UGALI WA BUKUJERO ULIPELEKEA NITOLEWE BIKIRA ZOTE NA WANAUME WATATU KWA WAKATI MMOJA
Namba 5
Tuliishia pale Esta alipopoteza fahamu baada ya wanaume wawili kumuingilia na kumuumiza sana
Endelea hapa…..
Nilipata kushtuka baada ya muda, nikashangaa niko wapi, kwa haraka haraka sikukumbuka kwamba mara mwisho nilikuwa kwenye gari.
Lakini niliinuka na kutazama niko wapi ndipo nikakuta niko kwenye kitanda cha hospitali, nimevalishwa nguo za wagonjwa, mkononi nimetundikiwa dripu halafu nilikuwa bado nasikia maumivu makali sana.
Nilijiuliza kwamba nani amenileta pale hospitalini, ndipo ghafla akaingia mama mmoja mwenye umri kati ya miaka hamsini hadi hamsini na tano, alikuwa amevaa kama nesi, akanikuta nimeketi kitandani nashangaa.
Akaniuliza
“Umeshaamka??”
Mimi nikamtazama tu, lakini akili yangu inanirudisha kule nilipokuwa mara ya mwisho huku nikikumbuka mateso makali niliyoyapata kwa muda mfupi sana kisa tu chakula cha shilingi elfu na mia tano.
Yule mwanamke alisogea na kusimama kando yangu halafu akaniuliza “Unajisikiaje??”
Nikamtazama, ni mtu ambaye simfahamu, badala nimjibu kile alichokuwa ameniuliza basi mimi nikamuuliza swali lingine “Hapa niko wapi??”
Yule mwanamke akanijibu “Hapa uko hospitali ya Arafa NHC” Nikashangaa hospitali yenyewe ipo Mawasiliano sasa sikujua nani aliyenileta pale
“Nani amenileta hapa??”
“Ah pole kuna mtu……” kabla hajamaliza sentensi alipata simu na aliipokea akawa anaongea ila sikusikia maneno ya mtu aliyekuwa anaongea naye, yule nesi akaanza kuongea “Uko wapi??…….Ndio ameshaamka………..sawa nitafanya hivyo lakini wewe hauji kumuona?…………….okay sawa ila sio vizuri vijana mnavyofanyia watoto wa kike” alisema yule mama “Haya sawa nakusubiri” alikata simu kisha akanitazama na kuniuliza “Utakula nini??”
“Niambie kwanza,kwanza sasa hivi saa ngapi?, mi sielewi, sina hela, simu yangu iko wapi, nani kanileta hapa, natakiwa niende darasani daaah” nilisema kwa uchungu vitu vingi visivyopangiliwa, machozi yalikuwa yananitoka nawaza
“Nani kanileta hapa??” alisema
“Oh pole” alisema na kuketi kitandani akanishika shavuni na kuniambia “Pumzika, kila kitu kitakaa sawa”
“Mama….mi sina hela ya kulipia hapa”
“Sawa kama hauna hela ndio usitibiwe?? Umebakwa na watu usiowafahamu je kama wamekuachia magonjwa?? Je unajua madhara ya kufanywa mapenzi kinyume na maumbile?? Kaa kwa kutulia gharama zote zitalipwa”
“Zitalipwa na nani??”
“Aliyekuleta”
“Ni nani huyo??” niliuliza na nilihitaji kujua kwa sababu mimi mwenyewe nilikuwa nimeshaona madhara ya kupewa huduma za bure bure ndipo kuliishia kubakwa na kutumika hovyo
“Mimi ni nesi hapa, lakini hii hospitali tumeweka hisa, kwa hiyo usiwe na wasiwasi”
“We ni nani??”
