KWA MAPENZI HAYA LAZIMA TU NIMSALITI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 16
“Sio kitu, nipo kawaida tu…hivi ule mzigo hawawezi kuiba kweli?” Niliamua kubadili mada
“Hawawezi, ile ni kampuni ambayo inaaminiwa na watu wengi, yaani hata ukikaa mwaka mmoja lazima mzigo wako utaukuta. Hata hivyo bado haujafika, si unajua tena meli ina bandari nyingi? Tutegemee baada ya siku 28 au 30 mzigo utafika”
Tuliendelea kupiga stori, jioni ya siku hiyo niliruhusiwa nitoke nje kwaajili ya kufanya mzoezi madogo madogo kama kutembea, kunyosha mikono juu na kadhalika. Joshua ndiye alikuwa akinisaidia kufanya mazoezi hayo, pia daktari ambaye alikuwa akinitibu alikuwa pamoja nami akichunguza afya yangu. Wiki ya pili ilikatika nikiwa hospitali, sikuhisi maumivu tena, pia niliacha kutembea kwa kutumia magongo, mkono wangu niliweza kuukunja na kuukunjua, kwa kifupi naweza sema nilipona kwa asilimia 90%. Nilifurahi sana kurudi kwenye hali yangu, kila nikikumbuka ajali ya ndege nilijikuta natoa machozi kisha nilimshukuru Mungu.
Tofauti nyingine ya hospitali za ulaya na zetu ni kwamba licha ya madaktari kuona nimepona kwa kiasi kikubwa lakini hawakuniruhusu niondoke, walitaka kuona kama afya yangu itazidi kuimalika au vipi. Ili wajihakikishie walinipa ratiba ya mazoezi, ndani ya hospitali kulikuwa na chumba cha mazoezi, sio kwaajili ya kunyanyua vifua au kutafuta six pack; hapana, bali ni kwaajili ya kuweka viungo sawa, kukomaza vilivyolegea na kuimarisha afya za wagonjwa. Nilifanya mazoezi kwa wiki moja, siku ya mwisho ya wiki nilikuwa ngangari, hata ukinipa jezi niliweza kucheza mpira, kukimbia hata kupigana. Hatimaye niliruhusiwa kurudi nyumbani, mimi na Joshua tulielekea nyumbani kwake.
****
Tulifika nyumbani kwa Joshua, kwanza nilipagawa kuona mjengo wa maana, japo sio wa ghorofa ila alijitahidi sana, nilimuuliza alijengaje jumba lote hilo? Alicheka kisha aliniambia alijenga kupitia mishe mishe za mjini. Nilimuuliza ni mishe gani anafanya lakini hakuniambia, nilipotezea kwa sababu watu wengine huwa hawataki kuweka wazi biashara zao. Pia kilichonipeleka marekani sio kujua biashara ya Joshua bali kufanya biashara yangu ya mchele.
Ilibaki wiki moja tupokee mzigo wa mchele, kabla hatujapokea ilibidi tutengeneze mazingira ya biashara. Kwanza tulitengeneza mpango kazi wa biashara, Joshua ndiye aliongoza kila kitu, alikuwa mchangamfu sana, alinielekeza namna biashara itakavyokuwa, wateja watatoka wapi, duka litakaa wapi, faida itapatikanaje kisha tulizungumza namna tutakavyosimamia biashara. Tulikubaliana kwamba yeye Joshua atasimamia kila kitu, pia katika mauzo yote atakuwa anachukua asilimia 30% ambazo ndiyo malipo ya ke. Baada ya kupanga kila kitu ilibidi tutafute frame kabla mzigo haujaingia, uzuri ni kwamba licha ya kupata ajali lakini pesa zangu zilikuwa benki; hivyo basi pesa zangu zilibaki salama. Tuliingia mtaani kutafuta eneo la biashara, kila tulikopita Joshua alijuana na watu kama wote, wengi walikuwa ni vijana wa mitaani, kutokana na umaarufu huo tulipata jengo flani hivi kubwa, jengo hilo lilifanana na majengo ya vibanda umiza vya huku kwetu Tanzania. Joshua aliniambia kuwa zamani katika jengo hilo kuna mtu alikuwa akionyesha sinema, hivyo basi ni jengo zuri kwa kuweka mizigo ya mchele kisha kuisambaza kwa watu. Kilichotakiwa ni ukarabati tu, tulielekea benki nilitoa fed h a kisha tulienda kulipa kodi ya jengo, nililipa kwa miezi mitatu.
Tulifanya ukarabati na matengenezo machache; jengo lilikaa poa kwaajili ya biashara.
