SITASAHAU JINSI MZUNGU ALIVYOTUTUMIKISHA KINGONO, MIMI NA MUME WANGU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Sehemu Ya 1
Naitwa Rosemary ni mama wa mtoto mmoja anaitwa Jack.Kwasasa sina mume kwani mume wangu alifariki toka mwaka juzi na alifariki kutokana na tamaa zake pengine ambapo ilinisababishia mpaka mimi niingie katika mkumbo wa hatari na kuiandika historia ambayo haiwezi kusahaulika katika maisha yangu.
Nakumbuka mambo yalianza kama mzahamzaha vile ila tukajikuta mimi na mume wangu tunaingia kwenye mtego ambao hatuwezi kutoka.
Ilikuwa ni jioni moja mume wangu aliporudi kazini kwake ambapo yeye alikuwa dreva tax akaniita sebuleni baada ya kuwa nishamtengea chakula ale na nakumbuka kipindi hicho mwanetu alikuwa na miaka miwili. “Mke wangu za kushinda”.
“Nzuri tu mume wangu” Niliitikia lakini Kwa mshangao kidogo kwani mume wangu alivyorudi tayari tulishasalimiana.
“Mke wangu unayaonaje maisha yetu?”. Ili swali lilinishangaza kidogo maana nikama halieleweki vile anamaanisha nini?
kuwa maisha yetu yakoje Kwa maana ipi? Ikabidi nimjibu tu hivyohivyo. “Mazuri tu mume wangu”. “Mmh ,Haya ni maisha mazuri Kweli wakati kuna muda mwingine tunakosa hata pesa ya matibabu ya mwanetu akiugua ghafla”.
“Kwa maisha tulionayo ni kumshukuru Mungu tu kwani nashukuru mume wangu toka umenioa sijawahi shinda na njaa,Na hayo mengine ni majaliwa tu ya Mungu Ila nashukuru sana mume wangu unaipigania sana familia yako”
Ilibidi nimpe moyo mume wangu maana alionyesha nikama mtu anayeyadharau maisha tulio kuwa nayo. Basi hapo nikamuona ni kama amekosa neno la kuongea baada ya mimi kuonyesha kuwa maisha tuliyonayo sisi mbona mazuri tu kuna watu wana Hali mbaya kuliko sisi.
Ila bado nikamuona nikama anatafuta maneno ya kuniambia lakini anakosa hivyo akaamua kuropoka tu ni kama Kwa hasira tu .
“Kwa hiyo umeridhika mwenyewe na maisha haya,Kumbuka kigari chenyewe kinachotuweka mjini ni cha watu mwenyewe akikitaka muda wowote tumeumbuka”.
Hapo nikashtuka kidogo ikabidi nimuulize “Mume wangu Leo una nini wewe mbona unaongea maneno ambayo hayaeleweki”
Hakunijibu kitu bali aliendelea kula kisha tukaingia kitandani kulala huko napo hakawa halali muda wote alikuwa akinitazama tu yahaani ni kama anataka kuniambia jambo anashindwa nami nikamuacha tu aendelee kusitasita Ila mwishowe akaropoka. “Mke wangu nikwambie kitu?”.
“Niambie”Ilibidi nimgeukie Kwa hamu na shauku ya kujua nini anataka kuniambia maana Leo toka amerudi amekuwa wa tofauti sana.
“Mke wangu Leo nimepata zari au naweza kusema tumepata zari la kutoka kimaisha”. “Zari lipi hilo mume wangu?”.
“Leo nimepata mzungu”.
Hapo nikawa sijamuelewa kwasababu kwa namna kazi yake jinsi ilivyo kumpakia mzungu ni kitu cha kawaida kwasababu yeye ni dreva taksi na anapaki maeneo ya feri ambapo kunaboti kutoka Zanzibar zinashusha watu mbalimbali ikiwepo wazungu hivyo kumpakia mzungu si jambo la ajabu la kunihadithia.
“Kivipi ,Nawe mume wangu si kila siku unapakia wazungu wewe”. “Hapana sio kihivyo,bali nimempata mwanamke wa kizungu ananitaka kimapenzi”.
Hilo neno lilinishtua sana maana sikutarajia kuwa anaweza akaniambia kitu cha kipuuzi kama hicho nami ni mke wake wa ndoa.
“Kwa hiyo unaniambia ili iweje”
Nilijikuta nimepaniki kidogo.
“Ni hivi mke wangu hii ni nafasi yetu ya kutoka kimaisha” “Kutoka kimaisha?”
Nilishtuka kisha kuendelea. “Mzungu ana mahusiano vipi nawe kutoka kimaisha”.
“Ni hivi ,Yule mzungu anapesa na kaniahidi kama nikimuoa basi atanipeleka Sweden”
“Kwa hiyo Lengo lako ni kututelekeza mimi na Jack?”Nilimuuliza Kwa hasira maana nilishaona huyu mwanaume yuko tayari kutelekeza Familia kwa sababu ya pesa.
