KWA MAPENZI HAYA LAZIMA TU NIMSALITI
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA 11
“Ningekuwa nataka ufe si ningekuacha uliwe na mamba” Aliniambia mara baada ya kuona naogopa kunywa maji.
“Sasa kwanini umetia mizizi na majani? Hayatonidhuru kweli?” “We kunywa, hii ni dawa. Babu yangu anaishi Arusha, yeye anajishughulisha na mambo ya tiba asili. Kuna siku ikitokea mama kanihudhi huwa naenda Arusha kwa babu, huko ndiko ambako huwa ananionyesha hizi dawa. Huu mzizi na majani yanaondoa sumu ya mamba, tena kunywa haraka kabla haijasambaa”
Baada ya kuambiwa hivyo sikutaka kuchelewesha, nilivuta kopo kisha nilijimiminia maji yote pamoja na mizizi na majani vyote nilikunywa kisha nilitulia nikisikilizia ladha ya chumvi chumvi, mwili wangu ulisisimka kuanzia kichwani kwenye unywele hadi miguuni kwenye ukucha. Docra alinishangaa kisha alitabasam, alinisimamisha akitaka tuondoke. Nilitembea nikiwa nachechemea, kuna sehemu tulikuta kibao kikiwa kimeandikwa ” ZOO”. Mwenzangu alielewa maana yake ila mimi kilaza hata sikuelewa kitu, hiyo “zoo” sikujua ina maana gani, hata hivyo nilikausha nikijidai najua kumbe hamna kitu. Tuliendelea na safari, kwa bahati nzuri tuliikuta barabara ya gari, mbele ya ile barabara kulikuwa na kibao kingine kikiwa kimeandikwa “KEEP QUIT, WILD ANIMALS”. Kama kawaida sikuelewa kitu, sikujua wana maana gani, mwenzangu alitulia kimya ila mimi nilianza kupiga makele. “Docra cheki kule….simba waleeeee”
“Wewe umeambiwa kaa kimyaa, usipige kelele” alininong’oneza “Kwani wapi wameandika nisipige kelele?’
“We hujaona kwenye kile kibao wameandika “Keep quit, wild animals”
“Kwani pale ndo wamesema nikae kimya? Sasa kwanini nisiongee?”
“Kuna wanyama wakali, kwani hujui maana ya “Zoo”?” “Ndo kinini hicho?” “Zoo ni bustani ya wanyama, ni kama mbuga vile, watu huwa wanatumia “Zoo” kusoma tabia za wanyama wa mwituni. Kuna wanyama ambao wanafugwa, si unaona wale simba wapo bandani?… sasa ukipiga kelele utawashtua, kuna Simba wengine hawajafungwa”
Tulikuwa tunazungumza kwa sauti za chini chini, tulitembea hadi eneo flani hivi kisha tulisimama tukitazama mbele, wote tulitabasam, tulikuwa tunafurahia kile ambacho tulikiona. Kwanza tuliona hema kubwa, pili tuliiona gari ya kitalii, tatu tuliwaona wazungu wawili wote wanaume. Mimi na Docra tulitazamana kisha tulikimbia kuelekea kwa wale watu. Mwenzangu alitangulia akiwa anakimbia kwa spidi kubwa, mimi na mguu wangu nilifuata nyuma nikiwa nachechemea. Tulivyofika pale tulikuta mtu mmoja akisuka nyavu za samaki, mwingine alikuwa anaandaa ndoano, walionekana ni wavuvi, bila shaka walitaka wakavue kwenye ule mto. Watu hao baada ya kutuona sisi waliacha kufanya kazi zao kisha walisimama wakitushangaa, mmoja alitoa bastola kisha alitunyoshea;
“Who are you?” Jamaa alituuliza, moyoni nikasema kumekucha
mana mimi kingereza sikijui, nilitulia kama sio mimi vile, uzuri ni kwamba nilikuwa na msomi ambaye alikuwa anashuka kimombo hadi sio poa.
