TULICHOMFANYA YULE MCHAWI HATAKUJA KUSAHAU KAMWE
SEHEMU YA 11
Safari mpya ya maisha ilianza rasmi pale nyumbani baada ya Maza mdogo kuja,kabla hajaja kutoka mjini tuliishi kwa kujiachia kama vile tupo mamtoni na tulikula na kunywa tutakavyo,lakini sasa yale maisha ya mwanzo yakatoweka,kula nyama ya kuku tena ilikuwa muujiza uliohitaji Mungu mwenyewe kuingilia kati!,kuku wale wa wikiendi walikuwa wakisafirishwa kupelekwa mjini na sisi hapo nyumbani kula Kayabo wa chukuchuku bila viungo,ilifikia sehemu ukila mboga iliyoungwa kwa mafuta na nyanya unamshukuru Mungu kwa muujiza wa kipekee!.
Kuku alipopikwa mimi na Ema vyetu ilikuwa ni miguu,shingo na kichwa na tunyama twa kuzugia kama tuwili hivi,nyama nyingine yote iliyobaki ilimuhusu Maza mdogo na mumewe!.
Tabia ile japo haikuwa nzuri lakini mumewe hakuwahi kuikemea,yeye alitulia tuli kana kwamba mkewe alichokuwa akitenda kilikuwa sawa.Sasa tulidhani siku si nyingi angeondoka lakini kumbe tulikuwa tunajidanganya!.Hatukufahamu kumbe kilichomleta hapo kijijini ilikuwa ni kuweka kambi kwa ajili ya biashara ya ushonaji wa nguo!.Pale senta kwa wakati ule hakukuwa na fundi cherehani,sasa nadhani mumewe alimwambia aichangamkie ile fursa iliyokuwa na hela za kutosha kwa kipindi kile hapo kijijini!.
Basi baada ya yule mzee Masumbuko kukataa ile miwa pamoja na mapapai alinikabidhi,nilimuomba anichumie majani ya mgomba ili nifungie ile miwa nipate urahisi kuibeba,yale mapapai aliniwekea kwenye kigunia cha chumvi chumvi(salfeti).Sasa nikanyanyua mzigo wa miwa nikajitwisha kisha nikamwambia yale mapapai aniwekee juu ya mzigo wa miwa ili nitandike kwato kuitafuta senta.
Ule mzigo haukuwa wa kitoto hata kidogo,lakini sikuwa na wakumdekea!,niliogopa endapo nikiutua ili nipumzike ni nani tena angenitwisha?,hivyo nilikomaa nao hivyo hivyo.Ingawaje Senta palikuwa mbali sikutaka kabisa kupumzika njiani,kuna muda nilikuwa nahisi shingo inauma lakini nilijikaza kisabauni kama mtoto wa kiume niliyetokea jamii ya Kikurya!.
Baada ya safari ndefu hatimaye nikafika senta.Sasa nilitafuta sehemu ambayo ni nzuri na yenye kivuli ili niweke ile miwa na mapapai nianze kuuza.Basi nilisogea kwenye mti mmoja ambao hakuwa mkubwa sana kisha nikaisimamisha ile miwa kwenye ule mti na yale mapapai nikayotoa kwenye ile salfeti nikayapanga yakawa tayari kwa kuuzwa!.
Nilipata taabu sana kuuza zile bidhaa kwasababu aliyesema nikauze hakuniambia niuzeje au alitaka faida ya kiasi gani!,nilichokuwa nakumbuka ni yeye kuununua ule mzigo kwa bei ya shilingi elfu 3.
Sasa ilibidi mimi mwenyewe nijiongeze kwenye namna ya uuzaji ili utoe hela ya watu na faida ipatikane.Nilianza kuuza ule mzigo hiyo mida ya saa 4 asubuhi lakini hakukuwa na wateja waliojitokeza kununua.Ilipofika mida ya saa 5 asubuhi,alikuja jamaa mmoja akiwa amefunga mzigo kwenye baiskeli na kuweka kambi lile eneo nililokuwepo.
Jamaa “Aisee mambo vipi?”
Mimi “Mambo poa”
Jamaa “Mbona umenivamia kwenye eneo langu?”
Mimi “Eneo lipi?”
Jamaa “Hapo ulipoweka mapapai ni eneo langu ambalo huwa naweka biashara yangu”
Mimi “Sikujua kaka,ngoja niondoe”
Jamaa “Hapana usiondoe,wewe sogeza kidogo kule kushoto ili na mimi nikipate kivuli”
Basi nikaamua kuyasogeza mapapai kushoto ya ule mti ambao nilikuwa nimesimamisha miwa.Yule jamaa alikuwa mstaarabu sana,japo kweli nilikuwa nimevamia eneo lake lakini hakutaka kunifukuza pale,alichoniambia ni kwamba nisogeze ili kila mmoja afaidi kivuli cha ule mti!.
Jamaa alifungua ule mzigo kwenye baiskeli kisha akatandika kavelo(turubai) ndipo akaanza kutoa kwenye boksi viatu aina ya kata mbuga(sendeu).Sasa kumbe jamaa ile ndiyo ilikuwa biashara yake pale siku zote ya uuzaji wa kata mbuga!.
Kiukweli baada ya jamaa kufika sikujiona tena mnyonge kwakuwa nilikuwa na mtu wa kupiga nays stori.
Muda ulipozidi kusonga na wateja wa miwa nao walianza kuja,sasa ishu ikawa ni kisu cha kukatia pingiri za miwa ningekitoa wapi!.Kuna kiduka kimoja ambacho kwa nyuma kulikuwa kuna nyumba,nikajongea mpaka pale nikaomba waniazime panga au kisu kwa ajili ya kukatia miwa halafu ningewarudishia!,yule aliyekuwa akiuza kwenye kile kiduka alikuwa mama mmoja ambaye alimuagiza mwanaye aniletee panga ila akasema nikimaliza nirudishe.
Kiukweli miwa niliuza sana ila mapapi hakuna aliyenunua hata moja.Sasa ilipofika mida ya saa 8 mchana nilikuwa nahisi njaa kishenzi na sikujua ningekula nini kwa wakati huo!,sikuwa na namna zaidi ya kukata pingiri tatu za muwa na kuanza kutafuna ili kupoza njaa!.Ilipofika mida ya saa 10 alasiri nilihesabu hela niliyokuwa nayo mfukoni ilikuwa jumla elfu 2600/=,Hiyo ilikuwa ya miwa pekee,papai hakuna lililonunuliwa mpaka muda huo.
Sasa nikiwa naendelea kuuza zile bidhaa pale,kwa mbali nikamuona Ba’mdogo akiwa anakuja pale senta,sasa kwakua alinicheki akiwa mbali hakupata taabu kunitafuta,hata hivyo ile senta haikuwa kubwa kiasi hicho mpaka nishindwe kuonekana.Alipofika niliona kama ananihurumia lakini hakutaka kuonyesha ile hali alijifanya kuvunga.
Ba’mdogo “biashara inaenda?”
Mimi “Ndiyo baba inaenda ila mapapai hayajanunuliwa”
Ba’mdogo “Ningejua ukaja na miwa tu,watu wa huku si walaji wa mapapai,wanapenda miwa”
Sikutaka kumjibu nikawa nimekaa kimya namtazama.
