NAOGOPA KUWA MWANAMKE 11
Sasa huo wanja na hizo rangi mdomoni zimefata nini!?..
iish.. Inamaana hazikufutika nilibaki nimezubaa wameshajua kuhusu mimi.
“Mwanamke mpumbavu sana huyu.. Ni mpenzi wangu itakuwa amenivizia mda nimelala.. Nilisema huku nikijifuta na kuwaacha peke sikujua watasema nini nilielekea chooni kujitazama kwenye kioo nikilaani kitendo cha kutoka nyumbani bila kujitazama kwa kioo.
Nilinawa uso na kuelekea kwa yule secretal baada ya kuniona alitabasamu..
“Ulimtolea wapi yule dada hakika sikutegemea nilijua nimeshafeli..
Nilikenua na kumuuliza “Nilishindwa kuja jana vipi alilitendea haki jukwaa!?..
“Sanaa.. Mpaka Boss Kelvin hakutegemea alimpatia 1 million.. waharikwa wote walifurahia.. Nilitabasamu na kuwaza haraka haraka kumbe jana nilikabidhiwa pesa ndefu hivyo ambazo sikuwahi kuzishika tangu nizaliwe nilitamani kurudi nyumbani nikahakikishe maana sikuzihesabu kabisa.
Niliagana nae na kuondoka mda wa kazi uliisha sikupanga kurudi kwa kina Bob nilitaka kwenda nyumbani nikiwa napiga hatua nilisimamishwa alikuwa ni Bob.
“Siku hizi umehama na geto kabisa..
“Hamna kuna mambo yangu naweka sawa.. Muhimu nakuja kazini. Nilimjibu Bob
Mda huohuo Brayton alifika mahali hapo akiwa na bahasha Bob aliondoka “Naona siku hizi umenitenga sana dogo.
“Ni harakati za kutafuta maisha Broo.. Nilimwambia huku nikijitahidi kumkwepa sikuwa namuamini kabisa Brayton.
“Sawa kuna picha nilikuja kuchukua ofisini kwenu..
“Picha za nini? Au kuna bidhaa unataka kuagizia.. Nilimuuliza Brayton.
“Licha ya bidhaa kuna dada alikuwa anadance sana jana kwenye event nilikuja kuchukua mawasiliano yake.. Alisema Brayton na kufanya nishikwe na kitete.
“Sasa wewe wa nini Broo.. Nilishindwa kuvumilia nilijikuta nimeuliza.
“Jana nilimsaidia sasa aliangusha mkufu wake kwenye gari langu… Nilitoa macho hayo nisiamini nilichokisikia kumbe ule mkufu wa thamani wa Mama G ulinidondoka..
“Unawaza Sana eti.. Kama sijampata nitauza tu.. Alisema Brayton huku akipiga hatua kuondoka nilibaki nimeduwaa nilimkimbilia na kumuuliza.
“Kwahiyo ulifanikiwa kupata namba zake!?..
“Kelvin ameninyima maana nahisi anafahamiana nae ila si muhimu sana.. Teyari alishawasha gari lake na kuondoka sikuwa na cha kusubiri tena niliwahi nyumbani uwenda ni uongo wa Brayton tu.
Kitu cha kwanza ilikuwa ni kuangalia ule mkufu kweli sikuuona kabisa nilipekua na kupekua haukuwepo niliikaribia bahasha yangu niliyokabidhiwa jana nilihesabu zile pesa haraka haraka zilikuwa ni milioni moja nilichomoa laki tatu na kuondoka..
Nilienda kutafuta sonala ili wanichongee mkufu kama ule lakini kila ninapoenda nikiwaelezea wanasema muundo wa zamani sana na ni mkufu ulioingia dhahabu nyingi sana bila milioni ishirini haliwezi kutengenezeka mwili ulikufa ganzi kabisa.m
Nilienda sehemu kama tano zote majibu yalikuwa yanafanana niliamua kurudi nyumbani tu nikiwa mlangoni nilisikia sauti ya Mama G ikiniita..