Hatim aye siku ya meli kuwasili ilifika, tulienda ofisi za ndege tulipokea mzigo wetu, tuliusafirisha hadi kwenye jengo la biashara. Kitu kilichonishangaza ni kwamba yaani ile tumefika tu nilishtuka kukuta foleni kubwa ya watu, kumbe Joshua ndiye alitoa matangazo kuhusu ujio wa mchele huo. Hadi muda huo duka langu halikuwa na jina, ila watu walikuwa wakipiga kelele wakisema “Tunataka mchele wa Tanzania, tunataka mchele wa Tanzania” Hapo sasa tulipata jina la duka ambalo ni “MCHELE WA TANZANIA”. Siku ile ile tulianza kuuza mchele, tuliuza kwa kutumia mifuko maalumu, yaani tunapima tunaweka kwenye mifuko kisha tunauza. Tofauti na kwetu, kule kwa wenzetu mchele kidogo pesa nyingi, gunia la elfu 80 bongo, kule kwa wenzetu unauza hadi laki tatu. Siku ya kwanza tu tuliuza kwa zaidi ya Dollar 2000 na mchele ulibaki wa kutosha. Siku ya pili wateja waliongezeka, tuliuza kwa dollar zaidi ya 3000, siku ya tatu dollar zaidi ya 4000, kuna ambao walikuwa wakija kisha walitaka kubeba mfuko mzima wa mchele. Wao hata kupima hawakutaka, mfuko wa dollar 2000 anakuambia nitalipia dollar 5000. Hadi inakatika wiki moja duka lilibaki jeupee, mifuko ya mchele ilibaki michache, ilibidi tusiuze kwa jumla; tulikubaliana tuuze kwa reja reja ili tu pate nafasi ya kuagiza mchele mwingine.
“Nilikuambia kuwa hii ni marekani sio bongo. Si umeona tulivyouza haraka haraka?” Joshua aliniuliza
“Kaka hadi nachanganyikiwa”
“Usichanganyikiwe, huu ni mwanzo tu lakini hadi sasa tushapiga zaidi ya millioni 150, hapa ukitoa gharama zingine zote unapata faida kama million 120 hivi….Sasa hapa inabidi huu mchele uliobaki niwe nauza taratibu, wewe itabidi urudi ukaandae mzigo mwingine; au umeishiwa?”
“Ah siwezi kuishiwa, kule nina roba za mchele kama zote”
Tulicheka kwa furaha ya ushindi, tulipata faida kubwa kuliko mategemeo yetu. Jioni tulirudi nyumbani kwa Joshua, kitu kingine kilichonishangaza ni kwamba mimi huwa najua kuwa Joshua kaoa, lakini hadi siku hiyo sikumuona mke wa Joshua. Mbaya zaidi kila siku usiku jamaa alikuwa anatembelewa na dem mpya, analala nae hadi asubuhi kisha dem huyo anaondoka. Nilijaribu kumuuliza kuhusu mke aliniambia hajaoa na wala hana mpango, siku hiyo alitaka anipeleke kwenye kumbi za starehe lakini nilikataa. Alinisisitiza akiniambia marekani ukiwa na pesa usizibanie, inabidi uburudike na watoto wakali lakini nilikataa. Kwakuwa ni rafiki yangu alinielewa, tulitulia nyumbani hadi usiku. Baada ya chakula cha usiku tulicheza game la mpira, mara mlango uligongwa, sikushangaa sana kwa sababu nilijua ni dem mpya wa Joshua. Ni kweli aliingia mtoto mkali, ila mrembo huyo hakuwa pekeyake; aliongozana na mwenzie mkali. Walionekana ni watoto wa mjini! Yaani ile wameingia tu; mrembo mmoja alienda kukaa juu ya mapaja ya Joshua, yule mwingine alikaa pembeni yangu.
SEHEMU YA 17
Michezo ambayo iliendelea muda huo ni ya kimapenzi, sikumshangaa sana Joshua kwa sababu hiyo ni tabia yake tangu tukiwa shule sekondari. Kuna muda aliacha kucheza game kisha alidendeka na mpenzi wake, sikutaka kushuhudia mengi; nilimuaga nilielekea chumbani kwangu kulala. Nikiwa kitandani nilimkumbuka mke wangu, nilitamani kama ningekuwa nae usiku huo. Mawazo ya mke wangu yaliisha mara baada ya kumkumbuka Docra, nilimuwaza hadi nilijikuta natoa machozi ya kijinga, hata mimi mwenyewe sikujua kwanini namlilia Docra; ila ukweli ni kwamba nilimmiss sana, nilitamani ule ukorofi wake na michezo yake, ukarimu na uchangamfu wake, kubwa zaidi alinijali sana.
