UGALI WA BUKUJERO ULIPELEKEA NITOLEWE BIKIRA ZOTE NA WANAUME WATATU KWA WAKATI MMOJA
Namba 13
Siku zilisogea kila mara niliuliza taarifa za msiba nikaambiwa mpaka baba alipozikwa sikufanikiwa kufika kabisa nyumbani kwa sababu nilikuwa nimeamua kusubiri mitihani nimalize kwanza ndio niende nyumbani.
Hata hivyo siku moja nilikuwa sijisikii kufanya mitihani kabisa ila nilijitia moyo kwamba nitafanikiwa kuifanya vizuri, ubaya mmoja semester iliyokuwa imepita, nilikuwa na mitihani miwili ambayo nilikuwa sijafanya vizuri, kwa kuzoeleka wanaita Supplementary, sikutaka kuongeza nyingine
Nilifanya mitihani nikiwa na mawazo mchanganyiko, roho ilikuwa inaniuma sana, mitihani ilikuwa ni migumu sana, nilipofikia mtihani wa tatu nikamfuata Mido na kumueleza akaniambia
“Ninahitaji niahirishe hii iliyobaki, nashindwa kufanya mitihani ni migumu, sielewi, akili yangu haipo shule kabisa, naomba niende nyumbani”
Mido alinishauri, kwamba nipambane nayo nimalize mitihani yote ndio niende nyumbani hata kama ni sup hazitakuwa nyingi nitakuja kuzifanya mwezi wa tisa.
Kwa kuwa nilikuwa namsikiliza sana, nilifanya mitihani kwa taabu sana mpaka nikamaliza.
Siku nilipomaliza, mapema tu niliondoka kesho yake na kueleka nyumbani Singida, nilipofika nyumbani nilikuta kumeshapoa kabisa, nikaenda kwenye kaburi nikalia sana, sana, sana….japo nilimpenda sana baba yangu, Mungu alimpenda zaidi.
Ulikuwa ni mwaka wa mateso katika maisha yangu sikuwahi kuteseka hivyo kabla, yaani muda wote ilikuwa ni stress ya kufa mtu, nilijiona mimi nina mkosi, nikajisemea moyoni kwamba ipo siku lakini siku yenyewe sikuijua ni siku gani.
Hata hivyo nilifikia mahali nikazoea maumivu makali na kuwa kidogo sawa.
Siku zilisogea mpaka mwezi wa nane huko katikati matokeo ya chuo nayo yakatoka, kila nilipojaribu kuingia mtandaoni nilikuwa nashindwa kwa sababu ya server kulemewa na watu wengi kwa wakati ule, nikatamani kumpigia rafiki yangu wa karibu Ally ili aniangalizie matokeo lakini nikaogopa sikutaka aone matokeo yangu maana kama nimefeli masomo mengi lazima angenitangaza tu.
Nilijaribu jaribu nikashindwa, mpaka ilipofika usiku ndipo nilimtumia Mido namba yangu ya usajili pamoja na password aweze kuniangalizia matokeo yangu yote,
Mido kuanzia muda huo hakupokea simu japo ilikuwa ni saa nne tu usiku na najua alikuwa analala saa saba au saa nane usiku tukiwa tunaongea kwenye simu au akiwa katika kazi zake za kila siku.
Nililala nikiwa na wasiwasi lakini asubuhi na mapema kabisa alinipigia simu, wala sikutaka kumuuliza kwamba kwanini hakupokea simu yangu kwani alikuwa ni kama kaka yangu tu nisingeweza kumpangia maisha yake.
“Umeamkaje?” aliniuliza
“Niko poa tu, jana ulilala mapema ee?”
“Ndio, nilikuwa nimechoka sana”
“Anhaa sawa, niangalizie basi matokeo nijue mapema”
Bila hata kupepesa macho aliniambia kabisa “Pole”
Nikamuuliza “Pole ya nini??”