“Mimi ni mama wa aliyekuleta” alisema kwa mkato huku akitabasamu, bado sikumuelewa nikabaki namshangaa kwanza akasema “sasa hivi ni saa nne asubuhi nikuletee kifungua kinywa cha aina gani??” aliniuliza
“Nataka aje huyo aliyenileta, na usikute ni wale wanyama wa jana” alisema
“Atakuja yupo kazini…nikuletee supu na chapatti??” aliniuliza nesi mi nikatulia kimya, ndipo akatoka bila kuongeza neno lingine
Nilishangaa ni mwanamke mwenye upendo wa ajabu sikupata kuona ghafla lakini kiukweli wasiwasi wangu ulikuwa ni mkubwa, sijui ni mwanamke mwenye lengo gani mpaka anisaidie vitu ambavyo nilijua siwezi kumlipa.
Baadaye alirudi na chapatti na supu akaniwekea nikaanza kula. Njaa ilikuwa ni kali lakini hamu ya kula sikuwa nayo kila nilipokuwa nikikumbuka niliyotendewa hakika niliumia sana moyoni, nilijikuta machozi yananitoka na kuamini kwamba sina bahati.’
Nilijuta kwenda chuo bila kuwa na uwezo….
Namba 6
Muda wa saa kumi ulipofika nilikuwa bado niko hospitalini, nashukuru walinisafisha ili nisiathirike na kuingiliwa, nilipewa dawa ambazo zingeniepusha na virusi vya ukimwi ambazo zinaitwa PEP.
Nikiwa nimelala tu kitandani nawaza mambo mengi sina mawasiliano na rafiki zangu wala ndugu zangu, ndipo alipoingia tena yule nesi akiwa ameshika simu yangu ile ya Tecno K7 mkononi. Akaniambia “Shika simu yako”
Nilifurahi nikaipokea na kuishangaa ni kweli ni ile ile tena ilikuwa na chaji asilimia mia “Umeipar wapi?” nilimuuliza
“Ameniletea mtoto wangu”
“Mtoto wako???” nilimuuliza kwa mshangao “Ananijua?” nilimuuliza
“Ndio anakuja muda sio mrefu ameenda nyumbani kuoga mara moja” aliniambia yule nesi
“Mtoto wako anaitwa nani??” niliuliza ili hata akinitajia jina huenda nikafahamu ni nani
“Anaitwa Lenard” alisema
“Lenard??” niliuliza huku nikifikiria Lenard ni yupi lakini kiukweli sikukumbuka hilo jina kama ni la mtu ninayemfahamu “Mbona mimi simjui??” niliuliza
“Hahaa…pole lakini yeye anakufahamu” aliniambia mama yule akiwa anatabasamu kiukweli alionekana kuwa na roho nzuri sana, nilimshangaa alikuwa mama wa aina gani.
“Naomba akija please anione” nilisema
“Usijali…basi mi nikuache narudi” alisema
“Okay”
Yule mama alitoka akaniacha pale ndani, kidogo furaha yangu ilianza kurudi, nilijiona sijatengwa sana na dunia, nikaangalia kuna watu walikuwa wamenipigia kwenye simu, nikajaribu kuwatafuta lakini kifurushi kilikuwa kimeshaisha muda wake.
Ilibidi nikope salio la elfu moja nikajiunga, nikaanza kuwapigia watu waliokuwa wamenitafuta, wa kwanza alikuwa ni Zena ambaye ni mmoja kati ya wale marafiki walioniacha matatizoni siku moja kabla.
“Zena” nilisema baada ya Zena kupokea simu
“Uko wapi shoga mbona hukurudi tena nyumbani” niliposikia sauti yake kiukweli nilighadhibika sana, niliona jinsi walivyo wanafiki yeye na Betina, hawakunijali kabisa, hawakujal afya yangu hata kidogo.
Nilijikuta machozi yanaanza tena kunitoka nikaanza kulia na kumuuliza “Ina maana kweli mliamua kuniuza kwa wanaume wenu?? Mlitaka waniue?? Nashukuru sana Zena ila Mungu atawalipa” nilisema kwa uchungu
“Pole….sisi hatukujua kama itakuwa hivyo, nasikia upo hospitalini, ni hospitali gani hiyo tuje kukuona??”
