KAMA INAUMA CHOMOA
ONYO: Wakubwa tu, kuanzia Miaka 18, ndio wasome hii Hadithi
SEHEMU YA THERASINI NA MOJA
ILIPOISHIA: Kama alifanikiwa kupata usingizi, basi ni masaa mawili au matatu, maana mpaka saa tisa alikuwa macho, ila saa kumi na mbili alikuwa amesha aamka, akamwamsha mke wake, ambae bado alikuwa amepotea kwenye usingizi mzito, “Ratifah!!! we Ratifah, ebu amka bwana uwai magari” alisema Damian kwa sauti iliyojaa hasira.. . . …endelea..
“niwai wapi bwana mwenzio nausingizi” alisema Ratifa huku anapapasa pembeni kutafuta shuka, hapo Damian akamzibua kofi la mgongoni, kwa nguvu sana, na kumfanya Ratifa akurupuke huku anapiga yowe la maumivu, “jamani Dami, nimekufanya nini?” aliuliza Ratifah, huku anajaribu kujikuna mgongoni, lakini mkono aukufikia, “beba kila kitu chako na uondoke, mimi nimeshindwa, yani mimi unaniambia mala hoooo! nimechoka, mala sijuwi tumbo linauma, alafu kumbe huko unatoa mpaka nyuma” alisema Damian kwa hasira.
Hapo Ratifa alitazama chini kwa aibu, akishindwa kusema chochote, nazani alikuwa anajiuliza Damiana amejuwaje, “nasema inuka uchukue vitu vyako uondoke, bwana” alisema Damian kwa hasira huku anamshika mkono Ratifah, na kumvuta atoke kitandani, “khaaa! niache bwana, naondoka mwenyewe, atakama nime fanywa nyuma simimi, tena kwa taarifa yako nimefaidi kweli kweli” alisema Ratifah, huku anajipapatua mkono wake toka kwa Damian, na kuanza kukusanya viatu vyake na vipodose toka mezani, kisha akaviweka kwenye shangazi kaja, na bila kupiga mswaki wala kunawa uso, akatoka nje, huku anaporomosha maneno ya hasira, “na utajuta kunifukuza mbwa wewe, kwa nyumbagani kama zizi la mbuzi, unajiita mwanaume kwa kipi ulicho nacho, au ulidudu lako, ata punda alo na analala zizini” alisema Ratifah, pasipo kujari watu waliojaa nje, ambao waliangua kicheko.
Damian, akujibu kitu zaidi ya kufunga mlango wake na kuanza kujiandaa kwenda gengeni kwake, wakati anajiandaa, akasikia vicheko na maneno ya kejeli, toka nje, “nilisema wataachana tu, hii ndiyo dar” huyo alikuwa ni mke wa Mdee, na wenzake wakacheka kishangingi, “mwenzio kazowea uwani wewe unaingia sebuleni, kwanini asitoke nje” alisema mwingine na kuendelea kucheka, lakini Damian akuwajari na kuendelea kujiandaa, ambapo alitumia kama dakika kumi tu, akatoka nje ambako aliwakuta baadhi ya wapangaji wenzake wakiwa wamekaa kwenye milango ya vyumba vyao, nikama walikuwa wanamsubiri, maana walimsindikiza kwa macho, na alipotoka kwa mita kama ishilini, aka sikia vicheko vya kishanganini toka kwa wale wanawake wapangaji wenzake, wakiongonzwa na mke wa Mdee.******
Damian alifika Gengeni kwake, na kumsimulia rafiki yake Kapate,ambae siku zote iwa anauzunihwa sana na hali inayomkuta rafiki yake, “kama ume mtimua umefanya jambo zuri sana, ujuwe mademu kama hao awafai kabisa, yani kuna wanawake na heshima zao wanatafuta waaume waaminifu wa kuishi nao, alafu yeye anakuchukulia poa” alisema Kapate, ambae akujuwa kama kuna jambo zito zaidi, linakuja kwa rafiki yake.
Maana wakati wanaendelea kuongea ili na lile, mala wakaoliona gari la polisi lina kuja na kusimama mbele ya genge la Damian, hapo Damian akujiuliza tena, akajuwa fika kuwa kinajirudia kile ambacho, kilimtokea miezi kadhaa iliyopita, siku ambayo alikamatwa na polisi kwa kosa la kumpiga Ratifah, “nimekwisha” alisema Damian kwa sauti ya cini iliyojaa unyonge, huku anatazama chini, akishindwa kuwatazama polisi wawili walioshuka kwenye gari na kumfwata kwa mwendo wa haraka, huku sura zao zikiwa zimejaa hasira, “Damian ndio nani kati yenu?” aliuliza mmoja kati ya wale polisi wawili, mala baada ya kufika pale walipokuwa wamesimama Damian na Kapete, ambae kiukweli alikuwa anatetemeka miguu yote miwili, huku jasho la unyayo likimchuruzika.
