NAOGOPA KUWA MWANAMKE 06
“Samahani Dada.. Umenionea Mimuh kwa siku ya leo..
“Hapana sijamuona.. Nilisema huku nikiingiza vyombo ndani kwani hata nilirudi tena nje mda wote Nilikuwa nikichungulia dirishani Brayton aliganda mda mrefu mwishowe aliondoka nilishukuru ..
“Mbona unachungulia chungulia?.. Lilikuwa swali kutoka kwa mama G kumbe mda wote alikuwa nyuma yangu akinitazama vyema..
“Hamna.. Nilisema huku nikikaa chini.
“Kesho kuna ugeni naomba utulie hivi hivi.. Alisema mama G huku akikaa pia.
“Ugeni wa nini Mama G!?.. Nilisema huku nikimsogelea..
“Umekua sasa Shamimu unahitaji familia siwezi kukuacha urudi ulikotoka.. Alisema mama G kwa hisia..
Nilikaa kimya sekunde kadhaa kisha nilisema huku nikitoka nje “Nahitaji mda kufikiria wala sio kurupu kurupu..
Nilitoka moja kwa moja na kuelekea nyumbani nilioga na kubadilisha mavazi nilivaa suluari yangu nibana viziwa vyangu na kupigilia Tshirt bila kusahau mzura wangu na ndevu..
Nilipanga kuelekea kwa Brayton kwani aliahidi kunitafutia kazi
Labda ameshanitafutia kazi ndio amekuja kuniulizia ila katika kazi ambazo sijaziweka akilini ni jeshi yaani hivi nilivyo mrahini rahini uko jeshini si nitakufa kabla ya mda.
Moja kwa moja nilielekea nyumbani kwa Brayton nilikuta geti lipo wazi..
Nilipita mlango nilikutana na viatu vya kike ni wazi kuwa Brayton alikuwa na mwanamke..
Niligonga alikuja Brayton kunifungulia “Dogo mbona umehadimika mno..
“Maisha tu Broo nilikuwa naangaika.. Nilisema huku nikiingia ndani..
“Anha sawa kuna mgeni wako.. Alisema Brayton huku tukiingia ndani nilikutana na yule dada ambaye alipolwa mkoba wake na soo likaniangukia mimi..
Walla sikuhitaji shobo nae nilipita moja kwa moja mpaka chumbani kule nikiwa bado nimekaa alikuja yule dada nilishtuka na kusimama.
“Unataka nini chumbani!?..
“Nataka kuongea na wewe Mimuh..
Alisema hivyo huku akijaribu kunisogelea sikushangaa jina langu kalijuaje itakuwa ni Brayton amemtajia “Unataka nini!?.
“Naomba unisamehe unajua nilikufikiria vibaya siku ile nikakusababishia…
Kabla hajamalizia nilimstopisha “Wala usijali unaweza kwenda..
Nilisema huku nikimfungulia mlango lakini bado hakuwa ametoka nilimgeukia na kumuuliza “Unataka nini et..
“Nakupenda Mimuh nimekubali ombi lako… Alisema huku akitaka kunikumbatia.
Nilimkwepa na kumshika mkono huku nikimtoa nje “Naomba uende wala sihitaji mahusiano..
Nilimtoa hadi nje kisha nikarudi sebren aliko Brayton “Mimi sijaja kukaa Broo naomba unipatie msingi mimi sina ndoto ya kuwa mwanajeshi na siiwezi hiyo kazi..
Nilisema hivyo na kufanya Brayton atoe macho kunitazama “Unataka kufanya kazi gani ikiwa huna elimu.. Unadhani huko jeshi unapita bure nimegharamikia na bado naendelea kukugharamikia..
Alisema Brayton na kufanya nikae kimya kisha aliendelea “Unadhani sina ndugu wanaohitaji msaada!?.. Ni vile tu nimekuchukulia kama ndugu yangu wala sihitaji uendelee kupitia magumu uliyopitia.
Alisema hivyo huku akiingia ndani kwake niwazi kuwa amekasirika nilibaki peke yangu nikiwaza sana..
