TULICHOMFANYA YULE MCHAWI HATAKUJA KUSAHAU KAMWE
SEHEMU YA 6
Haukupita muda ba’mdogo akawa amerudi ndani na kusema amejaribu kutazama kila pembe ya lile jiko hakuona mbuzi.Sasa tukawa tunajiuliza yule mbuzi alikuwa akilia mle ndani ya jiko au alikuwa akililia nje?,mashaka na hofu viliendelea kutawala sana.
“Naona hawa wajinga wanataka tena kurudia mambo yao” Alisema ba’mdogo.
“Hizi dalili siyo nzuri kabisa za kuendelea kuishi hapa,haya mambo yalinitesa sana kipindi fulani ila yalikoma,naona sasa yanaanza kurudi” Aliendelea kusema.
Tulikaa macho kiasi kwamba mpaka kukapambazuka mida ya saa 11 alfajiri.Sasa Ema nae akawa anajigeuza geuza akiugulia maumivu ya kipigo alichokuwa amepokea usiku.Ilipofika mida ya saa 1 asubuhi headmaster alielekea shuleni akisema angewahi kuja ili aelekee kwa mwenyekiti wa kijiji kutoa taarifa uenda ingesaidia kama mwanzo.
Mimi niliendelea na shughuli zangu za kawaida hapo nyumbani,sasa wakati nikiwa nje jamaa akawa ametoka anachechemea akaenda kukaa kwenye jiwe akawa anaota jua!.
Nilimsalimia lakini aliitikia kama vile hataki,sasa nikawa namdodosa ajaribu kunieleza usiku ilikuwaje mpaka kufikia kuning’inizwa kwenye makenji ya darasa,Jamaa alikuwa anasonya tu!,niliendelea kumsihi ajaribu kunieleza lakini akaendelea kukaa kimya!.
Baada ya kuona ana kiburi nilimuacha nikaendelea na mambo yangu.Ilipofika mida ya saa 5 headmaster alirudi pale nyumbani akiwa na wazee wawili ambao sikuwafahamu.
Sasa akaniita akaniambia “Hebu mwambia huyo aje hapa”
Nikatoka nje nikaenda kumuita jamaa aliyekuwa amejianika juani kama kibambala.Baada ya jamaa kuingia ndani ikabidi na mimi sasa nisogee karibu ili nisikie umbeya maana nilivyojaribu kumwambia aligoma kuniambia.
“Dogo mwenye ndo huyu hapa mwenyekiti” alisema ba’mdogo.
Aliendelea “yaani jana hatujalala kabisa”
Mwenyekiti “Eti wewe!,hebu tuambie ni nini kilikupata”
Ema “Mi sijui chochote,nilishituka nikaona nimefungwa juu ya mbao huku nikipigwa”
Mwenyekiti “Waliokuwa wanakupiga uliwaona?”
Ema “Hapana”
Ba’mdogo “Yaani ni hatari mwenyekiti,nadhani nilikueleza haya mambo ya kiendelea mi nitaondoka”
Mwenyekiti “Sasa mwalimu Wambura utaondoka halafu watoto wetu nani atawafundisha!?”
Ba’mdogo “Siwezi kuendelea kukaa hapa wakati unaona kabisa huu ni ushirikina”
Mwenyekiti “Sasa rafiki wakati wanakupiga hawakusema chochote?”
Ema “Mi wakati wananichapa nilikuwa nasikia wanacheka na nilikuwa napigwa na watu wawili,maana alipokuwa ananipiga huyu na mwingine pia ananipiga”
Mwenyekiti “Hebu toa shati nione”
Ema alivua shati alilokuwa amevaa akamgeuzia mgongo yule mwenyekiti.Ema hakuwa na majeraha lakini mgongo ulikuwa umeumuka kama andazi.
Mwenyekiti “Mwalimu hebu tuteremke na huyu kijana senta akapate dawa pale kwa Malimi”
Basi baada ya maongezi yalichokuwa takribani nusu saa waliondoka wote kuelekea huko Senta.Siku hiyo ilikuwa ngumu sana na sikutaka kabisa kuzurura hovyo,ilipofika mida ya saa 10 alasiri nilichukua zangu dumu nikaelekea lamboni kuchota maji ya kuoga.Usiku wa siku hiyo jamaa hakulala kabisa,japo alikuwa akijifanya mbishi lakini ilibidi arudi kitandani kulala maana aliona angeendelea kulala chini yangemkuta kama ya usiku ulokuwa umepita.
Sasa hali ya mambo ikawa shwari kwa siku kadhaa na yale mauzauza hatukuyaona.
Nakumbuka siku moja mida ya saa 11 jioni headmaster akiwa amerudi nyumbani,alinituma niende Senta nikanunue betri za redio,sasa wakati naondoka sikutaka kabisa kupita njia ya ile miembe kwasababu nilianza kuingiwa na hofu,ilinibidi nizungukie njia ya kwenye lambo japo ilikuwa ya mzunguko lakini ilikuwa salama kabisa.Sasa wakati nikiwa napita kando kando mwa lambo nikama nilimuona yule binti aliyekuwa na Ema pale kwa rafiki yake Jackson ule usiku wa varangati la yeye na Deborah.
Wakati namtazama alikuwa anachuma yale majani marefu huwa yanaota kando kando mwa maji yanayotumikaga kutengenezea majanvi.
Sasa wakati navuta taswira huku nikigeuka nyuma kumtazama ili nimpe hai!,ghafla sikumuona,nikashituka ikabidi nisimame nitazame vizuri,kweli hakuwepo.Sasa ile nageuka zangu mbele niendelee na safari ya kuelekea senta nikakutana naye uso kwa uso akiwa amejitwisha yale majani kichwani!,kiukweli niliogopa sana na nikajikuta nimepiga kelele “Mamaaaaaaa”.
