KAMA INAUMA CHOMOA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA THERASINI NA SITA
ILIPOISHIA: Hapo yule askari aka mtazama mwenzie na kumpa ishala ya kusogea pembeni, ambako waliongea mawili tatu, kisha Warioba akarudi pale kwenye banda la Kapate, “sasa nakuachia maagizo yake, ukimwona mwambie hivi, yani kwa usalama wake, aje mwenyewe ajisalimishe kituo cha polisi, cha mbezi kwa yusufu, kama tukitumia mafuta ya gari letu, nakumkamata, basi atalipia kuanzia mafuta, mpaka nguvu zetu” alisema kwa Jazba Warioba, “samahani kaka afande, kwani Damian amfanya kosa lolote?” aliuliza mmoja wawakina mama waofwanya biashara pale makondeko, ambae alikuwa anafahamu kisa chote, mwanzo mwisho. . . …endelea..
Hapo Warioba akamtazama yule mama kwa jicho la hasira, “ukitaka kujuwa njoo kituo cha polisi” alisema Warioba huku anatembea kuelekea kwenye gari, ambalo alikuchelewa kuanza safari, kuelekea mbezi kwa yusufu, huku wakiwaacha watu wote wakiwasindikiza kwa macho, na ata walipojihakikishia kuwa wamesha fika mbali, wakaangua vicheko vya ushindi kwa kuwafanya wenzao mabwege.
Nusu saa baadae tayari Damian alikuwa juu ya piki piki anakaribia kufika kwenye nyumba aliyo panga, sehemu ambayo alikuwa anaenda kwa lengo moja, yani kukusanya kila kilicho kuwa chake ili atoroke, ukweli hakuwa na vitu vingi sana, sana sana, ni kitanda cha kawaida tu, na godoro, nguo pamoja na hakiba yake ya fedha, ambayo alikuwa ameificha kwenye kijikaptulah, kifupi cha jinsi, hivyo vingine, hakuwa na inshu navyo sana, sijuwi mandoo ya maji na masufuria, akuona kama vya msingi sana, kwamba angepambana, na kununua nyingine.
Lakini baada ya kufika kwenye ile nyumba aliyokuwa amepanga, alikuta mlango umefungwa na kufuri mpya kabisa, tena kubwa na imara, kwamaana hiyo asingeweza tena kuingia mle ndani ya chumba chake, ata Damian alipouliza juu ya ufungwa kwa mlango wake, akaambiwa kuwa, mlango umefungwa na Johakim, tena mbele ya polisi, akitamka wazi wazi kuwa, Damian atakiwi kuingia mlendani, na popote atakapo patikana basi cha mtema kuni atakiona, “sikia Damian, inabidi twende ukamwone boss wa Johakim, inginevyo utazulumiwa kila kitu chako” alishauri yule boda boda, na pasipo kufikilia anachoenda kukutana nacho kule dukani, kinaweza kuwa kibaya zaidi au kizuri kwake, Damian alikubariana na yule boda boda, na safari ikaanza mala moja, wakitumia njia za uchochoroni.********
Wakati huo muda uliopita, Mdee akiwa dukani, mala kwa mala alikuwa anampigia mke wake, na kumuuliza kinachoendelea, ambapo tayari mke wake alisha mweleza jinsi polisi walivyofika pale nyumbani, na kufunga mlango wa chumba cha Damian, ilikuwa baada ya kumkosa, “tumesha fika hospital, na sasa polisi wanaenda kumkamata Damian” hayo yalikuwa ni maelezo ya mke wa Mdee.
Wakati, Mdee akiwa anaendelea kusikilizia taarifa ya huko hospital mala kwa kutumia vioo vikuwa vya madirisha ya duka lile, akaliona gari aina ya Toyota land cruzer V8 likiingia pale dukani, na kupitiliza upande wa nyuma wa maegesho ambayo utumiwa na boss wao pekee, ukweli Mdee alishtuka sana, ni kutokana na mambo mawili.
Mmoja ni kwamba, Johakim akuwepo, na nikosa kubwa sana kutoka wakati wakazi labda ikitokea uwe na zalula, pili Mdee alikuwa nafahamu jinsi Mde alivyo kuwa anaangaika kuweka sawa mahesabu yake, kutokana na fedha nyingi kutoweka bila utaratibu.
Lakini Mdee asingejuwa kama boss wake yupo mwenyewe, ndani ya gari, au yupo na mtu, mwingine, na pia asingeweza kumwona akiwa katika hali gani, yani ametabasamu au au amenuna, nikutokana na gari ilo kuwa lime pandishwa vioo vyake ya giza, yani tinted.
Mdee alilisindikiza lile gari kwa macho, mpaka lilipopotelea upande wa uwani wa duka lile, kubwa la kisasa, lenye nguo nyingi na vipodose vya kisasa, hapo Mdee kwa araka sana, akatazama kushoto na kulia, kama kuna muuzaji mwenzie yupo karibu, akamwona mmoja wakike, akamsogelea kwa haraka, akimwacha mteja ambae alikuwa anaitaji huduma, “leo mtu mfupi amepatika” alisema Mdee kwa sauti iliyojaa umbea na shahuku, huku anatoa simu yake na kupiga kwa Johakim, huku yule muuzaji mwenzie wakike, akiishia kuguna tu.