“Chaguo ni lako hakuna wa kukulazimisha.. Alisema hivyo huku akinikabidhi pesa mkononi…………
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 07
Chaguo ni lako hakuna wa kukulazimisha.. Alisema hivyo huku akinikabidhi pesa mkononi…….
Nilipokea tuliongea sana alinipa historia yake kwa ufupi..
“Tumezaliwa watatu mimi ndio wakiume pekee nina wadogo zangu wawili wanasoma nje ya nchi napendelea sana kwenda nyumbani kila mwisho wa mwezi wazazi wangu ni peace mno ipo siku nitakupeleka dogo..
Nilifurahi kusikia hivyo kisha akaendelea “Na nimeshapitia kwenye mahusiano mengi sasa lakini sijabahatika kuoa na wala sio ishu kubwa sana kwangu sababu bado napambana..
Mara Siku ya Brayton iliita alitoka pembeni kupokea baada ya dakika kadhaa alirudi akiwa anatabasamu..
“Mwanangu wewe ni kijukuu cha mtume..
Alisema Brayton na kufanya nicheke maana sikuelewa amemaanisha nini..
“Kwanini?..
“Ni hivi yule jamaa wangu wa kazi niloongeaga nae amesema inahitajika nafasi moja…
Nilitabasamu na kusema “Bora maana nilikuwa nawaza nikanunue karanga hapa..
Nilisema hivyo na kufanya Brayton acheke sana kisha akaendelea “Huyu jamaa wangu hana neno kama utazingua ni wewe..
Asubuhi nilijiandaa mapema Brayton alinipeleka huko kwenye kazi “Nadhani ulishamwambia utaratibu wote!?.
Aliuliza yule bosi Brayton alijibu “Ni vyema ungemwambia basi tutakutana baadae..
Alisema hivyo na kuondoka kazini maana teyari alishajiandaa Bosi alinigeukia na kusema “Kuna zamu hapa asubuhi na jioni sababu kazi ni masaa 24 hivyo mtakuwa mnabadilishana zamu kila wiki..
“Sawa bosi hilo halina shida..
“Kingine kwa nyinyi wafanya kazi wapya kuna hostel zipo mkiwa wazoefu mnaruhusiwa kwenda na kurudi tunataka mjijengee uaminifu kwanza.
Nilibaki kimya yaani mambo ya kushea vyumba tena na watu wa jinsia tofauti mbona kama nitaishindwa mapema ila kama nitakataa Brayton hatokuwa na moyo wa kunisaidia tena..
Nilikubaliana na yote siku hiyo nilikuwa naelekezwa vitu muhimu vya kufanya nikiwa kazini jioni nililejea kwa Brayton..
“Inabidi ukaze hapo.. Nikipata kazi nzuri sehemu nyengine nitakuunganisha..
Alisema Brayton baada ya yote nilibeba vitu vyangu baadhi na kuelekea kwa mama G..
“Afadhali umekuja Shamimu nimekutafuta sana kila nikikupigia hupatikani..
“Nilikuwa busy na mishe zangu..
“Naimani ushafikiria vya kutosha aya nipe jibu ulikuwa unasubiriwa wewe tu.. Alisema mama G kwa shauku.
“Siko teyari na usifikirie tena kuhusu mimi kuolewa sina mpango huo na sitarajii.. Nilisema hivyo na kutoka nje nilimuacha Mama G na sintofahamu nilielekea nyumbani niliandaa nguo zangu baadhi.
Kulivyokucha asubuhi nilishawasili eneo la kazi nilikuwa makini mda wa jioni nilikuwa ndani ya chumba na wenzangu watatu walioonekana kuwa wakubwa kiumri pia walionekana kuwa wenyeji sura zao zilikuwa ngumu tofauti na mimi yaani hakuna hata sekunde iliyopita nikiwa na amani mda wote nilikuwa mwenye hofu lakini nilijitahidi kuificha hofu yangu..
“Nitaweza Kweli kuishi aya mazingira!?..
Nilikuwa nikiwaza lakini nilishtuliwa na sauti ya mmoja wao “Vipi wewe uendi kuoga!?..
“Nitaenda tu Broo. Nilijibu kwa adabu zote huku mwili wangu ukikosa nguvu maana sauti yake ilikuwa nzito sana.