Akaniambia “Pole na matokeo yako, kati ya masomo saba uliyofanya, umepata supplementary tano, na hapa chini wamekuandikia discontinued” alimaanisha kwamba nimefeli chuo kabisa singeweza kuendelea labda nirudie mwaka wa kwanza tena
“Whaaat???” niliuliza kwa mshtuko wa hali ya juu
“Pole sana, ila usiwe na wasiwasi maisha sio laz…..” kabla hata hajamaliza sentensi yake, kutokana na stress zangu jumlisha kulemewa na msongo wa mawazo, nilijikuta nimedondoka chini tena na kupoteza fahamu kwa sababu presha ilikuwa juu
JE ESTER ANA MKOSI GANI?
KWANINI KILA KITU KWENYE MAISHA YAKE HAKIFANIKIWI?
NAMBA 14
Nyumbani hawakujua nina tatizo gani, nilikuwa na stress za chini kwa chini, ndani kwa ndani, nilikuwa sina mtu wa kunifariji zaidi ya Mido tu, sasa mambo yakishaingia moyoni mengi ndio kwanza husababisha mtu kuwa na presha.
Kutokana na hali ya kutokuwa na uchumi mzuri nyumbani, hawakunipeleka hospitalini ila tu walinipepea mpaka niliposhtuka, haikuchukua muda mrefu sana kutoka nilipozimia ndipo mama akaniuliza
“Vipi mwanangu kuna tatizo gani??” nikamtazama tu bila kujua nimjibu nini, ndio mawazo yananijia kwamba nimefeli chuo, nikaamka na kuwatazama ndugu zangu, ishu ya msiba haijawatoka vizuri, halafu mimi ndio kwanza ninataka kuwaletea mzigo mwingine
“Niko sawa mama” nilimuambia
“Uko sawa wakati umepoteza fahamu hapa?” aliniuliza
“Sijui, ni mshtuko tu” nilisema huku nikichukua simu ambayo alikuwa ameishika mdogo wangu Calvin
Niliingia ndani, wakawa wananishangaa tu, hawajui wanisaidieje, nilipofika ndani nilitazama simu yangu na kutazama kuna messages mbili za Mido ndefu
1. Jana nilishindwa kukupigia simu kwa sababu ilikuwa ni usiku, sikutaka kukukatia usingizi wako maana najua siku hizi una msongo mkubwa wa mawazo
2. usiwe na wasiwasi maisha ndivyo yalivyo hivyo kuna kufanikiwa na kutokufanikiwa, lakini vile vile usimuambie kwanza mtu yeyote hapo nyumbani subiri tuangalie kitu gani unaweza kufanya hapa mjini, au kama utakubali kurudi chuo tena
Niliposoma zile message nilikaa kimya, lakini vile vile nilimlaumu kwamba yeye ndiye chanzo cha mimi kudisco chuo kwa sababu nilimuambia sijisikii kufanya mitihani kwa sababu nilikuwa na stress lakini yeye akanifosi na kunifanya nisifanye vizuri hadi nikafeli
Niliwaza sana itakuwaje? Nilijiuliza kwanini shetani ananiandama sana tangu niiingie chuo? Muda mwingine nilihisi huenda ikawa ni majirani wasiopenda mafanikio yangu labda ndio walioniroga ili nisiweze kufanikiwa nikaisaidia familia.
Ni kweli kijijini kwetu kuna watu wengi sana wanaamini masuala ya kishirikina hivyo nilipata wasiwasi. Nikatulia kimya sikumuambia mtu mambo yaliyonikuta.
Kimya kilidumu kwa muda mrefu, mpaka siku moja nilipomtumia picha zangu za kijijini Mido akanihurumia sana
“Mbona umekonda kiasi hicho?” aliniuliza
“Nimekonda sana??” nilimuuliza swali
“Ndio umekonda, anyway najua umekuwa na misukosuko ya hapa na pale, ila kuna kitu ninataka kukuomba sijui utakubali??” aliniuliza nikajua sasa muda wa kulipa ule wema wake umefika.