“Vipi vitu vyangu vimerudi salama eh?.. Aya nipe mkufu wangu kwanza kesho kutwa nina mtoko na baba ako.. Nilizama mfukoni na kuchomoa laki moja.
“Sikia shika hizi naenda kumalizia kazi kesho nitakuletea.. Nilisema hivyo na kuondoka sikutaka kuingia ndani tena moja kwa moja nilienda kwa Brayton nilipanga kuuiba mana nisingeweza kujitokeza mbele yake nikiwa vile ni rahisi sana kwake kunitambua………………….
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 12
Sikia shika hizi naenda kumalizia kazi kesho nitakuletea.. Nilisema hivyo na kuondoka sikutaka kuingia ndani tena moja kwa moja nilienda kwa Brayton nilipanga kuuiba mana nisingeweza kujitokeza mbele yake nikiwa vile ni rahisi sana kwake kunitambua.
Nilifika nakumkuta Brayton akiwa amelala sebren pembeni yake niliuona ule mkufu..
“Mimuh kuna issue nataka ufanye..
“Ni ipi hiyo!?.. Niliuliza lakini akili yangu yote ilikuwa kwenye ule mkufu wa mama G.
“Ona ulivyotoa macho toa dongo tule nina njaa kinoma noma.. Alisema Brayton huku akitabasamu kuhusu kupika halikunipa shida niliandaa msosi chap baada ya sekunde kadhaa tulikuwa mezani tukipata chakula nilivunja ukimya..
“Vipi kama yule mwanamke hajatokea?.. Niliuliza swali la kizushi.
“Si nitauuza tu.. Alisema Brayton huku akipigilia chakula.
“Utauza pesa ngapi sasa ni vyema ungemkabidhi hata Kelvin si anamjua lazima atampa.. Nilisema hivyo kwasababu hata nikienda kwa Boss hawezi kunitambua..
“Siwezi kumpa Kelvin ni pesa ndefu hii kama hajatokea mwenyewe basi nitauza tu..
Hamu ya chakula ilikata ghafla nilinawa na kutoka nje niliitazama sana simu yangu nia yangu ilikuwa ni kumpigia Kelvin kwa kuwa nilikuwa na namba zake sikupata shida nikitumia ile line ambayo nilitumia kuwasiliana na secretary basi nilimuelezea shida yangu kuwa nimeangusha mkufu kwenye gari ya rafiki yake aliyenisaidia siku ile bila kujieleza sana alishanielewa..
“Subiri Mda si mrefu nitampigia jibu nitakalopata nitakwambia.. Nilikata simu na kurudi ndani kidogo moyo wangu ulitulia.
Nilikaa kwenye kiti huku akili yangu ikiwa kwenye simu ya Brayton mda si mrefu ilianza kuita alitazama jina na kupokea.
“Kelvin.. nambie mwanangu.
Sikusikia sauti ya upande wa pili “Mpe namba zangu nimpe maelekezo aje afate au kesho nikutane nae hapo ofisini.
Alisema hivyo na kukata simu nikibaki nimekodoa macho nilijifanya nimepokea simu ya dharula nikaondoka.
Nilifikiria kwenda tu kuuchukua ule mkufu sababu kesho mwenyewe ana uhitaji nilikamata simu yangu na kumpigia Kelvin alinambia kama alivyosema Brayton kisha alinipatia namba za Brayton.
Nilijiandaa vyema safari hii sikutaka aibu nilivaa viatu simpo tu nilielekea saloon ya kike kivyovyote make up ndio inayoweza kunibadilisha kwa siku ya leo..
“Samahani dada naomba unifanyie make up..
Nilimwabia dada huyo ambae alikuwa chap na kazi yake baada ya robo saa teyari nilishapendeza..
