Mimi Ni Single Mama Wa Mtoto Mmoja
Mimi ni single mama wa mtoto mmoja nina miaka 23, nilikata mawasiliano kabisa na baba mtoto baada ya kuikataa mimba ikiwa na mwezi1,,nilipoanza clinick kuna doctor nilizoeana nae sana hadi kipindi najifungua alikua kama ndy baba mtoto wangu hata bill hospital alilipa yeye na pesa ya uzazi alinipa alikua ananijali sana mwisho wa siku tukajikuta tumeanzisha mahusiano
Mtoto alipofika miezi 3 akaniambia kwavile baba ake amemkataa basi nimuite kwa majina yake, nikakubali akashughulikia cheti cha kuzaliwa na kadi la clinick tukabadilisha, rasmi mwanangu akaanza kuitwa kwa majina yake, yeye alikua hana mtoto, alisema tukijakuoana anapenda watoto wetu watumie jina moja. Mipango yetu ilikua mtoto akifika miaka miwili tutambulishane nyunbani tufunge ndoa tuanze kuishi pamoja,,,kunakipindi tuligombana hatukuongea kama mwezi1 ila pesa ya matumizi kwa ajili ya mtoto alikua anatoa,badae tukapatana maisha yakaendelea
Mtoto alipofika mwaka na miezi2 akasafiri kwenda kijijini kwao aliporudi alikua kabadilika anahasira muda wote ananifokea bila sababu,nikafatilia nikaja kugundua kuwa ameshamposa mwanamke mwingine nilipomuuliza akasema kipindi tumegombana alitafuta mwanamke wa kumtuliza bahati mbaya akampa mimba, wala hampendi ila wazazi wake wamekua wakali ikabidi atoe posa ili kuwapooza tu ila hawezi kumuoaa atalea tu mtoto wake basi.
Akanibembelezaa weee mwisho wa siku nikatulia, ilipita kama miezi6 siku moja nikasikia anaongea na mama yake anamueleza kuwa kuna binti kampa mimba soon ataitwa baba,,aliponiona akabadilisha mada .nikaja kukagua simu yake wanagroup la familia nikakuta amewaeleza ndugu zake kuwa anayofuraha soon ataitwa baba, kila mtu alimpongeza, nakutaman kumjua huyo mwanamke anaemuheshimisha binafsi niliumia sana ila sikujionyesha asije kusema simpendi mtoto wake, na sikutaka kufatilia tena kuhusu huyo mwanamke wala mtoto maana alikua anaonesha kunijali na mipango yetu ya ndoa ilikua palepale..
Mwanangu alipofika miaka miwili akaja kujitambulisha kwetu “kwa hiyari yake” badae akanipa simu niongee na mama yake nimsalimie mama ake alipokea vizuri na kuonyesha kutamani kunijua akijua mimi ndy mwanamke nilie zaa nae
Siku ananipeleka kwako kunitambulisha walikusanyika ndugu zake woote
Nilipofika mama ake akaanza mbona hamjaja na mtoto kila mtu akawa anamuulizia mtoto alipowaeleza hali halisi walibadilika furaha ikapotea gafla maneno yakaanza sisi hatumtaki huyu aende akaolewe alipozalishwa mawifi ndy midomo kama yote yani maneno ni mengi hawanitaki wanataka aliezaa nae, nilijikaza ile siku ikapita
Baadae mwanaume wangu akaniambia yeye ananipenda sana na hawezi kuniacha na hawezi pia kukosana na ndugu zake kwaiyo atalipa mahari kwetu tuanze kuishi bila ndoa, halafu yule aliezaa nae ndy wafunge nae ndoa, sikumpa jibu la kueleweka,nawaza itakuaje nikikubali kuishi kama mchepuko na ninawaza itakuje nikiachana nae nampenda sana,,mwanagu amesha mzoea anajua ndy baba yake na majina nilishabadilisha nipo njia panda sijui niamue nini naomba ushauri wenu nifanyaje!!


4 Comments
Excellent beat ! I wish to apprentice even as you amend your web site, how can i subscribe for a blog web site? The account aided me a acceptable deal. I had been a little bit acquainted of this your broadcast provided brilliant clear concept
Hello my friend! I wish to say that this post is awesome, nice written and include almost all significant infos. I would like to see more posts like this.
Great awesome things here. I am very glad to look your post. Thanks a lot and i’m taking a look forward to contact you. Will you kindly drop me a mail?
I not to mention my friends were actually going through the good secrets on the blog and then the sudden developed a horrible suspicion I had not expressed respect to the site owner for those tips. Most of the guys came for this reason very interested to read all of them and now have clearly been taking pleasure in them. Thank you for simply being really accommodating and for considering varieties of incredible things most people are really desperate to discover. Our honest apologies for not saying thanks to earlier.