BOSS NAONA AIBU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 11
“Nilipomaliza kidato cha sita kabla ya kuingia chuoni, baba alioa mwanamke mwingine, huyo aliharibu furaha ya mama na kutibua kila kitu kwenye familia yetu, familia yenye furaha na amani iligeuka familia yenye migogoro mingi sana, baba akawa analala nyumbani siku chache na siku nyingi anakwenda kulala kwa huyo mwanamke mdogo, aliyafanya hayo kwakua alipata pesa zake nyingi za mafao ya uafisa kilimo, kazi ambayo aliifanya kwa miaka mingi.
Baba angu alibadilika sana hata mimi nilipoingia chuo, kuzipata pesa zake zilikua kwa manati sana, mama alianza kuuza na kutembeza mboga za majani ili waweze kula nyumbani wakati huo baba anatumbua na huyo kimwana wake aliekua na umri sawa na dada angu wa kwanza kuzaliwa.
Miaka mitatu ya chuoni ilikwisha kwa bahati nzuri nilipata kazi kwenye hii kampuni angalau jua la utosi lililokua linaitesa familia yangu angalau lilipungua hivyo niliweza kuwahudumia na mama aliacha kuuza mboga kwa kutembeza majumbani kwa watu.
Baba pesa zake za mafao zilizopokwisha alikimbiwa na yule kimwana wake, akarudi kwa mama kuomba msamaha, mama akamsamehe maisha yakaendelea.
Ugomvi ulianza pale ambapo baba alitaka pesa zote nilizokua namtumia mama nimtumie yeye, nilimwelewa na kuanza kumtumia yeye ili ampe mama kumbe baba alirudiana kwa siri na yule kimwana wake, baba akawa hafikishi pesa kwa mama nyumbani ndipo nikaamua kufunga mrija wa pesa niliokua nautoa hapo ugomvi ukazuka kati yangu na yeye.
Baba alikua mkali sana na mimi nilimwambia siwezi kumpatia pesa kw sababu hii na hii, baba alinipa laana nyingi ndio maana mpaka leo hatuelewani kabisa” Sam aliweka kituo chake hapo na mimi nilipata jambo la kuchangia.
“Baba bado yupo na huyo kimwana wake au yupo nyumbani kwa mama?” niliuliza.
” Yupo nyumbani kwa mama”
“Bhasi unaonaje ukaamua kutengeneza nae suluhu, tuue kinyongo chote alichonacho dhidi yako, si upo tayari kwani kama itatokea mzee akafa na hiko kinyongo japo hatuombei itakua sio sawa kabisa”
“Tedy nyooka niambie tufanye hili na lile” “Nafikiria ukamwombe msamaha, japo kuna maeneo alikosea ila mkubwa hakosei, ni muhimu kushuka naamini atakuelewa tu na kuhusu maswala ya fedha unaweza kuja na mpango mpya ukawa unatenga pesa za baba unamtumia kivyake na zile za mama unamtumia kivyake, si imekaa sawa” Sam aliitikia kwamba atafanya kama nilivyomweleza.
Siku inayofuata tulifanya maandalizi tulinunua zawadi mbalimbali, tuliweka kwenye gari kwaajili ya safari ya kwenda kwa kina Sam.
Tulipanga siku hiyo, Sam akamwombe msamaha baba yake pia aitumie nafasi hiyo kunitambulisha.
“Unaamini mpango utalipa, nilimhakikishia kwa asilimia mia moja lazima mpango ulipe, kabla ya kuanza safari alinikumbatia, akanipiga busu, wote tunapenda lile deep hivyo tulipeana kwa dakika mbili tatu akawasha gari tukaanza safari yetu, tulienda mpaka nje ya geti la nyumbani kwao.
Mlinzi alifungua geti tuliingia ndani, alifika mama Sam kuja kutupokea gafla alitokea baba Sam akiwa na panga alianza kumkimbiza Sam akimtaka aondoke nyumbani kwake, kimbembe hiko.
Chapter 12
“Mume wangu tafadhali mwache mtoto jamani, usimfanyie hivyo” mama Sam alijitahidi kumtuliza mumewe lakini akili ya baba Sam Ilikua kama pilipili kichaa ndo kwanza ilizidi kuwasha.