“Sasa hapa hawezi kunitambua kwa lolote..
Nilikamata kisimu changu na kupiga namba ya Brayton kwa kutumia line yangu nyingine ambayo hata Brayton haifahamu alipokea nilijitambulisha kisha akanipa maelekezo..
Baada ya dakika kadhaa nilifika nyumbani kwa Brayton nilimkuta akinisubiri baada ya kuniona aliachia tabasamu..
“Sikujua Kama ungefika karibu ndani..
“Ahsante but now nina haraka sana.. Nilisema kwa mapozi huku nikijifanya kuchanganya lugha.
“Hapana ni vyema ungepita ndani sababu hata ulichokifata kipo ndani.. Nilijikaza na kupita ndani lakini sikuhitaji kukaa.
“Samahani Brayton nina haraka kuna mahali nahitaji kwenda..Nilisema hivyo na kufanya Brayton anipatie ule mkufu nilishukuru sana maana sikutegemea kama ingekuwa rahisi hivi.
Nilimshukuru na kupiga hatua kuondoka lakini nilivutwa mkono kurudishwa nyuma..
“Umekua mrembo mara dufu.. Alisema Brayton sikumjibu nilikuwa nikihema mfululizo ujasiri wangu na kujiamini kote kulipotea.
Safari hii alinibandanisha ukutani taratibu alianza kunisogelea usoni nilijawa na woga nilisema kwa sauti ya kukwama kwama sikuthubutu kumtazama mda wote macho yangu yalikuwa chini “Unataka ku..fa..nya ni..ni!?.
Kabla sijaendelea zaidi alinipa busu la paji la uso nilisisimka mwili mzima na kufanya nigande mbona nimekuwa mdhaifu hivyo.
“Ni ishara ya upendo.. Nadhani uwezi kunifikiria vibaya rafiki yangu.
Alisema huku akitoka nje nilimfuata pia lakini sikuwa na imani nae kabisa alipanda ndani ya gari nilitaka kuongoza njia lakini alinizuia..
“Njoo nitakupeleka..
Alisema Brayton niliona hapa kitakachonisaidia ni miguu yangu nilitazama upande wa geti kisha nilimtazama Brayton ambaye alikuwa busy kufunga mkanda..
Niliukamatia mkoba wangu vizuri sikuhitaji kuuliza nilitoka kibati bila kutazama nyuma kiatu changu kimoja kilinichomoka lakini sikujali na vile vichichoro vyote nilikuwa navijua nilifika nyumbani moja kwa moja nilipitiliza ndani nilifungua mkoba na kuutazama ule mkufu nilishukuru baada yakuona ndio wenyewe……………….
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 13
Nilimfuata mama G na kumkabidhi mkufu wake..
“Siku nyingine hata nikija kukuomba kwa bahati mbaya usinipe..
Nilisema huku nikifungua friji na kunywa maji maana nilikuwa sina pumzi za kutosha “Sijakuelewa ina maana umechukia..
Aliuliza mama G bila kuelewa nilimaanisha nini “We elewa hivyo tu.
Nilitoka mule ndani nilianza kuzipangilia pesa zangu vizuri “Kesho napokea mshahara wangu nikiongeza na hizi nitakuwa nina pesa ndefu zitanifaa kuanzia maisha nampango wa kuhama huu mji kabisa..
Yote yalikuwa mawazo yangu simu yangu ilikuwa ikiita na si mwengine alikuwa ni Brayton niliipotezea niliamua kumpigia Kelvin..
“Mambo Kelvin..
“Poa mrembo vipi ulifanikiwa kupata huo mkufu!?.. Aliuliza Kelvin.
“Ndio nilipata.. Nimekupigia kukushukuru Ahsante. Nilisema na kukata simu kisha niliiazima kabisa.
Hatimaye siku ilipita asubuhi niliamkia kazini kwakuwa ilikuwa ni tarehe ya mshahara sikutaka kuchelewa kabisa mapema tu nilikuwa kazini..
