BOSS NAONA AIBU
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
Chapter 6
“Sam unafanya nini eti, kwanini hivi lakini?” Saraphina aliongea huku akianza kulia, hakuwepo wakati sisi tunacheza, aliporudi alitukuta tumekumbatiana kwwa mahaba mazito, alitaka kunipiga lakini Sam alinikwepesha na kuniweka upande mwingine.
Watazamaji walizidi kushangazwa na jambo hilo, bado Sam alitaka kulazimisha kuendelea kunikumbatia, Saraphina alikua anazuia huku akilia kwa kilio kikubwa sana.
Watu wawili wafanyakazi pale ofisini walimwomba Sam aachane na swala la kunikumbatia, kila kitu kiliharibika hapo hapo ikabidi turudi hotelini hatukulala tena kwenye mahema kama tulivyotarajia
“Naomba unisamehe Tedy kwa kilichotokea, kama itawezekana naomba tuzungumze kwa kuonana” Sam alinitumia ujumbe mfupi akitaka tuonane.
“Hapana Sam wacha usiku upite tu tutaongea huko mbeleni” nilimjibu..
“Ni sawa ila nisamehe kwanza, hata ukisamehe bila kusahau siku ambayo nitakuelekeza kila kitu utanisamehe na kusahau ila sitaki nikupoteze wala nikukose, niamini mimi wewe ndo unaenifaa kwenye kwenye hii dunia Sam alijimaliza, hata mimi nilimpenda kiukweli ukweli lakini kwa kilichotokea kilikua kinanipa maswali mengi sana kichwani mwangu.
“Ni sawa nimekusamehe naomba tulale bhasi”
“Poa kipenzi changu ulale unono eeeh” nilimjibu jumbe hiyo na kumtaka asisahau kusali kabisa.
Nilijitupa kitandani, niliamka asubuhi, nilijiandaa kabisa, tulitoka nje kunywa chai na saa nne tulianza safari ya kutoka Mara kwenda mwanza tulipofika tukapanda ndege mpaka dar, tuliwasindikiza wageni wetu mpaka hotelini watakapolala na siku inayofuata wasafiri kurudi kwao uholanzi
Wakati wote nilikua karibu na Sam kwani ndie nilimzoea kuliko wote.
Kitendo hiko kilikua kinampa jaka la roho Saraphina kwani alichukizwa nacho sana, yeye alikua karibu na kaka mmoja hivi aliitwa Hussein ndie alikua akimfariji fariji kuna muda alimwomba nafasi Sam ili waweze kuzungumza ila Sam alikataa kabisa hivyo alizidi kunichukia mimi.
Dereva wa Sam alikuja kutupokea, aliniomba niende nae kwake, awamu hii ilibidi kukubali tu kwani sikua na mahali pengine pa kwenda sikua na mshahara wa kunifanya nipange chumba. kwani ilikua bado sijalipwa, pia sikutaka kuiuza simu yangu tena kwani niliona ina umuhimu mkubwa kwa shughuli mbalimbali za kiofisi kwani mpaka taarifa muhimu zilikua zinatumwa kwenye group la ofisini, kwahiyo nisingekua na simu ningepitwa na mambo mengi sana.
Tukaingia kwenye gari tukaondoka zetu kwenda mpaka nyumbani kwa Sam, jumba lilikua zuri sana, alikua anaishi kwenye jengo lenye hadhi kubwa sana, kulikua na watu watatu tu, mfanyakazi wa ndani, na mlinzi wa getini, dereva alikua anakuja na kuondoka.
Nilioneshwa chumba changu ambacho ningekitumia kilikua chumba kizuri sana.
Sam aliniita ili tuzungumze vizuri nami nilimwambia
“Usiku wa jana sijalala vizuri kabisa, nakuomba unielezee ni nini kilichopo nyuma ya Saraphina kuchukia namna ile, kwani umeniingiza kwenye uadui ambao sikutarajia, naomba unieleze kila kitu usinifiche kama vitaniumiza ni sawa ila kama vitanipa ahueni litakua jambo zuri sana kwangu kwani nitalala usiku huu kwa amani sana” nilimweleza vile ninavyojisikia.