“We are from Tanzania, our plane crushed last night, we both survived, we are currently looking for help to go to New york” Docra alijibu
“Oh! You are the ones who survived? we got your information, if so then no problem, you will wait for us to finish fishing then we will send you to New York”
“Thank you, we are also hungry, we need food”
Jamaa hakujibu, alimgeukia mwenzie kisha waliongea vitu flani, niliwaona wakikubaliana kitu kisha walicheka. Yule mwenye bastola alielekea kwenye gari yao alitoa boksi flani hivi, si unajua tena wavuvi huwa wanatembea na kila kitu, basi jamaa alituletea vyakula kama vyote; mikate, nyama, samaki, juisi na soda, nilijikuta nafurahi nusura nipae! Wao walielekea mtoni, mimi na Docra tulikaa chini tulianza kupiga menyu, na tulikula kweli kweli, tulihakikisha tumefuta kila kitu. Hadi tunamaliza kula vitumbo vilikuwa “ndi ndi ndi”. Nilimuuliza Docra kuhusu kumalizia safari yetu aliniambia tusubiri wavuvi wamalize kuvua kisha watatuchukua kwenye gari yao watatupeleka New York.
SEHEMU YA 12
Furaha ya Docra ilikuwa kubwa sana mara baada ya kuona tumepata watu wa kutusaidia, muda wote alikuwa ananiambia namna alivyomiss kwenda kutembea mitaa ya kwao, kuna muda alichomoa simu yake akitamani kuongea baba yake lakini kwa bahati mbaya simu ilivunjika kila kitu. Alitoa laini kisha aliniomba simu yangu akitaka kuweka laini zake kwenye simu yangu; nilimuambia kuwa hata yangu ilivunjika, alikosa raha. Akiwa hajui afanye nini mara aliiona simu ya mmoja wa wale wavuvi ikiwa juu ya kibegi flani hivi, bila woga wala hofu aliifuata aliichukua, alitoa laini moja aliweka laini yake. Pale pale alimpigia baba yake;
“Hallo baba….Ni kweli ndege yetu ilianguka ila mimi na mwenzangu mmoja tumenusurika Kwa sasa nipo kwenye hii bustani ya wanyama “Zoo”…unapafahamu?….basi ndo tupo hapa, tumekutana na wavuvi wawili wamesema tusubiri wamalize kuvua samaki kisha watatuchukua watatupeleka New York…Hallo…hallo baba…halloo” Kabla hajamaliza kuongea na baba yake kumbe simu ya watu ilizima chaji, baada ya kuona hivyo haraka haraka alitoa laini yake kisha alirudisha laini ya mwenye simu, aliweka simu pale pale juu ya begi kisha alikuja kukaa pembeni yangu.
*****
Huko Tanzania taarifa za ndege yetu kuanguka ilisambaa kila kona, kulikuwa na msiba mzito kwa sababu abiria wengi tulikuwa watanzania. Siku hiyo mke wangu akiwa anatazama taarifa ya habari alikutana na taarifa ya ndege yetu kudondoka, ubaya ni kwamba katika ile taarifa waliandika kuwa abiria wote walifariki, pale pale mke wangu alizimia. Alibebwa na majirani alipelekwa hosptali, baada ya matibabu alizinduka, kauli yake ya kwanza ilikuwa “Namtaka mume wangu”. Hospitali hapakukalika, alikuwa kama kichaa mwenda wazimu, licha ya kuwekewa drip lakini alizinyofoa alizitupilia mbali, alikimbia hadi nje akikimbizwa na madaktari.
“Nimesema niacheniii…namtaka mume wangu…namtaka baba Monicaaa….sitakiiii….”
“Subiri basi upone kwanza kisha utamtafuta”
“Mimi siumwiiii…Nani kasema naumwa? Mimi NAMTAKA MUME WANGU TU” Aliongea akiwa anakimbia, alizama kwenye taxi kisha alielekea katika ofisi za waandishi wa habari wa jijini Mbeya.
Kitu pekee ambacho alikihitaji ni uhakika wa kujua kama nimekufa au sijafa, ubaya ni kwamba hata wale waandishi wa habari hawakuwa na majibu ya uhakika kwa sababu ndege yetu ambayo ilianguka haikutokea Tanzania bali ilitokea Kenya. Walimpatia taarifa zile zile ambazo zilitapakaa katika mitandao ya kijamii, taatifa hizo zilisema kuwa ndege yetu imeanguka na imeua watu wote, kwa mara nyingine mke wangu alizimia tena, alirudishwa tena hospitali.
