Clickable WP Image
JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

NIGHT CLUB

Sehemu ya 41

Ilipoishia…………Erick katekwa bila kujua na Salim mume wa Maiya ambaye amemnyooshea bastola akitaka kumuua!!

Songa nayo…………

Sikuwa nimewahi kupigwa risasi kabla,Ila nilishawahi kunyooshewa na Aisha kipindi fulani baada ya kugundua nina mahusiano na jirani yangu!!

Mwili ulikufa ganzi,nilitetemeka haswa!Nilikiona kifo mbele yangu!

Salim alikuwa ameninyooshea bastola akitaka kuniua!

Haukuwa mzaha hata kidogo,moyoni nilianza kusali na kuomba sala zangu za mwisho!!

Salim aliikoki bastola nikafumba macho tayari kwa kuipokea adhabu yangu!!

Nilijuta na tabia yangu ya kuzoazoa wanawake nisiyowajua!!

Ulisikika mlio mkubwa wa risasi!ajabu sikuhisi maumivu yoyote!!

Nikajiuliza au tayari nilishafika mbinguni,maana wanasema roho inatokaga machoni!

Nilifumbua macho sikuamini bado nilikuwa kwenye kile chumba!

Nilijipapasa nione labda naweza kupata sehemu niliyopigwa risasi lakini sikuona chochote!!

Ndipo nikaangalia alipokuwa kasimama Salim,sikuamini Salim alikuwa chini anavuja damu kichwani katulia tuli!

Nilipoangaza nilimuona Maiyah kasimama kashika bastola!!

Ni kama kifo kilimgeukia  Salim,Maiyah alikuwa amemuua mumewe!!

“Maiya umeua??”

Nilisema kwa sauti kubwa huku nimeshika kichwa!

Maiya alinisogelea Karibu,akaniambia…

“Angeishi huyu wewe ungekufa!!”

“Unamaanisha nini Maiya!”

“Namaanisha alitaka kukuua,mwanangu lazima aishi na baba yake halisi,siyo wa kuunga unga!!”

“Maiyah umeua!!”

“Ebhu!tuliza akili Erick!ungekufa wewe acha wenge!”

Maiya alimsogelea Salim akampiga risasi tatu tena za kifuani!!

“Maiya si amekufa huyo!!”

“Erick ishi kama mwanaume naomba uondoke kuna gari litakurudisha kwako,ila zingatia hii ni siri!!’

Niliondoka haraka sana mpaka kwenye maegesho ya magari!

Tuliondoka huku nikiwa sijafungwa kitambaa huku nikaanza kuchunguza yake ni maeneo gani?

Niligundua ni maeneo ya mikocheni B!

Dereva alinipeleka hadi nyumbani kisha akaondoka zake!!

Nilifika nyumbani nikiwa siamini kama nimenusurika kufa!

“Mume wangu vipi?mbona unahemea juu juu!

Aliniuliza Patra baada ya kuniona siko sawa!

“Niko sawa mummy!”

“Okay,twende ukaoge mume wangu!!”

“Ngoja nipumzike kidogo!”

“Hapana utaoga ndiyo upumzike!”

Sikuwa na jinsi ndiyo raha yenyewe ya kuoa,japo ndoa bado ila nilihisi kwa raha anazonipa Patra naweza kutangaza nia hivi karibuni😆😆!!

Siku hiyo nilikuwa roho juu juu tu,muda wote nilikuwa nakumbuka tukio lililopita!

Kitendo cha Maiya kumuua Salim mbele yangu kilinipa wakati mgumu sana!

Nililala lakini nilishtuka mara nyingi usiku kwa kuota ndoto nyingi za kutisha!

**************

Siku hiyo nilishtuka saa mbili asubuhi kitu ambacho si kawaida yangu!

Nilikuwa peke yangu kitandani,Patra alikuwa ameshaamka tayari anafanya mambo mengine!

Niliamka kichovu nikaingia bafuni kufanya usafi wa mwili kisha nikajiandaa,nilipomaliza Patra akaingia!

“Baby chai tayari!!!”

“Mmhh!mbona ntanenepa mwaka huu!!”

“Hahahaaa!sitaki unenepe sana baby usije ukashindwa kunipa vitu vyanguuuu!!”

“Hahahaha!jasiri aachi asili!”