Kwa presha mama wa watu alikwenda chini moja kwa moja, hapo hakuna aliwaza swala kukimbia wala kukimbizwa, baba Sam anaita mke wangu.
Sam anaita mama, walianza kumpepea kwa dakika kumi ndipo mama Sam alizinduka walimbeba na kumpeleka ndani.
“Mama ako ameshazinduka sasa, mchukue kila kilicho cha kwenu muondoke sasa, sitaki kuwaona” Baba Sam aliirudisha mada mwanzo tena.
“Tulia bhasi mume wangu nikuombe ombi moja la mwisho najua hii presha inaweza kuniua muda wowote, nakuomba umsikilize mtoto, nataka wakati nitakaokufa bhasi uwe umemsikiliza japo kidogo mtoto, nakuomba sana mume wangu jamani ihhhhhh Mama Sam aliongea maneno mazito huku akilia, alionesha kutopendezwa na vita iliyokua inaendelea kati ya baba Sam na Sam.
“Bhasi mke wangu naomba unyamaze, hutokufa sasa baby, unataka ufe utaniacha na nani jamani, naomba ujitulize mahabuba wangu” Baba Sam alimbembeleza mkewe na vijimaneno fulani vya kimapenzi, nilijua kumbe mchombezo ambao nilikua naupata kwa Sam ni kwamba amerithi kutoka kwa baba yake.
“Ndo umsikilize sasa mtoto, ugomvi wenu utanipandisha presha na nijifie zangu, nimechoka vita zenu mimi”
“Sawa mke wangu nitamsikiliza mtoto, naomba usilie tena, hasira zitakupelekea pabaya. Enhe dogo niambie jambo gani limekuleta hapa?”
“Msamaha, nimekuja kukuomba msamaha baba angu, si vyema kuishi namna hii tunayoishi mimi na wewe kama baba na mwana, hii leo nilivyo mimi mchapakazi ni matokeo ya mambo mazuri uliyonifundisha huko nyuma, kama nimekubeba wewe mzima bhasi naomba unikunjulie moyo na unisamehe, huko nyuma niliongea maneno mabaya, naomba unisamehe ili maisha mengine yaendelee
“Umelijua kosa lako?” Baba Sam aliuliza.
“Ndio nimelijua ndo maana niko hapa, nahitaji msamaha baba angu ili niwe na amani ya moyo”
“Kama umelijua kosa lako bhasi nimekusamehe na nafuta maneno yote ya laana ambayo nilikutamkia ukafanikiwe mwanangu” Baba Sam alikunjua roho na moyo, alimsamehe Sam na kumtamkia maneno ya baraka. Wote tulifurahi sana, vicheko vilitawala, tuliwapa zawadi ambazo tulikuja nazo.
Pia Sam aliwapa account ya benki yenye millioni tano, aliwapa account hiyo ya pamoja ili iwafae katika mambo mbalimbali.
Wanawake wote tulipiga vigelegele. Kuku mkubwa na bata walichinjwa.
Tulikula kweli kweli, baada ya chakula Sam aliamua kunitambulisha kwa wazazi wake kama mimi ndie mwanamke wa maisha yake, hakuna ambae alipinga walinipongeza na kunikaribisha kwenye familia yao.
Nilijisikia furaha na amani kuwa hapo, niliitamani zaidi siku ya ndoa yetu, tuliaga na kuondoka. Tukiwa njiani Sam aliniambia kwamba siku inayofuata ni zamu ya kwenda kwa wazazi wangu, ila tuanze na kaka angu ambae tuligombana yeye atakapo nisamehe bhasi tutakua na ndoa yenye baraka kutoka pande zote mbili tulikubaliana kwamba siku inayofuata tutakwenda kwa kaka.
Chapter 13
Tulifanya maandalizi yote muhimu, tulinunua na zawadi muhimu, tukapanda gari na kwenda mpaka nyumbani kwa kaka, maajabu ambayo niliyakuta hapo yaliniumiza sana.
Kaka alikua nje anaosha vyombo na mkewe yupo busy akichat kwenye simu yake.
Kaka kuniona alijifanya kama anaacha hiyo kazi lakini mkewe alimzuia.
“Weee unakwenda wapi, acha kuosha vyombo nikuoneshe hutokula mchana wala usiku kwa siku mbili hiyo ndo adhabu yako” wifi yangu aliongea maneno hayo bila kujali uwepo wetu, nilimjua ni kiburi sana mwanamke huyo.
