Nilipata Mali kwa Njia ya Kishirikina, Leo Sijui Nifanye Nini
Dada yangu habari, nilikuwa naomba wewe unishauri au unipostie.
Mimi 2014 nilienda Kwa mganga, kipindi hicho Mimi na wenzangu tulikuwa tuna fanya kazi migodini, kweli pesa tulipata nyingi sana, Yani namaanisha tulikuwa matajiri kabisa.
Mganga alitupatia masharti mepesi tu, alituambia kama umeoa hakikisha kama ni kutoka nje ya ndoa usizidishe Mchepuko mmoja, Mimi badae nilikuja nikawa siendi tena Kwa huyo mganga Ili nijifute niache kuishi Kwa masharti, kweli niliacha na pesa zilizidi kuwa zinakuja tu ndo nikawa najiaminisha kuwa kumbe hata nikiwa na wanawake zaidi ya watatu hakuna shida.
Mwaka juzi 2023 nakumbuka ilikuwa siku ya pasaka nikatongoza mwanamke mmoja hivi, nikalala naye, Yani baada ya kumaliza tu mke wangu akanipigia simu mtoto kadondoka, Mtoto tulimpeleka hospital akakaa ICU miezi minne, Yani toka siku hiyo mwanangu viungo vyote havifanyi kazi licha ya kwamba anapumua lakini Kila kitu anamalizia hapo hapo alipo lala.
Ilibidi nirudi Kwa mganga mwaka Jana, mganga alinitukana sana na kunifukuza ila ikabidi nitulie pale pale na nililala nje, nilimbembeleza sana ila mwisho akanisikiliza, alinipa sharti na dawa Moja, sharti ni kuwa ni lazima nilale kimapenzi na dada yangu, na inabidi nimueleze ukweli, nikifanikiwa hivyo mtoto anakuwa mzima na Kila kitu kitakaa sawa.
Dada Mimi Toka mwaka jana nashindwa nianzie wapi kumueleza dada yangu, Kila nikitaka kujaribu napata hofu sana, na mwanangu anateseka sana na Hali yangu ya maisha inazidi kuwa mbaya imefikia hatua hata hela ya kula ni shida kupata dada yangu.

