JINSI NILIVYO TOBOA MAISHA
Episode 01
Naulizaje, ulishawahi kujihisi takataka baada tu ya kukosa kitu fulani 🙄 au ulishawahi kudharauliwa mpaka na mifugo ya nyumbani kwenu…yaani kama ni kuku au bata wakawa wanafanya mapenzi mbele yako 😏 na hata ukiwafukuza hawashtuki mpaka unaamua kuwapisha wewe?…..ngoja nikusimulie kidogo kuhusu Mimi my wangu
Baada ya kumaliza elimu ya kidato cha nne matokeo yangu hayakuwa mazuri, tena nahisi najipendelea nikisema hayakuwa mazuri….Mimi Scola nilipata sifuri siyo kwamba ni sifa kusema hivi hapana ni hali halisi si unajua tena nilizoea kufahulu mitihani yangu kwa chabo lakini mtihani wa mwisho wa kidato cha nne wasimamizi walikaza mbaya mbovu sikuweza hata kugeuza shingo yangu 🤭
Scola mie nilianza kuuona ugumu wa maisha…nikienda kisimani nilisemwa, nikienda dukani kwa Mangi nilisemwa, nikienda sehemu yoyote ili nilinyooshewa vidole aisee 😣 labda ni kwa sababu baba yangu Mzee Mpemba ni mcheza kamali maarufu au ni sababu Kaka yangu Mimi ni Mwanajeshi, huenda pia ni kwa sababu Baba yangu mie alikuwa anatamba mtaa mzima lazima nitakiwasha pindi matokeo yatakapotoka 😂
Marafiki zangu niliokuwa nasoma nao walipasua kiukweli, yaani kama ni kukiwasha basi vitu viliteketea.
Kama unavyojua maisha ya kijijini, mtu akitaka kwenda shule iliyo mbali na kijiji chake basi ni lazima sherehe kubwa itafanyika.
Sherehe ya kuwaaga marafiki zangu iliandaliwa….Mama yangu Bi Moza alichaguliwa kuwa mpishi Mkuu…. sijui walijifikiria nini…lakini taarifa hizo Mama alifikishiwa 😔
“Unajisikiaje kwenda kupikia watoto wa Mashujaa wakati wa kwako yupo anatapa tapa kama mlevi aliyefumaniwa akiiba pombe….” Baba aliongea huku akionesha makasiriko waziwazi 😫
“Kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake…” Mama alijibu kwa ufupi sana, imagine Baba kaongea maneno mengi ila yeye aliishia kuongea hivi
Baba alikasirika kujibiwa hivi yaani tangu Kaka awe mwanajeshi basi Baba yangu pia alishakuwa na pigo kama za Wajeda, alipiga teke bakuli la mboga likienda kule 🥺
“Mama yako ni fundi sana wa methali kwanini hizo methali asinge kufundisha ukajibia kwenye mtihani” Alifoka akitaka kunikanyaga na teke
Mama aliingilia kati… Baba alibaki kuongea tu…Kaka yangu alishaga mzuia kumpiga mama…vile baba anampenda Kaka basi alitulia….isitoshe baba yake mama ni Mwanajeshi mstaafu aliyekuwa na nyota kumi kwenye mkanda wake hivyo kuna namna huwa anaishi kwa uoga 😁
“Scola nenda ukalale kufeli shule siyo ugonjwa wala kilema….hawa wana nzengo wameamua kunidhihaki…nitaenda kuwapikia” Mama akiwa anaumia
niliamua kwenda kulala nikawaacha wakitupiana lawama 😔
Usiku nikiwa nimelala akili yangu iliwaza mbali sana
“Kwanini nisiondoke nyumbani… na kaa hapa kama nani? kila siku watu wamekuwa wakinitazama kama mfiwa au shujaa la mapenzi ya jinsia moja. Hapana ngoja niwapishe kidogo kwanza” Nilijiwazia kichwani mwangu 😣
Baada ya kufikia muafaka na kichwa changu sikulala…nilianza kupanga vitu vyangu ambavyo niliona vinafaa.
Nililala kwa tahadhari kubwa kwa sababu gari la kwanza kijijini kwetu huwa linaondoka saa 12 sikutaka nipitwe na gari hilo ✋
Sikuwa na hofu kuhusu Baba kumsumbua Mama kisa Mie kutoroka,
Asubuhi na mapema baada ya kusikia majogoo yakiwika nilitoka nje kama naenda kisimani kutafuta maji 🧐
Kwa wakati huu sikutaka kufikiria maisha ya wazazi wangu nilijifikiria Mimi…. baada ya kuingia kwenye gari nilitoa nauli.