Simu iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa na kabla aijakata, akaonekana Johakim, akiingia mle dukani kwa mwendo wa mbio mbio, na kupitiliza upande wa ofisini kwake, huku uso wake ikionekana wazi kuchanganyikiwa kwa hofu, ni wazi boss wake alikuwa amempigia simu, mala tu baada ya kumkosa, “mwone tumbo lake linavyo cheza” alisema Mdee akimalizia kwa kicheko cha chini chini, yule mhudumu akushangaa, maana anamfahamu Mdee kuwa ni rafiki mnafiki, na kigeu geu, ambae alitumia urafiki wake na Johakim kuwafukuzisha kazi, wafanyakazi kadhaa pale dukani, kwa taarifa za uongo na umbea.*******
Naam baada ya kumaliza matibabu, Ratifa na mke wa mdee walitoka pale pale hospital, na kusimama barabarani, huku Ratifah alie jaa bandage uso mzima, akizuwia mishono mbali mbali, akipga simu kwa Johakim, simu ambayo aikupokelewa ata kidogo, licha ya kurudia mala kadhaa, lakini aikupokelewa kabisa, ndipo walipo pata wazo la kupanda dala dala, na kuelekea nyumbani kwao ambako alifikia kwenye chumba cha mke wa mdee, maana mlango wa chumba, ambacho sasa alikuwa anakiita chake, ulifungwa na funguo alikuwanazo Johakim…
SEHEMU YA THERASINI NA SABA
Ratifa alijilaza juu ya kochi chakavu la watu wawili, ambalo ni pacha wa mwenzio la mtu mmoja, ambalo uchavu wake ulizidi lile la watu wawili, kochi ambalo ukikaa kwa dakika kumi, lazima uwe umesha piga chafya ishilini au therasini, na ukikaa zaidi ya dakika kumi, basi ukitoka hapo lazima ukajifukize kutokana na vumbi lililoja kwenye kochi ilo, “sijuwi kwanini apokei simu zangu” aliwaza Ratifa, ambae mala kwa mala alikuwa anajaribu tena kupiga simu kwa Johakim, sumu ambayo iliita mpaka inakatika bila kupokelewa.******
Yap! baada ya kula chochoro kwa chochoro, hatimae Damian na boda boda wake wakaibukia mbezi, na moja kwa moja wakaelekea barabara ya goba, mita chache toka stendi ya zamani, ambako sasa kulikuwa na round about, wakaibukia kwenye eneo la mbele la duka kubwa la kisasa, ambalo lilionekana kupokea wateja wengi, waliokuwa wanaingia na kutoka, na wao wakasimamisha pikipiki yao karibu kabisa na maegesho ya magari, “sasa naanzaje hapa kaka?” aliuliza Damian, akiwa amesimama pembeni ya pikipi, na mwenzie amekaa kwenye pikipiki, “we ingia ndani, omba kuonana na mwenye duka” alisema yule dereva wa boda boda, “poa wachaniende” alisema Damian, huku anapiga hatua kuufwata mlango wa lile duka.
Lakini hatua mbili tu, alizopiga akajikuta amesimama ghafla, huku anatazama mbele yake, sehemu ambayo lilikuwa limetazama Toyota Vitz, kwa macho ya mashaka na wasi wasi, “huyu mpuuzi atakuwa humu ndani” aliwaza Damian, huku anatazama ndani kupitia dirishani, akamwona Mdee akiwa busy na wateja, walio jaa mle ndani.
Hapo Damian aka geuka kwa haraka na kurudi pale alipotoka, yani kwa yule dereva wa boda boda, “kaka hapatufai hapa, ebu tuondoke haraka” alisema Damian, huku anakaa kwenye pikipiki, “hoya kuna nini?” aliuliza boda boda, huku anawasha pikipiki, na kuondoka kwa haraka, “Johakim yupo ndani, nimeliona gari lake, akiniona tu lazima awaambie polisi” alisema Damian, kwa sauti yenye mashaka makubwa, na wasi wasi ya hali ya juu, huku wanaishana na gari moja la polisi, aina ya Nissan Safari wagon, (yani lililozibwa kote/milango mitano) ambalo ndani yake kulikuwa lililokuwa linaingia pale dukani, ndani yake kulikuwa na watu kama watatu.
Wakwanza ni Dereva alie valia nguo za polisi, na cheo cha koplo, pia mwana mama mtu mzima, alie valia sare za kipolisi, huku nyota kadhaa kizikwa zime jipanga mabegani mwake, ambazo kwa haraka siwezi kuzielewa ukanielewa, ila nikikueleza kwa jina cheo iki, ni DCP, hakika ni wadhifa mkubwa sana, ndani ya jeshi la, nikama ngazi ya tatu au ya nne, toka juu kabisa ya uongozi wa jeshi ilo, na mala nyingi wenye cheo hicho, uwa ni wakuu wavitengo vya jeshi ilo kitaifa, mfano mkuu wa upelelezi, mkuu wa Traffic, na wengineo, tuyaache ayo maana ayatuhusi, watatu alikuwa ni mwanamke mrembo mwenye umri wakati ya miaka 24 mpaka 26, ila mrembo na wenye sura nzuri, sijuwi huko chini.