“Sawa kaa hapa nikupe kitu kidogo Sam aliniweka kwenye kochi vizuri alifungua friji na kuchukua kikontena, alikifungua kilikua na chocolate nyingi sana tena ya baridi.
Alichukua kijiko na kuchota Chocolate alinilisha. “Kula hii ni dawa ya mood mbaya, kwahiyo kula ujitulize ili niweze kukuelezea vizuri kabisa” nilikubali na kupokea kijiko cha chocolate nililishwa kama mtoto vijiko vitano hivi ndipo aliweka chini na kunambia sasa yupo tayari kunieleza kila kitu kuhusu Saraphina na yeye.
Chapter 7
“Unanitazama mimi, nina umri wa miaka thelathini, huko nyuma nilikua na malengo makubwa sana kwamba nitaoa kabla ya kuzidi umri wa miaka thelathini, katika pita pita zangu na kuona kwangu nilimwona Saraphina kama mwanamke atakae nifaa, nikiwa boss wake nilivunja mipaka ya uboss na kushusha maneno yaliyobeba hisia zangu za moyo, nilimweleza ninavyojisikia juu yake, pia nilimweleza malengo ya ndoa niliyokua nayo kwake, Iwamba sikutaka kumchezea kabisa, bahati nzuri Saraphina alinikubalia hiyo ilikua mwaka jana na nilipanga mwaka huu ndio tufunge ndoa takatifu, miezi sita iliyopita siku moja nikiwa ofisini nilikua naelekea ofisini kwa Hussein kabla ya kufungua mlango nilisikia maongezi kati ya Saraphina na Hussen na hapo ndipo nilijua kumbe Hussein na Saraphina walikua kwenye huba zito, kumbe Saraphina hakua akinipenda mimi hata kidogo, kunikubalia kwake ilikua ni sehemu ya shinikizo kutoka kwa Hussein kwamba anikubali aishi na mimi hata tukiingia kwenye ndoa baada ya miaka mitano atakua kachota pesa nyingi kutoka kwangu pia ataomba talaka, pesa tutakayo gawana kwa hizo mali pasu kwa pasu, achukue akaanzishe maisha na Hussein wake, nilipolijua hilo nilimshukuru sana Mungu kwani alinionesha picha halisi ya kiumbe ambacho nilitaka kukioa, sikumweleza kwamba nilijua kila kitu, nilijifanya mjinga mpaka siku nitakayotaka kuoa ajishuhudie mwenyewe kwamba mimi sikua boya kama wao walivyofikiria, ndio hivyo mama angu Sam alifunguka kila kitu kuhusu yeye na Saraphina.
“Umelijua kosa lako hapo?” nilimuuliza. “Mmmh hapana, niambie kama umeona “Ni hiko kipengele cha kutokumwambia kwani anahesabu mpaka sasa wewe ni mwanaume wake tena utamuoa, ndio maana hakupata utulivu pale ulipotaka kunivisha pete, hapa tunajitengenezea maadui wakubwa bila sisi kujua, unachotakiwa ni kufanya jambo moja tu, kuwaeleza kwamba umejua ukweli wote kuwahusu wao ili uwamalize nguvu zote za kutufuatilia” nilitoa ushauri wangu.
“Aiseeh umenishauri jambo zuri sana, kweli umejawa na hekima nyingi mke wangu mtarajiwa, kuna siri ambayo nitawapa wanaume wengi huko duniani ni kwamba haikuhitaji kutumia miaka mitano au sita ili kumjua mke wa kweli, wakati mwingine kwa uwezo wa Mungu ni siku mbili au tatu unajua mke mwema yupoje, namimi nilikupima kwenye hizo siku nikajua huu mgodi wa madini sitaki kuupoteza mimi, kiufupi nitakuganda mpaka nikuoe”
“Hahahaha wewe tena tulijikuta tunacheka wenyewe kwa furaha, alinisogeza karibu na kunikumbatia.