Sasa nikiwa bize namuwaza Docra mara mlango wa chumba changu uligongwa, niliganda nikishangaa kwa sababu sio kawaida. Nilihisi labda ni Joshua kuna kitu anataka kuniambia, nikiwa nimevaa bukta yangu nilienda kufungua mlango; badala ya kukutana na Joshua nilikutana na yule mrembo mwingine ambaye alikuja na dem wa Joshua, nilishtuka kidogo kisha nilitulia tukitazamana.
“Sweetheart, can I sleep with you tonight?'” aliniambia akiwa anatabasam, kabla hata sijamjibu alizama ndani alienda kukaa kitandani kwangu. Hakuishia hapo bali alivuta shuka alijifunika kisha aliniita kwa ishara ya mkono.
Bado niliganda mlangoni, nilihisi kama nimevamiwa na pepo la ajabu, yule changudoa baada ya kuona nimezubaa aliamua kunichangamsha na kunipagawisha; kwanza aliondoa shuka kisha alivua gauni ambalo alivaa, alibakiwa na chupi kama chupi, hapo sasa alianza kujigeuza pale kitandani, mara alikata mauno kama yondo sister, kuna muda aliinama alinionyesha madude yake ya nyuma ambayo yalitikisika kama matikiti vile, moyoni nilijisemea “kumekucha”. Licha ya mbwembwe zake lakini hata sikushtuka, nilikuwa kama nimehasiwa vile, nilitamani nimfuate pale pale nikamuondoe ila sikujua nitamuondoa kwa lugha gani kwa sababu mwenzangu anaongea kinge tu. Kuna muda niliwaza nikamuondoe kwa nguvu ila niliogopa kwa sababu hiyo ni nchi ya watu. Nikiwa najiuliza nini cha kufanya ghafla alinifuata kwa spidi, alinivuta hadi kitandani, alinikumbatia akitaka kunibaka.
“We mdada usinipandishe..ebu niachiee”
“What are you talking? Give me Love baby”
“We bebi wako nani nyau wewe, ila nyie makahaba wa marekani sijui mpoje…Mtu hata hunijui unanivamia tu…Sepa kabla sijakutwanga kofi.”
Kile kidada hakikusikia wala hakikuelewa, nilikitazama kwa macho makali kisha kimoyomoyo nilisema “kumbe wewe hunijui”, nilirusha kofi zito lilitua shavuni kwake, hapo sasa aliniachia, aliniogopa akijua mimi sio wa kunichezea, haraka haraka alivaa nguo zake kisha alikimbia alitoka nje, sikujua alielekea wapi, nilienda kufunga mlango kisha nilirudi kitandani nililala kwa raha zangu.
*****
Kulikucha asubuhi na mapema, baada ya kuamka nilikuta Joshua akifanya usafi wa nyumba, tulisalimiana kisha nilimsaidia. Alionekana sio mchangamfu sana, pia hata hakunitazama, alikuwa kama ananionea aibu vile. Mimi nilijua kwanini, nilijua ni kwa sababu ya kile kidem cha jana, nilijua kabisa kuwa ule ni mtego wa Joshua alidhani nitapiga yule dem; aliona aibu kwa sababu sikupiga. Sasa ili kumuondoa aibu niliamua kumpigisha stori.
“Unajua nini kaka? Hivi unajua kuwa yule dem aliyekuja na dem wako alinifuata chumbani jana usiku?’
“Wee! usiniambie” Alijidai kama hajui vile
“Ndo nakuambia hivyo, mwanzoni nilifurahi kuona nimetembelewa na mtoto mkali chumbani, ila unajua nini; mwanangu una nyota ya madem wakali”
“Ah ah ah! mi si unajuaga mambo yangu tangu enzi za school, mi bishoo! Madem wa hapa NY wananikubali kinoma, ndio mana unaona kila siku anazama dem mpya…Jana niliamua kuwaita madem wawili nilitaka kabla hujaondoka uonje ladha za wamarekani…Sasa kwanini hukupiga?’
“We acha tu, sio kwamba sikutaka; nilitaka sana ila nilishindwa kufanya hivyo kwakuwa sikuwa na king a”
“Ungesemaa, mi kinga ninazo za kutoshaa…dah ulifeli sana…ila haina noma, ukija tena tutaweka mambo sawa.”
“Haina shida kaka” Hadi kufikia hapo tayari niliiteka akili ya Joshua, nilifanya afurahi sana.
