AAAHHH BOSS TARATIBU JOMON UTANITOA KIZAZI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU 01
Nyie kumbe maboss nao huwa wanapagawa kwa wafanya kazi wao, mwanzo sikuwa naamini kitu kama hicho ila baada ya kutokea kwangu ndo nikaja kuamini kabisa kwamba jambo hili lipo kweli.
Yani nikama ndoto ila hii story ni yakweli kabisa,amini usiamini msomaji wa story hii,
Ni furaha kubwa kwangu kwa mara ya kwanza kupendwa na boss kabisa kwa kupitia kazi yangu yakuwaa dereva wake mwishowe naenda kuwa mama mwenyewe nyumba,, alafu nyumba ambayo kila mmoja alishangaa aswa alipopita sehemu hiyo jinsi nyumba hiyo lilivyokuwa nzuri ,kila aliyepita pale alibaki amepigwa na butwaa
ANZA NAYO
Katikati ya jiji la Dodoma kulikuwa Kuna jumba moja nzuri lilovutia watu wengi pale, kila mmoja aliepita pale alipenda kusimama na kubaki akiwa amelitazama.
Kwa Jina naitwa NEEMA nimtoto wa kwanza na wamwisho kwenye familia ya mzee JUMA, ila kwa bahati mbaya mzee wangu sinaye tena. nilizaliwa mmoja tu kwenye familia yangu sina mdogo wangu wala mkubwa wangu, kwasababu wazazi wangu walikuwa na tatizo kwenye kizazi hivyo walibahatika kupata mtoto mmoja tu! Ambaye nimimi.
Katika pita zangu za hapa na pale, ndani ya jiji la Dodoma, nilikumbana na watu wengi wakiwa wamesimama kushangaa nyumba hilo.
Kwangu haikuwa mara ya yangu ya kwanza kuiona nyumba hiyo.
Kiufupi ilikuwa nyumba nzuri yenye kupendeza na kuvutia na kila mmoja aliyepita maeneo hayo, lazima ashangae kwa kusimama .
Nilitamani sana kuingia ndani ya jengo hilo ila sikuwa na kibari chochote istoshe ilikuwa nyumba ya mtu binafsi tu mwenye pesa zake hapo Dodoma kijana mdogo tu,aliyejipambania hadi kufikia hapo.
Daah kila mgeni aliyepita maeneo hayo basi alisimama nakubali ametahamaki kwa mshangaa🥱🥱🥱 jengo hilo.
Lilikuwa jengo la kawaida ila lilijengwa kidigitali fulani hivi, lilivutiwa na kila mmoja.
Basi mimi huyo na safari zangu ,toka mdogo nilikuwa na ndoto yakuwa DRIVE Yani nilipenda sana. kuendesha magari, nilipenda sana kazi hiyo.
Kwahiyo hata nilivyokuwa nasoma , nilisoma tu kwa lengo hilo, nakweli ndoto yangu iliweza kutimia, basi hiyo siku nilikuwa natoka kwenye mafunzo ya kuendesha gari.
Nilipenda sana kupita maeneo hayo, kwa ajili ya kushangaza kidogo jengo hilo.
Tujiachana na maswala ya jengo, nilirudi nyumbani nakumkuta mama akiwa busy akicheza game, wow mrembo wangu huyo amerudi ” aliongea mama wakati huo anaiweka simu yake chini kwa ajili ya kunikumbatia,
Mama alikuwa ananipenda sana kwasababu me ndo nilikuwa mtoto wa kipeke, toka baba amefariki mama hakuwahi kuolewa tena, na alidai hatukuja kuolewa mpaka anafariki.
Jamani mama umeanza najua ndio mimi ni mrembo kukuzudi ata wewe piya ila neno mrembo halikuishi mdomoni mwako mama .
Nilijaliwa uzuri na shepu nzuri ya kuvutia, mtaa huo hakuwepo binti nzuri kama mimi,, sio kwamba najisifia hapana ila kila mmoja aliuona uzuri wangu ,vijana wa mtaa huo walikuwa wakigombana kwa sababau yangu kila mmoja akidai anampenda neema.
Walikuwa wakibishana mpaka kupelekea ugomvi mkubwa kwasababu yangu, ila me sikuwa hata na ratiba hiyo sijui mambo ya mapenzi hayakuwa mambo yangu, me nikiwazia kutimiza ndoto yangu ya kuwa DRIVE tu wala sio kingine.
