JINSI NILIVYO TOBOA MAISHA
Episode 12
Niliambiwa Amani yupo tayari ndani ya gari lake, nilimfuata
Niliingia kwenye gari baada ya kufunguliwa mlango, Amani alipunguza sauti ya mziki🎵
“Enhe umefikia wapi…” Aliniuliza kuhusu kazi aliyonipatia
“Nilikwambia nataka kuwa zaidi ya Mr’s Hudson…”
“Kwa kubuni nguo tu na kupika cake….Mr’s Hudson ana fahamu vitu vingi zaidi ya mia tatu usinitizame hivyo ukihisi pekee yako ndio una mfahamu 🥴… ana fundisha mambo mengi kuhusu ujasiliamali, kwa namna moja au nyingine namfahamu vizuri sana ✋….”
“Najua vitu vingi zaidi ya mia tatu…. siwezi kujionyesha kwa kila kitu pengine watu watahisi nimekuja kwenye hii nyumba kuwatawala…..Mrs Hudson hajui siasa hajui kamali…hajui kuchinja kuku….hajui kuendesha baiskeli…anajua kuimba lakini hajui kucheza…. ni fundi mzuri wa kuandika script lakini hajui kuigiza 🥴….” Niliongea kwa kujiamini
Amani aliachia tabasamu
“Acha ujinga wewe hapo hujui kuendesha gari….ndege huwezi….hujui kuongea lugha zingine tofauti na kiswahili pamoja na kisukuma….halafu kabila lako lina matusi…herufi za mwisho ni matusi” Amani aliongea akinipiga piga kichwani 😵
Nilikaa kimya ni kweli sikuwa nikijua vitu vyote alivyonitajia
“Baada ya harusi ya Dada Marie kuisha….nitakusaidia upo vizuri siyo kwamba na kusifia….kama ungekutana na Mimi mapema huenda ungekuwa na ndege sasa hivi ✋….” Amani aliongea kisha akaondoa gari
Nilianza kuyatafakari maneno yake…. alichukua earphone moja akanichomekea sikioni….kuna mziki mzuri ulikuwa unasikika ulihusu mapenzi sikujua kwanini kaniwekea mziki wa namna hiyo sikujali sana niliendelea kusikiliza
Tulifika nyumbani kwa Marie… nyumba yake ilikuwa ina fanana na nyumba ya Bibi
Amani alinifungulia mlango wa gari kama boss hivi 🤭
“Sijawa Mfanyakazi wako rasmi, nimekusaidia tu ni kijua hauwezi kufungua mlango 🥴…” Amani aliamua kunichana makavu
nilishuka kwenye gari….
Tuliongozana na Amani kuna Bibi alikuwa amekaa bustanini kalikuwa kamezeeka japo si sana
“Huyu ni Mama yake na Bibi…anampenda Marie ndio maana alishang’ang’ania huku” Amani aliongea
Japo Bibi alikuwa kazeeka lakini alionekana tajiri tu
nilimsalimia Bibi kwa kumshika miguu
“Amani hii mikono ina hela nyingi sana…..halafu ni mzuri unapaswa kumuoa 🥰”Bibi aliongea kwa kilugha
Nilishtuka ndani ya moyo lugha ya kina Amani huwa naisikia na kuielewa vizuri japo huwa sijionyeshi
Amani alicheka tu
“Tumekuja kwa Marie…endelea kuota jua”Amani aliongea
Bibi alivutiwa na bangili langu la mkononi alitaka nimuuzie 😄
“Hapana…Bibi chukua tu” Nilikataa hela
“Ah familia yetu huwa hatupendi vitu vya bure…..usiwe una kataa pesa ukienda kwa sonara utanunua lingine…” Bibi aliongea
Niliichukua hela
tuliingia mpaka sebuleni kwa Marie
Amani alinirekebishia nywele zangu kisha akatupisha tuzungumze.
