WAZAZI WALINILETEA MWANAUME AKANIOA, ANACHONIFANYIA SASA
Habari mimi ni binti, miaka yangu 24 shida yangu naomba ushauli kwa hili tatizo langu.
Kabla ya yote, nakumbuka nilipofika miaka 19 walezi wangu walinitafutia mume ilikuwa ngumu kwangu kukataa kwa sababu wazazi wangu ni wakali mno, hivo nikakubari kuolewa tu kulidhisha wazazi.
Sasa yule mwanaume alikuwa bado anaishi na wazazi wake kwa hiyo nikawa naishi na wakwe zangu pamoja na mawifi zangu, mwazo walikuwa kama wananijali vile kumbe maigizo tu tukaishi mwezi wa kwaza vizuri, mwezi wa pili vituko vikaaza kwa ndugu wa mume, kwa mama mkwe pamoja na mume mwenyewe. Mwazo tulikuwa tunapika pamoja lakini baadae ikawa nikipika mimi hawali, wanaacha tu wakipika nikila maneno mengi ya kejeli na kunionyeshea dharau kabisa, na nikimwambia mume hata hana muda kabisa na mimi.
Badae sasa, nikaja kusikia kwamba mume wangu ana mwanamke wake ambaye alitaka kuoa mwazo lakini wazazi wa mwanamke wakamkatalia sababu wao walikuwa wanamjuwa vizuri huyo mwanaume tabia zake na cha ajabu mwanaume wangu huyo tangu amenioa hajawahi kunigusa hata siku moja nikimuliza hata aniambii kitu kumbe akawa anakutana na huyo mwanamke wake nikimuliza kuhusu huyo mwanamke anasema wameachana aliponioa eti na nikimuliza sasa kwanini umenioa mimi wakati hata hujawahi kunipa haki yangu ya ndoa anakuwa mkali tu jibu la maana hakuna.
Sasa nikazani labda anaumwa lakini apana mzima wazazi wake wakawa wananinyanyasa nikawa navumilia tu hivo hivo tukaishi kama mwaka na miezi sita ivi mambo yakawa yale yale nikaona bora nimweleze kaka yake mkubwa maana yeye alikuwa anaishi mbali kidogo na kwao nikamwelezea kila kitu akasema ataongea nae alipoongea nae akapunguza baadhi ya tabia mbaya lakini siku zote hizo hajawai kushiliki na mimi tendo la ndoa tunaishi kama kaka na dada tu.
Sasa wazazi wake na dada zake wakawa wanasema mimi mgumba maana kalibia miaka miwili yote hii hata mimba ya bahati mbaya hamna, sasa ningeipataje mimba hali ya kuwa mtoto wao tunaishi kama kaka na dada tu nikimwambia kuhusu tendo anakua mkali kama nini, nikawa navumilia tu matusi yao sasa baba yake mkubwa yule mume wangu akaja siku moja akaona vile dada na mama zake wanavyo nichukulia akasema itabidi muhame hapa muishi kwenye nyumba yenu mimi nikakubali nikaona labda mume wangu huko atakuwa kawaida tukahama tukahamia kwenye nyumba yetu lakini sasa afadhali ya kule mengine alikuwa anaogopa kufanya mbele ya ndugu zake ikawa vituko tu na kule masimango matusi ya dada zake wanakuja huku huku kunitukania kwangu.
Siku moja nikasema yote kwa yote bado yule mama yake nikasema bora niende kuongea nae labda nimewahi kumkwaza bila kujuwa kibinadamu tu nikaenda nikamwambia Mama naomba tuongee akasema sawa nikamuliza mama kwani mimi nimewahi kukukosea labda kwa namna yoyote ile bila mimi kujuwa kama nimekukosea akasema hapana hujawahi nikosea.
Mmh..! sasa nikamuuliza Kwanini unanichukia akasema nakuchukia tu maana wewe sio chaguo langu wala la mwanangu kakuoa ili tu awe na mwanamke hatukupendi wala nini..!
Daah nililia sana siku ile sana yani basi ila nikamwabia sasa kwanini usimwambie huyo mwanao akamuoe huyo chaguo lenu itakuwa vizuri labda na mimi nitaheshimiwa kama mke niko tayari kuwa ukewenza mimi.
Nikaishia kuambulia matusi tu nikatimuliwa nikaondoka wazazi wangu wanaishi mbali na mimi kwa hiyo nikashindwa kuwaambia ili kuondoa kuwapa wasiwasi lakini huku alikuwepo bibi yangu nikamfanta nikamwelezea lakini hakuwa na msaada wowote na ukizingatia yeye ndio alielazimisha mimi kuolewa na huyu kaka.
Nikaona sina msaada wowote miaka mitatu ikapita sasa akawa harudi nyumbani kulala akawa analala mnje ukuiliza tu matusi hachi chakula wala matumizi nyumbani na akawa hataki nifanye kazi yoyote mwisho mimi nikachoka nikaona bora nitoloke lakini moyo ukakataa kufanya hivyo nikasema bora niombe talaka yangu lakini akawa hataki kutoa alivyoona hivyo akawa anakuja na wanawake zake ndani chumbani kwangu yaani dah tangu hapo sijawai kumwambia mtu tena kuhusu yeye.
Siku moja hivi iliyo na bahati nikaomba talaka cha ajabu akanipa kumbe alikuwa anataka kuoa huyo mwanamke wake sababu ana mimba yake wakati mimi miaka mitatu ya ndoa hajawai hata kunigusa hata siku moja nikaona sawa tu bora niondoke zangu.
Sasa nimeondoka mwaka mmoja sasa umepita kusema kweli sina imani na mwanaume yoyote yule kiufupi nawaogopa sana sana lakini nikavaa ujasili kidogo nipo kwenye mausioano.
Lakini uyo mwanaume yuko mbali na mie, mimi niko Zanzibar yeye yuko mwanza kikazi ila yani nisipo mtafuta hata wiki yeye pia hanitafuti sasa naogopa nisije jikuta kwenye shimo kubwa kuliko la mwazo alafu mkali naogopa kumuliza baadhi ya mambo mengine wakati mwengine ananifanya nijione kupendwa sana wakati mwingine ananipuuza sasa sielewi nifanye nini ndugu zake wananipenda sana hawana kipimo hata wao wakati mwengine wanamuogopa naomba ushauli wako nifanye nini.