Nilitamani hata siku mmoja niendeshe magari niajiliwe, Yani mambo hayo tu niendeshe watalii wanaotoka nje ya nchi Daah hayo ndo yalikuwa maisha niliyoyatamani siku zote.
Nyumbani kwetu hatukuwa na maisha ya kimasikini wala kitajiri tulikuwa size ya kati,mama aliniuliza ” binti yangu chakula gani? Nikuandalie leo, mama angu alinipanda kama kwamba hata nikitoka kwenda kwenye minangaiko yangu alikuwa mtu wa kusonekana, Daah.
Sehemu 02
Jamani mama hata me naweza kukuandalia kitu ambacho unapenda sio kila siku utakuwa mtu wakaniuliza nikuandalie nini? Binti yangu.
Binti yangu unajua kabisa wewe ndo binti yangu wa kipekee hivyo natamani nikupatie kila aina ya upendo ila kuna baadhi ya vitu sina uwezo navyo binti yangu, hivo ninavyokuuliza jambo sitamani unibishie my daugher
Daau!!! Mama angu aliongea “kwa Uzuni sana. Jamani mama me sipendi useme hivyo napata kila kitu mama kutoka kwako hivyo narizika nakila kitu hata kikiwa kidogo mama angu hata we pia nimtu pekee uliobaki kwenye maisha yangu sina ndugu , we ndo ndugu yangu. We ndo baba, ndo mama, hivyo ukihudhunika mama najisikia vibaya kweli.
Mama ninacho kuomba nikuzidi kuniombea dua ili nifanikisha hiki ninachokipigania kwenye maisha yangu.
Basi mama alinikumbatia na kudai yupo pamoja na me kwa kila jambo na nivyema kama tukimtegemea Mungu kwa kila jambo. Yeye ndo kila kitu kwenye maisha yangu.
Basi mama aliingia jikoni kwa ajili ya kuniandalia chakula cha mchana , mama angu alikuwa mtu mashuhuri kwenye upishi alikuwa akifanya kazi hotelini,
mama alikuwa muajiliwa wa hoteli kubwa huko Dodoma, hivyo hata mimi namshukuru pia alinifundisha kila aina ya mapishi ila me upishi haikuwa fani yangu kabisa.
Basi nilichukua simu yangu nakuanza kuchat na rafiki yangu, SUMAIYA japo nilipenda kumfupisha jina lake nilipendelea kumuita sumy, sumy alikuwa rafiki yangu mkubwa sana. Tulikutana huko chuo hivyo urafiki wetu ulianzia hapo hadi sasa sina rafiki muaminifu kama Sumy.
Basi tulianza kuchart huku tukibadilisha mawazo, alikuwa akidai kwamba amepata boyfriend mpya , jamani sijui huyo binti atampenda nani? Na amuache nani ?
Maana yeye alidai kila mwanaume anayekuja kwenye maisha yake anaishia kumuumiza ila bado tu mwenzangu hakomagi Yani yeye ndo kwanza kapata mpya mapenzi jamani hata uumizwe kiasi gani? Kupenda bado iko palepale.
Basi bhana tuliendelea kuchat tukiongea swaga za hapa na pale, nakumbuka ilikuwa imebaki miezi miwili me kumaliza mafunzo yangu ya udrive .
Kwasababu nilikuwa nishaanza kuona matokea yangu hayakuwa mabaya tayari nilikuwa nishakuwa mbunifu katika hilo, nilianza kutuma maombi ya kazi mtandao huku nikimuomba Sumy pia anisaidie katika hilo
Nayeye hakukataa kwasababu me nayeye tumetoka mbali na kweli aliifanya kazi yangu kwa uharaka zaidi maana nilisema nikisubiri serikalini iniajili nitasubiri sana. Nilitamani hata nikipata mtu binafsi mwenye kulipa pesa kubwa kidogo basi me niko tayari.
SEHEMU YA 3
Sumy alianza kupost kwenye mitandao ya kijamii kama facebook, instagram YouTube, alipost kila sehemu alikijaribu walau kunitafutia kazi hakutaka kabisa kuniona nikiangaika.
Siku zilizidi kusonga mbele wakati huo siku zilizidi kupungua za mimi kuhitimu mafunzo ya udrive.