“Sasa mke wangu si wageni wamefika nyumbani lazima tuwapokee na kuwasikiliza kwanza, karibuni sana” Kaka aliongea kwa sauti ya unyenyekevu na kutukaribisha.
“Nyumba, nyumba gani wee una nyumba hapa, nakwenda ndani nisikie unawaleta hao wajinga wenzako kwenye nyumba yangu ndio utanijua leo, wakiondoka unaondoka nao siwezi kufuga mbwa asiefugika mimi” Wifi aliongea maneno machafu dhidi yetu na dhidi ya kaka.
“Wee mwanamke ambae uliokotwa jalalani huko hujui kupika wala kula ndo unamuita nani mbwa koko?” Niliamua kuingilia ugomvi huo.
“Wewe na ukoo wako wenu wote yaani nyie wote ni mbwa ndo maana mmetoka huko kote kuja kwangu ili mje kula mikoko yaoneni kama majinga maneno na kiburi alichonacho dawa yake nilikua nayo mimi kwani kabla ya kaka kunifukuza nyumbani kwake nilishawahi mbutua, nikamfunga kamba na kumnyofoa nywele zake kichwani kwa dharau alizokua anajionesha, nilijua labda atakua na kumbukumbu na kipondo changu kumbe alikua hajakoma, nilimkamata nilimpiga vbao viwili vitatu vya moto.
Sam aliniwahi kunikamata, mikono nikarusha mteke ukamkwatua mtama chini akaanguka chini, alikimbilia mawe ili anipige nayo bahati nzuri mumewe akamkamata na kumfungia ndani, aliendelea kutukana matusi makubwa makubwa.
Kaka alituomba msamaha na kutukaribisha kwenye kivuli cha mti wa mwembe uliokua mahali hapo.
“Karibu sana mdogo angu naomba uniwie radhi kwa hiki kilichotokea naona umekuja na mgeni karibuni sana kaka aliongea kutuliza kile ambacho kilikua knaendelea mahali hapo.
“Ahsante kaka kwahiyo ndo ule mdomo mchafu utaishi nao mpaka lini si umrudishe kwao, ili akajifunze adabu nzuri, mwanamke gani anakua na mdomo mchafu kuzidi choo cha sokoni” “Acha tu mdogo angu nguvu hiyo sina tena kwani kila kilichokua cha kwangu huko nyuma. kimekua chakwake, ni ujinga ambao nilifanya mwenyewe sahivi najutia sana”
“Heee umeniacha hapo kaka sijakuelewa vizuri, kazia kidogo
“Mdogo angu kama kuna wajinga ambao ulikua unawajua kwenye hii dunia bhasi kwenye hiyo list niongezee na mimi, ulipokua unaniambia kwamba mke wangu ni mtu mbaya anaingiza wanaume ndani na wewe upo, nilijua unanidanganya labda umetumwa kuvunja ndoa yangu, baada ya kuzuzuliwa na upendo, nikaona kwakua wanaume wengi tunakufa mapema kuliko wanawake, nikaona ili ndugu msije msumbua mke wangu siku ambayo nitakufa, niliandika kila kitu kwa jina lake, hapo ndipo niliona makucha yake binafsi, alibadilika na kunioneshea ile tabia aliyokua nayo awali, akaanza kunitumikisha, upendo uliisha na hapa ninavyoongea ameambukizwa virusi vya ukimwi na ananilazimisha nilale nae bila hivyo ananifukuza nyumbani, nimekua napitia ugumu wa maisha sana mdogo angu” kaka aliongea kwa kutia huruma sana, nami nilimwonea huruma kaka angu nikampa pole na kumwuliza upi mpango wake wa maisha.
“Nilikua natafuta nauli ya kurudi nyumbani Songea ili nikalime tu bhasi, ndoa ilipofikia siwezi kuitibu tena, wacha nimwachie mali na kila kitu ili nikaanze upya namimi nilisapoti wazo hilo hivyo tulimgongea wifi afungue mlango ili kaka achukue nguo zake.