“Niko hospitalini? Nani kakuambia?? Sitaki nimuone mtu hapa, urafiki wangu na nyie, umeisha mmeshaniharibia maisha yangu” nilisema kukata simu yangu
Bado hili nalo liliniumiza ubongo, nilikuwa nawaza ni nani amewaambia kwamba niko hospitalini? Nikajua lazima aliyenileta pale hospitalini sio mwingine ni mtu ambaye anafahamiana nao.
Nilijisikia vibaya nikampigia simu mama yangu kijijini nikamuambia ukweli “Mama nataka kurudi nyumbani sitaki kusoma tena”
Mama akaniuliza “Mwanangu kwa nini unasema hivyo?”
Nikamjibu “Maisha ni magumu mama, sina hela, sina chakula, mnataka nijiuze??” niliuliza
“Pole mwanangu ukiona maisha yamekuwa magumu basi wewe rudi nyumbani sisi hatuna uwezo” alisema mama bila kunificha jambo lolote
“Sawa” nilisema na kukata simu nikashika tama na kuendelea kuwaza mambo mengi, na kila nilipokumbuka njia ngumu nilizopitia basi nilijikuta nadondosha machozi na hata kutamani kutoweka duniani.
Nikiwa nina mawazo yangu pale, nikapata jibu kwamba nimuombe yule mama nauli niondoke nirudi tu Singida, ila ghafla nikasikia sauti ya mwanamke na mwanaume wakiwa wanakuja kule wodini.
Nikaangalia mlangoni ndipo akaingia yule nesi pamoja na kijana ambaye jana alikuwa ni mmoja wa wale walionitoa kule mawasiliano park.
Alikuwa sio mwingine alikuwa ni Mido ambaye alikuwa ni mwenye gari ile iliyonichukua jana yake. Mido ndiye alituacha pale Ubungo Riverside akidai anaenda kutoa hela lakini akachelewa kurudi mpaka wale vijana wengine walipochukua gari na kunipeleka Novo.
Nilimtazama nikashtuka akaniambia “Mambow” lakini sikuitika nilikuwa namuangalia, naona aibu, najua alikuwa anajua kila kitu kilichonitokea kwa hiyo nilijisikia vibaya.
Nilimuona naye pia ni mkosaji sana kwangu, nikamuuliza “Kwanini umekuja hapa?”
Akaniambia “Mimi ndiye nilikuleta hapa hospitali” alisema na kumshikama yule nesi begani akaniambia “Huyu ni mama yangu” nikashtuka kidogo
“Nesi, huyu ndiye aliyenileta??”
Nesi akatabasamu na kunijibu “Ndiyo, huyu ni Lenard ambaye ni mwanangu” alisema
“mh” niliguna na kuinamisha kichwa, halafu nikainua na kumtazama, nilikuwa nalia yule mama akashangaa na kuuliza
“Mbona unalia tena? Kwani vipi”
Lenard ambaye kwa jina lingine ni mido alimgeukia mama yake na kumuambia “Mama, huyu analia kwa sababu nilikuwa naye jana kule mawasiliano Park, lakini baadaye wenzangu Dullah na Frank waliondoka naye ndio walimtorosha na gari yangu, wakamtendea yote haya”
“Anhaaa….mwanangu wale marafiki zako wana kazi gani? Si uachane na wapumbavu wale??” alisema mama
“Hapana, hata wewe ulihusika ulikuja mara ya mwisho, unafikiri sikujua?” nilisema kwa hisia tu ila sikuwa na uhakika
Mama akamtazama Lenard ila hakuzungumza chochote. Lenard akasema “Mama naomba uondoke kidogo nizungumze na huyu binti”
Mama akabetua mdomo kisha akageuka na kuondoka zake.
