweli
alivyozungumza naye kwa upole, macho yake ya dhati, na namna alivyomchekesha. Kwa mara ya kwanza, alihisi kuwa labda mapenzi haya yameiva kweli.
Kwa upande wa Samweli…
Baada ya kutoka cafeteria, alisimama nje ya hospitali na kufikiri:
“Isabella… kwa nini siwezi kuacha kufikiria kuhusu yeye? Nilishapitia mahusiano mengi lakini hili ni tofauti.”
Aliamua jioni ile amtafute Isabella
azungumze naye zaidi. Hakutaka tena kuchelewa kuonyesha hisia zake.
Usiku huo huo…
Gabriel akiwa nyumbani kwake aliandika ujumbe mfupi kwa Kelvin:
“Samahani kwa ngumi ya jana, nimezidiwa na hisia pamoja na hasira . Sikutaka tufike huko. Peace bro.”
Kelvin alitabasamu baada ya kuusoma. Aliandika jibu,
“Tunaweza kugombania mapenzi,
lakini tusigombane urafiki. Nitakuja kukuona kesho, rafiki yangu.”
Basi ndo wanaume walivyo huwa hawaweki visasi sana kidogo washapatana kabisa yaani mambo safi basi walisameheana ma urafiki wao ulikuwa imara sana na walikuwa washasameheana kabisa .
*******
Basi yule malaya wa mtaa kwa jina la Lucy alikuwa anaonekana anakimbizwa na mawanamke mmoha kwa jina la Vicky au muite mama
Neeema baada ya kumfumania na
mume wake . Lucy alifanikiwa kuchoropoka akiwa kavaa tu kufuri na mbele yake anakutana na samweli .
Samweli anashangaaa sana .
” Enheee na wewe na chupi zako umetoka wapi”
“aaaaaaaah aaaaah jamani hakuna kitu ata”
Nafanya mazoezi” “Mazoezi na chupi kweli”
“Bhana weeeee acha na mimi sawa” kisha akaondoka mbio mbio …….
Samweli alicheka na kusema
“mmmmh kumbe huyu dada ni malaya ningejichanganya tu ningekuwa nishapotea” naye akaondoka zake …
********
Huku olesta na Gabriel wametoana out huko mapenzi yamekorea watu wanapendana from zero to hero watu wako kwenye mapenzi mazito kila mtu akionyesha hisia za dhati kwa mwenzake yaaani penzi bam bam
penzi limenoga na wanapendana sana lakini sehemu hiyo hiyo ndio
wamekuja kelvin na mariamu hatimaye wanakutana na wote walionekana kupokeana na kusherekea pamoja kila
mti kinyongo kimeisha ….watu
wanasherekea
Lakini upande mwingine isabella na samweli nao wapo kwenye matembezi lakini kuna ukimya kila mtu akionyesha kuna kitu anataka kusema mwisho samweli alimshika mkono isabella na kila mtu akiwana hisia na furaha na mwenzake yaani kifupi wanapendana lakini mdomo mzito kilo mia hamsini
wacha tukutane katiKA FINAL EPISODE TUJUE NINI KITATOKEA KWA
MAHUSIANO HAYA MATATU NA NINI
KITATOKEA KWA LUCY BINTI MALAYA
Episode 15
Usiku ulikuwa umetanda juu ya kijiji cha Matema, anga likiwa safi, nyota zikimetameta kama ushahidi wa miujiza ya mapenzi inayochanua kwa kasi ya ajabu. Lakini pamoja na utulivu wa mazingira, mioyo ya baadhi ya vijana ilibeba chembechembe za hofu, furaha, na maamuzi mazito.
Kelvin na Mariamu walikuwa wamesimama karibu na ziwa, wameshikana mikono hawa wapendanao waliokwishavuka misitu ya lawama na mto wa mashaka. Kelvin alimtazama Mariamu kwa macho yaliyojaa upendo wa dhati.
“Najua tulianza kwa utata,” alisema kwa sauti ya chini, “lakini Mariamu, siku zote moyo wangu ulikupenda.
Naamini hata dunia ikigeuka, bado nitakupenda.”
Mariamu alinyamaza kidogo, machozi
yakimtoka kwa upole. “Kelvin… umenifanya niamini kuwa mapenzi sio tu hisia, bali ni safari. Na kama hii ni safari, basi nataka iwe na wewe.”
Walikumbatiana kwa nguvu, huku mawimbi ya ziwa yakipiga mwamba kwa upole, kana kwamba nayo yanashangilia muungano wao.
Upande wa Gabriel na Olesta, mapenzi yao yamekolea kwa kasi. Walikuwa wamekaa kwenye mwinuko mdogo uliotazama kijiji, wakiangalia
taa za mbali kutoka kwa nyumba za
watu na kucheka kwa bashasha.
“Gabriel,” Olesta alisema, “naona hatukuwa tumeumbiwa kuanza kwa haraka, lakini tuliumbwa kumalizia pamoja.”
“Hata mimi naona hivyo,” Gabriel alijibu, “ulikuwepo wakati nikiwa nalia, na sasa uko hapa nikiwa natabasamu. Sikuwahi kudhani kuwa nilichokuwa nikikikimbia, ndicho kingekuwa faraja yangu.”
Walikumbatiana kwa upendo,
wakapiga picha ya ‘selfie’ kwa simu ya Olesta, kisha wakaiangalia kwa bashasha.
“Hii picha ni ushahidi,” Olesta alisema, “kuwa hata vumbi likikaa, ukweli wa moyo hubaki.”
