MWANAFUNZI MCHAWI
Sehemu Ya 11
Aliongia mdani na kukutana na ukimya mzito. Kwa ujasiri na kujiamini sana Doreen aliingia chumbani kwa Mwalimu Jason na kukuta harufu Kali ya damu na mwili wa mwalimu Jason.
Kwa wakati huo Judith alikuwa tayari amechapa lapa ili kuiepuka kesi ya mauaji ambayo ingemkabili. Na kama angekuwepo ndani mle basi ingekuwa nyama ya Doreen kwani angetumia vizuri nafasi ile kupata titi la Judith.
Doreen aliutazama mwili wa Jason kisha akaachia sonyo Kali. Akakisogelea kitanda na kutafuta karatasi lake, akalikuta chini ya mto. Akachukua na kulitia kwenye mkoba wake kisha akaondoka zake.
Akashika njia kuelekea kituo cha mabasi cha mkoani Iringa ili atafute gari liendalo mkoani Mbeya aende huko. Alipokuwa njiani alitazama pesa aliyokuwa nayo alishtuka kidogo kwani ilikuwa ni shilingi elfu moja tu ambayo haitoshi kwa lolote. Akawaza kwa sekunde kadhaa jinsi ya kufanya akapata jibu kisha akaendelea na safari yake. Alipofika mbele kidogo aliona duka kubwa limeandikwa Sanga Mini Market akaingia mle.
“Karibu! ” sauti ya mwanaume mwenye duka ilimkaribisha.
“Asante! Nataka pop corn moja!”
“OK.. Ya 500 au 1000?.”
“Nipe ya 500..” Alisema Doreen na alijua kabisa ana shilingi elfu moja. Lakini kuna kitu alitaka kufanya, alitaka kuiba pesa kwa kutumia ile shilingi elfu moja yake.
Mzee yule alitoa popcorn na kumkabidhi Doreen. Doreen alichukua shilingi elfu moja kwenye mkoba wake na kumpa Muuza duka. Muuza duka alipokea akataka kumrudishia chenji lakini ghafla akasita.
“We mtoto unanichezea? Hebu rudisha hizo popcorn… Shika hela yako.. Mpuuzi mkubwa wewe unataka kuniletea wanga wako hapa?” Alifoka muuza duka yule kwa jazba kwani alipoipokea hela ile akaugundua mchezo mzima wa Doreen aliotaka kuifanya. Doreen alishtuka, akaona aibu.
“Kwani vipi baba?” Alisema Doreen kwa upole kwani uligundua Mzee yule in kiboko zaidi yake.
“Wewe mtoto ntakuumbua hapa? Toka zako….” Mzee yule aliitupa chini hela Doreen na kumnyang’anya kwa nguvu ile popcorn.
“Unafikiri tunauza kizembe? Wachezee huko huko hii namba tasa sio shufwa..!” Alisema Mzee yule Doreen akiwa anaondoka. Doreen aliona aibu sana lakini hakukata tamaa kwani alijua tu atapata mtu ambaye hana zindiko lolote.
Uzuri wake uliwachanganya wengi sana kwani kila alipopita alikuwa akitazamwa kama nyota ya alfajiri huku wengine wakimpigia miruzi na wengine wakijaribu kumwita majina wanayoyajua wenyewe ili tu wabahatishe jina lake. Ni kweli Doreen alikuwa mzuri kupindukia, aling’aa kama m balamwezi ila tabia zake za ndani zilitisha zilokuwa mbaya kama Israel mtoa roho.
Alitembea taratibu na kuingia kwenye mgahawa mmoja wa vyakula. Aliketi kisha akaagiza chipsi kavu za shilingi mia saba.
“Sahani moja elfu moja?”
“Samahani Dada nina mia saba tu nisaidie.. Nimetoka mbali na nina njaa sana..!” Alisema Doreen kwa upole sana ambapo aliweza kumshawishi kirahisi muuzaji, akamkubalia kwa kumuonea huruma.
Watu walikuwa wengi mhahawani mle, Doreen alijiinamia chini tu akisubiri aletewe chipsi zake. Kwa muoneakano wa haraka ilikuwa vigumu sana kubaini tabia za Doreen kwani alionekana mpole na mkarimu sana.
Chipsi sake zikaletwa, ilibidi atoe hela na arudishiwe chenji yake. Chenji ambayo ilikuwa tofauti na kiwango kinachostahili.
*****
Ulimi wa Mwalimu John ulikuwa mzito kutamka neno lolote. Kila akijaribu kusema chochote maneno yalikuwa hayaeleweki ndipo mkewe akabaini kuwa tayari mumewe amekuwa bubu. Roho ilimuuma sana kwani mumewe asingeweza kufanya kazi tena. Wataishi vipi mjini bila kazi? Aliwaza mkewe.
Lakini licha ya kuumia moyo ila alimshukuru Mungu kwa uhai alioachiwa mumewe. Siku zikaendelea kusonga. Ilikuwa saa mbili usiku nyumbani kwa mwalimu John. Ukimya ulitawala sebuleni pale kwani ndugu wote walikuwa wameenda majumbani mwao hivyo walibaki wawili tu, ghafla mlango uligongwa.
“Karibu! ” alikaribisha Leyla mke wa mwalimu John. Bila kutegemea aliingia Judith, kwani alikuwa akipafahamu vizuri nyumbani kwa mwalimu John. Na hii ilitokana na ukaribu waliokuwa nao mwalimu John na Jason, hivyo mwalimu Jason alimtambulisha Judith kama mkewe mtarajiwa.
“Karibu..” Alimkaribisha Leyla.
“Asante.. Za hapa!”
“Nzuri kiasi.. Umefika lini?”
“Tangu juzi..” Alisema Judith lakini alionekana mwenye hofu na mawazo mengi.
“Karibu.. Ulikuwa kwa Jason?”
Swali like liliibua kumbukumbu ya tukio aliloshuhudia kwa mpenzi wake. Machozi yalimshuka kwa kasi, lakini alishangaa sana kwanini tangu amefika Mwalimu John hajasema lolote.
“Hamjasikia chochote kuhusu Jason?”
“Ndio.. Kwani kuna nini?” Alishtuka sana Leyla.
“Ni stori ndefu sana ila mwalimu Jason alijiua!”
“Ati nini?”
“Ndio.. Inaniuma sana… Alitaka kuniua Mimi lakini akabadili msimamo na kusema bora ajiue yeye..” Aliendelea Julia Judith
“Kwanini?”
“Alisema ana sharti la..” Kabla Judith hajaendelea….
MR ALOYCE alichanganyikiwa sana baada ya kukuta damu ikiwa imetapakaa sakafuni chumbani kwa mwanaye. Alipigwa na butwaa huku hofu ya kuondokewa na mwanae ikiwa imemvaa ghafla.
“Eeeddy!” Alijikuta anaita kwa sauti Kali ili kama Eddy yupo mbali asikie na aitikie wito ule ambao ungemwondolea wasiwasi Mr Alloyce. Lakini wito ule haukuitikiwa na mtu yoyote zaidi ya ukimya uliokuwa umetawala ndani ya jumba lile la kifahari.
Mr Alloyce alijaribu kuita tena na tena lakini bado hakuitikiwa. Simanzi ikamjaa tele, akajua tayari amepata pigo lingine zito kabla hata kidonda cha mwanzo hakijapona kwani ndio kwanza kilikuwa kibichi.
“We Mungu wangu nimekukosea nini Mimi mbona unaniadhibu hivi? Nihurumie uikomboe familia yangu” alilia mr Alloyce akiwa amejibwaga sakafuni kwenye korido ya kuelekea sebuleni. Machozu yalimchuruzika kama mvua huku yakiteremka kama vijito kuelekea kwenye marumaru za rangi ya maziwa zilizochanganyika na weupe.
“We Mungu nitaishi vipi Mimi na upweke huu? Sina mke, sina mtoto?” Alilalamika kwa majonzi mr Alloyce. Aliwaza mengi sana yaliyozidisha simanzi yake moyoni, moyo wake ukajawa na maumivu makali sana kama mtu aliyechomwa na mkuki wa moto katikati ya moyo wake.
“Bora na Mimi nife kuliko kubaki kwenye hali kama hii…!” Aliwaza Mr Alloyce kisha akainuka pale sakafuni na kuelekea chumbani kwake. Aliingia chumbani na kuwasha taa, kisha akaisogelea droo ya dressing table akaifungua na kuanza kupekuapekua vitu.
Alipekua kwa muda kisha akapata karasi ya ranging ya kaki akafunua kwa umakini kisha akazikuta dawa alizozihitaji. Kulikuwa na vidonge Vingi sana ndani ya pakiti ile kaki, akavibeba na kuirudisha droo kama ilivyokuwa akatoka kuelekea sebuleni.
Alifika sebuleni na kuliendea jokofu ili achukue pombe Kali anywe pamoja na vile vidonge ili aondokane na ulimwengu huu wa mateso ambao alihisi umemtenga baada ya kumtenganisha na wapendwa wake. Akiwa anafungua jokofu na kichukua chupa moja ya konyagi ghafla alishtuka sana.
*****
Dorice aliyastaajabu mazingira aliyopelekwa kwani palikuwa na viumbe wengi wa ajabu ambao yeye hakuwahi kuwaona hats siku moja.
Ulikuwa kama ukumbi mkubwa sana uliotawaliwa na viumbe wale wa ajabu, alipopiga jicho mbele ya ukumbi ule aliona viti viwili vyenye rangi ya shaba vikiwa vimetengwa peke yake. Alimtazama Mansoor kwa sura ya maswali lakini Mansoor hakuzungumza neno lolote zaidi ya kumshika mkono Dorice na kuongozana nae mpaka kwenye vile viti. Walipovifikia tu, ghafla akatokea kiumbe mmoja wa kutisha sana kwani alikuwa na macho kama ya bundi, meno marefu yaliyochongoka na kucha ndefu za miguuni na mikononi. Mwili wake ulitawaliwa na manyoya na kila alipozungumza kinywa chake kilitema moshi mweusi. Doreen aliogopa sana, akajikuta anamsogelea Mansoor kwa hofu.
“Usiogope Mpenzi… Huyu ni mfungishaji ndoa!” Mansoor alimtoa hofu Dorice. Dorice alibaki kimya huku moyo wake ukibaki na woga wa hali ya juu.
“Leo ndio ile siku tuliyoisubiri kwa hamu sana, hatimaye kijana wetu mtoto wa mtukufu malkia amepata mwenza wake wa maisha!” Alisema kiumbe yule wa kutisha. Radi Kali zilipigwa ishara ya kufurahia kile kinachozungumzwa.
“Bi Aisha utakuwa mke halali wa Mansoor… Kwa kuivaa Pete hii ambayo hutakiwi kuivua maisha yako yote.” Alisema kiumbe yule huku akimkabidhi Mansoor Pete nzuri sana ya dhahabu, iling’aa kupita kawaida.