“Kitu gani tena??” nilimuuliza
“Hahaha” alituma message ya kucheka halafu akaniambia “Najua mawazo yako yameenda mbali lakini anyway, yule housegirl wetu alikimbilia kwao, ameenda kuolewa ndugu yangu” aliniambia
“Ameenda kuolewa??” aliniuliza
“Yes, halafu mama anaumwa, na mtoto ndio hivyo, nilikuwa naomba uje unisaidie kukaa kaa na mama kwa muda nikitafuta housegirl mwingine tafadhali” aliniambia
“Mh, kweli?”
“Ndio please, ukiwa umekaa hapa ndivyo tutakavyowaza kulitatua hili janga la wewe kufeli, halafu pale UDSM wanahongeka tukitoa hela kidogo tu wanakuruhusu kufanya mitihani yako na utaendelea vizuri tu” alisema maneno ambayo yalinitia moyo kidogo
“Kweli??” niliuliza
“Ndio kweli……njoo basi??”
“Sawa hamna shida ila nauli mi sina”
“Nakutumia”
Nilcheka kidogo halafu nikamuuliza “Hivi mwishowe mimi kwa wema ambao unanitendea hivi ninapaswa nikulipe nini Mido? Maana sijui hata ulitokea wapi kunipa furaha kwenye maisha yangu hasa pale ninapokuwa na matatizo”
“Hahaa…hamna cha kulipa, ila na wewe siku ukifanikiwa, unapaswa usaidie mtu mwingine, mimi mwenyewe nimesaidiwa kama wewe na ndio maana nakusaidia” alisema
“Umesaidiwa na nani??” niliuliza
“Basi tu nisikueleze kila jambo lakini wewe niambie nikutumie nauli kwenye namba ipi na uniambie kwamba unakuja lini”
“Niambie kwanza bhana” nilisema
“Nikuambie nini sasa?” aliniuliza Mido
“Niambie nani alikusaidia na ulikuwa na tatizo gani kubwa hivyo” nilisema
“Aah ukija nitakuelezea tukiwa wote”
“Jamani, utafanya siku yangu isiwe nzuri niambie sasa hivi”
“Daah sipendagi kumuhadithia mtu maisha yangu, lakini wewe nakuamini sana kwa sababu sijawahi kukusikia ukisema kitu chochote kibaya au kusengenya mtu, kila siku unaongelea maisha yako tu” aliniambia
“Mmmmh”
“Ndio, nikuambie kitu kimoja tu, aliyenisaidia ni yule mama ambaye ni nesi…”
“Mmmh sasa yule si ni mama yako?” nilisema
“Hapana mimi wazazi wangu wote walikwisha fariki kipindi naingia chuo cha polisi pale Moshi CCP mama yangu na baba yangu walipata ajali wakafa wote wawili”
“Wewe!!!” nilisema kwa mshangao sana “Kweli??”
“Ndio ni kweli, hakuna mtu anaweza kusema ukweli kama huu….huyu mama hana mtoto kabisa, hakufanikiwa kuwa na mtoto, ila ametulea vijana wengi na mimi ni mmoja wao, tunampenda naye anatupenda sana…tunamuita mama” aliniambia
“Mmmh pole jamani”
“Asante sana….kwa hiyo ninajua thamani ya kumsaidia mtu, hata wewe naamini uliona jinsi alivyokuwa anakujali kipindi ulipokuwa hospitalini pale”
“Ni kweli kaka, Mungu ambariki sana”
“Tumuombee”
“NItafanya hivyo, kumbe historia yako inasikitisha sana”
“Mno, ila mambo mengine nitakuambia ukija….niambie unakuja lini nikutumie nauli maana mama anaumwa sana”
“Okay, tuma tu hata kesho lakini mimi nitakuja baada ya siku mbili”
“Sawa, pumzika sasa, lakini ule ushibe punguza stress hujui tu ukinenepa unavyokuwa mzuri” aliniambia nikajikuta natabasamu, nilikuwa nimeshanogewa na kampani ya Mido, hakuwahi kukosea kuniambia kitu chochote, alikuwa anajua kuishi na mimi kama mdogo wake, lakini vile vile nilikuwa nikimkosa tu kuwasiliana naye, napata taabu najihisi mzito akilini mwangu.