“Hapana,Sina lengo hilo,Kwani hata mzungu mwenyewe nimemwambia nyumbani nina dada yangu anamtoto ananitegemea Kwa kila kitu hivyo nimemuomba nisafiri naye”.
Hapo aliniudhi kuliko maelezo yahaani kanitambulisha kwa mwanamke wake wa nje kama dada hali ya kuwa ni mke wake wa ndoa kabisa tena kanisani.
“Kwa hiyo umenitambulisha dada Kwa mwanamke wako,hivi we una akili timamu kweli?”Ilibidi nihoji uwezo wake wa kiakili.
“Sikiliza mke wangu,Usipaniki sana ebu fikiria namna ya kufanya ili tusipoteze dili hili”.
Bado tu aliendelea kunisisitiza ili nimkubalie maombi yake.
“We ni mpuuzi kweli ,hivi umeniletea mada kabisa ya kipuuzi kama hii na unataka tuijadili”Nilibwata kwa nguvu na kwa hasira huku nikimsukuma maana alikuwa kama amenikumbatia fulani hivi ili anieleze upuuzi wake. Wakati nimemsukuma,mtoto akaamka na kilio,
Nafikiri nikutokana na yale makelele yangu ndio yalisababisha mtoto aamke.
Basi nikamchukua Mwanangu na kutoka naye sebuleni kuanza kumbembeleza,mume wangu nilimuacha kitandani akiwa hana la kunieleza tena maana nikama ameumbuka hivi.
Nilimbembeleza Mwanangu lakini nikagundua ana joto kali mno ilibidi nirudi tena chumbani kumueleza baba yake hali ya mtoto ilivyo.
“Baba Jack, Mwanao homa imempanda tena”.
“Eehee ,Mungu wangu we tumeumbuka,Unajua mama Jack Leo nimerudi na shilingi elfu tano ambayo nilitegemea kesho ndo nikuachie pesa ya kula”.
“Ebu acha zako wewe,Leo si umejifanya umewapakia wazungu,Hao wazungu hawajakupa madola”.
“Ni hivi Leo wakati narudi nimepata mtihani wa kukamatwa na askari hivyo pesa imenitoka nikabaki na pesa kidogo nimepitia sheli kuweka mafuta ya kesho na ichi ndo kiasi kidogo kilichobaki kwaajili ya kesho”.
“Basi tumuwaishe kwanza mtoto hospital ya kesho tutayajua kesho hiyohiyo”.
Basi tulitoka hima hima mimi na mume wangu mpaka kwenye kizahanati kilichopo karibu,kumuona daktari tu ni shilingi elfu kumi nasi tuna elfu tano tu ,basi ikabidi tuombe hivyohivyo tukafanikiwa kumuona daktari tukamueleza tatizo la mwenetu huku tukidhani ni homa ya kawaida tu maana wiki iliyopita tulimkimbiza mtoto kwenye zahanati hii hii huku akiwa na homa kali hivyo wakamchoma sindano za kushusha homa na kutushauri tufanye baadhi ya vipimo lakini sisi tulikimbia kutokana na ukata,
Tukajinunulia vidonge vya malaria na kutuliza homa na kumpatia mtoto na hali yake ikatengemea kumbe ilikuwa kwa muda tu sasa Leo limetokea tena la kutokea ikabidi tumuwahishe zahanati ileile na bahati nzuri tulimkuta daktari yuleyule. Basi daktari kwa haraka sana akampokea yule mtoto maana nilimuona kabisa anatufanyia ubinadamu tu maana anajua hali yetu halisi,Wiki iliyopita tulikimbia matibabu na Leo kuanza na kuanza tu tumeshindwa kulipa hata gharama ya kumuona daktari.
Daktari alimkagua Jack kisha kutuliza
“Hii hali ya kupumua Kwa shida imeanza lini”. “Ni kama siku tatu hivi,Ila Kwa kuwa hana homa ilibidi tumuache tu”.
“Haraka muwaisheni hospitali ya Temeke muombe rufaa apelekwe muhimbili akafanyiwe vipimo Kwa hali yake ilivyo huwenda pua zake zimeziba au moyo wake mkubwa hivyo anahitaji kufanyiwa vipimo haraka ili ijulikane tatizo ni nini? Pia oparesheni ifate haraka msije mkampoteza mtoto”.
Basi hao mbio mbio kuelekea hospitali ya Temeke huku tukiwa hatuna hata shilingi mia mfukoni. Tulifika hospitali ya Temeke tukaambiwa Jambo la kwanza linalohitajika ni kadi,
Tumchukulie mtoto Kadi mapokezi,kitu ambacho kilihitaji pesa na sisi tukawa hatuna hata mia,Wakati huo nilimuona mume wangu akiwa anaangaika kupiga simu huku na huku huku akionyesha kuchanganyikiwa akijaribu kuomba msaada Kwa Ndugu na jamaa wajaribu japo kumsaidia pesa kidogo lakini ilikuwa tabu mno kupata msaada na kwa bahati nzuri ndugu yake mmoja akamtumia shilingi elfu 30.