Wakina Damian ambao walikuwa wameshtushwa na gari lile, walipishana nalo huku wakiwa wanatetemeka, kwa kujuwa kuwa polisi wanakuja kumkamata Damin, lakini baada ya kuona waliokuwepo ndani, wakapoa kidogo mioyo yao, na kwenda kusimama mita kadhaa toka pale dukani, kisha wakatazama kule dukani, ambako waliliona gari lile la polisi likiwa limesha simama, na akashuka yule yule mama polisi, pamoja na yule mwanamke mwingine, ambae sasa waliweza kumwona jinsi alivyo jaliwa umo zuri la kutamanisha, ikionyesha ni mwanamke toka familia bora, nao wakaingia ndani ya duka.
“Dah! mwanangu nilijuwa tayari umesha kamatwa” alisema derea wa boda boda, yani ilibakia kidogo niruke alafu nikimbie, yani kaka kule kituoni, siyo kwa kurudi ata kidogo alisema Damian, kwa sauti ambayo kiukweli ungejuwa kuwa alikuwa ametoka kwenye hofu kubwa sana, wote waacheka kwa pamoja, “sasa kaka tunafanyaje, maana yule mshenzi yupo pale na ni kisema niende hivyo hivyo, lazima akiniona tu, ata piga simu polisi, alafu watanikamata?” aliuliza Damian, ambae sasa alishuka kwenye pikipi na kusimama pembeni, akimwacha mwenzie amekaa juu ya pikipiki.
“Hapa cha msingi, ni kuumiza kichwa, tuone tuna fanyaje, maana kwa nza atuna uhakika kama yupo pale dukani, pengine yupo kwenye maduka yake mengine” alisema dereva wa boda boda, na hapo wakaanza kujadiriana kwa kina mpaka wakapata jibu, kwamba dereva wa boda boda aende pale dukani peke yake, aka angalie kama boss wao yupo, na kama yupo je inawezekana kuongea nae, kisha aje amjulishe Damian.
Naam ikawa hivyo dereva wa boda boda akaacha pikipiki pale pale, na kuelekea dukani kwa miguu, huku Damian akiwa amesimama pembeni ya pikipiki kwa tahadhari kubwa sana, akisubiria taarifa muhimu toka kwa dereva wa boda boda, ambae alipotelea huku kwa dakika kama ishilini na tano au therasini kabisa, kisha akarudi huku akonekana kuwa katika hali ya unyonge, kiasi cha kumshtua Damian, “kaka vipi kuna usalama huko utokako?” aliuliza Damian, kwa sauti iliyojaa mashaka na wasi wasi, “mwanangu tutafute ela, vinginevyo tutakosa vitu vizuri duniani” alisema yule dereva wa boda boda, kwa sauti yenyekujawa na unyonge mkubwa.
Ukweli hiyo ilimshangaza kidogo Damian, ambae alikuwa amelenga kwenye jibu kuhusu kile walicho kusudia, “kivipi kaka, mbona sikuelewi?” aliuliza Damian kwa mshangao, “kaka kuna mademu wazuri, yani sijuwi Ratifah, angekuwa kama hivi, alafu anakuletea inshu kama hizi, ingekuwaje, hakika unaweza kuuwa mtu” alisema yule boda boda, kwa sauti ambayo ilikuwa na msisitizo wa hali ya juu, kiasi kwamba Damian akacheka kidogo, “ushaanza kumtamani yule mwanamke wa gari la polisi?” aliuliza Damian huku anacha kidogo, “mh! ile taka taka kwa huyo boss wao, ni demu mkali kinoma, yani sijuwi kama utaweza kuongea nae vizuri, maana nahisi unaweza kuanza kumshangaa baada ya kumweleza kilicho kupeleka” alisema boda boda, pasipo dalili ya kwamba alikuwa anatania.******
Ilikuwa hivi, baada ya boda boda kufika pale dukani, na kuingia moja kwa moja ndani, ambako aliwakuta wateja wengi wakiendelea na manunuzi, ya nguo mbali mbali na vipodose, huku wateja wengi wakiwa ni wakike, pamoja na yule polisi manyota, na mschana mrembo alie ongozana nae ambae mala kwa mala alikuwa anamwita mama, pia wawili wale walikuwa wana hudumiwa na kusindikizwa na mwanamke mmoja mrembo hatari, alie kuwa na umri kati ya miaka ishilini na nane mpaka therasini. …
SEHEMU YA THERASINI NA NANE
ILIPOISHIA: Ilikuwa hivi, baada ya boda boda kufika pale dukani, na kuingia moja kwa moja ndani, ambako aliwakuta wateja wengi wakiendelea na manunuzi, ya nguo mbali mbali na vipodose, huku wateja wengi wakiwa ni wakike, pamoja na yule polisi manyota, na mschana mrembo alie ongozana nae ambae mala kwa mala alikuwa anamwita mama, pia wawili wale walikuwa wana hudumiwa na kusindikizwa na mwanamke mmoja mrembo hatari, alie kuwa na umri kati ya miaka ishilini na nane mpaka therasini. …endelea..