Damian, ambae akutaka kusumbua chombo cha dola, aka inua usowake kumtazama askari alie uliza, maana sauti yake aikuwa ngeni sana masikioni mwake, ni kutokana na rafudhi yake ya kikurya, alimkumbuka kwa haraka sana, kuwa ndie yule askari ambae sikiile alimzabua mtama wanguvu, “ni mimi hapa afande naomba msinipige, naenda mwenyewe kituoni” alisema Damian kwa sauti ya kunyenyekea iliyojaa uoga na kukubembeleza, huku anapiga magoti, na iganja vya mikono yake amevikusanya pamoja, mfano wa mtu anae sali, “mshenzi sana wewe, ebu inuka haraka, siunajiona unaweza kupigana siyo” kauri hiyo ya yule askari ilienda sambamba na teke moja la nguvu kifuani, teke ambalo lilimsukuma Damian na kuangukia mgongo. . . …
SEHEMU YA THERASINI NA MBILI
ILIPOISHIA: ni kutokana na rafudhi yake ya kikurya, alimkumbuka kwa haraka sana, kuwa ndie yule askari ambae sikiile alimzabua mtama wanguvu, “ni mimi hapa afande naomba msinipige, naenda mwenyewe kituoni” alisema Damian kwa sauti ya kunyenyekea iliyojaa uoga na kukubembeleza, huku anapiga magoti, na iganja vya mikono yake amevikusanya pamoja, mfano wa mtu anae sali, “mshenzi sana wewe, ebu inuka haraka, siunajiona unaweza kupigana siyo” kauri hiyo ya yule askari ilienda sambamba na teke moja la nguvu kifuani, teke ambalo lilimsukuma Damian na kuangukia mgongo. . . …endelea..
Hapo sasa, Kapate aliweza kushuhudia mwenzie anapkea kichapo cha nguvu, kabla yakunyakuliwa na kutupiwa kwenye gari, kama mwizi au mbakaji, kisha safari ya mbezi ikaanza, huku Kapate akiwasikiza kwa macho, mpaka walipo toweka kabisa, mbele ya upeo wa macho yake, huku madereva wa boda boda na wafanya biashara wenzao, wakiwa waaongealea tukio la kuchukuliwa kwa Damian, bila wao kufahamu sababu.
Hakika roho ilimuuma sana Kapate, ambae alitulia kwa masaa kwadhaa akifikilia maisha magumu ambayo anaishi mwenzie, “kwahiyo huyu mwanamke anapata wapi nguvu ya kumfanyia Damian namna hii?” alijiuliza Kapate, ambae baadae alishauriwa na wenzake aende kituo cha polisi kupata sababu za kukamatwa kwa mwenzao, mida ya saa sita za mchana Kapate alifunga banda la rafiki yake pamoja na banda lake, kisha akaelekea kituo cha polisi, akiongozana na wezake watatu, wawili wakiwa ni madereva wa boda na mmoja mfanya biashara mwenzake.
Naam kule kituo cha polisi, marafiki wale awakupewa nafasi ya kumwona Damian, zaidi walielezwa kosa la Damian, kuwa ni kumshambulia mwanamke na kumtukana hadharani, pia kumnyanyasa na kumfukuza nyumbani, kama kuna mtu aliudhunika juu ya jambo ilo, basi ni Kapate, alikuwa anafahamu sababu ya Damian kumpiga Ratifah, “afande samahani, lakini ata wewe lazima ungelazimika kufanya hivyo, kama mkeo angekufanyia kama alivyo fanyiwa Damian” alisema Kapate, huku akitumia sauti yake kunyesha jinsi anavyojisikia moyoni mwake, kwakile ambacho anafanyiwa Damian, “kijana ebu chunga kauri zako, unawezaje kumfananisha mke wangu na wanawake waajabu abu, ebu ondokeni kabla amja jiunga na mwenzenu huko ndani” aling’aka yue askari wa mapokezi akionesha kuchukizwa na kitendo cha Kapate kufananisha matendo ya Ratifa na mke wake, niwazi walikuwa wanafahamu Ratifa anacho kifanya kwa Damian.