“Utaenda saa ngapi!?.. twende mtoni tukaoge eneo hili maji ni shida sana kila ifikapo jioni huwa tunaenda kuoga mtoni kuepuka usumbufu wa maji..
Alisema huku akivua T-shirt yake niliona kilichobaki ni kukataa tu nitaendaje kuoga mtoni pamoja nao si watanijua tu “Broo leo siko sawa nimepiga kazi sana mpaka kichwa kinauma..
Niliongopa na kufanya waondoke peke yao nilibaki nikihema nilikamata simu yangu nilitamani kumpigia Brayton aongee na bosi niwe naenda na kurudi tu.
“Broo jaribu kuongea na bosi ikiwezekana niwe naenda nakurudi siyawezi maisha haya..
“Nilishaongea nae kabla.. Ila wanapima uaminifu wenu kwakuwa nimemuomba sana una mwezi mmoja tu hapo ukimaliza utakuwa unakwenda na kurudi..
Baada ya kusikia hivyo nilivuta pumzi maana mwezi mmoja sio mbali nitavumilia tu nilinyanyuka na kuchukua maji nikajimwagie nilioga faster nilivaa kaptula chapu kabla sijabana maziwa yangu mlango ulianza kugongwa..
“Dogo fungua mlango..
Jasho jembamba lilianza kunitiririka kwa hofu niliyona nayo……………..
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 08
Dogo fungua mlango..
Jasho jembamba lilianza kunitiririka nilimalizia kuvaa haraka haraka na kufungua mlango..
“Vipi ulikuwa na demu dogo..
Walisema huku wakiingia ndani wala sikusema chochote nilitoka nje kukaa ilivyofika mda wa kulala nilitandika nguo chini na kujilaza..
Waliniuliza sababu za kulala chini nilijibu kuwa kitandani tunabanana joto ni kali..
Zilipita siku kadhaa nikiwa nawakwepa kwenda kuoga mtoni na usiku pia sikuwa nalala nao kitandani..
Siku hiyo nilipanga kwenda kwa Brayton nilimjulisha kwahiyo aliniagia kwa Bosi nilifika kwa Brayton mda wa usiku sana nilimkuta akiwa ameshalala vile nilikuwa nimechoka pia nilipitia chumbani moja kwa moja nilivua nguo zangu na kuvaa taulo nikipitiliza bafuni..
Nilitoka chooni nikiwa nimejifunga taulo kabla sijaanza kuvaa Brayton aliingia niliwahi kuziba sehemu ya maziwa na viganja vyangu..
“Hodi muhimu.. Nilisema nikiwa nimempa mgongo lakini alikuwa kimya niligeuka kumbe alikuwa ameshaondoka.
Nilikimbilia mlangoni na kuulock na kitasa kisha nilivuta pumzi ndefu nilivaa na kukaa sikuwa hata na hamu ya kutoka nje..
Nikiwa chumbani mlango uligongwa nilifungua alikuwa ni Brayton tulielekea sebreni kulikuwa na ugeni..
“Huyu ni mdogo wangu wa mwisho amekuja kutoka China..
Alinitambulisha Brayton nilitasamu na kunyoosha mkono ishara ya kumsalimia lakini Brayton aliuputa mkono wangu na kubaki nikishangaa shangaa..
“Ooh.. Karibu sister naitwa Mimuh..
“Haina haja ya kujitambulisha nilikuleta ujue tu kama kuna mgeni hivyo leo atalala kule.. Alisema Brayton mpaka nilishangaa mbona leo kawa serious namna hii au kwasababu ya dada yake anahisi tunaweza kujenga ukaribu..
Niligeuza kurudi kule chumbani nilibadilisha mashuka pamoja na mapanzia nilivyohakikisha kila kitu kiko sawa nilitoa baadhi ya vitu vyangu..
“Unaenda wapi ingia jikoni mgeni hajala..
Alisema Brayton baada ya kuona nimebeba begi la nguo niliegesha begi langu na kuelekea jikoni kwa kuwa kulikuwa na kila kitu sikupata shida nilikaangiza haraka haraka..
“Chakula ni kitamu sana.. Alisema Dada yake na Brayton kukisifia chakula nilichopika hakuna aliyejibu chochote..