Mara simu yake ya mkononi ilianza kuita, aliitazama mpigaji ni Hussein.
“Boss boss Saraphina anakunywa sumu huku, boss wahili umtulize anasema usipokuja anakufa” Hussein alitoa taarifa mbaya kutokea upande wa pili wa simu.
“Mko wapi, hebu niambie nije hapo haraka” “Niko nae nyumbani kwake boss, jitahidi uwahi mkuu”
“Sawa nakuja simu ilikata na Sam alikua ananitazama mimi.
“Usiende” nilimwambia kwa uwazi kabisa sikuona kama kuna wema kwenye safari hiyo. “Hata kama simpendi ila ni binadamu mwenzangu anayo haki ya kuishi ngoja nikamuokoe akipona kwenye hili sitokua na hatia, narudi muda sio mrefu” Sam aliongea na kuondoka, sikuweza kumzuia nilimwacha aende tu kama alivyotaka.
Chapter 8
Sam aliondoka mwenyewe kwani wakati huo hakutaka kumsumbua dereva alishaenda kupumzika nyumbani kwake, Sam alikua kwenye mwendo mkali ili kufika nyumbani kwa Saraphina haraka ili aweze kuyanusuru maisha ya mwanamke huyo.
Akiwa njiani alijitahidi kulikwenda lori moja la mizigo lililokua linaendeshwa na dereva mlevi, Sam alishindwa kulihimili gari alijikuta anaingia mtaloni na gari kupinduka hapo hapo.
Watu waliokua karibu na eneo hilo waliwahi kutoa msaada walimtoa nje Sam akiwa hajitambui, walitoa taarifa police, Ambulace ilifika na kumchukua Sam kumpeleka hospitalini kwaajili ya matibabu zaidi.
Mimi nilipewa taarifa asubuhi, niliwahi hospitalini haraka, niliomba kumwona mgonjwa nilielezwa kwamba bado alikua kwenye usaidizi wa kitabibu, niliendelea kusubiri hapo huku nikimwomba sana Mungu aweze kumponya Sam wangu, jioni ndipo niliruhusiwa kumwona japo niliambiwa nisimguse wala kumpigia kelele kwani ningemsababishia mengine, niliingia humo chumbani nilikuta bandeji imezunguka kichwa ni sehemu ya uso tu ndo ilikua wazi, mwilini sikuweza kutazama zaidi kwani alikua kafunikwa kwa shuka.
Nilishindwa kuzuia machozi yangu kunitoka, kumwona mwanaume huyo katika hali hiyo nilijikuta naumia sana moyoni mwangu, nesi aliingia na kunambia muda wangu umekwisha nimfuate.
Tuliongozana na nesi mpaka kwa daktari ofisini kwake, nilikaribishwa na kukaa kwenye kiti.
“Wewe ndo mtu wa karibu na mgonjwa, wacha nikueleze tu ukweli ni kwamba kutokana na ajari ambayo ameipata mgonjwa, figo zote mbili zimepata changamoto kubwa hivyo anatakiwa kuchangiwa figo mpya haraka sana ili kunusuru uhai wake nenda kazungumze na ndugu wengine huko, ili tuwapime kwa pamoja akipatikana mwenye figo zinazoendana bhasi amchangie mgonjwa ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida” niliyakubali maneno ya dokta japo yalikua na uchungu ndani yake, nilitoka mpaka walipokua wafanyakazi wezangu, niliwapata taarifa hiyo juu ya kumchangia Sam figo.
Hussein na Saraphina walikua ni watu wa kwanza kuondoka, walifuatia wengine kila mmoja kwa kijisababu chake.