Sikuwa na sehemu ya kwenda nilichojua Mimi ni kufika mjini tu
tulitumia masaa 3 mpaka tulipo tokelezea kwenye barabara ya lami Kijijini kwetu tunaitaga mtelezo 😂 baada tu ya kuona lami niliomba kushushwa nilibeba kibegi changu mgongoni, niliamua kuchekecha akili kwa wepesi zaidi
“Kwanini nisitafute kazi za ndani….” nilijiwazia huku nikitazama hadhi ya nyumba za watu
Kuna nyumba ilikuwa imekaa kama hotel hata sikuiogopa niliamua kwenda kugonga geti….niligonga mpaka mikono ikaauma 😬
“Bonyeza hiyo button getini vinginevyo utagonga mpaka moto uwake” Mpita njia mwenye huruma aliongea
Ndipo niliiona button nyeusi niliibonyeza kwa nguvu mpaka ikawa kama inalegea.
Mlinzi alikuja kufungua akiwa amekunja sura ☹
“Hujui kusoma….pale pameandikwa ubonyeze mara moja….sasa imekuwa kelele….mpaka mbwa wa Boss kaamka…utambembeleza mpaka alale ndipo nakusikiliza shida yako” Mlinzi alifoka
Kweli alikuwa hatanii alinikabidhi mbwa aliyejaa manyoya mwili mzima nikaanza kumbembeleza alale…mbwa alianza kubweka wakati alikuwa ametulia
Mlinzi alinisogelea akanikagua mikono 😫
“Mikono migumu kiasi hiki unafikiri atapata usingizi…. hebu sema shida yako ni nini..”
“Natafuta kazi za ndani….”
“Simama hapa hapa nije…..” Mlinzi aliongea kisha akaondoka na Mbwa yaani jinsi yule mbwa anavyo bembelezwa nilijikuta nikicheka 😂
Episode 02
Baada ya kukaa kama dakika saba hivi alikuja Bibi mmoja wa kishua hivi 😍
“Jet( mbwa) mpaka sasa hivi hajalala….”Bibi aliuliza kwa mshangao
Mlinzi alishindwa ajitetee vipi, aliishia kunitazama kwa jicho kali kinouma 😫
“Hakikisha analala Amani amekaribia kurudi” Bibi aliongea, inaonekana huyo Amani aliyetajwa ndio mmiliki wa huyu Mbwa
Nlijiongeza nikamsogelea baada ya kugundua Mlinzi hawezi kunisemea shida yangu tena 😔
Nilimsalimia kisha nikamweleza shida yangu
“Katoe copy cheti chako cha form four…” Bibi aliongea huku akinisotea sehemu machine ilipo
macho yalinitoka 🙄 mie huyu natoa wapi hicho cheti na hata kama ningekuwa nacho nisingeweza kutoa copy kwa kutumia mashine
“Cheti cha form four sina…” Niliongea
“Basi toa hata cha form six kwa muonekano wako tu bado hujafika chuo…nimekuwa Mwalimu wa chuo kwa miaka 20 sasa” Bibi huyu alinichanganya kabisa 🥵
”Hata cheti cha form six sina…” Niliongea
Bibi alinitizama vizuri
“Kwa kuwa umekuja kuomba kazi hapa sitakufukuza kwa sababu hauna vyeti….mwili wako unaonekana kuwa na nguvu….karibu”Bibi aliongea kisha akaongoza njia nilimfuata kwa nyuma 😉
Nyumba ya huyu bibi ilikuwa ni kama Ikulu fulani hivi
alinizungusha nyumba yote mpaka ulimi ukawa una bembea 😪
“Mimi ni mzee lakini naweza kuzunguka hii chumba mara kumi bila kuchoka…” Bibi baada ya kuniona nimechoka.
Nimezoea kutembea kwenye sakafu ya cement na si hizi tiles za kishua 🧐
Alibonyeza alarm watumishi wengine kama 20 hivi walikuja mbio
“Huyu ni mgeni….unaitwa nani…” Bibi aliniuliza
“Naitwa Scola…”
watumishi wote walicheka nilibaki kuduwaa kwanini wamecheka hasa baada ya kuzungumza jina langu 🥺
“Kuna paka alikuwa anapenda kuja hapa….pamoja na nyumba hii kuwa na ulinzi mkubwa na geti refu lakini aliingia tu….kuna mjukuu wangu anaitwa Amani sasa hivi yupo Ghana… alimbatiza paka huyo jina la Scola ndio maana wenzako wamecheka” Bibi aliongea huku akicheka pia 😄
Sikuwa na namna zaidi ya kujifanya nimeelewa ila sikupendezwa yaani jina langu nililopewa na bibi yangu ndio jina la paka hakika hii ni dharau kubwa kuliko hata ile ya mifugo wa nyumbani kwetu ☹
Bibi alitoa amri nipatiwe sehemu ya kulala
“Usisahau kumpa kitabu cha kanuni na sheria za hapa” Bibi aliongea kisha akaondoka.