Mimi na Lenard tulibaki pale ndani peke yetu, ile ward haikuwa na wagonjwa wengine ndipo Mido akaniambia “Samahani kwa yote yaliyotokea jana, najua unaumia sana unaponiona hapa. Nilikuonea huruma sana baada ya kuja kwenye gari na kukuta marafiki zangu wamekutendea mambo magumu kama yale, naomba unisamehe mimi kwa niaba yao, nimeamua kuachana na marafiki wa hovyo kwa sababu wananifanya naonekana muhuni wakati sio kweli, pole sana”
“Mido” niliita kwa hasira
“Unanifahamu jina??”
“Nakujua ndio, kama kweli umeamua kunisaidia naomba tukawafungulie kesi, wamenidhalilisha sana hao wajinga…”
Mido alinitazama kwa muda mrefu sikujua anawaza nini, ila baadaye aliniambia sentensi ambayo ilinifanya nimshangae kwanza………
JE MIDO ALISEMAJE?
Namba 7
Mido alinitazama kwa muda mrefu sikujua anawaza nini, ila baadaye aliniambia sentensi ambayo ilinifanya nimshangae kwanza
“unasemaje Mido?” nilimuuliza
“Nimeshawakamatisha wapo kituo cha polisi”
“Kisa nini??” niliuliza
“Kwa sababu yako…kiukweli nilikasirika sana, walitaka kuniharibia gari yangu kisa upumbavu wao, halafu yule mdogo mdogo ana ugonjwa” aliongea nikashtuka
“Ugonjwa gani??” niliuliza huku moyo ukinienda mbio
“Sorry, ana ukimwi” aliniambia nikajikuta nimeinuka nikamrukia na kumkaba koo
“UKIMWI? Ukimwi mmeamua kuniua??” nilimuuliza
“Usijali huwezi ukapata ugonjwa huo”
“Kivipi? Naomba uniambie ukweli, mi nitajiua et” nilisema huku nikitokwa na machozi tayari
“Kuna vidonge mama yangu atakupatia vinaitwa PEP ni vidonge ambavyo vinasaidia kuua virusi vya UKIMWI vinavyoingia mwilini ndani ya masaa sabini na mbili, utavitumia kwa miezi sita”
“Wewe..kwanini mmenifanyia hivi lakini Mido….kwanini??” nilisema kwa uchungu nikajiangusha, sikuamini kama kweli kuna kupona ugonjwa mkubwa kama ukimwi.
Kiukweli niliumia sana, nilikuwa nawaza nimemkosea nini Mungu, nimejilinda miaka yote mpaka nimefikisha miaka 20 sijaguswa na mwanaume yeyote, halafu mwishoni Mungu anaamua kunipa adhabu ya ugonjwa kweli? Nilijisikia vibaya, nilimlaumu sana Mungu.
Nililala nikilia sana, ndipo Mido akaketi kando yangu na kuniambia “Samahani sana ila nimeamua kukupa msaada kama huu utimize ndoto zako, najua unahitaji kuendelea kusoma”
“Hapana. Bora nisingekuja chuo, hapa chuoni ndipo nimepatia haya mateso, kwanza mimi mtoto wa masikini sitaki kusoma tena” nilisema kwa uchungu
“Pole sana….kwani hauna mkopo chuo??”
“Ningekuwa nao nisingekuwa na marafiki wa hovyo kama Zena na Betina, wao ndio chanzo cha mimi kupata tabu hivi, kiukweli ninawachukia sana wanawake wale daaaah” nilijifuta na shuka kwa uchungu sana.
BAADA YA SIKU TATU
Nilikuwa nimeshakuwa sawa, test one ilikuwa imekaribia, nilikuwa nang’ang’ania sana kwenda chuo, nilikuwa nataka nikasoma kwa sababu nilijua vitu vingi vimeshanipita.
Mama yake Lenard aliniruhusu niondoke, lakini nilikuwa na rundo ya vidonge vya kuendelea kumeza kila siku mpaka vikiisha nifuate vingine pale.
Kiukweli sikugharamia kitu chochote pale hospitalini, vyote walinilipia familia ya mama Lenard. Kikubwa zaidi Lenard alimpatia mama yake shilingi elfu hamsini inisaidie nikienda hostel wakati najiweka sawa.