Ili kuondoa aibu ya kiume,nikajifanya “Umenishitua”.
Yule binti akaanza kucheka huku akiniambia “kumbe na wewe shemeji yangu ni muoga hivo eeenh”.
Mimi “vipi lakini”
Yeye “freshi”
Mimi “Huonekani”
Yeye “Mi nipo,ndugu yako hajambo?”
Mimi “Yeye mzima”
Yeye “Wapi mbona upo spidi?”
Mimi “Naelekea senta mara moja”
Yeye ” sawa shemeji tutaonana,ngoja niwahi nyumbani kupika”
Niliondoka nikiwa namtazama yule binti lakini sikummaliza hata kidogo,nilijiuliza maswali mengi sana ambayo kiukweli sikupata majibu.
Basi nilifika Senta nikachukua nilichokuwa nimekifuata na kurudi zangu nyumbani.
Nilipofika nyumbani baada ya kukabidhi zile betri kwa Headmaster nilirudi kule kwenye chumba chetu,sasa safari hii jamaa akaanza kuongea na mimi kwa furaha sana,sikujua ile furaha alikuwa ameitoa wapi maana kwa siku kadhaa alikuwa ameninunia kama mwanamke.
Ema “Baadae nataka unisindikize kwa debo kaka”
Mimi “Kuna nini?”
Ema “Tulipo onana shule aliniambia niende kwao baadae”
Mimi “Mlishayamaliza?”
Ema “Tuliyaongea yakaisha kaka”
Mimi “Sasa baadae ya saa ngapi?”
Ema “Tusubiri kwanza headmaster akilala tuondoke”
Mimi “Haitakuwa noma?”
Ema “Hapana,huwa akiingia kulala ni mpaka asubuhi”
Mimi “Sawa nitakusindikiza”.
Kweli,baada ya kupata msosi wa usiku,tuliingia ndani kwenye chumba chetu na headmaster alifunga mlango wa sebuleni akaingia chumbani kwake.
Sasa ilipofika mida ya saa 3 ikabidi jamaa anaimbie tusepe.Kule kijijini kutembea usiku ilikuwa ni kitu cha kawaida sana,kulikuwa hakuna majambazi wala vibaka,changamoto ya kule ilikuwa hayo mambo ya kishirikina.
Tukiwa njiani tuelekea kwao debo,nikamwambia jamaa nilikutana na demu wake alikuwa anamsalimia.
Mimi “Hivi huwa mnasoma nae?”
Ema “Kale kademu nilionana nako pale mashineni siku moja nikienda kusaga”
Mimi “Ooh sawa,nikajua labda ni kanafunzi”
Ema “Halafu siku ile nilikaambia kaondoke kakawa kanang’ang’ania kulala kaka”
Mimi “Kwahiyo baada sisi kuondoka ulilala nako mpaka asubuhi?”
Ema ” Niliamua kulala nako kaka,yaani huwezi amini siku ile Deborah nilikuwa namuona kama mavi pamoja na uzuri wake wote”
Mimi “Inaonekana kalikupa vitu ambavyo debo hajawahi kukupa”
Baada ya kumwambia hivyo jamaa akaanza kucheka sana huku akiniambia “Hamna kaka ni kawaida tu”
Mimi ” Huwa anakaa wapi?”
Ema “Anakaa kule Masairo”
Sasa baada ya jamaa kuniambia hiyo sehemu inayoitwa masairo na nikipiga umbali niliomkuta yule binti pale lamboni nilibaki nimechoka,hiyo Masairo aliyoniambia jamaa kutoka tu hapo senta mpaka hapo masairo si chini ya kilometa 7,sasa vuta picha kutoka pale lamboni ambapo ilikuwa jirani na shule mpaka huko masairo,kiukweli ilikua ni mbali mno kikawaida tena kwa mtoto wa kike ndipo nikabaki najiuliza maswali yasiyokuwa na idadi.
Sikutaka kumwambia jamaa kile nilichokuwa nimekiona pale lamboni wakati ule,ilibidi nikaushe ili niendelee kujifanya bwege stori zinoge.
SEHEMU YA 7
Tulitembea kwa muda kidogo hatimaye tukawa tumefika kwao Deborah,sasa tulipofika mbwa walianza kubweka sana,kwakuwa jamaa alikuwa akifahamika pale,aliwapigia wale mbwa mruzi hatimaye wakawa wanamfuata wakitikisa mikia.
Tulisonga mpaka kwenye kile kinyumba alichokuwa anakaa debora na mdogo wake,sasa kwa muda ule alikuwa debora mwenyewe na yule mdogo wake nadhani alilala nyumba kubwa.Ema alianza kugonga mlango hatimaye binti wa watu alifungua!.
Ema “Ulikuwa umelala?”
Debo “mmh” aliitikia huku akipiga miayo.
Basi nilimwambia Deborah aniletee kiti mie nikae kwa nje kama wao walikuwa na mazungumzo marefu,Debo akanitaka niingie tu ndani!.Basi niliingia ndani hatimaye taa ya chemri ikawashwa,sasa kwakuwa hakukuwa na mazungumzo yeyote ya maana,mimi ilibidi nijiongeze nitoke nje ili jamaa achakate papuchi.
