MKASA WANGU BAADA YA KUMUACHA MWANAUME ALIYENIPENDA
Mimi ni dada wa miaka 28. Nimekua na mahusiano na mwanaume wa miaka 34 imekuea takribani miaka 5 sasa.
Kiukweli amekua akinipenda na kunijari kipindi chote hicho japo ugomvi wangu na yeye ni pale tu amekua akiniahidi kwenda nyumbani kutoa mahari lakni hatekelezi, hivyo nikaona ananipotezea mda.
Mimi nina kazi yangu nzuri hata yeye pia ni mtumishi wa serikali na kipato chake ni kizuri hivyo tulifungua biashara pamoja ya stationari na kwao walikua wanafahamu duka lilipo japo kwetu hakuna aliejua nakowekeza.
Mimi mwaka huu mwezi wa 3, nilimuomba tuachane baada ya kuona napoteza mda na mtu asietaka kuniweka kwake wa halali huku amenihakikishia kua hana mke na ni kweli maana yake miaka yote hiyo sikuwahi kuona dalili za mke mwingine kwake japo aliwahi kuoa na ana watoto 2, na mke aliezaa naye aliolewa tayari pengine na ana maisha yake nje ya nchi miaka zaidi ya 17 sasa.
Kweli nilifanya timbwili tukaachana japo aliugua na kulia sana hata alienda kwa ndugu zangu na kuomba turudiane lakini nikagoma. Baada ya mda nikapata mpenzi mwingine nikaingia mahusiano japo sikua na amani make kila siku yule baba alikua ananililia kwa simu akidai nisiende mbali na yeye.
Dada penzi jipya likanipotosha nikazama kwa hyo kijana, sasa kilichonikuta ni moto juu ya moto kumbe alikua ni tapeli tena wale wa mjini baada ya mwezi akaanza kusema nichukue mkopo tufanye biashara nikagoma kwani hakua amenioa rasmi baada ya kuona kila njia ya kuniibia inagoma alisema tuachane nikasema sawa baadae akanizushia kesi kua ananidai pesa nyingi hivyo anataka pesa zake.
Niliona kitu cha ajabu yule kaka alianza kuhesabu hadi siku alizonitoa auti kua natakiwa kulipia akapiga hesabu ikaja million 2 na zaidi, heey huwezi amini alichukua vyeti vyangu vya taaruma na kuvificha akidai nisipomlipa sitaviona tena na mbaya zaidi kwa mda niliokaa naye niligundua anaconnetion kubwa hapa mjini na akanit!sh!a atanipoteza kama nitakua msumbufu na pesa aliitaka ndani ya masaa 12 tu.
Dada vyeti vyangu ni mhimu zaidi nikasema sawa kumpa hiyo pesa na uhakika wa kuipata nilikua nao, akasema nilete mashine za stationary ashike ili aniamini na ukweli nikazileta maana yake yule baba aliniachia zote.
Sasa la ajabu pesa nikapata naipereka kwake anipe vyeti na mashine zangu nikakuta amehama na mashine zote kapeleka vyeti kaacha sebleni na kwa simu hapatini.
Kilichonileta kwako dada yule mpenzi wangu wa kwanza hakuacha kunipenda hadi leo hii nimerudina naye tena ameshapeleka barua kua anenda kutoa mahari mwezi wa 10 nyumbani kwetu japo kila akiuliza mbona duka nilifunga namjibu kwamba baada ya kuachana nilikosa kodi nikatoa mashine nikazitunza nikiambatanisha na uongo mwingi.
Duuh ukweli naogopa kumwambia kilichonitokea naogopa kumpoteza tena lakini ni aibu maana yake hizo mashine haikua chini ya millioni 7.5 na mchango mkubwa ulikua wake.
Naomba msaada nifanyeje Samahani kwa kuandika kitabu kirefu.
Hapa kuna mambo mawili, ombi la ushauri na kujifunza pia hii story ikufunze na utoe ushauri kwa wengine tunasoma comments