Tulifanya taratibu za kimatibabu pale Temeke na baada ya hapo tukapata rufaa ya kwenda muhimbili na wakati huo elfu 30 yote ilishapotea palepale Temeke imebaki shilingi elfu moja tu huku mume wangu akiwa anaumiza kichwa huku akiendesha gari kuelekea muhimbili.
“Yahaani hiyo elfu 30 ,tumeipata Kwa mbinde,Sijui huko muhimbili tunaanzia wapi?”.
Kwa sababu nilishuhudia kabisa akiwapigia simu karibia rafiki zake na ndugu zake wote, pia hata ndugu zangu pia na kuambulia elfu 30 kwa mbinde nikajua huko tunapokwenda muhimbili hakuna matumaini kabisa ya kupata msaada ikabidi nimuulize
“Yule mzungu wa mchana ulimpeleka hoteli gani?”
. Mume wangu alinitazama kwa huzuni kisha kunijibu. “Hata mimi nilikuwa nafikiria hivyohivyo,Ila sikupanga nikuhudhi bali nilitaka nifanye siri”.
Aliongea Kwa uchungu sana huku machozi yanamtoka kisha akaendelea kusema
“Nasikitika sana mke wangu Rosemary nimekuangusha sana katika maisha, Wewe ni mwanamke mrembo sana hata ukiachika na mimi unaweza ukampata mwanaume wa maana kuliko mimi,Mwanaume mpiganaji kuliko mimi nahisi kama nakupotezea muda wako tu”.
Aliongea kwa huzuni sana kiasi hata mimi kuniliza kwani nampenda sana mume wangu.
“Usiseme hivyo mume wangu mi mwenyewe naona bahati kuolewa na wewe,Mwanaume uliyekamilika haswa mkweli na unaipigania familia yako,
Matatizo katika maisha ni jambo la kupita tu,Usijidharau sana mume wangu unanihudhunisha hata mimi, Cha msingi tumpambanie mwanetu kwanza”. Basi uelekeo wa gari ulibadilishwa maana tulishafika
“Fire”Ilikuwa ni hatua chache tuingie kwenye Kona ya muhimbili lakini yeye akabadilisha uelekeo na kuelekea maeneo ya posta mpya ambapo ndipo kuna hoteli aliyofikia yule mzungu. Tulipaki kwa nje kisha mume wangu akampigia simu yule mzungu maana alimpa business card yake.
“Kiukweli,Mke wangu roho inaniuma pia naona aibu mara mbili kwako na kwake,Kwanza naona aibu kwako Kwa kukusaliti mbele yako yahaani nampigia simu mwanamke mbele yako kisa pesa alafu mimi ndiye mwanaume unayenitegemea,Pili namuonea aibu huyu tunayempigia simu kwani nimekutana naye Leo Leo na namlilia shida Leo leo”.
“Usijali mume wangu,Jikaze wala usione aibu ,we fikiria tu Afya ya mtoto”.Maneno yangu yalimfanya mume wangu (Frank) amuangalie mtoto Kwa majonzi mazito huku simu yake ikiwa masikioni tayari ameshampigia mzungu.
“Hallow”. “Hallow”. Simu ilipokelewa na mzungu. “Nani mwenzangu?” Mzungu alikuwa anaongea Kiswahili safi,Huyu anaonyesha amekaa sana Afrika Mashariki hasa Dar es salaam, Zanzibar na Mombasa ndo maana Kiswahili chake kimenyooka.
“Frank Yule Dreva taksi” Mume wangu alijitambulisha. “Aahaa Frank ,
Tayari sasa ushakuwa na jibu langu”. “Ndio ninalo jibu lako ,lakini ninashida kidogo naomba utoke hotelini nipo kwa nje tuongee”.
“Woow, Umekuja kunitembelea? Nakuja haraka nisubiri” Mzungu alikata simu kisha akaanza kushuka hotelini.
“Samahani,Mke wangu nitakutambulisha kama dada yangu “.
Alisema hayo wakati tunamsubiri mzungu nami nikamjibu.
“Usijali mume wangu, La muhimu mtoto apone”. Basi mzungu alifika Chini na mume wangu akatoka kwenye gari ili kumpokea,Mzungu alipomuona tu mume wangu alimkimbilia na kumkumbatia,Kwa kweli niliumia sana ila iliniuma zaidi
Mzungu akampa na mate mume wangu mbele yangu hapo roho iliniuma sana ila ikanibidi nijikaze nisiwaangalie bali akili yangu niielekeze kumuangalia mtoto. Baada ya makisi yao ya hapa na pale mume wangu alimshika mkono na kuja naye yule mzungu kwenye gari hapo mimi nikajiongeza kwa kupita siti ya nyuma,Yeye na mzungu wake wakakaa siti za mbele.