*****
llikuwa ni saa saba mchana, masaa matano yalikatika tangu wale wavuvi waelekee kuvua. Mimi na Docra tulichoka kukaa chini, taratibu tulisimama kisha tulianza kutembea huku na huko, alionekana anapenda sana kucheza, kuna muda alinichokoza makusudi ili nimkimbize, ni kweli nilimkimbiza, tulizungushana huku na huko hadi ule mguu wangu ulipona. Michezo haikuisha, hata mimi kuna muda nilimchokoza kisha alinifukuza, mara nilijikwaa nilidondoka, mrembo alidondokea kifuani kwangu, tulibaki tunatazamana tu, alafu hata hakuogopa kunitazama, alinitazama akiwa anacheka kwa furaha! Kuna muda hisia zangu zilisafiri zilienda mbali, nilihisi kama nacheza na mke wangu, tulishtushwa na sauti za yule mvuvi ambaye alitushikia bastola, jamaa alisimama nyuma yetu akiwa anatuchora tu, nilimtazama kwa makini niligundua amechukia kuona namna ambavyo tulikuwa tunacheza.
“You guys are Lovers?” Jamaa alituuliza akiwa amenuna
“No, we are just friends”Docra alijibu
“Now why are you holding on like that? You are not allowed, and if you continue we will not help you”
Jamaa aliongea kwa hasıra akionyesha kuchukizwa na kitendo chetu cha kukumbatiana, alituonya kuwa tukiendelea hawatotupatia msaada wa kupelekwa New York. Japo sijui kingereza ila kimoja kimoja huwa naokota, pia kupitia uso wake nilielewa alichotuambia, kiukweli nilishangaa sana, hata Docra alishindwa kuelewa. Ili tusimkosee jamaa tuliamua kuachiana, alituambia tumfuate kule kwenye gari, kwanza alitupatia chakula cha mchana kisha yeye alielekea mtoni kwenda kuendelea kuvua. Baada ya kuondoka tu mimi na Docra tulitazamana kisha tulicheka, tulikuwa tunamcheka yule jamaa kutokana na wivu wake, mara Docra alianza ukorofi wake, mwanzoni niliogopa kucheza nae ila baadae nilijikuta nipo chini kisha Docra alikuwa juu akinisimulia hadithi za uongo na ukweli. Tukiwa tumekolea kwenye hadithi mara tulisikia sauti nzito;
“How did I tell you? Now I am separating you. You man go sit in the Car and you daughter let’s go to the tent” alikuwa anaongea kwa ishara, alinionyesha nikakae kwenye gari, aliongea akiwa amenishikia bastola.
Kutokana na woga niliondoka haraka nilielekea kwenye gari, Docra hakupenda kitendo hicho, alitaka aongee kitu lakini alitulizwa kwa ishara ya mdomo aliambiwa akae kimya, alishikwa mkono alivutwa kuelekea kwenye hema. Nilijaribu kufungua mlango wa gari ulikuwa wazi, hata hivyo sikutaka kuingia, mara nilimuona mvuvi mwingine akiwa amebeba tenga la samaki, alikuja hadi pale kwenye gari kisha alifungua buti aliweka wale samaki. Jamaa hakuniona, baada ya kuweka samaki aliondoka alielekea kwenye hema. Kiukweli sikujua nini kiliendelea huko ila nilijikuta nakosa amani, nikiwa natafakari nini kinaendelea mara niliona hema likitikisika, ilionekana kama kuna mchezo uliendelea kule kwenye hema, sikujua ni mchezo gani. Nilitega sikio nikisikiliza, kwa mbali nilisikia sauti za kilio; hata hivyo sikujua ni kilio cha mahaba au kilio gani, nilishindwa kuelewa.
SEHEMU YA 13
Machale yalinicheza, nilihisi wanataka kumfanya Docra kitu kibaya, japo niliogopa ila sikutaka kukubali, nikiwa nataka kuwafuata huko huko mara niliwaona wale wavuvi wakitoka ndani ya hema wakiwa wamekunjana roba, haraka haraka nilirudi nyuma ya gari nilijificha kisha nilichungulia nikitaka kuona nini kitatokea. Huwezi amini wale jamaa walianza kupigana pale pale, waligeuzana wakitwangana ngumi, pia kwa mbali nilimuona Docra akitoka nje ya hema akiwa amejiziba kifuani, alikimbia alikuja kwangu,
“Derick tuondoke, tukimbie haraka, wale wavuvi sio watu wa kawaida”
“Kwanini? Na mbona wanapigana?”