“Ulinambia unaitwa Mimuh hivi mlifahamiana vipi na Brayton!?..
Nilikaa kimya badala yake alijibu Brayton “Ni muda wa kula huu..
“Sasa kwani mimi kuuliza kuna ubaya kaka.. Ok Mimuh unafanya kazi gani!?.
Kwakuwa nilishajua Brayton hataki niwe na mazoea na dad yake nilijibu shortcut sababu mimi pia sipendagi nazoea na wanawake..
“Ni mbeba mzigo stend..
Nilisema hivyo nakufanya dada yake aangue kicheko sikujisikia vibaya hata nilinawa na kuyaelekea mabegi yangu.
“Sasa Broo Mimi nasepa.
“Wapi usiku huu ingiza mabegi chumbani kwangu kesho unaamkia kazini.. Alisema Brayton ila kiukweli sikutaka kulala chumba kimoja na yeye.
Nilivuta pumzi na kusema huku nikielekea chumbani..
“Napeleka mizigo tu.. Nitalala sebreni.
Baada ya mda nilitoka nikuwa na blanket nilitandika kwenye moja ya sofa la pale sebren na kujilaza kabla sijapitiwa na usingizi simu yangu ilianza kuita alikuwa ni Mama G kabla sijapokea nilitoka nje..
“Vipi Shamimu bint yangu huko wapi!?..
“Mama G mimi nipo kazini.. Kuna tatizo. Nilisema huku nikibabaika kutazama pande zote.
“Kuna mchumba mwengine kajitokeza.. Usikatae hii bahati Shamimu acha kujikomaza na maisha ya kiume..
“Kiukweli Mimi jibu langu ni hapana.. Na hilo jina Shamimu silitaki.. Mimi ni Mimuh kidume cha mbegu..
Nilisema hivyo na kukata simu niligeuka kuelekea ndani lakini nilishikwa na butwaa baada ya kumuona Brayton amesimama mlangoni niliganda dakika kadhaa..
“Una mtoto wa kike kumbe? Wewe ni msiri sana.. Alisema Brayton nilishusha pumzi kuhema maana niligundua hajafahamu chochote.
Ninae ila yupo mkoani na mama yake siku nitawaleta nilijibu nikiingia ndani sikutaka maswali tena nilirudi kwenye kochi langu na kujilaza nilipitiwa na usingizi mda huo huo..
Nilishtuka baada ya kusikia sauti za ndege ishara kwamba kumekucha..
Nilifumbua macho nilikuta Brayton akinitazama usoni nusu nizimie kwa mshtuko nilijivuta kwa nyuma kutaka kunyanyuka lakini alinishika mkono kunirudisha kwenye sofa tena safari hii alisogeza sura yake usoni mwangu akikazana kunitazama machoni..
Nilimpa kibao cha uso na kunyanyuka faster huku nikihema licha ya hasira ule mguso nilioupata mda amenikamata ulileta msisimko ndani ya mwili wangu…………..
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 09
Nilifumbua macho nilikuta Brayton akinitazama usoni nusu nizimie kwa mshtuko nilijivuta kwa nyuma kutaka kunyanyuka lakini alinishika mkono kunirudisha kwenye sofa tena safari hii alisogeza sura yake usoni mwangu akikazana kunitazama machoni..
Nilimpa kibao cha uso na kunyanyuka faster huku nikihema licha ya hasira ule mguso nilioupata mda amenikamata ulileta msisimko ndani ya mwili wangu..
“Mbona unanikagua sana!?.
Nilimuuliza huku nikiondoka bila kusubiri jibu lolote kutoka kwake nilibeba begi langu kisha niliondoka kazini nilipiga kazi mda wa jioni nikichukua simu yangu kumpigia mama G.
“Kama atakuja mwanaume yoyote kukuuliza chochote kuhusu mimi kausha.. Nina zawadi yako hapa
Hofu yangu ilikuwa kwa Brayton uwenda ananihisi kwahiyo sikutaka hajue chochote kuhusu mimi nilimaliza kuongea na simu na kutoka nje niliwakuta wenzangu wakiwa wanapiga stori..
