MTI UNAOMWAGIKA DAMU
Part 1
Jua liliendelea kuangaza taratibu huku kiza kikizidi kuaga. Sauti za ndege zilisikika na kufanya asubuhi ile iwe yenye kuvutia. Wanawake walitoka ndani wakiwa na mafyagio, wengine vyombo vinavyotaliwa kuoshwa, wengine ndoo za maji kama walivyokuwa wakifanya siku zote asubuhi.
Lakini asubuhi hiyo ilikuwa tofauti na siku zote. Waliokuwa wakienda visimani walikutana na maajabu yaliotisha. Si rahisi kustahimili hasa kwa wanawake. Hofu zikawatanda na wenye roho nyepesi walitimua mbio.
Ilikuwa damu inayotiririka kutoka kwenye mti wa mbuyu ulio kando kidogo na makazi ya watu, njia ya kuelekea sokoni, visimani na hata wale wanaokwenda mashambani.
“Hii siyo sawa” Alisema mama Janeth, mmoja kati wa mashuhuda wa tukio lile.
Yowe zikasikika. Vilio vya kuomba msahada kwa mashuhuda waliokuwa wakitimua mbio. Punde wanakijiji walijaa kushuhudia tukio lile la kushangaza.
“Hii ni damu kweli” Mzee mmoja alisema baada ya kuigusa. Ilikuwa mbichi, nyepesi na ya joto kama ya binadamu au Mnyama.
Mwenyekiti wa Kijiji, Mzee Magoye alifika na kuungana na wanao shangaa.
“Hii siyo kawaida kijijini hapa” Alisikika mwenyekiti akisema.
“Aitwe Mganga wa Kijiji haraka” Aliongeza mwenyekiti huyo.
PART 2
Mzee Mware, Mganga mkongwe pale kijijini alifika na mkoba wake wa uganga. Watu wakiwa nyuma yake, aliuzunguka mara kadhaa ule mti unaomwagika damu. Kisha akapiga magoti na kuishika ile damu kwa kidole chake.
“Ni damu kweli! Damu ya binadamu” Alisema Mganga.
Sasa akauchukua msinga wake na kuurusha mara tatu kuelekeza kwenye ule mti. Akachukua kopo moja lenye dawa na kulifungua. Akachukua kidogo na kuinyunyuzia kwenye ile damu na Kisha akatulia kidogo.
“Kuna jambo halipo sawa” alisema Mganga na kuongeza
“Kuna ushetani ulifanyika kwenye huu mti”
Punde upepo mkali ulianza kuvuma kwenye kile Kijiji. Sauti ya mtoto ikaanza kusikika ukilia kwenye ule mti. Watu wakazidi kuogopa. Mganga akarudi nyuma. Wanawake wakaanza kupiga yowe ya woga. Watoto wakawa wanalia. Ule mti ukaanza kusogea taratibu kutoka sehemu uliopo.
Usiku wa siku hiyo ulikuwa kimya sana. Hakuna mtu aliyetoka nje. Hata wanyama waliogopa. Bundi wenye kupiga kelele usiku hakuthubutu hata. Kimya kilitawala Kijiji chote.
Mtoto mdogo aitwaye Mwandamo yeye licha ya kuonywa na wazazi wake ya kuwa asijaribu kuusogelea ule mti lakini hakusikia….
PART 3
Mwandamo usiku ule hakulala mapema. Alifungua mlango na kutoka nje hadi karibu na ule mti. Alichokiona kilikuwa kinatisha sana. Alimuona mwanamke aliyelowa damu huku akilia. Taswira ya yule mwanamke haikumjia vizuri kutokana na mwanga hafifu wa giza. Mwandamo alimtazama tu kutoka sehemu alipojificha.
Yule mwanamke alikuwa akivuja damu Kila sehemu. Mwandamo hakuona mti usiku ule ila yule mwanamke anayevuja damu.
Aliamua kurudi nyumbani na asubuhi yake akamweleza mama yake juu ya kile alichokiona.
“Mjinga wewe, nani aliyekwambia uende? Ule mti umeraaniwa. Acha kuusogelea” Aliongea mama yake.
Siku hiyo mwenyekiti aliitisha mkutano na wanakijiji wote walikusanyika. Kama ilivyo kawaida yao wote waliketi kwenye mikeka iliyotandikwa eneo lile.
“Shetani amevamia Kijiji chetu, tunalazimika kufanya jambo kuondosha jambo hili” Alizungumza Mwenyekiti.
Bibi mmoja mkongwe alisimama na kusema jambo
“Miaka mingi iliyopita, kuna ushetani mkubwa ulifanyika eneo lile la mbuyu. Ukweli huu ulizikwa palepale hakuna aliyethubutu kusema. Sasa mti unalia na kutoa machozi ya damu sawa na damu iliyomwagika pale.” Yule bibi alinyamaza kwa kuruhusu funde la mate lipite vyema kwenye kinywa chake Kisha aliendelea
“Yaliyopita yamerudi Sasa” alimaza hivyo na kuketi chini…..
Dah, Inaendelea…………