Ba’mdogo “mpaka sasa umeuza shilingi ngapi?”
Mimi “Nimeuza elfu mbili na mia sita baba”.
Ba’mdogo “Sawa nipe hiyo hela”
Basi nikatoa ile hela mfukoni nikampatia akawa ameondoka kuelekea kwenye maduka yaliyokuwa upande wangu wa kulia.Hakukaa sana kule akawa amerejea nilipokuwepo.
Ba’mdogo “Yule mama anamuona?”
Akawa anionyesha kwa kidole uelekeo alipokuwa mwanamke mmoja aliyekuwa amekaa kwenye matofali ya kuchoma.
Mimi “Ndiyo baba namuona”
Ba’mdogo “Ikifika jioni hayo mapapai hujauza,nenda umpelekee yule mama,nimemwambia tayari”
Mimi “sawa”
Baada ya maelekezo yale yeye akawa ameondoka na mimi kubaki pale.
Ilipofika mida ya saa 12 jioni,kweli nilimpelekea yule mama yale mamapai baada ya kudoda kutwa nzima pale chini!.
Miwa nayo ikawa imebaki miwili,sasa nikaona nimuombe yule mama aliyeniazima kisu ile miwa niilaze pale kwake ningekuja kuifuata asubuhi,yule mama hakuwa na tatizo alikubali!.
Sasa nikaanza kuwaza wakati wa kurudi nyumbani nipite njia ipi,je nipite ile ya mzunguko wa lamboni au nipite ileile fupi iliyokuwa katikati ya ile miembe mikubwa!.Wakati huo mfukoni nilikuwa nina shilingi 700.Basi nikaone ni heri nipite ile fupi ili niwahi kufika nyumbani.
Nilimuaga yule jamaa tuliyekuwa tukiuza wote hapo nikamwambia tungeonana kesho yake,jamaa nae akawa ameniambia naye angeondoka muda si mrefu.
Nikaanza kupiga kwato mdogo mdogo kurudi nyumbani.Wakati natembea kiukweli nilikuwa nina mawazo mengi sana,ukizingatia nilikuwa sijala chochote zaidi ya kutafuna vipande kadhaa vya muwa!.Niliona kabisa mambo endapo yangenishinda ningerudi nyumbani!.Wakati huo giza nalo lilikuwa halichezi mbali maana ilikuwa mida ya saa 1 usiku.
Sasa wakati natembea huwaga nina kawaida ya kuangalia chini kama kondoo,huwa naangalia mbele,kushoto na kulia kwa muda mfupi sana lakini muda mwingi huwa natazama chini!,sijajua ni kwanini uenda ndivyo nilivyozaliwa na kurithi kwa mzee wangu!.
Sasa wakati nakwenda sikumuona mtu nyuma yangu wala mbele yangu akiwa anakuja,nilishitukia tu ghafla naitwa jina langu na mzee ambaye nilikuwa napata taabu kumkumbuka.
Mzee “Hujambo Umughaka”
Nikashituka sana!,nikabaki nashangaa ametokea wapi yule mzee mtu mzima!,nikadhani uenda muda ambao nilikuwa natembea huku nikitazama chini sikumuona.
Mimi “Sijambo,shikamoo”
Mzee “Marhaba,vipi mwalimu yupo?”
Mimi “Eenh yupo”
Mzee “sawa utamsalimia”
Mimi “Sawa,nimwambie nani vile!”
Mzee “we mwambie Makono anamsalimia”
Mimi “Sawa”
Yule mzee nilianza kuvuta taswira nimewahi kumuona wapi lakini nikawa sikumbuki vizuri!.Alikuwa mtu mzima mwenye miaka kama 50 -60 hivi!.
Sasa wakati natembea zangu nikawa nageuka nyuma ila cha ajabu yule mzee sikumuona!,nikabaki nashangaa kwasababu lile eneo pembe zoni hakukuwa na njia ya mchepuko,pia kulikuwa na katani za kutosha ambazo kama ungejifanya kuchepuka basi zingekuchoma na ile miba yake mpaka uchanganyikiwe na kile kibarabara kilikuwa kimenyooka moja kwa moja.Tulikuwa tumetoka kuzungumza kwa sekunde kadhaa tu lakini cha ajabu kugeuka nyuma sikumuona tena!,Kuhusu jina langu sikuwaza sana nikawa nasema huenda Ba’mdogo aliwahi kumwambia mimi ni kijana wake na jina langu ni umughaka.
Basi namshukuru Mungu siku hiyo niletembea kwa amani kabisa hakukuwa na viroja wala vituko nilivyokutana navyo pale kwenye miembe.Nilifika nyumbani mida ya saa 2 usiku.Sasa wakati usiku tukiwa tunakula Ba’mdogo akawa ameniambia hela niliyokuwa nayo nihakikishe asubuhi naelekea kwa mzee masumbuko kufata miwa mingine ili nikauze kwa kuwa hiyo ndiyo iliyokuwa kazi yangu.
Tulipokuwa tukiendelea kula nikamwambia Ba’mdogo alikuwa anasalimiwa na yule mzee niliyekutana naye muda si mrefu.
Ba’mdogo “Makono?,makono ndiyo nani?”
Mimi “mimi sijui baba,yeye ameniambia nikwambie hivyo utamfahamu”
Ba’mdogo “Uenda atakuwa mzee mwalukala huyo,yule ndiye huwa anamajina mengi ya utani”
Basi mimi sikutaka makuu,nilipomaliza kula nilielekea zangu kulala kwakuwa nilikuwa nimechoka,Ema yeye alipoingia ndani akaanza kupiga buku kama kawaida.
Sasa picha ya yule mzee ikaanza kunijia vizuri na nikakumbuka ni yule mzee ambaye alikuja na mwenyekiti pale nyumbani siku ile ambayo Ema alikuwa ametoka kukung’utwa viboko darasani na watu wasiofahamika.Yule mwenyekiti wakati anakuja na headmaster pale nyumbani kumohoji Ema alikuwa na huyo mzee,ndipo nikawa nimemkumbuka vizuri.
Basi asubuhi mida ya saa 1,niliwahi kuamka lakini sikumuona Ema,nikasema uenda aliwahi mapema kwenda shuleni wakati mimi nikiwa nimelala.Nilipomaliza kupiga mswaki wakati navaa viatu ili niende nikamsalimie Maza mdogo na mumewe ili niondoke zangu,mara nikaanza kusikia sauti za wanafunzi huko shuleni wakipiga kelele kwa nguvu.
SEHEMU YA 12
Zile kelele za wanafunzi hazikunishitua sana kwakuwa nilidhani uenda ingekuwa mambo ya kiuanafunzi tu huko shuleni.
Niliingia ndani kumsalimia Ba’mdogo na mkewe halafu mimi niondoke zangu nikachukue miwa ili nielekee kuuza.Sasa nilimsalimia Ba’mdogo lakini hakuwa akijibu,nilidhani uenda angekuwa amewahi shuleni,nilimsalimia pia Maza mdogo lakini nae hakujibu chochote,sasa nikasema Maza mdogo yeye nikimsalimiaga huwa kama kawaida yake anauchuna!.Niliamua kuondoka zangu niwahi kwa mzee Masumbuko.