Tukiwa hapo simu ya Bob iliita kabla hajapokea aliangalia jina..
“Nyamazeni Secretal anapiga..
Alitunyamazisha na kupokea simu sote tulikua tukimsubiri amalize kuongea.
Alimaliza kuongea na simu na kutusogelea “Mnajua kama wiki ijayo kuna bonge la sherehe sote tunahitajika kuuzulia sababu kuna wageni kibao kutoka nchi mbali mbali..
“Lakini kubwa kuliko nimeambiwa kama nina connection na nadance wa kike nimtafute mmoja tu wa kutoa Shoo siku hiyo..
Alisema hivyo huku na kuendelea maana sote tulikua kimya tukimsikiliza..
“Huyo dance analipwa pesa ndefu mno nadhani ni mara tatu ya mshahara wetu muhimu awe anajua tu..
Nilivyosikia ni mara tatu ya mshahara wetu nilishtuka yaani siku moja tu alipwe pesa yote hiyo..
Siku nne nzima Bob alikuwa anahangaika kutafuta dance wa kike lakini alikosa..
Asubuhi tulielekea kazini tulipiga kazi nikiwa naendelea na kazi nilimuona Bob akiwa anamkimbilia secretary wa bosi..
Mda si mrefu nilimuona secretary kama analalamika fulani nilijisogeza kusikiliza “Sasa shughuli ndio imeshakaribia unazani bosi atanielewa kweli ungeniambia tangu siku ile..
Alilalamika mmama huyo nilijisogeza karibu yake na kumuuliza “Kuna tatizo Madam.
“Kaendelee na kazi zako ya huku hayakuhusu.. Alinijibu mbovu lakini hata sikupiga hatua nilijua tu kuwa Bob amempa taarifa kuwa amekosa dance nilijitazama..
“Mbona bado umeganda hutaki kufanya kazi.. Aliuliza tena niligeuka nyuma kumtazama Bob alikuwa ameshatokomea nilimsogelea karibu kisha nikasema kwa sauti ya upole.
“Kama unahitaji Dance wa kike.. Mimi ninae anajua kudance kuliko maelezo.. Nilisema hivyo huku nikimtazama.
“Ujue hii kitu iko serious.. Aya nipatie namba zake nimtafute lazima nione uwezo wake kwanza anahitajika kupanda juu ya jukwaa kubwa hivyo sitaki aibu kutoka kwa viongozi..
“Sasa namba zake sina labda nipe ruhusa leo nikamtafute harafu kesho asubuhi kabla ya tamasha atakuja umuone..
Secretary alinitazama sana kisha akaniuliza “Na asipokuja je?.
Basi nilimuhakikishia kuwa lazima aje hivyo niliomba ruhusa ya siku mbili nilirudi nyumbani haraka haraka..
Zamani huwa tulikosa ela tunakusanyana na watoto wenzangu wa mtaani tunaenda kudance baa huwa tunajipatia pesa za walevi hivyo baadhi ya vitu havikuwa vikinipiga chenga maana baadhi ya style tulikuwa tukiiba kwa madance wanapocheza kwenye matamasha makubwa..
“Nahitaji mazoezi ya kutosha pia nijifunze style mpya kuipata laki sita kwa siku moja sio kitu kidogo nikipata hizo pesa nitaenda mbali na mji huu. Niliwaza mwenyewe huku nikijikumbushia baadhi ya style za zamani ninazo zijua nikitoka ndani na kuelekea kwa mama G.
“Mama G unaweza kuniazima Redio yako kubwa inayotumia flash ile.
Kweli alinipatia nilirudi nyumbani na kuconnect nyimbo niliyoona inafaa nilipiga mazoezi sana kuna mda nilikuwa naangalia performance za baadhi ya madance maarufu ili niweze kupata mawili matatu kwa kuwa nilikuwa mwepesi haikunipa shida..
Siku zilizosalia zote sikwenda kazini nilikuwa nafanya mazoezi ya kudance tu nilimpigia simu secretal kumtoa wasiwasi kuwa lazima huyo dance atakuja tu..
Siku ya tukio iliwadia niliamka mapema sana nilifanya mazoezi kama kawaida niliwaza namna ya kuvaa nilipata wazo la kwenda kuazima baadhi ya vitu kwa Mama G..
