KAMA INAUMA CHOMOA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
ILIPOISHIA: Naam zilipita siku tatu, huku Damiana akiishi kwa kujiicha asionekanane mbele ya polisi, huku akishindwa kujieleza kwa Shwifat, juu ya kile kilicho tokea kati yake na Ratifah, maana ingemlazimu, kueleza kuwa alikuwa amesha chumbia mwanamke mwingine, hakika akutaka kumkosa mwanamke huyu, ambae ukiachilia uzuri na utajiri wake, Damian alikuwa anampenda Shwifat toka moyoni, ata siku ya jumamosi ilipofika walienda nyumbani kwa kina Shwifat, yani kule kwa wazazi wake, ambao kiukweli walimpokea vizuri na kuongea nao kama wazazi wengine wanavyoongea na wakwe zao, huku wakimsisitiza kuishi vizuri na binti yao. . …endelea…
Wakati huo upande Ratifah, mambo ayakuwa mazuri sana, maana licha yakuanza kupona vidonda vyake, vilivyo mwachia makovu makubwa na yakutika katika uso wake, lakini tofauti na alivyotegemea kwamba, saa yupo huru na Johakim at, kuwa anakuja mala kwa mala pale nyumbani, kinyume chake, toka juzi, Johakim alienda pale mala mbili tu, na akukaa sana, yani ndani ya lisaa limoja tu, angeondo zake, na asinge rudi tena, hii kitu ilimshangaza na Ratifah, ambae sasa alikuwa anakula kwa Mdee, tena siku yaleo, jumamosi mke wa Mdee nikama alimfanyia makusudi, maana licha kufahamu kuwa mwenzie akuwa na chochoe cha kupika ndani kwake, yeye akaondoka bila ata kuaga na kuotokomea zake, mpaka usiku wa saa tatu, na kurudi akiwa ameshiba tayari.
Hakika kama Ratifa alilala siku ile, basi alitumia lisaa limoja tu, huku masaamengin yote akitumia kusikiliza miungurumo ya tumbo lake, lililokuwa lina mchonyota kwa njaa, “hivi huyu anawezaje kutoka wakati anajuwa mimi naumwa na sina kitu ndani, alafu anarudi anasema tayari amesha kula” alilalamika kimoyo moyo Ratifah, aliejilaza kitandani, huku macho yake ameyaelekeza juu ya paa la nyumba hii aliyoitazama kwa kwa uwazi kabisa, “kwanini sasa Johakim nae ajaniletea chakula jamani” aliwaza Ratifa, ambae sasa alikuwa anahesabu migongo ya bati, ambayo alikuwa anaiona wazi wazi, kutokana na kuto kupigwa siling board, “yani njaa inanuma hiyo, angekuwepo Damian vyakula visinge pungua humu ndani” aliwaza Ratifah, ambae masaa manne yaliyopita alikuwa ametoka kuongea na wazazi wake ambao walimweleza kuwa wamepiga simu ya Damian, lakini aipokelewi, ila lengo lao ni kwamba wanaitaji fedha za matibabu ya mtoto Fatuma.
Hakika ilikuwa ni mkanganyiko wa ajabu kichwani mwa Ratifah, “yani Johakim nae amebadirika sana , siku hizi anakuja mala chache, na akija ata akai sana” alijilalamisha Ratifa, ambae alisha badiri mikao yote na kukosa mkao ambao ungepunguza maumivu ya njaa, tumboni mwake, huku akizidi kulalamikia mabadiriko ya mpenzi wake Johakim, ambae siku za hivi karibu ata akimpigia simu alikuwa apokei, na wakati mingine kuikata kabisa.
Johakim nae kiukweli, sijuwi ni kwanini, ila alikuwa amemchoka ghafla mschana wetu toka mitimbi, ilifikia hatua ni kwamba akutaka ata kuiona namba yake ikimpigia, aliishia kutoa sauti na kuieka pembeni, na kuiacha ikiendelea kuita mpaka ilipokatik yenyewe.
Wakati karata dume ikikaa upande wa Ratifah, huku kijana wetu Damian, alikuwa akihisi maisha ambayo akuwai kuyaota ata siku moja, tena siyo kuishi yeye, japo ata kuwa karibu na watu wenye maisha kama hayo, huku mida ya jioni akienda kutembelea wakina Kapate, ambao sasa alikuwa amesha wasimulia mkasa mzima wakile kilicho mtokea, na kwanini sasa anaishi maisha aya ya kifahari. ******
Yaaap! siku moja siku ambayo ilizuwa kizaa zaa, ilikuwa ni siku ya juma tano, mida ya saa sita mchana, mida ambayo Shwifat alikuwa ametulia ma mpenzi wake ambae sasa alikuwa anamwita mume, wakiwa wamekaa upande wa nyuma ya nyumba yao ile kubwa ya kifahari, ambako kulikuwa na bustani nzuri ya mauwa na bwawa lenye ukubwa wastani, mahalumu kwa kuogelea, wamejilaza kwenye vitanda mahalumu vya kupumzikia.