Mfanyakazi mmoja alinichukua akanipeleka chumbani kisha akanipatia kitabu kikubwa kuliko hata dictionary ya Oxford 🥵
“Soma hiki kitabu chote mpaka ukimalize….kama unahitaji kudumu hapa zingatia yote yaliyo andikwa humo ✋” Nilipatiwa maagizo kisha akaondoka
Kwa nilivyokuwa nimechoka baada ya kuzungushwa nyumba nzima na Bibi wa Kishua nilikujikuta nikitamani kulala 😴
Sikuwa na muda wa kuanza kushangaa shangaa mazingira ya hiki chumba…. nilijitupa kitandani nikaanza kusinzia kwa kuibia…. sikuwa na tofauti na ule msemo usemao bandu bandu humaliza gogo😄 mwisho kabisa nilijiachia kabisa.
Sikumbuki ilikuaje….mpaka nilipokuja kushtuliwa na hodi mlangoni…..nilijua huo ndio mwisho wangu wa kuwa hapa kwa sababu kitabu cha sheria na kanuni sikuwa nimekifunua hata kidogo 😣
Nilienda kufungua mlango
“Toka nje kuna kikao cha dharula….”Niliambiwa
Sikuwa na muda wa kufikiria zaidi ya kutoka.
Nilimkuta Bibi akiwa kachachamaa
“Wafanyakazi wote hawa hamjui kupika cake?….cake gani hii mmetengeneza……Amani ndio atakuja kukata cake ya hivi I can’t believe my eyes……wote kuanzia sasa hamna kazi” Bibi kwa kumaanisha ✋
Nilishindwa kuamini ina maana hata na Mimi niliyefika leo nimeunganishwa kwa hawa wa zamani au ndio ule msemo samaki mmoja akioza wote wameaoza 🙄
“Bibi…nitarudia kutengeneza cake upya..” nilisema kwa sauti…kila mmoja alinigeukia kwa macho ya mshangao
Episode 03
“Una uhakika unaweza kutengeneza cake nzuri kuliko hii….” Bibi aliuliza huku akiichambua chambua na kidole 🤩
“Ndiyo naweza…” Nilijibu kwa kujiamini ingawa nilikulia kijijini lakini nafahamu vitu vingi sana hasa vya jikoni, kipindi nasoma sikuwa nikihudhuria darasani mara kwa mara, badala yake nilikaa nyumbani kwa kina Sara (rafiki yangu) kutazama TV 🙈…nilijifunza vitu vingi sana….ndoto yangu Mimi nikuwa Mbunifu kama Mr’s Hudson…. huyu Dada anakaa California kwangu namuona kama mfano wa kuigwa basi tu sijapata hii nafasi ya kuonesha uwezo wangu ✋
Baada ya Bibi kuona nimejibu kwa kujiamini hakuwa na shaka…alitoa amri kwa Wafanyakazi wengine waniletee vitendea kazi, nilikuwa kama boss hivi nikisema leta kile na kile waliondoka kwa kukimbia. Hatma yao na yangu ilitegemea keki ninayotaka kuitengeneza 😉
Nilianza kufanya yangu, kila niliponyanyua kichwa nilikutana na macho ya Wafanyakazi wote wakinitazama kwa huruma sana 😒
“Acheni kumtazama kwa huruma badala yake pigeni dua katika nafsi zenu….endapo akiharibu wote hapa hamtakuwa na kazi hata yeye tu hatakuwa na kazi bila kujali amekuja leo, sitaki kujua kina nani au nani alipika ile keki….sheria namba 5 inasema samaki mmoja akioza wote wameoza ☹….” Bibi aliongea, mie huyu nilishtuka baada ya kuisikia sheria namba tano, sikuwa nimeisoma hata kidogo
Bibi aliondoka kwa jazba, niliendelea kutengeneza keki huku nikiya tafakari maisha ya sehemu hii, ilikuwa ni zaidi ya Ikulu
Baada ya dakika 30 kupita, keki ilikuwa imekamilika….siyo kwamba najisifia hapana cake niliipamba kwa rangi adimu
Wafanyakazi wote walinisifia kazi ilibaki kwa Bibi 😫
Bibi alienda kugongewa chumbani kwake, alikuja akiwa kashika kitabu cheusi
baada ya kuiona keki aliachia tabasamu 😊