Mara tulisikia “ngo ngo n g o” mlango uligongwa, Joshua alinitazama kisha alitabasam, aliniambia kuwa hiyo ni supu ya ke ya asubuhi. Yaani jamaa anawazaga ngono muda wote, haraka haraka alikimbia hadi mlangoni kisha alifungua, alikutana na mtoto mkali, toto la nguvu, si unajua tena Joshua mzee wa madem? Alitaka amkumbatie binti wa watu lakini mrembo alikwepa kisha alizama ndani alikuja kunikumbatia, alinitwanga mabusu kama yote, sikuamini kama ningeweza kukutana tena na Docra, wote wawili tulijikuta tunatoa machozi ya furaha, nilimtazama Joshua nilimuona akinionea wivu, kwa aibu jamaa alielekea chumbani kwake.
SEHEMU YA 18
Mimi na Docra tulikumbatiana kwa dakika zaidi ya 3, hakuna aliyetamani kumuachia mwenzie, hata sisi wenyewe hatukujua kwanini tulikumbatiana kwa namna ile, ni Mungu pekee ndiye alijua. Baada ya burudani tamu ya dakika chache Docra aliniachia kisha alinitazama usoni, alitabasam kwa furaha kisha alinikumbatia kwa mara ya pili. Safari hii alitoa machozi ya ukweli ukweli, alilala kifuani kwangu kisha alilia kabisa, nilimtuliza kwa kuzichezea nywele zake, nilimpapasa taratibu hadi alitulia. “Tangu ile siku tumeachana nilifungiwa ndani, baba hakuniruhusu nitoke nje. Nilitegemea wewe ungenitafuta hadi upajue nyumbani kwetu lakini hukufanya hivyo; kwanini hukunitafuta? Au ulinisahau? Hukuwa na muda na mimi? Hukunikumbuka tena? Hukunimiss?” Aliniambia akijitoa kifuani kwangu kisha alinitazama kwa uchungu. “Nisamehe sana ila kila siku nilikuwa nakuota”
“Kweli?”
“Ndiyo. Hakuna siku ilipita alafu nisikukumbuke. Nilishindwa kukutafuta kwa sababu mbalimbali, kwanza nililazwa hospitali kwa wiki tatu, tangu nipone nina wiki moja, bado siijui mitaa, na katika hiyo wiki moja nilikuwa nakamilisha ile biashara ambayo nilikuambia…Nisamehe tena na tena, ukweli ni kwamba nakukumbuka muda wote, nakujali na nimekuwa nikikumiss muda na masaa yote…Docra” Nilimuita kwa sauti ndogo
“Abee”
“Wewe ni mwanamke ambaye sidhani kama nitakuja kukusahau, sijui nikuite nani kwa sasa, ila nakuona kama binti aliyeshushwa toka juu mbinguni, umekuja ili unionyeshe umuhimu wa upendo wa kweli”
Baada ya kuongea mashairi yangu alinikumbatia kwa mara ya tatu, safari hii hakunipiga busu la shavuni ila la mdomoni, ukimuondoa mke wangu sipendagi mwanamke mwingine anipige busu la mdomoni lakini kwa Docra nilishindwa kuzuia, nilimuacha anibusu tu. Busu halikudumu kwa muda mrefu, aliniachia kisha alinielezea namna alivyoishi kwa tabu kutokana na kuniwaza sana, alinieleza kuwa ni mara nyingi alijaribu kutoroka nyumbani ila alikamatwa na walinzi. Pia hata siku ambayo alienda shopping hakwenda pekeyake bali alipelekwa na mabodigadi. Nilimuuliza ilikuwaje siku hiyo alipata nafasi? Aliniambia kuwa amewatoroka walinzi.
“Na ulijuaje kama nipo hapa?”
“Baada ya kuwatoroka walinzi nilielekea kwenye hospitali ya jeshi, kule waliniambia umepelekwa hospitali ya “The Bronx”. Nilielekea hadi huko ambako waliniambia kuwa umeondoka na Joshua” “Kwani wewe unamjua Joshua?” Nilimuuliza kwa shauku ya kutaka kujua
“Sio sana..naomba tutoke tukatembee, kuna kitu nataka nikakuambie”
“Dah! Kwa leo itashindikana kwa sababu naondoka naelekea Tanzania kuandaa mzigo mwingine, ule wa mwanzo umeisha” “Wee kweli? kumbe mchele unauzika hivyo? hongera sana…Basi kama ni hivyo naomba tuondoke wote”
Nilishtuka kuona Docra anataka tuondoke wote, nilimuuliza kwanini? Alinijibu kuwa likizo imeisha pia alitaka asafiri na mimi. Pia nilipata wasiwasi kuwa baba yake anaweza akakataa, aliniambia kuwa kwenye masuala ya kurudi chuoni mzee wake huwa hazingui. Nilifurahi kusikia hivyo kwa sababu hata mimi nilitamani muda wote niwe karibu na Docra, nilimuita Joshua nilimuaga rasmi; Jamaa alitaka atupeleke ila Docra alizuia alimuambia Joshua abaki tu. Kabla sijaondoka Joshua aliniita pembeni kisha aliniuliza kuhusu Docra, nilimueleza kuwa mimi na Docra ndio watu ambao tulipona kwenye ndege. Joshua baada ya kusikia hivyo alinipa ÅŸifa kemkem, aliniambia kuwa nimepata bahati ya kuwa karibu na mrembo wa nguvu, pia aliniomba namba ya Docra lakini nilikataa. Alinilazimisha sana niliamua kumpa ya uongo. Mwisho alinikumbusha kuhusu kuwaisha mzigo, baada ya mzungumzo mafupi mimi na Docra tuliondoka.