“Ana Maria naomba nikutambulishe Kwa dada yangu kipenzi na mwanaye, Dada yangu anaitwa Rosemary na mwanaye anaitwa Jack”.
“Woow ni vizuri kuonana,Mi ni mchumba wa kaka yako ,hivyo wewe ni wifi yangu”
Naye alijitambulisha huku akinipa mkono kama ishara ya urafiki,nami nikaupokea mkono Ila cha ajabu alivyonishika mkono hakunishika kikawaida bali alikuwa kama ananipapasa vile mimi nikajikuta namshangaa huyu mzungu vipi kisha akaongezea.
“Dada yako ni mzuri sana, Inaelekea familia yenu wote ni wazuri ,Kaka mzuri na Dada mzuri”.
Aliongea hayo huku akiniangalia Kwa macho ya mahaba mpaka nikaona aibu ikabidi nitazame chini kumuangalia mwanangu huku nikiutoa mkono wangu kwake Kwa nguvu ambao bado alikuwa kaushikilia huku anauchezeachezea
Bado mzungu aliendelea kuniangalia kwa jicho la tamaa na aliponiona na muangalia mwanangu aliamishia mada kwa Mwanangu “Mwanao,Anaitwa Nani?”.
Hapo mume wangu akadakia “Anaitwa Jack” Ndipo Yule mzungu aligeuza macho yake kwa mume wangu kumuangalia aliyemjibu.
“Mwanae anaumwa,Nami sina pesa ya kumpeleka hospitali hivyo nimeona bora nikushirikishe ili uweze kunisaidia”. Hapo mzungu ndo akawa kama kachochewa kuniangalia kwa tamaa na kuniangalia akaona haitoshi akaibetua siti na kupita siti ya nyuma kabisa ambapo nipo mimi nimemkumbatia Mwanangu ambaye alikuwa amelala.
Nilipomuona anakuja nilitetemeka sana nikaanza kuhofia anataka kufanya nini huyu? Alipofika akamchukua mtoto kutoka mikononi mwangu.
“Ana joto sana,Tumuwahishe hospitali” Aliongea hayo mara tu baada ya kumpakata mwanangu na kumkagua kichwani.
“Frank ,Fanya haraka tuwahi hospitali” Mzungu alijifanya anahofu kubwa kuliko hata sisi. Basi mume wangu akaondoa gari kuelekea hospitali huku mimi na Mzungu tukiwa siti ya nyuma ,Mimi nikiwa na muhofia Mzungu anataka kufanya nini huyu?
Wakati namuhofia hivyo nikamuona Mzungu kachukua mkono wake mmoja na kuniwekea mapajani kwakweli sikuweza kuutoa kwani niliamini kama nitautoa au nitamzuia Kwa namna yeyote basi kunaweza kuzuka ugomvi ambao utapelekea tukose msaada kabisa .
Basi niliuacha mkono wa Mzungu uwe juu ya mapaja yangu ambapo nilikuwa nimevaa sketi fupi inayoishia magotini yeye alivyoona hapati upinzani mkono wake kuwa juu ya mapaja yangu akasonga mbele zaidi.
Akaupeleka mkono wake kwenye magoti yangu ambapo akaivuta sketi yangu na kuacha mapaja yangu kuwa wazi kisha akaweka mkono wake tena juu ya mapaja yangu na kuanza kuyatomasa taratibu hapo nikaona ujinga nikaukamata mkono wake taratibu na Kwa upole nikautoa kwenye mapaja yangu kisha kurudishia sketi yangu ilivyo.
Basi nilipoutoa mkono wake juu ya mapaja yangu akahisi nimekasirika hivyo akaanza kuniuliza maswali ya hapa na pale huku akijichekesha. “Mwanao,Ana umri gani?
“. “Miaka miwili”Nilimjibu lakini sikutaka kumuangalia usoni maana ukimuangalia usoni ni wazi unamuona mtu anakutamani isivyokawaida. “Nawe una miaka mingapi?”.
Maswali yake yaliniboa Ila sikuwa na jeuri ya kuacha kuyajibu kwasababu huu ndo ulikuwa msaada pekee tunaoutegemea.
“Namiaka 26”. “Woow Mimi ni mkubwa kwenu Mimi namiaka 30 hata Frank naye kaniambia yeye anamiaka 28”. Alijichekesha kidogo kisha akaniuliza swali “Unaogopa Sana kuhusu Mwanao kuumwa?