Kusikia kuwa wanapelekwa mahabusu, kama mwenzao Damian, hivyo walielekea moja kwa moja mpaka makondeko, pale kijiweni kwao, na kuanza kujadiri juu ya swala lile, “imaana Kapate unafahamu sababu ya kukamatwa kwa Damian?” aliuliza mmoja kati wafanya biashara wenzake, na hapo Kapate akasimulia kama alivyo simuliwa na Damian, hakika ilimuumiza kila mtu pale walipo kuwepo.
“Kapate unasema anae mchukulia mke wake, ni yule jamaa wa pale DS anaetembelea kivitz?” aliuliza mmoja wa dereva wa boda boda, akionyesha kuwa na mashaka flani, “ndio ni yeye, jamaa nasikia mama yake anaela chafu, ndio zimpa kiburi na kuingilia ndoa ya watu, na kuonga mapolisi wamtese jamaa” alisema Kapate, ambae japo wenzake walioyesha kuumizwa na jambo lile, lakini yeye alionekana kuumia zaidi, “hapana bwana, mimi namfahamu sana Johakim, kuna siku nilimpelekea kidebe nyumbani kwake, lile duka siyo la kwake wala nini, tena amepanga Kimara anaishi kimara na mke wake, na anawatoto watatu” alisema yule boda boda, alitilia mashaka kuwa Johakim ni tajiri na mmilikiwa wa duka la DS BEAUTY POINT, lakini mbona Damian amesema kuwa, ni duka la yule jamaa, na kuna mpangaji mwenzao anafanyakazi kwenye duka lile” alisema Kapate, akionekana kuwa na uhakika na kile anacho kisema, “mimi nakuambia sasa, huyu Damian amedanganywa tu, Johakim pale ni msimamizi tu, tena yale maduka yapo mengi tu hapa Dar, lipo karia koo lipo mwenge, sinza, tegeta ata Masaki pia lipo, na sehemu zote hizo una wasimamizi wake” alisema yule dereva wa boda boda.
Naam hapo ukazuka mjadara mpya kabisa, “hivi kwanini Damian asiende kumweleza boss wa huyo pimbi, pengine inaweza kusaidia?” aliuliza mmoja kati yao, “kweli bwana ilo wazo zuri, nina mfahamu yule mama ni mtu mzuri sana, ata ukimkuta dukani anakuhudumia vizuri sana” alisema mwingine, na mmoja wao akadakia, “tena huyo Johakim mwenyewe anamwogopa sana, kuna siku nilimkuta pale sukani anamsema sana Johakim, kwaajili ya kutoa kauri mbaya kwa mteja, uwa ataki uonevu” kila mmoja alisema la kwake, huku mwingine akiongeazea “lakini akisha mweleza boss wake, na yeye aondoke kabisa huu mtaa, vinginevyo, anaweza kuja kumsumbua” alishauri mmoja wao, lakini mwingine akapingana nao, “hakuna aja ya kuondoka, unazani ayakuwa na uwezo wa kumsumbua tena , sababu atokuwa na uwezo wa kuonga polisi, maana naamini kabisa yule boss wake ata mfukuza kazi” hapo wote wakaunga mkono swala ilo, sasa swali likaja, Damiana atatokalini mahabusu, na atatokaje.*******
Wakati wao wanajiuliza juu ya swala ilo, huku kituo cha polisi, mambo yalikuwa ni mazito na yakuumiza kwa Damian, maana wakati ule alipoletwa kituo cha polisi, alipelekwa kwenye kijichumba flani kidogo, na kuanza kupewa kichapo kilichokosa mpangilio, yani kama angepigwa mtama wa nguvu na kuanguka sakafuni, basi linge fwatia teke la tumbo, na wakati anaugulia maumivu, basi angeshtuka ngumi ikitua shavuni, ile anapeleka kupooza ngumi ya shavu, angezinduliwa na kofi la uso, ambalo linge mletea nyota nyingi usoni wake, na kabla aja fahamu idadi na rangi ya nyota zile basi ange ongezewa teke lamgongo, hapo Damian angeachia kilio cha mnguvu, kama vile anakamuliwa jipu, au kufanyiwa operation bila ganzi, “mamaaa na kufaaaa, naomba mnisameeeeee sirudii tena kumpiga” alilia sana Damian, kiukweli ilitia huruma. . . . …
SEHEMU YA THERASINI NA TATU
ILIPOISHIA: yani kama angepigwa mtama wa nguvu na kuanguka sakafuni, basi linge fwatia teke la tumbo, na wakati anaugulia maumivu, basi angeshtuka ngumi ikitua shavuni, ile anapeleka kupooza ngumi ya shavu, angezinduliwa na kofi la uso, ambalo linge mletea nyota nyingi usoni wake, na kabla aja fahamu idadi na rangi ya nyota zile basi ange ongezewa teke lamgongo, hapo Damian angeachia kilio cha mnguvu, kama vile anakamuliwa jipu, au kufanyiwa operation bila ganzi, “mamaaa na kufaaaa, naomba mnisameeeeee sirudii tena kumpiga” alilia sana Damian, kiukweli ilitia huruma. . . . …endelea..