Siku ambayo Damian, alikuwa ameamua kumweleza Shwifat juu ya masaibu yaliyo mkuta juu ya mwanamke alie enda kumchukuwa kijijini, baada ya kukata tamaa ya kumpata yeye, Damian ambae aliofia kuwa endapo Shwifat angejuwa habari ile kupitia mtu mwingine na kumkasirikia, alieleza kila kitu, mpaka jinsi Johakim alivyo mchukuwa mke wake, na kwenda kuonga polisi, waliomsumbua na kumpiga kama mwizi, huku wakiwaacha wakina Johakim na ratifah wanafaidiana viungo vyao vya uzazi, na wakati mwingine wakipitishana milango ya dhalura, ambyo sehemu nyingi uwekwa upande wa nyuma wa nyumba au gari.
Hakika ni hadithi ambayo ilimchanganya na kumtia uchungu mkubwa mwanadada Shwifat, “Jamani kumbe huyu kijana ni mshenzi hivi, ndio maana mahesabu yake ayaeleweki, kumbe alitumia fedha zangu kumuumiza mume wangu, mimi naenda kumfukuza kazi leo leo” alisema Shwifat, kwa sauti iliyojaa machungu na hasira, “aina aja shwifat, mimi nimesha msamehe, maana najuwa kuna funzo watalipata” alisema Damian kwa sauti ya kusihi, na kuombeleza, “lakini kwanini afanye hivi, uoni kama alikunyanyasa sana, tena kwa fedha za mke wako, hapana aiwezekani siwezi kukubariana na ilo, na watarudisha kila kitu chako, na hao polisi sema nimekosa ushaidi tu, vinginevyo wangetambua gharama ya mambo waliyo kufanyia” alisema Shwifat, kwa saut ya kuto kumsikiliza mtu yoyote. juu maamuzi yake ya kumtimia Johakim kazi, jambo ambalo Damian alipinga na mke wake.
Waliongea na kubishana kwa muda mrefu sana, “lakini kosa litakuwa ni lakwangu, mimi ndie nilie mpiga Ratifah, ukifanya hivyo wataenda kunisemea polisi na kuja kunikamata” alisema Damian, akitetea uamuzi wake wakuachana na swala lile, la wakina Johakim, “hivi baba Alvin, unaongea serious kabisaaaa, yani mume wangu aishi kwa kujificha ficha kwaajili ya mfanyakazi wangu, hiyo aiwezekani taka usitake lazima swala ili tulipatie ufumbuzi, tena leo leo, ngoja nimpigie mama Mbaga, nione ananisaidiaje, juu ya ili” alisema Shwifat, na bila kuchelewa akachukuwa simu yake na kupiga kwa afisa huyu, wa ngazi za juu kabisa wa jeshi la polisi, anae simamia kitengo cha dawati la jinsia, sijuwi waliongea nini, ila kuna jambo lilipangwa.*******
Ilikuwa hivi, mida ya saa moja moja, kagiza kausoni kakiwa kana zidi kutanda na kufunika anga, Ratifah akiwa pale nyumbani, yani walipo panga, amekaa kwenye ngazi za mlango, kama wenzie waliokaa mbele ya milango ya vyumba vyao, wakiongea ili na lile tofauti na Ratifah, alie kuwa amekaa peke yake, huku njaa na mwazo zikimchonyota, maana alikuwa amekosa chakula toka asubuhi, macho yake yalikuwa kwenye barabara ya kutokea mjini, ambako mke wa mdee alielekea toka saa nne asubuhi, “sijuwi kwanini Johakim ananifanyia hivi, au sababu nampenda sana, yani ata simu yangu apokei” aliwaza Ratifah, ambae alishapiga sana simu ya Johakim pasipo kupokelewa, hakika limuweka katika njia panda na mgagasiko Ratifa wa mpitimbi, ambae leo ni siku ya nne fululizo alikuwa anapokea simu toka kwa mama na baba yake, zikimtaka kutuma fedha kwaajili ya matibabu ya binti yake Fatuma.
Dakika chache baadae mke wa Mdee akaingia pale nyumbani akitokea mjini, akawasalimia wenzake na kuingia ndani, kisha akafunga mlango, ungejuwa kuwa anaitaji kubadiri nguo, hivyo Ratifah, akaona kuwa itakuwa vyema kisuburi kwanza rafiki yake huyu, amalize kubadiri nguo, ndipo na yeye aende akabahatishe chochote, cha kuweka mdomoni, japo mala nyingi akirudi kama hivi ujuwe akuna chochote kitakacho pikwa, maana anakuwa amesha kula alikotoka.
Naam wakati Ratifa akiwa anamsubiri mke wa mdee afungue mlango, mala kwambali akamwona kijana mmoja alie fanana kwa umbo na na mtembeo na Damian, akija upande wa nyumba yao, . …
SEHEMU YA AROBAINI NA SABA
alishindwa kumtambua kwa sura, kwakuwa mtu yule alikuwa gizani “huyu siyo Damian huyu, anafwata nini hapa, aogopi?” alijiuliza Ratifah, huku anakaza macho kuangalia ile taswila gizani.