Mapigo ya moyo wangu yalivurugika kisa nimetengenezewa nywele tu 😩
Itaendelea 💥
Episode 13
“Wewe na Amani mnaonekana ni watani wazuri 🤭” Marie aliongea
Kuna namna nilijisikia aibu ndani ya moyo wangu 😌
Sikutaka kusikia aibu zaidi niliingiza maada za harusi
Tulianza kuongea mambo mengi yanayohusu harusi…Marie alipendezwa na ubunifu wangu niliokuwa namuelekeza
“Nimefurahi hakika…. umemuona Bibi yetu mkubwa ” Marie aliniuliza
Nilitikisa kichwa kuashiria ndiyo 🤗
“Sasa yule mngekaa wote mngepatana anapenda mambo ya ubunifu…..hivi vitambaa vyote kashona yeye” Marie aliongea
Nilivitazama vitambaa vilivyowekwa sebuleni kwa sekunde kadhaa
“Hakika ni fundi….hata muonekano wake tu si wa Nchi hii, niliongea ukweli na si kwamba nilikuwa nasifia ✋”
“Kwa kuwa tushaelewana basi tuishie hapa kuna vitu naenda kufanya na Mume wangu mtarajiwa, please Scola usiniangushe ujue Mimi na marafiki wengi ila siwaelewi ni kama hawanipi support kutoka moyoni…halafu na Mimi huwa ni mbinafsi nikiona kama una kuwa mzito kutoa support huwa narudi hatua kumi nyuma…muulize Amani 🙂 hivyo nategemea msaada wako zaidi “Marie aliongea
“Usijali nitafanya kwa uhakika…”
Tuliagana na Marie…Amani alikuwa nje na Bibi mkubwa baada ya kuniona alinikaribia
“Mmeshaelewana…”
“Ndiyo…”
“Bado mapema sana…kuna vitu nataka ukaviangalie Michael anajua kwenda na muda atakupigia simu muda si mrefu…tuondoke”Amani aliongea
Sikuweza kuongea sana zaidi ya kumfuata
tulienda mpaka kwenye maduka makubwa ya vitambaa 😜
“Kuna mzigo nilimuagiza Johnson jana nilimuambia atauacha hapa…” Amani aliongea na muuzaji
“Yeah mzigo upo, ngoja nikutolee hata hivyo nilitaka nikupigie simu boss” Muuzaji aliongea, alikuwa na lugha za kujipendekeza huyu 🤭…Sijui alienda wapi lakini alirudi na boksi kubwa sana hakubeba pekee yake alisaidiana na watu wawili
“Mzigo ndio huu hapa…halafu Johnson alisema hii ngoma ni adimu sana kama asingefika jana nahisi mpaka week ijayo ndio angefanikisha…” Muuzaji aliongea
“Siyo mbaya Johnson anakuwaga makini sana namfahamu….” Amani aliongea huku akaniangalia Mie huyu badala ya muuzaji 😌
Niligeukia pembeni sikuona sababu ya yeye kuniangalia mbele za watu
mzigo uliwekwa kwenye gari kisha tukapanda
“Nilikuagizia vitambaa India…ni vitambaa adimu nitafurahi kama na wewe utajishonea ki nguo kimoja…si unaviona” Amani aliongea akinionesha kwenye simu yake 😋
“Ni vizuri… ahsante”
“Hatuendi nyumbani Bibi nimeblock kwa muda huwa ana tabia ya kunisumbua sana anapenda tutazamane tu kama taa za barabarani….” Amani aliongea 😄
“Umemblock kwanini… hutaki akujulie hali..”
“Yule tunajuana…halafu siku hizi umeanza kunizoea unaongea tu hata sijakuruhusu haya bwana” Amani aliongea utafikiri namuonea kutokana na swali nililomuuliza 🤭
Niligeukia pembeni nikacheka
Amani alianza kuendesha gari….tulifika mpaka kwenye eneo moja lililokuwa tupu…
tulishuka kwenye gari.