Boda boda ilibakia kidogo asahau kilicho mpeleka mle ndani, kwa kumshangaa yule mwanamke alie kuwa anawasindikiza wakina polisi na binti yake, maana licha ya kwamba mle ndani kulikuwa na waschana wengi warembo, lakini huyu mwanamke alikuwa mzuri sana, tena alionekana kuwa nyadhifa flani mle ndani, maana kuna wakati alikuwa anatoa maelekezo flani flani kwa wafanyakazi wa mle ndani, akiwepo Johakim mwenyewe, ambae alikuwa amesimama kiunyonge anawatazama polisi wale wanawake ambao sasa walikuwa wawili, huku wakati mwingine Johakim akijichekesha chekesha.
Wakati huo pia alimwona Mdee, aliekuwa anamtazama Johakim kwa jicho flani kama la kumsimanga au akumchukia flani, ilishangaza kidogo, kwa watu wanao ufahamu urafiki wao, maana ule mtazamo, ulionyesha wazi kuwa Mdee alikuwa anakijiroho flani cha chuki na wivu ndani yake.
Hapo boda boda wetu ambae kiukweli alichanganyikiwa kwa uzuri wa boss wa Johakim Mdee, ajaachana na mambo ya kina Mdee, na kusogea mpaka sehemu alipokuwepo muuzaji mmoja wakike, alie kuwa peke yake, “habari dada” alisalimia boda boda wetu, “safi tu, karibu kaka yangu” aliitikia yule muuzaji wakike, huku anaachia tabasamu pana usoni mwake, “asante dada yangu, lakini mimi siyo mteja, ila nilikuwa nashida moja tu, naitaji kuonana boss wa duka ili” alijieleza boda boda, “boss yupi, meneja au madam mwenyewe?” aliuliza yule mwanamke, huku akitazama kule alikokuwepo yule polisi.
Hapo boda boda nae akatazama kule alikotazama yule muuzaji, akaona anawatazama wale wanawake waliokuwa na polisi,ambao niwazi wailikuwa wanachagua vitu vya sherehe flani, ambayo inamuhusu yule mwanamke, aliekuja na yule mama Polisi, kama siyo harusi basi ni send off au kitche party, maana kila kilicho nunuliwa kulionekana ni kwaajili yake, na mwonekano wa vitu vile ulionekana ni wakung’aa sana, “naitaji kuonana na boss mwenyewe kabisa, siyo meneja” alijibu boda boda, huku macho yake yakitazama kule alikokuwa yule mwanamke mrembo sana, alie kuwa anawasaidia madam polisi, na binti yake.
“nazani unamwona alivyo busy, na akitoka hapo nazani wataongozana kwenye duka la vitu vya ndani, kuchagua zawadi za bibi harusi, ambazo yule mama polisi, anataka kumpatia yule binti yake siku ya harusi yake” alisema yule muuzaji wa duka, huku anatazama kule walikokuwepo wakina mama polisi, “unamaanisha boss wenu ndiyo yule dada?” aliuliza boda boda kwa mshangao, “ndiyo, ndie boss wetu, mbona umeshangaa?” aliuliza yule mwanamke muuzaji, wakati huo huo akaja mteja kwaajili ya kupata maelekezo juu ya bidhaa flani.
Ilichukuwa dakika kadhaa, mpaka kumaliza maongezi na yule mteja, huku boda boda akisubiri mpaka alipo maliza, wakati huo yeye alikuwa anamtazama yule mmilikiwa duka lile la DS, “kwahiyo dada nawezaje kumpata boss na kuongea nae?” aliuliza boda boda wetu, “kwani utaka kuomba kazi, siumfwate pale pale ukamweleze” alisema yule mhudumu wa duka, “ni swala binafsi siwezi nikaongea nae juu juu” alisema boda boda wetu, ambae macho yake aya kubanduka kwa yule mmiliki wa DS beauty point, “basi kama ni hivyo jioni umfwate nyumbani kwake” alishauri yule mwanamke.
Hapo boda boda alishtuka wazi wazi, “weeeee! nyumbani kwake, si ata nifukuza kama mwizi, hapa yenyewe kuongeanae naogopa” alisema boda boda akionyesha wasi wasi wa hali ya juu, na kumfanya yule mwanamke acheke kidogo, “kwanini unasema hivyo mbona boss ni mtu poa sana, wala awezi kukufukuza” alisema yule mwanamke, na kwauhakika akamshauri kuwa nivyeka kama atamweleza juu ya kwenda kwake nyumbani jioni, “inabdi uende ukamweleze wewe mimi siwezi” alisema boda boda, na bahati nzuri yule mwanamke, akakubaliana na boda boda,”aya nisubiri hapa hapa” alisema yule mwanamke huku anaondoka na kumfwata boss wake ambae bado alikuwa anaambatana na wale wageni wake, ndani ya duka,
Mwanamke alimfikia boss wao, na kumweleza kama alivyo kubaliana na boda boda wetu, kisha akarudisha jibu kwa boda boda, “amesema ata kuwepo nyumbani kwake, mida ya saa mbili za usiku” ilo ndilo jibu ambalo yule mwanamke alimweleza boda boda, na kumwelekeza uelekeo wa mtaa wa anakokaa boss wao, “ukishuka kibanda cha mkaa fwata barabara ya upande huu ulioshukia, pale utakuta boda boda, unaweza kuuliza nyumbani kwa mama Alvin, wata kupeleka mpaka kwake, tena nauli ni elfu moja tu” alieleza yule mwanamke.