Lakini kadiri alivyo sogelea nyumba yao, na kuanza kuangaziwa kwa mwanga ndivyo alivyozidi kuchanganyikiwa na badaa ya kupata picha kamili ya mtu anaekuja, yeye ndio kwanza akazidi kupoteza uwezo wakutambua, maana ukweli alimwona Damian kuwa ndie mtu anaekuja mbele yake, lakini tofauti ni kwamba, huyu alikuwa amevaa vizuri na kupendeza kuliko Damian, anae mfahamu, huyu licha ya kuvaa vizuri, kuanzia tidhert jinsi na raba zake nzuri, vyote vikionekana kuwa ni vipta kabisa, pia ata sura na ngozi ya mwili ya mwili wake, vilionekana kuwa ng’aa na kuwa na afya nzuri ya matunzo, “ni yeye, imekuwaje amekuwa hivi?” alijiuliza Ratifah, huku anamtazama Damian ambae alikuwa amesha ingia kwenye viunga vya ile nyumba, huku wapangaji wenzake wakimsaidia kumshangaa Damian.
Naam Damian akiwa mwenye kujiamini, akawasalimia wapangaji wenzake wa zamani, ambao walimshangaa bila kificho, “habari za siku jamani” alisalimia Damian kwa sauti yake ya siku zote, yani sauti iliyojaa uchangamfu, “safi tu shemeji habari ya huko utokako” alijibu mmoja wao, huku akionekana kujichangamsha, “salama kabisa zaidi nashukuru nime wakuta mpo vizuri” aliitikia Damian, huku anatembea taratibu kuufwata mlango wa chumba chake, “sisi tupo karibu sana shemeji, naona mambo yako siyo mabaya” alisema mwigine, huku wote wakionyesha sura za tabasamu, na mshangao kwambali, “asanteni sana” alisema Damian, huku anasimama mbele ya mlango, yani pale alipokaa Ratifah.
Hbari za leo Ratifah, pole sana kwa maumivu” alisalimia Damian, huku anamtazama Ratifah, aliekuwa amekaa kwenya ngazi, huku mkono amejishika tama yani kaweka mkono shavuni na kutazama pembeni, ata aliposalimiwa akujibu salamu, baada yake alibinua midomo kwa dharau, wakati huo mke wa Mdee alifungua mlango, na kutoka nje kwakuonekana anafunga kanga, niwazi alikuja kujihakikishia, kama anae salimiwa ni kweli Damian kama alivyofananisha sauti au ni mtu mwingine.
Mke wa Mdee alipomwona Damian akiwa kwenye malango wa chumba ambacho kwa sasa walikiita chumba cha Ratifah, alitoa macho kwa mshangao, kumshangaa kijana huyu, ambae alionekana kupendeza na kuvutia machoni pake, “macho yangu au naota” alijisemea mke Mdee, kwa sauti ya chini, huku anashindwa ata kujifanya ajashangaa, maana alitoa macho kwamshangao mkubwa, huku anamtazama kijana huyu mtanashati, ambae sasa aliweza kumwona akiingia ndani, “hivi huyu mshenzi ana kizizi au, si tuliambiwa ameenda songea huyu?” alijiuliza mke wa Mdee, huku anaingia ndani na kutoa simu yake, kisha akampigia mume wake.
Bahati nzuri au mbaya, kwa mke wa Mdee mume wake akapokea simu mala moja, “niambie kuna inshu, si tumetoka kuongea sasa hivi hapa ukiniambia kuwa unakaribia nyumbani…” aliuliza mdee ambae kwa sauti za nyuma yake, ilionyesha yupo kwenye dala dala, “tulia wewe nikupe umbea, mwenzio Damian yupo hapa, amependeza huyo, sijuwi amepata dili gani huko aliko” alisema mke wa Mdee kwa sauti ya chini, “weeee unasema Damian yupo hapo nyumbani, basi wacha nimpigie Johakim aje na polisi” alisema Mdee, na kabla ajakata simu mke wai akawai, “mwambie aje na polisi, wambomoe sura yake anayo jidai nayo” alisisitiza mke wa Mdee na hapo simu ikakatwa na mke wa Mdee akatoka nje na kutazama kule alikokuwepo Ratifah, ambae alikuwa amekaa kwenye ngazi pake yake, ana bofya bofya simu yake, kuandika ujumbe kwenda kwa Johakim, huku kichwani mwake, akihisi maumivu makali moyoni, “yani amenitoa nyumbani kwa wazazi wangu, kuja kunifanyia hivi, alafu yeye ana zidi kupendeza tu,” aliwaza Ratifa huku anamaliza kuandika ujumbe na kuutuma kwenda kwa mpenzi wake, ambae anaamini kuwa siku yoyote anatangaza ndoa.