“Ila baby mi natoka leo,ntarud kesho sababu kule ninapoishi sijaacha mtu na pia sikubeba hata nguo ya kubadili!”

“Sa si urudi jioni!”

“Hapana baby,ntarud kesho na mabegi yangu!”

“Okay,ntakumiss nimezoea kulala na wewe sasa itakuwaje!!”

“Baby bhana leo tu!”

“Sawaaaa!ntakumbatia mto!”

“Aya baby kunywa chai mimi ngoja nikaoge!”

“Situnywe wote!”

“Jamani kunywa bhana!”

Patra aliniacha nakunywa chai nzito ya maziwa na chapati nzito za mayai!

Wakati naendelea kunywa simu ya Patra iliingia meseji ikatokea juu ivyo niliweza kuisoma bila kuifungua!!

“WATU WAMEMISS SANA SHOO YAKO WANASUMBUA SANA,NA MADANGA YAKO YANASUMBUA HATARI USINIANGUSHE!”

Moyo wangu uliuma,mapigo ya moyo yakaenda mbio,ndiyo kwanza nilikuwa nimekula chapati moja tu lakini sikutamani kuendelea!

Chapati nilizoziona tamu ziligeuka shubiri ghafla!

Pale nilipoamua kutuliza moyo wangu usitangetange nakutana na mauzauza ya ajabu!!

Moyo uliniuma sana,ghafla niliwakumbuka wanawake wengi niliowapoteza kwenye maisha yangu,kipindi kile bado moyo wangu haujaamua kutulia!!

Nilimkumbuka Amanda,Aisha na wengine kibao!

Kuna wanawake unaweza wapoteza na usije kuwapata kabisa,ukaishia kupata pasua kichwa tu.

Vivyo ivyo tu hata kwa mwanamke unaweza kupoteza mwanaume ambaye utakuja kujutia maisha yako yote,kwa kumkosa kama yeye,pengine ulimuacha kwa mapungufu machache tena yanayovumilika na kurekebishika!

Nilitamani nimfuate Patra bafuni nikampige lakini nikajiuliza tabia za Uchebe nimeanza lini??

Niliamua kuigiza kama kila kitu kiko sawa kabisa,hakuna nilichokiona!

Nilikula chapati zote kwa hasira na kunywa chai ya maziwa kisha nikatulia!

Patra alitoka chumbani akiwa tayari amejiandaa!

“Vipi tayari mume wangu tuondoke!”

“Mimi tayari Patra,kwani wewe haunywi?”

“Aah!sijiskii ntakunywa huko!”

“Okay, tuondoke basi!!”

JE ERICK ATAFANYA NINI AKIMKUTA PATRA CASINO?

NA JE NI KWELI PATRA ANAENDA CASINO AU NYUMBANI!

Sehemu ya 42

Ilipoishia………. Cleopatra anamuaga Erick akisema anaenda nyumbani,lakini Erick anagundua Patra ana mambo mengine nyuma ya pazia…….

Songa nayo……….

Sikumuonyesha kama kuna kitu nimekifahamu,nilikuwa Kanumba siku ile, nilitabasamu ilihali moyo wangu unavuja damu!

Tuliachana mbele mimi nikaenda zangu kazini na yeye akaondoka zake kwake!!

Nilipofika kazini Abobo alinipigia simu.

“Oyaa!uko wapi mwanangu?”

“Nipo naenda karume mzee vipi?’

“Sikia unamkumbuka yule shemeji yangu tulitambulishwa na Anti Suzy siku ile?”

“Ndiyo Kaka!”

“Tumepewa taarifa amefariki bhana,amevamiwa na majambazi!”

“Dahh pole sanaa sasa itakuwaje?”

“Usijali wewe nenda tu karume Ila Kessy nipo naye huku tayari kwahiyo simamia shoo zote!!”

Siku hiyo nilishinda ovyo ovyo tu,mawazo yalinitawala kichwani!

Maana huu msiba wa Salim najua hakuuliwa na majambazi,ameuwawa na mkewe sababu yangu!

Sasa nikifikria ya Salim na aya ya Patra nahisi kichwa kinabomoka!

Nilishawahi kusikia mapenzi yanauma,lakini sikujua kama yanauma kiasi kile!!

Uzuri na umbo la Cleopatra lilinifanya niamini hata tabia yake iko ivyo!