“Umeitengeneza hii cake vizuri sana 🎂….hata Mr’s Hudson hajakufikia hapa”
Nilishangaa kiasi kumbe hata Bibi anamfahamu Mr’s Hudson 😲
“Scola kawaokoa….hiki kitabu cheusi kilikuja kuwasomea makosa yenu kisha niwafukuze 🧐” Bibi aliongea
Nilishangaa kwa mara nyingine… yaani kwenye hii nyumba kuna hadi kusomeana hukumu ukifanya kosa, hakika kuna watu wanaendesha maisha yao kama wapo sayari ya saba hivi 🤥
“Naomba cake ihifadhiwe sehemu nzuri…..Amani kanipigia simu yupo airport…naomba Wafanyakazi sita wajiandae wakampokee, wengine endeleeni kurekebisha mazingira…..Scola Moyo wangu unaniambia haujasoma kitabu cha sheria na kanuni za hapa……ratiba zingine zikiwa zinaendelea naomba ukasome hicho kitabu…..” Bibi aliongea kisha akaondoka 😫
Sikuwa na namna zaidi ya kusoma kitabu nilicho kifananisha na ukubwa wa dictionary ya Oxford
nilijitahidi kukariri yote yaliyokuwa yameandikwa…nikiwa naendelea kusoma nilisikia makelele mengi kwa umbeya niliyokuwa nao sikutakwa kupitwa nilitoka kwa kunyata 👣
Ndipo nilipomuona kijana mtanashati akiwa kazungukwa na wafanyakazi utafikiri Mwana wa Mfalme….moja kwa moja nilifahamu huyo ndio Amani tuliyekuwa tuna mtengenezea cake kwa presha 😄
Baada ya kujiridhisha nilirudi chumbani kwangu niliendelea kusoma kitabu.
Mlango wangu uligongwa aliingia Mfanyakazi….kwa umri wake nilipaswa kumuita Dada
“Scola naomba unisaidie kitu kimoja…..Amani kaniagiza nimunyoshee shati yake bahati mbaya nimeuunguza….kwa kuwa wewe ni mgeni ni rahisi kusamehewa….tafadhali sana kama nikifukuzwa kazi hapa mtoto wangu atateseka, Baba yake alishanitelekezea majukumu”Dada Toshi huku akilia 😭
Nilijisikia vibaya sana ina maana kwenye hii nyumba hakuna bahati mbaya nilijikuta nikipata hasira hata kitabu nilikitupa kule 🧐
“Usijali Dada Toshi nitabeba hili jukumu hata kama nikifukuzwa hapa nitapata kazi sehemu nyingine” Nilivimba eti 🤩
Dada Toshi hakuamini kama nimekubali kubeba hili jukumu…tukiwa tunatazamana kengele ya dharula iligongwa
“Twende tuna hitajika” Toshi aliongea
Nilimfuata kwa nyuma,
tulifika sebuleni tukamkuta Amani akiwa kashikilia shati
“Nani kafanya hii kazi ya kuniunguzia shati langu” Amani aliuliza kwa sauti iliyotulia lakini nzito hivi. Kwa kifupi ilikuwa inashawishi kuendelea kusikiliza 😍
Aisee niliishiwa pozi, kisehemu kilichokuwa kimepatwa hitilafu ni kidogo sana kiasi kwamba ni mpaka mtu akukague kwa umakini ndio atagundua pameungua.
Nilijitokeza mbele nikiwa nimetazama chini Amani ni mrefu sikutaka anitie kizungu zungu mwenzenu mie ni mfupi ✋
Amani alinitupia shati lake
“Nimelinunua kwa gharama kubwa hata nikikupatia pesa uzunguke Nchi nzima huwezi pata shati kama hili…..hebu ondokeni 🧐” Amani alifoka kisha akasepa
Tulibakia kutazamana kwa jinsi Mjukuu wa Bibi alivyoondoka kwa ghadhabu 😫
“Wewe ndio ulikuwa unanyoosha hili shati kwanini unambebesha mzigo Scola” Mfanyakazi wa kiume aliuliza kwa sauti ya juu kidogo. Kama hili jambo litasikika basi italeta shida ilinilazimu kuingilia kati
Itaendelea 💥
Episode 04
“Tayari nimeshabeba hili jukumu huna haja ya kukasirika ✋” Nilifunga mjadala
Ilitulazimu kutawanyika kwa sababu tuliambiwa.