“Nakupenda sana, nakuoa leo, naahidi kukulinda Siku zote kama mke wangu. Tafadhali sana usije ukaivua Pete hii hats Mara moja!” Alisema Mansoor na kumvisha Pete Dorice. Dorice alikuwa anaogopa sana, machozi yalimlengalenga machoni kwani hakuamini kama kweli anaolewa na jini. Ndoa ilifungwa na Dorice alipewa onto la kutoivua Pete yake ya ndoa hata Mara moja.
*****
Doreen alimkabidhi pesa ile muuz mgahawa kisha akaendelea kula chipsi zake kwa haraka sana utadhani anakimbizwa na polisi, hata kabla ya kumaliza akaziacha mezani pale na kumfuata yule mama muuzaji kisha akamdai chenji.
Mwanamama yule alitoa shilingi mia tatu kwenye pochi ndogo aliyokuwa akihifadhi pesa kisha akamkabidhi Doreen. Lakini cha ajabu baada ya kumkabidhi tu Doreen pesa zile, kitita cha pesa zote alizouza siku ile zikaenda kwa Doreen bila yeye mwenyewe kujua. Zilikuwa kama elfu sitini na tatu halafu yeye akabakiwa na shilingi mia tatu.
Doreen alipozichukua pesa zile akapiga hatua kubwakubwa kuelekea kituo cha mabadi kwani tayari alikuwa amepata nauli na pesa ya kutumia njiani kuelekea mkoani Mbeya.
Yule mama aliendelea na shughuli zake kama kawaida, alimhudumia mteja mmoja kisha mteja yule alimpa shilingi elfu kumi na akahitaji chenji. Bila wasiwasi mwanamke yule aliiendea pochi yake na kutaka kuchukua hela lakini alipoishika tu pochi ile akahisi kitu, maana pochi ilikuwa nyepesi kuliko kawaida. Alishtuka kidogo kisha akaifungua. Hakutaka kuamini macho yake kwa alichokiona.
“Hela zangu!!!!!!” Aliongea kwa mshtuko mkali kisha wote wakamtazama mama yule .
“Hela zaaangu mieee!” Alianza kushusha kilio huku akizitafuta huku na kule lakini hakuziona.
“Fety wapi hela zangu?” Mama yule alimuuliza mfanya kazi wake.
“Hela? Si uliziweka humo?”
“Ndio mbona sizioni sasa? Sema tu kama umechukua! Hakuna mwingine ni we we Fety..!’ Mama yule alilia huku akimkunja mfanyakazi wake akihisi ndiye aliyemwibia.
“Mama tangu lini nimekuibia?”
“Nani angechukua!? Nani nakuuliza?” Mama yule aliongea kwa hasira sana.
“Sio Mimi mama unanionea Bure..!”
“Na utanilipa shenzi wewe..!” Alizidi kumkunja.
“Labda umemzidishia yule mteja aliyeondoka?”
“Tutamfata kama si yeye utanikoma..!” Aliongea kwa hasira sana mama yule kwani mtaji wote alikuwa amechukua pesa za mkopo. Hivyo alichanganyikiwa sana.
Waliamua kumfuatilia Doreen kule alikoenda. …
.MR ALLOYCE alishtuka sana baada ya kusikia kishindo kalikali nyuma yake. Aliachia chupa ya konyagi kisha akageuka haraka kutazama nini kinaendelea nyuma yake. Hakuamini kumuona mwanaye akiwa amejibwaga chini kama gunia la viazi. Alikuwa anathema kupita maelezo.
“Eddy!” Mr Aloyce aliita kwa mshangao mkubwa. Lakini Eddy hakuitikia zaidi ya kuendelea kuhema kwa nguvu. Mr Alloyce alitupa chini vidonge alivyokuwa amevishika, akamwinamia Mwanaye na kumgusa kifuani ili kusikiliza mapigo ya moyo. Aligundua kuwa mwanaye ni mzima alimsgukuru Mungu. Killed home hang a za Mr Alloyce ni kwamba pindi anarudi sebuleni pale, hakukuta mtu yeyote na wala hakusikia mtu akifungua mlango.
“Ba…ba..!” Aliita Eddy kwa shida sana.
“Sema mwanangu…Mimi hapa” aliitikia Mr Aloyce.
“Usife. .!”
“Sifi nani kasema Mimi nakufa? Vipi lakini uko sawa?” Aliuliza mr Alloyce akiwa na hofu sana, alihofia kumpoteza mwanaye kipenzi. Eddy aliitikia kwa kichwa tu akimhakikishia baba yake kuwa yuko sawa.
Mr Alloyce aliendelea kumkagua Mwanaye kila sehemu akidhani labda ana majeraha kwani damu alizozikuta chumbani kwa Eddy zilimtisha Sana. Lakini alipomtazama mwanaye akagundua hana jeraha lolote mwilini mwake, hivyo maswali mengi yalijitokeza akilini mwake. Alijihoji maswali mengi lakini hakuwa na majibu yake.
“Baba… Mama anateseka sana!” Eddy aliongea sauti ndogo ya kujivuta sana akiwa bado amelala pale sakafuni.
“Anateseka wapi?” Mr Alloyce alishtuka sana.
“Alikuja hapa.. Anateseka sana na yote kwa sababu yangu…!” Alisema Eddy kwa huzuni sana huku machozi yakimlengalenga machoni.
“Eddy! Upo sawa kweli?” Mr Alloyce alihisi Eddy hayupo sawa hivyo anaropoka tu anachojisikia.
“Nimefanya makosa sana.. Namtesa mama yangu…”
“Eddy usiseme hivyo.. Unamtesa na nini?”
“Alivyotaka kunipeleka kwa mganga wameamua kumuadhibu…!”
“Kina nani?”
“Wachawi…!”
“Oh My God..”
Maneno Yale yalizidi kumchanganya Mr Alloyce, alishundwa afanyaje kwani ilikuwa ni Mara yake ya kwanza maishani mwake kukumbana na mauzauza ya namna ile. Mara nyingi alizoea kutazama kwenye luninga tu lakini hakujua kama inaweza kumtokea kweli. Maisha yake yalikuwa machungu ndani ya muda mfupi tu kwanu matatizo aliyokuwanayo yalikuwa mazito tena yanaumiza kama gunia la misumari.
“Baba.. Nakupenda..!”
“Nakupenda pia mwanangu!”
Mr Aloyce alijikuta anashusha mchozi tu kila anapomtazama mwanaye kwanu siku zote aliamini mwanaye atakuwa mtu mkubwa sana kutokana na uwezo wake darasani. Alikuwa na akili nyingi lakini Leo amekuwa mtu wa kuteseka tu. Aliwachukia wanadamu wenzake kwa ukatili wanaoufanya juu ya familia yake.
“Baba..”
“Naam mwanangu..”
“Chukua hii.” Eddy alimkabidhi baba yake kipande cha karatasi. Mr Aloyce alishtuka kidogo kisha akapokea karatasi like na kulikunjua ili alisome. Ujumbe uliokuwepo pale ulimshtua sana Mr Alloyce. Aliurudia tena”CHAGUA MOJA.
EDDY APONE TATIZO LAKE, MAMA YAKE APOTEE DAIMA. AU MAMA EDDY ARUDI, EDDY ABAKI NA TATIZO LAKE”
Mr Aloyce alibaki mdomo wazi kwa mshangao, kwani ule ulikuwa mtihani mgumu kwake.”Karatasi limetoka wapi?”
*****
Mama muuza mgahawa alikuwa kama mwehu baada ya pesa zake kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Aliambatana na mfanyakazi wake ili wamfate Doreen. Waliifuata njia aliyoelekea Doreen na kumtazama huku na kule lakini licha ya kumfuatilia kwa muda mrefu hawakufanikiwa kumuona. Walifika mpaka kituo cha mabasi kumtafuta lakini pia hawakumuona.
Sehemu Ya 12
Mama muuza mgahawa alikuwa kama mwehu baada ya pesa zake kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Aliambatana na mfanyakazi wake ili wamfate Doreen. Waliifuata njia aliyoelekea Doreen na kumtazama huku na kule lakini licha ya kumfuatilia kwa muda mrefu hawakufanikiwa kumuona. Walifika mpaka kituo cha mabasi kumtafuta lakini pia hawakumuona.
“Luna msichana alipita hapa, mweupe amevaa sweta jeusi na sketi ya kahawia?” Aliuliza Fetty mfanyakazi wa yule mama muuza mgahawa.
“Ni mzuri sana?”
“Ndio!”
“Alipanda basi la Mbeya na limeondoka!”
Aliwajibu kijana mmoja ambaye alionekana ni kondakta wa basi.Yule mama aliangua kilio kikali palepale kwenye kituo cha mabasi bila kujali wingi wa watu. Alilia kwa sauti Kali akiwa ameweka mikono kichwani. Watu walimshangaa mama yule wakaanza kumkusanyikia.
“Hela zaangu.. Hela zaaangu… Nitalipa nini Mimi…!”
“Mama twende basi..!”
“Nataka hela zangu… Nitafanyaje hela za watu.. Hela za mkopo”
Alilia mama yule kwa uchungu na hasira nyingi. Watu waliendelea kumshangaa pale, lakini tayari alikuwa amelizwa na binti Doreen.
Huku mama yule akiwa analilia pesa zake, Doreen alikuwa na furaha sana kwa kupata pesa zile kwani zilimsaidia katka nauli ya kutoka Iringa kwenda Mbeya.
Doreen hakuwa na ndugu yeyote jijini Mbeya ila aliamua kwenda Huko kwaajili ya kukamilisha kazi zake hasa hasa ikiwa kupata titi la msichana mrembo.
Akiwa ndani ya basi, Doreen hakuweza kuzungumza na mtu yeyote. Alitulia kimya akiwa amejiinamia. Alionekana mwenye mawazo mengi sana tena mwenye huzuni kupita kiasi. Jirani yake Doreen ambaye ni mwanamama wa makamo kiasi kama miaka 40 au 45 alimuona Doreen akiwa katika hali ile. Alimwonea huruma na kuamua kumuita.
“We binti hujambo!” Alisema mama yule lakini Doreen alibaki kimya kama vile hakusikia anavyoitwa.
“We mdada!” Aliita na kumgusa began Doreen. Doreen aliinua kichwa na kumtazama mwanamke yule.
“Shkamoo mama!” Doreen alimsalimia kwa heshima na adabu mwanamke yule.
“Marhaba.. Mie naitwa Bi Carolina.. Unaitwa nani?”
“Naitwa Doreen!”
“Asante.. Mbona una mawazo sana? Tangu umeingia kwenye gari huna raha hata kidogo.. Una tatizo gani?” Aliuliza mwanamke yule kwa upole sana.
