Tukiwa Kitandani, Alikuwa Akinibadilishia Njia, Na Kuniwekea Kinyume Na Maumbile
Kaka Habari za majukumu……, Naomba unipostie kwa fans wako wanipe ushauri maji yamenifika shingoni. Ni story ndefu ila naombeni ushauri wenu.
Naitwa…… naishi Kahama ni mwajiriwa nina umri wa miaka 38 ila mahusiano kwangu yamenikataa kiasi cha kujikatia tamaa maana hadi sasa nimeoa na kuachana na wanawake watatu ambapo ni mmoja tu niliyezaa naye mtoto mmoja ambaye ni wa kwanza.
Huyu wa kwanza ilikuwa enzi za ujana baada ya kumpa ujauzito tulipeleka mahari kwao nikaanza kuishi naye lakini baada ya mtoto kukua alienda masomoni Dar es salaam miaka mitatu na mtoto nilimpeleka kijijini kwa wazazi wangu. Akiwa masomoni tulikuwa tukipishana kauli mara kwa mara na mara kadhaa nilisafiri kwenda Dar es salaam kuonana naye lakini alikataa na baada ya kuona amebadilika sana nilianzisha mahusiano mengine.
Mahusiano ya mwanamke wa pili yalidumu miaka zaidi mitano alikuwa ni mwalimu huko Njombe ila shida ikawa hashiki ujauzito. Kwa sababu kipindi namuoa nilimkuta ana mtoto na mimi pia nina mtoto tulishauriana nimchukue yule wa kwangu akakae kwake. Ugomvi ulianzia siku nimeenda Njombe na kukuta mwanangu amechoka na hana nuru kabisa, kachakaa hana viatu wala nguo zinazoeleweka licha ya kumtumia pesa za matumizi ila yule wa kwake alikuwa anatimiziwa kila anachotaka wa kwangu aligeuzwa house girl. Kitendo kila kilisababisha nimchukue mwanangu na kumrudisha tena kijijini na hapo ndipo chanzo cha mafarakano kilipoanzia hadi kuachana.
Mwanamke wangu wa tatu nilikutana naye chuo nilipoenda kujiendeleza huko Morogoro (SUA) tulipendana sana na alikuwa akinitii hadi nilianza kujutia kuchelewa kuonana naye na mwisho tulienda kwao nikamtolea mahari wazazi wao wakaniambia niwe na subira amalize masomo maana alikuwa mwaka wa mwisho.
Baada ya kumaliza chuo tukaanza kuishi pamoja (naombeni mniwie radhi hiki nitakachokieleza) baada ya kiishi naye takribani miezi zaidi ya 6 ndo nilikuja kugundua changamoto aliyokuwa nayo alikuwa anamchezo wa kufanya kinyume na maumbile na hadi kujua ilikuwa hivi, mara kadhaa tukiwa kitandani alikuwa akinibadilishia njia kuniwekea kinyume na maumbile (nadhani mmenielewa) kitendo kile kilikuwa kinanipa shida sana maana kila akiniwekea huko nikishahisi hali hiyo jogoo anaishiwa pawa nikimuuliza anajifanya kakosea kwa bahati mbaya na kuniomba nimsamehe.
Iliendelea hivyo hadi nikawa napoteza hisia naye. Baadae alikuja kusema ukweli kuwa yeye alishazoea na alianza mchezo huo muda sana so bila kupita njia hiyo hajisikii kitu na mimi nilimwambia huko sipawezi. Kwa kuwa sikuwa nikimridhisha njia hiyo ya kando alianza kutoka nje ya ndoa.
Ninavyozunguza sasa siko naye alienda kwao na mimi ile hali imenishinda. Ndugu zangu naombeni ushauri wenu ni mimi mwenye changamoto au hao wapenzi niliokutana nao sio sahihi kwangu? Nampende sana ila hiyo hali nashindwa kuivumilia japo kuwa yeye anaomba arudi kwa madai ameacha.
Nisaidieni nifanyeje?????