Nilienda chumbani kwangu nikiwa na shati la Amani….nilifikiria kwa haraka nikapata jibu kuhusu kitu gani nilitendee 😊
Nilifungua begi langu nikachukua sindano ya mkono pamoja na uzi mweusi….kwa sababu shati hili lilikuwa na rangi nyeupe niliamua kulidizaini kwa akili zaidi
Baada ya kumaliza nililitazama kwa uhakika zaidi…shati lilikuwa linavutia….nililinyoosha upya kisha nikampelekea Amani
nilitembea nikiwa na sali maana watoto wa matajiri mara nyingi wanakuwaga na visirani tu hata ukiwatendea wema 😪
Kwa kuwa nilikuwa mgeni hapa nilijikuta nikipoteza mwelekeo….pamoja na Bibi kunitembeza nyumba nzima kichwa changu kilikuwa na shida ya kushika vitu kwa haraka, pengine ndio maana nilipata sifuri kwenye matokeo ya kidato cha nne ✋
Nilibaki kusimama… mara nilihisi kama natekenywa miguuni, ile kutizama alikuwa ni Jet mbwa wa Amani anayelelewa kwa kubembelezwa kama mtoto wa Beyonce….sikumjali sana
baada ya kuona sina mazoea naye aliondoka…nilimchungulia sehemu anayoenda nilimuona akiganda kwenye mlango 😲
Niligundua pale ndipo kilipo chumba cha Amani….nilisogea pia nikasubiri mlango ufunguliwe
kama sekunde kupita Amani alifungua mlango
Jet aliingia ndani
“Shati lako nimelifanyia marekebisho” Niliongea nikiwa nimeinamisha kichwa utadhani namsujudia Mfalme Juha 🙈
Amani alilipokea shati, alilikunjua zilimchukua dakika 4 kulikagua…
“Umefanya wewe au umepeleka huko nje”
“Nimefanya mwenyewe…”
“Umedizaini vizuri….. haya ondoka” Amani kisha akafunga mlango.
Nilikasirika pamoja na kumrekebishia shati lake analodai halipatikani Nchi nzima kashindwa kusema hata ahsante
niliondoka nikiwa nimenuna kwa kiasi kikubwa 😬
Nilifika sebuleni nikakuta meza imechafuliwa bila shaka kuna wageni walikuwa wanakuja
Bibi baada ya kuniona aliniita
“Kidogo wewe unaonekana makini….kuna wageni wanakuja hapa…utashirikiana na Toshi kusikiliza wanachokitaka…nenda ukaoge haraka mje kukaa hapo” alisema Bibi
Nilifata utaratibu wa Bibi nilienda kuoga….baada ya kumaliza Mimi na Dada Toshi tulisimama kama minara ya Vodacom 😁
Wageni walifika…..Amani na Bibi waliwapokea, kwa jinsi walivyovaa walionekana ni zaidi ya mboga saba
walimpongeza Amani kwa kuhitimu Masters…..
tulianza kutekeleza kile walichokuwa wanataka.
Jet alikuwa kajilaza kwenye kochi kwa kuzubaa
“Scola hebu mchezeshe Jet huko nje tangu asubuhi hayupo sawa au Amani mmegombana na Jet” Bibi aliuliza 😄
Amani alijitia hasikii
nilimchukua Jet nikaenda naye nje….nilianza kumzungusha zungusha kidogo alianza kuchangamka
Nilijikuta nikichoka zaidi maana Jet alikuwa hachoki alichotaka yeye ni kukimbia kimbia tu,
yaani kama Mzee Mpemba angetokea akaniona kazi nayoifanya nahisi angenipasua ubongo kwa maneno yake
niliacha kumcheza Jet nilikaa kwenye nyasi….mazingira ya hapa yanavutia kweli 😉
Jet aliniletea kadi ya harusi sijui aliitoa wapi
Niliipitia ndipo nikagundua wageni waliokuja ni Bibi na Bwana harusi watarajiwa
kuna kitu kiliniijia kichwani
“Kwanini usiombe nafasi ya kumtengenezea gauni la harusi Bibi harusi”
Baada ya kupata wazo hili niliamua kumcheza Jet mpaka akapata usingizi nilimbeba kwa heshima kama mtoto wa Mfalme….nilifanya yote haya ili kumfurahisha Bibi 🤥
Baada ya kumuingiza ndani Jet…Amani aliniambia nikamlaze chumbani kwake
nilitamani kucheka Jet anaheshimika kwenye hii nyumba acha tu
Niliingia chumbani kwa Amani nikamuweka Jet
Nilianza kukishangaa chumba cha Amani….. bila kujishtukia nilinogewa….nilisogea kwenye kioo kujiangalia nilivyopendeza kwa muda mfupi niliokaa kwa Bibi.