“Kwenda zako huko uliniona wapi nimenenepa”
“Hahaa..kipindi umehamisha Shekilango, ulinenepa sana”
“Hahaha….unajua kumtunza mtu, ina maana mke wako huwa anafurahi sana” nilisema
“Mke???” aliniuliza
“Ndio, huyo uliyezaa naye yule mtoto wako, si mke wako au??” nilijikuta namuuliza maswali fulani hata sikujua namuuliza ya nini lakini mikono ilikuwa inajikuta tu inatuma message za aina hiyo.
“Embu lala huko, sasa ningekuwa na mke ningekuwa nakupigia simu hadi saa saba usiku?” aliniuliza
“hhaaha ila kweli,….basi ulale unono mimi nina usingizi”
“Okay kesho nitakutumia hiyo pesa uje” aliniambia
“Sawa….usiku mwema”
“Na wewe pia”
JE UNATABIRI NINI?
NAMBA 15
Siku iliyofuata Mido alinitumia nauli ya kutoka Singida mpaka Dar ili niende nikamsaidie.
Niliwaambia ndugu na mama yangu kwamba kuna mitihani naenda kufanya wakaniruhusu nikaondoka siku moja baadaye.
Nilifika Dar. Na kwa kawaida nilishuka katika kile chumba ambacho alikuwa amenilipia Mido, mitaa ya Shekilango.
Sikufanikiwa kuonana naye siku hiyo kwani alikuwa bize sana na kazi lakini kwa sababu nilikuwa napajua kwao kesho yake asubuhi sana niliamua kwenda moja kwa moja kwa mama yake ambaye ni wa kumlea.
Nilipofika pale kwao nilimkuta yule mwanamke akiwa katika hali mbaya sana. Alikuwa kitandani kalala peke yake
Mjukuu alikuwa ameshaenda shuleni ambaye ni mtoto wa Mido, nikamfuata mama
“Mama Lenard shikamoo” nilimsalimia nikiwa nampa mkono yupo kitandani
“Marahaba, umekuja asubuhi sana mbona??” Aliniuliza huku akishikilia mkono wangu na tabasamu likiwa usoni
“Akinisisitiza sana mwanao Lenard akaniambia nije…nikusaidie maana upo mwenyewe”
“Ndio nashukuru sana”
Baada ya kusalimiana pale, mwanzo nilikuwa sielewi nianze kazi ipi, lakini kwa sababu mi ni mwanamke nilifanikiwa kufanya usafi nikafua, nikadeki, nikaosha vyombo, nikafua niaamua kumpikia chai pamoja na kazi nyingine.
Baada ya kufanya usafi niliketi sebuleni nikawa nachezea simu, nikamtext Mido
“Uko wapi”
Akanijibu “niko bize sana, nitakucheki jioni si ushaenda kwa mama?”
Nikamjibu “ndio niko hapa”
“Okay….nitakucheki”
Nikiwa nimekosa jambo la kufanya kabisa nilianza kupiga selfie, kwenye snapchat na kadhalika, ghafla nikiwa pale nilisikia geti limefunguliwa nje, nikashtuka na kuinua macho nikatazama nje kupitia dirishani.