Kwanza Docra alitaka kunipeleka kwao, njia nzima nilikuwa namkatalia lakini alinilazimisha kwa nguvu zote, aliniambia kuwa kwa muda huo baba yake hakuwepo. Nilikubali kishingo upande, alichukua uber tulizama ndani tulielekea kwao. Ulikuwa ni bonge la mjengo, alinishika mkono alinivuta kuelekea ndani. Mlangoni tulikutana na kizuizi, walinzi hawakutaka kuniruhusu niingie, hata hivyo kutokana na kauli za Docra waliamua kuniacha nizame ndani, Docra aliwafokea walinzi kama wadogo zake vile. Tulifika ndani ya mjengo, hakukuwa na mtu hata mmoja, ni sisi tu ndo tulitawala nyumba. Tatizo la Docra ana mambo mengi, badala ya kujiandaa tuondoke eti alifungulia mziki kisha alianza kucheza m bele yangu, mara alinivuta akitaka tucheze, nilikataa nilimwambia tuondoke lakini alisema bila kucheza hatuondoki. Ilibidi nicheze tu, sasa ningefanyaje?. Tulitulizwa na mlango ambao ulifunguliwa, haraka haraka nilikimbia nilienda kukaa kwenye sofa nikidhani ni baba yake Docra, lakini hakuwa baba yake bali ni bodgadi ambaye alionekana kumtafuta Docra. “Ulikuwa wapi? kwanini ulitutoroka? Baba yako unamjua, ulitaka atuachishe kazi au?” Bodgadi aliongea kwa masikitiko
“Mimi sio mtoto mdogo, hamuwezi mkanilinda kila sehemu…Kwanza mpigie daddy mwambie naondoka narudi nyumbani”
SEHEMU YA 19
Bodgadi alifanya kama alivyoambiwa, alimpigia baba yake Docra kisha alimueleza kuhusu safari ya mwanae. Mzee alikubali ila alimuambia bodgad ampeleke Docra hadi uwanja wa ndege hata hivyo Docra alikataa kupelekwa na bodgadi, yeye alitaka aongozane na mimi tu, tuliondoka tulielekea uwanja wa ndege wa New York, njiani alinipitisha shopping, alinunua vitu pia alininunulia zawadi nyingi tu. Moja ya zawadi ambayo sitoisahau ni boksa, bila hata aibu alininunulia boksa nzuri kabisa. Nilishindwa kukataa, niliipokea kwa mikono miwili. Alafu sasa alivyo msumbufu aliniambia na mimi nimnunulie zawadi nzuri ambayo angeikubali. Nilimnunulia hereni lakini alikataa, nilimnunulia bangili alikataa, vipodozi alikataa, gauni na suruali alikataa, nilimnunulia chupi alikubali kwa mikono miwili; alinikumbatia kwa nguvu kisha alinibusu kwa furaha ya ajabu. Maajabu ya zawadi hayakuishia hapo, tulizunguka madukani kisha tulisimama pembeni ya duka kubwa la simu;
“Derick”
“Naam”
“Najua kwa sasa una pesa, sio kwamba nataka nikuchune; hapana, ila naomba uninunulie simu”
“Nikununulie simu?” Nilishtuka pia nilimshangaa aliniomba nifanye kitu ambacho sikutarajia
“Yeah, na nimesikia Iphone wametoa simu mpya, nitafurahi nikiwa wa kwanza kutumia simu hiyo”
Angekuwa mwanamke mwingine ningesema kuwa ameanza kunichuna, lakini kwa mwanamke kama Docra aliongea vile kwa sababu ya upendo tu. Simu ambayo Docra aliitaka ni Apple Iphone 12 pro max ambazo ni toleo jipya, simu hizo ziliachiwa rasmi October 2020 na gharama yake kibongobongo ni 2,650,000. Ni pesa nyingi, na ukizingatia mimi nilishazoea kutumia simu za laki moja na nusu hadi laki 3 alafu eti nitoe mamilioni nimnunulie mtu simu? Dah! Ukisikia majaribu ya shetani ndo kama hayo. Pesa nilikuwanayo ila ni pesa ya biashara, sipendagi kabisa kuchanganya biashara na ishu zingine. Hata hivyo licha ya ubahili wangu sijui nilikumbwa na jinamizi gani mimi, nikiwa natabasam nilikubali kumnunulia Docra simu ya mamilioni, tulielekea dukani kisha nilimnunulia, alifurahi sana.