“Walitaka kunibaka, kila mmoja alitaka aanze, mwisho walijikuta wanapigana…Tukimbie kabla hawajatukuta”
Bila kupepesa macho tulianza kukimbia, hatukufika mbali mara tulisikia “paah”, pale pale nilidondoka chini, risasi ilitua kwenye mguu wangu wa kushoto, haikuzama ndani ila ilinichana iliniachia jeraha kubwa. Docra alinifuata alinishika kisha alinivuta akitaka tuendelee kukimbia; mimi hata kusimama tu nilishindwa, nilibaki najiburuza kama nyoka, maumivu ambayo niliyapata nashindwa hata kusimulia. Yule mvuvi ambaye alikuwa hatupendi alitufikia pale tulipo, kama kawaida yake alitunyoshea bastola, alinisisitiza nikae kimya kabla hajanitwanga risasi, yeye hakuwa na shida na mimi bali alimuhitaji Docra. Alimkamata kwa nguvu kisha alimvuta kuelekea kwenye hema, Docra aligeuka nyuma alinitazama mimi alinipa ishara kuwa nikamsaidie. Mwanaume licha ya kupigwa risasi lakini nilipata nguvu za miujiza, nilisimama kisha niliuburuza mguu nilimfuata jamaa, pembeni ya hema nilikuta mwili wa mvuvi mwingine ukivuja damu.
“You fool go away, leave me with this girl, if you continue to bother me I will kill you like this fellow fool…And you lady calm down, give me love so that I can help you” Mvuvi aliongea akiniambia nikae mbali kabla hajaniua kama alivyomuua mvuvi mwenzie, pia alimwambia Docra kuwa hawezi kumsaidia bila kufanya mapenzi.
“We don’t need your help, we will help ourselves”.
“Shut your mouth, and I will rape you”
“You can’t, may be if I die”
Sikutaka kujua wanaongea vitu gani, kitu pekee ambacho nilielewa ni kwamba jamaa alitaka kumbaka Docra. Alimvuta hadi ndani ya hema, nami nilifuata nyuma ila kabla sijazama ndani nilipigwa teke la nguvu niliangukia nje, na ukicheki miguu yangu yote ni mibovu, ilikuwa ni shuguli nzito kupambana na yule jangili. Kule ndani Docra alilia akilitaja jina langu, kitendo cha kunitaja kiliniongezea hasira, nilikamata hema nilianza kulivuta, nilivuta hovyo hovyo hadi niling’oa nilitupa pembeni, nilimkuta jamaa kashachana suruali ya Docra, alikuwa akihangaika kuondoa chupi. Nilirusha teke kali lilitua juu ya kichwa cha mvuvi, jamaa alidondokea pembeni, sikumuacha; nilimfuata nilianza kumtwanga mangumi, nilimpa za uso, alafu kumbe jamaa mwenyewe boya tu, ngumi hata hawezi ila anategemea bastola, alikuwa anatafuta upenyo wa kunitwanga risasi, fasta nilibana ule mkono ambao alishika bastola, alinitisha nimuache kabla hajaniua lakini sikumuacha. Docra alikuja kunisaidia, eti badala tumchangie jamaa tumpige; yeye alinivuta akitaka tuondoke. Sasa kitendo cha Docra kunivuta kilimpa jamaa nguvu ya kufyatua risasi, alianza kupiga hovyo hovyo, kuna moja ilinipata begani, mkono wangu wote ulikufa ganzi, nguvu zote ziliniisha, jamaa alinyanyuka kisha alituweka chini ya ulinzi.
“Are you giving me love or should I kill your friend?” alimuuliza Docra
“Kill us all, it will be nice if you start with me” Docra alijibu kwa jeuri kisha alisogea alisimama mbele yangu, alitaka kama ni kupigwa risasi aanze kupigwa yeye afe kisha mimi nifuate.