“yule mshenzi yupo hapa waambie polisi wako waje wambebe” ndivyo ulivyosomeka ujumbe huo, ambao jibu lake lilirudi haraka sana, “Mdee amesha niambia, leo ndio mwisho wake huyo mshenzi, ngoja niwasiliane na polisi” ndivyo ilivyosomeka hiyo sms, ambayo baada ya dakika kama tatu hivi, ikaja sms nyingine, bado yupo ndani?” aliuliza Johakim, na yeye Ratifah akajibu haraka, “bado yupo anapekuwa pekuwa ndani” alijibu Ratifah, na kutuma sms kwenda kwa Johakim, sekunde chache baadae sms ikaingia kwenye simu ya Ratifah, aliyo nunuliwa na Damian mwaka mmoja uliopita, “mfungie kwa nje, weka komeo kabisa, sisi tupo njiani na polisi, tunakuja”
Baada ya kupokea maagizo hayo, toka kwa mwanaume wa ndoto yake mwanaume mwenye gari, Ratifa akainuka na kuingia ndani, akamtazama Damian alie kuwa anapekuwa kwenye nguo zake zilizowekwa kwenye fuko kubwa, yani kiroba, na sasa alikuwa anaibuka na kaptula fupi ya jinsi, kisha akaingiza mkono mfukononi, na kuibuka na kitita cha fedha, hakika ilimshtua sana, Ratifah, ambae siku zote alikuwa anaishi kwa tabu, maisha ya kukosa fedha, kumbe kwenye kile koroba, kulikuwa na fedha nyingi kiasi hiki, “mama yangu, kwanini sikupekuwa nguo zake” alijilahumu Ratifa, ambae baadae akaata wazo la kwamba, endapo wakija polisi, ata singizia kuwa Damian ameiba fedha zake, nao wata mpekuwa na kumpatia zile fedha.
Hivyo Ratifah, akatoka nje haraka na kuubana mlango, kisha akautia komeo, hapo Damian akaachia tabasamu la ushindi, “we Ratifah, unafanya nini ebu nifungulie niondoke zangu bwana” alisema Damian kwa sauti ya kulalamika, ungesema huko ndani alikuwa ameshiwka na uoga mkubwa sana, “wewe siunajifanya kidume, aya sasa subiri ukutane na vidume wenzio” ilikuwa ni sauti ya Ratifah, iliyojaa kejeri, ikiwafwatiwa na sauti hiyo hiyo ya ratifah, akiongea na simu, “tayari nimesha mfungia fanyani haraka mje” aliongea Ratifa kwa sauti ya juu na yakupayuka, japo akusikika mtu wa upande wapili, lakini ungeweza kujuwa anazungumzia nini, “tena waambie polisi kuwa ameniibia ela zangu, bado anazo mfukoni” alisema Ratifah bila aibu, wakati huo huo watu walianza kusogea eneo la tukio, pamoja na mke wa Mdee, ambae alisogea pale alipokuwepo Ratifah, “umefanya vizuri Ratifah, huyu mshenzi aje akione cha moto, anajifanya amependeza kumbe mshenzi tu” alisema mke wa Mdee, wakati huo sauti ya Damian iliendelea kusikika toka ndani, “jamani naomba mnisaidie ameita polisi waje kunichukuwa, mimi nilifwata ela zangu nilikuwa nimezificha kwenye kaptula yangu” sauti ya Damian ilitia huruma. , . …
SEHEMU YA AROBAINI NA NANE
Wakati huo huo, ikasikika pikipiki ikiingia kwa fujo mahali pale, wote wakageuka kutazama huyu alikuwa ni Mdee, “bwana hee, hao polisi wenyewe awaangalii pande zote, wao wanaangalia aliewai kushitaki, mimi na mfungulia” alisema yule kijana huku anausogelea mlango, lakini kabla ajaufikia mlango, tayari mdee alikuwa amechomoka mbio toka kwenye pikipiki na kumkumba yule jamaa, alie taka kugusa komeo la mlango kiasi cha kuyumba na kuanguka chini, “inakuhusu nini mpaka ufungue mlango?” alisema Mdee akionekana mwenye hasira kali, ungesema alie kuwepo ndani, aliwai kumwibia mke wake, kwa jinsi alivyokuwa na hasira nae.
Hapo yule jamaa alie sukumwa na Mdee akusubiri ata dakika moja, aliinuka haraka na kumfwata Mdee kwa jazba kali, huku Mdee nae akijuwa kuwa lazima jamaa atarusha ngumi, hivyo akajiandaa kwa lolote, lakini akujuwa kuwa jambo lile liliwachukiza wengi, maana ile anajweka sawa kumkabiri yule mpangaji mwenzao, “kwani wewe inakuhusu, wewe namkeo ndio mliosababisha huyu mwanamke mpumbavu, akasaliti mume wake, na kuzuzuka na yule fala muuza duka mwenzio, huku mkimdanganya kuwa lile duka ni la kwake, kumbe na yeye nifanyakazi kama wewe” alieongea hivyo akuwa yule alieangusha chini, alikuwa ni mtu mwingine.