“Asante Derick, asante kwa zawadi hii…Hatimaye leo nimepata zawadi ya simu toka kwa mwanaume, nashukuru sana”
“Usijali”
“Najua hukutarajia kama ungetoa pesa nyingi kuninunulia zawadi, pia najua umetoa pesa zako za biashara, najua tangu uzaliwe hujawahi kununua simu ya bei kubwa kama hii, mbaya zaidi umeninunulia mimi ambaye tangu tujuane hata wiki 6 hatujamaliza. Hata hivyo nashukuru kuna kitu kimekushawishi uninunulie, sidhani kama umeona hasara kuninunulia, eti umepata hasara?”
“Sidhani kama itatokea siku nitajuta kukununulia chochote, binafsi hata kama ungeniambia nikununulie gari sijui kama ningekataa..Wewe ni mtu ambaye nashindwa kukuelezea” “Asante, na kama umepata hasara bası naomba wote tupate hasara, nawe nakununulia simu kama yangu ili wote tuwe sawa”
Nilidhani anatania, mara alifungua pochi yake alihesabu mamilioni kisha alininunulia simu kama ile ambayo nilimnunulia, nilijikuta nafurahi tu. Baada ya manunuzi tuliondoka tukiwa tumebeba zawadi mikononi, tulifika uwanja wa ndege, tulichukua ticketi kisha tulizama ndani. Kama kawaida yetu tulikaa pamoja, kwa ufupi ni kwamba tulianza kufanana, tulikuwa kama mapacha, mara anipige picha, mara nimpige picha, kuna muda tulipiga picha ya pamoja, vuruÄŸu za Docra zilifanya nisahau mambo mengi, hata mke wangu mwenyewe nilimsahau. Kabla muhudumu hajatuambia tufunge mkanda nilimkumbusha Docra afunge mkanda, alicheka kwa furaha kisha aliniambia kuwa nimeanza kumkosha. Ndege yetu ilianza safari mida ya saa tano asubuhi, tulimuomba Mungu akatufikishe salama huko tuendako.
*****
Saa moja usiku tulifika salama nchini Kenya. Mipango yetu ilikuwa ni kufika Dar siku hiyo hiyo, hata hivyo tulikosa usafiri. Hakukuwa na ndege wala basi litokalo Kenya kwenda Tanzania usiku huo. Sote wawili tulikubaliana tukalale hoteli kisha asubuhi turudi nyumbani. Pembeni ya uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta kulikuwa na hoteli nyingi tu, tena za bei kali. Docra yeye aling’ang’ania tukalale hotel za gharama, mi nilikataa, tulienda kwenye hoteli moja hivi ya bei nafuu iitwayo Zarita boutique. Ilikuwa ni hoteli ya kawaida tu lakini ina kila kitu.
Kwakuwa sisi ni jinsia tofauti ilibidi tulale vyumba tofauti, na ukicheki mimi na Docra sio wapenzi, kwanza nishakula kiapo cha kutokusaliti; sikutaka kabisa kulala na mwanamke katika godoro moja. Tulichukua vyumba viwili, Docra aliingia chumbani kwake; nami nilizama kwangu. Niliingia bafuni nilioga kisha nilirudi chumbani nilivaa nguo zangu zile zile. Ukiondoa nguo ambazo nilinunuliwa na Docra sikuwa na nguo zingine kwa sababu zile za mwanzo zilipotelea kwenye ndege. Muhudumu aliniletea chakula kisha aliondoka, sikutaka kula pekeyangu, nilijua lazima Docra atataka tule pamoja. Ni kweli kabla sijakaa sawa mlango wa chumba changu ulifunguliwa, aliingia Docra akiwa amevaa kigauni cha kulalia, pia mkononi alibeba chakula alikiweka mezani. Alinishangaa kuona nimevaa nguo zangu zile zile.
“Kwanini umevaa manguo machafu? We si nilikununulia nguo? Ebu zivae bwana…Tena vaa hapa hapa nikuone..” Aliongea kama utanı lakini hakutania, nilimkatalia lakini Docra ni mbishi sijapata kuona, alafu hapendi kukataliwa vitu, ukimkatalia analia au ananuna.