Mawazo yalinizidia kabisa nilikuja kushtulia na Amani
“kitu gani unafanya…”
Episode 05
“Aam..aah….najua kutengeneza gauni la harusi kama kuna watu wana hitaji tafadhali nijulishe…” niliongea bila kufikiria bila kusahau kujichekesha hasa nilipoona Amani kanikazia macho😁
Sijui alinionaje alinicheka kisha akanigonga gonga kichwani na ufunguo
“Nenda Bibi anakuita….” Amani aliongea kisha akajitupa kitandani
nilitoka nje nikiwa sielewi kitu gani kimemfanya Amani acheke….pengine ni kwa sababu Mimi ni mfupi au naonekana mdogo…mpuuzi huyu sikutaka kumjali na hata nilijilaani kwanini nimemuomba connection 😬
Nilienda mpaka sebuleni alipo Bibi…wageni walikuwa wameshaondoka
“Scola nataka unisaidie kuangalia magauni mazuri ya harusi nadhani umemuona binti yangu…anaolewa wiki ijayo” Bibi aliongea… yaani sijui tu ilikuaje ila Bibi alitokea kunipenda tu hata tukifanya makosa madogo amekuwa akisamehe tofauti na zamani 😍
Niliyatazama magauni yote sikuyapenda….nilikuwa na dizaini yangu mpya kabisa ambayo sijawahi ona imetengenezwa….sikutaka kuficha ninacho kijua nilimtazama Bibi kwa uso wa kujiamini 🌝
“Bibi najua kutengeneza nguo za harusi nipe nafasi nimtengenezee binti yako…”
Bibi siyo kama Amani ukiongea kitu huwa hapingi 👏
“Kweli unaweza kutengeneza…”
“Ndiyo…..”
“Njoo chumbani kwangu nina kitambaa kizuri kabisa kinafaa kutengenezea gauni la harusi…”
Tuliongozana na Bibi mpaka chumbani kwake.
Chumba cha bibi kilikuwa kizuri….
Mshamba mie, nilijikuta nikiishangaa picha ya bibi akiwa binti bado
“Bibi ulikuwa mrembo sana 😍…” Nilimwaga sifa
“Mimi ni mrembo haswaa….yaani mjukuu wangu Amani alinifanana Mimi ndio maana nampenda”
“Hakika…. “
Bibi alifungua kabati akatoa bonge la kitambaa kiasi kwamba nilimeza mate…kilikuwa ni kitambaa kizuri sana
“Hiki kitambaa adimu sana ndio maana nilikuwa sijakivuruga…..nitakuagizia cherehani ya kisasa….kuhusu mapambo ya kuongezea kwenye hiki kitambaa Amani atakupeleka ukachague….Scola sina wasiwasi na wewe moyo wangu haugopi kabisa 😘.” Bibi aliongea huku akikunjua kitambaa.
Nilifurahi kusikia Bibi hana mashaka na Mimi
Amani na Mimi tuliongozana kwenye maduka makubwa yanayouza mapambo ya maharusi
nilianza kuchagua kwa uhakika sikutaka kufanya makosa….baada ya kumaliza kuchagua Amani alilipia aliniomba tuingie supermarket kuna vitu anahitaji kuchukua 🙄
“Hayo mapambo yaache ndani ya gari hakuna mtu anaweza kuiba” Amani aliongea baada ya kuona nina mashaka
Kwa kuwa kasema sikutaka kupinga, niliviacha vitu ndani ya gari
Tuliingia supermarket, sikuwa na kisabengo cha kuchagua kwa sababu sikuwa na hela 🤗
Amani alianza kuchagua vitu ambavyo siku vielewa baada ya kuona na zubaa zubaa aliniambia na Mimi nichague vitu nilivyovipenda
nilijikuta nikiogopa….