Baada ya kazi tuliambiwa pesa zimeshaingiza kwenye account zetu..
Nilirudi nyumbani nikiwa na furaha niliiwasha simu ambayo nilikuwa nimeizima ziliingia sms mfululizo kutoka kwa Kelvin..
“Nakupenda naomba unikubalie hutojuta kuwa na mimi”..
Nilitabasamu na kuwaza hivi Boss ndio amenipenda mimi hajui kama mimi kidume mwenzake mda huohuo iliingia sms kwenye simu yangu ilitoka kwa Brayton..
“Una shukrani mbaya sana..
Niliachana nayo sikutaka kujibu chochote nilienda kibandani kununua chakula nilivyohakikisha niko sawa nilirudi nyumbani moja kwa moja nilielekea kwa mama G.
“Mimi nimekubali kuolewa ila nataka niende mbali na hapa ikiwezekana hata nchi nyengine..
Nilimwambia mama G ambaye alionekana kufurahia taarifa zangu “Shamimu katika siku umenifurahisha basi leo ondoa shaka umepata tena nina kaka yangu anakaa Amerika huyo ndio anakufaa.
“Lakini naogopa sana… Nilisema nikiwa nimeinamia chini.
“Usiogope.. Siwezi kukukabidhisha sehemu nisiyoiamini ni jukumu lako kuwa na Familia.
“Vua nguo zako usiung’ang’anie huo muonekano wako itakuwa ni ngumu kwako kupata mchumba..
Nilivuta pumzi ndefu na kuitikia sawa nilipanga niende kwa Brayton kumuaga rasmi kuwa nasafiri ili sisumbuke kunitafuta Brayton amenisaidia sana na ana moyo wa kipekee.
Nilijiandaa na kuelekea kwa Brayton nilimkuta akiwa amekaa aanachezea compyuta yake hakunichangamkia kabisa na haikuwa kawaida yake nilimsalimia..
“Nimekuja kukuaga kesho ninasafiri..
Bado alikuwa kimya hakuniuliza chochote “Asante kwa kila kitu tutaonana mungu akipenda.
Nilimshukuru na kupiga hatua kuondoka nikiwa naondoka sauti ya Brayton ilisema..
“Kabla hujaondoka mdogo wangu anapart yake leo ningeomba twende..
“Sijapanga mizigo yangu siwezi kwenda kwenye hiyo sherehe.. Nilisema hivyo na kupiga hatua nilifika hadi getini lakini Brayton alinifuata..
“Hutochelewa ni part fupi tu Dogo…
Nilirudi kukaa sebren alienda ndani kujiandaa baada ya mda alitoka akiwa ameulamba kinoma nilipata kumuona uzuri jinsi alivyopendeza..
“Kuna nguo pale kitandani nilikununulia jana.
Alisema Brayton huku akikaa nilikimbilia ndani haraka haraka nikijua lazima na mimi nipendeze maana Brayton kwenye swala la kuchagua nguo hajawahi kukosea..
Nilifika chumbani kwake nilikuta mfuko mzuri nilitabasamu na kuusogelea kitu cha kwanza kutoa ilikuwa ni chupi ya kike moyo ulinilipuka niliingiaza tena mkono nilitoa kiatu cha kike nilishindwa kuendelea kuangalia nilinyanyuka na kutaka kuelekea nje mlangoni nilikutana na Brayton akiwa amenikazia macho nilianza kutetemeka huku nikimuangalia kwa woga………………..
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 14
Nilifika chumbani kwake nilikuta mfuko mzuri nilitabasamu na kuusogelea kitu cha kwanza kutoa ilikuwa ni chupi ya kike moyo ulinilipuka niliingiaza tena mkono nilitoa kiatu cha kike nilishindwa kuendelea kuangalia nilinyanyuka na kutaka kuelekea nje mlangoni nilikutana na Brayton akiwa amenikazia macho nilianza kutetemeka huku nikimuangalia kwa woga..