Wakaingia vijana watatu wa kiume, wawili walionekana kuwa na umri mkubwa kama wa Mido, lakini mmoja alionekana rika langu kabisa,
“Hodi….Bi mkubwaa” waliita na mimi nikainuka
“Karibuni” nilisema huku nikiwatazama nilikuwa siwafahamu kabisa
“Asante sana” walisema huku wakiingia sebuleni na kunitazama wote nafikiri kichwani mwao walikuwa wanajiuliza ni nani
“Hivi bi mkubwa ameshaleta demu mwingine??” Aliuliza mmoja kati ya wale wakubwa wawili
“Ndo nashangaa baabu” alisema mwenzake
Nilibaki natabasamu, nafikiri walihisi mimi ni housegirl mpya baaada ya yule wa mwanzo kuwatoroka
“Mambow” alisema yule mdogo ambaye alikuwa mweusi mno, ila alivyokuwa anatabasamu basi alikuwa na meno meupe peee.
“Safi karibuni” nilisema lakini wao walipita hadi kwenye chumba alichokuwa amelala mama yule mgonjwa.
Mimi niliendelea kubaki sebuleni kwa muda, ila hata hivyo yule kijana mweusi alirudi sebuleni na kuwasha TV halafu akaketi kwenye sofa.
Alikuwa mchangamfu mwenye maneno mengi sana, akaniuliza “unaitwa nani??”
“Mi naitwa aaah Esta” niliposema hivi, aliguna kidogo halafu akaniambia
“Hilo jina la kwako kweli au, maana umelifikiria kwanza kama vile unalitunga”
“Ahahaha…ni jina langu kweli” nilisema
“Okay sawa, i hope wewe ni dada mpya wa kazi au??” Aliniuliza
“Hapana….” nilisema
Yule kijana alitabasamu, hakutaka kujua hata nimetokea wapi, alikuwa na mihemko sana kwa sababu alikuwa bado mdogo miaka kwenye 23 hivi ndo kwanza damu inamchemka.
“Anyways mi naitwa David….”
“Ooh David”
“Yeah”
Tukiwa tunaongea ongea pale wale wenzake wakatoka na kuketi pale kwenye kochi wakaanza kupiga story namna ya kumsaidia mama aliyewalea kwani wote wale walikuwa wamelelewa na yule mama ambaye ni nesi.
Walipofikia makubaliano, waliamua kuondoka, ila yule David alinigeukia na kunitazama, alioneokana kuna kitu anataka kuniambia lakini hakusema mbele ya wale ndugu zake.
Wakaniaga na kuondoka zao
JE ITAKUWAJE?
NAMBA 16
Niliendelea kubaki pale nyumbani mpaka usiku sana kwa kuwa yule mama hakuumwa sana, aliweza kuoga pekee yake.
Mimi nilihakikisha anakula vizuri na vidonge aliluwa anameza, nikampigia simu Mido ili kumuuliza yuko wapi.
Mido aliniambia kwamba yupo mbali sana hawezi kufika
“Mimi naondoka sasa” nilisema
“Usiondoke, naomba ulale hicho chumba cha housegirl hapo”
“Kipi??”
“Huyo dogo si yupo?” Aliniuliza kama mtoto wake yupo, na alikuwepo kwa sababu alisharudi kutoka shule
“Ndio yupo” nilisema
“Mwambie akuonyeshe chumba alichokuwa analala binti wa kazi”
“Sawa…lakini kwa hiyo wewe uko bize sana leo??” Nilimuuliza
“Niko mbali kuna kazi nafanya lakini, nitakupigia baadaye kidogo tupige pige story mbili tatu”
“Poa nashukuru”
“Asante”
Nilimuuliza mtoto wake kwamba kile chumba ni kipi akanionyesha chumba kilipo, na nilipoingia ndani kulikuwa kuzuri sana.
Nilikuwa upweke bado sikujua hatma ya maisha yangu ya elimu ni ipi, nilikuwa nawaza vitu vingi, nilikuwa namuomba Mungu anijalie niweze kufanikiwa katika hilo suala la kurudi chuo nimalizie elimu yangu.
