NILIMPA LIMBWATA MUME WANGU HIVI SASA MAMBO YAMEBADILIKA
Naomba ushauri wenu wapendwa. Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 29 na ni mama wa watoto wawili . Niliolewa miaka mitano iliyopita, nikiwa na matumaini na ndoto nyingi kuhusu ndoa yangu. Nilimpenda sana mume wangu na nilitamani tuishi kwa amani na upendo. Kwa nia ya kutunza ndoa yangu na kuhakikisha anatulia, nilimpa ribwata ili asiwe na wanawake wengine nje. Kwa muda fulani kweli alitulia, maisha yalionekana kuwa sawa, nikadhani pengine tumefungua ukurasa mpya wa uaminifu na heshima
.
Lakini hali imebadilika kabisa siku hizi . Sijui kama ile dawa imeisha nguvu ama ilifunikia tu tabia ya muda. Kwa sasa mume wangu amekuwa muhuni kupita kiasi. Kila mwanamke anamtaka, lakini pia yeye kila mwanamke anamtafuta
. Siwezi hata kuajiri mfanyakazi wa nyumbani kwa sababu wote anawatongoza na wengine hata anatembea nao. Hali ni mbaya hadi majirani na wanafunzi wa mtaani wameshaanza kuwa sehemu ya tabia zake chafu
.
Najikuta nikihisi fedheha kila ninapotoka nje, watu wananitazama kwa huruma au dhihaka, na nimechoka kuishi maisha ya mashaka na aibu kila siku. Nimekuwa nikivumilia kwa ajili ya watoto wangu, lakini sasa najiuliza: je, navumilia kwa ajili yao au najiumiza bila sababu?
Nahitaji ushauri wa kina kutoka kwa watu waliowahi kupitia hali kama hii au wale wenye hekima ya maisha ya ndoa. Je, kuna njia ya kumrekebisha tena? Au ni wakati wa mimi kujiokoa kabla sijapotea kabisa?
Naomba msaada wenu