“Nina matatizo makubwa sana mama?” Alisema Doreen kwa unyonge wa hali ya juu.
“Tatizo gani?”
“Ni hadithi ndefu sana mama angu!” Alisema Dorice safari hii machozi yalimlengalenga machoni. Maneno Yale yalivuta usikivu wa Bi Carolina. Alitamani amsikilize zaidi.
“Mama! Acha tu.. Dunia ina mateso sana..! Sina hamu!” Doreen aliachia mchozi uliokuwa ukimlengalenga machoni. Bi Carolina alimtazama kwa huruma Doreen na kumtaka aendelee kumsimulia.
“Mama! Iringa nilikuwa naishi na mjomba wangu, tumbo moja na mama yangu! Na alinichukua baada ya wazazi wangu kufariki, aliahidi atanisomesha lakini hakufanya hivyo.
Alikuwa akininyanyasa, hanipi chakula, ananifanyisha kazi ngumu wakati anajua kabisa naumwa moyo, jana kanifukuza usiku wa manane akidai namchafulia hali ya hewa nyumbani kwake, sina hadhi. Nimeteseka sana, sins hata kwa kwenda!” Alisema Doreen kwa uchungu huku akilia. Simulizi yake ilimuumiza sana Bi Carolina akatamani kumsaidia Doreen.
“Pole sana Doreen.. Kwahiyo Mbeya unaenda kwa nani?”
“Sina ndugu huko.. Naenda tu hata kutafuta vibarua..!” Aliendelea Julia Doreen akachukua leso yake na kujifuta machozi.
“Dash pole sana.. Kwangu naishi na mume wangu na binti yangu.. Naomba nikusaidie ukaishi kwangu..” Alisema yule mama kwa huruma sana .Doreen alifurahi sana kimoyomoyo has a alivoambiwa kuna binti anaishi pale.
Mr Aloyce alilishikilia karatasi lile akiwa ameinamisha kichwa chake chini, mawazo yalimjaa tele kichwani mwake. Aliwaza achague lipi kati ya Yale aliyoamriwa.
Alijiona ana mtihani mzito sana ambao alishindwa kufaulu kwa haraka. Akawaza ni heri amrudishe mkewe ili waendelee kushughulikia tatizo la mtoto wao wakiwa pamoja.
“Namtaka mke wangu” alisema Mr Alloyce kwa sauti ya chini kisha ghafla akasikia sauti ya kicheko kikali kisha akatazama huku na kule bila kumuona mchekaji. Aliogopa kupita kiasi. Alitetemeka kama mtu aliyeshikwa na baridi Kali.
“Umechagua vyema maana ungetaka mwanao apone.. Ungepoteza kila kitu… Mkeo yupo kule Kule alikopotelea, hajafa ila tulitaka kumfundisha adabu tu kwa kulazimisha mambo.” Ilisikika sauti ile iliyoambatana na mwangwi mkali.
Mr Alloyce alizidi kuogopa, akaangaza macho huku na kule lakini hakuona mtu. Woga ulimzidia sana baada ya karatasi alilokuwa ameshika mkononi kutoweka bila kujua limeenda wapi. Alitafuta pale sakafuni lakini hakuliona, akazidi kupigwa na butwaa. Maneno aliyoambiwa kuhusu mkewe yalizidi kujirudia kichwani mwake. Alihisi kama alikuwa akidanganywa tu, mkewe alishafariki na hawezi kurudi.
“Mtu alishafariki, nitakaaje nae tena? Mh! Dunia ina maajabu…!” Aliwaza Mr Alloyce.”Kweli nitamwona mke wangu? Sijui niende Leo? Mh sasa hivi ni usiku sana!” Mr Aloyce aliwaza na kuwazua ubongoni mwake. Aliamua kuwa na subira, asiwe na papara. Aliamua kuisubiri kesho yake asubuhi ili aende sehemu ambayo mkewe alipotelea ili akamchukue.
Usiku ule ulikuwa mrefu sana kwa Mr Aloyce kwani hakuwa na hata lepe la usingizi, kila dakika alikuwa akiyafikiria matukio yote yaliyomtokea kwenye familia yake akahisi ndoto tu au mchezo wa kuigiza lakini ilikuwa kweli kabisa na alishuhudia kwa macho yake.
“Eddy! Mama yako mzima, tutaenda kumfata kesho asubuhi!” Mr Aloyce aliongea.
“Baba kweli?” Eddy alishtuka kusikia vile kwani sauti iliyokuwa ikisikika ndani mle na kumpa maelekezo Mr Alloyce, Eddy hakuisikia kabisa.
“Kweli mwanangu!”Eddy aliachia tabasamu mwanana usoni kwake. Kwani hakika taarifa zile zilimfurahisha sana.
“Kesho asubuhi na mapema nitamfuata kule aliko..”
“Yuko wapi?” Kabla Mr Aloyce hajajibu swali la mwanae alishtushwa na mlio wa simu yake . simu iliita kwa sauti kutokea kwenye moja ya sofa pale sebuleni. Mr Aloyce aliinuka na kuifuata lakini alipotazama kwenye kioo alishtuka kidogo.
*****
Gari ilitembea kwa mwendo mrefu sana mpaka ilipofika eneo la uyole jijini Mbeya. Ndipo Bi Carolina alipoamua kuchukua simu yake na kupitisha vidole vyake laini vilivyonakshiwa kwa kucha nzuri zilizopakwa ranging nyekundu. Akatafuta namba Fulani kisha akapiga.
“Mume wangu uko wapi? Tumefika hapa uyole sio muda mrefu tutaingia hapo Nanenane!” Alisema Bi Carolina .
“Kwani upo na nani?” Ilisikika sauti ya upande wa pili.
“Aah bwana .. Tupo na abiria wenzangu… Niambie uko wapi?”
“Utanikuta Hapahapa Nanenane stendi .. Nimefika kitambo nakusubiri mke wangu!” Alisema mume wa Bi Carolina kisha simu ikakatika.
Majira ya saa moja na nusu hivi, Bi Carolina na Doreen walikuwa tayari wamewasili katika kituo cha mabasi cha Nanenane jijini Mbeya. Bi Carolina alionesha kumjali sana Doreen kwa kumkaribisha Binti huyo jijini Mbeya .
“Hii ndio Mbeya Doreen… Baridi hapa ndo kwake… Karibu sana”
“Asante mama!” Aliitikia Doreen kwa sauti ya upole sana akiwa ameachia tabasamu usoni pake.
Ghafla simu ya Bi Carolina ikaita, alipotazama ilikuwa namba ya mume wake akapokea kisha akasikiliza maelekezo . Akaelewa gari ya mumewe ilipo wakaelekea pale na kuikuta gari aina ya Prado ikiwa imepaki pembezoni mwa Barbara karibu na mango la kuingilia uwanja wa maonesho ya Nanenane.
Tabasamu pana kutoka kwa mwanaume mfupi kiasi, mnene, mwenye rangi ya kunde likamkaribisha Bi Carolina. Lakini punde tabasamu hilo la mume wa Bi Carolina likayeyuka ghafla baada ya kuona mkewe ameambatana na mtu asiyemfahamu.
“Mke wangu vipi?” Aliuliza mumewe huku akimtazama Doreen.
“Kwani vipi mume wangu?”
“Huyu nani?” Aliuliza
“Mgeni wetu..”
“Ndugu yako?”
“Hapana.. Tuachane na hayo.. Tutaongea tukifika” alisema Bi Carolina.
“Shkamoo..!” Alisalimia Doreen kwa upole sana . lakini mume wa Bi Carolina hakuitikia salamu ile.
“Mke wangu.. Usiniletee uchuro.. Huyu wa wapi..!” Alifoka
“Baba Pamela mume wangu.. Mbona uko hivo? Kuna ubaya gani kuja na mgeni?”
“Hakuna tatizo kama ungenijulisha.. Kwani ni ndugu yako?”
“Sio.. Ni mtoto tu nimeamua kumsaidia ana matatizo makubwa sana!” Alijitetea Bi Carolina lakini bado mumewe hakutaka kukubaliana nae. Hakumtaka kabisa Doreen.
“Tupeleke nyumbani…” Aliomba Bi Carolina.
“Ntakubeba peke yako.. Bila huyo mgeni wako..”
“Kuwa na roho ya utu mume wangu.. Tutamwachaje huyu mtoto barabarani hapa? Si ukatili huo.
“Nimesema simtaki mgeni wako nyumbani kwangu… Jifanye una huruma utaokota mpaka majini!” Alisema mume wa Bi Carolina kisha akafunga mlango wa gari na kuondoka zake huku akimwacha mkewe na Doreen palepale.
Bi Carolina alibaki akishangaa kitendo cha mumewe siku ile. Alimtazama Doreen aligundua kuwa analia, tena Analia kwa uchungu sana.
“Usilie mwanangu tutaenda hata na daladala..” Alisema Bi Carolina kwa upole.
“Hapana mama.. Mi niache tu wewe nenda… Nisijekuharibu familia yenu bure” alisema Doreen huku akilia.
“Siwezi kukuacha hapa Doreen, usiku sasa!” Alisema Bi Carolina.
“Hapana mama nenda!” Alisisitiza Doreen lakini Bi Carolina alizidi kumbembeleza waondoke wote. Ghafla simu ya Bi Carolina ikaita, akapokea.
“Mama Pamela! Ukitaka kuja na huyo mgeni wako, usifike kwangu… Ishia hukohuko..!”
..Baada ya kutazama kioo cha simu Mr Alloyce alishtuka kidogo baada ya kukuta namba ya shemeji yake. Aliitazama kwa muda, huku akitafakari jibu la kumpa shemeji yake kwani tayari alimtaarifu kwamba aje kesho yake asubuhi. Aliamua kupokea simu ile huku akivuta pumzi ndefu na kuishusha taratibu sana.
“Halloo Shem! mbona ulikata simu kabla hujaniambia kuna tatizo gani?” Alisema Bi Sandra Dada wa mama Eddy.
“Ah..ah..Shem.. Usije kesho… Nimetatua ..tayari Shem!” Mr Aloyce alijikuta anapata kigugumizi cha ghafla kwani hakuwa na jibu sahihi la kumjibu shemeji yake.
“Umetatua SAA ngapi? Mbona sikuelewi shemeji? Si umesema nije kesho?” Sandra alishangaa.
“Ha..hapana Shem usije kwanza.. Usije!”
“Shem sikuelewi.. Nitakuja kesho..”
Alisikika Sandra kisha simu ikakatika.
Usiku ulikuwa ni mrefu sana kwa familia ile ya Mr Aloyce, walikesha wakiwa sebuleni yeye na mwanae. Usingizi ulimpitia kwa dakika chache kisha akashtuka. Akatazama saa yake ya mkononi ilikuwa tayari ni Saa kumi na moja alfajiri.