Ukweli Ratifah alishtushwa sana na ile kauri, kwamba Johakim akuwa na duka, ila nimfanyakazi kama Mdee, nasiyo mmiliki waduka, “sasa kama duka siyo la kwake, inausu nini, kwani mimi nilimlazimisha, siwao wenyewe wamependana bwana” alijibu Mdee, ambae kabla ajamaliza kujibu, alishtuka akikwatuliwa mtama wanguvu, na kurushwa juu kama mwanasarakasi, kisha kujibwaga chini kama papai pichi lililoangushwa na popo, akifikia mkono ambao ulisikika ukitoa sauti kama ya kijiti kikavu kilicho katika, “mamaaaa mkono wangu” alipiga kelele Mdee, lakini aikusaidia, maana tayari yule fundi ujenzi, alikuwa amesha inua mguu wake na kuushusha kwanguvu kwenye mguu wa Mdee na kukita kama vile alikuwa anakanyaga nyoka kichwani.
Ukweli Ratifah, licha ya kile kilicho kuwa kinaendelea, huku kichwani mwake zikimjia kauri mbili, ni ile ya huyu kijana, ya kwamba duka siyo la Johakim, na ile ya mdee kuwa walipendana wenyewe, na hapo Ratifa alianza kuhisi kuna jambo limesha mtokea, au kuna kamsemo kawahenga kaenda kutimia kwake, na kasiyo hivyo, basi kuna kamsemo kampya kanaweza kuanzishwa kwaajili yake.
Jamani mume wangu amewakosea nini, alie mfungia ndani si huyo mke wake…” alisema mke wa Mdee, na kabla ajamaliza kuongea tayari nguminzito ya mdomo ilisha tuwa, na kumfanya amaze kipande cha jino lake, “mshenzi wewe, sindio ulikuwa unashabikia hapa” alisema yule alie mtandika ngumi mke wa Mdee, wakati huo Ratifah alimwona mmotu mmoja kwa haraka sana akifungua mlango wachumba kile na Damian akatoka nje, “Ratifah, kikubwa nini nilicho kukosea” aliuliza Damian huku anamtazama Ratifah, ambae alikuwa ameinamisha kichwa chini na watu wanamzomea kwa fujo, rafiki zake Mdee na mke wake, wakiwa wanaugulia maumivu, “naona uwezi kunijibu, ila kwakukusaidia, sasa hivi nakuacha free, uishi na huyo mwanaume ulie mchagua” alisema Damian, wakati huo huo, magari mawili yakaingia pale nyumbani.
Naaam watu walipo yatambua magari yale, ambayo moja lilikuwa ni la[plisi na polisi watatu nyuma, huku jingine ni Toyota vitz mali ya DS beauty Point, lililoendeshwa na kijana mmoja mfuoi mwenye kitambi kikubwa na miguu membamba kama penseli, alie shika haraka toka kwenye gari sambamba na polisi watatu walioruka toka nyuma yagari huku polisi mwingine mwenye nyota moja, akishuka toka kwenye seat ya mbele ya abiria ya gari ilo la polisi, kuona hivyo Ratifah akapingana na maneno yaliyopita, “kama nimfanyakazi tu pale dukani, anapata wapi uwezo wa kuhonga polisi na kununua gari, “usijari shemeji leo atakiona cha mtema kuni” alisema polisi mwenye nyota moja, ambae alionekana kukasilishwa na matendo ya Damian.
Kuona hiyo raia wote wakatawanyika, na kuwaacha Damian Ratifah, Mdee aliekuwa amelala chini anagala gala kwa maumivu, pamoja na mke wake alie kuwa analia kwa uchungu wa kutolewa jino, “yule pale mshenzi, amejileta mwenyewe” alisema Johakim akimwonyeshea Damian, huku askari polisi wale wanne wakimfwata Damian, ambae aikuwa amesimama anawatazama kama vile akuwa na uoga wowote, sijuwi sababu awakuwa na bunduki, lakini alikuwa anaijuwa kazi ya Warioba, ambae ni mmoja kati ya askari wale, “amewatuma watu wampige Mdee na mke wake, na pia aliingia ndani na kuiba ela” alisema Ratifah, huku akiangua kilio cha uongo.
Johakim akiwa anafwata kundi la askari wale, waliokuwa wanamsogelea Damian, alie kuwa amesimama anawatazama, kama vile akukuwa na chochote kibaya wanachotaka kumfanyia, “kijana leo utajuwa kwanini gendere ana pumbu za kijani” alisema yule mwenye nyota moja, huku anavuta mkono kwanguvu, na kuuvulumisha kwenda kwa Damian, usawa wa usoni, Damian nae akakwepa na kumfanya yule polisi ayumbea nusu ya kuanguka chini, huku wananchi wakiwa wamesimama mita kadhaa wakitazama tukio lile, la kiburudani. . , . …
SEHEMU YA AROBAINI NA TISA
Sijuwi ni kwanini, polisi upatwa na hasira kali pale mtu anapokwepa kipigo chake, “we mshenzi unajifanya kukwepa” alisema Wariona huku anachomoka kumfwata Damian, kwaajili ya kumshushia kipigo kama kawaida yake, lakini ghafla akashtuka na kutazama kwenye barabara ya kutokea mjini, ni baada ya kuona wanamulikwa na mwanga mkali wa taa za gari, yeye pamoja nawenzake wakatazama kule mwanga ulikotokea.