Sasa nilipotoka nje kukiwa kumeshamiri mapambazuko,niliendelea kusikia wanafunzi wakipiga kelele kwa mshangao huku wengine wakicheka na kuzungumza kisukuma!,kwakuwa njia ile iliyokuwa ikipita lamboni kuelekea kwa mzee Masumbuko ilikuwa ikipita nyuma ya madarasa ya shule!,ikabidi nisimame kuwaangalia na kuwatazama wale wanafunzi kilichokuwa kinawafanya wapige kelele na kuendelea kucheka huku wengine wakiteta kwa lugha ya kisukuma.
Basi kwakuwa walikuwa wanachungulia darasani ikabidi na mimi nisogee kuchungulia kuona walichokuwa wanashangaa,sasa ile nimefika kuchungulia nikamuona Ema na mama mdogo wakiwa wamelala kwenye sakafu wakiwa wamejifunika shuka jeupe,yaani walivyokuwa wamelala ni kama mtu na mkewe.
Nilihamaki na kushangaa sana,ikabidi nizunguke haraka kuingia darasani nione nini kilikuwa kinaendelea!.Sasa mpaka wakati huo hakukua na mwalimu hata mmoja pale shuleni,wanafunzi nao walikuwa wachache huku wengi wakiwa wanaongezeka kuja shuleni.Nilipoingia ndani ya darasa ambapo niliwakuta wanafunzi wengine wakishangaa,sikutaka kuuliza maana ile ilikuwa ni aibu ya karne.
Nilianza kumwamsha Ema kwa kumshitua na kumpiga piga mabega hatimaye akashituka,aliposhituka akaanza kupiga miayo na kujinyoosha kana kwamba ni mtu aliyekuwa na hangover ya pombe,baada ya kushituka na kujitambua alikuta wanafunzi wengi wakicheka na wengine wakiwa wanashangaa;mara ghafla Maza mdogo naye akawa ameshituka ghafla mpaka kupelekea sehemu ya kifua chake kubaki wazi na maziwa kuonekana mbele ya wanafunzi,alibaki anahamaki kama mwendawazimu!.
Kwakuwa walikuwa wamejifunika shuka moja na wote wakiwa uchi,nilimaambia dogo mmoja avue sweta limsitiri Ema ili akimbie nyumbani,ndivyo ilivyokuwa.
Nilimpa lile sweta Ema nikamwambia asimame alivae liwe kama sketi ili atoke aende nyumbani,ingawaje aliposimama alikuwa uchi na wanafunzi walishuhudia kila kitu!,mama mdogo yeye alikuwa akivuta lile shuka ili kujisitiri na ndipo nilimnyanyua na kuondoka naye huku akiendelea kushangaa amefikaje hapo na nini kilikuwa kinaendelea.Wanafunzi waliokuwepo mpaka wakati huo wengi walikuwa wakicheka na wengine kushangaa ni kitu gani kile!.
Sasa tulipofika nyumbani Maza mdogo alikuwa akiniuliza ni nini kimetokea na kwanini wamejikuta wakiwa uchi pale darasani.Mimi sikuwa na majibu zaidi ya kushangaa.Kumbe wakati huo tunajadili pale headmaster alikuwa amelala chumbani,sikufahamu wakati namsalimia alikuwa akinisikia ama la!.
Ba’mdogo “Hebu niwekee maji ya kuoga”
Alikuwa akimwambia mkewe lakini mkewe akawa anamshangaa headmaster.
Maza “Ina maana ba’Mary kinachoendelea wewe hukijui?”
Ba’mdogo “Kuna nini?”
Maza “Nimefikaje shuleni tena nikiwa uchi mbele ya wanafunzi?”
Ba’mdogo “Shuleni uchi,uchi kivipi?”
Ba’mdogo “wewe siumetoka muda si mrefu kuniamsha ukaniambia nachelewa shuleni,sasa umetoka saa ngapi kwenda shule ukiwa uchi?”
Baada ya kauli ile ya Ba’mdogo nikajisemea ndo yale yale ya Ema ya siku ile kuning’inizwa juu ya kenji.Baba mdogo ni kama alikuwa aelewi chochote kabisa na muda huo yeye alikuwa anadai Maza mdogo alikuwa ndani amelala.
Maza “Mungu wangu hiki ni nini?”
Basi hakutaka kupoteza muda akawa ameingia ndani!,basi Headmaster nilijaribu kumuelezea lile tukio lilivyokuwa lakini ni mtu ambaye ilionekana kama hakubaliani nalo,yeye akakomaa kwamba mkewe alikuwa chumbani na ndiye aliyemuamsha awahi shuleni.
Siku hiyo ikawa gumzo hapo kijijini na shuleni pia,talk of the town ikawa hiyo stori ya mke wa mwalimu!,Mazungumzo ya wengi walisema uenda mke wa mwalimu walikuwa na mahusiano na Ema na siku hiyo baada ya mizagamuano ya muda mrefu walichoka wakapitiwa na usingizi,wengi waliamini hivyo japo mimi niliamini lile tukio halikuwa la kawaida!.
Siku hiyo sikuondoka kuelekea kufata miwa ikabidi nitulie nyumbani,sasa nilijaribu kumuuliza Ema uenda alikuwa amifahamu jambo lolote!.
Ema “Yaani sielewi hata nilifikaje pale”
Mimi “Ina maana hukujua kama umelala na Maza mdogo?”
Ema “Mimi nimeshituka tu naona wanafunzi kaka,sielewi kiukweli nilifikaje pale”
Kiukweli hali ile haikuwa nzuri lakini nilibaki kucheka kama mazuri vile lakini hali ilikuwa inatisha sana,japo halikuwa jambo jema,lakini kimoyo moyo nilikuwa nasema angalau sasa Maza mdogo atapunguza mdomo wake!.
Headmaster baada ya kwenda shule muda haukupita alirudi nyumbani,sasa akawa anajaribu kumuuliza mke wake kama lile jambo ni kweli!,basi kumbe kuna wanafunzi shuleni pia walikuwa wamemueleza vilevile kama ambavyo nilimueleza,sasa akaamua kuwarudisha wanafunzi wote nyumbani na kikaitishwa kikao cha kijiji siku hiyo hiyo.Sikutaka kukosa kwenye kile kikao kwasababu nilikuwa mmoja wa mashuhuda na wanafunzi kadhaa!.
Kikao kile kilizungumza mambo mengi mno,kila mwanakijiji alikuwa akizingumza jambo lake.Wapo ambao walikuwa wanasema hizo tabia za kijinga zikome mara moja na wapo wengine waliokuwa hawakubalini na lile jambo.
Sasa yule mzee ambaye nilikutana naye ile jioni wakati natoka kuuza miwa akaniambia nimsalimie mwalimu,yeye pia alikuwa ni mmoja wa watu waliofika kwenye kile kikao na hakukubaliana na lile jambo.
Mzee “Kwanini kila siku ni nyie tu na siyo kwa watu wengine?”