Boda boda alimweleza Damian kila kitu, “yani Damian kuna watu wanafaidi, kama mume wa huyo demu, yani huyo demu ni mzuri kinyama” alihitimisha boda boda kumweleza kijana wetu Damian, na hapo wakapanda pikipiki kwa lengo la kwamba jioni waende huko mbezi kibanda cha mkaa, anakoishi boss lady.*******
Naam Damian alipelekwa moja kwa moja nyumbani kwa Kapate, kule kibamba kwa Mangi, kisha boda boda akaendelea na minzunguko yake wakisubiri jioni, wande waende kumwona boss.
Yaap masaa ya lienda, huku mala kwa mala Damian akipokea simu toka kwa Kapate akiambiwa kuwa polisi walikuwa wanazungukia pale kijiweni mala kwa mala, kusaka yeye, huku akisisitizwa kuto kutoka pale nyumbani, nae akajifungua ndani akaiuchapa usingizi, mpaka mida ya saa saa moja za jioni, mida ambayo walipanga kwenda kwa boss lady wa DS beauty point, lakini boda boda akutokea, ndipo Damian, akaamua mpigia simu yule boda boda, na bahati nzuri ilipokelewa mapema sana, “damian, sijuwi tuta fanyaje nipo Tondoroni na abiria, sijuwi amekuja hapa kwa ganga, yani toka saa kumi mpaka saa hizi ajatoka” alisema boda boda kwa sauti ya kulalamika, “dah! sasa tuna fanyaje, kama vipi wacha niende na dala dala” alisema Damian, kwa sauti ya kinyonge, ukweli aliona ni vigumu sana kulikabiri kwenyewe swala la kwenda kumwona, huyo boss wa wakina Johakim, “poa poa, utakuwa umefanya vizuri, maana zaidi ya hapa nitakuchelewesha” alijibu boda boda.
Na bila kuchelewa Damian akaanza safari kuelekea barabarani, ambako alipanda dala dala, na ata wakati anapita pale kijiweni kwao makondeko, akaliona gari la polisi likiondoka maali pale, sambamba na gari la johakim, ndani ya gari akiwa na Mdee, na wakati gari la polisi likielekea mbezi, gari la Johakim lilielekea kule alikopanga yeye, hakika roho ilimuuma sana Damian, ambae moyoni mwake alikili kuwa kama siyo uwezo wa Johakim wakutumia polisi, angekuwa amesha mpasua muda mrefu uliopita. …
SEHEMU YA THERASINI NA TISA
ILIPOISHIA: Na bila kuchelewa Damian akaanza safari kuelekea barabarani, ambako alipanda dala dala, na ata wakati anapita pale kijiweni kwao makondeko, akaliona gari la polisi likiondoka maali pale, sambamba na gari la johakim, ndani ya gari akiwa na Mdee, na wakati gari la polisi likielekea mbezi, gari la Johakim lilielekea kule alikopanga yeye, hakika roho ilimuuma sana Damian, ambae moyoni mwake alikili kuwa kama siyo uwezo wa Johakim wakutumia polisi, angekuwa amesha mpasua muda mrefu uliopita. …endelea..
Hapo hapo Damian aka toa simu yake, na kumpigia Kapate, akimweleza kuwa alikuwa njiani anaelekea mbezi kibanda cha mkaa, kumwona boss wa DS, “poa kaka ukitoka huko utanipigia nikueleze nipo wapi, kama ni hapa kijiweni au ghetto” alisema Kapate, ambae alikuwa na shahuku ya kujuwa mafanikio ya rafiki yake.
Naam ukweli ni kwamba, kapate alisubiri sana simu ya Damian, mpaka saa sita za usiku, pasipo kupokea simu yoyote toka kwa Damian, ujumbe mfupi wa maandishi, kuna wakati Kapate akajaribu kuipiga namba ya simu ya rafiki yake, lakini akaambiwa kuwa aipatikani, hapo akaanza kuingiwa na wasi wasi juu ya rafiki yake, ambae akumwona mpaka kuna kucha, yani siku ya pili, nae alipofika jiweni akawasimulia wenzake, ambao waliingiwa na wasi wasi mkubwa, na kuamini kuwa ata kuwa alikamatwa na polisi, hivyo wakajadiliana nani aende kituo cha polisi kumtazama Damian maana walikuwa wanaamini kuwa, atakuwa ameangukia mkononi mwa polisi.
Lakini tatizo likaja nani ataenda polisi, ilikuwa kama ile hadithi ya kikao cha paka, kuhusu kumfunga paka kengere, hakika wote waiogopa, na mwishoni kabisa wakakubariana kuwa, wakae mpaka kesho asubuhi endapo awato mwona Damian, basi waende wote kwapamoja mpaka kituo cha polisi.