Nilitoka nje nikakaa kwa muda kama saa nzima.Walipotoka ili kupotezea nikajifanya kama najipigisha mruzi wa uongo na kweli ili kupotezea.Nilimuona jamaa ni mshamba sana kwasababu hawezi kunitembeza usiku wote huo kisa tu yeye anakwenda kuchakata papuchi kwa demu wake,nilichukia sana lakini ikabidi nivunge tu.Mimi nilidhani wanakwenda kuzungumza vitu vya maana ambavyo ilinipasa niwepo ili nitoe ushauri kumbe ilikuwa ni uchakataji wa papuchi.
Basi bana hatukumaliza muda debo akawa anatusindikiza,sasa tulipotoka nje ya fensi ya miti ya boma lao ilibidi nimgusie kuhusu yule binti ambaye nilimuona lamboni akiwa anafua.Sasa baada ya kuwa nimempa specifications za namna yule binti alivyo,debo alicheka sana.
Debo “Jamani shem,mwanamke gani yule sasa”
Ema akadakia “Kwani ni nani?”
Debo “Si yule Mwise!”
Ema “Wewe umejuaje ni Mwise?”
Debo “Sasa ni nani Pale shuleni mwenye matako makubwa kama siyo Mwise?”
Basi kwa namna nilivyomuelezea Debora namna yule binti alivyo alikuwa ameshamfahamu kabisa.Sasa mimi kiukweli yule binti nilitokea kumtamani sana kulingana na umbo lake namna lilivyokuwa,kiukweli sura ilikuwa ya baba yake(mbaya) lakini umbo lilikuwa la mama yake(zuri),Kuhusu sura kwangu haikuwa tatizo,mimi nilichotaka ni kuchakata papuchi tu!.
Debo “Shem yule hata hakufai,hata hamuendani!”
Mimi “Shem mbona yupo freshi tu!”
Debo “Yaani ulivyo smati hivyo utembee na yule binti?,hapana kwa kweli”
Debo “Wewe usijali shem mimi nitakupa rafiki yangu,ni mzuri kweli nahisi utampenda”
Basi kiukweli yale maneno ya Debo ni kama yalitaka kunikata stimu lakini moyoni bado tamanio langu ni kuwa na mtoto Mwise matako makubwa maana ndivyo vitu nilivyokuwa nikivipenda kwa miaka hiyo!.Kweli,baada ya yale mazungumzo tuliondoka kurejea nyumbani kama kawaida,hiyo ilikuwa yapata saa 5 usiku.
Sasa kuna siku mwanakijiji mmoja alileta Jogoo mkubwa pale nyumbani,kama nilivyosena hapo awali ya kwamba,pale kwa Headmaster wakati ule kila siku alikuwa analetewa kidumu cha maziwa fresh cha lita tano na kila wikiendi alikuwa akiletewa kuku na wanakijiji tofauti tofauti,hii ilikuwa ni kama bonasi ya Mwalimu mkuu kwasababu ile shule ilikuwa ikifanya vizuri kimasomo.Sasa wikiendi hiyo headmaster hakwenda mjini kama kawaida yake,nilimchinja yule Kuku na hatimaye mchana tukawa tume mla tukabakiza mboga ya usiku.
Baadae mida ya mchana saa 8 ba’mdogo akasema anashuka senta na baadae angerudi na mama mdogo kwasababu walikuwa wanatokea mjini kuja hapo kijijini,hivyo akasema angekaa huko mpaka mida atakayompokea mke wake waje nae.Pale kijijini kulikuwaga na gari aina ya Hiace ambayo ilikuwa ikitoka mjini inalala hapo na kesho yake inaondoka,hivyo kama ulikuwa unakwenda mjini na hiyo gari ikikuacha basi inakubidi uhairishe safari.
Ba’mdogo “Hiyo mboga muiche kwa ajili ya wageni,nyie chambueni dagaa ambazo mtalia ugali usiku”
Mimi “Sawa baba”
Basi bana huo mchana nikaingia zangu kupumzika,Ema yeye alikuwa ameenda madarasani huko kusoma na wanafunzi wenzie.Ilipofika saa kumi na moja nikaanza kutengeneza dagaa kwa ajili ya kitoweo cha usiku.
Ilipofika saa 12 niliwasha jiko ili sasa nipashe yule kuku tuliyemla mchana halafu baada ya hapo nipike wale dagaa.
Nimeenda kuchukua sufuria ile ili niweke kwenye jiko nakuta ni nyepesi mno,kufungua mfuniko na kutazama ndani nakuta mboga hamna,ilikuwa ni mifupa tu inanikodorea macho!,yaani hata mchuzi ulikuwa umelambwa wote!.Nilishituka sana na nikajiuliza hiyo mboga ni nani atakuwa amekula?
Nilitoka nje ili niende pale darasani kumshitua Ema kumuuliza yawezekana yeye ndiye aliyekula ile mboga ili headmaster atakaporudi aweze kujibu.
Sasa wakati nakwenda kule madarasani nikamuona na yeye akiwa anakuja.
Mimi “Ndo mnatoka?”
Ema “eeenh ndo tumemaliza pindi”
Mimi “Yule kuku ulimla wewe?”
Ema “Kuku?,kuku yupi?”
Mimi “Si ile mboga tuliyokula mchana”
Ema “Kwani imekuwaje?”
Mimi “Aiseee twende ukajionee mwenyewe”.
Basi tulipofika ndani moja kwa moja jikoni.
Ema “Daaaah sa nani kala?”
Mimi “mimi sijui,nimelala mchana nikaamka ili niipashe ndo kama unavyoona”.
Mimi “Na dingi alisema anakuja na mama mdogo,sasa sijui itakuaje maana alisema kuku tuache kwa ajili ya mgeni na sisi tupike dagaa”
Tuliendelea kutazamana pale tusijue cha kufanya.Nilimwambia Ema tutamwambia dingi kilichotokea lakini Ema ni kama alisita sana.