Amani alivaa miwani sababu ya upepo mwenzangu na Mimi nilipambana na vimchanga vilivyokuwa vinaingia machoni 😄
“Msingi wa maisha yako utaanzia hapa endapo utakuwa serious…”
“Una maana gani…”
“Katika eneo hili tupu tulilosimana tutajenga kampuni kwa ajili yako… kumfikia Mrs Hudson inahitaji akili na nguvu….” Amani aliongea
Mie huyu niliishia kumtazama tu kwa kitu kizuri alichoniambia 🥺
Episode 14
Upepo ulizidi kuvuma kiasi kwamba nikawa sioni vizuri, tobaaaa 😵 Amani alinikumbatia tena akanificha kabisa uso nisipatwe na upepo
“Kuwa mwalimu inahitaji moyo….nahitaji uwe mwepesi na mwelewa…..hapa kuna upepo kwa sababu kuna ziwa jirani….nimetoa hela nyingi kupata hiki kiwanja kwa sababu ni eneo zuri….” Amani alizidi kuongea ….naelewa basi maneno yake nilikuwa bize na tetemeka mwili mzima 🤭
“Okay… tuondoke”Amani alisema akanitoa kifuani kwake
Nilikuwa sijielewi miguu nahisi ilifungwa na kamba ya miujiza
nikiwa bado na babaika babaika…Amani alinipiga denda uwiii yaani nilihisi kuumwa akili 😜 huyu kanileta kunionesha uwanja au kunipiga denda 🤭
“Sa…sa…samahani…… nakupenda najua nimekushtukiza lakini sina namna nyingine ya kueleza hisia zangu….wewe si msichana wa hadhi yangu lakini najikuta navutiwa na wewe…Scola nakupenda 😘” Amani alinitambia akiwa kanishika mabega, vile ni mrefu sasa nilijikuta nikipata tabu kumuangalia
“Ngoja nijifikirie nitakujibu” niliongea kwa sauti ya kukwama kwama utafikiri nimevuta kemikali 😄
Amani alinipiga denda tena mpaka nikawa nachoka….lilikuwa ni busu zuri balaa hapa boyfriend wangu wa form iv Samuel Malomo nakuchana makavu ulikuwa unanipaka mate samahani lakini kwa kukutaja lakini ✋
Amani aliniachia
“Okay nasubiria jibu lako Mimi sina haraka ..”Amani aliongea
tuliingia kwenye gari tukaanza safari ya kurudi kwa Bibi
Baada ya kufika nilisingizia tumbo linauma….Bibi alinipatia dawa kisha akaniruhusu nilale
nilijitupa kitandani nikiwa siamini kama nimetamkiwa maneno kama yale na Amani 🙄
Nilijifikiria mengi pengine niliwaza labda Mama yangu Bi Moza alikunywa maji ya mti wa mpendwa pendwa….hapana! nafsi nyingine ili niambia na uzuri una changia lakini nafsi nyingine iliniambia ubunifu wangu ndio umemteka Amani
nilianza kubishana na kichwa changu mwenyewe…. ka usingizi kalinipitia kabisa
nilikuja kushtuka giza likiwa limeshaanza kuingia…niliingia bafuni ni kaoga baada ya kumaliza nilitoka nje nikiwa na hofu ya kukutana na Amani 😩
“Tumbo bado linakuuma” Bibi aliuliza baada ya kuniona
“Hapana….”
“kidogo nishangae kwa hiyo dawa niliyokupa lazima tu lingeachia….mlielewana na Marie”
“Ndiyo Bibi kila kitu kilienda sawa…”
“Mpelekee Amani hii karatasi yuko huko bustanini…tutaonana kesho nataka nijiandae niende kwa Marie nitalala huko huko” Bibi aliongea akikusanya magazeti yake ✋
“Haya utawasalimia” Nilimjibu Bibi kisha nikachukua karatasi
nilifika bustanini, Amani alikuwa anaongea na simu
nilimpatia karatasi kisha nikasubiri niruhusiwe kuondoka 🥺
“Tumbo bado linakuuma…” Amani aliniuliza baada ya kumaliza kuongea na simu
“Hapana…”
“Hapa nje kuna baridi au ni Mimi tu” Amani aliniuliza
“Kuna baridi si unaona hata Jet alivyojikunyata” Niliongea
Amani aliniangalia machoni mpaka nikapoteza ujasiri wa kumtazama
“Twende ndani kuna baridi hapa” Amani aliongea kisha akamchukua Jet
tuliongozana hadi ndani
Hatukukomea sebuleni tulienda chumbani kwa Amani
“Jet nenda kwa Dada Toshi akupe chakula… tumbo limepotea” Amani aliongea
Jet aliondoka yaani watu wa hapa wote anatujua majina
“Unajua Jet aliletwa na Mama yangu kutoka China…tunampenda ana akili sana kama angekuwa darasani angekuwa anapasua kinoma” Amani aliongea 😄
Sikujua hata nimjibu nini, alisimama akanikalisha kitandani
“Bado hujamaliza kufikiria….”