Wakati wakina Kapate wanajadiri juu ya swala ilo, huku nako mambo yalikuwa tofauti, maana ile jana, mala baada ya Johakim kufika pale ofisini na akiwa amepigiwa simu na boss wake, ambae akuwa amemkuta ofisini, alimkuta boss wake amekasirika vibaya sana, japo siyo kawaida yake, “Johakim, nime soma aya mahesabu yako mbna ayaeleweki, hizi laki saba zimeenda wapi?” aliuliza boss yule wakike, ambae ata boda boda aliukubari uzuri wake, na kustaajabika, “haaam… boss unajuwa.. aya mahesabu bado sijakamilisha, nitakuelezea vizuri tu” alisema Johakim kwa sauti yenye kigugumizi cha ghafla, “lakini hapa inaonyesha wazi, kuna ubabaifu, ebu ona hapa, hiilaki tatu imetoka bila maelezo, nah ii lakimoja na nusu, imetoka bila maelezo, kuna laki mbili na nanusu, umeandika nauri ya wafanya wakati nilisha jumisha kwenye mishara yao, ebu niwekee sawa aya mahesabu, sitaki tukosane, alisema yule boss, huku ana itoa simu yake ambayo niwazi ilikuwa inaita kwa mtetemo, akaipokea na kuweka sikioni, “ndio mama Mbaga….. hooo! usiofu nipo humu ndani, ingieni tu nakuja” alisema boss mzuri mzuri, ambae kiukweli sidhani kama tuna aja ya kumfahamu jina lake, huku anatoka nje ya ofisi, akimwacha Johakim, ambae alikuwa anaisikilizia simu yake iliyokuwa inaita toka mfukoni mwake.
Johakim alipoona simu inaita sana, akaitoa na kuitazama na alipoona jina la Ratifah, akairudisha mfukoni na kuelekea upande wa duka, ambako alimwoka boss wake akiwa na wageni wake, nae akasimama na kuwakodolea macho, huku anawaza namna ya kudanganya kuhusu zile fedha, ambazo kiukweli alizitumia yeye mwenyewe, tena kwa starehe zake na Ratifah, ikiwa na kuonga polisi, ili wamkamate Damian, mchezo ambao naufanyaga mala kwa mala kwa mala pale Damian anapozingua na kumwekea kauzibe kwenye penzi lake na Ratifah, ambae kitu kimoja wapo kinachomfanya ampende ni kuwa mchepuko usio na gharama nyingi, ukiachia kunywesha pombe, na kuonga polisi, Johakim akuwa na gharama yoyote, kuanzia chakula na maladhi, labda siku moja moja akiamua kumnunulia nguo, viatu na vitu vidogo vidogo.
Zaidi ya hapo akuangaika Ratifa leo anakula nini, wala analalaje, au nani analipa kodi ya nyumba, maana alijuwa fika kuwa kuna bwege analipa na kugharamia kila kitu, huku yeye ana kula kitumbua na vingine ambavyo aviluhusiwi kuliwa, vitu ambavyo ata mwenyewe alie mleta toka kijijini, akuwai kuthubutu ata kuomba, au kujaribu kama vinalika, “nitajuwa namna ya kufanya, lazima atakubariana namimi” aliwaza Johakim, huku anamtazama boss wake, ambae kiukweli licha ya kukaa hapa dukani kwa miaka miwili, lakini akuwai kuuzowea uzuri wa mwanamke huyu, amba ajuwi alifanywa nini na wanaume, maana licha ya kuwa na mtoto mmoja, lakini hakuwa na mume na wala akuwai kumwona ata mala moja, kiwa na mwanaume, ambae unaweza kushuku kuwa ni mwanaume wake, kwamaana ya mpenzi.