Kwa upande wa Samweli na Isabella, kimya kilichokuwa kimewatawala hatimaye kilipasuliwa na ujasiri.
Wakiwa wamekaa kwenye kibanda cha mbao kilichopo karibu na fukwe,
Samweli alimshika Isabella mkono na
kusema kwa sauti iliyojaa uaminifu:
“Isabella, siku hizi chache umekuwa zaidi ya rafiki. Nahisi moyo wangu unakuona kama sehemu ya maisha yangu. Sipendi tena kukaa kimya.”
Isabella alitabasamu, macho yake yakiangaza kwa furaha. “Mimi pia Samweli. Nilikuwa naogopa… lakini sasa naona wazi kabisa, moyo wangu haupo tena peke yake.”
Walikumbatiana kwa hisia kali,
wakisahau kila huzuni waliyopitia kabla ya hapo. Majira yao yalikuwa yamefika.
Na kwa upande wa Lucy…
Siku iliyofuata, kijiji kilikuwa kimetulia kwa kawaida yake. Lakini Lucy alikuwa kimya sana tofauti na kawaida yake.
Alikuwa amevaa gauni ndefu la heshima, kichwa chake kikiwa kimefunikwa kwa ushungi mweupe. Alienda hadi kanisani akaingia ndani, akakaa mbele kabisa, macho yake
yakiwa yametazama msalaba kwa
huzuni kubwa.
Mchungaji alimuona akilia kimya kimya na akamfuata baada ya ibada.
“Lucy,” alisema kwa upole, “unaweza ukazungumza nami?”
Lucy alitikisa kichwa. “Mchungaji… nimechoka. Nimechoka kuwa mtu ambaye kila mtu anamcheka. Najua nimeharibu, lakini natamani kubadilika. Nataka maisha mapya.”
Mchungaji alimtazama kwa huruma.
“Hakuna anayekamilika, Lucy. Na kila mtu anahitaji nafasi ya pili. Mungu hakumtupa hata mwanadamu wa kwanza alipoanguka.”
Lucy alilia kwa sauti, na siku hiyo ikawa mwanzo wa mabadiliko yake makubwa. Alianza kujitolea kusaidia wagonjwa hospitalini na kutafuta kazi ya heshima.
Siku mbili baadaye…
Watu wote wa kijiji waliitwa kwenye
uwanja wa wazi, kwa ajili ya sherehe kubwa ya upatanisho na maamuzi ya maisha mapya.
Mwenyekiti wa kijiji alisimama na kusema, “Leo ni siku ya furaha.
Tumeshuhudia vijana wetu wakipigania, wakilia, lakini hatimaye kupenda kwa dhati. Leo tunasherehekea siyo tu mapenzi, bali ushindi wa mioyo iliyoamua kusamehe na kusonga mbele.”
Kelvin alisimama huku akiwa
amemshika Mariamu mkono, Gabriel akiwa amemshika Olesta, na Samweli akiwa na Isabella. Wote walitabasamu mbele ya watu, kila mmoja akiwa tayari kusema neno.
Kelvin alichukua kipaza sauti. “Nimejifunza kuwa mapenzi ya kweli hayajifichi kwenye urembo au pesa, bali kwenye moyo unaochagua kusamehe. Leo, namchagua Mariamu, sio kwa sababu ya tulivyopitia tu, bali kwa sababu ni mwanamke ambaye moyo wangu umeamua.”
Gabriel naye akasema, “Nilipendwa na mtu ambaye sikuamini anaweza kunipenda. Leo natangaza wazi,
Olesta ni moyo wangu.”
Samweli alitabasamu. “Nilidhani ni mwanamke mwingine tu wa hospitali. Lakini kumbe ni sehemu ya maisha yangu. Isabella, nakupenda.”
Kijiji kililipuka kwa furaha, watu wakipiga makofi, wengine wakitoa machozi ya furaha. Hali ilikuwa ya upendo uliokomaa.
Siku mbili baadaye…
Harusi ya pamoja ilifanyika. Kelvin na Mariamu, Gabriel na Olesta, Samweli na Isabella wote waliamua kufunga ndoa kwa pamoja, tukio ambalo halijawahi kutokea Matema.
Lucy alikuwepo kama mgeni wa heshima, akiwa ameandaliwa hotuba fupi. Alisimama mbele ya umati akiwa na amani isiyoelezeka.
“Nimefanya makosa. Lakini moyo wa binadamu sio wa kuhukumu, bali wa
kuelewa. Leo nimeona kuwa mapenzi
si maneno tu, ni matendo ya kweli. Nawapongeza wote waliopenda kwa dhati.”
Alimaliza kwa kusema, “Na mimi, nitapenda kwa kweli siku moja. Sio kwa mwili, bali kwa heshima.”
Muziki ulipigwa, watu wakacheza, machozi yakamwagika kwa furaha, na kijiji kikafunikwa na baraka za mapenzi yaliyoshinda mitihani.
Na ndivyo hadithi ya “PISI YA KIJIJI” inavyofika mwisho…
Mapenzi yamekamilika. Maadui wamekuwa marafiki. Waliochukiwa wamegeuka wapendwa. Na kila moyo umepata mahali pa kupumzika.
Kwa wote waliopitia mateso ya mapenzi, hadithi hii inasema:
“Moyo ukiamua kupenda, haujali jana lilitokeaje. Hujali watu wanasemaje.
Moyo wa kweli hupenda, husamehe, na husonga mbele.”THE END.”