Mr Aloyce aliinuka kitini na kwenda bafuni, alioga haraka kisha akaingia chumbani na kubadili nguo.
Hakutaka kujichelewesha sana, akarudi sebuleni na kumuaga Eddy.
“Naondoka Eddy!”
“Baba naogopa kubaki peke yangu!”
“Jitahidi Mwanangu, siwezi kuondoka na wewe!”
“Twende wote baba!”
Eddy alizidi kumkazania baba yake lakini Mr Aloyce hakukubali hata kidogo kuondoka nae kwani alihofia misukosuko ambayo ingejitokeza wakiwa huko.
“Baki na mlinzi basi!”
Eddy aliinuka na kutoka na baba yake, nje kulikuwa bado hakujapambazuka vizuri hivyo kulikuwa na kigizagiza ingawa walisaidiwa na mwanga wa taa.
Mr Aloyce alichukua gari yake nyingine na kuiwasha haraka kisha akapiga honi ili mlinzi afungue geti.
“Bosi mbona usiku? Unaenda wapi?” Aliuliza mlinzi.
“Hayakuhusu.. Fungua geti nitoke, baki na Eddy!”
“Sawa bosi wangu.. Samahani kwa maswali!” Alisema mlinzi kisha akafungua geti Mr Aloyce akatoka na kuelekea kule alikopotelea mkewe.
Eddy alibaki na mlinzi wao pale nje, alikuwa na mawazo mengi sana kichwani hivyo alikuwa amejiinamia kimya tu bila kuzungumza chochote.
“Eddy mbona unawaza sana?” Aliuliza mlinzi. Lakini Eddy hakujibu kitu akabaki kimya amejiinamia.
“Eddy si naongea na wewe husikii au?” Aliuliza tena kwa sauti ya ukali kidogo. Safari hii Eddy aliinua kichwa na kumtazama.
“Demu wako amekutosa nini? Maana sielewi elewi humu ndani.. Mara mtoke mara muingie kimaajabu ajabu siwaelewi kabisa.!”
Sehemu Ya 13
“Eddy mbona unawaza sana?” Aliuliza mlinzi. Lakini Eddy hakujibu kitu akabaki kimya amejiinamia.
“Eddy si naongea na wewe husikii au?” Aliuliza tena kwa sauti ya ukali kidogo. Safari hii Eddy aliinua kichwa na kumtazama.
“Demu wako amekutosa nini? Maana sielewi elewi humu ndani.. Mara mtoke mara muingie kimaajabu ajabu siwaelewi kabisa.!”
“Yanakuhusu?”
“Yanaweza kunihusu kwa sehemu.. !” Alisema mlinzi yule kwa masikhara.
“Sitaki kelele..” Alisema Eddy na kujiinamia.
“Sikia Eddy… Mnanionaga chizi chizi sana ila nina akili zangu… Tatizo lako nalijua na ninaweza kukusaidia…. Sasa endelea hivohivo… Ila jua mficha uchi hazai..!” Alisema mlinzi kisha akasogea pembeni na kuchukua shuka lake ili ajifunike.
“Anko! Umesemaje?”
“Sijasema chochote ..!”
“Anko nisamehe.. Umesema unaweza kunisaidia tatizo langu?”
“Ndio na ni kazi ndogo… Ila endelea kunifanya mwehu kila siku….!”
Eddy alimtazama mlinzi wao kwa mshangao wa hali ya juu.
********
Bi Carolina hakuwa tayari kumuacha Doreen abaki peke yake kwenye kituo cha mabasi ilhali alimuahidi kumsaidia. Hakujali kabisa maneno ya mume wake kwani alijua tu kuwa mumewe hapendi wageni nyumbani kwake.
Bila kuchelewa wakabeba mizigo na kufuata taxi iliyokuwa mbele yao kisha wakapanda.
“Mnaelekea wapi?”
“Forest Mpya..”
Dereva aliondoa gari haraka kuelekea Forest Mpya. Doreen alikuwa amekaa karibu kabisa na dereva wa taxi. Macho ya dereva yalikuwa hayakauki usoni kwa Doreen kwani kila mara alimtazama kiwizi binti yule.
“Mama! Hivi huyu ni mwanao!?” Aliuliza Dereva taxi.
“Ndio! Kwani vipi?”
“Daaah Mama umezaa mtoto mzuri kuzidi malaika.. Kha! Kuna wazuri ila huyu mwanao kazidi!” Alisema dereva taxi na kumfanya Doreen atabasamu huku akiinamisha kichwa chini kwa aibu.
“We dereva bwana..” Alisema Bi Carolina na kucheka.
“Ningekuwa sijaoa ningekuja kuchumbia huyu mtoto..!” Alizidi kutania dereva yule ingawa utani wake ulikuwa na ukweli ndani yake.
“Oa mke wa pili!” Alitania Bi Carolina.
“Mke wangu atajinyonga.. Maana ana wivu sana, tena akigundua Bi mdogo kamzidi uzuri ndo basi tena”
Wakati wakiendelea kuzungumza hayo walikuwa tayari wamefika eneo la Mbeya Carnival na muda mfupi baadae walifika kwenye jumba moja la kifahari, lililovutia sana.
“Tumefika dereva!”alisema Bi Carolina dereva akapaki gari wakashusha mizigo. Kisha Bi Carolina akatoa pesa na kumpa dereva.
“Asante mama.. Ila nitunzie huyo bibie..!”
Wote wakacheka kisha wakaingia ndani na kuiacha taxi ile ikiondoka kwa fujo.
“Karibu Doreen hapa ndo nyumbani jisikie uko nyumbani… Sawa mama?” Alisema Bi Carolina huku wakiingia ndani.
“Asante mama kwa ukarimu wako”
“Wala usijali..” Bi Carolina alimkaribisha vizuri sana Doreen bila kujua kuwa alikuwa akimkaribisha shetani mbaya mwenye kila sifa ya kuitwa katili. Alikuwa kama fisi anayekaribishwa buchani kwa ukarimu sana wakati nyama ikiwa imejaa. Doreen alifurahi sana moyoni mwake alijua ushindi wake upo karibu.
Waliingia ndani na kumkuta baba Pamela akiwa ameketi kwenye sofa akitazama televisheni huku akiwa ameshika rimoti na kubadili Chanel.
“Za kutangulia mume wangu..” Alisema Bi Carolina.
“Mama Pamela!”
“Abee!”
“Hakuna heshima tens katika ndoa yetu sio?”
“Ipo mume wangu..!”
“Nimekuambia usije na huyo binti hujanisikia… Bila haya unaniambia eti ‘habari za kutangulia?’ Hivi una akili kweli?” Alifoka baba Pamela.
“Nisamehe mume wangu ila inabidi utumie utu sio kila wakati unakuwa na roho mbaya!”
“Ok sawa.. Naheshimu maamuzi yako ila ipo siku utanikumbuka..!” Alisema Baba Pamela mbele ya Doreen kisha akaondoka zake na kwenda chumbani.
Bi Carolina hakuzielewa kauli za mumewe aliona kama ana roho mbaya isiyojali wageni wala kuwathamini wanyonge. Aliamua kuachana na maneno ya mumewe badala take akamkaribisha kiti Doreen na baada ya kupumzika kwa muda akampeleka kwenye chumba kimoja ndani ya nyumba yao na kumkabidhi Doreen.
“Utalala humu.. Na hiki kitakuwa chumba chako..” Alisema Bi Carolina akitabasamu.
“Ahsante.. Mama naomba niulize kidogo..!”
“Uliza tu usijali..”
“Dada Pamela yuko wapi?”
“Pamela yupo kwa shangazi yake.. Atarudi kesho kutwa mtakuwa pamoja!”
“Asante”
Bi Carolina aliingia jikoni na kuandaa chakula kizuri. Wakala kisha wakaenda kulala.
Wakiwa chumbani baba Pamela hakutaka kuzungumza lolote na mkewe mpaka usingizi ulipowachukua wote wawili.
Majira ya SAA kumi alfajiri Baba Pamela aliishtuka usingizini na kumshtua mkewe kwa nguvu.
“Vipi?”aliuliza Mama Pamela kwa sauti ya nyono kwani bado alikuwa na usingizi.
“Amka nataka nikuambie jambo..!” Alisema baba Pamela.
********
Baada ya ndoa ya Mansoor na Dorice, maisha mapya ya ndoa yalianza. Penzi zito la Mansoor kwa Dorice lilijidhihirisha rasmi na alimpenda kwa dhati mkewe. Furaha take aliyoitafuta kwa muda mrefu sasa ilitawala moyoni mwa Mansoor kwani tayari alishampata ampendae. Dorice hakuwa na furaha sana na ndoa yake kwani mawazo yake yote yalikuwa juu ya uhai wa mpenzi wake wa Moyo Eddy Alloyce. Kila mara alimfikiria Eddy, na aliona amefanya kosa kubwa sana kufunga ndoa na jini.
Wakiwa wametulia tuli katika pozi la mahaba, Dorice na Mansoor. Dorice alifungua kinywa na kuyasema Yale yanayomsibu, masuala yanayousumbua moyo wake kwa kipindi kirefu.
“Mansoor..!”
“Niite Mume wangu..” Alisema Mansoor, Dorice akacheka kidogo.
“Mume wangu!”
“Naam! Hapo sawa mke wangu.!”
“Nataka nikukumbushe kitu.”
“Sema tu mpenzi wa roho yangu!”
“Vipi kuhusu ahadi yako ya kunipeleka duniani na kumwokoa Eddy?”
Maneno hayo yaliupasua moyo wa Mansoor na kuiyeyusha ghafla furaha yake. Hakutamani wala hakuwa tayari kuwa mbali na mkewe, alimpenda sana na alitamani awe wake daima milele. Kwake, Doreen alikuwa kama chanda ambayo bila hiyo Pete haina uthamanu wowote, machozi yalimlenga machoni mwake.
“Unataka kuondoka?”
“Ikumbuke ahadi yako…”
“Mke wangu unataka kunitenga? Unadhani ukienda duniani utakuwa wangu tena????”alisema Mansoor. Dorice akamtazama kwa mshangao.
..DORICE alimshangaa Mumewe Mansoor kwa maneno yake. Machozi yalimlengalenga machoni mwake kisha akajiondoa kifuani kwa Mansoor na kujitenga kando.
“Vipi mke wangu?”
“Najuta Mansoor.. Najuta sana kukukubalia, sikujua kama hautakuwa mwaminifu kwa ahadi zako!” Alisema Dorice kwa hasira.
“Sina maana mbaya mke wangu mpenzi.. Usinielewe vibaya tafadhali…Nakupenda sana!”