“Ulisema hauna haraka bado sijaanza kufikiria… nikimaliza kushona nguo za Michael nitaanza kufikiria” Nilimjibu Amani
“Alright ni wewe tu….”
“Naweza kwenda” Nilimuuliza
“Sijisikii vizuri naomba nilale kifudi fudi halafu ulale juu yangu….haufanyi bure nitakulipa” Amani aliongea
Nilishtuka sana 😳….kazi gani hiyo napewa eti alale kifudi fudi halafu Mimi nilale mgongoni kwake
“Kama hutaki usijilazimishe unaweza kwenda…” Aliongea kwa kununa 😄
“Lala nitafanya hivyo,” Sikutaka iwe shida
Amani bila kuniuliza mara mbili alilala kifudi fudi kisha nikalala juu yake nilichukua blanket tukajifunika
nilikuwa napiga dua Amani asije kujigeuza ikawa hatari 😩..pengine nilihisi anatumia njia hiyo ili nitoe jibu kwa haraka
“Ulisema unajua vitu vingi….. nisimulie hadithi ambayo inaisha vibaya…”
“vibaya? kwanini…”
“Nataka nione nitajisikiaje baada ya hadithi kuisha vibaya…..”
“Sitakubembeleza baada ya hadithi kuisha vibaya nina uhakika utalia kwa sababu nitakusimulia hadithi inayoumiza….ni hadithi ambayo hujawahi kuisikia wala kufikiria” Niliongea kwa kujinadi 👌
“Usinitishe nisimulie…..”
Nilianza kumsimulia Amani badala ya kulia yeye nilianza kulia Mimi
Amani alinizuia baada ya kuona nateseka 😄…..kama nilivyotarajia tu Amani aligeuka chali
nilihisi vitu vimegusana tu
“Naomba ukibakiza nguo moja unijibu Mimi siyo jiwe lisilo na hisia hivyo jitahidi kushona kwa haraka ✋…..”Amani aliongea kwa sauti tofauti na niliyoizoea
“Sawa nitajitahidi kukujibu pindi nitakapo bakiza nguo moja”
“Sawa toka juu yangu…..nenda kalale chumbani kwako”
kusikia hivi nilitoka haraka
Amani alinivuta
“Hakika wewe ni mbinafsi….najuta kukufahamu….sijui hata kwanini nipo hapa muda kama huu ningekuwa ofisini…..sababu yako kila siku nimekuwa najiongezea likizo ….” Amani aliongea akanifanya nishangae eti anaendelea kujiongezea likizo kisa Mimi 😧
“Kwani nikikujibu kitu gani utafanya” Nilimuuliza baada ya kuona anaongea kwa sauti ya chini kuliko kawaida
“Naomba ulale hapa sitakufanya chochote……. swali lako la ajabu ndio maana ulipata zero” Amani aliongea kisha akatoka juu yangu aligeukia upande mwingine tayari kwa kulala……Mimi pia nilala niligeukia mgongoni kwa Amani
nilianza kuwaza vitu ambavyo Amani angeingia kichwani mwangu angekula tunda bila kipangamizi 😄
Hii akili niliitoa wapi sijui nilisogea mpaka mgongoni kwa Amani sikuona sababu ya kumsubirisha ikiwa sina sababu inayonifanya nifanye hivyo
niliamua kumjibu kwa ubunifu……nilianza kumchokoza kwa kutumia ulimi alitulia kama hayupo
Sitaki kusema sana lakini kwa kifupi usiku ulikuwa mrefu kwetu….👌👌👌👌
Episode 15
Kulivyo pambazuka nilishtuliwa na mguso wa Jet..Amani alikuwa busy anajichana nywele
“Mtoe Jet nje nataka kuvaa” Niliongea
“Ni mdogo huyu ndio kwanza ana miaka 4 unene wake usikutishe” Amani aliongea 😄
“Amani…. hebu mtoe bwana unataka na yeye aone uchi wangu ulivyo” Niliongea kwa sauti kubwa 😁
Jet wa watu alijiongeza akaenda nje…nilianza kuvaa ila nilihisi uchi wangu unawaka moto
“Amani mambo mengine siyo vita…hakika umenikomoa” sikusita kumwambia Amani….ngoja nikwambie yaani kuna vitu vikishafanyika aibu na wasiwasi kama teja aliyepishana na polisi huwa vinaisha
Amani aliligundua hilo alinitizama tu kisha akacheka 😄 alifahamu fika kwa sasa simuogopi tena
“Nguo za Michael katengeneze nishaongea naye….halafu kuanzia leo usifanye kazi za humu ndani pengine kama umetaka”
“Kwanini….”