“Sipendi kuongozana na watu ambao hawajui matumizi ya pesa….Bibi alivyonambia nitakupeleka ukachague mapambo ya harusi nilitenga bajeti ya wawili…..hebu acha kunikera chagua vitu mpaka nitakapo kuambia vimetosha… ” Amani aliongea 😲
Niliona isiwe kesi nilianza kuchagua bites nyingi nyingi.
Amani alinifuata
“Vitu gani hivi una chagua…..kaa pembeni ni chague Mimi” Alisukuma kidogo
Alianza kunichagulia vitu vikubwa vikubwa nguo….viatu….marashi ya kila rangi…huyu mkaka alikuwa na sifa mpaka nguo za ndani alininunulia…viatu alichukua bila kujali vinanitosha au la lengo lake lilikuwa ni kutumia pesa tu aliyoiandaa 😄
Baada ya kumaliza tulibebewa vitu vikawekwa kwenye gari
“Sijakununulia vitu hivi bure….lile shati ulilidizaini vizuri kila mtu alilipenda so nimefanya kurudisha shukurani 😉…”
“Ahsante….”
“Haya endesha gari….ni muda wa Mimi kupumzika” Amani alitoa amri 😫
Niliona kama ana nitukana tofauti na kulipanda gari sijui hata jinsi linavyo washwa
“Sijui kuendesha gari….”
Amani alishangaa
“Wafanyakazi wote wa nyumbani kabla hawaja ruhusiwa kufanya kazi pale sharti la kwanza ni lazima wajue kuendesha gari….wewe.. uliajiriwa kwa kupendelewa au🙄….” Amani aliuliza
Sikuwa na majibu…nilijikuta nikipata hasira toka asubuhi hajafanya kazi yoyote lakini hata kuendesha gari anaona kazi
“Tutakaa hapa mpaka utakapojua kuendesha gari…” Alivimba
“Kwani kuanzia asubuhi umefanya kazi gani? ” Nilijikuta nikimuuliza
Amani alinitazama tu bila kuongea
“Ukiendesha gari sasa hivi unapungukiwa nini….” Nilizidi kuuliza
Amani alishuka kwenye gari akanitolea vitu vyangu vyote
“Tafuta namna ya kufika nyumbani…. next time usiwe unaniuliza maswali badala ya kutekeleza…” Amani aliongea kisha akawasha gari kama utani vile aliondoka 😪😪😪😪
Episode 06
Sikuwa na namna nilikusanya vitu kisha nikabeba kichwani vingine nilibeba mkononi….nilitembea kwa haraka zaidi si unajua tena nimezoea kubeba zigo la kuni kichwani hivi vitu havikunipa tabu ✋
Nilifika nyumbani kwa Bibi nikabonyeza button ya getini Mlinzi alikuja kunifungulia…..niliingia ndani nikihisi maumivu ya shingo, huu mzigo niliuchukulia poa lakini ulinipa tabu 😣
Bibi alikuja kuangalia mapambo niliyo chagua hakuuliza hata kwanini nimekuja nimebeba vitu kichwani badala ya kusaidiwa na gari 🌝
baada ya kujiridhisha na mapambo alinionesha cherehani ilipo….nilikuwa na hasira sana hata vitu alivyoninunulia Amani sikuwa na shida navyo tena nilivikusanya nikavifungia kwenye kabati 😬
Akili yangu iliwaza kutengeneza gauni la harusi
nilijifungia ndani nikaanza kushona kwa kukadria umbo la mtoto wa Bibi….sikutaka kula mpaka nimalize kulitengeneza,
sikujua kwanini lakini nilikuwa na shona huku machozi yananitoka
“Watoto wa matajiri wana roho za ajabu sana….hawajui pesa zina tafutwaje ndio maana jeuri haiwaishi usoni mwao” Niliongea pekee yangu nikimlenga Amani 🧐
Nikiwa bado najilalamikia, mlango wangu uligongwa…. nilienda kufungua, nilishtuka baada ya kumuona Amani.
“Nifuate…” Amani alitoa amri utadhani ni Mwalimu wa zamu
Nilimfuata kwa nyuma….tulifika mpaka chumbani kwakeb🙄
“Kuna kikaratasi cha rangi ya bluu sikioni naomba unisaidie kukitafuta….ni cha dizaini hii” Amani aliongea kwa kunioneshea mfano wa karatasi anayoitaka
Sikujua ananifikiriaje au kwa kuwa Mimi ni mdogo kati ya wafanyakazi wote.
