ILIANZA KAMA MZAHA ILA IMENIGHALIMU MAISHA MPAKA SASA
Nilikuwa na miaka 19 tu nilipopata mimba yangu ya kwanza. Wakati huo bado nilikuwa mwanafunzi wa kidato cha nne . Yule aliyenipa mimba alikuwa dereva wa bodaboda kutoka mtaani kwetu
, mtu mzima aliyenizidi kwa miaka 12.
Tulianza kwa mizaha midogo midogo , baadaye tukawa tunaongea mara kwa mara. Akaanza kunifuata hadi shuleni
.
Mimi nilikuwa msichana wa kawaida kabisa binti wa mama mjane , aliyekuwa anauza chai na maandazi sokoni
. Nguo zangu za shule zilikuwa zimepauka, viatu vilikuwa vimechanika
, lakini bado nilikuwa naamini kuwa elimu itanitoa
.
Alinifanyia mzaha mwingi, akaninunulia vocha , chipsi
, na hata bando za intaneti
. Wenzangu walikuwa wakinicheka wakisema, “Umejipatia baba wa maisha!”
Na kwa kweli, nilianza kuamini hivyo.
Nikajikuta nampa mwili wangu , nikiamini pia kuwa napata moyo wake
.
Mimba ilipotokea , mama alilia sana
. Lakini baada ya siku mbili, alichukua kitenge akanambia:
“Kwa kuwa amekubali kukuoa, usijali. Maisha ya ndoa ni kujifunza.”
Nikaolewa. Sio kwa harusi, bali kwa kulazwa tu kwake .
Ndoto zangu zikazikwa bila jeneza .
Miezi ya mwanzo nilihisi pengine ananipenda kwa dhati . Lakini baada ya mtoto kuzaliwa
, upande wake halisi ukaanza kuonekana…
Alianza kunitukana kila anapotoka nyumbani . Alikuwa anarudi usiku na harufu ya pombe
. Akanilazimisha niuze kahawa na maandazi asubuhi
, usiku niandae chakula, nioshe vyombo, nisafishe nyumba
.
Nikaanza kupotea taratibu… Sikuwa tena yule msichana mchangamfu wa awali . Nilianza kuongea na ukuta
. Nilianza kulia kimya kimya kila usiku
.
Nilipomwambia mama, akaniambia:
“Mwanaume ndivyo walivyo. Endelea kuvumilia, hata mimi nilivumilia marehemu baba yako.”
Nikamwendea shemeji yangu , akanicheka akasema:
“Bado mdogo. Subiri miaka kumi ndo uongee kuhusu ndoa.”
Nikaenda kwa mchungaji , akanambia:
“Mume ni kichwa cha familia. Utumwa wako kwake ni ibada.”
Jamii yote ilininyamazisha . Nikabaki kuumia kimya kimya
Mpaka siku moja, usiku alirudi na mwanamke mwingine . Akaniambia mbele ya mtoto wetu:
“Huyu ndiye mke wa roho yangu. Wewe ni mama wa mtoto tu. Kaa pale.”
Nililala sakafuni nikilia kimya kimya .
Mpaka siku moja alfajiri, nikaamka nikiwa najua nikikaa hapo nitakufa bila hata watu kujua .
Nikambeba mwanangu mgongoni , nikaondoka bila hata viatu mguuni
. Nikaenda kwa mama.
Mama aliniona akasema:
“Umerudi? Mbona wajifedhehesha?”
Nikamuambia:
“Nimeamua kufedheheka kuliko kufa kimya kimya kwenye ndoa ya jamii iliyonisukumia.”
Lakini kilichonileta hapa ni kwamba…
Huyu bwana hachangii matumizi ya mtoto.
Na hajawahi hata kuniuliza hali ya mwanangu .
Shule nimepoteza ,
Ndoa nimepoteza ,
Nimebaki na mtoto tu tena mtoto ambaye hajawahi kupata matunzo kutoka kwa baba yake .
Sijui hata nianze wapi
Naomba ushauri nifanye nini ili niweze kusimama tena?