“Poa nabadili, ila naombatoka nje”
“Nitoke nje ili iweje? Kwan i nikiwa hapa nguo hazivaliki?…alafu nikuambie kitu Derick”
“Niambie”
“Asante sana kwa ile chupi ambayo ulininunulia, tangu nizaliwe sijawahi pewa zawadi kama ile…kubwa zaidi nimependa namna ambavyo ulijua kukadiria umbo langu, ile chupi imenitosha na imenipendeza sana…Bila shaka utapenda nikuonyeshe namna ambavyo imenipendeza, subiri nikuonyeshe”
SEHEMU YA 20
Nilitaka kukataa lakini nilichelewa, Docra alipandisha nguo ya kulalia juu kisha alinionyesha chupi yake, nisiwe mnafiki jamani, naomba niongee ukweli; licha ya kiapo nilichokula kwa mke wangu nilijikuta nameza mate ya tamaa, umbo la Docra lilinichanganya, mbaya zaidi hata kule chini kwangu kulianza kutetemeka, nilipandwa na joto tamu la mahaba, nilijikuta nimezubaa kama chizi aliyerogwa tena, nilitamani kama mimi ndiye ningeivua ile chupi ya mwanamke niliyemuona mbele yangu kisha ningeutumia mwili wake; lakini ndo hivyo ilishindikana, niliapa kwamba endapo nitasaliti basi nitakufa hapo hapo, niliogopa kuuvunja huo mwiko!. Kumbe wakati nimezubaa nikimtazama mtoto mkali, Docra nae aliganda akitazama suruali yangu ambayo ilienda mbele nyuma, mtoto wa watu alimeza mate ya utamu utamu kisha aliniita;
“Derick”
“Naam”
“Naomba nawe uvae boksa ambayo nilikununulia, nataka nikuone” Sijui hata nilivurugwa na shetani gani, kwanza nilianza na shati niliivua niliitupia pembeni, nilishika suruali niliivua, ndani nilibakiwa na boksa yangu ya zamani, nilivuta boksa mpya nikitaka kuivaa, Docra aliona aibu; aligeuka nyuma ili asinione nikiwa nabadili nguo yangu ya ndani. Kwa muda huo sikuona aibu wala nini, nilivua boksa ya zamani kisha nilivaa boksa mpya, taratibu nilimfuata Docra kisha nilimshika begani; weuwee! Alishtuka kwa nguvu kisha alitetemeka kama ana degedege vile, nusura azimie kwa mshtuko, alikosa nguvu, pia niliyasikia mate yake yakitoka mdomoni kisha yalishuka chini ya koromeo, alikuwa kama anataka kukimbia vile.
“Docra asante kwa kunijali pia asante kwa zawadi hii ya boksa nzuri, hata mimi nashangaa kuona umeninunulia kitu ambacho kimenitosha kama ulinipima vile, haya naomba ugeuke ili unione” Nilimuambia nikimgeuza ili ageuke lakini hakutaka kugeuka.
Zilipita sekunde nyingi Docra alisimama vile vile kama roboti, hakutaka kugeuka kunitazama, kwa hali aliyokuwanayo muda huo unaweza sema ni katoto kadogo ambako hakajui kusoma wala kuandika, aliniogopa hadi nilijiuliza kwanini aliniambia nivue nguo. Nikiwa najiuliza atageuka muda gani mara ghafla aligeuka alinitazama kidogo tu kisha alikimbia kwa spidi kali alielekea chumbani kwake, nilibaki nacheka kama kichaa vile.
Baada ya Docra kuondoka hapo sasa akili zangu timamu zilirudi, nilitikisa kichwa kulia kushoto nikiweka ubongo wangu sawa, pia nilijipiga vibao nilijiadhibu kwa ushetani wangu wa kumvulia nguo mwanamke haÅŸiye mke wangu, japo hatukutumiana lakini tulichokifanya ni ujinga wa hali ya juu. Nilitazama kwenye mfuko wa zawadi ambazo nilinunuliwa na Docra nilikuta kuna suruali ya track, niliivaa kisha nilielekea kwenye meza ya chakula, nilibeba vyakula vyote nilimfuata Docra chumbani kwake; nilimkuta kalala kitandani akiwa amejifunika shuka gubigubi hadi kichwani, nilicheka kwa raha zangu! niliweka chakula mezani kisha nilienda kumuamsha. Ilikuwa ni shughuli, hakutaka kuamka kwa sababu alinionea aibu, mwili wake haukufanana na aibu ambazo alinionyesha; hakufanana kabisa. Nilichukua chakula nilikipeleka pale pale kitandani, nilimbembeleza hadi aliamka, ili kumchanganya zaidi niliamua kumlisha, mara alichangamka, nae alianza kunilisha, tulisahau yaliyopita kisha tuliganga yajayo.