Ema “Wewe headmaster humjui vizuri,usione anakuchekea hapa ukamfanyia utani,niulize mimi”
Mimi “Yule ni baba yangu mdogo na nina mfahamu vema,sasa kama hatujala sisi tufanyeje?
Ema “Yule hawezi kuamini kaka”
Ema “Sikiliza,mimi ngoja nikimbie kwao Debo nimwambie anikamatie kuku tuje kuchinja,vinginevyo itakuwa hatari”
Mimi “Mbona kama muda umeenda sana,na wao nadhani wanaweza kuwahi kurudi”
Ema “Headmaster namjua,hawezi kurudi saa hizi,hapo mpaka ngoma tatu ndo unamuona hapa na mkewe”
Basi jamaa ilibidi aondoke anakimbia kwenda kwa demu wake kufata kuku wakuja ku-replace.Kiukweli ile hali haikuwa ya kawaida kabisa,pamoja na vile vitisho lakini wanaume bado tuliendelea kukomaa!.Ilipofika mida ya saa moja usiku nilikuwa nikismubiri jamaa lakini sikuona,sasa baada ya kupika wale dagaa na jamaa alikuwa haonekani,niliona nikimbie nimfuate,nilisema yawezekana alipofika kwa demu wake uchakataji ukaanza akasahau mambo ya kuku.
Nikafunga mlango nikaondoka zangu,nimetembea sana bila kukutana na jamaa njiani,nilikuwa nimekasirika sana na hakuna siku niliyomuona jamaa ni mpumbavu kama siku hiyo,sasa nimefika kwao Deborah nakuta jamaa amekaa kwenye kiti tena amekunja kabisa nne.
Mimi ” Sasa ema umefika tena umekaa?”
Ema ” Hapana kaka sijakaa kama unavyodhani,Deborah amesema anampika kabisa ili tukifika sisi ni kusonga ugali tu kaka”
Basi ikabidi nikae tusubiri huyo kukua aive,kiukweli nilikuwa nimechukia sana kwa namna jamaa ambavyo alikuwa hachukulii vitu serious!.
Sasa tumekaa pale mpaka mida ya saa tatu usiku ndipo kuku akawa ameiva,nilikuwa nawaza tukimkuta dingi kafika tutamueleza tulikuwa wapi!.
Baada ya Deborah kutukabidhi yule kuku kwenye hotpot tukaanza mwendo wa kutembea haraka kuwahi nyumbani,sasa cha ajabu tulitembea sana lakini tukawa hatufiki,Aisee kiukweli wasukuma nawanyooshea mikono.
Yaani fikiria tunatembea lakini kila tukiangalia hatufiki,sasa nikamwambia jamaa “hebu tusimame kwanza”.
Mimi “Isije kuwa hii njia tumeichanganya Ema”.
Ema ” Kaka njia ndiyo hii”.
Mimi “Mbona sasa tumetumia muda mrefu sana?”
Jamaa akaniambia “twende nzetu tutafika kaka,najua una kimuhe muhe cha dingi yako”.
Jamaa alikuwa anafanya masihara lakini kiukweli tulipiga sana makitaimu.
Sasa wakati tunatembea hatuna hili wala lile,tukasikia sauti nyuma yetu ikiita “Emaaa mpenziiii”.
Aiseee sitakuja kuisahau ile siku,kila mtu alipita chocho lake na tulikutana nyumbani asubuhi.
SEHEMU YA 8
Niliruka nikaingia kwenye shamba la mahindi ambayo bado yalikuwa madogo kiukweli nilikimbia sana na sikufahamu nilikuwa naelekea wapi!.Nilifika sehemu ambapo kulikuwa na kimlima ikabidi nisimame nishike magoti huku nikiwa nahema kama mbwa!.Sasa akili iliporudi nikaanza kujiuliza hivi nilichokuwa nina kimbia ni nini?,kwanini nikimbie kama labda nimeua mtu?,lakini pia aliyefanya na mimi kukimbia alikuwa Ema baada ya kushituka akaanza kukimbia ndipo na mimi kuitafuta njia yangu!.
Basi nikaanza kuteremka kurudi nilikotoka,nilitembea kwenye yale mashamba usiku ule bahati nzuri hakukuwa na giza kubwa ambalo lingezuia mimi kutazama vizuri!,nilijaribu kuitafuta njia ya kuelekea nyumbani lakini sikuweza kuifahamu maana nilikuwa nimekimbia umbali mrefu!.Sasa wakati natembea ili kulitafuta barabara kuu ambalo pengine lingenipa muongozo wa kuelekea nyumbani,mara ghafla nikasikia watu zaidi ya mmoja wakiwa wanakuja wanazungumza,ikabidi nilale chini ili wasinione maana ilikuwa usiku pengine kuhisi mimi ni mwizi!.Wale watu walipita walikuwa wakizungunza mambo yao tu kwa lugha ya kisukuma,nilipoona wamefika mbele na mimi sasa nikaanza kuwafuata kwa nyuma nikisi uenda ile njia ingenirudisha mpaka mahali ambapo nilikuwa napatambua ili iwe rahisi kufika nyumbani.
Sasa niliendelea kutembea lakini nikawa naona kabisa naelekea kwenye mazingira ambayo sikuwahi kufika,ikabidi nisimame huku hofu ikitanda,kumbuka mida hiyo ilikuwa yapata saa 4 kuelekea saa 5 usiku.Ikabidi nirudi tena na ile njia,nimetembea sana na hofu ilipokuwa ikizidi nikaanza kukimbia huku napiga mruzi wa uoga ili kujipa matumaini hata kama kuna kitu kibaya basi kiogope.