Yap! mala baada ya boss kumalizana na wageni wake, ambao walinunua mzigo mkubwa wakueleweka, akaondoka zake pamoja na wageni wale, yani mama Polisi, alie fahamika kwa jina la mama Mbaga, huku akimsisitiza jambo Johakim, “andaa vitabu vyote, vya mauzo, na pia matumizi nikija tutakaa pamoja na kupiga mahesabu upya”
Hapo Johakim alihisi kuwa tumbo la unguruma, kwamaana ata minyoo ilishtuka kwa maagizo yale mazito, maana Johakim akutegemea ata kidogo, kama jambo ilo lingefanyika, na hakika kwa jinsi hiyo, asingeweza kudanganya atahesabu moja, “dah! hapo nime patikana” aliwaza Johakim, huku ana rudi ofisini kwake, ambako alikaa kutwa nzima akijaribu kuptia mahesabu yake vizuri, ilikuona atadanganya vipi, wakati yeye anaumiza kichwa juu ya ilo, huku rafiki yake Mdee, alikuwa anachekea kwapani, na huku koo likimwasha akitamani kuusambaza umbea ule kwa mkewake, hivyo akaenda chooni na kujifungia kisha kupiga simu kwa mke wake, ili kumpa umbea, wafumanizi jepesi lililomkuta Johakim.*******
Wakati Johakim akiwa tumbo joto, huku nako Ratifah, ambae aliona kuwa mafanikio yanakaribia, kwamba Damian ametoroka, na ajulikani alipo, hivyo chumba kile kita kuwa cha kwake, na kumsaidia kuanza maisha mapya, huku akifurahia na mpenzi wake Johakim, mwanaume ambae kuwa nae nisawa na kutimiza moja ya ndoto yake kubwa sana, katika maisha yake, ndoto ambayo alikuwanayo toka utotoni, ni ndoto ya kuwa na mwanaume mwenye gari…
SEHEMU YA AROBAINI
ILIPOISHIA: Wakati Johakim akiwa tumbo joto, huku nako Ratifah, ambae aliona kuwa mafanikio yanakaribia, kwamba Damian ametoroka, na ajulikani alipo, hivyo chumba kile kita kuwa cha kwake, na kumsaidia kuanza maisha mapya, huku akifurahia na mpenzi wake Johakim, mwanaume ambae kuwa nae nisawa na kutimiza moja ya ndoto yake kubwa sana, katika maisha yake, ndoto ambayo alikuwanayo toka utotoni, ni ndoto ya kuwa na mwanaume mwenye gari…endelea..
Ratifah, siku zote alikuwa anawaza na kuvuta picha, ya siku ambayo ataingia pale kijijini kwao Mpitimbi, jinsi watu watakavyokuwa wanamtazama kwa macho ya staajabiko, na wengine wakimwonea wivu, na jinsi atakavyokuwa anawatazama kwa jicho la dharau, huku wakitumiliwa umbi na gari lao, yani lile vitz, ambalo mimi binafsi siwezi kulidharau, maana sina ata ata baskeri.
Kitendo cha kuto kupokea simu zake, kilimchanganya na kumkosesha raha, mpaka mke wamdee alipopigiwa simu na mume wake, nae kama alijuwa, maana alipokea na kutoka nayo nje, “vipi hupo nae karibu hapo?” aliuliza Mdee, mala baada ya mke wake kupokea simu, “nimetoka nje, vipi kuna jipya huko?” aliuliza mke wa Mdee, kwa sauti ya chini yenye shahuku kubwa, “mtu mfupi huku tumbo joto, amefumaniwa na boss akiwa hayupo, na sijuwi amemwambia nini, naona toka amejifungia ofisini atoki” alisema Mdee kwa sauti iliyojaa umbea na hukuda, “weeee! awato mfukuzakazi kweli, sasa itakuwaje kuhusu Ratifa masikini?” aliuliza mke wa Mdee, kwa haraka haraka ungesema anaona huruma juu ya Ratifah, lakini uwezi amini usowake ulikuwa umejawa na furaha kuu, “ata jijuwa kwani akujuwa kwamba anachokifanya ni ujinga, yeye sialiona raha kupapasa tumbo la huyu mjinga, mwache aijuwe dar” alisema Mdee huku anacheka kwa sauti ya chini, ilioyesha wazi alikuwa amejibanza sehemu akipiga simu, “basi huku mwenzio bidada anaangaika kumpigia simu, na ata zipokelewi, utazani anapiga kwa customer care” alisema mke wa Mdee, huku ana cheka kicheko cha chini, kama ambavyo mume wake anafanya.
Baada ya maongezi mawili matatu, wakaagana na kukata simu, kisha mke wa Mdee akarudi ndani, “kumbe unaangaika kupiga simu, wakati mwenzio yupo busy kama nini, maana mama yake amekuja pale dukani, kuna mzigo wanaipanga dukani” alisema mke wa Mdee, ambae sikuzote Ratifah, umchukulia kama rafiki, “kumbeeee, ndio maana basi apokei simu” alisema Ratifah, kwa sauti iliyotoka kwa shida kwenye mdomo uliovimba na kushondwa nyuzi tatu, kwenye lips ya juu, ya mwanadada huyu, ambae sizani kama atatazamika, maana akiwa ajapata ajari hii, alikuwa anatazamika kwa shida sasa unazani itakuwaje,
Masaa yalikumbia polisi wakiendelea kumsaka Damian, mala kijiweni mala nyumbani, lakini awakumwona Damian, ambae walipania kumshikisha adabu, endapo wata mkamata, lakini ilikuwa ni sawa na kuandaa ugari kwa samaki ambae bado ajavuliwa toka mtoni, maana awakumpata kabisaaa, mpaka mida ya saa moja za jioni alipopanga safari ya kwenda tena kijiweni, wakiongozana na Johakim.
Walifika pale kijiweni na jibu likawa lile lile, kuwa toka asubuhi, Damian ajaonekana pale kijiweni, “nasema hivi, nyie endeleeni kumficha tu, ila ikibainika kuwa nmajuwa sehemu alipo na mnamficha, mtajuwa kuwa udanganyifu ni kosa la jinai” alisema askari Warioba, kwa sauti yenye kujaa vitisho, huku Johakim aliekuwa ndani ya gari na Mdee, akiwatazama wale jamaa wakijiweni, yani wafanya biashara na madereva wa boda boda, kwa jicho la hasira.