Hapo alipigwa kwa dakika kadhaa, kisha akapelekwa mahabusu, ambako alikaa, huku akiwaza na kutafakari juu ya yale yanayo mtokea, kwamba ni sababu ya nini, au ni lahana ya kutembea na mama Shukuru, huku akiwa ni mwanamke wa mzee Mhando, lakini hawara anaga lahana, sasa hii ni kwaajili ya nini.
Wakati na waza hayo na ajapata jibu, mala Damian akaja kuchukuliwa mida ya saa mbili za usiku, na kijana yule yule mpigaji, kuendelea kupata kichapo, pasipo kupata chakula chochote, ukweli leo Damian, alihisi kuwa ndio mwisho wa maisha yake, na kwamba anaenda poteza uhai, hakika alitia huruma.
Lakini uwezi amini, yani yule askari mpigaji aliendeleza kipigo kama kawaida, mpaka alipoingia askari mwingine mwenye nyota moja, “Warioba, acha kwanza ningee nae huyu mpuuzi” alisema yule askari mwenye nyota moja” na hapo ndio ikawa afadhari yake, na yule askari akamwachia Damian alie kuwamelala chini kwa kujikunyata anasikilizia maumivu.
Hapo yule askari mwenye nyota mmoja, akamsogelea Damian, na kuchuchumaa pale alipolala Damian, “dogo shida nini, kwanini unasumbua watu kwa vitu dogo?” aliuliza yule sakari kwa sauti tulivu na yaupole, hapo kiukweli Damian akujuwa ajibu nini, akaaki ametulia anasikilizia maumivu, “sikia kijana mimi nakushahuri kitu kimoja, ebu acha kushindana na watu wenye mji huu, sasa sisi tuna kuachia kwa mala ya mwisho, ukiletwa tena kwa kesi ya kumpiga, au kumfukuza mkeo, utakiona cha mtema kuni” alisema yule askari kisha akainuka, “Warioba mwachie aende zake, kama ajaelewa safari hii basi ili ni sikio la kufa” alisema yule polisi, huku anatoka zake nje ya chumba kile.
Naam Damian aliachia mida ya saa mbili, na kuelekea Makondeko, bahati nzuri kwake alikuwa na elfu mbili, hivyo alitumia usafiri wa piki piki, kufika nyumbani kwake, alikopanga, huku njiani akipanga kuto kubari huduma yoyote toka kwa Ratifa, endapo atafanya kama siku ile, na alipanga kuto kumsemesha kwa lolote.
Damian alifika nyumbani mida ya saa tatu, na kama alivyo tarajia, alimkuta Ratifa akiwa ndani, amejilaza kitandani, anaongea na simu, niwazi alikuwa anaongea na mpenzi wake, maana alikuwa anaongea kwa kujibebisha, Damian aliingia ndani na kuua nguo alizo kuwa amevaa akachukuwa maji na kwenda kuoga, huku Ratifa ambae akuonyesha kumjari, akiendelea kuongea na simu, “baby jamani fanya basi unipangie chumba, mwenzio siwezi tena kuishi hapa” moja baadhi ya neno aliloliongea Ratifa na kusikika masikioni kwa Damian, ambae aliombea jambo ilo litokee ata leo.
Baada ya kumaliza kuoga, Damian akavaa ngo zake vizuri, nakutoka nje akaenda madukani, ambako miaka ya nyuma alikuwa anapata chakula siku ambazo akuwa na mpango wa kupika, maana kulikuwa na mama ntilie kadhaa.
Licha ya kula mapema na kumaliza, Damian ambae chumba alichopanga mwenyewe alikiona kichungu, alikaa pale madukani, mpaka mida ya saa tano za usiku, kisha akaanza safari ya kurudi nyumbani kwake, ambako ni kama mita mia mbili hivi toka madukani, huku njiani akimpigia simu Kapate na kumjulisha kuwa amesha achiwa, toka kituo cha polisi, “dah! ungeniambia mapema kaka, lakini afadhari wamekuachia, chamsingi Ratifa umesha achana nae” alisema Kapate kwa sauti yenye kuchangamka, hapo kiukweli nafsi ilimsuta sana Damian, maana bado Ratifa alikuwa nyumbani kwake, “ndio hivyo kaka, ata mimi nashukuru sana kuachana na yule mwanamke” Damian alilazimika kudanganya, maana licha ya urafiki wake na Kapate, lakini awakuwa na utamaduni wa kutembeleana.