Mzee “Hapo naanza kupata mashaka kidogo”
Mzee aliendelea “Juzi ilikuwa kwa kijana wako na tukaja mpaka kwako mwalimu,leo tena mambo ni yaleyale,ili jambo lingekuwa kwa watu wengine hapo kungekuwa na walakini,kila siku mambo haya yawapate nyie tu?,sisi tutaamini vipi mwalimu?,kama hutaki kuendelea na shule basi bwana na uache lakini hatuwezi kila siku hatuwezi kuwa tunazungumzia mambo yale yale yanayotokea kwa mtu yuleyule”
Mzee “Ingekuwa uchawi hata sisi ungetupata pia,sasa yawezekana mkeo na huyo kijana anayekaa kwako ni wapenzi!”
Sasa hili suala la Ema na Maza mdogo kuwa wapenzi naona wanakijiji wengi walilishupalia kama kweli vile!.
Akasimama mwana kijiji mwengine akasema “Hiki kituko hakijawahi kutokea kwenye hiki kijiji,na mimi sikubaliani na kwamba eti ni uchawi,haiwezekani kabisa!,huyo dogo na mkeo watakuwa wapenzi na uenda mkeo alitoka ndani akakuacha umelala wao wakaja kufanya yao na wakapitiwa na usingizi,hivyo mwalimu nikuombe umchunguze mkeo!”
Watu wengi waliunga mkono ile kauli ya mzee na huyo jamaa.
Headmaster alishindwa aseme nini mbele ya ile kadamnasi,sasa mwenyekiti wa kile kijiji ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kile kikao alisema kile kijiji hapo mwanzo ni kweli kulikuwaga na habari za washirikina,lakini baada ya kuitisha vikao kadhaa yale mambo yakapotea.
Mwenyekiti ” Mimi niseme tu kwamba,yawezekana haya mambo yakawa yamerudi,mimi pia nikiongozi wa kimila na kama haya mambo yamejirudia ningefahamu mapema sana,sasa nadhani Mwalimu unakumbuka tukio la kijana wako,na nilikwambia pia tusiendelee kudhani ni ushirikina kumbe kijana wako ndiye mkorofi amewachokoza wenzie wakaamua kumuadhibu kwa style ile,hivyo nikuombe umchunguze na kijana wako pia”.
Basi kile kikao baada ya kuchukua masaa kadhaa kikawa kimemalizika lakini jibu lilikuwa ni kwamba Ema yawezekana alikuwa na mahusiano na mke wa mwalimu.Tulitawanyika pale na kila mtu kwenda kuendelea na shughuli zake.
Headmaster hakutaka kabisa kuamini ya kwamba siku hiyo Ema alilala na Mkewe kwenye darasa,alichoamini yeye ni kwamba siku hiyo mkewe alikuwa chumbani wamelala wote,yaani ni kama mtu ambaye alikuwa amepofushwa!
Kiukweli lile tukio lilikuwa ni gumzo sana hasa ukienda hadi senta huko na nadhani pia kwa upande wa Maza mdogo ni tukio ambalo hatokuja kulisahau kwenye maisha yake.Baada ya siku kusonga lile tukio likawa kama linafifia.
Sasa Maza mdogo akawa naye ameanza kushona cherehani pale senta,alikuwa akitoka asubuhi anarejea jioni,muda ambao mimi nilikuwa nikimaliza shughuli ya kuuza miwa inabidi nimshubiri na yeye amalize tuongozane kurejea nyumbani.
Sasa nakumbuka siku moja nimeamka asubuhi mida ya saa 12 ili niwahi kusudi kuepuka jam ile ya asubuhi bafuni,nimeoga nimemaliza nikavaa kama kawaida ili niende sasa kusalimia kule ndani halafu niondoke zangu mdogo mdogo kuchukua miwa.
Nilifungua mlango wa pale sebuleni ili kuingia ndani niwasalimie Headmaster na mkewe,sasa ile nimengia ndani hapo sebuleni,aiseee nilishuhudia mzigo mkubwa wa mavi ambayo kikawaida kama ungeyapima kwenye sufuria,basi yangeweza kufikia kilo 3,mavi yale yalikuwa yamenyewa juu ya meza na ilionekana aliyekuwa ameyanya alikuwa amekula ugali wa mtama,kwasababu kile tunachokula ndiyo tunachokinya!,Sasa harufu ilikuwa kali sana na kiukweli nilishindwa kuelewa waliwezaje kulala ndani kukiwa na harufu kali kiasi kile,baada kushuhudia ule mzigo nikarudishia mlango kwenda kumshitua Ema ili aje ajionee!.
SEHEMU YA 13
Jamaa alipokuja akafungua mlango na kutazama aliondoka ghafla ameshika pua kutokana na ile harufu namna ilivyo kuwa ya kutisha.
Ema “Nani Kanya hayo mavi?”
Mimi “Sijui”
Mimi “Nimeamka kuja kusalimia ndiyo nakutana na hii hali”
Ema “Headmaster bado amelala?”
Mimi “Bado sijajua,hebu ngoja niwagongee”
Nilienda kujaribu kugonga ule mlango lakini ulifunguka wenyewe kuashiria ulikuwa wazi,basi nikaanza kuita lakini hakukuwa na mtu mle chumbani aliyeitikia!,niliamua kusukuma ule mlango na kuchungulia chumbani kwa Headmaster lakini hakukuwa na mtu!.
Basi nilitoka nikamwambia Ema Headmaster na Mkewe hawapo chumbani.
Ema “Mmmh huu mji aisee mimi utanishinda”
Mimi “kwanini?”
Ema “Hivi unadhani hii hali niya kawaida?,hivi siunakumbuka nilikwambia kuna siku nimekuta mavi kwenye lile debe la unga!”
Ema “Haya mambo si yakawaida,mimi shule ikifungwa sidhani kama nitarudi huku tena”
Mimi “Dingi atakuwa ameenda wapi?”
Ema “Inaonekana wameamka mapema kuna mahali watakuwa wameenda,na nadhani haya mavi niya muda huu tu,Headmaster angekuwa ameyaona najua angetuamsha!”.
Basi nilimwambia Ema tuibebe ile meza na kuitoa nje ili kuifanyia usafi,niliingia stooni nikachua jembe nikawa nakokota yale mavi kutoka mezani na kuangukia chini,baada ya kuisha juu ya meza,nilienda kuzoa michanga na kuyafukia yale ya pale chini na kuanza kuyazoa na kwenda kuyatupa huko nje!.Baada ya kuiosha ile meza ikabidi niianike juani ili ipigwe na jua la kutosha!.
Nilipomaliza na kufanya ndani usafi niliondoka zangu kuelekea kwa mzee masumbuko kwa ajili kufata miwa.Sasa siku hiyo sikuona kile kibanda cha Maza mdogo kikifunguliwa,nilihisi uenda aliamua asije tu kwa kuchoka kwasababu kama kweli walitoka yawezekana akawa alichoka.Ile jioni baada ya kumaliza biashara yangu ya uuzaji miwa nikaamua kurudi zangu nyumbani kama kawaida.
Nimefika nyumbani mida ya saa 2 usiku nikakuta hapo uwani yupo mzee mmoja ambaye alikuwa amekaa kwenye stuli,nilimsalimia na kuingia zangu chumbani kwetu.Sasa muda kidogo nikasikia sauti ya Headmaster ikisema “umesharudi?”