“Unastahili….halafu usiwe unaniuliza kwanini… uumh tafuta nguo nzuri kama hauna sema nikupe hela ukanunue jioni tutatoka…” Amani aliongea kisha akaondoka ✋
Nilibaki kuganda kama simu inavyokuwaga katika maisha yangu yote sikuwahi kutoka out
sikuhitaji kujiuliza sana nilienda chumbani kwangu nikiwa nafungua mlango Dada Toshi aliniona huyu Dada ana umbeya wa asili alinifuata, kwanza alininyanganya funguo
“Hauna nguvu yoyote ngoja nikusaidie kufungua…. nimekupikia supu” Toshi alijiongelesha
“Supu ya nini kwani naumwa…”
“Jana Amani alisahau kitabu chake sebuleni ile nakileta chumbani kwake nilikusikia tu unatubu dhambi zako zote kuhusu kumugawia Samuel tunda kumbe fundi mahiri yupo kajificha kwa Bibi…hahahaaa mtoto una mambo wewe…” Dada Toshi aliongea huku akicheka 😄
“Wewe Dada Toshi….” Niliita kwa aibu 😔
“Nini…si nilikwambia Mimi ni Mmbeya wa kuzaliwa….nilikaa pale nijue kama ana kubaka au ni kwa hiari yako….nilivyosikia Amani chukua yote ni mali yako niliondoka haraka sana…. mpaka hapo unacha kuniambia bi Dada 👌”
Nilibaki kucheka tu nilikubali aniletee supu kwani nilikuwa nahisi njaa
“Amani ni mzuri…ana pesa nyingi… kasoma….Scola ulipata zero halafu hata usomaji wako na mashaka nao…..ngoja nikuambie yule demu wa Amani anaonekana alikuwa mbovu hadi kitandani….sasa nakwambiaje mpe vurugu za uhakika Amani….halafu una kipaji kizuri sana kikazanie….watu wa hapa wanapenda watu watafutaji ✋” Toshi alinipa mbinu ya kivita
Nilikuwa na msikiliza huku nikikata vitambaa
baada ya kuona tumeelewana alinifatia supu
“Bila kunielewa supu niliyopika nisingekupa….” Toshi aliongea kisha akaondoka
Nilipata nguvu baada ya kunywa supu nilianza kushona nguo za Michael kwa haraka zaidi kama mnavyojua kitu ukiwa una utaalamu nacho huwa ni rahisi kufanyika
kuna muda nilikuwa na kumbuka vita aliyonionesha Amani usiku nilijikuta nikimkumbuka bure.