Kiutuuzima nilikielewa kitendo hiko kwamba walikwepa kumchangia figo Sam, ndio maana waliondoka kwa mtindo huo, nilikumbuka namna walivyokua wanaonesha wanampenda huko ofisini nikaringanishe na hali ya hapo nikapata jambo moja kichwani kwamba pata matatizo uwajue walio wakwako na ambao sio wakwako. Nilijikuta peke angu na mgonjwa, nikiwa sina msaada mwingine wa mtu yeyote.
Chapter 9
Nikiwa kwenye dimbwi la mawazo alifika mfanyakazi wa ndani, nilimwuliza kama kuna ndugu wa Sam anawafahamu, alinijibu ndio, nilimuuliz kuhusu namba zao hilo lilikua gumu kwake, maana hakua na hizo namba, tuliulizia kwa madaktari juu ya simu ya Sam ili tutafute namba huko napo hatukufua dafu kwani namba ya simu ilikosekana.
Nikarudi nyumbani na mfanyakazi tulianza kupekua hapa na pale tuliikuta namba moja kwenye nitebook ya zamani kweli, iliandikwa Hero, niliipiga namba hiyo, alipokea mzee fulani nilisalimia kwa heshima zote, mzee alinitaka niende moja kwa moja kwenye sababu ya kumpigia nilinwambia juu ya ajari ya Sam, mzee alinijibu.
“Hilo mimi halinihusu binti, mtafute mama ake, haiwezekani mimi nimsomeshe na kumfikisha hapo alipo ila akitaka kufanya jambo lolote lazima amshirikishe mama ake, akitaka kutuma pesa nyumbani anamtumia mama ake, wakati anasoma akiwa na shida ya ada au pesa ya matumizi alikua anajua kuna baba, saivi ana mali na maisha mazuri, baba kaniweka wa mwisho, sio mbaya mimi nimemwachia Mungu ndo maana nasema hivi kwenye hayo matatizo mwambie mama ake mzee aliongea kwa uchungu namna alivyokua anatengwa kwenye matunda ya mtoto wake huyo, aliona Sam amempa kipaumbele sana mama ake.
“Samahani baba, sasa namba za mama mimi sina naomba unitumie ili tuokoe maisha ya Sam yupo kwenye hali mbaya baba angu nakwambia” nilinyenyekea zaidi ili mzee anielewe.
“Weeee mtoto, hizo namba mimi sitoi mtoto ambae hana faida na mimi wa nini acha afe tu” mzee aliongea maneno machafu yalionesha chuki nzito aliyonayo kwa Sam.
Sikutaka kumpigia tena hivyo niliendelea kupekua notebook hiyo, mwishoni nikakuta namba nyingine imeandikwa my everything, niliipiga namba hiyo alipokea mmama, nilimsalimia aliitikia nilimpa taarifa juu ya ajari aliyoipata Sam, nilimuwahi na kumtuliza atulie kwanza kwani mgonjwa anaendelea vizuri, sikutaka kumpa taarifa kwamba anahitaji figo.
Nilihofia kufanya hivyo kwani mama angezimia au lolote baya lingempata, nilimweleza ni hospitali gani yupo, mimi na mfanyakazi tulitoka kuelekea hospitalini huko nilikutana na mama Sam akiwa na dada zake wawili, tulienda ofisi ya daktari.
Walipewa taarifa hiyo ya Sam kuhitaji kuchangiwa figo, wote watatu walikua tayari kumchangia figo lakini daktari alikataa kwa mama ila kwa hao dada zake ilikua sawa, walipelekwa chumba cha uchunguzi baada ya masaa matatu, daktari alitoka akiwa na karatasi ya majibu mkononi mwake, wote tulitulia ili kumsikiliza.
“Majibu yanaonesha wote wawili hamuwezi kumchangia figo mgonjwa labda mlete mtu mwingine wa kumchangia” taarifa hiyo ya daktari iliibua simanzi, ilizima mwanga hafifu uliokua unaonekana.
Mama Sam alipiga magoti mbele yangu na kuniomba huku akilia kwamba nimchangie mwanae figo, dada zake pia walinisihi nimchangie kaka yao figo.