Wote kwa pamoja wakayaona magari manne yaliyo ongozana, yakiingia lake nyumbani kwa kina Mdee na kusimama kwa fujo, kasoro moja la mwisho, ambalo lilikuwa linatembea taratibu, na kuja kusimama nyuma ya magri yale matatu ya mbele, hakika iliwashtua sana, siyo kuona magari yana ingia pale ila aina ya mari yaliyo ingia, mahali pale.
Ukiachilia hari la mwisho la kiraia gari la kifahari, kulikuwa na magari matatu ya polisi, kati yao mawili Toyota Land cruzer yaliyobeba askari wanne kila gari, tena wenye bunduki, kati yao wawili ni wakike, pia gari aina ya Nissan Safari linalo tumiwa na mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia, “Johakim mbona sielewi, nini kinaendelea” aliuliza yule askari mwenye nyota moja, huku wakina Warioba wakiangalia namna ya kukimbia, “ata mimi sijuwi, labda nikuulize wewe awa si polisi wenzako” alisema Johakim, ambae sasa mapigo ya moyo, yalikuwa yanaanza kwenda mbio, akijaribu kutafakari kama lile gari aliloliona nyuma kabisa, ni la boss wake au yamefanana tu.
Wajati huo tayari askari wale wenye bunduki wakiwa wamesha wazunguka wakina Warioba, na sasa akashuka mama Mbaga toka kwenye gari lake akiongozana na askari wengine wawili, wenye bunduki mikononi mwao, na kuanza kutembea kuwasogelea, huku wakina Warioba wakimtazama afande wao, ambae anashugulika na kesi za manyanyaso kwenye ndoa, na familia.
Naam akiwa anatetemka kwa kujuwa kitu kinachoenda kumtokea mahakami, yule polisi mwenye nyota moja, akamtazama Damian, kwa jicho kali sana, bahati mbaya alimwona Damian akiwa ameimama bila wasi wasi, huku anaachia tabasamu la ushindi, “umejifanya mjanja leo, lakini siku nyingine utajuta” alisema yule polisi, kwa sauti iliyojaa chuki na hasira, “zamu yako sasa” alisema Damian ambae sijuwi huu ujasiri aliupataje, pengine baada ya kumwona mama Mbaga, aliekuwa ameshakaribia kabisa pale walipokuwepo wakina Damian, “afisa wewe na wenzako mpo chini ya ulinzi, kwa kutumia vibaya madaraka na imani mliyopewa na jeshi la polisi, kunyanyasa na kuhatarisha maisha ya raia” alisema mama Mbaga, sauti ya ya chini huku anamtazama yule afisa mwenye nyota moja, “lakini afande tume kuja kumkamata huyu mwalifu, alifanya tuio baya sana, la kumshambilia na kumjeluhi, mwanamke huyo hapo, kisha kukimbia baada ya kujuwa anatafutwa na jeshi la polisi” alisema yule askari mwenye nyota moja, kwa sauti ya kulalamika, “wewe ungevumilia kuishi na mwanamke ambae anatembea na mwanaume mwingine, tena na nyie mkisaidia kumlazimisha amuudumie huyu mwanamke, ambae anatmbea namtu ambae anawalipa kwa kazi hiyo” alisema mama Mbaga, kwa sauti ya kumsimanga yule askari, “afande sisi atukujuwa kama anafanya hivyo, sisi tume kuja kwa kshi ya kushambulia tu, na siyo nyingine” alisema mama yule afisa, kwa sauti ya kusihi na kuomboleza, “kesi ya kumshambulia hawara wa mfadhiri wako, ambae amekupigia simu kukuamboa kuwa Damia amaesha fungiwa ndani mje kumkamata” alisema mama Mbaga, kisha aka akawatazama wale skari aliokuja nao funga pingu awa askari wote, na muwapakize kwenye gari, dereva apeleke ilo gari kituo kikuu, kama ushaidi, na awa wapelekwe wizarani, alisema mama Mbaga, ambae akuwajumuhisha Johakim, Mdee Ratifa na mke wa Mdee, ambao walikuwa wanasikilizia msala wao.
Haraka sana, polisi wakaanza kuwafunga pingu polisi wenzao, “hii siyo haki afande unatetea mwarif….” alisema Warioba kwa sauti iliyojaa jeuri, huku anakataa kuvishwa pingu, hapo alishtuka akipigwa kitako cha bunduki kilichotuwa mdomoni mwake na kwenda kujipamiza ukutani kisha akaanguka chini, “amka we mpuuzi” alisema askari alie mtwanga Warioba, huku anamzibua teke la mbavu, hapo Waliona akainuka na kumvamia yule askari, bahati nzuri askari huyu alikuwa mwepesi sana, alimkwepa na kumzibua teke la tumbo, ile Warioba anashika tumbo tayari askari wawili walisha ongezeka kumthibiti, hivyo alishtuka akiziuliwa teke la usoni, ambalo lilimpata sawa sawa, kati kati ya macho na mdomo, kwama ya kwamba kwenye mgongo wa pua, wakati huo miguu yake ina kwatuliwa, miguu yote miwili na kupaishwa juu kisha kujibwaga chini, ambako sasa akuamka tena, kwamaa alijuwa akiamka tu, ataendeea kutembezwwa mkong’oto, “aya mfungeni pigu mpandisheni kwenye gari” alisema mama Mbaga, au DCP Mariam Mbaga, na wale askari waka mfunga pingu na kumpakiza kwenye gari, huku anavuja damu sehemu mbali mbali za uso wake, huku raia wakiwazomea.