Naam huo ulikuwa ni ukurasa mpya na mfup wa maisha mapya ya Ratifa na Damian, waliishi chumba kimoja, kama kaka na dada, kwamaana ya kwamba akuna dudu hakuna kitumbua, kila mmoja na mambo yake japo kuna wakati, Ratifa alionekana kukosa fedha na kuamua kupika vyakula ambavyo Damian alikuwa ananunua kwaajili yake, na wakati alipoamua kuwa mkali juu ya vitu vyake, Ratifa ange mkumbusha jambo, “umesahau hen, kwahiyo unataka nikale wapi, wewe sindio umenileta huku dar” hapo Damian angekuwa mpole na kuendelea kutoa huduma.
Ratifa akuwajibika kwa lolote kama mke, ukiachilia kutokutoa unyumba, pia akujiangaisha ata kumfuria, hiyo kupika yenyewe ni siku ambazo, akuwa na fedha ya kutumia, japo walilala kitanda kimoja, lakini Ratifa aliweza kuongea na simu mbele ya Damian, huku akibembelezana na mpenzi wake huyo, kitu ambacho Damian kimfurahisha nikwamba, akuwa anaongea usiku, zaidi walikuwa wanachati tu, kwakutumiana sms, “hivi Ratifa tutaishi hivi mpaka lini, kama unapendana na huyo jamaa yako siuende ukaishi nae” alisema Damian, ambae sasa alianza kumchoka Ratifa ambae kuna wakati alikuwa anarudi usiku sana, tena akiwa amelewa chakari, na yeye kulazimika kumfungulia mlango muda wowote atakao rudi. . . …
SEHEMU YA THERASINI NA NNE
ILIPOISHIA: Ratifa akuwajibika kwa lolote kama mke, ukiachilia kutokutoa unyumba, pia akujiangaisha ata kumfuria, hiyo kupika yenyewe ni siku ambazo, akuwa na fedha ya kutumia, japo walilala kitanda kimoja, lakini Ratifa aliweza kuongea na simu mbele ya Damian, huku akibembelezana na mpenzi wake huyo, kitu ambacho Damian kimfurahisha nikwamba, akuwa anaongea usiku, zaidi walikuwa wanachati tu, kwakutumiana sms, “hivi Ratifa tutaishi hivi mpaka lini, kama unapendana na huyo jamaa yako siuende ukaishi nae” alisema Damian, ambae sasa alianza kumchoka Ratifa ambae kuna wakati alikuwa anarudi usiku sana, tena akiwa amelewa chakari, na yeye kulazimika kumfungulia mlango muda wowote atakao rudi. . . …endelea..
Hakika iliwashanga sana majilani, huku wakina Mdee wakiwa wanamcheka na kumsimanga Damian, “bwanaeee kwani mimi nikikaa hapa ninakukela nini, au ndio unaanza kunichokoza” aliuliza Ratifa kwa sauti iliyojaa ujeuri wa hali ya juu, “lakini Ratifa unazani mimi najisikiaje kuona mwanamke ambae nime mgharamia toka songea tena vijijini anakuja kufanya mambo kama aya?” alisema Damian, kwa sauti iliyojaa hasira, wakati wanaongea siku moja asubuhi, siku ambayo jana yake usiku Ratifah alirudi akiwa amelewa kabisa, na bahati nzuri siku hizi, Damian alikuwa ameshaacha ile tabia ya kumnyandua Ratifa akiwa aulevini, “sasa ndio nini, kwani lazima, au unataka nikurudishie nauri yako?” aliuliza Ratifa kwa sauti iliyo jaa dharau na kejeri, “Ratifa ujuwi mimi naumia kiasi gani unazani ningekufanyia wewe ungefurahi kweli?” aliuliza Damian ambae muda woye alikuwa anajizuwia asifanye jambo lolote ambalo linge mtia hatiani, “bwaneee usinipigie kelele, unavyo umia unavyo umia, kama inauma si uchomoe” alisema Ratifa huku anapiga hatua kutoka nje,
Ukweli sidhani kama Damian alifikilia mala mbili, au sijuwi kama alidhamilia kufanya vile, na kwamba ilitokea kwa bahari mbaya tu, maana lilimtoka teke moja zito sana ambalo lilitua mgongoni kwa Ratifa ambae alienda kujibamiza uso wake, kwenye kingo ya mlango, ambayo ilikita uswa wa mdomo, nakubomoa meno mawili, moja lajuu na moja la chini, hapo aka kurudishwa nyuma ambako alikutana na kofi la shavuni, alakini lililotokea nyuma. huku Ratifa mwenyewe akishindwa kupiga kelele ata moja, kutokana damu kujaa mdomoni, kofi lilimtupa Ratifa chini, ambapo alifwatiwa na ngumi nzuti ya usawa wapua, “bola polisi wakaniuwe, lakini nawewe ushike adabu yako” alisema Damian huku akiendelea kupeleka ngumi mfululizo zilizo tua usoni kwa Ratifa, ambae sasa alianza kutoa kilio kilichoenda sambamba na mtoko wa damu nyingi sana, mdomoni na puani.
