Mke Wangu Alimuua Mwanangu, Nikamtetea Asifungwe, Leo Najutia
Mimi nilifiwa na mke wangu kipindi anajifungia ila mtoto yeye alibaki, mtoto tulimlea Kwa shida sana nikisaidiana na mama yangu na ndugu zangu hasa dada zangu mpaka akakua.
Baada ya miaka mitano niliamua nioe mwanamke mwingine, Sasa nilivyo muoa akawa anasema siyo vizuri yeye awepo halafu mwanangu aendelee kuishi Kwa mama yangu mzazi, baada ya kuona anasisitiza hicho kitu niliona acha tu nikamchukue mtoto aje tuishi naye.
Mwanzoni mtoto aliishi vizuri tu, shida ilianzia pale mke wangu alipo pata mtoto wakwake, ndo nikaanza kuona mabadiliko Kwa mwanangu, mtoto alianza kuwa mnyonge sana, nikawa najitia moyo labda ni Kwa sababu mama yake Kwa Sasa upendo ame ugawa Kwa watoto wawili, Kila nikiondoka na kurudi safari namkuta mtoto kanyongonyea sana, nikikaa naye kumuuliza Nini shida Hasemi.
Kuna kipindi nilisafiri kwenda musoma, jirani akanipigia simu akaniambia huyu mtoto Bora nimpeleke sehemu nyingine mana hapa naona atakuja kuwagombanisha, nikamwuliza kwani Kuna shida gani? Hakusema, nilivyo rudi nyumbani nilikuta Hali ya mtoto ikiwa inazidi kuwa mbaya, siyo kwamba ni mgonjwa, hapana Bali upole ulikuwa umezidi kitu ambacho siyo kawaida yake, siku hiyo nilimchukua nikaenda naye sehemu nikamnunulia vitu vingi Ili ale lakini alikula kidogo tu akaacha, nikawa namuuliza Nini shida mwanangu? Unaumwa? Anajibu, hapana. Mama yako anakupiga? Hajibu chochote.
Mwisho nilipanga nikitoka safari awamu nyingine nimrudishe Kwa mama mana niliona mtoto sasa anaelekea sehemu mbaya sana, haongei na muda wote kajitenga.
Mwezi wa tatu mwaka huu nikiwa safari mke wangu alinipigia simu kuwa mtoto wangu kalazwa eti alidondoka kwenye mpapai, nikamuuliza kuhusu Hali yake akasema siyo nzuri, siku hiyo hiyo nikawa najiandaa Ili kesho yake nirudi nyumbani, mida ya jioni ndo jirani akanipigia simu akanieleza tukio Zima, walisikia mtoto akipigwa siku tatu nyuma, toka siku hiyo hawakumuona tena mtoto hata akienda shule hivyo kipigo Cha mama yake ndo sababu ya kulazwa Wala siyo kudondoka.
Nilivyo rudi nilienda hospital Moja Kwa Moja, dakitari alinipa majibu kuwa mtoto kaumia sana kifua na mbavu upande wa kushoto zime bonyea, ilibidi nirudi Kwa mtoto nikawa namwuliza mwuliza pale na mwisho ndo akaniambia ni mama yake kampiga na huwa anampiga mara Kwa mara.
Bahati mbaya jioni ya siku hiyo hiyo mwanangu alifariki, niliumia sana mpaka Leo, najiona kama Mimi ndo niliye muua mwanangu,
Baada ya kifo Cha mwanangu majirani walitaka wakamshitaki mke wangu nikawaomba waache, niliwasihi sana na nikawaomba mwanangu azikwe tu, wao waliendelea kusema waende polisi lakini nilijaribu Kwa Kila namna Ili waache na mwisho wakanielewa, mwanangu akazikwa.
Leo hii natamani ni Bora kipindi kile ningeruhusu mke wangu akafungwa, Kwa anayo nifanyia ni basi tu.