“Unanipenda? Unanipenda nini uongo mtupu..!” Alisema Dorice kwa hasira huku machozi yakimshuka mashavuni mwake. Alijikuta anamchukia Mansoor kupita kiasi. Hakutaka hata kumsogelea karibu.
“Baby! Nimekuelewa basi naomba uwe na amani moyoni mwako” alisema Mansoor huku akimsogelea Dorice na kutaka kumkumbatia lakini Dorice alimsukumia kando Mansoor na kuongeza kilio chake.
“Sitaki uniguse mpaka utakaponiambia ni lini utatimiza ahadi yako”
“Baada ya wiki moja nitaitimiza ahadi yako..!” Alisema Mansoor kwa huzuni kwani alijua ni kiasi gani Dorice alimpenda Eddy na alijua kwamba endapo angemrudisha Dorice duniani basi angemsahau Yeye na kuponda raha na Eddy. Kila alipofikiria hilo Mansoor aliumia sana moyoni mwake. Hakutamani kumkosa Dorice lakini hakuwa na jinsi zaidi ya kutunza uaminifu wa kutimiza ahadi yake.
“Una uhakika utanipeleka baada ya wiki moja?” Aliuliza Dorice akimtazama Mansoor.
“Ndio.. Usijali!” Mansoor alijibu kwa unyonge sana.
“Hapo umenifurahisha!” Alisema Dorice na kumkumbatia Mansoor.
“Lakini kabla haujaenda huko kuna kitu muhimu unatakiwa ufanye!” Alisema Mansoor akiwa bado amemkumbatia Doreen.
“Kitu gani?” Aliuliza Dorice.
Mansoor alimuachia Dorice kisha akanyoosha mkono wake na kumuonesha Dorice kiganja cha mkono wake. Kwa mshangao kidogo, Dorice akatazama kiganja cha Mansoor.
“Unaona nini hapa?”
“Sioni kitu..”
“Huoni kitu? Hebu tazama vizuri”
“Naona Pete” alijibu Dorice kwa mshangao.
*********
Eddy alimtazama kwa mshangao mlinzi wao. Alimkazia macho huku akimwomba msamaha kwa kumjibu vibaya hapo mwanzo.
“Usijali.. Najua matatizo yako yanakufanya uwe hivyo” alisema mlinzi.
“Sasa utanisaidiaje? Maana nateseka sana!”
“Nitakusaidia tu wala usiwe na haraka… “
“Lazima niwe na haraka Anko maana mpaka sasa hivi sijawahi hata kukojoa!”
“Mmh! Haraka zilimponza chura zikafanya awe na mabaka. Vuta subira tu maana umefanyiwa mchezo mbaya sana.” Alisema mlinzi yule huku akijifunika vyema shuka lake na kujigesha ukutani ili amalizie usingizi wake. Lakini ghafla akapigwa Kofi zito shavuni, aliruka kama kuku aliyeona hatari. Kabla hajakaa sawa Kofi lingine zito lilitua shavuni kwake, akajishika shavu na kutazama kama alikuwa amechanika lakini haikuwa hivyo kwani hakukuwa na damu yoyote ile.
Mlinzi yule akatazama huku na kule lakini hakuona Mtu aliyempiga makofi Yale mazito yaliyotua shavuni kama radi wakati wa mvya Kali.
“Vipi Anko?”
“Ah.. Hanna kitu.. Niko sawa tu..”
“Mbona umeruka sana?”
“Usijali Eddy.. Mimi nimeaga kwetu Musoma.. Niliwaaga wajita wenzangu..!” Alisema Mlinzi huku akisikilizia maumivu makali ya vibao alivyopigwa.
“Sikuelewi Anko .”
“Nimeaga.. Hakuna wa kunichezea!” Alizidi kuropoka mlinzi yule kisha akatulia kimya. Mawazo tele yakamjaa kuhusu vibao vile alivyopigwa kiuchawi. Aliwaza sana kwani alikuwa ana zindiko kubwa sana, sasa kwanini apigwe vile wakati ana kings anayoiamini? Alijiuliza sana bila kupata jibu.
Kulipambazuka kabisa, kimwanga kidogo cha jua kilianza kuchomoza kwa mbali. Wakati huo Mr Alloyce alikuwa kwenye gari take kuelekea msituni alikopotelea Mama Eddy.
Kichwani mwake alifikiria sana jinsi ya kutatua matatizo yanayoikumba familia yake. Hakupata njia kamili ya kuweza kutatua matatizo yake.
Aliendesha gari kwa mwendo wa SAA moja na nusu hatimaye akawasili kwenye eneo alilotakiwa kufika, akashuka kwenye gari na kuangaza macho yake huku na kule kuona kama atamwona mkewe.
******
“Amka mama Pamela kuna jambo nataka nikuambie”
“Bwana utaniambia asubuhi”
“Huu ndo muda mzuri wa kukuambia lakini kama hutaki basi.. ” Alisema baba Pamela kwa sauti ya utulivu sana . Licha ya ubishi aliokuwa nao mama Pamela katika suala la kuamka lakini ilimbidi tu aamke ili amsikilize mume wake. Kwani alijua huenda ana jambo muhimu anataka kumueleza wakati ule.
“Niambie basi mume wangu!” Alisema mama Pamela huku akipiga miayo ya uchovu wa usingizi.
“Asubuhi ya Leo nina safari kikazi..”
“Unaenda wapi?” Aliuliza mama Pamela.
“Naenda Arusha mke wangu… Nilitemea nikuambie Jana ila uliniudhi mpaka nikashindwa kukuambia”
Sehemu Ya 14
“Niambie basi mume wangu!” Alisema mama Pamela huku akipiga miayo ya uchovu wa usingizi.
“Asubuhi ya Leo nina safari kikazi..”
“Unaenda wapi?” Aliuliza mama Pamela.
“Naenda Arusha mke wangu… Nilitemea nikuambie Jana ila uliniudhi mpaka nikashindwa kukuambia”
“Mmh! Utakaa muda gani?”
“Mwezi mmoja!”
“Mwezi mzima? Mbona mrefu hivyo?”
“Ndio hivyo mke wangu ni masuala ya kazi tu, sina jinsi”
“Imekuwa ghafla!”
“Ndio nimepewa taarifa juzi jioni, lakini….”
“Lakini nini?” Alishtuka mama Pamela
“Nikiondoka tu, na huyo mgeni wako atoke hapa nyumbani kwangu”
Alisema Baba Pamela kwa sauti ya msisitizo sana akidhihirisha kuwa alimaanisha kile alichokisema.
“Baba Pamela utaniudhi.. Sitaki maudhi yako na hiyo roho mbaya yako”
“IPO siku utafahamu kwanini nasema hivo.. Kaa vizuri na Mungu utafahamu mengi!” Alisema Baba Pamela kisha akajifunika vizuri na kulala ili aamke baada ya nusu saa.
Mama Pamela alibaki na mawazo mengi sana ila katu hakuwa tayari kumwacha Doreen aende zake. Alimwonea huruma binti yule kwani alishamwambia historian nzima ya maisha yake.’ Mime wangu sijui yukoje siku hizi.. Ana roho mbaya.. Simfukuzi ng’oo Doreen. Mtoto ana adabu tena mstaarabu’ aliwaza Bi Carolina.
Asubuhi na Mapema Baba Pamela alijiandaa na kuwahi uwanja wa ndege, Bi Carolina alimsindikiza mumewe hadi uwanja wa Songwe Airport Kisha akamuaga.
“Ila tekeleza nilichokuambia”
“Sawa !” Alijibu Bi Carolina kisha akaingia kwenye gari na kuondoa gari kuelekea nyumbani kwake.
Haukupita muda mrefu Bi Carolina alitia timu nyimbani kwake, akapaki gari na kuingia ndani. Lakini alipoingia ndani alikutana na hali ya utofauti.
.BI CAROLINA alipiga hatua za taratibu kuelekea sebuleni lakini hali iliyokuwemo ndani mle ilizidi kumshangaza kwani alisikia harufu Kali na mbaya ya kitu kuungulia. Alifika sebuleni lakini hakukuta Mtu yeyote, akaamua kwenda jikoni.
Alipoingia jikoni tu, alipiga chafya tatu mfululizo kutokana na moshi mzito ulioambatana na harufu Kali sana uliotawala jikoni mle. Aliisogelea mpaka sehemu ya kupikia akagundua moto uliwashwa na kuna kitu kilichomwa. Akaangalia sufuria zote lakini hakukuta kitu chochote, akabaki na mshangao.
“Doreen!” Aliita Bi Carolina akiwa ameshika mkono kiunoni.
“Abee mama!” Sauti ya Doreen ilisikika kutoka chumbani.
“Njoo huku jikoni”
Bila ya kuchelewa Doreen alifika jikoni kule na kumkuta Bi Carolina akiwa ameshika kiuno akimsubiri kwa hamu amuulize kilichotokea.
“Abee mama” aliitikia Doreen kwa adabu sana.
“Nini kimetokea huku jikoni?”
“Nisamehe mama… Nilitaka kupika.. Ila kwa bahati mbaya nikaunguza kwani sijui kutumia jiko la gesi.” Alijitetea Doreen huku akitia huruma sana.
“Ulitaka upike nini asubuhi yote hii?”
“Nili…nilikuta maziwa.. Nyama kwenye friji nikataka nipike..”
“Mara maziwa mara nyama.. Mbona sikuelewi? Haya ulipikia sufuria gani?” Bi Carolina alishindwa kumuelewa Doreen ila kutokana na ugeni aliokuwa nao hakuweza kumfokea sana kwa kuhofu kuwa atajisikia vibaya.
“Nilichukua nyama… Sufuria ilipoungua sana nikaamua kuiosha..” Alisema Doreen akidai kutetemeka kwa woga.
“Sawa ila usirudie tena.. Nitakufundisha jinsi ya kupikia jiko la gesi..”
“Sawa mama” alisema Doreen kwa sauti ya upole iliyojaa hekima ya viwango vya juu.
“Sawa mwanangu nenda kaendelee na kazi zako”
Doreen alitoka jikoni mle na kuelekea chumbani kwake. Alichukua kimfuko cheusi kidogodogo kisha akafungua na kuutoa ungaunga mweusi. Kisha akaweka kiganjani na kusogelea kila kona ya chumba kile na kuupuliza kwa midomo yake. Alifanya hivyo mpaka unga ule ilipoisha, akasogelea kitanda chake na kukaa.
“Hapa sasa nimemaliza kazi… Mpaka huo moshi uishe nitakuwa nimefanikiwa kabisa.” Alisema Doreen akitabasamu kwani ule moshi uliotapakaa ndani mle ulisababishwa na Doreen. Alikuwa amechoma dawa ambayo ingewafanya wakaaji wa nyumba ile kumpenda Doreen kupita kiasi, na wasingeweza kumfukuza hata iweje mpaka pale atakapoamua kuondoka yeye mwenyewe.