Kilio kilikusanya watu wengi sana nje ya nyumba ile, lakini akuna ata moja alie jaribu kuingilia ugomvi ule, ambao uliendelea mpaka Damian alipoona kuwa imetosha, na kwamba kipigo alicho kitoa kinaweza kukufidia maumivu ambayo ataenda kuyapata huko kituo cha polisi, akamwacha Ratifah, na kuondoka zake, kuelekea kijiweni, ya ni kule Makondeko, akiacha watu wanamshangaa Ratifah, alie kuwa amepondeka zibaya sana, na wengine walidiriki kumzomea kabisa, “ulizania kuna mwanaume bwege moja kwa moja” huku wengine wakisema, “afadhari yule kaka amemtolea uvivu, yani alikuwa anatia kinyaa, sasa akadange vizuri” nikweli watu walionyesha kutopendezwa na tabia za Ratifah, na walilizika na kile kipigo alicho pewa yule mwanamke, yani Ratifah, ikiwa ni malipo ya matendo yake
Kati yao mke wa Mdee nae ambae alikuwa anachekea pembeni, yeye alichukuwa simu yake na kumpigia mume wake, simu ambayo bahati nzuri nikwamba simu ile aikuchelewa kupokelewa, “ndugu yangu tayari wamesha tifuana huku” alisema mke wa Mdee kwa sauti iliyojaa umbea na yshakunaku, “nani wakina Ratifah?” aliuliza Mdee nae kwa sauti ile ile iliyo jaa umbea, kama ya mke wake, nani mwingine, ni hao hao, yani Damian ame mpiga tarifah, sijuwi kama atatazamika tena, yani amembomoa uso wote” alisema mke wa Mdee kipashikuna, huku anamalizia kwa kicheko cha kimbea, “basi ngoja ni mwabie Johakim akamsweke ndani huyo mshenzi” alisema Mdee kwa shahuku kubwa, “tena mwambie afanye haraka, kabla Damian ajafikambali, ametoka anaelekea barabarani” alisema mke wa Mdee, kabla awajakata simu, kisha mke wa Mdee ndio akajifanya kwenda kumtazama Ratifah, ambae bado alikuwa ndani, akiendelea kuangua kilio na damu zime mjaa puani na mdomoni.*********
Damian baada ya kutoka nyumbani kwake, alitembea kwa haraka, na tahadhari kubwa, huku akiwa mwenye wasi wasi mwingi sana, Damian aliofia kukutana na polisi, ambao aliamini kuwa endapo wekimkamata leo hii, watammaliza kabisa kama siyo kumwacha na kilema cha maisha.
Lakini bahati nzuri alifika barabarani, na kukutana na rafiki yake Kapate, “kaka vipi, mbona kama una onekana una wasi wasi sana, kuna tatizo?” aliuliza Kapate, baada ya kuona hali ya rafiki yake Damian, Ukweli Damian alikuwa katika hali ya kuto kujuwa cha kusema, maana alisha wai kumdanganya kuwa Ratifah alisha ondoka nyumbani kwake.
Mwisho Kapate Damian akuwa na namna, zaidi ya kumweleza ukweli Kapate, alimweleza kuanzia alivyo ambiwa pale kituo cha polisi, nikwamba analazimika kuishi na Ratifah, pasipo kujari chochote anacho kifanya mwana mke huyo, Damiana akamsimulia kila kitu na maisha waliyokuwa wanaishi, baada ya kutoka kituo cha polisi, mauzi na machukizo yaliyo jaa dharau aliyo fanyiwa na Ratifah, kiasi cha kuamua kumpiga.