Mimi “Ndiyo baba,shikamoo”
Ba’mdogo “Nani umughaka?”
Mimi “Ndiyo baba ni mimi”
Ba’mdogo “aah mi nilidhani ni huyo mpumbavu,nimemwagiza muda sasa sijui linafanya nini huko”
Ba’mdogo “Hebu nenda ukamuangalie huyo mjinga kwa mzee masalu,ukimkuta umwambie achume kabisa na fimbo aje nazo”
Mimi “Sawa baba”
Ba’mdogo “Kimbia bhana na muwahi hapa”.
Basi nikatoka nduki kuelekea kwa mzee mmoja aliyekuwa na ng’ombe wa kutosha hapo kijijini akifahamika kama mzee masalu,sikuwahi kufika kwa huyo mzee ila kwasababu ya umaarufu wake pale kijijini nilikuwa nikimfahamu na kwake pia palikuwa pakifahamika.Nilifanikiwa kufika kwa huyo mzee hiyo mida ya saa 2 kuelekea saa 3 usiku.
Nilipofika nilikuta bado watu wako nje wakipiga soga,nilisogea kwa mtu mmoja ambaye ni mwanamke nikamsalimia na kujitambulisha ya kwamba nilikuwa nimeagizwa na mwalimu Wambura.Basi nikawa nimemuomba aniitie mzee masalu ili niweze kumuulizia kuhusu Ema.
Yule mama aliniambia “Hebu Nenda kwenye lile zizi kule utamkuta huko anakagua mbuzi”
Basi nikazunguka nyuma ya nyumba kuliko kuwa na zizi la mbuzi,nilimkuta mzee akiwa na vijana kama 3 wakiendelea kusavei kwenye lile zizi huku wakiongea kisukuma,nilimsalimia mzee na ndipo nikajitambulisha kwake.
Mzee Masalu ” Ooh yule kijana wa mwalimu wambura mbona nimempa na ameondoka muda mrefu”
Mzee masalu “Uenda mtakuwa mmepishana,ametoka hapa muda si mrefu”
Mimi “Sawa mzee mimi naondoka”
Mzee Masalu “Sawa msalimie mwalimu”.
Basi sikutaka kupoteza muda nikatoka nduki kurudi nyumbani kumpelekea taarifa Headmaster.Nilipofika nyumbani nilimkuta Ema naye akiwa amefika lakini inaonekana Headmaster alikuwa amemgombeza sana maana alikuwa amevimba kama chura!.
Sasa kumbe jamaa alikuwa ameagizwa damu ya ng’ombe,na yule mzee niliyemkuta pale nyumbani wakati mimi natoka senta kuuza miwa alikuwa mganga,hivyo alikuja kwa ajili ya kufanya zindiko pale nyumbani.Wakati wa asubuhi kumbe Headmaster na mkewe walidamka kwenda kijiji kingine kwa ajili ya kumleta huyo mtaalamu na kiboko ya wachawi kama alivyojinasibu!.
Tulitakiwa kila mtu kuvua shati na kupigwa chale kichwani,mgongoni na kwenye mbavu!,basi lile zoezi lilipokamilika kuna dawa huyo mganga akawa ameichimbia katikati ya nyumba na kututaka kila mmoja kukaa kwa matako huku tukiangalia mashariki na kisha kutamka maneno aliyokuwa akituelekeza!.
Baada ya kumaliza kufanya vimbwanga vyake akawa ameaga ya kwamba aondoke na sisi tukae kwa amani huku tukisubiri kuona matokeo!.
Sasa usiku wakati tukiwa tumelala Ema akawa ananiambia.
Ema “mwanangu unajua nilipita kwa Deborah”
Mimi “Muda gani?”
Ema “Si wakati Headmaster ameniagiza”
Mimi “Kumbe ndiyo maana tumepishana”
Ema “Headmaster naye mnoko tu!”
Mimi “Kwanini?”
Ema “Mwanangu amenitukana kishenzi?”
Mimi “Ni-kupiga kimya tu,sasa utafanyaje”
Ema “Mwanangu halafu debo aneniambia yule mtoto ameeleweka”
Mimi “Nani,Mwise au?”
Ema “Si alikwambia atakupa rafiki yake!.”
Mimi “Daaah mi nikajua Mwise”
Ema “Mwanangu yule sura mbaya kakuroga nini!,mbona unampenda hivyo”
Mimi “we acha tu!”
Ema “Halafu lile mbona jepesi tu,wewe subiri kesho shule”
Basi tulilala siku hiyo na hakukuwa na mauzauza hata kidogo.Kutokana na yale mauzauza pale nyumbani ilifika sehemu tukayaona niya kawaida kabisa!.
Kulipopambazuka kama kawaida niliamka nikajiandaa na kwenda kuwasalimia Headmaster na mkewe kisha nikaondoka zangu kwenye kibarua cha uuzaji wa miwa.
Sasa siku hiyo ilipofika mida ya saa 10 jioni nilimuona Ema akiwa anakuja na yule binti mwenye shepu iliyokuwa ikiichanganya nafsi yangu akifahamika kwa jina la Mwise,baada ya kuwaona kwa mbali nilianza kuufuta mdomo wangu ambao ulikuwa umetapakaa uchafu wa miwa na ndipo nikakaa sawa sawa kumkabili Mwise!.
Ema “Ooya demu wako huyu hapa bhana nimemleta akusaidie kuuza miwa”.
Ema alivyokuwa mpumbavu alikuwa ananiambia halafu anacheka!,daah nilisikia uchungu wa aibu lakini ningefanya nini?,basi baada ya jamaa kumfikisha yule demu pale aliondoka akaelekea kibandani kwa Maza mdogo ili sisi tuendelee na mazungumzo.
Kiukweli yule binti nilikuwa nampenda ingawaje alionekana sura haivutii.
Sasa nikawa najiuma uma pale hata cha kumwambia nikakosa,nashukuru yeye alikuwa mcheshi na akawa amenianza!.
Mwise “Hivi wewe ndiye unakaaga pale kwa Headmaster eeeh”
Mimi “Yeah ni mimi,yule ni baba yangu mdogo”
Mwise “oooh,kumbeee”
Mwise “Mmh niambie sasa maana nataka kuwahi nyumbani”
Mimi “kwani Ema hajakwambia?”
Mwise “Huyo mjinga amenitoa nyumbani hata hajaniambia chochote”
Mimi “Lini utapata muda nina maongezi na wewe”
Mwise “jamani muda wenyewe ndiyo huu,wewe niambie tu”
Mimi “Unaitwa nani?”
Mwise “Ina maana Ema hajakwambia jina langu?”
Mimi “Ema hajaniambia”
Mwise “Naitwa Mwise”
Mimi “ooh Mwise,unajua mimi nakupenda”
Mwise “ndo hicho tu ulitaka kuniambia?”
Mimi “Yes,ndi hicho tu”
Mwise “Sawa mimi naondoka”
Basi yule binti akaondoka huku nikiendelea kumtazama anavyotingisha dunia kwa msambwanda wake aliyotunukiwa.Nilijiona mjinga na domo zege kwa kumbwelambwela kwa mwanamke niliyekuwa nikimtamani kwa muda mrefu!.