“Vyote nitakupa lakini mkufu wangu siwezi kutoa.. Alisema Mama G na kufanya ninyongee.
“Nitakurudishia leo ninaenda kupiga pesa ndefu sana ni kama laki sita sasa unadhani nikipata hizo pesa nitakuacha hivi hivi lazima nikufute jasho.. Nilijiplaud mbele ya Mama G.
“Huu mkufu nilipewa zawadi siku ya ndoa na wakwe zangu ni wazamani sana pia ni dhahabu og… Alisema Mama G huku akiwa ameushikiria mkufu wake unaong’aa.
“Shika ni kwasababu nakuamini tu.. Na imani utarudi salama ngoja nikakuchukulia viatu.. Alisema Mama G na kwenda ndani kunichukulia sikonkonko.
Baada ya mda alirudi na viatu virefu pamoja na wigi nilitabasamu niliona nimeshamaliza yaani kilichobaki ni nguo tu ambayo haikunipa shida hata ya mtumba si inavalika………….
NAOGOPA KUWA MWANAMKE 10
Shika ni kwasababu nakuamini tu.. Na imani utarudi salama ngoja nikakuchukulia viatu.. Alisema Mama G na kwenda ndani kunichukulia sikonkonko.
Baada ya mda alirudi na viatu virefu pamoja na wigi nilitabasamu niliona nimeshamaliza yaani kilichobaki ni nguo tu ambayo haikunipa shida hata ya mtumba si inavalika….
Nilivuta mda na kwenda kutafuta kigauni cha mtumba kilikuwa kifupi kiasi kilifunika nagoti tu licha ya kwamba haikuwa nguo ya ghalama lakini ilinikaa vyema basi mda uliobaki niliutumia kumalizia kufanya mazoezi ya kutembelea sikonkonko.
Jioni nilijiandaa mama G alinipaka poda kiasi nilivyoridhika na muonekano wangu niliondoka.
Nilifika ukumbini nilikuta wingi wa watu.. Watu walikuwa wengi sana mpaka nilijawa na hofu kama nitaweza kuperform vizuri basi nilipokelewa na Secretary..
“Ni huku Miss..
Alisema huku akinishika mkono na kunipeleka ndani ya chumba kilichomo katika jengo hilo..
“Ahsante sana Madam..
Nilimshukuru na kusogelea kwenye kioo nikijitazama “Kumbe nikiwa hivi napendeza sana..
“Unapendeza sana.. na unavutia pia. Ilikuwa ni sauti iliyonishtua niligeuka alikuwa ni boss wangu nilitabasamu..
“Bila shaka wewe ndio Miss Angel nimeelekezwa nije humu..
Nilijibu kwa kubana sauti yangu ya base na kufanya nitoe sauti rahini “Yeah.. Ndio mimi.
“OK.. Natumai ushapewa maelekezo ifanye hii event iwe Babu kubwa.. Alisema hivyo na kutoka nilibaki peke yangu nikihema jasho ya meno ilikuwa ikinitoka..
Mda wa kuperform jukwaani uliwadia taa za stejini zilizimwa nilikaa katikati nilisikia sekunde zikihesabiwa tu..
One… Two.. Three
Tayari Dj alishaplay Music nilianza mdogo mdogo hofu yangu yote niliiondoa sikuwa na mda wa kutazama watu nilideal na jukwaa tu..
Nilidance sana hakuna kitu ambacho niliacha kati ya nilivyojifunza sikutaka kuikosa pesa niliyoahidiwa ukumbi mzima ulikuwa ukinishangilia ilinipa moyo yaani siku hiyo niligeuka beyonce ghafla nilipiga style zote..
Baada ya kumaliza kupareform nikielekea ndani ya kile chumba na kunywa maji maana kiu kilinishika nikiwa namalizia kunywa maji aliingia bosi wangu mda wote hakuweza kunitambua kabisa..
“Sikutegemea Kama ungeweza kudance namna ile.. Alisema huku akitabasamu.
“Ahsante Boss.. Nilisema huku nikiachia tabasamu mnadhani hizo ela nitazipata vipi bila kuzitolea utashi.