Aliangalia SAA yake ya mkononi ilikuwa tayari ni saa nne na nusu asubuhi. Doreen alisikia sauti ya Bi Carolina ikimwita. Akatii wito na kumfuata Bi Carolina.
“Abee mama” aliitikia kwa heshima.
“Umeoga?”
“Bado”
“Kaoge unywe chai.”
“Sawa mama”
Doreen alitoka sebuleni pale na kwenda bafuni kuoga. Alipomaliza alipaka mafuta na kuvaa tena nguo alizokuwa amevaa kabla ya kuoga kisha akaenda sebuleni. Akamkuta Bi Carolina akiwa amekaa huku akitazama televisheni.
“Mbona umevaa nguo chafu?”
“Sina zingine”
“OK.. Baadae tutaenda Mwanjelwa ukatafute nguo za kuvaa.. Sasa hivi nenda ukanywe chai..” Alisema Bi Carolina.
“Sawa mama.. Vipi kuhusu Dada Pamela?” Aliuliza Doreen.
“Atakuja si muda mrefu.. Ameniambia yupo njiani. Baada ya kumwambia hivyo ghafla mlango ukagongwa . Akaingia msichana mmoja mrefu kiasi, mweupe, matiti yenye ukubwa kiasi, kiuno chembamba kama sindano na makalio makubwa kama milima miwili iliyopangana vyema. Wote walishtuka kidogo.
“Ah Pamela kumbr ulikuwa jirani tu.. Tumekuongelea sasa hivi hapa..”
“Sikuwa mbali”
“Karibu sana” alisema Bi Carolina wakati huo Pamela alikuwa akiketi sofani na kuweka pembeni mkoba wake. Kwa muda wote huo Doreen alikuwa akimtazama Pamela katika maeneo ya kifuani.
“Shkamoo Dada Pamela” alisalimia Doreen
“Marhaba hujambo? Wewe ndo Doreen?”
“Ndio..” Aliitikia Doreen huku akimgeukia mama Pamela “kumbe una mtoto mzuri namna hii?” Alisema.
Bi Carolina na Pamela walicheka tu.
“Huyu ndo mwanangu mpenzi… Yuko peke yake kama Tanzanite…” Alisema Mama Pamela huku akicheka.
Doreen aliwaacha wakiendelea na mazungumzo kisha yeye akaenda chumba cha kulia chakula (dinning). Moyoni mwake alifurahi sana kwani kwa uzuri aliokuwa nao Pamela titi lake lilifaa sana kwa kazi ya Doreen.
********
Dorice aliitazama Pete ya Mansoor kwa mshangao kwani hakujua lengo kamili la Mansoor kutaka kuitazama Pete ile.
“Umeitazama vizuri Pete hiyo?”
“Ndio”
“Hii Pete, si kama Pete za kawaida, ina nguvu nyingi sana ambayo inazidi nguvu za kaeaida.” Alisema Mansoor kisha akakohoa kidogo ili kusafisha koo lake kisha akaendelea.
“Pete hii nilipewa na babu yangu ambaye anaishi mbali sana katika sayari nyingine kabisa, alinipa kwaajili ya ulinzi wangu binafsi kwasababu alikuwa ananipenda. Na Mimi nitakupa wewe pete hii kwasababu nakupenda sana, ili ikusaidie katika kumuokoa mtu umpendae sana.” Alisema Mansoor huku akimtazama Dorice. Dorice aliendelelea kumsikiliza kwa umakini sana Mansoor.
“Pete hii ni ya ufalme wangu pale nitakapopewa ufalme na mama yangu… Wewe kwasababu ni mke wangu utakuwa malkia…”
“Nini?”
“Unashangaa nini? Sina njia nyingine ya kukusaidia mbali na hii.. Kama upon tayari nitakupa pete hii na utakuwa na uwezo mkubwa sana wa kijini… Utarudi duniani na utafanya kila unalotaka…” Alisema Mansoor. Maneno yake yalikuwa mazuri masikoni mwa Dorice ingawa yalimpa utata wa kiwango cha juu alijiuliza maswali mengi kichwani mwake juu ya suala la umalkia. Lakini akayapotezea maswali yake kwani alitamani sana kurudi duniani kumuokoa mpenzi wake Eddy na kwenda kwa wazazi wake ambao hakuwaona kwa muda mrefu.
“Sawa… Nipe tu..!” Alisema Dorice akionesha kukubali masharti ya Mansoor.
“Nitakupa Mke wangu lakini kuna jambo muhimu unalotakiwa kuzingatia pindi utakapokuwa na hii pete”
“Jambo Gani?” Dorice alishtuka.
“Hii ni pete ys heshma sana, ambayo haihitaju uchafu wa aina yoyote.. Kwahiyo ukiivaa na kwenda Nayo duniani hutakiwi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine zaidi yangu Mimi!” Alisema Mansoor huku akimtazama mkewe kwa macho yaliyoonesha msisitizo kwa kile alichokizungumza.
“Mmh!” Aliguna Dorice kwani alikuwa na wazo la kumsaliti Mansoor pindi atakaporudi duniani. Na alikuwa na lengo la kutorudi tena katika himaya ile ya majini. Hivyo basi masharti ya pete ile yalikuwa magumu sana kwake na kumuweka katika wakati mgumu sana.
“Mbona unaguna?”
“Kwani hakuna msaada mwingine mbali na hiyo pete” aliuliza Doreen
“Upo!”
“UPI.. Nipe msaada mwingine Mansoor tafadhali”
“Unataka njia nyingine?”
“Ndio..” Alijibu Dorice haraka.
**********
Mr Aloyce alitembeatembea katika eneo lile akimsubiri mkewe atokeze lakini muda ukazidi kwenda Vila kuona dalili yoyote. Mr Aloyce alianza kukata tamaa ya kumpata mkewe akahisi huenda alikuwa anadanganywa tu. Akataka kuondoka lakini moyo wake ulisita sana baada ya kuumbuka msemo usemao “atafutaye hachoki, akichoka keshapata” akaamua kuwa mvumilivu kwani siku zote mvumilivu hula mbivu.
Ajasogelea eneo tulivu lenye nyasi fupi kisha akaketi pale. Mawazo mengi yalifurika kichwani mwake, “nimekuwa mtumwa… Mtumwa wa nguvu za giza hii hali mpaka lini? Kila siku yanaibuka mapya… Mmh! Yote hii ni kwasababu ya Eddy.. Ila sipaswi kumlaumu” alijiwazia Mr Alloyce huku machozi yakimtiririka.
Ghafla upepo mkali ulianza kupuliza eneo lile na kumwondoa mawazoni Mr Aloyce. Alinyanyuka pale chini na kutazama juu lakini hakuona chochote.
Upepo ukazidi kupuliza kwa kasi sana mpaka miti ikaanza kuyumbayumba. Miti iliyumba kwa kasi sana na ile isiyo na nguvu ikaanguka. Mr Aloyce aliogopa sana.
Baada ya upepo ule radi Kali zikapiga mfululizo, zikazidi kumtisha Mr Aloyce. Alipiga hatua kuelekea kwenye gari yake ili akajifiche mle maana hali ilitishs lakini ghafla akasikia sauti ya kilio kikali.
“Nisaidie mume wangu.. Nisaidiee!” Mr Aloyce alishtuka sana kwani sauti ile aliijua fika. Ilikuwa ni sauti ya mkewe mpenzi. Akabaki amesimama wima kama mlingoti ili asubiri kitakachoendelea.
Akiwa bado amesimama alishtushwa na kitu kikipita miguuni mwake, akatulia kimya huku akipiga jicho kutazama kilikuwa kitu gani.
“Mamaaa” mr Aloyce alipiga ukunga kwa woga na hofu baada ya kuonana uso kwa uso na chatu aliyekuwa akijiviringa kwa kasi mwilini mwake.
…… MR ALOYCE alibaki kimya akiwa ametulia kimya kama vile amegandishwa na gundi ngumu. Haja ndogo ilipita taratibu katikati ya mapaja yake na kushuka chini ardhini. Alitamani ardhi ipasuke ili walau akajifiche chini ya ardhi kuliko kuendelea kushuhudia tukio lililokuwa linaendelea kwa wakati ule. Akili ilisimama, mwili ulinyong’onyea kwani hakuwa na lolote la kuweza kufikikiria kwa wakati ule. “Nimekamatika kwenye mtego” ndilo wazo pekee lililomjia akilini mwake.
Chatu yule aliendelea kujiviringisha kwa madaha na mbwembwe nyingi mwilini mwa Mr Aloyce na kumfanya mwanaume yule ajihisi mfu aliyebakisha roho yake tu kabla ya mazishi. “Nisaidie Mungu wangu” Mr Aloyce alisali kimoyo moyo akiamini kwamba huenda Mungu atasikia maombi yake na kumkumkumbuka katika Mateso yake. Machozi hayakumtoka hata chembe kwani hofu ilimzidia mpaka chozi lilimkauka.
Akiwa katika hali hiyo ngumu isiyoelezeka Mr Alloyce hakuona mtu yeyote wala dalili ya kiumbe chochote katika eneo lile. Ghafla upepo mkali ukapuliza eneo lile, ulikuwa kama kimbunga kinachoweza kuleta maafa kwa makazi ya watu. Mr Aloyce alijishangaa sana kuona mwili wake ukiwa mwepesi sana tena umejiachia kupita kiasi. Moyo wake ukafurahi na akatumia nafasi hiyo kujitazama mwilini mwake, akagundua yule chatu hayupo tena mwilini mwake Bali amesogea pembeni kidogo na kujituliza kama gogo.
Macho yalimtoka kama njugu akimtazama yule Chatu, ghafla akapigwa na mshangao wa ajabu baada yule chatu kubadilika umbile na kuwa na umbo la mtu. Mr Alloyce akamkazia macho MTU yule aliyetokana na chatu. Hakuamini macho yake pale alipogundua mtu yule alikuwa mkewe, Aloyce alitetemeka sana. Ndipo mwanamke yule alipoachia kicheko kikali sana huku akimsogelea Mr Aloyce. “Nilikukumbuka sana mume wangu.. Ila nasikitika unaniogopa” alisema mwanamke yule mwenye sura na umbile la mama Eddy. Mr Aloyce alitetemeka sana, akapiga hatua za kinyumenyume kumkwepa mwanamke yule.
“Mume wangu! Mbona unaniogopa?” Alisema mwanamke yule.
****
Dorice alimtazama Mansoor na kumsikiliza kwa umakini huku akiwa na hamu kubwa ya kutaka kujua njia nyingine ya kuweza kuondoka katika himaya ile ya kijini na kurudi duniani ili kumkomboa Eddy mpenzi wake wa dhati.