Nilitamani kuzitumia ndoto zangu, kwasababu sikuwa natka kumuona mama alipitia wakati mgumu ikiwa mimi bado nipo hai.
Wakati huo nami sikutaka kumuachia Sumy kila japo kwakuwa alikubali kunisaidia basi hata mimi pia nilianza kupost huku nilitamani walau nipate mtu binafsi wa kujisajili kwa ajili ya kupata riziki yeyote ile.
Siku hiyo iliweza kupita oasipo kupata taarifa yeyote ile hata kwa Sumy pia ilikuwa hivyo, sikukata tamaa niliamini ipo siku moja tu Mungu atanifungulia mirango ya riziki Yangu.
Niliendelea na mafunzo yangu ya udrive huku kila siku alipokuwa kuna mosi na jumapili ilikuwa siku ya mapumziko kwetu.
Hivyo tukibaki nyumbani kusaidia familia zetu majumbani, nakuomba ilikuwa siku ya ijumaa, wakati nipo zangu nyumbani nishatoka mafunzoni, simu ya Yangu iliita ,
Nikiwa jikoni wakati huo simu yangu ilikuwa sebreni chaji, nilitoka nafuraha sana. Niliamini wenda nitakuwa nimepata boss wakuniajili kazi.
Nilishikwa na hasira baada ya kugundua kwa Sumy ndo anaenipigia simu, Yani ile napokea simu yake basi nilianza matusi yangu ya kiutani
We zombi nilijua me kuna mtu labda ameona post yangu ya mtandaoni,kumbe niwewe nyau kabisa. Sumy alikuwa kashanizoe tu yeye alibaki tu kucheka akidai sijui lini nitaacha utoto wangu.
Haya nimekupigia tu simu kukwambia nimefunga chuo wiki mbili hivyo nimekumisi sana kesho nataka nije.
Jamani nilifurahi sana baada ya kusikia sumy Wangu anataka kuja, nilimwambia ” umechelewa wapi? Sasa kwanini usingekuja hata mda huu jamani .
Sehemu 04
Baada ya maongezi ya mda mrefu nilikata simu kisha nikaendelea na kazi zangu za hapa na pale wakati huo mama angu bado alikuwa kazini kwake hivyo isingekuwa vizuri kutoka kazini nakukuta ndani vitu vimezagaa kila kona
Majira ya saa kumi na mbili jioni nilipigiwa simu na namba ngeni, niliwahi kupokea ila nilikuja kukerwa baada ya kugundua ni sauti ya kelven kijana ambaye alikuwa ananitaka kimapenzi ila me sikuwa natayari kuwa naye kwenye mahusiano istoshe kitu mapenzi hakikuwa kwenye akili yangu.
Na mara nyingi nilipenda kumwambia me sipo tayari kuwa nayeye kwenye mahusiano ila yeye alikuwa king’ang’anizi sana. Yani mpaka kero.
Kiukweli nilimtukana sana. Nakumwambia akome kunitafuta na kila namba ambayo aniitumia kunitafutia huwa nazibrock ila yeye hakuchoka kubadilisha namba mpya akidai amenimic niliwahi kumtukana kila aina ya matusi ila aliona jambo la kawaida kwa upande wake.
Sijui hata namba yangu lilitolea wapi? Maana kila nilivyojaribu kumuuliza ninani aliyempatia namba yangu yeye huwa anadai namba kapata kwenye mtandao.
Kauri ambayo ilikuwa ikinikera sana.nilimwambia kuanzia leo akome kunitafuta kwasababu amekuwa msumbufu kwangu na baada ya hapo nilimkatia simu.
Ila hakuacha kupiga alinipiga tena na tena huku message za kila aina zikimiminika kwenye simu yangu, nilimuona kijana wa hovyo kweli hata hakujua kukataliwa jamani
Yani kuna wanaume vingang’anizi na kelvin alikuwa mwanaume kig’ang’anizi kweli hadi kero.
Baada ya kuona sms zimekuwa nyingi na mess call za kila aina niliamua kuibrock hiyo namba kwasababu sikutaka kabisa mazoea naye.
Niliendelea na kazi zangu za hapa na pale huku nikiandaa chakula cha usiku maana sikutaka kabisa mama atoke kazini kwake tena aanze kuingia jikoni. Japo yeye hakutaka kabisa kuniona napika
Baada ya kumaliza madiko diko huko jikoni na tayari ilikuwa imefika saa moja mda wakuangalia tamthilia niliweka vitu sawa kisha nikaketi sebreni kwa ajili ya kuianza tamthilia yangu THE Good son .
