Mwanamke Aanguka na Kufa, Akiwa Kwenye Mtoko wa Kimapenzi
Kijana mmoja kutoka Kimilili, Kaunti ya Bungoma, anatatizika kukubaliana na kifo cha ghafla cha mpenziwe, Edith Nanjala Ajuma, aliyeaga dunia katika hali ya kuhuzunisha baada ya kutoka kimapenzi.
Kulingana na mpenzi wake, Emmanuel Makokha, wawili hao walikuwa wameenda matembezini mkasa ulipotokea.
Alisema walipokuwa wakitembea, Nanjala aliteleza na kuanguka.
Alipojaribu kuinuka, alianguka tena, akaumia mkono na kutengua mguu wake.
Makokha alisema walikimbilia katika zahanati ya jirani kwa ajili ya kupata huduma ya kwanza, ambapo Nanjala alitibiwa na kupewa dawa.
Baadaye alirejelewa katika hospitali ya kaunti ndogo baada ya hali yake kuwa mbaya.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 23, ambaye alikuwa na mtoto wa miezi tisa, alisisitiza kusalia wodini na mtoto wake licha ya wauguzi kuonya kwamba afya ya mtoto huyo inaweza kuwa hatarini.
Baadaye, afya yake ilianza kuzorota haraka. Makokha alisimulia kuwa Nanjala alinyamaza ghafla na hakuweza kuongea tena, alibaki akitazama tu bila kutamka neno lolote.
Madaktari walimshauri afanyiwe uchunguzi wa CT scan ili kuangalia uwezekano wa kuharibika kwa ubongo, lakini hakuna masuala yoyote yaliyopatikana, na bado alibakia hana la kusema.
Madaktari hao baadaye walimhamisha katika hospitali ya kaunti kwa matibabu zaidi, lakini alifariki muda mfupi baada ya kuwasili.
Uchunguzi wa maiti bado haujafanywa ili kubaini chanzo cha kifo.
Akiwa amehuzunishwa na msiba huo, Makokha alisema bado yuko kwenye mshtuko na hajapona maumivu.
Familia hiyo sasa inatafuta usaidizi wa kifedha ili kulipa bili za hospitali na kumpa Nanjala kwaheri nzuri.
Chanzo: RIP: Beautiful Photo of Bungoma Woman Who Collapsed and Died While on Romantic Date with Boyfriend