Ile njia ilinipeleka mpaka kwenye uwanja mmoja ambao ulikuwa ukifanyika mnada kila tarehe 15 ya kila mwezi,nilipofika hapo niliweza sasa angalau kupata picha uelekeo wa nyumbani.Sasa nikatembea ili niende kukamata njia ya uelekeo wa kule lamboni ambako kungenipeleka moja kwa moja hadi nyumbani.
Sasa wakati natembea nikasikia sauti ya kike ikiimba nyimbo kwa lugha ya kisukuma,nilipogeuka kwa mbali kidogo nikaona huyo mtu akawa anakuja uelekeo niliokuwa nikielekea mimi,sikuwa na hofu nilijua ni mpita njia kama mimi.Sasa wakati natembea na yule mtu naye anakuja kwa kasi,alipofika karibu yangu ndipo kumtazama vizuri alikuwa yule binti demu ya Ema,akajifanya kama hajaniona!.
Sasa moyoni nikawa najiuliza,kwanini kila mara mimi hukutana huyu binti?,na mazingira ninayokutana nae siyo mazingira rafiki hata kidogo.
Akanipita na kiukweli sifahamu kama hakuniona au aliniona ila akaamua kuuchuna!.
Mimi “Shem!” Niliita kwa nguvu.
Akasimama akageuka.
Binti “Aah shem,kumbe ni wewe”
Mimi “Unaenda wapi usiku wote huu?”.
Binti “We acha tu,mama aliniagiza mahali ndiyo narudi”
Mimi “unawezaje kutembea usiku hivi tena uogopi?”
Binti “Nikuulize wewe maana sisi huku vijijini tulishazoea”
Kale kabinti siyo kwamba kalikuwa kabaya sana,La hasha!,kiukweli kama huna hili wala lile kalifaa kuzugia kwa hapo bushi.
Binti “Mbona upo mwenyewe,mwenzio yuko wapi?”
Mimi “Yuko nyumbani”
Binti “Na huku unatoka wapi?”
Mimi “Kuna mgeni natoka kumsindikiza ndo narudi nyumbani”
Baada ya kukadanganya hivyo mara ghafla kakaanza kucheka sana na kile kicheko hakika kilikuwa cha dharau,na kiukweli sikuelewa maana yake nini.
Binti “mmmh sawa bana utamsalimia mwenzio”
Mimi “Mbona lakini unacheka?”
Binti “Nacheka kwasababu nakuhurumia wewe mwenyewe unawezaje kutembea usiku huu hapa kijijini tena ukiwa mgeni!”
Sasa baada ya kusema maneno yale mara ghafla tamaa ya ngono ikanijia usiku ule na kichwani nikawaza kwakuwa tulikuwa wawili tu yale maeneo ndipo ilikuwa nafasi ya kukadanganya ili kanipatie papuchi nipunguze ugwadu wa muda mrefu.
Mimi “lakini unajua mwenzio huwaga Nakupenda”
Binti “Jamani wewe sini shemeji yangu lakini!”
Mimi “Sawa!,lakini kwani nani atajua!?”
Binti “utaniweza lakini?”
Mimi “nitakuweza,wewe nipe tu japo kidogo hakuna atakayejua”
Yule binti tena akaanza kucheka vilevile kwa dharau ya hali ya juu na sikuelewa lile cheko kwa wakati ule lakini kwa baadae nilikuja kufahamu ni kwanini alikuwa akicheka vile.
Basi nikakasogelea nikaanza kukashika pale huku mimi wakati huo abdala kichwa wazi ametuna kama kijiti!.
Binti “Kwanini tusiende nyumbani kwetu”
Mimi ” kwenu ni mbali,wewe tufanye tu hapa kidogo halafu kila mtu aondoke kwao”
Binti “Aliyekwambia kwetu mbali ni nani?”
Mimi “Kwenu sini kule masairo?”
Binti “Jamani,sasa hapo Masairo kwani ni mbali?”.
Sasa wakati yeye anasema si mbali,kumbuka pale tulipokuwa nikipiga umbali wa kutoka hapo mpaka kwao,si chini ya kilometa 4 lakini binti anakwambia si mbali.Basi kwakuwa nilikuwa nina hamu ya kuchakata papuchi ikabidi niwe bwege nimkubalie binti tuelekee kwao.
Basi tulitembea na jambo la kushangaza safari tulitembea kidogo tukawa tumefika hapo kwao,nilibaki najiuliza maswali kibao kichwani lakini sikuwa na majibu.
Nikawa najiuliza,kwanini leo hapo Kjijini Masairo pamekuwa karibu kiasi hicho?,au kwasababu nilikuwa nina ugwadu kiasi kwamba sikuona ni mbali?,sasa akili yangu ni kwamba nifike nichakate papuchi na ikiwezekana niondoke nirudi nyumbani hata kama ikiwa ni usiku wa manane,cha msingi nisilale nje tu!.
Sasa tulipofika hapo kwao na binti mara moja akawa amenipeleka kwenye kinyumba cha nyasi ambacho ndani kulikuwa na giza ila chini kulikuwa na godoro limetandikwa.
Binti “Kaa humu unisubiri niende kwa mama kwanza”
Sasa pale nje kulikuwa na moto ambao ulikuwa una fifia fifia ikionyesha yawezekana kulikuwa na watu wakiota muda si mrefu!.
Sikutakaa kabisa kukaa na nikawa tayari kutoka nduki endapo ningehisi hatari,nikasogea kwenye mlango nikawa nachungulia!.