Warioba alimfwata Johakim pale kwenye gari, nae akashusha kioo cha dereva, “Jo, nazani wewe mwenyewe umeona, huyu fala ata kuwa amesha kimbia mji, kama vipi wacha tufanye mambo mengine, ila kama ukimwona au kupata taarifa yoyote kuhusu yeye, tujulishe, maana sasa atutomfwatilia ata kidogo, hapo sasa kama yupo hapa mjini, lazima ata jitokeza, kwa kuona kuwa yamekwisha” alisema Warioba, na wakakubariana hivyo, kisha wakaagana na kuopndoka zao,
Wakati wakina Johakim wanaelekea nyumbani kwa kina Mdee, huku polisi wakielekea kituoni, “ujuwe nini Mdee, yule fala atakuwa amesha kimbia mji, kilichobakia nikumfungulia Ratifa lile geto, na mimi sito lazimika kwenda guest house, nitakuwa namalizia humo humo” alisema Johakim, kwa sauti yenye furaha, “hitakuwa poa sana, unajichukulia bia zako unajifungia ndani na mtoto” alisema Mdee, kwasauti kama ya kuunga mkono, japo licha ya kufurahi kilichomtokea Damian, lakini ukweli nikwamba Mdee akupenda jinsi wawili awa watakavyokuwa wakifaidi kutumia chumba cha Damian kufaidi kitumbua, siyo kwamba alionea huruma mari za mwanaume kutumiwa na mwanaume mwingine, ila aliona wivu, kwa jinsi wawili awa walivyo tumia njia za mkato, kujipatia chumba kilicho lipiwa miezi sita, na kina vitu ndani yake.
“sema sasa nini Mdee, yule fala alikuwa na faida zake, maana alikuwa ana nunua chakula, lakini hakuna ubaya, nitamnunulia kadiri navyoweza, maana boss nae machale kama vile yameanza kumcheza” alisema Johakim na hapo ndipo Mdee alipotapa nafasi ya kudodosa, “kwani alikuwa anaongea nini wakati anaondoka, maana saa zile nakupigia simu kukuambia kuwa boss anakuja, naona hupokei” alisema Mdee, akiwa mwenyewenia ya kusikia chochote toka kwa Johakim, ambae alifunguka mwanzo mwisho kilicho tokea kati yake na dada boss, “lakini anitishi, nita weka mambo sawa” alisema Johakim kwa sauti ya kujiamini.
Dakika kumi ndizo walizo tumia kufika nyumbani, na pasipo kujari macho ya watu waliokuwa wanamtazama, Johakim akafungua mlango wa chumba cha Damian, ungesema ndie mwenye chumba, kisha akaingia ndani na kuwasha taa, akatazama mazingira na kisha aka akanza kuweka sawa, huku Mdee nae akija kumsaidia, waliweka sawa mle chumbani, unge sema kuwa ni chumba chao, na baada ya kuona wamelizika, na kile walicho kifanya,
Ndipo wakarudi kwenye chumba cha Damian, na kutulia hapo huku wakipiga story mbili tatu, mgojwa akiagizwa chips, na wao wakila wali maharage, ata walipo maliza kula Johakim na Ratifa wakingia chumbani kwao, ambako Johakim akukaa sana, maana asingeweza kumfanya chochote Ratifah, kutokana na hali yake, hivyo aliondoka pale saa nne za usiku, akiwai nyumbani kwake, yani kwa mke wake na watoto wake, akimwacha Ratifah, alie amini kuwa Johakim anawai nyumbani kwa mama yake.
Siku ya pili Johakim akiwa amesha weka mambo sawa, alimsubiri boss wake aje wakague mahesabu, lakini mpaka saa nne za asubuhi akukuwa na dalili yoyote, hivyo akaamua kutulia kusikilizia, mpaka saa sita ikawa kimya, lakini mida hiyo akapokea simu toka kwa boss wake akimweleza kuwa leo asingekuja, na baada yake angekuja siku inayo fwata, maana alikuwa na mgeni nyumbani kwake, na hapo ndio Johakim alipoona kuwa hiyo ndiyo nafasi ya kwenda kumwona Ratifah, akujuwa kuwa yajayo yana furahisha.******
Naam upande wa wakina Kapate nako, bado walikuwa na sinto fahamu, kwa maana ya kwamba, siku ya tatu leo walikuwa bado awajamwona Damian, na wala simu yake ilikuwa aipatikani, hakika iliwachanganya kidogo, akukuwa na polisi wala mtu yoyote ambae alikuwa anamfwatilia Damian pale kituoni, ilionyesha wazi kuwa tayari Damian alikuwa ameshatiwa mbaloni, “jamani sasa hivi ni saa sita, bado ajarudi, sasa tunafanyaje?” aliuliza mama mmoja ambae uuza chakula pale kijiweni, hapa cha msingi twendeni polisi, wasije kumuuwa Damian” alisema Kapate, na wote wakaunga mkono, “nikweli jamani, twende kituoni, tusije kumpoteza kijana wetu” alisema boda boda, yule alie mpeleka Damian dukani. …
INAENDELEA…………….