Wifi aligoma kabisa kufungua mlango hivyo tuliondoka hivyo hivyo, tuliondoka mahali hapo kwa kutumia gari tulikwenda mpaka kwa Sam, tulilala usiku huo kesho yake tulikua kwenye ndege kuelekea Songea, tulishukia uwanja wa ndege wa Ruhuwiko, tukachukua gari mpaka Peramiho walipokua wanaishi wazazi wangu, kukanyaga tu Peramiho mazito yalinikumba.
Chapter 14 & 15
Tulifika siku hiyo tulipokelewa kwa furaha zote, wazazi walituchinjia kuku wawili wa kienyeji tulikula kwa furaha sana, tulilala na siku Inayofuata tulishinda, ilipofika jioni Sam aliniomba twende tukatembee angalau tufike hata dukani tuweze kununua vocha, tulikubaliana na kwenda, japo wakati tunaondoka mama alituomba tuwahi kabla ya giza kuzama.
Tulikubali tulipofika dukani tulinunua vocha na kuanza kurudi nyumbani taratibu sana njiani nilikutana na Vick alikuwa rafiki angu kweli ambae nilisoma nae shule ya msingi, tulisimama kusalimiana pale, alinieleza kwamba anao watoto wanne na hakua ameolewa mpaka wakati huo, nilimpa pole kwa changanoto hiyo, aliniuliza juu ya Sam kama ni shemeji ake, nilimkatalia katakata na kumwambia ni rafiki angu tu amepitia nyumbani mara moja, akakubali na majibu yangu japo aliniomba pesa akapate kununua mboga ya kupika na watoto wake.
Sam alimwonea huruma kutokana na mwonekano wake na watoto aliokua nao tena anawalea peke ake bila msaada wa baba alitoa wallet na kutoa noti mbili za elfu kumi kumi na kumkabidhi Vick, nilitamani kuzuia japo nilishindwa kwa kuonekana nina roho mbaya ila niliwajua watu wa kijiji hiko wasivyo na wema unaweza toa kitu kwa mapenzi na upendo wote Ila wao wakageuza fimbo ya kukuchapia.
Vick alishukuru sana huku akipiga magoti kwa shukrani hizo, tulimuaga na kuondoka zetu mpaka nyumbani, tulikula tena ugali na nyama ya ng’ombe, siku mbili hizo zilikua nzuri sana, nilimtambulisha Sam kwamba ni mchumba wangu nae alitoa barua ya uchumba, wazazi walipokea barua hiyo wakati tunaendelea kuongea mara nikaanza kuona malue lue, mara nawataja ndugu zangu waliokufa, nikaanza kukimbia wakanikamata na kunifunga kamba.
Mume wangu mtarajiwa Sam alihisi kuchanganyikiwa kwa jambo hilo, usiku huo huo kaka alienda kijiji cha mpitimbi kwenda kumfuata bibi mmoja ambae ni mtaalamu wa manyanga, yule bibi alipofika alianza kufanya mambo yake, kwenye chungu kila mmoja akaona namna ambavyo Vick alichota mchanga mahali ambapo nilikanyaga na kwenda kufanyia mambo yake ya dawa ili nichanganyikiwe na nibaki hapo hapo kijijini ila marafiki mmmmh, wanapenda wote tuendelee kuwa wa chinintu ukionesha kupanda kidogo tayari umeshakua mbaya kwao lazima watafute namna ya kukushusha tu.
Kaka alienda mpaka kwa kina Vick, alimwomba Vick waongozane kuja nyumbani. Vick alikataa kabisa, kaka akamwambia usinitanie akaanza kumvuta kwa nguvu alitoka mama Vick ili kumtetea mwanae alipigwa ngumi moja ya mdomo jiko kule, Vick alivutwa kwa nguvu mpaka nyumbani.
Kaka angu alikua na ubabe wake wa asili sijui kwanini alikua anateswa na mkewe au ndo kusema hata mwenye nguvu Samsoni alikutana na chuma cha kuitwa delilah.
Vick aliwekwa mbele yangu anitazame nilivyokua nahangaika, aliambiwa anitoe mavitu yake mabaya aliyonitumia kuivuruga akili yangu, Vick aligoma kwamba hausiki kwa lolote lile.
Yule bibi mganga akaanza manyanga yake akauchukua ugonjwa na kumtumia Vick, akawa anaweweseka yaani hali niliyokua nayo mimi ndo ikamvaa yeye, bibi mganga alikua kiboko.
Inaendelea…….