Naam akiwa anajuwa tayari amesha pona, huku moyoni akipanga kuto kujiusisha tena na Ratifah, mala akamwona yule mama polisi akiwatazama wakina Mdee na mke wake, ambao walikuwa wamekaa kimya sasa, wakisikilizia kitakacho wapata, “Damian na awa ndio wakina nani, na imekuwaje wapo hivi” aliuliza mama Mbaga, lakini swali ilo alikujibiwa na Damian, ila lilijibiwa na mtu mngine kabisa, “mama Mbaga, hao ndio wale nilio kueleza” hapo siyo Mdee au Johakim, wote walishtuka na kutazama ilikotokea sauti, hakika ulikuwa nimshtuko mkubwa sana kwa wawili awa, ambao waliweza kumwona boss wao yani bi Shwifat akisogelea pale walipo, huku amemshika mkono wa mtoto mdogo wa kiume. . . , . …
SEHEMU YA HAMSINI
Hapo Ratifa aliweza kumwona mpenzi wake Johakim, akigeuka na kumtazama yule mwanamke mrembo na mzuri kupita kiasi, kwa macho ya kuomba na kuomboleza, “boss naomba unisamehe nishetani alinipitia” alisema Johakim huku akikusanya viganja vya mikono yake kifuani na kufanya kama anataka kusali, ilimshangaza sana Ratifah, baada ya kusikia Johakim anamwita yule mwana dada kuwa ni boss, lakini Shwifat akumjari Johakim, zaidi akaendelea kueleza, “huyu anaitwa Johakim, ndie meneja wangu, ambae ndie mwizi wa mke wamtu, amekuwa akiniibia fedha zangu kila siku kwaajili ya kuhonga polisi” alisema boss lady, ambae alizidi kumshangaza Ratifah, ambae kiukweli alianza kuona vimuli muli usoni mwake, wakati huo wale wananchi waliokimbia mwanzo wakianza kurudi na kusogea pale walipokuwepo wakina Damian, na kusikilza kilichokuwa kinaendelea.
Shifwat akuishia hapo, akaendelea kueleza, “na huyu alie lala hapo, nae pia ni mfanyazi wangu, yeye ndie kuwadi wa mwenzie” alisema Shwifat au mama Alvin, huku anaenda kusimama karibu kabisa na mama Mbaga, huku mtoto Alvin, akiachia mkono wa mama yake na kumfwata baba yake huku wakina Mdee na mke wake pamoja na Ratifah, wakisahu maumivu yao na kushangaa kile wanacho kiuona, “kwahiyo Johakim, kuanzia leo, wewe na Mdee siyo wafanyakazi wangu tena, hii ni kwa kuto kufaa katika jamii” alisema boss Lady, na hapo Ratifa ambae sasa ndio kwanza alikuwa anaujuwa ukweli wamambo, alimwona mtu ambae aliamini kuwa ndie mmiliki wa duka lile kubwa la DS, akishtuka vibaya sana, na kupiga magoti mbele “boss tumetoka mbali mama yangu naomba unisamehe, wewe nisawa na mzazi wangu, namba usinifukuze kazi, nina mke na watoto, wananitegemea” alisema Johakim kwa sauti ya kubembeleza, huku sauti yake ikiwa na dalilizote za kuangua kilio, “huku Mdee akidakia “lakini bass mimi nausika vipi, yeye ndie anae usika, isitoshe boss sisi niwafanya kazi wako wa muda mrefu, huyu umefahamiana nae juzi tu” alisema Mdee na kumanya Damian acheke kidogo, labda kuna kutu mnapaswa kujuwa Mdee, huyu Damian ndie mumewa nguu wa pekee na ndie baba wa huyo mtoto, nilipotezana nae kwamuda tu, na akaangukia kwa huyu mwanamke asie na bahati, kwa hiyo basi uwezi kunishawishi kwa lolote lile” kauri ile ya Shwifat ilimfanya Ratifah, asikie mchunzi una churuzika kwenye vungu za mapajani mwake, kwamaana tayari alisha ingia kwenye siku zak kwa ghafla.
“Eti mke wa Damian, na huyu ni mtoto wake” alijiuliza Ratifah, ambae aligeuza uso wake kumtazama Johakim, “wewe ulinidanganya mimi kuwa lile duka nilako kumbe wewe ni kibaru….” hapo kabla Ratifa ajamalizia kauri yake, Johakim akamdaka juu kwa juu, “kelele we nuksi, mimi nawaza kuhsu familia yangu, wewe unaongea upambavu wako” alisema Johakim kwa hasira, kisha akamtazama tena boss wake, naomba unisaidie boss ninafamilia boss, nina watoto…” alisema Johakim na kabla ajamaliza, hapo mama Mbaga akamkatisha, “inatosha, mala iliuwa a familia siunge jiheshimu na kuheshimu maisha ya wenzako, tena kwa taarifa yako nyie wote wanne mtambatana na sisi kwenda kituo cha polisi kuchukuwa maelezo yenu, na kikiwezekana mtabakia huko kusubiri kesi yenu ipelekwe mahakakamani, kuhusu matibabu itajulikana huko huko” alisema mama Mbaga, na hapo bila kuchelewa, polisi waka anza kuwafunga pingu wakina mdee, ambae alivunjika mkono.