Sikuwa na tumaini sana lakini kadri siku zilivyosogea ndivyo nilivyokuwa nakosa muelekeo,
Siku zaidi ya tano sikumuona Mido, alikuwa tu anawasiliana na mimi kwenye simu akidai yuko bize sana na kazi, sikujua yuko wapi lakini nilitaka tu anieleweshe kuhusu hatma yangu ili nijue naelekea wapi na nitafanya mambo gani.
Nikiwa nimekaa nje ya nyumba yao siku ya jumamosi, nacheza na mtoto Calvin, ambaye ni mtoto wa Mido niliona geti limefunguliwa.
Nilipotazama alikuwa ni yule David ambaye ni mmoja wa vijana ambao walilelewa na yule mama, aliingia ndani.
“Woow” alisema kwa furaha baada ya kuniona nikiwa nimekaa pale nje
“Karibu” nilisema huku nikimtazama, amevaa amependeza kweli kweli
“Asante sana, za tangu siku ile?” Aliniuliza
“Salama tu”
“Ah…mh nilikosa muda wa kuja kukusalimia lakini nilikuwa nimepanga nije muda mrefu sana. Ila nilitingwa” alisema na kuketi barazani “vipi lakini bi mkubwa anaendeleaje?” Aliuliza
“Amepata nafuu, naona anataka aanze kazi jumatatu”
“Wao angalau…..” alisema na kumtazama Calvin “dogo hujambo??” Aliuliza
Nikamfokea mtoto “halafu kwanini huamkii watu wazima wewe??”
“Shikamoo anko”
“Marahaba” alisema David halafu akanitazama na kutabasamu akaniuliza “Vipi wikiendi hii hautoki??” Aliniuliza
“Ah mh hapana, sasa nitaenda wapi??” Niliuliza
“Ukipata mualiko??”
“Ahaha labda, na inategemea ni mualiko wa nani sio kila mtu” nilisema
“Hahaha mfano mualiko kutoka kwangu??” Aliniuliza
“Haaha may be, kama nitakuwa nishamaliza majukumu yangu, kwanza unajua mimi tangu nije Dar sijawahi kwenda hata beach” nilisema
“Weee….ulikuja lini??” Niliuliza
“Nakaribia mwaka sasa” nilisema
“Oooh ni muda mrefu sana lakini usiogope, tutaenda” alisema na kutoa simu mfukoni ilikuwa ni iPhone 13 Pro max, nayaona macho matatu yake, na ndilo lilikuwa tole jipya zaidi la iPhone kipindi hicho.
“Nipe namba yako halafu tutawasiliana basi” aliniambia
“Ok, andika 07…………” nilipomaliza kumtajia akainuka na kuniambia “basi mi naondoka
“Khe humsalimii mama??” Niliuliza
Akaweka kidole mdomoni mwake na kusema “ssssssh hatakiwi ajue nimekuja” alisema
“Ok sawa”
NAMBA 17
Kwa jinsi alivyoonekana David bado ujana ulikuwa unamsumbua sana, licha ya kuvaa nguo za gharama lakini hakuwa smart kiakili kama wale wengine, alionekana mdogo na wa kupapatika.
Sikumuwaza sana, aliondoka zake na mimi nikaendelea na mambo yangu.
Kesho yake tulienda kanisani asubuhi sana, kanisa alilokuwa akisali mama halikuwa mbali sana na pale nyumbani kwa mama.