” Kwakweli maswali yake yalikuwa yanaboa hivyo nikaitikia Kwa kutikisa kichwa tu. Basi hapo hapo mkono wake akaupitisha kiunoni kwangu na kunipapasa nikataka kuruka lakini akaniambia maneno ambayo ni kama fumbo vile
“Kuwa mtulivu wala usiogope ,Kwa gharama yeyote nitahakikisha Mwanao anatibiwa na kupona
“.Basi ikabidi niwe mtulivu tu nimuache anichezee kiuno anavyotaka yeye huku mi mawazo yangu yakiwa juu ya mwanangu licha ya kuamini kuwa mzungu ni kama ananidhalilisha vile alikuwa ananishikashika kiuno huku akijifanya yupo bize anaongea na Frank mambo mbalimbali. Basi tulifika hospitali mzungu aligharamia pesa nyingi mpaka tukapatiwa chumba cha binafsi (Private room) na vipimo vya moyo na pua kuziba viliendelea kwa Jack ambapo pia ilipaswa tusubiri siku moja au mbili ili kupata majibu ya vipimo hivyo ilipaswa kulala pale hospitali.
Baada ya vipimo vyote na matibabu kidogo ya kumuweka mtoto katika hali nzuri wakati akisubiria majibu ilifika hatua sasa inabidi tulale palepale hospitali na mtoto.
Mimi kuwa pale hospitali kama mama na mtoto si tatizo Ila Tatizo lilikuja kwa mume wangu yeye naye alitaka kulala pale ili kuangalia afya ya mtoto lakini Mzungu akatoa ushauri.
“Inapaswa alale mmoja,Ili mwingine aje kesho kumpokea mwenzake maana hamuwezi kujua kuwa mtoto atalazwa kwa siku ngapi hapa maana vipimo tu tumeambiwa siku mbili Je matibabu Je?
Hivyo Frank arudi kulala kesho aje kukupokea”. Hilo nililiafiki lakini kimoyomoyo nikawa napata presha kuhusu huyu Mzungu maana simuamini sana kitabia ni kweli anaongea kwa nia ya dhati kuwa nilale mimi peke yangu?au analengo lingine la kulala na mume wangu leo?
Dah maana hata akilala naye anajua mimi yule ni kaka yangu tu,
Je mume wangu anaweza asinisaliti kweli usiku wa Leo mbele ya Mzungu?
Je huyu Mzungu anania gani mbona alinishikashika sana kwenye gari, anania nzuri kweli huyu?
Hayo ndo maswali niliyokuwa najiuliza nikiwa hospitalini huku nikiwasindikiza kwa macho mume wangu na Mzungu wakiwa wanaondoka hospitalini
Sehemu Ya 2
Kilichoendelea baina ya mzungu na mume wangu usiku ule sikutaka kujua na wala sikutaka kufahamu ila walirejea wote asubuhi ya saa kumi na mbili mida ya kuwaona wagonjwa wakiwa na uji wa mtoto, Mzungu alijisifia kuwa huo uji ameuandaa yeye hii ilinipa wasiwasi kidogo kuwa hawa watu wawili walilala sehemu moja au asubuhi ndo walipitiana hilo sikulijali lakini mume wangu alikuwa hawezi kunitazama machoni ni kama vile ananionea aibu hii ikanipa wasiwasi ikabidi nimvute chemba kidogo huku nikimuacha Mzungu anamnywesha uji mtoto. “Vipi,Jana umenisaliti wewe?” Nilimuuliza mume wangu ambaye alikuwa hawezi kabisa kuniangalia usoni kutokana na aibu. “Nisamehee mke wangu nisingeweza kukataa, Si unajua kitanda anacholalia Jack ni elfu 30 Kwa siku na bado kuna gharama kibao kama nikimzingua huyu Mzungu tumekwisha”. Roho iliniuma sana ila nikajikuta sina la kufanya zaidi ya kuwa mpole ila machozi yalinitoka kidogo nakujikuta nauchukia umasikini. “Nisamehee mke wangu kama nimekuumiza” Alinifuta machozi nami nikamjibu kumpa moyo. “Usijali mume wangu,Cha msingi ni kuhakikisha Jack anakaa sawa hayo mambo mengine ni ya kupita tu”. Basi tulirejea chumbani ambapo tulimkuta Mzungu kashamaliza kumywesha uji mtoto na sasa anacheza naye. Tulikaa pamoja huku Mzungu akiwa ndo muongeaji mkubwa maana binafsi sijawahi kukutana na Mzungu anaongea kama huyu yahaani utafikiri mzaramu kila jambo anajua yeye. Muda wa kuona wagonjwa uliisha nami nikataka niendelee kukaa lakini Mzungu akatoa wazo “Safari hii muache Frank akusaidie kumuangalia mtoto mpaka saa kumi wewe unapaswa urudi nyumbani ,ukaoge na kubadilisha nguo,pia kupumzika ili ujiandae na kibarua cha usiku tena”. Wazo la Mzungu