Yule binti akaelekea mpaka kwenye nyumba iliyokuwa imeezekwa kwa nyasi lakini ilikuwa kubwa kiasi,kwa muonekano ni kama ilikuwa chumba na sebule.Alipofika akaanza kugonga mlango huku akiongea kwa lugha ya kisukuma.
Basi alifungua mlango mwanamke mmoja ambaye bila shaka alikuwa mama yake kwa mujibu wa maelekezo yake!.Wakaanza kuongea kwa kisukuma ambapo sikujua walikuwa wanaongea nini!.Ghafla baada ya maongezi ya yale maongezi yule mama akawa anakuja kule kwenye kile kinyumba nilichokuwamo,sasa ikabidi nitoke pale mlangoni nikarudi kukaa kwenye godoro chini nione nini kilikuwa kinaendelea.Alipofika akaanza kugonga mlango.
Mimi “Karibu”
Mama “Hujambo Umughaka?”
Ooooh!,nikawaza huyu mama jina langu kalijulia wapi?,hata huyo binti yake tu hakuwahi kulifahamu jina langu zaidi ya kuniita shemeji.Sikutaka kuonyesha nimeshangazwa lakini akili kukichwa zikaanza kuchaji ghafla!.
Mimi “Sijambo mama”
Mama “Mwalimu mkuu yeye mzima?”
Mimi “Yeye mzima kabisa”
Mama “Sawa,karibu mwanangu”
Baada ya ile salamu akaondoka zake kuelekea kwake na binti yake alikuja akafunga mlango,kiukweli nilikuwa nina hamu na papuchi lakini ghafla hamu ikawa inakata.Nilijiuliza maswali mengi mno.
Inawezekanaje huyo mama akalijua jina langu?,au uenda alikuwa akifahamiana na ba’mdogo sasa akamtajia jina langu?,lakini bado nilikataa!,inawezekanaje mama ambaye ndiyo ameniona mara moja tu akanichangamkia kiasi kile?,Je ni ulikuwa ni utaratibu wa kabila la kisukuma kuruhusu mabinti zao kuchakatwa ovyo bila mama kuonyesha kuchukizwa?.Mimi nilidhani uenda binti angegombezwa na mama yake mimi kwenda pale lakini mama ndiye alionekana kufurahia ugeni wangu!.
Basi sikuwa na hiyana ikabidi uchakataji wa papuchi uchukue nafasi kwa usiku ule,sasa kuna wakati tukiwa tunavuta pumzi baada ya mizagamuano ya muda mrefu,binti akawa anaanzisha stori ambazo zilikuwa zinazidi kunichanganya!.
Binti “Unajua mama yangu anakupendaga sana wewe”.
Daaah!,kiukweli ile sentensi ya anakupendaga sana wewe ndiyo ikazidi kunichanganya.
Mimi “Kwani mama yako amewahi kuniona wapi?”
Binti “wewe unajiona hapa kijijini kama mgeni wakati unafahamika sana tu”
Binti “wewe si kuna siku ulimsaidia mama kubeba kuni kuleta nyumbani,au umesahau”
Mimi “Hapana,siyo mimi labda mama yako atakuwa amenifananisha”
Binti “Mama yangu huwa asahau”
Sasa nikawa navuta picha ni lini nimemsaidia huyo mama kubeba kuni lakini nikawa sikumbuki kabisa,lakini binti akawa anakomaa kwamba ni mimi.
Lakini kuna muda nikasema huenda ikawa kweli,lakini ni siku ipi?,mbona mimi siikumbuki hiyo siku?,na jina langu huyo mama alilijuaje?,Kiukweli maswali hayakuisha ila kwakuwa papuchi ndilo kusudio la mimi kwenda pale,nikasema liwalo na liwe!.
SEHEMU YA 9
Basi mizagamuano ilipamba moto kiukweli hadi nikasahau kurejea nyumbani nikajikuta nimepitiwa na usingizi.Nimekuja kushituka ni saa 1 asubuhi sikumuona yule binti kwenye godoro.Nikakurupuka kuamka nikavaa zangu nguo na kutoka nje.
Sasa ile nimetoka nje na endelea kushangaa shangaa kumuangalia yule binti, nikamuona akiwa anakuja amejitwisha ndoo ya maji kichwani.Alipofika nikamsaidia kumtua.
Binti “Mbona mapema?”
Mimi “mapema tena!,mimi naondoka!”
Binti “Subiri basi nimebandika michembe ule ndiyo uende”
Basi kwakuwa nilikuwa nina njaa sikula tangia nilipokula kule nyumbani mchana wa ile siku tuliyokula kuku,sikuwa na namna ikabidi nisubiri michembe iive nipakuliwe nile,kiukweli nilikuwa nina njaa sana!.Aliingia ndani akawa amenitolea kiti nimekaa zangu pale nje huku nikiendelea kuyaangalia mazingira ya pale kwao.
Kiukweli pale kwao miji ya majarani ilikuwa mbali sana na kilichokuwa kimezunguka nyumba ni mashamba ya mahindi na mihogo.
Mimi “Mama yuko wapi?”
Binti “Ameenda shambani”
Basi baada ya kuniambia mama yake amekwenda shambani nilikaa kwa kujiachia nikapata amani sasa.Sikuona mtu mwingine pale kwao tofauti na yule binti pamoja na mama yake,sasa sikuweza kufahamu kwa haraka haraka wanaishi wao wawili tu au kuna watu wengine,sikutaka kabisa kupeleleza peleleza.
Ile michembe ilipoiva alinipakulia pamoja na uji uliokuwa umejazwa maziwa ya kutosha,ingawa uji haukuwa na sukari lakini ulikuwa mtamu.