Mansoor alimtazama Dorice kwa unyonge sana, sura yake ilidhihirisha huzuni aliyokuwa nayo moyoni mwake. Akasogeza mkono wake na kuushika mkono wa Dorice kisha akausogeza karibu kabisa na midomo yake mizuri. Akaachia mabusu mazito mfululizo huku chozi likimdondoka. Kisha akainua macho yake na kumtazama Dorice.
“Dorice kwanini hunipendi?” Aliuliza Mansoor. Dorice alimtazama Mansoor bila kujibu chochote.
“Kwanini hunipendi?” Aliuliza tena Mansoor huku macho yake yakizidi kuwa mekundu kama pilipili. Kisha taratibu machozi yake yalianza kubadilika rangi na kuwa kama damu.
“Dorice! Naumia sana moyoni mwangu kumpenda mtu asiyenipenda! Najilaumu sana ingawa sio kosa language ila ni kosa la moyo wangu ambao haukumchagua yeyote ila wewe.. Natamani ungejua thamani ya upendo wangu kabla haujaenda duniani ili unikumbuke moyoni mwako” alisema Mansoor huku machozi mekundu yakizidi kudondokea kwenye mikono mizuri na laini ya Dorice. Maneno Yale yaliugusa moyo wa Dorice, akahisi ni mkosaji sana kwa kuutesa moyo wa Mansoor. Machozi yalimlengalenga machoni mwake akajikuta anamkumbatia Mansoor na kumtakia maneno ambayo hakuwahi kumtamkia hata Mara moja.
“NAKUPENDA SANA MANSOOR” alisema Dorice huku midomo yake ikibusu shingo ya Mansoor kwa huba, na mikono yake ilitembea taratibu mgongoni kwa Mansoor na macho yake yalikuwa yamefumba na kumpa nafasi zaidi ya kuzitafakari kwa kina hisia za mapenzi zilizokuwa kichwani mwake.
“Asante sana mpenzi wangu… Nakupenda na nitazidi kukupenda milele..” Ilisikika sauti iliyojaa huba na mahaba mazito ya Mansoor.
“Asante mpenzi… Lakini naomba unisaidie kwa lile suala langu.. Na umesema kwamba kuna njia nyingine..” Alisema Dorice akiwa bado amemkumbatia Mansoor.
Swali lile lilikuwa kero kwa Mabsoor kwani alijua Dorice hatozungumzia tens suala lile baada ya kumpa maneno matamu zaidi ya asali.
“Mh! Nitakusaidia… ” alisema Mansoor.
“Lini?”
“Kuwa na subira… Wala usijali… ” Mansoor alimwondoa shaka Dorice. Baada ya muda mfupi Mansoor alimuaga Dorice kisha akatoweka machoni pake huku akimuahidi kuwa atarudi baada ya muda mfupi tu.
Hazikupita dakika nyingi Mansoor alijitokeza tena kwa Doreen lakini alikuwa na kitu kilichomshtua Doreen na kumfanya aogope sana.
******
Siku ya kwanza ndani ya nyumba ya mama Pamela iliisha vizuri sana wakiwa na Doreen. Usiku majira ya SAA NNE baada ya kula na kutazama televisheni huku wakipiga soga za hapa na pale wakaagana na kila mmoja alienda kulala kwenye chumba chake.
Usiku ule Mama Pamela alihisi kuna utofauti ambao hakuuzoea kabisa.
Paka walilia Mfululizo na kumfanya Mama Pamela ahamaki kidogo, sauti ya paka kutoka batini ilisikika ikilia kama mtoto mchanga jambo ambalo lilimtisha mama Pamela. Na haikuwa hivyo kwa mama Pamela tu bali pia hata kwa Pamela kwani alikuwa anaogopa kupita kiasi.
Ghafla usingizi wa ajabu ukampitia Mama Pamela, macho yalikuwa mazito kiasi kwamba alishindwa hata kuyafumbua ingawa akili yake bado ilikuwa inaendelea kuwaza . akajishangaa na kujiuliza usingizi ule ulikuwa wa aina gani kwani kwa kawaida mtu akilala hata akili pia inalala. Ghafla kitu kizito militia juu yake, akashindwa kupumua vizuri na kila alipojaribu kujiinua alishindwa. Akahisi anakabwa sana shingoni na kila alipojaribu kuinua mkono wake ili ajiokoe alishindwa. Akazidi kuhema kwa nguvu.
Nusu SAA nzima hali ile ilizidi kumsumbua mpaka aliposhtuka na kukaa kitandani huku jasho likimtoka kwa kasi kana vile yupo jijini Dar kumbe yupo Mbeya kwenye baridi Kali. Alikaa kitandani huku akihema sana ghafla akasikia kishindo kikali sana kilichomshtua na kumfanya atahamaki.
“Mamaaaa! Mamaa ” sauti ya Pamela ilimshtua sana Bi Carolina. Akatamani ainuke kitandani pale ili akamtazame mwanaye, Mara taa ikazimwa. Akajua umeme umekatika lakini kilichomshangaza ………
Sehemu Ya 15
Nusu SAA nzima hali ile ilizidi kumsumbua mpaka aliposhtuka na kukaa kitandani huku jasho likimtoka kwa kasi kana vile yupo jijini Dar kumbe yupo Mbeya kwenye baridi Kali. Alikaa kitandani huku akihema sana ghafla akasikia kishindo kikali sana kilichomshtua na kumfanya atahamaki.
“Mamaaaa! Mamaa ” sauti ya Pamela ilimshtua sana Bi Carolina. Akatamani ainuke kitandani pale ili akamtazame mwanaye, Mara taa ikazimwa. Akajua umeme umekatika lakini kilichomshangaza ………
…. Leyla alikuwa amechanganyikiwa sana baada ya mumewe kuwa katika Hali ile. Alishindwa kuelewa atafanyaje ili kujimudu katika familia yake kwani Mwalimu John ambaye ni mumewe asingeweza kurudi tena kazini. Kilichomfanya anyong’onyee zaidi ni hali ya Judith kwani hakuweza kuongea wala kusikia. Leyla alikosa raha sana, akakaa kitini akiwa na mawazo mengi sana. Alijiuliza afanye nini ili aweze kuwaokoa wahanga wa tatizo asilojua limetona na nini.
Akiwa katika kutafakari hayo yote ghafla wazo muhimu lilimjia kichwani mwake. Leyla alichukua simu yake na kutafutw namba fulani kisha akapiga. Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa kisha ikakakata. Leyla hakukata tamaa akapiga tena lakini majibu yakabaki Yale Yale, simu haikupokelewa akajaribu tena na tens simu ikapokelewa.
“Bwana asifiwe mchungaji..” Alizungumza Leyla kwa sauti ya unyenyekevu sana kwani aliyempigia alikuwa ni mchungaji wake.
“Amen.. Unasemaje?” Alijibu mchungaji yule kama vile hataki kuzungumza.
“Samahani mchungaji nina shida… Naomba msaada wako!” Alisema Leyla.
“Shida gani”
“Kuhusu familia yangu!”.
“Kama ni mumeo mama… Chukua imani hapo ulipoanza maombi Mimi sina muda… Nina mambo mengi ya kufanya..” Alisema mchungaji yule kwa ukali kiasi jambo lililomtisha sana Leyla kwani hakutegemea kama mchungaji wake angemjibu vile.
“Pastor! Tafadhali nisaidie..” Leyla alimbembeleza mchungaji lakini hakumuelewa. Na mchungaji huyu ndiye aliyefanya mazishi ya mwalimu John.
“Kwasasa sipo nyumbani.. Nipo mbali kikazi…” Alisema Mchungaji yule. Kiukweli ilikuwa vigumu kwa Leyla kuamini maneno ya mchungaji wake kwani Siku zote aliamini mchungaji wake angekuwa ndiye mfariji lakini haikuwa hivyo.
“Cha kukusaidia labda nitawaita wanamaombi waje kukusaidia” alisema mchungaji na kukata simu.
Leyla alishindwa afanye nini kwani hata ndugu zake walimtenga. Ilipita nusu SAA nzima , mlango wake ukagongwa. Alifurahi sana kwani alijua tayari mchungaji amewasiliana na wanamaombi ili waje kuombea familia yake. Alinyanyuka kitini na kwenda moja kwa moja kufungua mlango.
*****
Mama Pamela alizidi kutetemeka kwa woga sana, alijikunyata kama mgonjwa kitandani kwake. Lakini alizidi kuisikia sauti ya mwanae ikiendelea kumwita. Mama Pamela akazidi kupata hofu, japo aliogopa sana lakini aliamua kuinuka kitandani na kunyata taratibu kuelekea chumbani kwa Pamela. Na hii ni kwa sababu damu nzito kuliko maji .
Nyumba ilitawaliwa na kiza kizito sana, hivyo ilimpa shida sana Mama Pamela kuelekea chumbani kwa mwanae. Aliingia chumbani kwa Pamela na kuita taratibu “Pamela! Pamela!” Lakini Pamela hakuitikia. Mama Pamela alisogelea kitanda cha Pamela na kuanza kupapasa papasa lakini cha ajabu hakuona dalili zozote za uwepo wa mtu kitandani pale. Mama Pamela alizidi kuchanganyikiwa sana.
Akaita tena “Pamela! Pamela!” Lakini bado hakukuwa na sauti yoyote iliyoitikia. Mama Pamela alihisi akili yake inavurugika. Akauvua woga wake na kumuita Pamela kwa sauti kubwa lakini bado hakuitikia.
Mama Pamela alirudi chumbanu kwake na kupapada sehemu ilipokuwepo simu yake na baada ya kuipata alimshukuru Mungu. Kisha akawasha tochi na kuanza kumulika kila chumba.
Aliingia chumba cha kwanza akamulika lakini hakuona MTU, akamulika, cha pili, cha tatu na kisha akaingia jikoni lakini bado hakumuona Pamela. Roho ya Mama Pamela iliingiwa simanzi, akajua mwanaye amepotea kwa mazingira ya kutatanisha . akaingia bafuni na kumulika lakini Hakumkuta Pamela. Mama Pamela alizidi kuchanganyikiwa zaidi.
“We Mungu bora wangenichukua Mimi sio mwanangu Pamela,” alisema Mama Pamela akiingia chooni.
Mama Pamela alistaajabu sana alichokutana nacho. Alimkuta Pamela akiwa amelala chooni huku kajifunika blanketi lake vizuri.”
“Pamelaa!” Aliita mama Pamela kwa mshangao na mpaka wakati huo mama Pamela hakujua Doreen anaendeleaje.
****
Mr Alloyce alibaki njia panda, alikuwa haelewi cha kufanya juu ya mwanamke yule. Alijiuliza amkubalie kama mkewe au asimwamini? Mawazo yake hayo mawili yalimezwa na ukarimu wa mwanamke yule kwa jinsi alivyoonesha kumjali Mr Aloyce.