“Kaka sindiria shingapi?”

Ilikuwa ni sauti ya mdada mmoja mzuri tu wa kawaida!

“Ooh!Karibu hizo chini elfu tatu tatu juu hapo elfu tano tano!”

“Aaah!Kaka mbona hizi zina bei Sana?”

“Huo mtumba grade one yani hizo alivaa Beyonce na Rihanna ndiyo zikashuka bongo!!”

“We Kaka unanichota etii hahahaha!”

“Kweli zicheki mwenyewe hizi wengine wanauza buku teni lakini mi wanawake wote dada zangu nauza nusu bei tu!”

“Una maneno wewe mkaka jamani!”

Aliongea yule dada akaanza kuchagua akapata sindiria nzuri mbili akalipia elfu kumi!!

“Duh!Kaka nipe namba yako kabisa ili nikitaka kuja nikuambie uniandalie nzuri nzuri kama hizi!!”

“Hahahahaa!usijali andika!”

“Okay nitajie!”

“0716352102”

“Okay, ahsante sana kaka!”

“Okay nibipu nipate zako!”

Alinibipu nikaipata kisha nikamuuliza.

“Niandike nani Sasa?”

“Ooh!naitwa Beatrice!”

“Okay mi naitwa Erick!”

Yule dada aliondoka Kisha nikaendelea na mambo mengine!

Ndiyo nilivyo,linapokuja suala la kuongea na mteja,hata kama nimevurugwa huwa naweka mawazo pembeni,naongea kwa uchangamfu na lugha yenye ushawishi katika biashara!!

Siku iliisha nikarudi nyumbani nikiwa na unyonye wangu Ila kabla hata sijatulia meseji ikaingia kutoka kwa Maiya!

“Msiba ukiisha tutaishi kwa amani baby usijali nakupenda!”

Yaani katika siku nilikuwa na mawazo ni hizi,yaani sikupumzishwa linatoka hili linakuja hili!

Nilikaa nikisubiri usiku uingie niende zangu Casino kumshika chauwongo wangu!

Kama kawaida muda unachelewa lakini unafika!

Usiku uliingia nikavaa nguo ambazo si rahisi mtu kunijua!

Nikavaa na kofia ambayo ilinibadilisha na kunipa muonekano tofauti kabisa!

Nilitoka nikatafuta usafiri mpaka Casino!

Nilifika nikaingia ndani nikaagiza bia zangu mbili nikawa nakunywa taratibu!

Sikutaka kulewa siku ile ili nisije nikaharibu,maana pombe haina adabu!!

Muda ulienda kama kawaida walianza wale madada wanaocheza na kukalia chupa,Kisha baada ya hapo ikaja shoo niliyokuwa naisubiri.

Shoo ya mwanamke niliyeamua kumkubali na madhaifu yake,nikamuweka moyoni nikiamini atabadilika lakini kumbe haikuwa ivyo!!

Kama nilivyohisi na kutegemea ndivyo ilivyokuwa!

Aliingia Cleopatra au Queen Patra kama kawaida yake,alikuwa amevaa chupi tu hata juu aliacha chuchu zake wazi!

Niliumia sana moyoni,yani vyote anavyonionyesha chumbani anavionyesha wazi!

Nilijiuliza kuna haja gani ya mwanamke huyu kujiita ana sehemu za Siri?kwanini asiwe anatembea hata uchi barabarani tujue moja,tujue huyu mwanamke hana sehemu ya siri!!

Kama tukimuona mtu anatembea uchi huwa tunamuita chizi,je huyu ni nani?

Machozi yakinitiririka kwa hasira na wivu!

Cleopatra hakuwa na habari alicheza na kujisheua kama chizi!

Nilijitahidi kuyapa ujasiri macho yangu,japo muda mwingi yalifunikwa na machozi!!

Nililia sana siku ule kofia na miwani vilinisitiri.

Ulifika muda wake wa kuvua chupi, Cleopatra akabaki kama alivyozaliwa!

Akachukua chupi yake akairusha,bahati mbaya ikanirukia usoni!

Niliishika nikatoka eneo lile nikaenda nje nikalia sana!

Nilimkumbuka Aisha japo anavuta bangi lakini alihitaji kitu kimoja tu abadilike,Aisha alihitaji upendo wangu na uaminifu tu angeacha kila kitu na kuwa mwema!