“Asante sana mama Mungu akubariki” nilisema huku nikipanda bajaji inipeleke hostel
“Sawa, chukua namba yangu halafu halafu utanitafuta, usisite kunipigia simu ukiwa na tatizo” alisema yule mama
“Sawa” nilisema na kutoa simu nikaanza kuandika namba yake.
Niliondoka, mpaka nikafika hostel, nikaingia ndani nikakuta wanafunzi wengine wamekaa pale wananishangaa “Heee Ester ulikuwa wapi jamani siku zote hizo” aliniuliza mmoja lakini mi sikujibu nilipita zangu mpaka room.
Nikaketi kitandani nikawa nawaza mambo mengi bado sikujua kipi cha kufanya.
*
Mimi sio mtu wa kupenda kuomba omba sana, nilikuwa sijafahamu kwanini mama yake Lenard alikuwa ameamua kunitendea wema kiasi kile, sikuthubutu kumtafuta licha ya yeye kunipa namba na kunisisitiza niweze kumtafuta na kama nahitaji msaada wowote niwe nampigia simu.
Niliachana na marafiki zangu kina Zena na Betina, niligeuka mpweke nilipenda kuishi peke yangu, sikuona msaada wowote nilikuwa nikiupata kwao zaidi ya dharau na maumivu makali ambayo yamegeuka kovu katika moyo wangu.
Ilipita wiki moja nzima, nasoma peke yangu labda kwenye group discussion ndipo nilikuwa nakutana na watu wengine, nilijisikia kuishi peke yangu umasikini wangu ungenitosha mimi pekee, nilisali nikiamini Mungu atanijalia.
Nilijisemea moyoni kwamba kama nikiona maisha yamekuwa magumu nitaondoka chuoni kwa sababu sio lazima kusoma kama ni kupata tabu kiasi kile, nilikuwa najua pia hata nikisoma, ishu ya kupata ajira ni ngumu kuliko kipindi cha zamani.
Maisha yalisogea siku zikaenda kama wiki tatu mfululizo nilikuwa nameza zile dawa za pep zikapelekea mimi kubabuka upande mmoja wa mwili wangu kuanzia shingo hadi tumboni na mkono wa kushoto, nikaogopa. Siku moja nikiwa zangu hostel mida ya saa moja jioni, akanifuata Betina
“Mambo vipi Ester?”
Nikamjibu “Safi tu”
“Unatafutwa pale nje”
“Na nani??” niliuliza
“Mido anakuita” alisema Betina
“Mh” niliguna kidogo kwa sababu nilikuwa nimeshaanza kumsahau Mido ambaye alikuwa amenipa msaada wiki kadhaa kipindi cha nyuma, bado sikuhitaji kuishi karibu na watu walioijua hiyo siri. “Ananiitia nini??” niliuliza
“Sijui” alinijibu Betina kisha akatoka nje na kuniacha mimi ndani nimekaaa.
Nilitafakari kwa dakika nzima, mwishowe nikaamua niende nikamsikilize labda anaweza akanipa neno ambalo lingenifariji katika maisha yangu. Nikatoka nje ya room na kumfuata, ilikuwa ni nje ya hostel kabisa barabarani.
Nikamkuta ameegemea gari yake anachezea simu, nikamfuata “shikamoo” halafu nikaweka mikono kifuani na kutazama mbali
“Mambo vipi” alisema huku akiweka simu mfukoni, badala aseme marahaba naye ananisalimia kihuni
“Poa tu” nilisema “Nimeambiwa unaniita na Betina”
“Okay ni kweli, nimekuja kukuona unaendeleaje, sikuwa na namba yako na wala sikutaka kuomba kwa mtu, kwa sababu mama alikupa namba na hukutaka kumtafuta sijui alikukosea nini”
“Hapana hajanikosea, nilikuwa nakosa kitu cha kumuambia mama ako”
“Okay..unaendeleaje na afya yako?”