Bibi alikuja kunigongea nilienda kumfungulia huku nikiwa na aibu kubwa usoni 😌
Episode 16
“Unajituma wewe, umebakiza nguo ngapi…” Bibi aliuliza
“kama sita hivi…”
“Aah utamalizia hata kesho huyu Michael asikupande kichwani….njoo chumbani kwangu tusaidiane kitu kimoja”
Bibi aliongea
Nilimfuata chumbani kwake…. tulianza kukunja mashuka….Bibi ana mashuka mengi kuliko maelezo ✋
Tulikunja yote mpaka tukamaliza….kuna picha ilikuwa imedondoka chini nilimuokotea Bibi
“Mtazame Amani alivyokuwa na mwaka mmoja…” Bibi aliongea akinirudishia picha
Tobaa!! nilijikuta nikicheka Amani alikuwa kifutu kama mtoto wa kiboko 😄
“Bibi mbona alikuwa mnene hivyo…” Niliuliza huku nikicheka
“Alikuwa habebeki huyo…unajua niliogopa sana tulijua atapatwa na tatizo la moyo lakini wapi….”Bibi aliongea
Nilikuwa sina mbavu Mimi…. nilirudi chumbani nikaendelea kushona lakini picha ya Amani ilinimaliza nguvu kila nilipo kumbuka 🤣
Amani alikuja kunigongea ile namuona tu nilimcheka kwanza mpaka akataka kuondoka… nilimkumbatia kwa nyuma… ngoja tuwekane sawa hapa kwanza, najua kubembeleza balaa siyo sifa ni ukweli ✋
“Unaenda wapi badala ya kunipa pole…mikono inauma please” Niliongea kwa kudeka
Wanaume ni dhaifu tu kama alivyo mbwa mbele ya mfupa….Amani alinigeukia
“Hebu nione….”Amani aliongea akinikagua mikono…alianza kuibusu busu vile mwenyewe nikafurahi
“Polee….ulikuwa unachekea nini..” Amani aliuliza 🙄
“Hapana, kuna vitu nimekumbuka tu….ushakula” nilimuuliza Amani sikutaka anune
“Yeah nimekula hotelini…..nimerudi sababu ya Bibi pia nimekumbuka nilisema tutatoka out….na ndio maana nimerudi… halafu wewe mjinga harusi ya Dada Marie kesho kutwa…mbona hausemi vitu gani unataka…. pia kwanini haulizi kuhusu pesa kama Michael kanipa au la”Amani Aliuza 🥴
“Nakuamini….kuhusu vitu vya harusi vilivyopo vinatosha….sina mbwembwe nyingi ✋”
Amani alinisogeza karibu akanipa deep kiss…nilijikuta nikihisi burudani tu Mwanaume mzuri…msafi ana nukia perfume… yaani Mimi huwa na kuwa kichaa kwa mwanaume anayenukia perfume…. aliniachia kisha akaondoka hakuwa na cha kuongea… nilibaki kusimama tu
Baada ya wenge kuisha nilifungua kabati langu nilichagua nguo moja ambayo nilikubali na kuiheshimu….sijui nisemeje ni ile nguo ambayo ukivaa lazima watu wote wageuke….niliitizama kisha nikaikumbatia 😄
Jioni ilifika Amani aliniijia vile alikuwa amependeza acha tu alijipulizia marashi ya kunikomoa…hakusita kunisifia kama nimependeza…hatari! tulipita sebuleni Bibi na Mkoloni walikuwa wanaongea nilitaka kurudi Amani alinirudisha mpaka nikahisi aibu 😔
“Bibi….natoka mara moja na Scola” Amani aliongea utafikiri sifa
Bibi aliitikia tu kwa kichwa
“Muage Bibi…” Amani alinifundisha
“Bibi….baadae” nilizungumza kwa kutitia kama barabara linavyo kandamizwa na Lori lililo sheheni mikungu ya ndizi kutoka Bukoba 😄
Bibi aliitikia kwa kichwa
tulitoka nje na Amani sikusita kumpiga ngumi nzito ya mgongoni
“Kwanini hukusema kama Bibi yuko hapo unajua kiasi gani naogopa”
“Shida iko wapi kwani….anyway isiwe shida hofu yako naielewa….Bibi mbona anajua kuhusu sisi au ulitaka mpaka aitishe kikao cha dharula ndio uelewe kama anajua 🥴..” Amani aliongea
Nilichoka kumbe Bibi huwa ananichora tu kama katuni ya Bwakila 😩
Tuliingia kwenye gari,
Amani hakutaka kuniongelesha alifahamu fika bado na presha,
tuliongozana mpaka kwenye hotel moja hivi…kuna mkaka jina lake aliitwa Oscar alitupungia mkono….tulisogea mpaka sehemu aliyokuwa amekaa nasi tulikaa
kwa mwonekano tu alionekana ni Mbunifu…alikuwa kaweka hereni sikioni
“Oscar…. huyu anaitwa Scola…shemeji yako huyu” Amani alitambulisha 👌
Oscar alinibusu mkononi
“hellow cute…. naitwa Oscar rafiki yake Amani nimefurahi kukuona….. wewe ni mrembo sana macho yakomazuri….ngozi yako laini kama ya mende….siyo mfupi siyo mrefu….nimempenda” Oscar alimwaga sifa 😁
Nilibaki kuduwaa ngozi ya mende tena 😄
Inaendelea……………