Unahisi mwisho wa kelvin kwangu utakuwa mwisho wa aina gani maana nilijaribu kila njia ila bado anaendelea kuwa king’ang’anizi kwa upande wangu.
Sehemu 05
Siku hiyo iliweza kupita na kesho yake majira ya saa saba mchana Sumy aliwasili nyumbani, nilifurahi sana nilimkumbatia sana nakudai nilikuwa nimemmic sana.
Siku hiyo mama naye hakuwa amenda kazini hivo siku hiyo tulishinda naye nyumbani tukipiga story za hapa na pale siku hiyo.
Story za hapa na pale basi nimuuliza Sumy je kama kuna mtu amepatikana katika post zetu ” aliniambia wamepatika wawili ila mmoja yupo dar es salaam na mwingine yupo Arusha ila mshahara wao nikama mdogo vile laki tatu kwa mwezi.
DAAH haikuwa riziki yangu Sumy kwasababu me sikutaka kabisa kwenda mbali na mzazi wangu nilitaka boss ambaye anapatikana ndani ya jiji hili la Dodoma maana sikutaka kabisa kwenda mbali na mama angu.
Waliniitia moyo” nakunimbia kwamba nisijali nitapata tu Sehemu iliyopo karibu na nyumbani , kwamba watajiri wameisha ndani ya jiji la Dodoma tulikuwa tumebaki siku chache kumaliza mafunzo ya udrive.
Mafunzo ya udrive ilikuwa miezi sita hadi mwaka kwa wale ambao walikuwa bado hawajaelewa hivo iliwalazimu wasome mwaka mzima.
Me sikuwa tena na ile kurudia kwasababu kila sheria ya udereva tayari nilikuwa nimeijua na namna ya kuendesha gari hivyo ilinilazimu nijifunze tu miezi sita.
Siku zilizidi kusonga mbele hatimaye siku ya kuhitimu iliwadia , tulifanya sherehe fulani la kujipongeza na baada ya hapo tulirudi majumbani kwetu huku tukisubiri ajira itakapo patika basi tuunge kambi
Tulirudi nyumbani huku nikusubiri nipigiwe tu simu kwasababu tayari nilikuwa nimetuma maombi ya kazi.
Zilipita siku tatu pasipo na muafaka wowote ule nilijikuta najikatia tamaa, ila mama pamoja na Sumy walinitia moyo wakidai Subra huvuta kheri .
Ni wiki mmoja sasa imepita yalikuwa majira ya usiku tukiwa busy na tamthilia yetu, simu yangu iliita namba ilikuwa ngeni.nilihisi wenda atakuwa kelvin amebadilisha tena Namba nyingine, nilisita kwenda ila Sumy pamoja na ” waliniambia nipokee wenda itakuwa simu ya kazi.
Nilienda kuipokea.
“Haloo.
” Sauti ya kiume ilisikika ikiwa tulivu kwenye ngome ya masikio yangu
” Habari neema. Kwa jina naitwa ABDU HAKIMU Nimeona tangazo kwenye mitandao ya kijamii hivyo nilikuwa nahitaji dereva wakuniendesha wakuwa ananipeleka kazini na jioni atakuwa anaifuta kwa ajili ya kunirudisha nyumbani,
Nipo dodoma mjini kwenye jengo la kubwa kuliko yote baada ya kusema hivo dhahiri nilijua kabisa litakuwa lile jengo ambalo kila mmoja akipita lazima ashangae.
Nilimjibu nakusema ” nipo tayari kufanya kazi ila sijui mshahara nikiasi gani? Mshahara ni laki saba kwa mwezi hivyo nakupa siku mbili ukiwa tayari basi ripota nyumbani kwangu asubuhi mapema ukiwa na vyeti vyako vya udereva .
Sawa boss nabaada ya mazungumzo nilikata simu, DAAH sikuwa naamini kabisa kama ndo nimepata kazi neema kweli mtoto wa juma .
Nilifurahi sana . Yani nikama bado sikuwa naamini yaani mpaka Sumy alivyonifinya, ndipo niliamini kabisa sio ndoto bali nikweli
INAENDELEA