Mimi akili haikua hapo nilifikiria kuhusu swala hilo nilikumbuka visa vya watu waliowahi kuchangia figo kisa mapenzi na wakaachwa vibaya sana huku wakikosa mahali pa kujishikiza, nilikua kwenye mvutano mkubwa wa mawazo na akili.
Chapter 10
“Usipige magoti mama, nipo tayari kumchangia” niliamua kukubali tu, nilijivika mabomu kama siku nitaachwa ni sawa tu kwanza sikujiumba pili ipo siku nitakufa tu, wacha nifanye msaada iwe sadaka yangu kwa maisha ya mtu.
Nilichukuliwa na kupelekwa chumba cha uchunguzi, huko walifanya mambo yao, niliruhusiwa kutoka. Majibu yaliyokuja yalikua mazuri sana kwani figo yangu na yake zilikua zinaendana, pia nikitolewa figo bado nitaweza kuendelea na maisha ya kawaida pasipo figo kuleta shida yoyote, tulimshukuru Mungu kwa hatua hiyo.
Niliandaliwa na kupelekwa chumba cha upasuaji, nilichumwa sindano ya nusu kaputi, figo yangu iliondolewa mwilini mwangu na kuwekwa kwa Sam, nilizinduka baada ya siku tatu, nilifumbua macho yangu taratibu na kutazama pembeni, kulikua na kitandana, nilimwona Sam amelala juu yake akinitazama, alinisalimia kwa tabasamu, nami nilimjibu kwa tabasamu, hizo zilikua lugha za mapenzi, hatukufungua vinywa vyetu bali tuliiruhusu mioyo yetu iweze kuzungumza.
Tulikaa hospitalini kwa wiki mbili, madaktari wakituwekea ukaribu zaidi na kutuchunguza maendeleo ya figo zetu ndipo tuliruhusiwa kutoka na kurudi nyumbani, tulikaa wiki mbili nyingine pasipo kwenda kazini, mpaka pale tulipokua wazima kabisa.
Siku moja tukiwa eneo la bustani, nilikaa na Sam tukisukumana kwenye bembea, alikua ananifundisha namna ya kubembea kwani nilikua mwoga sana wa kubembea tangu udogoni sikupenda kabisa, kwani nilikua nahisi kizunguzungu endapo mtu atanisukuma kwenda mbali, pia nilikua mwoga wa kuanguka na kuumia, bila Sam kunilazimisha wala nisingekaa kwenye hiyo bembea yake.
“Naomba nikuulize swali hivi uko sawa na baba ako aliekuzaa, kwani tangu uumwe na umepona sijawahi mwona akija nyumbani hapa kukutembelea hata mara moja, hii sio kawaida kabisa
“Tuachane na mambo ya mzee muhimu tumepona na maisha yanaendelea ni vizuri inatosha”
“Hapana nieleze kuna nini, ulisema tutaambatana kwenye haya maisha sioni sababu ya kuendelea kufichana kama kweli tumeamua kusafiri pamoja kwenye hii safari ya upendo”
“Aaaaaaah ukianza kung’ang’ania lako sasa ndo utalibeba weeeh, haya nakueleza leo ila sitaki uniulize tena kwani mambo haya huwa sipendi kuyaongelea kabisa”
“Sawa niambie, sitokuuliza tena”
“Unajua mimi na mzee tulikua kitu kimoja na tulipendana sana na baba yangu, ila kuna jambo moja alilifanya hilo ndo lilifanya tupishane na yeye kunitamkia maneno ya laana kabisa, huenda ni mtu anaetamani nife hata kesho, kuliko kuniona naendelea kuishi, huenda Inamchukiza sana” Sam aliongea, nilikua tayari kusikiliza jambo hilo alilolifanya mpaka kutamkiwa maneno ya laana na mzazi, tena baba kutamani mtoto wake kufa, yalikua ni maajabu mengine ya dunia ambayo nilikua nayasikia.
Inaendelea………