MAMBO KUMI USIYOYAFAHAMU KUHUSU WANAWAKE WALIOKO KWENYE NDOA!
1. Ukimya unaashiria ana zaidi ya hasira (amekasirika sana), kuwa makini.
Kwahiyo, iwapo umemkosea mke wako au mwanamke uliyenaye kwenye mahusiano na yuko kimya, kuwa makini tambua anaweza kupanga mipango ya hatari ya kukudhuru wewe au yeye mwenyewe.
2. Anatambua harufu yako!
Harufu yako anaifahamu, utakapojaribu kumsaliti au kupaka mafuta yeyote yasiyo toka nyumbani au kukumbatiana na yeyote. Tambua kuwa, mke wako atajua tu!
3. Anatambua mavazi yako,viatu vyako na nguo zako za ndani.
Vyote unavyovaa kwenye mwili wako anavifahamu. Chochote kipya ambacho utapokea kama mavazi au kukinunua pasipo kumshirikisha jiandae kujibu maswali ya “Umevitoa wapi?”, “Umenunua lini?”, Umepewa zawadi na nani?” na maswali mengi yenye kufanana na hayo.
4. Anakulinganisha na wanaume wengine.
Tambua kuwa mke wako au mwanaume wako anakulinganisha na baba yake, ex wake, marafiki zake wa kiume huko zamani,Kaka zake na pengine watu maarufu wenye jinsia ya kiume. Jitofautishe kuwa bora zaidi yao angalau hata kidogo ili kulinda heshima yako!
5. Anakuongelea akiwa na marafiki zake kipenzi.
Hivyo basi, muonye kama inawezekana kwa mustakabali wa ndoa yenu na uchumi wenu. Hapaswi kuongelea siri za ndoa kwa yeyote yule iwapo mnaishi vizuri kwenye nyumba yenu, wenye wivu watajipanga vita na nyinyi kuwavuruga! VITA KWENYE NDOA KWA ASILIMIA KUBWA INAANZIA NJE.
6. Anaweza kukusamehe, lakini hawezi kusahau.
Hivyo basi jitahidi usimuumize au kumfanyia vitendo vya kikatiri. Unaweza fikiri amekusamehe kumbe anajipanga kukulipiza, wanawake ni rahaisi kusamehe lakini ni wagumu kusahau MAUMIVU.
7. Atakuepuka iwapo amekukosea au amekuumiza
Kama amekufanyia jambo baya sana pengine USALITI, ataanza kukuepuka au kujitenga na wewe. Mara nyingi katika kipindi hiki anakua akijutia makosa yake, wengi huishia kujiua au kujidhuru.
8. Ana mpango wa pili(Plan B) ya mahusiano yenu iwapo yatafeli.
Wanawake wana plan B ya ndoa au maisha yao. Hivyo basi, mnaishi naye kwenye ndoa lakini ataonyesha ishara ya ubinafsi kwenye “matumizi ya pesa na mali”. Yaani, cha mwanaume ni cha familia lakini cha kwake ni cha peke yake kwasababu anajaribu kulinda PLAN B YAKE ISIHARIBIKE.
9. Anatamani angekuwa shupavu kimwili kama alivyo mwanaume ili asiweze kunyanyasika.
Kuna wakati anajutia namna alivyoumbwa mwanamke. Kuna wakati anatamani na yeye angekuwa mwenye nguvu apambane na wanao mnyanyasa au kumuumiza.
10. Anaweza kukudanganya kwa makusudi ili kukulinda pasipo kujali matokeo ya yeye kukudanganya.
Mwanamke kuna wakati atakudanganya au kufanya jambo baya kwa siri(kubeba mimba nje ya ndoa iwapo mwanaume ana tatizo la uzazi), kushiriki ubaya wowote(kwenda kwa waganga wa kienyeji) ili tu kukulinda wewe au familia yenu. Yote haya atayafanya pasipo kumshirikisha mume wake pasipo kujali matokeo mabaya.