“Vipi??.. Aliuliza Brayton Kama mtu asiyeelewa kitu nilituliza papala na kusema.
“Unanipatia nguo za kike.. Mara hii woga ulitoweka.
“Aah sorry itakuwa nimechanganya mifuko.. Alisema Brayton huku akiutoa ule mfuko na kunipatia mfuko mwengine uliofanana na ule niliupokea na kutazama ndani kulikuwa kuna Jeans, T-shirt ,Kofia pamoja na Raba nilitabasamu na kutoka mule ndani.
Nilivaa na kupendeza kinoma niliuchana mustach wangu na kutoka nje Brayton aliniangalia na kunionyeshea dole gumba kuwa hapo sawa..
Tulitoka moja kwa moja kwenye gari lake tulipitiwa moja kwa moja kwao ambako ndio kulikuwa kuna part hakuna sehemu aliyonitambulisha nilichukulia poa tu.
Part iliisha mda narudi nyumbani simu yangu iliita alikuwa ni mama G nilishindwa kupokea kabisa Nilikuwa nikiikata..
“Broo nipeleke home moja kwa moja tu mda umeshaenda.
“Nitakupeleka ila baadae now nina mazungumzo na wewe.. Alisema Brayton huku akiongeza mwendo nilikuwa nikiwaza sana ni mazungumzo gani hayo.
Aliendesha gari tulifika sehemu akasimamisha “Vipi mbona hatujafika!?.
“Wee shuka tu.. Alisema huku akiwa amekaza sura nilishuka na kumfata kulikuwa kuna Bar kubwa alichagua meza iliyojificha na kukaa aliagiza bia za kutosha pamoja na nyama choma.
“Umesema una mtoto Shamimu!?..
Aliuliza na kufanya nishtuke maana sikuelewa hiyo Shamimu amemaanisha nini maana kama ameniita mimi vile..
“Ndi..o anaitwa Shamimu.
Nilijiongeza kujibu hivyo niliona Brayton akitabasamu na kukamata chupa ya bia aliimaliza kwa sekunde chache mda wote moyo ulikuwa ukienda mbio hakuniuliza tena chochote kwa kuwa sikuwa mnywaji nilikuwa nakunywa maji tu..
Simu yangu ilianza kuita alikuwa ni Mama G nilisogea eneo lile na kupokea..
“We mtoto huko wapi kesho asubuhi kuna ugeni unatoka Arusha usinitie aibu tafadhali.
Nilivuta pumzi na kusema “Usijali kuhusu mimi kesho nitafika hapo mapema sana ila usinichomeshe usiseme vingi kuhusu mimi vingine vikaushie.
Nilimaliza kuongea na Mama G nikarudi kukaa Brayton pombe ilishaanza kumkolea..
“Broo tuondoke mda umeenda sana.
Alinivuta mkono na kunikalisha chini “Sijawahi kupenda kabla ila sasa nahisi kuchizika..
Alisema Brayton na kufanya niwe makini kumsikiliza “Sasa pombe ndio suluhisho kama kuna mtu umempenda ziweke wazi hisia zako.
Nilisema kwa hisia sana sikupenda kumuona Brayton akiwa katika hali hii na ndio maana tangu nije kwake alikuwa mnyonge sana kumbe mapenzi yanamtesa..
“Mimi nimeshindwa kumwambia sababu ana utoto mwingi sana.
Alisema huku akinitazama usoni macho yake yalibadilika sana mpaka nilikuwa naogopa niliwaza sana ni nani huyo anayependwa na Broo harafu anamchinjia baharini..
“Kama umeshindwa kumwambia mimi nitamuita nimwambie..
Nilisema huku nikimtazama Brayton ambaye pombe ilikuwa imemkolea aswa.
“Mimi najua hawezi kuja.