halikuwa baya ni wazo zuri hivyo lilipita lakini sina uhakika kama ili wazo alilitoa Kwa nia njema au anayake mengine. Basi Safari hii tulitoka Mimi na Mzungu pale hospital na kumuacha mume wangu na mtoto akaenaye hadi saa kumi nije kumpokea. Sikuwa hata na shilingi mia mfukoni ya nauli na nilipojaribu kumuomba nauli mume wangu aliniambia kila kitu hata maliza Mzungu maana hata yeye mwenyewe hakuwa na kitu mfukoni Jana walitoka yeye na Mzungu wakaenda kulala kwenye hoteli aliyofikia Mzungu hivyo hakupata hata muda wakutafuta pesa ambayo ingenisaidia Mimi kurudi nyumbani. Basi Kwa kuwa Mzungu kaamua kutusaidia na mume wangu kanipa ruhusa kuwa kila kitu atamaliza Mzungu basi ilibidi nitoke naye huku nikimtegemea nauli. Tulivyotoka tu hospitali Mzungu aliita taksi tupande mimi nikamwambia Mzungu. “Samahani Ana Maria naomba unisaidie kiasi kidogo cha pesa ili nipande daladala za kwenda kwetu mbagala”. “Hapana,Usiende mbagala muda huu saa kumi sio mbali ,Wewe unahitaji kurudi nyumbani haraka ,uoge na kupumzika kisha upike chakula cha kuleta hospitali ukirudi mbagala utakosa muda wa kufanya yote hayo hivyo twende hotelini kwangu”. Maneno yake yalinipa mshtuko kidogo nilitamani kusema hata hapana lakini nikakumbuka sina hata hiyo nauli ya kwenda mbagala na hata nikienda naenda kufanya nini maana sina hata pesa ya kupika kwaajili ya mgonjwa pesa zote zinapaswa zitoke Kwa Mzungu na Mzungu mwenyewe ndo hivyo anasema niende hotelini kwake. Basi tukapanda kwenye taksi huku moyo ukinidunda maana huyu Mzungu Jana tu kwenye taksi ya mume wangu kanishikashika sasa ananipeleka hotelini kwake tunabaki wawili unafikiri itakuwaje ikabidi nitafute namna ya kumkwepa huyu Mzungu. “Lakini Ana Maria, Tafadhari naomba uniruhusu nirudi kwetu mbagala maana hata nikija kwako nikaoga nitakosa nguo za kuvaa”. “Usijali ,Mimi ninazo nguo nyingi ukioga nitakupa za kubadilishia” Alisema hayo kisha akanichungulia nikiwa siti ya nyuma yeye yuko siti ya mbele na dereva alafu akanipa ishara ya kunibusu na mkono,Dah Kwakweli alinichanganya maana sikujua amekusudia kunifanya nini huko hotelini hali ya kuwa yeye ni mwanamke mwenzangu.
Basi tulipofika hotelini tulishuka kwenye taksi,Mzungu alikuwa na furaha isivyokawaida alichukua mkono wake mmoja na kunishika begani tukawa tunatembea kuelekea hotelini anapoishi. “Jisikie huru” Mzungu aliniambia maana nilijisikia aibu kubwa hasa tulipokuwa tunaingia hotelini watu wote walituangalia sisi huku mimi mikono yangu nikiwa sina namna ya kuiweka maana mzungu amenibana na kifua chake na mkono wake amenivutia Kwa kwake huku tunatembea yahaani ni kama mtu na bwana wake. Basi hao tuliingia chumbani Mzungu akajitupia kitandani. “Jisikie huru,Rosemary kama unahisi uchovu unaweza ukaenda kuoga kisha kupumzika ,bafu ilo hapo” Mzungu alinionyesha bafu kwa ishara ya mkono ,kisha akajifanya kulalamika kama mtu ambaye anauchovu mwingi sana “Ooh my God am so tired”. Mimi baada ya kuonyeshwa bafu lilipo ilibidi niingie ili nikapate maji maana nilijihisi mwili unanata kutokana na uchovu. Basi niliingia bafuni na kuvua nguo zote kisha kufungua bomba la mvua na kuanza kukoga maji nilijisikia raha sana maana maji yalikuwa ni kama ya uvuguvugu hivyo nikajiachia kwa maraha kufurahia maji yanavyotiririka kwenye mwili wangu lakini ghafla nikaona mlango wa bafuni unafunguliwa nilipata mshtuko atakuwa ni nani? Ila swali lilikuwa ni la kitoto sana kwani awe nani zaidi ya mzungu?Ndio ni kweli alikuwa ni mzungu tena akiwa uchi wa mnyama huku akiwa amezishika taulo mbili mkononi. Nilitamani kuacha kuoga na kuvaa haraka haraka lakini sikuona sababu ya kufanya hivyo kwani Mzungu ni mwanamke kama mimi tofauti tu ni rangi zetu.Mzungu alifungua mlango