“Niko sawa tu, ila kuna taabu nazipata nimebabuka mwili, nimeenda kwa daktari ameniambia kwamba ni zile dawa zinaniathiri”
Mido alitoa simu mfukoni akanimulika akaniambia “Pole sana, ni kweli zile dawa ni kali kwa sababu zinapambana na seli, kwa hiyo usiwe na wasiwasi, siku ukimaliza dozi, utarudi katika hali yako ya kawaida”
“Sawa” nilisema
“Anyway umepungua pia, una mawazo??”
Nikatazama chini kisha nikainua uso na kumtazama nikasema “Ninakosaje mawazo kwa mfano, lile sio jambo la kawaida kunitokea, limenikosesha raha, sina rafiki, najitenga natamani hata kufa darasani sielewi, nikimaliza semester hii, nitaahirisha mwaka”
“Pole” aliniambia “Anyway, nilikuwa nakutafuta kumbuka kuna kesi inaendelea mahakamani, wewe unapaswa uwe kama shahidi wa wale vijana waliokufanyia kitendo cha kinyama, kwa hiyo jumatano ijayo naomba tukutane asubuhi sana” alisema
“Kesi??” nilishtuka
“Ndio, niliwakamata vijana wale, ninaandaa ushahidi kwa ajili yako”
“Hapana, sidhani kama nitapata faida yoyote, achana nao Mungu atalipa kwa ajili yangu” nilisema huku machozi yakinitoka “Sihitaji kuonana nao, ninawachukia” aliniambia
“Sawa, usilie sasa……nipe namba yako tutawasiliana zaidi” alisema Mido
Nilimtajia namba, akanipa shilingi elfu kumi halafu akaondoka, mimi ni masikini sikujua kwanini Mido aliamua kunisaidia katika maisha yale ambayo sikuwa na rafiki yoyote mwenye uwezo…..
Namba 8
Alipoondoka na mimi niliondoka nikaenda hostel, nikajisomea kisha nikalala zangu mapema tu.
Kuanzia siku ile tukawa tunawasiliana mara kwa mara mimi na Mido, ananisaidia mambo mengi, ushauri na hata kunipa kampani akawa ni rafiki wa karibu japo alikuwa mkubwa sana kwangu.
Mara zote nilikuwa sitaki rafiki wa kike, kwa sababu lile suala lilishaniharibu kisaikolojia, nilihisi rafiki wote ni sawa na Zena na Betina.
Nilikuwa nikiwaona najisikia vibaya, ni moja ya watu ambao niliwapa siri nyingi za maisha yangu, na udhaifu walipoujua waliutumia kuniharibia mipango yangu yote.
Usiku nikiwa naongea kwenye simu na Mido nilimuuliza
“Kwanini wewe uliamua kunisaidia mimi??”
Akanijibu “Mh mambo haya ni kama kutoa sadaka tu, sio kwamba nilishindwa kukutelekeza pale, either ufe au upate ukombozi, labda ungeshakuwa kahaba au tushakusahau. Kwa kuwa mimi sio mmoja wa watu wanaopendelea vitu kama hivi kiukweli mimi sio mtu wa kawaida kama wengi wanavyodhani”
Haya maneno yalinishtua kidogo na kumuuliza “Wewe sio mtu wa kawaida kivipi??”
Akajikoholesha na kunisemesha “Unajua Ester…..wale washikaji wangu Dullah na Frank walikuwa ni marafiki wapya kabisa kwangu…tulikuwa tuna wiki mbili tu tangu tujuane, lakini hawakujua kwamba mimi sio mwenzao…. walihisi mimi ni mwenye tabia ka maza kwao, an ndio maana walichukua gari yangu kienyeji tu na kwenda kufanya nayo uhalifu, sipo hivyo”
“Mh una maana gani kusema hivyo???”