Tukiwa bado tumesimama mara juu yetu tulisikia muungurumo wa ndege, wote watatu tuliinua macho juu tuliona chopper ndogo ikishuka taratibu; chopper hiyo ilitua pembeni yetu kisha walishuka wanajeshi watatu, Docra aliwakimbilia watu hao akipiga kelele “Dadyyy!” alienda kumkumbatia mmoja wa wale wajeda. Nilijikuta natabasam kuona baba yake Docra kaja, alikuwa ni mtu mzima wa makamo wala sio mzee. Wakiwa wamekumbatiana Baba yake Docra alishangaa kuona nguo za mwanae zikiwa zimechanika, aliuliza kulikoni ndipo Docra alieleza kwa ufupi yote yaliyotokea kisha alimnyoshea kidole mvuvi. Mvuvi baada ya kuona hivyo aliacha kuninyoshea bastola kisha alianza kukimbia alielekea kwenye gari yake, kabla hajaingia kwenye gari alipigwa risasi ya bega, aliongezwa shaba ya mguu alidondoka chini.
Walimkamata kisha walimuhoji maswali mbali mbali lakini mvuvi hakujibu, walimfunga pingu mikononi, walimfunga kamba miguuni kisha walimzamisha kwenye garı yake, mwanajeshi mmoja aliendesha garı hiyo ya mvuvi kisha waliondoka. Muda huo wote mimi bado nilikuwa chini nikivuja damu miguuni na begani. Risasa ya mguu wa kushoto ilinikwaruza lakini risasi ya bega la kushoto ilizama begani. Sikuwa na uwezo wa kusimama wala kunyosha mkono, upande wa kushoto wa mwili wangu ulikuwa haufanyi kazi. Docra aliachana na baba yake kisha alinikimbilia mimi akitaka kuja kunisaidia, baba yake naye alinifuata akiwa na mwanajeshi mwingine. Niliogopa kwa sababu walinifuata wakiwa wameninyoshea bastola.
SEHEMU YA 14
“Na wewe ni nani?” Baba yake Docra aliniuliza
“Baba huyu ndiye ambaye tulinusurika kwenye ajali”
“Na imekuwaje hadi aumie kiasi hicho?”
“Alikuwa ananiokoa mimi nisibakwe na yule mvuvi, kwa bahati m baya alipigwa risasi mbili, ya mguuni na begani”
‘Kijana pole sana”
“Asante” Nilijibu kwa utulivu
Walinisimamisha, nilisimama kwa mguu mmoja, baba yake Docra alinisaidia kutembea hadi kwenye chopper, nilikaa kwenye siti ya nyuma kabisa. Wao nao walizama ndani kisha tulipaa kuelekea Newyork. Tukiwa ndani mimi nilikaa siti ya nyuma pekeyangu, Docra alikaaa na baba yake kwenye siti za katikati, muda wote alikuwa anadeka, mara amlalie begani, mara amlalie kifuani, si unajua tena watoto wa kishua tabu tupu. Kuna muda Docra alinikumbuka, hapo sasa aliachana na baba yake kisha alinitazama alinikuta nimetulia kimya, nilijidai kutazama pembeni, hata hivyo uvumilivu ulinishinda; niligeuza macho nilimtazama, macho yetu yalikutana, wote wawili tulitabasam, huwezi amini mtoto mzuri alimuacha baba yake kisha alikuja kukaa pembeni yangu; alinipa pole kutokana na maumivu ambayo niliyapata, safari iliendelea.
*****
Majira ya saa 10 mchana tulifika Newyork, kwakuwa ilikuwa ni chopper ya jeshi hakukuwa na haja ya kwenda hadi uwanja wa ndege, tulitua katika uwanja wa jeshi ambalo baba yake Docra alikuwa akifanya kazi. Yaani ile tumetua tu; gari ya hospitali ilikuja kutuchukua; mimi, Docra na baba yake tulizama kwenye gari kisha tulielekea katika hospitali ya jeshi. Hospitali za wenzetu ni tofauti na zetu, huku kwetu bila foleni hujahudumiwa lakini kule kwa wenzetu sidhani kama kuna foleni. ile tumefika tu manesi walinidaka, walinikimbiza hadi kwenye vyumba maalumu, sikujua kwa upande wa Docra nini kiliendelea, mimi walinigombania kwa sababu hali yangu haikuwa nzuri hata kidogo. Nililazwa kitandani, huduma ya kwanza ilikuwa ni kutolewa risasi ya begani, walitega mashine zao za X-rays kisha waliitazama risasi ambayo ilitulia ndani ya bega langu, ilibidi wanifanyie operesheni ndogo, nilichomwa sindano ya ganzi, kilichofuata hapo hata sikukifahamu.