kisha akaniangalia alafu akatabasamu “Rosemary umesahau taulo za kujifutia”. Baada ya hapo Mzungu aliingia bafuni kisha kuweka taulo sehemu ya kichuma cha kuwekea taulo na kuja huku akiwa uchi wa unyama akinifata nilipo ,uso wake ulijawa na tabasamu muda wote hali iliyoanza kunisababisa nianze kumuogopa tena hasa nikikumbuka matukio yake ya kwenye gari,Nikataka kutoka kwenye bomba la mvua ili nikajifute na taulo nitoke lakini mzungu akanidaka mkono. “Ushamaliza kuoga kwani?” Aliniuliza huku akiniangalia kimahaba zaidi yahaani ni kama mtu anayetaka kunirukia. “Ndio”Nilijibu huku natetemeka. “Yahaani sabuni zote kwenye nywele alafu unasema ushamaliza kuoga”. Basi nikaweka mkono kichwani ili kuhakikisha kweli nywele zina sabuni lakini hamna kitu. “Hamna bwana”. Nilimjibu huku akiwa bado kaendelea kunishika mkono kisha akanivuta kuelekea bomba la mvua. “Mimi ndo nakuona kichogoni kuwa unasabuni,Basi acha nikuogeshe kama umeshindwa mwenyewe kuoga”. Mzungu aliniweka katikati ya bomba la mvua kisha kuanza kunipaka sabuni “Kiukweli mi sijazoea kuogeshwa naomba uniruhusu niende sipo comfortable na hili” Nilimwambia kisha kutaka kuondoka lakini alinikumbatia Kwa nguvu alafu akanizuia palepale kwenye bomba la mvua kisha kuanza kujiliza hapo nikamshangaa analia nini ikabidi nimcheki kama yupo sawa “Ana Maria upo sawa kweli”. “Sipo sawa”.Alijibu huku bado akiendelea kulia huku kanikumbatia. “Unaumwa?” Nilimuuliza. “Hapana siumwi ila nimemkumbuka marehemu dada yangu,yeye alikuwa ananikogesha kila siku tafadhari Rosemary naomba uchukue nafasi yake,Naomba unikogeshe”. Hapo nikaona isiwe tabu kama shida tu ni kumkogesha basi acha nimkogeshe.Nikachukua sabuni kisha kuanza kumpaka sabuni kichwani hapo nikaona kaniachia nikampaka maeneo yote ya mwili wake huku ila kila nikimgusa sehemu muhimu lazima atoe milio ya mahaba dah kwakweli ilikuwa ni mtihani sana siku hiyo . Baada ya kumaliza kupaka sabuni na kumsuuza na bomba la mvua akaniambia. “Rosemary tafadhari naomba unisugue na mgongoni” Sikuwa na hiyana maana ni mgongo basi nikamwambia ageuke lakini ajabu alijipindua kabisa kama mkao wa mapenzi eti madai yake nimsugue vizuri ,Mimi Sikuwa na hiyana nilimsugua anavyotaka na mara nyingi sasa ilipaswa niyaguse makalio yake Kwa sehemu yangu ya mbele ili niweze kuufikia mgongo wake vizuri na mara zote alitoa miguno ya mahaba. Zoezi la kumsugua mgongo wa Mzungu liliisha akaniambia. “Samahani kama nakuchosha Ila pia naomba nisugue na matakoni vizuri”. Basi nikawa namsugu huku yeye akijiliza kimahaba na baada ya muda mfupi Mzungu alikuwa yuko safi nishamkogesha vizuri Ila akanikumbatia tena kisha kuniambia kimahaba huku jicho lake likiwa nyanya (Yahaani limezingirwa na machozi”. “Samahani naomba na wewe nikukogeshe “
Kabla sijajibu chochote mzungu alishachukua sabuni na kuanza kunipaka kichwani.Nikataka nijikomboe kwenye mikono yake lakini akanitaiti kabisa na mwili wake ili nisichomoke basi nikaona isiwe tabu kama shida ni yeye kuniogesha tu basi acha aniogeshe.Alinipaka sabuni kichwani kisha akashuka kwenye maziwa hapo nikaona ameganda ameganda kwa muda mrefu kidogo anayachezea maziwa yangu huku anapaka sabuni ikabidi nimwambie. “Inatosha jamani”. Mzungu akatoa kilio cha mahaba. “Aahaa ” Alafu akasema Kwa tabu huku ananiangalia usoni kwa jicho la mahaba. “Nimeshindwa kujizuia Rosemary, Nakupenda sana tafadhari naomba uwe mpenzi wangu”. Hapo nikabaki nimemshangaa tu maana sikuwahi kutarajia kwamba eti siku moja naweza kuambiwa na mwanamke mwenzangu maneno kama Yale.Wakati mi namshangaa mzungu hakupoteza nafasi bali alinirukia mdomoni na kuanza kunipa mate sasa hapo ndo nikaona sasa amezidisha ujinga ikabidi nimsukume Kwa nguvu mzungu akaanguka