SAFARI YANGU YA MAPENZI: KUTAPELIWA, KUCHEZEWA, NA HATIMAYE KUPATA MUME WA KWELI
..
Sehemu Ya Tatu
MTOTO WA KISHUA ALIYENIFANYA NIHISI NIMEPATA MUME WA KWELI
Baada ya kuumizwa na mwanaume wa kazini, nilijikuta nikivutwa na mwanaume mwingine tofauti kabisa—mtoto wa kishua.
Alikuwa mdogo kwangu kiumri, lakini alijua kupenda. Alikuwa na pesa, alinitreat kama malkia, na alinipa uhakika wa maisha mazuri. Tulikuwa na mahusiano ya kifahari—dinner kwenye hoteli kubwa, vacations, na shopping za gharama.
Kwa mara ya kwanza, nilihisi kuwa labda huyu ndiye mume wa ndoto zangu. Alionyesha upendo wa dhati na alionekana kama mtu aliyekuwa tayari kujenga familia na mimi.
Lakini, baada ya muda, alianza kubadilika. Mawasiliano yakawa haba, na alizidi kuwa mbali nami. Nilijaribu kumuuliza kilichokuwa kinaendelea, lakini hakutoa jibu lolote.
Siku moja, ghafla alipotea. Aliniacha bila taarifa, bila sababu, na bila hata kuniambia neno la mwisho. Nilihisi dunia imenisaliti tena.
Nilijifunza kuwa hata wanaume wenye pesa na maisha mazuri wanaweza kucheza na moyo wa mtu. Nilichoka na mahusiano ya drama, na nilijiambia kwamba sitawahi tena kuingia kwenye mahusiano yasiyo na uhakika.
Sehemu Ya Nne (Mwisho)
KUPATA MUME WA KWELI
Baada ya safari ndefu ya mahusiano yenye maumivu, nilihisi kama ningepoteza tumaini la ndoa kabisa. Nilihisi labda mimi siyo mtu wa bahati katika mapenzi.
Lakini siku moja, nilihudhuria event fulani, na kwa bahati nzuri, nikakutana na classmate wangu wa primary, anaitwa Jamal. Tulikumbatiana kwa furaha baada ya miaka mingi kupita.
Tulikumbushana enzi za utoto, tukacheka, na baadaye tukabadilishana contacts. Tulianza kuchat mara kwa mara, lakini kwangu, nilimchukulia kama rafiki tu. Sikuwa na interest naye ya kimapenzi.
Kadri siku zilivyopita, nilianza kuona utofauti wake. Hakuwa tajiri kama yule wa Johannesburg, hakuwa na muonekano wa kuvutia kama yule wa kazini, wala hakuwa na maisha ya kifahari kama mtoto wa kishua. Lakini alikuwa na kitu ambacho sikuwahi kupata kwa wanaume wengine—alikuwa na mapenzi ya kweli.
Alinijali, alinisikiliza, na hakunichezea kama wengine. Tulianza kama marafiki, na taratibu tukajenga uhusiano wetu kwa msingi wa ukweli.
Baada ya miaka miwili ya mahusiano yenye furaha na amani, alinipropose, na hatimaye tukafunga ndoa. Leo hii, ninapotazama nyuma, najua kuwa nilifanya makosa mengi katika mahusiano. Nilijifunza kupitia machungu, kutapeliwa, kuchezewa, na kutumiwa. Lakini yote yalikuwa darasa la kunifanya niwe mwanamke bora zaidi, mwenye msimamo na anayejua thamani yake.
Swali kwa Wana Raha Special:
Je, wanawake wengi wanapitia safari kama hii ya mahusiano yenye changamoto kabla ya kupata mume wa kweli? Na kwa wale waliopata waume, walikutana nao vipi?