“Mime wangu… Mbona hunichangamkii? Baba Eddy jamani” alisema mwanamke yule na kumsogelea Mr Aloyce “hivi kweli we ni Mke wangu? Mama Eddy?” Aliuliza Mr Alloyce kwa wasiwasi.
“Kha! Kumbe huniamini mume wangu?” Alisema
“Mbona ulitokea kama Chatu?”
“Hahahah unatakiwa kuniamini mume wangu!” Alisema mwanake yule na kumsogelea Baba Eddy kisha akamkumbatia.
Mr Aloyce alitamani kumwamini mwanamke yule kama ndo mkewe lakini moyo wake ulisita. Alimsogelea na kumkumbatia lakini moyoni make alikuwa na mashaka sana.
“Nakupenda mume wangu.. Naomba tuwahi nyumbani ili nikamwone mwanangu” alisema mama Eddy.
“Sawa” alisema Baba Eddy huku akifungua mlango wa gari.
“Lakini unanishangaza mume wangu?”
“Nakushangaza na nini?”
“Huna amani moyoni mwako.. Kwanini?”
“Usijali Niko sawa…”
Wallingia kwenye gari kisha Mr Aloyce aliwasha gari na kuanza kuendesha. Aligeuka kumtazama mkewe yule aliyekuwa ameketi pembeni yake, lakini kuna kitu kilimshangaza…..
.MR Aloyce alizidi kumkazia macho mkewe akahisi ni mrembo zaidi ya Mama Eddy yule anayemfahamu yeye. Halafu alikuwa na madaha sana kuzidi vile alivyomzoea. Wasiwasi ukamtanda akilini make na kumfanya asimwamini sana mwanamke yule kuwa ndiye mkewe halisi.
“Mbona unaniangalia sana? Umemisi busu langu nini?” Aliuliza Mama Eddy.
“Hapana wala usijali”
“Ok kama wewe hukumiss basi Mimi nilimisi sana kiss lako mpenzi”.
Alisema Mama Eddy huku akimsogelea Mr Aloyce kwa ukaribu zaidi na kumshikashika kidevu kwa mahaba. Mr Aloyce alionesha kutojali mguso ule aliopapaswa na mikono laini ya mkewe. Hakuelewa ni sababu zipi zilizomfanya asimjali mwanamke yule kwa kiasi kile ila moyo wake ulikuwa mzito sana.
“Baby mbona hivyo…? Embu usiwashe gari kwanza mpaka unibusu” alisema Mama Eddy kwa sauti iliyojaa mdeko wa kimahaba. Mr Aloyce hakutaka kukiri udhaifu, akaachia usukani na kusogeza mdomo wake karibu na mdomo wa mkewe kisha akambusu.
Busu lile lilimpa nafasi nzuri sana Mama Eddy ya kupenyezapenyeza mpaka kuingiza ulimi wake mdomoni kwa Mr Aloyce. Kisha wakabadilishana mate yao kwa mahaba. Lakini wakati tendon hilo likiendelea, Mwanamke yule alimwachia vitu Fulani Mr Aloyce bila yeye mwenyewe kujua. Na ilikuwa ni dawa Kali ya kumfanya Mr Aloyce amwamini mwanamke yule kuwa ndiye mkewe halisi wakati hakuwa yeye. Alikuwa ni mwanamke kutoka himaya ya akina Doreen na alitumwa nyumbani kwa Mr Aloyce ili afanye kazi muhimu sana aliyotumwa.
Kwa vile alivyomfanyia Mr Aloyce, alifanikiwa kuziteka akili za Mwanaume yule. Baada tu ya busu lile la huba, Mr Aloyce alijkuta akimpenda sana mwanamke yule akijua ndie Mkewe halisi na kumbe haikuwa hivyo. Wasiwasi wake ulifutika kichwani mwake, pendo la dhati likatawala moyoni mwake.
“Tuondoke mume wangu” alisema mama Eddy kwa sauti ya upole iliyojaa huba huku akiwa ameachia tabasamu pana usoni mwake.
“Usijali mke wangu.. Nilikukumbuka sana… Nina imani hata mwanetu anakusubiri kwa hamu sana.” Alisema Mr Aloyce huku akishikilia vizuri usukanu na kuondoa gari kwa kasi sana.
Mr Aloyce aliendesha gari kwa kasi ya ajabu na baada ya masaa machache tu waliwasili eneo la Ipogoro Iringa kisha wakaelekea nyumbani kwao.
Walifika getini wakapiga honi geti lilifunguliwa. Mr Aloyce aliegesha gari pembeni kisha akashuka kwa furaha kubwa, na baada ya hapo akaelekea upande wa pili wa gari yake na kumfungulia mkewe huku tabasamu mwanana likiwa limechanua mdomoni mwake.
“Shuka malkia wangu… Tumeshafika kwetu..” Alisema Mr Aloyce huku mwanamke yule anayefanana kwa kila kitu na Mama Eddy akishuka kwa madaha kisha akamkumbatia Mr Aloyce na kumbusu. Wakati yote hayo yakiendelea Mlinzi alikuwa pembeni yao akishuhudia penzi la zamani lililochipua upya tena kwa kasi ya ajabu.
“Mh bosi naona mama Amerejea..” Alisema mlinzi kimzaha.
“Ndio..”alijibu Mr Aloyce kwa furaha.
“Baby nataka kuongea jambo na mlinzi wetu naomba utuache kidogo..” Alisema Mama Eddy.
“Ok ila kuwa makini tu nisije kupinduliwa na houseboy..” Alisema Mr Aloyce na kuondoka zake huku akimsisitiza mkewe asichelewe.
Baada ya Mr Aloyce kuondoka pale, Mwanamke yule alimsogelea mlinzi na kumtazama kwa ghadhabu Kali. Hali hiyo ilimtisha sana mlinzi na kumfanya ajiulize maswali mengi ambayo alishindwa kujijibu mwenyewe.
****
Mama Pamela aliishiwa nguvu kabisa. Alijiuliza sana ni kwanini mwanaye amelala chooni kule ilhali ana kitanda kizuri cha kumfaa? Maswali yake hayakuwa na majibu akajikuta anaishia kupiga makofi kwa mshangao.
“Pamela!” Alimwamsha mwanae ambaye bado alionekana ana usingizi mzito sana. Alimtikisa tikisa mpaka alipofanikiwa kumwamsha kabisa. Pamela aliinuka, lakini alibaki mdomo wazi baada kuona mazingira aliyopo si ya kitandani kwake.
“Mama nipo wapi hapa? Mbona kama chooni?” Aliuliza Pamela kwa mshangao.
“Nikuulize wewe mwanangu.. Umefikafikafikaje mpaka ukalala chooni?” Aliuliza Mama Pamela.
“Mbona sielewi mama” alisema Pamela.
“Haya chukua hilo shuka lako twende chumbani.. Hayo mengine tutajua huko huko..”
Walitoka chooni mle na kuelekea chumbani kwa mama Pamela. Pamela alitoa nguo aliyokuwa amevaa kwaajili ya kulalia kisha akavaa nyingine kwani ile tayari ilishapata unyevunyevu wa chooni.
“Lakini mama mbona Doreen hatujaenda kumwangalia si atahisi tunamtenga..” Alisema Pamela.
“Ila kweli”
“Tumfate basi..” Alisema Pamela kisha wakainuka na kwenda chumbani kwa Doreen. Kulikuwa na Giza totoro ambalo bila msaada wa tochi basi wasingeona chochote. Walimulika kitandani kwa Doreen na kumwona Doreen akiwa amelala fofofo. Walimsogelea kwa ukaribu na kumwamsha lakini Doreen hakuitikia. Pamela na mama yake walitazamana mshangao.
“Mbona haamki?” Walinong’ona taratibu.
“Isije ikawa ndo amek.. Amepata matatizo mengine” alisema Pamela.
“Doreen! Doreen” Mama Pamela aliita kwa sauti kubwa lakini Doreen bado hakuamka.
“Tumuache basi tutamkuta kesho yawezekana mwenzetu hajakumbwa na mauzauza” alisema Pamela kisha wakarudi chumbani kwa Mama Pamela kupumzika kidogo maana Pamela asingeweza kulala peke yake kutokans na woga aliokuwa nao kwa usiku ule.
*****
“Umeshika nini hicho Mansoor” aliuliza Dorice kwa woga .
“Nimeshika Pete” alijibu Mansoor. Jibu hilo lilimshangaza Dorice kwani alichokiona mkononi kwa Mansoor haikuwa Pete Bali alikuwa nyoka mkubwa aliyejiviringisha kama Duara kiganjani kwa Mansoor.
“Pete gani hiyo?” Dorice alizidi kuogopa.
“Ni pete ya kukupa wewe ili uwe na nguvu ya kurudi duniani na kufanya lolote utakalo…”
“Mbona namuona Nyoka?”
“Fumba macho kisha ufumbue nikikuruhusu” alisema Mansoor kisha Dorice alifanya kama alivyoambiwa.
Mansoor alisogeza mkono wa Dorice kisha akchuku kidole Chanda na kumwambia Dorice afumbue macho yake.
Dorice alifumbua macho yake na kutazama kidole chake. Alishtuka kuona pete inayong’aa sana kidoleni mwake.
“Umenivisha SAA ngapi?”
“Nimekuvisha ulipofumba macho”
“Mbona sikuhisi chochote? Na je yule nyoka yuko wapi?”
“Sikushika nyoka.. Nilishika pete” alisema Mansoor.
Ghafla Dorice alijiona wa tofauti sana. Kichwa kikaanza kumgonga kwa kasi sana, akaanza kulalamika. Na kadri alivyolalamika ndivyo kadri maumivu yalivyomzidia.
Machozi yalianza kuchuruzika lakini cha ajabu, matone ya machozi yake hayakuwa ya kawaida kwani kila tone alilodondosha lilikuwa damu. Dorice alijishangaa sana lakini Mansoor akaangua kicheko kikali kilichomshangaza Dorice.
.Dorice aliendelea Julia huku matone yake ya machozi yakiwa damu. Ghafla akajikuta ana uwezo wa ajabu ambao hajawahi kuufikiria kuwa nao hata siku moja. Alijibadilisha sura na kuwa kiumbe wa kutisha, macho yalikuwa kama ya paka, uso wake ukawa mweusi tii kama mkaa, kucha zake zikawa ndefu sana na meno yake mawili yalichomoza nje ya kinywa chake. Mansoor alicheka kicheko kikali cha kutisha huku sauti ya kicheko chake ikiambatana na mwangwi. Radio zikapiga mfululizo Dorice akatoweka ghafla na kumuacha Mansoor.
INAENDELEA