“Kwanini sikumpenda Aisha nakuja kupenda hili gumegume!!”

Nilijiuliza muda huo nimeishika ile chupi,nikapanda bodaboda mpaka nyumbani kwangu!

Usiku ulikuwa mrefu sana siku ile,usingizi niliupata kwa tabu sana!

Nilikuja kushtuka asubuhi baada ya simu yangu kuingia meseji!

Nilipoifungua ilitoka kwa Cleopatra!

“NIKO NJIANI NAKUJA MUME WANGU!”

Nilijifikria cha kufanya nilipopata jibu nikamjibu kwa meseji!

“KARIBU PATRA!”

JE ERICK ATAMFANYA NINI PATRA?

KUNA USALAMA KWELI?

VIPI UNGEKUWA WEWE UNGEFANYAJE!!

Sehemu ya 43

Ilipoishia………Erick anamshuhudia Cleopatra akirudi kucheza uchi Casino,licha ya kusema amecha Ila ni wazi hawezi kuacha!!

Songa nayo………..

Kitendo cha Cleopatra kuniambia anakuja kilinipa hasira nikajiuliza nifanye nini?

Kila nilichowaza niliona hakipo sawa kabisa,mwisho kuna nafsi iliniambia nivumilie pengine ndiyo ilikuwa siku yake ya mwisho!

Niliificha ile chupi yake nikaamka nikajiandaa,wakati yeye anafika mimi nikatoka!!

Cleopatra alikuja,lakini hakuja na begi kama alivyosema!

Alikuja na nguo alizovaa tu,nilimchangamkia kama hakuna kilichotokea!!

Nilimuaga nikaondoka zangu kazini,nilipofika nilifanya yangu kama kawaida nikatulia nikaanza kupokea mteja mmoja mmoja!!

Japo sikuwa kawaida ila nilijitahidi Sana mtu hasijue!

“Dahh!mwanangu yule shemeji yake Abobo kauliwa vibaya Sana yani uso hautamaniki!”

Alisema Kessy kitu ambacho niliona ananichanganya tu sababu najua nani aliyemuua na pia nilikuwepo,ilikuwa nife mimi siku ule!!

“Aah!Kessy achana na hizo stori mwanangu,mtu akifa muache apumzike,marehemu haongelewi!!”

“Ila kweli basi poa leta stori zingine!!”

Kama nilivyohisi ndivyo ilivyotokea, Cleopatra alinipigia akiniambia shangazi yake anaumwa hivyo anaondoka atarudi baada ya siku mbili!!

Sikumuuliza maswali mengi,sababu nilijua anakoenda!

Nilimruhusu nikasubiri muda ufike niende nikachukue chupi yake nyingine!

Hakukuwa na shangazi wala nini,Patra alienda Casino kucheza uchi!!

Nilivyokuwa na bahati mbaya siku ile pia alipoirusha chupi yake nikaipata mimi nikaondoka zangu!!

Kesho yake tena nilienda nikiwa na shauku ya kupata chupi yake nyingine!

Nilikaa mpaka muda wa shoo, Cleopatra akaingia tena,akicheza uchi kama kawaida yake!

Siku ile sikubahatika kupata chupi yake,iliangukia kwa mtu mwingine!!

Kwa kuwa lengo langu lilikuwa kupata chupi na si vingine,niliamka nikaenda nikamfuata yule jamaa aliyepata chupi!!

“Inakuwaje mwanangu!!”

“Safi aliitikia!”,aliitikia yule jamaa!

“Samahani unaweza kujipa hiyo chupi?”

Yule jamaa aliniangalia kwanza kwa dharau Kisha akasema!!

“Ivi hujui ukipata hii ni tiketi ya kulala na Queen Patra kwa nusu bei!!”

Nilishtuka!sikujua kumbe kuna maana kupata nguo ya ndani ya Patra!

“Sikia mi nakulipa nipe hiyo chupi?”

“Wanaume wote unaowaona hapa Wana ndoto ya kulala na Cleopatra,unahisi mimi sina ndoto hiyo?”

“Unalipia shingapi kufanya naye mapenzi bila chupi?”

“Ni zaidi ya laki tano!”

“Nakupa laki tano!”

“Kweli!!”

“Ndiyo!”

