BABA MDOGO ALINIBAKA NA KUNITOA USICHANA WANGU PORINI
Naomba unipostie kwa fansi wako labda nitatua mzigo mzito kichwani mwangu
Mimi ni mtoto wa pili kati ya watoto nane wa wazazi wetu nikiwa mdogo nilikuwa natatizo la kuumwa na kupelekwa hospital na baba kulazwa bila mama, mama alibaki nyumbani nilipofika darasa la nne nilipona nikawa siumwi tena, mimi nilikuwa nampenda sana baba yangu, ila nilianzwa kutengwa na wazazi wangu na kaka zangu walikuwa wakinipiga sana kila siku nikisema kwa wazazi hawaguswi
Nilipofika darasa la 6 baba aliniambia mimi sio mwanae sijui alichokuwa anamaanisha nini ila alisema hivyo nililia na sikuuliza maswali baba akawa ana niambia unasoma utafika wapi na nani atakae kusomesha nikawa mnyonge sana hata shule niliiogopa sana nilianza kufanya vibaya nakumbuka hata walimu wa ile shule walikuwa wana maneno ya kunikatisha tamaa sana niliendelea kusoma huku nikiwa nawaogopa walimu wote
Na nilipofika darasa la 7 baba alirudia kauli yake ya wewe sio mwanangu sitaki kukuona kwangu mama yangu alikuwepo na hakuwa anasema kitu chochote kile ila yule mzee alinichukia bila sababu , mtihani wa la saba nilifeli na nilipo chaguliwa kwenda shule nyingine hawakushughulika..
Baba aliongea na jirani nikatafutiwa kazi ya mgahawa nikaenda kufanya hela wanachukuwa nilifanya mwezi yule mama akasema mimi ni mdogo natakiwa kwenda kufanya kazi za ndani kulea mtoto nilienda maana kichwani ile roho ya mimi sina nyumbani ilikuwa inanisumbua nilifanya kazi mwaka na miezi mitano nalipwa 30000 kwa mwezi yule mama akasema ananiwekea hela nilifanya hiyo kazi toka 2014 hadi 15
Nikarudi kinacho shangaza nilipewa 70000 na mwajiri wangu zingine zote alisema amempa baba na sijui kama ni kweli maana nilikuwa namuogopa baba nikimuona.. nilirudi nyumbani na ile hela yote nilimpa mama aniwekee mwisho aliniambia sijamlipa malezi kwa hiyo hawezi nirudishia hiyo hela nikabakiwa sina kitu
Mimi nikiwa nyumbani nilikuwa nafukuzwa usiku na baba na kuambiwa asinikute, baba alinitafutia kazi nyingine na alinipeleka mwenyewe kwa hapo nilikuwa na miaka 15 nilifanya kazi mama ntilie nalipwa 2000 kwa siku ikawa kila siku nikutuma hela nyumbani
Baada ya ya miezi mitatu.nilianza kupoteza hela.kila hela ninayo shika inapotea mpaka nilipofika 2016 mwezi wa nne boss wangu alinirudisha nyumbani na kuwaambia wazazi mimi nina mimba, wakati anasema hayo hata mwanaume simjui kiukweli kutoka moyoni nakumbuka binti wa yule mama ndio alikuwa halali nyumbani
Baba na mama hawakuniuliza ni walianza wee malaya…. njoo unywe maziwa mtoto akuwe nilipitia magumu sana nililia bila msaada sina wa kumwambia ninayopitia ndugu zangu wana pendwa kwanini mimi kila siku matusi nikienda kanisani mama anasema fulani umetoka kanisani au kufanya umalaya na Jumapili kanisani wanaenda inaumiza sana baada ya miezi miwili nikiwa nimetoka kanisani saa kumi na mbili jioni kwetu sisi ni kijijini na kuna miti ya mbaazi nilikutana na baba yangu mdogo alikuwa anaelekea kwetu
Tulifika karibu na korongo nilikuwa simuogopi maana kwangu ni sawa na baba cha ajabu aliniziba mdomo na kunivutia korongoni na kusema piga kelele nikutupie korongoni alinibaka na kunitoa usichana wangu porini alivyomaliza akaniacha hapo na kuondoka ,nililia sana sikuwa na wakusema nilichechemea na kwenda nyumbani mama akauliza nimefanyaje wala baba ningemwambia nani maana ni aibu kufanyiwa hivyo
Wazazi wenyewe wapo kama hawajnizaa nilitaka kufa kila siku niliwaza kufa niliondoka nyumbani kwenda Moshi kwa bibi na nilipofika kule baada ya muda nilitaka kuwa na mtoto ili nikifa niache uzao kikwetu ukifa bila mtoto wana kufanyia ukatili nilijenga uhusiano dhumuni likiwa ni mimba na kweli nilijikuta nina mimba na nilirudi nyumbani ili rasmi wakalee matunda ya midomo yao