Haukupita muda Ema naye akawa amekuja pale huku akitaka kujua nini kimeendelea,niliamua kumdanganya Ema kwamba binti kakubali na ameniahidi tungeonana siku si nyingi kumbe haikuwa hivyo!.Basi tuliendelea kupiga stori hapo kijiweni na ilipofika mida ya saa 12 nilifunga mzigo nikapeleka kwa yule mama aliyekuwa akinihifadhia na mimi kuondoka na Ema kuelekea nyumbani.
Basi wakati tukiwa tunatembea kuelekea nyumbani huku tukipiga stori za hapa na pale,ghafla kwa mbele nikamuona yule binti Monica demu wa Ema akija akiwa na mabinti wenzie wawili!.
Mimi “Demu wako huyo anakuja”
Ema “Mkaushie,mi sikataki wala nini!”
Basi tulipowafikia yule binti akatusalimu,Ema aliuchuna lakini mimi nilimuitikia.Sasa Ema yeye akawa anaendelea na safari bila kujali,mimi nikaona isiwe kesi ngoja niongee nae.
Monica “Huyo mwenzako mbona asalamii”
Mimi “Mi sijui bhana”
Mimi “Unatoka wapi?”
Monica “Natoka kwa mama mdogo naelekea nyumbani”
Monica “Huyo ndugu yako tangu awe na huyo debora wake kiburi kimemjaa,ngoja tutaona”
Basi sikutaka kusema kitu ikabidi ninyamaze.
Monica “Njoo basi nyumbani leo”
Mimi “Itakuwa ngumu Monica”
Monica “Kwanini?”
Mimi “Sitoweza kutoka,wewe siunajua itakuwa usiku na nalala na Ema,nitaaga naenda wapi?”
Monica “Mimi nakupenda sana na wewe ndiye mama yangu anakufahamu ,usijali nakuja kukufata”
Mimi “Sasa ukija itakuwaje?”
Monica “Hilo niachie mimi,kwanza leo nyumbani kuna ngoma za mwana lemi,nakufata”
Mimi “Unajua inabidi iwe siri isifahamike”
Monica “Hata wakijua wewe ni mtu wangu,hakuna wakunitisha”
Monica “Naenda lakini narudi,hivyo kajiandae”.
Basi niliondoka nikawa namkimbilia Ema ambaye alikuwa amefika mbali.
Ema “Huyo mjinga anakwambia nini!”
Mimi “Nilikuwa tu namtuliza ili asijisikie vibaya”
Ema “Mimi sikataki ila kenyewe kutwa kunitafuta tu”
Basi kwakuwa hakujua nilikuwa namtafuna,sikutaka kabisa na mimi kumwambia chochote.
Ingawaje kale kabinti hakakuwa na ndundu(msambwanda)kama wa mwise,mimi nilikuwa ninapooza njaa tu!,sikutaka mambo mengi.
Sasa ilipofika mida ya saa 3 usiku,niliskia sauti ya Monica ikiniita nje,niliamka kujifanya najinyoosha na nilipomtazama Ema nilikuta amelala isivyo kawaida.
SEHEMU YA 14
Niliamka taratibu nikajifanya kumshitua jamaa ili nione kama alikuwa akisikia,nilitaka kama angenisikia basi nimwambie naelekea chooni!,sasa kwakuwa alikuwa amelala usingizi wa pono,niliamka nikafungua mlango taratibu kisha nikairudishia!.Nilifungua mlango wa nje taratibu nikatoka nikakuta yule binti Monica akiwa nje ananisubiri!.
Monica “Yaani muda huu mlikuwa mmelala?”
Mimi “Kwani saa ngapi sasa?”
Monica “Bado mapema sana”
Sasa muda huo ninazungumza naye ilikuwa yapata mida ya saa 5 usiku,sikuwa na saa lakini kwa makadirio sisi tuliingia kulala mida ya saa 3 usiku na baada ya yeye kuja ilikuwa imepita muda kidogo!.
Sasa kwakuwa nilikuwa tayari nishakuwa na hamu na papuchi,sikutaka kabisa kuwaza umbali tutakao tembea kwenda kwao,cha msingi ni mimi kufika na kumcharaza stiki za kutosha na kurudi mapema nyumbani.Kwakuwa mpaka muda huo hapo kijijini sikuwa kabisa na demu mwingine wa kuzugia ilibidi niwe mpole tu kwa yule binti ili angalau niwe napooza njaa ya mashine!.
Basi tulianza kutembea kwa haraka huku nikiwa nimemshika kiuno kana kwamba atanitoroka!.
Monica “Mimi nakupenda sana wewe umughaka,yaani sasa hivi najikuta tu nakupenda”
Mimi “Lakini Moni mimi na wewe tunaiba tu,Ema akijua najua tutakosana”
Monica “Wewe achana nae huyo,mbona yeye anatembea na Deborah”
Monica “Huyo mjinga nitamkomesha aliniambia atanioa kumbe alitaka kupata anachokitaka kwangu halafu aniletee dharau,hanijui vizuri binti Makoye”.
Aliendelea kusema “Nilikwambia leo nyumbani kuna ngoma za mwana lemi,ndo maana nimekuja kukuchukua”
Mimi “Ngoma za mwana lemi ndiyo ngoma gani?”
Monica “Wewe twende tu utaona”
Monica “Tukifika nyumbani utafanya kila nitakachokuambia lakini,sawa?”
Mimi “Sawa”
Sasa mwanaume nikadhani ile kuniambia nitafanya kila atakachosema ilikuwa ni kumbadili kila style wakati wa mizaguamuano,moyoni nilifurahi sana na nikawa nina shauku ya kufika nyumbani kwao haraka ili nikaikung’ute papuchi mpaka ichakae!.
Mimi “Mama yako yupo?”
Monica “Yupo ila atakuwa bize kwenye ngoma”.
Basi tulitembea kwa dakika kadhaa tu tukawa tumekaribia nyumbani kwao,nilipata mshangao sana kwakuwa haikuwa kawaida kwasababu nyumbani kwao ilikuwa mbali sana!,sasa nikawa najiuliza au kwasababu ni usiku na hakuna kashikashi njiani ndo maana tumefika mapema?,niliwaza pia siku ile nilivyokutana na Monica pale kwenye viwanja vya mnada na namna tulivyokwenda kwao haikuchukua muda mrefu,nilidhani uenda kwasababu ilikuwa usiku hivyo kujikuta unatembea kwa haraka kwasababu hakuna jua wala nini!.
Sikuwa kabisa na mawazo uenda yule binti anaweza kufanya namna yeyote kwasababu hakuwahi kunionyesha jambo lolote baya nala kutisha mpaka nimtilie shaka,isipokuwa ni ile siku moja tu ambayo nilimuona pale lamboni akichuma yale majani ya kutengeneza majamvi ndipo kama nilishangaa namna alivyotokea mbele yangu ghafla!.Basi nikajipa moyo kwasababu alikuwa ananipenda hata kama angekuwa ni mbaya asingenifanyia ubaya mimi.