“Itume fastaaaa!kwanza nimehairisha ntalala naye siku nyingine!”

“Okay nipe namba yako!”

“07448762552!”

“Okay poa!

Roho iliniuma sana,kununua chupi ya elfu tano au tatu kwa laki tano!

Nilimtumia yule jamaa zile hela huku chozi linanitoka, sikuwahi kufikiria kama kuna siku ningefanya mambo ya ajabu hivi kisa mapenzi!!

Yule jamaa alinipa ile chupi kisha nikaondoka zangu!!

“Vipi kaka?mbona unaondoka?”

Nilimuacha nyuma yule kijana akiniita Ila sikumjibu!

Nadhani alijua nataka kulala na Cleopatra kwa nusu bei!!

Niliondoka zangu kwa hasira nikachukua usafiri mpaka nyumbani!!

Nilifika nikazichukua zile chupi huku roho inaniuma sana!

Niliziweka mezani nikajiuliza Ina maana zile chupi nimenunua kwa laki tano?

Nilicheka mwenyewe na kujiona mjinga sana,mapenzi yalinifikisha pabaya aiseeh!!!

Niliwakumbuka sana wanawake ambao niliwachezea na kuwaona wa kupita ila walinipenda kwa dhati!!

Nilichukua simu nikampigia Aisha simu ikaita ikakata,nikapiga tena ikapokelewa!!

“Haloo Aisha!’

“Haloo Nani?”

Niliumia kuona kumbe Aisha alishafuta na namba yangu,Ila nikajipa moyo pengine moyoni bado,nikaona siyo mbaya ngoja nijitambulishe!!

“Ni Mimi Erick!”

“We malaya unataka nini mbwa wewe,ukome kunipigia simu kunguru we……tititi….!!

Nilikata simu nikatulia,katika kutafakari nikamkumbuka Amanda,nikaitafuta namba yake nikampigia!!

“Haloo,niliita!”

“Haloo!”,iliskika sauti ya kiume!!”

Nilikata simu nikajicheka mwenyewe  kama bahati nilishaichezea ngoja niyaone ya dunia Erick!😂😂

Nilichukua mzinga wa pombe  nikaanza kulewa,yani bahati nzuri hakukuwa na bangi,nahisi ingekuwepo ningejaribu kuvuta siku ile!

Usingizi ulinipitia palepale,mbu waliniuma sana siku ile,sasa hawana shamba wakalime wapi waache wale ndiyo chakula chao!!😆

Asubuhi niliamshwa na simu yangu, Cleopatra ndiye alikuwa ananipigia simu!!

Nilipokea nikaiweka sikioni….

“Mume wangu umelala bado nakuja babaangu,nimechoka kweli niko njiani!!”

“Sawa karibu mimi nipo!!”

“Nakuja na begi mume wangu!!”

“Karibu!”

Cleopatra alikata simu,niliamka kwa hasira nikatoka hadi sebuleni!!

Nilipofika sebuleni nilizitandaza zile chupi mezani kisha nikaenda kuoga!

Nilipomaliza nikakaa zangu nikaanza kulewa asubuhi asubuhi!!

Nilikaa kwenye sofa nikimsubiri Cleopatra!

Alifika akaingia mpaka ndani,akanikuta nakunywa zangu pombe kali!

” Mume wangu leo umeamua kulewa asu……!!”

Cleopatra alisita akashituka baada ya kuona chupi zile juu ya meza!!!

 PATRA ATAFANYA NINI?

NA VIPI ERICK ATAMFANYA NINI PATRA?

Sehemu ya 44

Ilipoishia…….. Cleopatra bila kujua kama Erick anajua kila kitu kuhusu tabia yake ya kucheza uchi Casino,anakuja na mabegi yake kabisa akijua sasa anaenda kuolewa na Erick!!

Songa nayo………..

Hakuna siku nilijaribu kutuliza hasira zangu kwa kiasi kikubwa,angekuwa uchebe hakika kuna mtu angeenda mochwari siku hiyo!!!

Cleopatra aliingia na begi lake la nguo akaufunga mlango huku anatabasamu!!

“Mume wangu leo umeamua kulewa asu……!”

Alisita baada ya kuona chupi tatu anazozifahamu zikiwa juu ya meza!!