Tulitembea tu kwa miguu, tukiwa njiani mama akaniambia
“Wewe ni msichana wa kipekee sana”
“Kwanini mama??” Niliuliza
“Nimesaidia wasichana wengi sana, lakini angalia wanaokuja kila siku kunisalimia ni vijana wa kiume, kweli wameshindwq kurudisha fadhila hata kidogo, ila wewe umekuwa bora sana kwangu”
Nilifurahi sana kusikia maneno yale “asante mama”
Akaendelea “nimekaa na wewe siku hizi chache, nimekuchunguza wewe ni binti mzuri, nafikiri umekuzwa vyema sana”
“Jamani asante sana mama”
Tulienda hadi ibadani, tukamaliza kusali tukarudi nyumbani, tukiwa nyumbani nilifanya kazi zinazopaswa kufanyika, mpaka saa 10 nilikuwa niko free kabisa.
Kama vile David alijua, akanipigia simu “hello Esta, uko wapi??” Aliuliza
“Niko nyumbani”
“Uko free nije nikuchukue??” Aliniuliza
“We David au??”
“Ndio”
“Haya niko free nimekaa tu”
“Haya poa”
Ilipopita kama dakika kumi alinitumia ujumbe akaniambia yuko getini
Nikamuambia mama “mama natoka kidogo nitarudi baadaye naenda kule shekilango” alisema
“Sawa mwanangu, usichelewe kurudi sawa?”
“Sawa”
Kuna kitu kilikuwa kinanizuzua nimeshasahau yale yaliyonikuta siku za nyuma mara baada tu ya kula ugali wa buku jero nikalipwa maumivu makali.
Nilitoka nje ya geti nikakuta David amekuja na gari, sikujua ni lake au ameazima tu, lakini mi nilipanda tukaondoka naye mpaka mbezi beach.
Siku ile kidogo niliujua mji, alitumia gharama zake sikujua ana lengo gani.
Sasa tukiwa mezani tunakunywa juisi taratibu, David akaniambia “Esta kuna kitu nataka nikuambie”
“Kitu gani??” Nilimuuliza
Kabla hajasema kitu chochote nilipata simu, na nilipoitoa kwenye simu nikakuta ni Mido ananipigia simu.
Nikapokea bila kujali maana sikuwa kwenye mapenzi na yeyote kati yao wawili
“Hallo kaka Lenard” nilisema kwa bashasha
“Eeh vipi unaendeleaje??” Aliniuliza
“Niko poa tu wewe umepotea” nilisema
“Nakuja kesho huko sawa???” Aliniuliza
“Sawa karibu sana”
“Okay, uko wapi mbona kuna kelele??”
“Ahahaa niko Mbezi beach” nilisema
“Mbezi Beach??” Aliniuliza kwa mshtuko kidogo
“Ndio, niko na David…..amenileta”
“David gani huyo mweusi??” Aliniuliza
“Ndio……”
“Anhaa, sawa hamna shida…..” aliniambia
“Ndio kaka”
“Poa basi kuleni maisha” aliongea kawaida wala hakuonekana tofauti, alikata simu yake mi nikaendelea kuongea na David
David akaniuliza “huyo nani??”
“Huyo kaka yako Lenard”
“Oh hivi Lenard ndo amekuleta pale??”
“Ndio, ana roho nzuri sana kaka yako” nilisema huku nikinywa juisi lakini David alionekana kama kabadilika ghafla tu.
“Enhee niambie ulitaka kusemaje?? Niliuliza na kunywa juisi ila ghafla tena akapiga Mido nikapokea
“Kaka”
“Upo na David hapo??” Aliniuliza
“Ndio”
“Embu mpe simu” aliniambia.
Nilimpa simu David wakaongea lakini sikuelewa waliongea nini, baada ya kuongea akanipa simu nikaendelea kuongea na mido
Mido akasema “Rudi nyumbani mama anakujitaji sasa hivi” alisema
“Sawa kaka” nilisema
JE KWELI MAMA ANAMUHITAJI ESTA AU SABABU YA MIDO KUSEMA HIVYO NI IPI??
1 Comment
Well well well. Mtiririko safi, matukio kwa mda wake nahisia mseto kulingana na mapito. Hongera sana