Baada ya chakula kama kawaida yetu tulisimuliana stori na simulizi nyingi, hadi inafika saa tano usiku bado tulikuwa macho. Mida ya saa sita wote tuliisi uchovu, Docra alianza kusinzia, tuliagana kisha nilielekea chumbani kwangu, nilijitupa kitandani nililala, licha ya uchovu lakini nilichelewa kupata usingizi, muda wote nilimuwazia Docra sikumpatia majibu, hatim aye nilipitiwa na usingizi.
****
Kulikucha asubuhi na mapema, mimi ndiye nilianza kuamka, baada ya kumshukuru Mungu kwa kunipa siku mpya kitu cha pili kukikumbuka ilikuwa ni simu yangu, nilikutana na meseji nyingi toka kwa watu ila nyingi zilitoka kwa mke wangu, pia missed call za mke wangu zilijaa kwenye simu. Alitaka kujua nipo wapi kwa sababu nilimuambia kuwa narudi nyumbani. Nilimpigia simu kisha nilimuambia kuwa nipo Kenya najiandaa kurudi nyumbani Mbeya Tanzania. Mke wangu alifurahi sana, pia alinimiss sana kwa sababu hatukukutana kwa mwezi mzima.
Baada ya kuongea na mke wangu sikutaka kupitia meseji zingine. Japo zilikuwa nyingi ila sikuwa na mpango nazo, kwanza sikutaka kutumia simu kwa muda huo bali nilitaka kujiandaa kwaajili ya safari. Niliweka simu pembeni kisha nilisimama, kabla sijafanya lolote kuna meseji iliingia kwenye simu yangu. Kama ujuavyo meseji ikiingia ni lazima simu iwake, niligeuza macho nilitazama simu yangu nikitaka kuona nani kanitumia meseji hiyo, nilikutana na jina “Docra”, weuwee! Nilipagawa, haraka haraka nilivuta simu yangu kisha nilisoma meseji hiyo, aliniandikia ujumbe ambao ulisomeka hivi “Ni ngumu kumsalimia kila mtu ila ni rahisi kujua hali ya mtu mwenye faida kwako, asubuhi njema”. Nilijikuta nameza mate kisha nilikaa chini, raha ambazo nilizipata moyoni nilitamani kama nijikojolee pale pale ili nipate joto tamu la mkojo wangu. Mara nyingi watu wengi huwa wananitumia meseji za asubuhi njema ila huwa siwajibu, lakini meseji hiyo ya Docra ilitaka kunitoa roho yangu, hata ungekuwa wewe ungekaa kimya pasipo kumjibu mwanamke wa faida kama Docra? bila shaka hiyo haiwezekani. Nilifungua uwanja wa meseji kisha nilianza kuandika meseji nzuri ambayo ilisindikizwa na hisia kali za moyo wangu, niliandika ujumbe mrefu kisha niliufuta, niliandika tena kisha nilifuta, nilikosa maneno mazuri ya kumuambia. Kwa jinsi ambavyo nilihangaika unaweza ukanionea huruma, kwanza laiti kama ungekuwa unaniona nadhani ungeniita majina yote ya kibwege na kilofa, hata mimi mwenyewe sikujua nimekuwaje, sikujielewa wala sikujitambua, kijana wa watu nilipatikana.
Kutokana na kukosa maneno mazuri ya kumpa Docra niliamua kuzama “google”, nilitafuta maneno mazuri ya kumwambia binti mzuri nyakati za asubuhi, google nao walivyo wambea walinipa maneno kama yote, alafu sasa kila neno lilikuwa la motoo! Kwa kifupi mambo ni moto! Kila kitu ni balaa. Hatim aye nilipata maneno mafupi ila matamu, maneno kutoka kwa Manshyne! maneno hayo yaliandikwa hivi “Usihangaike na dunia kutafuta vya amani, dunia imeumbika imetengenezwa kwa ramani, macho yataona mengi ila yatapenda kutamani, Ni Mungu pekee atakupa mtu wa thamani, asubuhi na iwe njema kwako”. Baada ya kumtumia ujumbe huo nilitulia nikitazama jinsi ambavyo atausoma, nilitaka kuona kama atanijibu kitu, mara niliona “delivery riport”, ghafla kwa mbali nilisikia mtu akirukaruka juu ya godoro, kabla sijakaa sawa nilisikia mtu akikimbia, mlango wa chumba changu ulifunguliwa kwa kasi, Docra alinivamia mwilini.
MWISHO WA SEASON 01
Endelea na SEASON 02