“Nisamehe kwa hili Esta…..nilikuingiza matatizoni” aliniambia
“Matatizoni?? Kivipi”
“Nikikuambia kitu utakiweka moyoni au utamuambia mtu??” aliniuliza
“Hapana sitamuambia mtu, niamini”
“Ester” aliniita
“Abee”
“Wakati nilipoacha gari pale Riverside siku ile nikajifanya naenda kutoa hela haikuwa kweli” alisema
“Mh” nikaguna
“Nilienda kukaa mahali, nikaangalia kitu wanachofanya vijana wale, na walipoondoka na wewe sikujali kwa sababu gari ilikuwa na GPRS nikijua nitaiona kila inapoelekea”
“Mh kwa hiyo uliona wakiniteka ukaniacha??”
“Hapana, nilikuwa kazini”
“Kazi gani??”
“Ah mimi ni askari upelelezi….nilikuwa nahitaji ushahidi ukamilike ili niwakamate vijana wale”
“Wewe” nilisema kwa mshangao, sikujua kama Mido alikuwa ni askari
“Ndio hivyo…kwa hiyo nilipoona madhara ni makubwa kwako, ilibidi nikupeleke hospitali ukatibiwe lakini kiukweli wale majamaa pale mahakamani hawachomoki…..mimi niko nyuma ya hili, tuko hapa Dar kufanya mji uwe salama”
Ni kweli aliongea jambo la maana lakini liliniumiza zaidi nikaona kama alinikosea sana kunifanya niumie, niteseke, nipate maumivu na nidhalilike kwa ajili tu ya ushahidi.
Nilijikuta nalia, na kumlaumu Mido nikimuona hana huruma hata kidogo, nilitulia kimya huku simu ikiendelea kuwa hewani akawa ananiita
“Esta…….Esta……..Esta” lakini mimi nikawa kimya.
Baada ya dakika moja aliona ni heri akate simu kisha akanipigia tena, nikapokea nikiwa nadhani labda kuna kitu fulani kinanifanya nimuamini, nikamuuliza “Vipi??”
“Nisamehe esta”
“Hapana kwa hili kiukweli kukusamehe ngumu, nimeharibiwa maisha kwa sababu ya kesi kweli??? Bora ungetumia njia nyingine”
“Sikutarajia kama ingekuwa hivyo nisamehe, vile vile mama yangu ana foundation inayo-deal na wazungu, naomba nikuunganishe naye atakusaidia usome mpaka umalize chuo” aliniambia kidogo maneno yaliyonifariji na kujikuta hasira zinapungua.
“Daaah…..naumia sana….hili jambo litafutika lini akilini mwangu Mido…..kwanini uko hivi?”
“Nisamehe” alizidi kuniomba msamaha
“Daah aiii” nilisema na kufuta machozi, nilikuwa nimeharibikiwa kisaikolojia kabisa, niliona dunia chungu
“Umenisamehe??”
“Tatizo sio kukusamehe….tatizo nakosa amani, kila mara nikikutana na watu wanajua nilichofanyiwa, hapa hostel kwenyewe sikai kwa amani, ninasikia uchungu…..nasikia maumivu”
“Okay kwa sababu nimekufanya ujisikie vibaya, i promise you, nitakutafutia chumba, nitakupangishia na kila kitu nitakuwekea, utaishi mwenyewe ili saikolojia ikae sawa”
“No sitaki” nilisema kwa hasira
“Tafadhali ondoka hostel, nitakupatia room nzuri sana, au kama unaona vipi, pale nyumbani utakaa na mama, yupo na mtoto wangu mdogo na housegirl maisha mazuri tu, usiogope…..”
“Hapana Mido bado nitazidi kuumia”
“Sina nia mbaya, sihitaji penzi lako, sihitaji chochote, ila ninajisikia kukusaidia, najua maisha magumu ya chuo ndiyo yalikupelekea ukutane na yale maswahibu, kwa hiyo niko tayari kukufanya uwe na furaha”
DAAA NILISHINDWA NIMJIBU NINI…….
INAENDELEAAA