Chupi hizo zinamaanisha ni siku tau,kwa hiyo katika siku tatu alizoniaga ndiyo zikapatikana!!

Patra aliliachia begi lake likaanguka chini,akashika kichwa kwa mikono miwili huku ametumbua macho!!

Muda huo nilikuwa nakunywa zangu pombe kali kwa hasira sana!!

Patra nguvu zilimuisha akakaa chini machozi yakamtoka!

Bado sikujua alikuwa analia nini?na sikutaka kumuuliza tena,sikuwa na sababu hiyo niliendelea kunywa pombe kali tu bila maneno!

Patra alilia nahisi hakuona kama kuna sababu ya kuomba msamaha,na hata angeomba hakukuwa na sababu ya kumsamehe!

Kwangu nilimuona shetani kabisa,mtu hasiyefaa!!

Wanasema mtenda akitendewa inauma sana,mwanzoni sikuwahi kutendwa niliona kawaida Aisha alipolia mbele yangu kisa mapenzi!!

Sasa Patra kanifundisha kuwa mapenzi siyo kitu cha kuchezea,mapenzi yanauma!

Patra alisimama akasogea akakusanya chupi zake akazitia kwenye begi lake kisha akaniangalia huku analia!!

Mimi binafsi sikutaka hata kumwangalia,nilikuwa bize na pombe kali tu!!

Patra alishika begi lake akafungua mlango taratibu akaanza kujivuta mpaka akaishia zake!

Moyo uliniuma lakini sikuwa na jinsi,kuna muda unatakiwa uviache unavyovipenda kwa usalama wa maisha yako!

Niliendelea kunywa zangu pombe kali kama kawaida!!

Siku ile sikutokea kazini kabisa,nilishinda naomboleza kifo cha penzi langu na Patra!

Kesho yake nilienda kazini kama kawaida yangu!

Nikafungua banda na kuendelea kuuza kama kawaida!!

“Oi mbona jana hukutokea?”,aliniuliza Kessy!

“Nilikuwa naumwa!”

“Dahh!pole sana mwanangu!”

“Nilishapoa vipi biashara Jana!’

“Ilikuwa poa nilikuuzia kama laki na nusu ivi!!

“Oohh! ahsante!!”

“Vipi yule demu!”

“Demu gani tena!”

“Si yule Cleopatra!”

“Achana na mademu Kessy tufanye kazi!!”

Sikutaka kusikia habari za mapenzi kabisa kipindi kile!

Nilitaka kufanya kazi,mapenzi yanapoteza sana muda wa mtu,hasa mahusiano ambayo hayana uhakika!

Kuna vitu vya ajabu kwenye maisha yani unakuta watu wanajua kabisa huyu hawezi kunioa lakini bado mnaishi!

Katika mahusiano yoyote hamna kitu kinauma kama muda,unampotezea mtu muda huku ukijua huwezi kuwa naye!

Kuna mahusiano yapo yapo tu kama jongoo huwezi kujua kichwa upi mkia upi!

**********

Siku ilipita,zikapita hatimaye wiki,nazo zikakatika nikatimiza mwezi bila kuonana wala kuwasliana naye!!

Hamna kitu kigumu katika maisha ya nyoka unapofika muda wa kujivua gamba!!

Hujitenga peke yake mbali huku akipitia mateso makali sana!

Ndivyo binadamu tunavyoishi tukitaka kuwasahau tuliowapenda na wakatuumiza!

Ndiyo maana usipotulia unaweza kujikuta umeanguka kwenye ulevi au uvutaji wa madawa ya kulevya!

Kwangu nashukuru nilifanikiwa,niliblock namba zake zote na kuzifuta!

Siyo unamuacha mtu halafu unaona status zake ndugu utakufa na kihoro!!

Na vile binadamu wana makusudi,akijua unaangalia status zake memes zitakuua kunguru wewe!!😆😆

Ukimuacha mtu mblock mpaka rohoni yani piga block kote!

Nakumbuka siku hii nilikuwa na jamaa yangu Kessy tunapigwa na jua,kama unavyojua mwenzetu kaoa au tuseme sijui kaolewa dah!

Tulikuwa tunapiga stori za hapa na pale!

“Ivi mwanangu si tunaweza kubadilisha biashara tukafanya mambo makubwa zaidi!!”,nilimuuliza Kessy!