Habari hiyo ya kufurahisha na kushtua, ilimchanganya sana Kapate, “Damian, hapa hapakufai, polisi wataingia sasa hivi” alisema Kapate kwa sauti iliyojaa wasi wasi, “sasa niataenda wapi Kapate wacha wanikamate tu, unazani nitawezaje kuwakimbia polisi” alisema Damian, kwa sauti iliyopoa, yenye kila dalili za wazi za kukata tamaa, “hapana Damian, chukuwa funguo nenda getho kwangu” alisema Kapate huku ana mpatia funguo Damian, ambae aliupokea mala moja na kuanza safari ya kuelekea kibamba kwa mangi, ambako anaishi Kapate, alikuwa bado ajaowa.
Kumbe basi, mala baada ya Mdee kupigiwa simu na mke wake, na kumweleza kilicho tokea, Mdee aliekuwa ana hudumia wateja aliacha mala moja na kwenda ofisini kwa meneja, ambae alimkuta anajaribu kuweka sawa mahesabu za fedha alizo tumia kwa matumizi yake binafsi, katika njia hisyo halali, na ukizingatia kuwa, alitakiwa kufunga mahesabu ya week, “kaka yule jamaa kasha mpiga tena Ratifah” alisema Mdee kwa sauti iliyojaa umbea na uchochezi. . . …
SEHEMU YA THERASINI NA TANO
ILIPOISHIA: Kumbe basi, mala baada ya Mdee kupigiwa simu na mke wake, na kumweleza kilicho tokea, Mdee aliekuwa ana hudumia wateja aliacha mala moja na kwenda ofisini kwa meneja, ambae alimkuta anajaribu kuweka sawa mahesabu za fedha alizo tumia kwa matumizi yake binafsi, katika njia hisyo halali, na ukizingatia kuwa, alitakiwa kufunga mahesabu ya week, “kaka yule jamaa kasha mpiga tena Ratifah” alisema Mdee kwa sauti iliyojaa umbea na uchochezi. . . …endelea..
Hakika Johakim alishtuka sana, na kushikwa na hasira za ghafla, huyu mshenzi safari hii napotezea huko huko jela, bora akafungwe kabisa” alisema Johakim, huku anainuka toka kwenye kiti, “tena itakuwa poa sana, ukimfunga alafu Ratifah, anabakia pale ndani mwenyewe, anakuwa amekupunguzia kazi ya mkupania chumba” alisema Mdee, huku anamtazama Johakim, aliekuwa anajipekuwa mifukoni, kutafuta simu, ambayo ilikuwa imefunikwa na karatasi mezani, “we ngoja tu, kama siyo kumfunga, basi ata kimbia mwenyewe na kuachia kile chumba” alisema Johakim, ambae sasa aliamia kupekuwa mezani, na kuipata simu yake.
Naam mala baada ya kuipata simu yake, akabofya namba flani, na kuipiga, kisha akaiweka sikioni, huku anachukuwa funguo za gari, na kuanza kutoka nje, huku Mdee akimfwata nyuma, “hallow habari za siku kaka” aliongea Johakim, huku anatembea kwa haraka kutoka nje, akipitiliza sehemu ya duka kubwa, lilijaa wateja, na kutoka nje, huku akiendelea kuongea pasipo watu wengine kusikia pande wapili wasimu, “kaka mambo mabaya, nasikia jamaa amempiga tena yule demu….. ndiyo kaka, kama kawaida, ila safari hii, nataka tumalize kabisa swala hili…… nazani tukikutana tutaongea, mwambie Warioba anapajuwa nyumbani…. sawa watanikuta, mimi ndio naelekea huko huko” alisema Johakim, na maongezi yakaishia hapo, kwa maana ya kukata simu, huku anaingia kwenye gari, yani Toyota Vitz, akaliwasha na kuondoka kwa speed kuelekea upande wa kibamba.
Wakati huo Mdee akiwa amesimama kwenye mlango wa duka, anasindikiza gari kwa macho, mpaka lilipotokomea, ndipo alipo toa simu yake na kumpigia mke wake, ambae nikama alikuwa anaisubiri simu ile, maana aliipokea mala moja, “enhee niambie, vipi tayari umesha mwambia?” aliuliza mke wa Mdee kwa sauti iliyojaa shahuku, “unauliza kumwambia, nazani huko aliko anakaribia kufika sasa” alisema Mdee kwa sauti ya kipashikuna, akiongeza na chumvi, “yani anaendesha gari kama la zimamoto” hapo wote wakacheka, “basi tusubiri tuone mtiti” alisema mke wa Mdee, kabla awajakata simu.
