Wakaazi wa mji wa Migori walisalia katika sintofahamu baada ya mwanamume mmoja anayedaiwa kuvunja duka la simu kukamatwa na kundi la nyuki wanaosemekana kutumwa na mganga wa kiroho.
Kulingana na walioshuhudia tukio hilo, mshukiwa alionekana akikimbia sokoni akipiga kelele za kuomba msaada huku akiwa amefunikwa na nyuki wenye hasira ambao walimvamia usoni, shingoni na mikononi mwake. Mwanamume huyo aliripotiwa kukiri kwamba alikuwa ameiba simu kadhaa za rununu kutoka kwa duka la mahali hapo mapema asubuhi hiyo.
Walioshuhudia wanadai nyuki hao walianza kumzunguka mshukiwa huyo muda mfupi baada ya wizi huo, na kumlazimu kuacha vitu vilivyoibiwa na kupiga magoti chini kwa maumivu. Mmiliki wa duka Bw. Otieno, ambaye awali alitafuta usaidizi wa kiroho kutoka kwa huyo mganga baada ya kuibiwa mara kadhaa, alisema alishtuka lakini amefarijika.
“Nilikuwa nimepoteza simu nne katika wiki iliyopita. Nilimpigia simu mganga kwa usaidizi. Aliniambia nisiwe na wasiwasi – kwamba yeyote aliyehusika atakamatwa kwa njia ambayo hakuna mtu angesahau,” Otieno aliwaambia wanahabari.
Ndani ya saa chache, mshukiwa huyo alionekana barabarani akiwa amezungukwa na nyuki, akiomba msamaha na kuahidi kurudisha kila kitu.
Mganga anawaonya wengine dhidi ya wizi na ukosefu wa uaminifu
Alipotafutwa huyu mganga alithibitisha kufahamu tukio hilo lakini akawataka wananchi kutoona kazi yake ya kiroho kuwa yenye madhara.
“Ninatumia tu uwezo wa ukweli kuwafichua wakosaji,” alisema.
“Yeyote anayefanya wema hana hofu yoyote.”
Maafisa wa polisi baadaye walimuokoa mshukiwa na kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Migori kuhojiwa baada ya nyuki hao kuripotiwa kutawanyika wenyewe.
Wakazi wamemsifu huyo mganga kwa kile wanachotaja kuwa “haki ya kimungu,” wakisema kuingilia kati kwake kumerejesha utulivu na hofu miongoni mwa wezi wadogo katika eneo hilo.
Chanzo: Pulse News