“Kwanini?”

“Sababu mi naona nina mtaji naweza kuanzisha biashara nyingine kubwa nikapiga hela nzuri!”

“Unazingua,inshu siyo kubadilisha biashara,inshu ni kupanua biashara iwe kubwa!!”

“Kivipi Kessy mwanangu?”

“Yani hapa unaweza ukaajiri mtu halafu ukatafuta masoko nje ya Dar na ukifanikiwa unaweza hata kwenda nje ya Tanzania huko kenya,Uganda lakini siyo uache moja kwa moja kazi inayokuweka mjini!!”

“Daah!halafu mwanangu nakuonaga boya,kumbe we domo zege tu ila akili ya maisha unayo!!”

“Hahahahaaa!acha zako!”

“Sasa sikia tufanye hiyo ki…..!”

Ghafla nilisita baada ya kumuona mtu nisiyemtegemea kasimama mbele yangu!

Macho yangu yaliganda mpaka Kessy naye ikabidi aangalie nimeona nini,alivyoona hakuamini alishtuka nusu azimie!!!

“Saidaaaaaaaaaaa!!”

Msichana yule alikuwa amesimama machozi yakiwa yanamtoka!!

“Kessy nisamehe!!”

Alisema Saida huku anapiga magoti chini bila kujali watu wanamuona!

JE KESSY ATAMSAMEHE MWANAMKE ALIYEMUIBIA MARA MBILI?

Sehemu ya 45

Ilipoishia…………Saida mwanamke ambaye aliwahi kumuibia Kessy gesti na nyumbani kwake,leo amekuja kumuomba radhi Kessy….

Songa nayo………

Ilikuwa ni kama sinema,Saida licha ya yote aliyofanya leo kasimama mbele ya Kessy anamuomba radhi!!

Sikujua anaigiza au anafanya nini,ila uso wake ulionyesha ni mtu anayejutia.

Hakuwa amechoka labda tuseme amepigwa na maisha ndiyo karudi la hasha!Saida uzuri wake uliongezeka,alinenepa kidogo na kufanya avutie zaidi!

Kusema ukweli katika wanawake wote nimewahi kumuona nao Kessy,Saida ni mrembo zaidi!

Ana shepu namba nane,mrefu na mrembo kama mnyarwanda!!

Kitendo cha Saida kupiga magoti chini huku analia,Kessy hakukikubali kabisa!

Haraka alimshika mkono akamuinua akaingia naye kwenye banda lake!

Sikuwa nyuma,nilitaka kujua nini Saida atasema maana hasije na maneno yake tu ya kipuuzi halafu amsamehe akabonyeze kekundu tena bomu likalipuka!

“Eeheeh!Saida kulikoni tena huku na machozi!!”

Mimi ndiyo niliuliza baada ya kumuona Kessy amezubaa tu mapenzi haya jamani!

“Saida nakuuliza kulikoni,naomba useme hayo machozi hayatokusaidia kitu,wewe ni samaki chozi lako halina thamani!”

“Shem…sheme…ji…mi..tu..na..na…!”

“Sema kabisa siyo nana iyo nyimbo ya Mr fleva na Diamond!”

“Naomba msamaha!”

“Unaona ni rahisi?mtu kukusamehe mara mbili unamuibia,ulimuacha na boksa gesti kakusamehe,ukaona haitoshi ukabeba mpaka vijiko nyumba ukaiacha kama ndiyo mkandarasi kaikabidhi leo!!”

Saida alikuwa analia tu kwa kwikwi maneno yangu yalimchoma!!

“Saida vitu vyangu viko wapi??”,kwa Mara ya kwanza Kessy aliuliza kwa sauti yenye utulivu!

“Vipo!vipo Kessy!haki ya nani Kessy hata ukitaka tukavichukue saivi navileta!!”

“Viko wapi?”,nilimuuliza!

“Viko kwa mama yangu Chamazi!”

Nilikaa kimya sasa nimsikie Kessy atasema nini?

“Kwanini umerudi?na huko tayari kurudsha vitu ulivyochukua!!”,aliuliza Kessy!

“Kessy!Nimekukosea sana,katika maisha yangu sijawahi kukutana na mwanaume mwenye upendo kama wako,nimezunguka kote lakini sijaona kabisa!”