Tumbo lilikuwa dogo hakuna aliyejua niliporudi nyumbani mwendo wakufukuzwa na kulala nje uliendelea na kama unavyojua vijijini unakutana na vitu vingi sana nililala nje mara tano mpaka kumi kwa mwezi na sikuwa muhuni nikifukuzwa nalala nje ya mlango ,nakumbuka mimba yangu ikiwa na miezi nane na wiki moja ndio ilianza kutokea kwa mbali mama.aliona siku moja nikiwa nimevaa tisheti laini akauliza mbona pamejichonga nikamwambia mama nina mimba alishtuka akaondoka ,
Baadae alimwambia mume wake na kesho yake baba akasema nenda kwa baba mtoto wako nimekulea mwenyewe sio natakiwa kulea jeshi sikuondoka ,siku moja baba alisema hata nikikuta umeshikwa na uchungu sitakuinua hapa kweli baada ya muda mfupi niliumwa uchungu nakumbuka baba alikuwepo mama alikuwa ameenda mjini baba ana ona kabisa nalia ila anasema nikapike chai
Siku hiyo uchungu ulikaa mpaka alipoondoka kwenda mjini na mama akarudi nyumbani.. mama alinipeleka.hospitali na nilijifungua salama na ule uchungu ulinipa nafasi ya kuishi na nilimlea mwanangu nikiwa na wiki mbili baba aliniambia nitoke nikawakatie ng’ombe wake majani mama akamwambia mzazi anawezaje kukata majani?
Nililea mtoto alipofika miezi mitatu nikaanza kufukunzwa nyumbani… nilipitia changamoto,mpaka mtoto alipofikisha mwaka mmoja na miezi mitatu baba alinifukuza na rungu siku hiyo na nililala na mwanangu nje siku tatu mimi sijui kwanini mama alikuwa hanitetei ila mara nyingi nikifukuzwa na mtoto ataweka chakula juu ya bati au popote ukiona ule baada ya hapo nilimwambia baba mwanangu anatakiwa kukua kwa amani sio kuona haya mazingaombwe nikweli umefanya vingi ila sijawahi kukuchukia ninacho jiuliza baba yangu ni nani? ila kwa kuwa mlinilea bado nipo hai mtabaki wazazi wangu
Niliondoka niliwaachia mtoto nikaenda kufanya kazi nikawa nikipata 70000 ,natuma laki moja na kuendelea toka hapo nimekuwa nikituma pesa zote za mshahara, mwanangu ametimiza miaka miwili nikamfuata ila baba na mama wakasema wanampenda mwanangu niwaachie maana sitaweza kutafuta hela na mtoto kilichoniumiza nguo nilizo mwacha nazo ndio nilizomkuta nazo hakuna anachonunuliwa kwa hela ninazotuma sikuwa na cha kuuliza maana watoto wao wana soma vizuri na baba alipataga ajali hivyo hasaidii nyumbani
Kwanza hata ukimwambia uliwahi nifukuza anakuuliza lini ,nilimwacha mtoto na amelelewa nyumbani naenda kumuona mara mbili kwa mwaka ,na leo hii ni miaka nane kilichonifanya nije kwenu ni kwamba nimechoka sana mwaka wa nane sijajinunulia hata nguo mwaka wa nane huu sijui kula vizuri mwaka wa nane mwanangu hanunuliwi nguo wakati kila mwezi ukifika hata kama nalipwa laki mbili mama atapiga simu atakwambia matatizo yao yote na hesabu inakuja kwenye hela uliyonayo na mimi nina roho ya huruma sana lazima nitume kama ni kubakiwa labda 20 na nikimtaka mtoto wangu hawanipi, kaka yangu mdogo aliwahi niambia kuwa mama amesema nikimchukuwa mtoto sintarudi nyumbani na hawata pata hela
Na mimi nahitaji kuwa na maisha yangu sitaki tena kuwa mtumwa nikiwa na hela wanacheka na mimi ila nikiwa sina natukanwa si kitu nikiona simu ya nyumbani ujue ni wanataka hela kujua naishi wapii naendeleaje sio jukumu lao natamani kuwa na biashara yangu na ndoto zangu pia ,kwa njia yeyote nisaidieni kujua ni jinsi gani nitatoka huku nina miaka 25 mwanangu ana miaka 8
nishaurini ,nikipi nikifanye nitoke kwenye kifungo hiki na unavyo ona kweli kuna mzazi anaweza fanya haya?
Nishauri pia kaka yangu nifanyeje maana wadogo zangu wakiwa na shida napewa mzigo niwabebe na sijawahi waacha lakini mimi hata wasikie nimelazwa hawatingishiki nishauri nifanyaje hii nyimbo ya mimi sio mtoto wao initoke?