sikutaka kufikiria sana nilianza kutafuta kikaratasi nilichoambiwa…..nilitumia kama dakika 10 mwisho nilikiona nilimpatia….nilitaka kuondoka lakini alinizuia 🤗.alitoa nguo zote kabati zima
“Kanifulie hizi nguo….” Amri ilitolewa
Safari hii nilifika ukomo wa uvumilivu kam ile text ya Vodacom kuwa umefikia kikomo cha kifurushi cha internet
nilimtazama Amani bila kukwepesha macho 🧐
“Watoto wa matajiri hamjui kama kuna kuchoka kwa sababu kazi zote mnafanyiwa…..nimechoka….hapa ndani kuna Wafanyajazi wengine wapatie hii kazi wafanye…..usinichukulie kama punda Mimi pia nachoka ✋” Nilimwambia Amani nikidondosha machozi hasira niliyokuwa nayo ilikuwa haipimiki
“Haya ondoka….” Amani aliongea kwa ufupi
Nilitaka kuondoka lakini alikuwa kaegemea mlangoni
“Naomba nipite….”
“Nimekwambia uondoke unaniomba nini tena…”
Nilishindwa kumuelewa Amani yaani kaegemea mlangoni halafu anasema niondoke
nilibaki kusimama na yeye hakutoka mlangoni tulikuwa tunatazamana tu hakuna aliyepepesa macho yake….🧐
Mwisho alitoka mlangoni alinifungulia bila kuongea kitu…..na Mimi sikujisikia kuongea kitu niliondoka nilienda kuendelea kushona gauni la mtoto wa Bibi 🤥
Baada ya kumaliza gauni nilimpelekea Bibi
“Scola hakika umetengeneza gauni zuri Mr’s Hudson haoni ndani…..Marie atafurahi kuliona” Bibi akiligeuza geuza
aliniomba nimsogezee simu yake….. baada ya kumpatia alimpigia simu Marie
Nikiwa nimesimama, Amani alikuja sebuleni akakaa karibu na Bibi
“Nini tena mbona kama umezubaa…” Bibi alimjali
“Huoni kama mkono unaniuma….”Aman aliongea kwa kujidekeza sijui alikuwa ananitishia anajua yeye
Bibi alimkagua mkono Amani 😄
“Scola hebu nenda chumbani kwangu kuna dawa ya kuchua uniletee…” Bibi aliniagiza
nilienda kwa haraka…..baada ya kuipata dawa nilirudi sebuleni
“Mpakae kwenye huo mkono” Bibi aliongea akili yake yote ilikuwa kwenye gauni
nilianza kumhudumia Amani…….niligundua Amani ananiangalia ngoja niwaambie kitu siyo kwamba najisifia Mimi ni mzuri…..ingawa naonekana mdogo lakini uzuri wangu haujifichi 😄
Baada ya kumaliza kumpaka dawa Amani nilienda kufungua mlango…. alikuwa ni Marie mtoto wa Bibi
“Mama hili gauni umelinunulia wapi…” Marie kwa mshangao 🙄
“Scola kashona….yaani leo kajua kunifurahisha….Amani ona nguo alishona Scola” Bibi aliongea,
Marie alinikumbatia kisha akanivuta vuta mashavu kama mdori hivi 🤩
“Umefanya kazi nzuri…..nikupe kiasi gani cha pesa…” Aliuliza Marie
”Hapana Dada nimeshona kwa ajili yako sihitaji pesa”
“Scola usije kurudia kusema hivyo….umetumia nguvu na akili….duniani hakuna kitu cha bure….Marie hebu vaa hilo gauni nikupige picha kisha nimtumie Michael atuambie linafaa kuuzwa kwa kiasi gani 😊” Alisema Bibi
Marie alienda kuvaa gauni kisha Bibi akampiga picha walimtumia Michael
baada ya dakika tano Michael alitoa thamani ya bei iliyoniacha mdomo wazi
“Amani utampati Scola million 3 nitakurudishia nikifika nyumbani” Marie aliongea 😘
Amani aliitikia kwa kichwa tu hakujisikia kujibu kwa sauti
“Michael anauliza gauni nimelinunua wapi anataka atume order sijamjibu…..” Bibi aliongea
“Mjibu Scola si yupo atamtengenezea” Amani aliongea
“Ndiyo mjibu…..tutakuwa tuna mdhulumu Scola haki yake” Alisema Marie huku akiligeuza geuza gauni anaonekana alikuwa haamini
“Scola twende ukachukue pesa yako”Amani aliongea akiongoza njia
nilimfuata huku nikichekelea namna anavyo tembea mwendo ka kihuni tangu nije hapa sikuwahi kumzingatia 😄
Inaendelea………………