“Sio Boss niite Kelvin.. Alisema huku akinipatia Business card na alinikabidhi mzigo wangu cash nilitamani kumkumbatia kwa furaha nilo nayo.
Baada ya yote nilitoka nje event bado ilikuwa inaendelea kwa kuwa nilishamaliza kazi iliyonipeleka hakukuwa na umuhimu wa mimi kuendelea kubaki niliondoka nikiwa natoka nje kwa mbali nilimuona Brayton akiwa na marafiki zake nikiwa bado nashangaa kiatu kulinifanya kitu mbaya nikianyaga jiwe na vile sikuwa na uzoefu navyo nilijikwaa na kuanguka chini Puuuuh!!.
Yaani dakika kadhaa watu walikuwa wameshajaa utadhani walikuwa wananisubiri nianguke..
“Hamna.. Hamna sijaumia.. Nilisema huku nikiukumbatia mkoba wangu wenye pesa nakujaribu kunyanyuka kwani hata niliweza kunyanyuka sasa.. mguu wangu uliteguka.
Nikiwa bado niko pale chini nikisikia sauti ya Brayton “Mtu kaumia baada ya kumpa msaada mnamshangaa.. Poteaaa.
Sauti yake iliwatawanyisha watu wote na kufanya nibaki peke yangu nilibaki naomba mungu Brayton asisogee eneo hilo..
“Vipi mrembo umeumia sana eeh.. Alisema huku akinishika mkono ishara ya kunisaidia kunyanyuka japo nilipata maumivu lakini nilijikaza kisabuni..
“Asante kaka angu naweza kwenda.. Nilisema huku nikinyanyua mguu kuondoka nilipiga hatua chache tu nikudondoka tena Mungu wangu balaa gani hili.
Brayton alinisogelea na kuchuchumaa mbele yangu nilikwepesha uso wangu kwa kutazama chini alinibeba na kutoka na mimi nje ya eneo lile mda wote nilikuwa nikitazama pembeni..
“Miss Angel…. Ilikuwa ni sauti ya Boss Kelvin..
Brayton aligeuka kuangalia aliyeita “Ooh Kelvin.. Kumbe unafahamiana na huyu bint..
“Yeah.. Yeye ndio aliyetuburudisha ukumbini leo naona ameumia..
Bado walikuwa wanaongelea kuhusu mimi lakini wala sikuwa najali kuhusu ilo nilikuwa nahofia Brayton asije kunijua..
Bosi Kelvin alituacha na kuondoka “Niko sawa sasa naweza kwenda tu..
Brayton hakunijibu alinipeleka hadi kwenye gari yake..
“Unakaa wapi nikupeleke?..
Niliwaza dakika kadhaa kisha nilitaja sehemu nyengine kabisa ni maeneo ambayo wanaishi matajiri maana hata sikuwahi kufika alinipeleka hadi eneo nililomtajia nilishuka na kumshukuru…
Sasa nilibaki nashangaa shangaa njia ya kurudia maana nilikuwa mgeni maeneo haya nilichechemea hadi kituoni na kupanda daladala za kwetu..
Nilifikia kulala tu maana nilichoka sana nilishtuka asubuhi mda umeenda sana simu yangu pia ilikuwa ikiita kuangalia mpigaji alikuwa ni Brayton nilipokea..
“Oya dogo kama umeacha kazi katoe taarifa kazini sitaki kusumbuliwa..
Alisema hivyo na kukata simu basi nilijinyanyua kitandani na kwenda kuoga nilivaa mavazi yangu bila kusahau ndevu moja kwa moja nilielekea kazini..
Niliwakuta wakina Bob wakiwa wamekaa niliwasogelea na kuwasalimia.
“Dogo sio riziki nini.. Alisema Bob na kufanya nijishtukie niligusa kifua chapu nilidhani labda sijabana waziwa yangu lakini sivyo..
“Sijakuelewa.. Nilisema kwa kukaza sauti na kufanya wote wacheke.
“Sasa huo wanja na hizo rangi mdomoni zimefata nini!?..
iish.. Inamaana hazikufutika nilibaki nimezubaa wameshajua kuhusu mimi………………..