Kabla ya kwenda kuingia ndani,aliniambia nimsubiri kwanza anarudi.Aliondoka akaenda akazunguka nyuma ya nyumba yao ambako kulikuwa na shamba la mihogo akaingia ndani!.Nilimsubiri pale kwa takribani dakika 5 hivi akawa amekuja na kimfuko cha rambo kilichokuwa kimefungwa ambacho sikufahamu ndani kulikuwa na nini!.
Monica “Chuchumaa chini”
Basi nikachuchuma chini,akakifungua kila kimfuko kisha akatoa vijifuko vingi vingi vilivyokuwa vimefungwa kwa kukazwa sana!.Sikumuuliza chochote nikawa nabaki kumuangalia anataka kufanya jambo gani.
Sasa kwakuwa lilikuwa giza totoro,sikuweza kuona mle ndani ya tule tujifuko tudogo tudogo kulikuwa na kitu gani.
Monica “Kama nilivyokwambia leo hapa nyumbani kuna ngoma,nataka nikupake hii dawa ili wakati wa ngoma usije kuonekana na wacheza ngoma wanaweza kukufanya kitu kibaya na mimi nitaadhibiwa”
Basi akilini mwangu nikasema uenda alitaka kabla ya mizagamuano tukacheze ngoma ya kisukuma iliyoitwa “Mwana lemi” kama alivyokuwa ameniambia hapo awali.
Basi alianza kunipaka ile dawa usoni,miguuni na mikononi na kuna nyingine akawa amenipa ili niirambe.Baada ya lile zoezi akaniambia tuondoke twende ndani!.Safari hii wakati tunaelekea kwenye kile kinyumba cha nyasi alichokuwa akilala Monica tulizunguka kwa nyuma ambako ilibidi kukanyaga matuta ya mihogo na kuingia ndani,ile siku ya kwanza kulala hapo nakumbuka tulipitia moja kwa moja mbele ya nyumba,ila safari hii imekuwa tofauti!.
Nilipofika ndani Monica aliniambia nikae kwa kutulia na kila atakachukuwa akiniambia basi nifanye.Alinisogelea karibu akanivua nguo zote nikabaki mtupu,alipomaliza alianza na yeye kuvua nguo zote,kwakuwa mle ndani kulikuwa na giza totoro hakuna aliyemuona mwenzie kiufasaha,sasa sikujua kama yeye alikuwa akiniona ama la!,alianza kunipaka dawa ambayo sikuitambua mwili mzima na alipomaliza alinipatia mkononi na mimi akasema nimpake,sasa wakati nampaka kufika kiunoni nikakuta amevaa shanga!,nilishangaa sana siku hiyo kumuona ana shanga kiunoni kwasababu siku ile ya kwanza hakuwa na shanga kabisa!.
Basi nikaendelea kumpaka ile dawa kuzunguka mwili mzima,wakati huo abdala kichwa wazi alikuwa amesimama akionyesha kuwa na kiu ya maji ya mdimu!.
Baada ya kumaliza lile zoezi,Monica akawa amenitaka nikae kwenye godoro.
Monica “Umughaka mimi nakupenda sana na nia yangu ni kukusaidia”
Mimi “Kunisaidia na nini Moni?”
Monica “Wewe unadhani uko salama?,hivi huwa hujiulizi kwanini wewe hayakukuti?”
Mimi “Ma nini ambayo hayanikuti”
Monica “Yaani wewe nae umezidi utahira,pamoja na kukueleza tu hujiongezi!”
Aliendelea “Subiri utajionea ila naomba usije kupiga kelele,sawa?”
Mimi “Sawa”
Basi wakati tukiwa mle ndani tukiongea,ghafla nikaona miale ya moto ikitokea nje,ilionekana kuna moto ulikuwa umewashwa,Sasa Monica akanifanyia ishara ya kwamba nifunge domo langu na nisishituke!.Baada ya muda nikaanza kusikia ngoma zinapigwa kwa nguvu huku sauti za kina mama na wanaume wakiwa wanaimba kwa kisukuma.
Zile ngoma zikaanza kukolea huku nikisikia vishindo vya watu kama wakiruka na kucheza!.Sasa baada muda kupita kidogo,Monica akanifanyia ishara ya kwamba nisimame nimsogelee alipokuwa,niliposogea ndipo akaniambia nichungulie kwenye upenyo wa ule mlango wa bati!.Sasa kile kinyumba kilivyokuwa kimejengwa kilikuwa cha mviringo kama simtank(nadhani waliokulia vijijini watakuwa wanazifahamu nyumba hizo),sasa kutokana na kile kinyumba kilivyokuwa kimejengwa,mlango wa kile kinyumba hata kama ungefungwaje,kwa juu kulikuwa na uwazi mkubwa uliowezesha kuchungulia nje na kuona kwa uzuri!.
Basi nikachungulia nje nikaona moto mkubwa mno ukiwa umewashwa pale mbele ya nyumba yao Monica,pia nikawaona watu wake kwa waume wakiwa uchi kama walivyozaliwa(uchi wa mnyama)wakicheza kwa kuzunguka mduara,mpiga ngoma alikuwa mwanaume ambaye yeye alikuwa pembeni kabisa,sasa wakati wakiwa wanazunguka ule mduara huku wakiimba ngoma,nikamuona mama yake Monica naye akiwa mmoja wao,nilipoendelea kutazama vizuri nikamuona na yule mzee ambaye nimewahi kukutana naye jioni wakati natoka Senta akanisalimia kisha akaniambia nimsalimie headmaster,nilipomuuliza jina akaniambia anaitwa Makono.
Pia ni huyu huyu mzee wakati wa kikao pale shuleni baada ya lile sakata la Ema na Maza kukutwa wamelala darasani ndiye aliyekuwa akichangia na akisema mambo ya ushirikina hayakuwepo hapo Kjijini.
Nikabaki nimekodoa macho na nikawa kimya kabisa,sasa baada ya zile ngoma kupigwa kwa sana na wao kuuzunguka ule moto,ghafla kuna mzee akapiga kelele kwa kisukuma akisema “Bhebheeeeeeee”,kisha mpiga ngoma akaacha kupiga ile ngoma na watu wote wakasimama.
SEHEMU YA 15
Kila mcheza ngoma alisimama ghafla na kumtizama yule mzee ambaye ilionekana kabisa alikuwa kiongozi wao.Baada ya hapo alinyoosha mkono juu akiwa ameshika usinga(mkia wa mnyama)ambao sikuweza kufahamu ulikuwa wa mnyama pori au mnyama wa kufugwa!.
Alipoteremsha mkono chini niliona watu wote wameweka mikono mbele kuonyesha unyenyekevu huku vichwa vikitazama chini.Sasa yule mzee alianza kuongea kwa sauti kubwa mno!.
Mzee alisema “Ng’wana Charles”
Aliendelea “Ng’wana ndekeja”
Baada ya kusema hivyo nikaona ananyoosha usinga kuwapa ishara hao aliowaita wasogee mbele,sasa nikaona wazee wawili wamesogea mbele huku wakiwa wameinamisha nyuso chini na mikono imewekwa mbele kuashiria unyenyekevu wa hali ya juu!.