Alitandika jamvi chini akaweka chakula kile tukaanza kula.Sasa wakati tunakula kiukweli nilikuwa nikimtazama yule binti na mambo aliyonipa usiku vilikuwa haviendani, binti alikuwa wa umri mdogo tu kama miaka 17 lakini alikuwa na mambo yaliyowazidi wakubwa wengi tu!.,Japo hakuwa mnene lakini alikuwa na umbo la wastani,kiukweli sura ilimbeba sana.
Mimi kwa wakati huo nilichojua ni kupunguza tu ugwadu,hizo habari nyingine za sijui matako makubwa mimi kwa wakati huo sikutaka kuzisikia,cha msingi nilikuwa nimepunguza ugwadu basi mambo mengine yangefahamika mbele kwa mbele.Sasa wakati tunakula akawa ananiambia.
Binti “Usije kabisa ukamwambia Ema”
Mimi “Hapana siwezi kusema chochote,mimi siyo mjinga”
Binti “Unajua Ema aliniambia atanioa”
Mimi “Kweli eeeh”.
Binti “Kweli kabisa”
Mimi “Kama ndivyo atakuoa wala usijali”.
Sasa kwa akili ya yule ndugu yangu hayo maneno ya kumuoa binti wa watu nilijua kabisa ni uongo na asingeweza kumuoa zaidi ya kumpotezea muda tu!.
Binti “Unajua yule Deborah ningemfanya kitu kibaya sana,sema tu mama yake anafahamiana na mama na ni marafiki tangu zamani,lakini isingekuwa hivyo angenitambua!”
Sasa nilikuwa naangalia binti aliyekuwa anasema angemfanya Deborah kitu kibaya nabaki namshangaa tu kwasababu ukiwapima yeye na Deborah hata hawaendani kimuonekano na kimabavu,Deborah alikuwa na nguvu kumshinda!.
Basi baada ya kula nikashiba ikabidi nimwambie anionyeshe njia ya kuelekea senta ili mimi niende zangu nyumbani.
Alinisindikiza huku akiendelea kunisisitiza nisije kumwambia mpenzi wake jambo tulilokuwa tumefanya.Mimi nikamhakikishia sitoweza kumwambia.
Nilitembea zangu kuitafuta senta ili niwahi nyumbani.Nilifika nyumbani mida ya saa 4 asubuhi moja kwa moja nikaingia ndani kupitia mlango wa uani!.Sikutaka kupoteza muda nikaingia jikoni nikachukua dumu la maji ili nielekee lamboni kuchota maji nije kuoga.
Sasa nadhani wakati nafungua mlango maza mdogo akawa amesikia hivyo akatoka kuja kuangalia ni nani aliyekuwa akifungua mlango.
Mimi “Oooh mama,shikamoo!”
Maza “Marhaba,vipi?”
Mimi “poa,za mjini?”
Maza “Nzuri”
Maza “Sijakuona,ulikuwa umelala nini?”
Mimi “Hapana kuna mahali nilienda mara moja ndo narudi”
Maza “Aaah sawa,kuna uji humo kwenye chupa utakunywa”
Mimi “Sawa mama”.
Baada ya salamu na mazungumzo alirudi ndani.Sasa wakati nashuka zangu lamboni nikawa najiuliza jana ilikuwaje?,Je yeye na headmaster walielewa jambo hivyo kaamua kuuchuna au hakuna walichoelewa?,sikutaka mambo yawe mengi,niliamini jamaa angekuwa shule na angetoka ningemuuliza ishu za jana zilienda vipi.
Basi baada ya kuoga nikachukua ule uji nikapiga vikombe viwili,japo nilikuwa nimeshiba lakini nikanywa tu kwa kujilazimisha!.Niliingia kulala na nilishitushwa na jamaa akinishika miguu akiniamsha kwa kunitingisha!.
Nilipoamka baada ya jamaa kuniona tukajikuta tunaanza kucheka!.
Ema “Mwanangu jana ulipotelea wapi?”
Mimi “Wewe acha tu!,sinilikimbia nikajikuta hata njia ya kurudi home nimeisahau!”.
Ema “Sasa ulilala wapi?
Mimi ” Kuna mahali nilifika nikakuta jamaa wamekoka moto ikabidi nijumuike nao”
Sasa nilimdanganya ili maswali yasiwe mengi,ingawaje na yeye alishindwa kuelewa ya kwamba ule niliyomwambia ulikuaa uongo kabisa kwasababu kwa miezi ile ilikuwa miezi ya palizi na mvua zilikuwa zikinyesha.Jamaa yeye alikuwa akicheka tu bila mpango.
Mimi “Wewe ulilala home?”
Ema “mwanangu mimi nilikimbia na lile hotpot japo nilifika nyumbani nimeloana na michuzi lakini sikujali”
Mimi “Ulikuta dingi ameshafika?”
Ema “Alikuwa bado hajaja,mimi nilikwambia huyu namfahamu vizuri,tena akiwa na mke wake ndiyo kabisaa!”
Ema “Walikuja wakagonga nikaamka kuwafungulia,hata chakula chenyewe hawakula”.
Baada ya jamaa kunieleza vile angalau sasa moyo wangu ukatulia.
Ema “Lakini ile sauti nilisikia ilikuwa kama ya Monica!”
Mimi “Monica!,Monica yupi tena?”
Ema “Si kile kidemu changu cha kule Masairo!”
Mimi “oooh sawa”
Mimi “Sasa kama ilikuaa sauti ya demu wako mbona tulikimbia?”
Ema “Mi nilishituka tu nikajikuta nakimbia”
Mimi “Lakini una uhakika alikuwa Monica?”