“Ntakuamini vipi?nilikuamini Mara mbili ukaniliza?”

“Mi..mi..nimeacha saivi hayo mambo,nina kazi zangu kabisa nimeacha kudanga na kila kitu,ukikubali ntakupeleka kwetu ukamuone mama yangu Kessy nisamehe!siyo kwamba nimerudi sababu sina maisha hapana,ninajiweza Ila natafuta upendo wa kweli naukosa babaangu naomba unisamehe!!”

“Oyah!Erick nipishe kidogo niongee na Saida!!”

Moyoni nikasema nikasema kumekuchaaa!nikainuka nikawaacha wapendanao,maana ukiingilia mapenzi ya watu utaumbuka!!

Siku zote usiingilie Mambo ya watu wanaoshea kitanda kimoja,utajuta!

Sijui kwanini ila huwa kuna kitu kinamkereketa kusema tu,utamsikia tu “yani baby yule rafiki yako simpendi,mnafiki kwanza kaniambia eti unatoka na Jenny,ivi wewe kweli ni wa kutoka na rafiki yangu!!”😆😆

Ya ngoswe mwachie ngoswe!nilikaa zangu nje kusubiri matokeo!!

Punde alitoka Kessy akiwa na tabasamu pana!

“Sasa mwanangu!”,aliniambia.

“Nambie!!”

“Mi nakuacha hapa mara moja naondoka na Saida nyumbani nikichelewa wewe utanifungia banda langu!!”

“Heeeee!Ina maana mshayamaliza!!?”

“Kakaaaa!Mimi nilishakuambiaga,sababu hata nikisema nimkatae ntaudhulumu moyo wangu kaka!”

“Dah!Mimi sikushauri kabisa yani!!”

“Binadamu anapokuja kukuomba radhi,inabidi umpe nafasi!”

“Samahani nyingine za kejeli tu,mwingine anakuja anakuona uko poa anataka aharibu tena!!”

“Subiri uone saivi nacheza kama pele yani mpira gambani shuti wayaaa!!”

“Ulisemaga ivyo ivyooo!!”

“We tulia nichekie mwanangu!”

“Poa!!”

Basi bwana ndiyo kama ivyo bwana Kessy kaondoka na Saida tena mpaka nyumbani!

Hamna siku nilimtukana rafiki yangu kama siku ile,japo hakusikia Ila moyoni nilimtukana kichizi!!

Nilichukua simu nikampigia Abobo,ili nimwambie kilichotokea,bahati mbaya hakupokea simu kabisa!

Imekuwa kawaida yake siku hizi,ukimpigia simu Abobo hapokei kwa wakati au hasipokee kabisa kiufupi ushikaji ulipungua sana!

“Huyu mjinga anajiona Jay Z kudadeki sijui Bilget au Bakhresa atatukuta tu!!”

Nilijisemea moyoni nikaendelea zangu na biashara japo ulikuwa mtihani kusimamia mabanda yote peke yangu!!

Simu yangu iliita na nilipoangalia ni Maiya ananipigia!!

“We mwanaume,umekaa kimya na ukijua wewe ni baba Kijacho hujui mtoto anataka joto lako huku?”

“Sasa Maiya kwani mi nimekaaje kimya?”

“Hupigi simu hutumi meseji upo upo tu kama hujui we ni baba mtarajiwa!!”

“Nakuwa Sina salio Maiya!”

“Sasa sikia ukimaliza kazi zako leo njoo nyumbani na pia nakuunga bando la mwezi mzima sijui utasingizia nini?”

“Maiya leo siwezi kuja!!”

“Umeanza lini kubishana na mimi?haya niambie unakuja hauji?”

Nilibaki njia panda,nilimuogopa Maiya sana,kitendo cha kumuua mumewe mbele yangu kilininyima ujasiri mbele yake!

Niliogopa kuonana naye sababu anaweza kunipiga risasi muda wowote na pia nikikataa akituma mabaunsa yake yanifuate itakuwaje?

“Erick nasubiri jibu unakuja au hauji?”

Aliuliza Maiya kwa ukali,kwa sauti ambayo sikuwahi kumsikia ananikaripia namna ile,nilitetemeka kwa uoga!

JE ERICK ATAMJIBU NINI MAIYA!

NA NINI HATIMA YAO?

Share.
Leave A Reply

error: Content is protected !!