Mzee akasema “Ng’wenagi umnho ng’wenuyo aha”
Basi wale wazee waliondoka na kuingia kwenye ile nyumba ya mama yake Monica,hawakuchukua muda wakawa wametoka ndani huku wakiwa wamembeba mtu ambaye sikumuona kwa haraka,sasa baada ya kumfikisha yule mtu na kumbwaga pale kando ya ule moto ndipo nikamuona vizuri nikawa nimemtambua!,alikuwa ni mzee ambaye alijinasibu ni mganga aliyekuja pale nyumbani kuweka zindiko na kutupiga chale za kutosha!.
Basi yule mzee ambaye ilionekana ndiye mkubwa pale akawa toa amri tena ya kuanza kupiga ngoma na kucheza!,sasa wakati wanacheza kwa kuzunguka ule moto,akajitokeza mama mmoja ambaye alikuwa amejifunga shanga kiunoni na kiremba cheusi kichwani huku mkononi akiwa ameshika kisu!,sasa akamsogelea yule mzee ambaye alikuwa akishanga shangaa kama tahira pale chini,yule mama akafika akamkamata kichwa akaanza kumyoa nywele!.
Wakati mambo yote hayo yanaendelea,mimi na Monica tupo tunachungulia kwenye ule upenyo wa mlango na Monica alinizuia kabisa kutopiga kelele!.
Sasa baada ya lile tukio la kumnyoa yule mzee nywele kukamilika,yule mama alichukua zile nywele akaziweka kwenye kitu kama sahani halafu akamkabidhi yule ambaye alionekana ni kiongozi,sasa wakati anamkabidhi kama kawaida uso uliinama chini kuashiria unyenyekevu!.Baada ya hapo yule mama akaanza kumvua yule mzee nguo zake zote!,alipomaliza aliinama chini kwenye akachukua vitu ambavyo sikuvifahamu akaanza kumpaka yule mzee!.Baada ya kumaliza lile tukio la kumpaka yule mzee vitu visisvyo julikana,akaondoka kinyume nyume kurudi kwenye mstari kuuungana na wenzie kuendelea kucheza ngoma.
Sasa haukupita muda yule mzee tena akatoa ishara ile ngoma ikasitishwa!,baada ya hapo ilikuwa kitendo cha kufumba na kufumbua wakawa wametoweka pale kwenye lile eneo na ghafla kukawa na giza kuu!,nilitaka kufahamu kiliendelea nini na hivyo ikabidi nimuulize Monica.
Mimi “Mbona hawaonekani?”
Monica “Unataka nikupeleke walipoelekea?”
Mimi “Hapana”
Monica “Nakupenda wewe sana ndiyo maana nimekuleta ujionee mwenyewe”
Monica “Mimi nitakulinda wala usiogope”
Aliendelea kusema “Wameelekea kwenye sherehe za kula nyama”
Monica “Ile miembe miwili mikubwa ya kwenye ile njia ambayo tumekutana si unaikumbuka?”
Mimi “Ndiyo”
Monica “Ndo wako hapo”
Mimi “Sasa hapa wameondokaje?”
Monica “wewe bado mdogo ukikuwa utaacha kuuliza uliza maswali”
Sasa nilikuwa nashangaa binti anayeniambia mimi mdogo nabaki kumshangaa kwasababu ulikuwa ukiniangalia mimi na yeye utajua kabisa yeye ndiye mdogo!.
Monica “Halafu wewe una mizimu mikali sana ndiyo maana nataka uwe mume wangu”
Mimi “Mizimu mikali?,mizimu mikali kivipi?”
Monica “Umekuwa ukiwasumbua sana wanapokuwa wakila nyama zao”
Nikashituka sana nikabaki nashangaa mle ndani ambako mpaka muda huo kulikuwa na giza totoro!.
Monica “Unakumbuka siku unapita pale kwenye miembe usiku uliona nini?”
Mimi “Nakumbuka kuna siku nilikuwa natoka senta kuangalia mpira nikaona moto unawaka kwenye ile miembe”
Monica “Achana na mambo ya moto,wewe hukuwahi kuona mtu pale?”
Aisee,sasa nikawa najiuliza huyu binti matukio yote hayo yeye alionaje?,kiukweli nilianza kuingia uoga ila akawa ananisihi ya kwamba nisiogope na yeye yupo kwa ajili ya kunisaidia!.
Monica “Yule mtu uliyemuona siku ile aliliwa nyama,sasa wewe umekuwa ukiwasumbua kupita ile njia kwasababu hakuna mtu anayepita ile njia usiku kama ule”.
Aliendelea kusema “Kwa ujasiri ulionao waliona wakujaribu kuona kama unawaona na ndiyo maana walikutega na kukutisha na ulivyotishika na kukimbia wakaona kumbe huna lolote”
Mimi “Sasa nawatesaje?”
Monica “Pale kwenu ni wewe ndiye ambaye huwezekaniki na sijui kwanini,wewe unanyota nzuri mno”
Mimi “Yule mganga amefanya kosa gani”
Monica “Yule ni mjeuri,anaenda kuliwa nyama”.
Akaendelea kusema “Kuna siku mama yangu alienda kusenya kuni na mlikutana njiani ukamsaidia zile kuni,hivyo mama yangu akakupenda sana”
Mimi “Mbona sikumbuki siku ambayo nimebeba kuni za mama yako?”
Monica “Wewe bado mtoto mdogo nimekwambia acha maswali utaelewa tu”.
Kiukweli nilikuwa ninawaza na kujiuliza sana lakini nakosa majibu!,ndipo sasa nikajua uenda matukio mengi pale nyumbani yalikuwa yanasababishwa na hilo kosi hatari lilikuwa likicheza ngoma,sikutaka kumwambia mama yake ni mchawi ingawa nilimshuhudia kwa macho yangu,nilidhani uenda ningemwambia kuhusu mama yake angenibadirikia mle ndani na nikaipata freshi,sikutaka kabisa kutengeneza matatizo!.
Baada ya maongezi ya muda mrefu mizagamuano ikachukua nafasi!,sasa nikawa nimemwambia Monica inapaswa baada ya mizagamuano ikifika saa 10 usiku anisindikize kurudi nyumbani ili asije akajua mtu yeyote kwamba nilitoka usiku.
Monica “Nalekotogwa natokoreka”
Mimi “Ndiyo nini?”
Monica “Wewe naye,utajifunza lini kisukuma!”
Monica “Nakwambia nakupenda na sitokuacha”
Basi sikutaka kumjibu na mimi akili yangu haikuwa kwake kabisa,kilichokuwa kinanipeleka kwake ni kumpatia maji ya uzima wa milele abdala kichwa wazi ili asihangaike na kiu.
Basi baada ya kasi ya mizagamuano ni kama Monica alipitiwa na usingizi,mimi sikuweza kabisa kupata usingizi kwasababu ya kile nilichokuwa nimetoka kukishuhudia pale!.
Sasa baada ya muda kupita nikiwa natafakari huku usingizi ukianza kunipitia,ghafla nikasikia kishindo kikubwa nyuma ya ile nyumba tulimolala!,sasa nikajaribu kupeleka mkono ili nimpapase Monica ashituke ili na yeye asikie lakini hakukuwa na mtu kwenye godoro!.
Nilikurupuka nikaanza kupiga kelele za uoga kama mwehu!
INAENDELEA……..