Nilikuja kushtuka saa mbili usiku, mwili wangu wote ulikuwa mzito sana, bega langu lilifungwa bandeji, mguuni nilifungwa bandage, usoni nilifungwa bandage, kila sehemu ni bandage tu. Nilidhani nimeachwa pekeyangu chumbani, lakini pembeni yangu nilihisi kuna mtu akinitazama, niligeuza macho nilikutana na tabasam zuri toka kwa Docra.
“Woow! Afadhali umeamka, muda wote nilikuwa nakuombea upone, vipi unajisikiaje?”
“Salama”
“Bila shaka una njaa, subiri nikuletee maji na chakula, nakuletea na juisi” Aliondoka akiwa anakimbia, baada ya muda mchache alirudi akiwa na sahani ya vyakula vya kila aina.
Aliniinua alinikalisha kitandani, alininawisha maji kisha aliniambia nile, sikuvunga wala nini; nilianza kula taratibu. Hiyo haikutosha, kitendo cha mimi kula taratibu aliona kama sishibi, alihisi chakula sikitendei haki, faÅŸta alinawa mikono ya ke kisha alianza kunilisha, nilishindwa kubisha, nilimuacha afanye anachokitaka. Kuna muda nilihisi tumbo limejaa lakini alinilazimisha nile nijigalagaze! Muda huo alikuwa amekaa pembeni yangu, miili yetu ilikuwa imegusana, mara ghafla mlango ulifunguliwa; wote tulitazama mlangoni, tulidhani angeingia daktari, lakini badala ya daktari aliingia baba ya ke Docra. Mzee aliganda mlangoni akitutazama namna tulivyokaa karibu, kingine kilichomgandisha ni kuona mwanae akinilisha chakula, alianza kuona tunampanda kichwani, usoni alichukia.
SEHEMU YA 15
“Docra ebu tuondoke, twende nyumbani”
“Dady na vipi kuhusu mgonjwa?’
“Nimesema tuondoke…kwani safari yenu ilikuwa ya pamoja?”
“Hapana lakini tulikutana kwenye ndege, tumesafiri pamoja, tulipata ajali pamoja, tumepona pamoja na tumekuja hapa pamoja” “Hongereni kwa hilo ila kwa sasa hamtokuwa pamoja”
Mzee alimchukua binti ya ke alimvuta kisha waliondoka, niliumia sana kutenganishwa na mtu mwenye roho nzuri kama Docra; hata hivyo sikuwa na jinsi kwa sababu mwenye mtoto ndiye kaamua. Nilijilaza kitandani niliwaza safari yangu nzima ilivyokuwa tangu natoka Mbeya nafika dar, natoka dar nafika Kenya, kisha natoka Kenya kuelekea marekani hatimaye tulipata ajali, nilipiga ishara ya msalaba mara baada ya ku ku m buka kuwa watu wote walifariki kasoro mimi na Docra, bila shaka Mungu alikuwa ana mipango na mimi, kwa sauti niliongea nikisema “ASANTE MUNGU WANGU”.
Pia nilimkumbuka m ke wangu na mwanangu, kuna hisia ziliniambia kuwa lazıma taarifa za ndege yetu kuanguka zimemfikia mke wangu, sasa kama amejua atakuwa kwenye hali gani? nilipagawa! Mara nesi aliingia, kabla hajaniuliza chochote nilimuomba simu yake ili niwasiliane na mke wangu, bila kupepesa macho aliniazima simu kisha nilimpigia mke wangu. ****
Huko Mbeya mke wangu bado alikuwa kalazwa hospitali, pembeni alizungukwa na madaktari ambao walikuwa karibu kucheki afya yake, licha ya kuzimia lakini mkononi alishika simu yake, tena aliikamata haswaa! Simu nyingi zilipigwa lakini hazikupokelewa kwa sababu muhusika bado alikuwa kazimia. Hatimaye simu yangu iliita kwenye simu yake, hapo sasa hata madaktari walishangaa, mke wangu alishtuka toka usingizini, macho yake yalitua kwenye simu yake, alikutana na jina “MY HUSBAND”, nusura azimie tena; haraka haraka alipokea simu.
“Hallo mume wangu, mzima wewe?, niambie kama umepona..Naomba niambie haraka” Aliongea kwa shauku ya kutaka kujua kama nimekufa au nimepona.