Alisema Brayton huku akinikabidhi simu yake nimpigie huyo mwanamke nilimuuliza jina alinitajia nilisearch na kupiga nilishtuka baada ya kuona simu ikibablet mfukoni mwangu ina maana simu yangu ndio ilikuwa ikiita..
“Vipi hataki kupokea.. Aliuliza Brayton baada ya kuona nimezubaa huku ikiwa sikioni.
“Anatumika nyanyuka tuondoke.. Nilisema hivyo na kukata sim…………………
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 15
Alisema Brayton huku akinikabidhi simu yake nimpigie huyo mwanamke nilimuuliza jina alinitajia nilisearch na kupiga nilishtuka baada ya kuona simu ikibablet mfukoni mwangu ina maana simu yangu ndio ilikuwa ikiita..
“Vipi hataki kupokea.. Aliuliza Brayton baada ya kuona nimezubaa huku ikiwa sikioni.
“Anatumika nyanyuka tuondoke.. Nilisema hivyo na kukata simu nilimnyanyua Brayton aliyekuwa anapepesuka moja kwa moja tulielekea kwenye gari..
“Mpigie mdogo wako aje kukufata huwezi kuendesha gari ukiwa hiv.. Kwani hata alinielewa ndio kwanza alikaa kwa dereva sikutaka kupanda nilikuwa nimesimama tu..
Nilimuona Brayton akiondoa gari niliwaza nitarudije nyumbani usiku huu nisije kubakwa bure na hakuna kitu na ogopa kama hiko yaani..
Nilianza kuikimbilia gari ya Brayton alikuwa ananiona kupitia side mirror lakini hakutaka kusimama nilimkimbilia mpaka nilichoka maana gari ilishafika mbali niliamua kusimama tu..
Hakukuwa na msaada mwingine kwangu nilisogea pembeni ya barabara na kujikunyata mawingu yalitanda kuashiria mvua inakwenda kunyesha nilikuwa naogopa sana mvua yaani tangu utotoni nikinyeshewa na mvua huwa ni dhaifu sana.
Nilinyanyuka pale chini kabla mvua haijaanza nilikuwa na angaika kutafuta sehemu ya kujifichia maana teyari vinyunyu vilishaanza kudondoka kabla sijapata sehemu ya kujihifadhi mvua ilianza kunyesha kwa kasi sana nilishindwa kuendelea kutembea nilibaki pale pale nimesimama baridi ilianza kunipiga ukizingatia mazingira hayakuwa rafiki..
Sikuona msaada wowote nilianza kulia nilijuta kumfahamu Brayton kama ningelijua wala nisingelihanga kumkimbilia ningebaki palepale Bar.
Kwa mbali niliona kundi la wakaka likija nilipo sikuwa na ujanja nilibaki nikitetemeka nikisubiri hatima yangu.
Niliona bora nichuchumae kama watataka kunidhuru aya ngoja niikabidhishe roho yangu kwa mungu.
“Oya wanangu nyama hiyo imekosa mwenyewe..
Alisema mmoja wao baada ya kunikaribia nilikua nahofu kwelikweli..
“Mambo mrembo mbona uko peje yako unatetemeka baridi twende huku nikakusaidie..
Nilikuwa ni sauti ya mwengine tena alikuwa teyari ameshanikamata mkono..
Nilibaki najiuliza hivi hawanioni kama mimi mwanamme au?
Kumbe ndevu zangu bandia zilibanduka na kuanguka chini kwasababu zililowa maji niligundua baada ya kujigusa kidevu..
Wakiwa bado wanang’ang’ania kuondoka na mimi niliiona gari ya Brayton ikifunga break mbele yetu kisha alishuka na kusema huku akisogea nilipokaa..
“Muachieni huyo..
Walikuwa wabishi Brayton alichomo bastora na kuipiga juu mlio wa risasi uliwatawanya wote na kufanya wakimbie………………….