Ema “Kaka ile sauti niya kwake kabisa,na siunakumbuka aliniita Mpenzi?”
Mimi “Sasa alikuwa anatoka wapi muda ule?”
Ema “Yawezekana alikuwa akitufuatilia,unajua kale nako ni kajanja kajanja sana”
Basi nilianza kuvuta picha na kuunganisha,sasa nikawa najiuliza yule binti ni binti wa namna gani?,Kama mpaka muda ule wa saa 3 usiku hakuwa kwao nilibaki nashangaa,ukiacha hivyo ule muda niliyokutana nae kule kwenye uwanja wa mnadani ilikuwa usiku mnene lakini hata hawazi,niliendelea sana kupata mashaka kuhusu binti Monica.
Basi kuna siku headmaster akawa ametuambia isije ikatokea kufika saa 12 jioni mtu akakosa hapo nyumbani,alisema yaani ikifika saa 12 na ukawa hujarudi nyumbani basi utafute pa kwenda!.Kwa upande wangu nilijisikia vibaya kwasababu sasa zile mechi za Arsenal zilizokuwa zikichezwa usiku ningekuwa nazikosa!,kiukweli niliumia sana.
Sasa siku moja nakumbuka Maza mdogo akawa amenituma mafuta ya kupaka kule senta ambayo ni losheni,sasa akawa ameniandikia jina la ile losheni akanipatia na hela nikaondoka zangu!.,Sasa nilipofika nikakuta yale mafuta yapo ya aina 2,muuzaji akawa ameniuliza ni yapi kati ya hayo ninahitaji?,ikabidi nimuulize ambayo kina mama wanapendelea sana kati ya hayo mawili ni yapi?,yule mama akasema kina mama wengi wanapendelea yaliyokuwa na harufu ya cocoa,basi nikamwambia anipatie hayo hayo yenye harufu ya cocoa!.
Niliporudi nyumbani Maza akawaka sana,kwamba ni mafuta gani yale nimemletea,nikajaribu kumwambia kwamba niliyakuta yapo ya aina mbili na yeye hakuniambia nichukue yapi niache yapi.
Maza “Chukua ya kopo la maziwa bhana”
Maza “Ushakuwa mtu mzima hebu uwe unajiongeza”
Kiukweli nilikasirika sana na kwakuwa alikuwa Maza mdogo ikabidi niuchune,kiukweli sema alijikuta tu amekuwa Maza mdogo basi heshima ilibidi ichukue mkondo wake lakini kwa upande wa umri hakuwa mkubwa wala nini!.
Maza “Hebu rudi ukanichukulie yale mengine”.
Basi ikabidi niwe mpole nirudishe tena midenge yangu kule senta,yeye alikuwa afahamu kwamba senta palikuwa mbali,kwenda na kurudi si chini ya kilometa 6,sasa nilipoenda mara mbili maana yake nikajikuta natembea zaidi ya kilometa 12.Nilichukia sana lakini sasa ningefanyaje?,ilibdi nienda nikayafuate tu!.
Sasa wakati narudi ilikuwa mida ya 10 jioni.Nikamgongea mlango nikampa mafuta yake lakini nikiwa nimechukia sana!.
Maza “Siku nyingine nikiwa nakuagiza uwe unaniletea haya siyo yale uliyorudisha”
Mimi “Sawa mama haina shida”
Basi yeye kwa akili yake alidhani mpaka hayo mafuta yaishe mimi ningeendelea kuwa hapo,kwa maisha aliyoanza kuyaonyesha kwa siku chache hizo tu,yalionyesha tungekuja kukwazana sana.
Sasa nikaingia zangu kupumzika kitandani kwasababu nilikuwa nimechoka halafu jua lilikuwa kali.Nikiwa nimejiegesha kuutafuta usingizi kwa mbali,mara ghafla nikasikia sauti ya Maza mdogo akipika kelele!.
Sasa ile nafungua mlango nakuta anakomaa kufungua mlango wa bafuni yeye akiwa kwa ndani,ndipo nikasogea kwenda kumsaidia,sasa ile nimefika mlangoni nataka kuusukuma maana alikuwa akiomba msaada na mimi nikadhani uenda aliingiliwa na nyoka bafuni lakini kumbe yeye alikuwa naya kwake.
Maza “Yaani umughaka kabisa umekuja kunishika matako mimi!”
Maza akaendelea “Wewe niwa kunishika matako mimi nakuuliza?”
Nilibaki nimepigwa na butwa nikawa hata kuongea siwezi nabaki kujing’ata ng’ata tu kwa mshangao.
Mimi “Mimi mbona nilikuwa nimelala!”
Maza “Wewe ngoja baba yako arudi”
Mimi “Mama mimi nimekuja kukusaidia baada ya kusikia kelele”
Maza “Peleka huko utahira wako mbwa wewe”
Maza “Yaani wewe ni wakuja kunishika mimi matako?”
Basi baada ya kusema maneno yale kwa ukali akawa ameingia ndani.Sasa nikabaki najiuliza maswali yasiyokuwa na majibu,Je ni kweli ameshikwa matako?,na kama ameshikwa matako ni nani kamshika?,ina maana hakuona kama mlango alikuwa amelock kwa ndani na mimi ningengiaje bafuni?,Au uenda ni style tu za kunifukuza pale ki-aina?.
Uenda aliona kama tunammalizia mumewe chakula au yale maziwa aliyokuwa akiletewa kila siku!.Kiukweli moyo wangu uliuma sana.
Kumbuka mpaka mida hiyo nipo tu mimi na yeye hapo nyumbani,Ema na Headmaster wako shuleni,swali nililokuwa nalo kichwani ni nani ataniamini?
INAENDELEA……..