Dakika chache baada ya Damian kuondoka pale kijiweni, mala Kapate akaliona gari la polisi lililokuwa lina ongozana na vitz nyeusi, yakieleke kule anakoishi Damian, hapo kapate akajuwa kuwa tayari mambo yameshaanza, na rafiki yake anaanza kusakamwa, hivyo Kapate akawaita wafanya biashara wenzake, pamoja nabaadhi ya madereva wa boda boda, nakuanza kuwasimulia, mkasa mzima unao muhusu Damian, na kilicho mtokea asubuhi ya siku ile, “nahivi tunavyoongea polisi wameshaenda nyumbani kwa Damian kumsaka” alisema Kapate, akiwa anamalizia kuwa simulia alicho kifanya Damian, “kwahiyo bado alikuwa anaishi nae, si alisema amesha mtimua?” aliuliza mmoja kati yao, kwasauti iliyojaa mshangao na sjaajabiko, “dah! ata mimi nilishangaa sana, ila ukweli ni kwamba, jamaa aliamua kuficha ukweli, ujuwe alilazimishwa kukaa nae, na siyo kama mke, ila ni kama kaka na dada” alisema Kapate, ambae alisimulia kila kitu kama kilivyo kuwa.
Naam wakati wanaendelea kusimuliana, ndipo walipoliona gari la polisi, likitoka kule liliko elekea, yani mtaani kwa kina Damian, “kazi hipo, kweli njaa mbaya, yani mtu awa jamaa wanaamua kuuza haki ya mtu kwa fedha” alisema mama mmoja, alie kuwa anafanya biashara ya kuuza viazi mvilingo, kwa sauti iliyojaa masikitiko makubwa sana, huku wanalitazama gari lile ambalo, lilinyoosha barabarani, kuelekea upande wa kibaha, nyuma yake wakionekana polisi kadhaa, waliosimama, pamoja na Ratifah, na mke wa Mdee, waliokuwa wamekaa.
Nawakati huo huo wakaliona gari lile Toyota Vitz, likielekea upande wa Mbezi, “jamani inabidi tufanye jambo kumsaidia Damian, aondokane na ilijambo” alishauri mmoja kati ya madereva wa boda boda, “hapa cha kumsaidia Damian, nikumshauri achague moja, kama siyo kukutana na boss wa Johakim, basi arudi kijijini kwao” alisema mwingine, “ilo nalo nijambo la msingi, kama vipi bora aendazake songea, vinginevyo watamuuwa” aliunga mkono mwingine, “lakini ata kama ataenda songea, lazima kwanza akamweleze boss wa yule mjinga, bila hivyo atazidi kuwaonea watu” alisema yule dereva waboda boda, na mwisho wakakubaliana hivyo.
Hapo wakamchangia dereva mmoja boda boda, ambae alikubari kwenda kumchukuwa Damian nyumbani kwa Kapate, kumchukuwa Damian, na kwenda nyumbani kwa Damian kuamisha vitu ya kijana wetu, ambae akutakiwa tena kurudi pale nyumbani kwake, lakini ile kijana wa boda boda anatoka tu, polisi nao wanaingia na gari lao, ambalo walilisimamisha pale na polisi wawili wakashuka, kama kawaida yao, moja kwa moja wakaenda kwenye banda la Damian, ambalo lipo karibu kabisa na banda la Kapate, “mwenye banda ili yupo wapi?” aliuliza askari, ambae week chache zilizopita wakina Kapate, walimshuhudia akimtembezea kichapo mwenzao Damian, “leo aja fungua kabisa” alijibu Kapate, huku anajifanya anapanga panga matunda kwenye meza kubwa ya pale bandani kwake, “una uhakika kuwa ajafungua kabisa leo?” aliuliza kwa sauti yakitisho askari Warioba, “ndiyo ajafungua siunaona bado pame fungwa” alisema Kapate, kwa kujiamini, huku akiendelea kujifanya yupo busy.
Hapo yule askari aka mtazama mwenzie na kumpa ishala ya kusogea pembeni, ambako waliongea mawili tatu, kisha Warioba akarudi pale kwenye banda la Kapate, “sasa nakuachia maagizo yake, ukimwona mwambie hivi, yani kwa usalama wake, aje mwenyewe ajisalimishe kituo cha polisi, cha mbezi kwa yusufu, kama tukitumia mafuta ya gari letu, nakumkamata, basi atalipia kuanzia mafuta, mpaka nguvu zetu” alisema kwa Jazba Warioba, “samahani kaka afande, kwani Damian amfanya kosa lolote?” aliuliza mmoja wawakina mama waofwanya biashara pale makondeko, ambae alikuwa anafahamu kisa chote, mwanzo mwisho. . . …
INAENDELEA………..