Wakati polisi wakike wakiwafunga pingu wakina Ratifah, pia wakiume waliwafunga pingu wakina Mdee na Johakim, ambae alinyang’anywa funguo na kukikabidhiwa Damian, hapo Ratifah, akaanza kuangua kilio kikubwa, “jamani mume wangu Dami, naomba unisamehe, nilidanganywa na huyu mwanamke, siwezi kuvumilia kiona mume wangu ukiondoka na manamke mwingine, naumia mwenzio, bado nakupenda, nishetani tu alinipitia” alisema Ratifah, huku aangua kilio kikuu, kusikia hivyo, Damian aka cheka kidogo, kisha akamwambia Ratifah, “kama inauma chomoa, unakumbuka hiyo mama Tuma, nitakacho kusaidia ni kukurudisha nyumbani, kama utakuwa tayari kufanya hivyo, mala baada ya swala ili kumalizika”.
Naam hivyo ndivyo ilivyokuwa, polisi wanne wakiongozwa na yule polisi wenye nyota moja, walifukuzwa kazi na kufungwa miaka kumi na mbili jela, huku mdee na mke wake wakiachiwa huru, baada ya kupatika awana hatia, lakini Mdee licha ya kuomba sana asamehewe asifukuzwe kazi, wakati mwingine akimfwata Damian amsamehe na kumwombea arudishwe kazini, kitu ambacho kilimshangaza sana Damian, kwamba Mdee anapatawapi moyo wa kumwambia jambo lile, “kaka inaga urafiki wa kipumbavu kama huo” ilo ndilo lilikuwa jibu la Damian, na ukweli Mdee akuwa na lakufanya, akarudi kijijini kwao mwanga stesheni kule Kilimanjaro, huku mke wake akigomea mjini na sasa anadanga kwenye baa za mwendapole huko kibaha, Ratifah ambae aliachiwa huru, alijaribu kuomba kwa Damian asamehewe, huku akidai kuwa yupo tayari kua mke wa pili, au nyummba ndogo, lakini Damian alimfukuzilia mbali, na baadae kumpatia nauri ya kurudi kijijini kwa wazazi wake Mpitimbi, huku sura yake ikifanana na bwana Zidadu Hassan yani mzee Mangeu (soma hadithi ya kifo cha hawara).
Ratifah, akuacha kujuta kwa kumpoteza Damian ambae alikuwa msaada mkubwa sana kwake na wazazi wake, pamoja na binti yake, kalicho kuja kugundua ni kwamba, kwa johakim akuambulia chochote zaidi ya kuchezewa tu na kuaribu maisha yake, ukichukulia yeye aliamua kumfata Johakim kwa kujuwa kuwa ni mtu mwenye fedha na gari, akujari upendo aliokuwa anapewa na Damian, nje na ndani kitandani, akujari uchovu wa Johakim kitandani, yeye aliamini kuwa hipo siku ataingia Mpitimbi, kama mlikia tena ndani yagari, sasa alikuwa anamshuhudia Damian akija Mpitimbi na gari zuri la kifahari, miziwadi kibao ka wazazi na majirani, huku akiambatana na mke wake na mtoto wao.
Johakim alibainika na kosa la kufanya ujuma kwenye familia ya mwenzie, na kupewa adhabu ya kulipa fidia ya tsh milio mbili, au kwenda jela miaka mwaka mmoja, hakika fidia ile ilimshinda, na kwenda jela kutumikia adhabu ya jela mwaka mmoja, wakati huo huo miezi sita ya mwanzo ya kifungo chake, tayari mke wake alikuwa amesha uza kila kitu na kurudi kijijini kwao yeye na watoto wake, ambako akukaa ata mwezi mmoja akapata mwanume na kuolewa nae, taarifa zilipo mfikia Johakim kule gerezani, alizimia mala kdhaa, sijuwi kwaajili ya mke au kile alicho kipoteza, yani vitu ambavyo mke wake aliviuza, kwamba akitoka gerezani ajuwi pa kuanzia, sikuzote alikuwa anajutia kile alicho kifanya na kusababisha maisha yake yabadilike kabisa.
Maisha yalikuwa mazuri kwa Damian, na Shwifat, ambao licha yakuongeza biashara nyingine na kufungua matawi ya DS mkoani Ruvuma, pia walijenga nyumba nyingine tatu kubwa na za kifahari, na sasa wanaishi kwa raha mustarehe.
Nisema Asante kwa kuwa pamoja na mimi manzo mpaka mwisho wa Hadithi hii ambayo naamini umepata chakujifunza japo kidogo, naomba endelea kufuatilia mikasa mingine mingi itakayo kujia hapa hapa Raha Special.