kule nusu aende chini Ila akajitahidi kujizuia kwenye jakuzi asianguke chini.Mimi nikavaa nguo yangu niliyokuja nayo kisha kuanza kutoka bafuni.Mzungu akaniwahi “Sikiliza Rosemary unaenda wapi?” Sikumjibu kitu bali nikawa nautafuta mlango wa kutokea kwenye chumba chake “Rosemary,Naomba unisamehe” Bado siku msikiliza nilikuwa nataka nitoke nje tu sikujali nini wala nini maana niliona huyu mzungu ni mshenzi tu Jana kalala na mume wangu Leo anajifanya anataka kunisaga na mie. Sikumsikiliza nilitoka nje kwa hasira bila kuwaza nini wala nini kama umasikini acha nife na umasikini wangu kuliko kudhalilika namna Ile. Nakumbuka sikuwa na hata mia mfukoni wakati huo lakini nikajifanya masikini jeuri nikatoka mpaka kituo cha mabasi ya mbagala nikaomba msaada kwa kondakta anipakie bure naye akanisaidia nikafika mpaka nyumbani. Nilipofika nyumbani nikakopa baadhi ya mahitaji kwa mangi na kiasi kama cha shilingi elfu 10.Kwa kuwa mangi ananijua mimi sio mbabaishaji akanikopesha huku nikiwaza saa kumi ikifika nikamtoe mume wangu hospitali alafu nimwambie akapambane kutafuta pesa Kwa ajili ya matibabu aachane na habari za mzungu yeye ni mwanaume anapaswa kupambana sio kukaa na kumtegemea Yule Malaya wa kizungu. Saa nane kamili nilitoka mbagala kuelekea muhimbili Ila kutokana nafoleni za hapa na pale nikafika saa kumi na robo hivyo nikama nimechelewa robo saa tu kulingana na ule muda halisi wa kuona wagonjwa hivyo ilibidi niwahi mbio mbio mpaka kwenye chumba alicholazwa Mwanangu.Nikamkuta mume wangu kama amechanganyikiwa vile moja haikai wala mbili haikai yahaani anazungukazunguka kwenye kitanda cha mtoto ambaye muda huo alikuwa kalala. Nilipoingia tu mume wangu akanikumbati Kwa nguvu alafu akaniuliza ” Vipi Mzungu yuko wapi?”Aise aliniudhi sana sema tu nikajikaza. “Sijui ,mi nilipotoka hapa nilienda mbagala moja Kwa moja kwani vipi?”. “Majibu ya vipimo yametoka toka saa Saba na muda wote huo nimekupigia simu ili kukutaarifu majibu ya vipimo ikiwezekana umpitie mzungu uje naye lakini hukupokea,Pia nimejaribu kumpigia simu mzungu pia naye hakupokea hivyo ndo maana nimechanganyikiwa hapa”. Hapo nikajisachi mfukoni kuangalia simu yangu iko wapi ndipo nikakumbuka simu yangu nimeisahau hotelini,basi nikauliza Kwa woga “Majibu yanasemaje kwani?”. “Majibu yanaonyesha Jack ana moyo mkubwa,hivyo inahitajika akafanyiwe operation India au South Africa hapa hawawezi kufanya hiyo operation”. Nusu nianguke kwa presha maana hiyo pesa ya operation na nauli ya kwenda huko India sijui itatoka wapi maana msaada pekee tuliokuwa tunautegemea ni kutoka Kwa mzungu na mzungu mwenyewe ndo hivyo hapatikani kwenye simu na kutokana na nilivyomuhudhi huwenda ataki tena kutusaidia. Basi ikabidi niweke chupa chini nakutoka nje huku nakimbia kumuwahi mzungu hotelini asije akapata wazo la kubadilisha hoteli maana kama hapatikani kwenye simu maana yake hataki kuwasiliana nasi na yeye ndo tunayemtegemea kama ataondoka kabisa pale hotelini basi tutakosa msaada kabisa “Vip unaenda wapi?” Aliniuliza mume wangu wakati natoka lakini sikumjibu kitu bali nikukimbia tu ili kumuwahi mzungu kabla hajabadilisha hoteli Nilichukua bodaboda fasta mpaka hoteli aliyofikia mzungu ,nilishuka mbio mbio hadi chumbani Kwa mzungu kujaribu kufungua chumba kimefungwa,hivyo nikashuka mapokezi harakaharaka huku nikiwa natetemeka. “Hivi yule mzungu kaondoka?”. Nilimuuliza mtu wa mapokezi “Mzungu yupi huyo maana hapa wazungu ni wengi dada”. “Ana Maria”. “Ana Maria,Ana Maria”Alisema huku anapekuwa kwenye komputa. “Huyo ,kasharudisha funguo”. Basi moyo ukapiga paaha nikaanza kujutia kwanini nilimkataa huyu mzungu ona sasa mwanangu atakufa Kwa kukosa msaada nikajikuta nabubujikwa na machozi
INAENDELEA