“Usijali mke wangu, Tumshukuru Mungu ameniokoa kwenye ajali, kwa sasa nipo hospitali nauguza majeraha ila naendelea vizuri” Sikutaka kumuambia habari za kupigwa risasi kwa sababu ningemshtua zaidi.
“Siamini mimi…Mbona niliambiwa watu wote wamekufa?”
“Mimi sijafa, Mungu hakutaka nife ili nikuache, si unajua kama nakupenda sana?’
“Ndiyo najua, hata mimi nakupenda sana, nilichanganyikiwa mara baada ya kuambiwa ndege yenu imedondoka kisha watu wote wamekufa, nilizimia, hata sasa nipo hospitali”
“Pole sana mke wangu kipenzi, huna haja ya kuumia tena. Vipi mwanangu Monica ni mzima?”
“Ndiyo ni mzima ila muda wote analia tu”
“Ebu muambie kuwa mimi baba yake ni mzima, kama yupo karibu mpe simu”
Mke wangu alimpa simu mwanangu, niliongea nae, tulicheka, walinipigia kuitia wasap video ili wanione, nao niliwaona, furaha ilirudi, muda huo huo mke wangu alikuwa mzima wa afya, aliruhusiwa kurudi nyumbani.
*****
Kulikucha asubuhi na mapema, bado nililazwa katika hospitali ya jeshi. Mtu wa kwanza kunitembelea asubuhi hiyo alikuwa ni baba yake Docra, aliniuliza maswali mengi kuhusu safari yangu, nilimsimulia kila kitu, nilimwambia kuhusu Joshua ambaye ndiye mwenyeji wangu, alinipa simu niwasiliane na Joshua. Kwa muonekano tu baba yake Docra hakutamani niendelee kubaki hospitalini kwa sababu aliogopa mwanae hasije akanitembelea. Nami kwakuwa nilioa wala sikuwa na shaka, sikutaka kumpa plesha mzee wa watu kwa sababu licha ya uzuri na tabia njema za Docra lakini mimi nilikula kiapo cha damu na mke wangu. Nilipokea simu niliweka laini yangu kisha nilimpigia Joshua; “Hallo Derick, ni wewe?” Joshua aliniuliza kwa wasiwasi
“Ndiyo ni mimi kaka”
“Nimekutafuta sana; kupitia TV niliona ndege yenu imeanguka, walisema kuwa watu wawili wamepona, nilienda hadi ofisi za ndege yenu niliulizia taarifa zako lakini walisema hawajui kama umekufa au umepona, asiee kumbe umepona ndugu yangu, tumshukuru Mungu…kwahiyo upo wapi?”
“Nipo hospitali ya jeshi ya hapa New York”
Kwakuwa Joshua ni mwenyeji sikupata tabu ya kumuelekeza sana, alitambua nipo kwenye hospitali ipi, baada ya dakika 30 alinifuata hospitali, licha ya kwamba nilikuwa bado sijapona lakini baba yake Docra alituambia tuondoke tukatibiwe katika hospitali zilizopo katika mitaa ya kina Joshua. Joshua yeye alikuwa akiishi mtaa flani hivi uitwao “The Bronx”. Mzee huyo ili kuhakikisha tunaondoka haraka alitupatia pesa kwaajili ya gharama za matibabu kisha alitupatia usafiri wa gari la jeshi ambalo lilitupeleka hadi mitaa flani ya uswazi iliyopo The Bronx. Tulifikishwa hospitali, matibabu yaliendelea.
Nilikaa hospitali kwa wiki 1 nikipata matibabu, mwili bado uliuma pia hata kutembea nilitembelea magongo, mkono wangu wa kushoto ulijikunja; sio kwamba nilishindwa kuunyosha, hapana, bali kila nikijaribu nilipata maumivu makali. Kuna muda nilikuwa namkumbuka Docra ila ndo hivyo sikujua anaishi wapi, sikujua kama nitakutana nae tena, mbaya zaidi hata namba zetu hatukupeana. Moyoni nilianza kukata tamaa ya kumuona tena, japo nilivumilia nisimuwaze ila nilimuwaza sana kiasi cha kukosa raha.
“Derick vipi? Mbona kama huna rah a?” Joshua ambaye ndiye mwenyeji na muuguzi wangu aliniuliza
INAENDELEA