House Girl Aliyeua Familiya Nzima Arithi Mali
Ni mwaka 2019 tu hapo, hili tukio lilitokea huko Kerala nchini India.
Mwanamke anayeitwa kwa jina la Jolly Joseph alikuwa akifanya kazi kama dada wa kazi ndani ya nyumba moja hivi.
Alikuwa mwanamke mpole, mwenye heshima, mcheshi, aliishi na familia hiyo kwa miaka 14 ila kulikuwa na kitu kikubwa kilichojificha nyuma yake. Kitu cha kusisimua na kutisha mno.
Watu sita ndani ya familia hiyo aliyokuwa akifanya kazi walikufa, mmoja baada ya mwingine. Kila mtu aliyekuwa akifariki, dokta alikuwa akisema kwamba ni magonjwa ya moyo ndiyo yaliyokuwa yakiishambulia familia hiyo.
Ukweli ni upi?
Jolly alikuwa akiwalisha sumu iitwayo cyanide ambayo alikuwa akiwawekea kwenye chakula, supu na hata maji.
Waliokufa walikuwa….
Baba mwenye nyumba.
Mkwewe.
Mtoto wa miaka miwili.
Mpaka mume mpya wa mama mwenye nyumba.
Polisi wakaamua kuingia kazini na kuchimba kuhusu vifo hivyo. Wakaanza kupata muunganiko wa matukio hayo.
Vifo vyote vilifanana kwa namna moja ama nyingine. Jolly alikuwa mtu pekee aliyekuwa akiwaandalia chakula.
Lengo ni lipi?
Alikuwa na tamaa ya kumiliki mali, kuwa na kontroo kubwa. Alihitaji nyumba hiyo na maisha mapya ya kifahari.
Alikamatwa mwaka 2019