Clickable WP Image
JOIN US WHATSAPP CLICK HERE
JOIN US TELEGRAM CLICK HERE

SITAMANI TENA KUOA

PART: 06

ILIPOISHIA,

Rashid aliwekwa chini ya ulinzi huku akisubiriwa kumaliziwa nakutupwa kusiko julikana.

SONGA NAYO…

“Hee!, nimewakosea nini?, aliwauliza huku akiwa anatetemeka.

Baada yakutoa kauli hiyo, Salum alinyanyua panga juu nakulishusha kwa nguvu huku likiwa limetegeshwa kwenye utosi wa kinywa cha Rashid.

“Mama!..mama!” Alikwepa panga hilo huku akipiga kelele.

“‘Nyoosha miguu na mikono hiyo…” walimuamrisha..

Rashid alifanya hivo . Kosa moja alilolifanya Salum, ni kuweka panga chini na kutaka kuanza kumfunga kamba ndipo aliponyanyuka na kutimua mbio na kuwaacha wakiwa hawaamini.

Hakutaka hata kuangalia nyuma mpaka alipofika nyumbani.

Alitamani kumwambia lakini aliogopa mara baada ya kukumbuka maneno yake yakumkanya.

Sura yake ilionekana yenye hofu kweli huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio.

“Hoo…!hooo!, asante Maulana kwakuniepusha na kifo. Sirudi tena …hoo..!” Alitamka huku akimkwepa mama yake asimuone.

Baada ya kuwakimbia, waliimarisha ulinzi pamoja na mazoezi ya kila siku.

Maisha yaliendelea huku furaha ikizidi kunoga kati ya Sikudhani na Salum.

Wakati wanazidi kunenepeana na kunawiri, Zuwena alijikuta anazidi kukonda kila kukicha mara baada yakumkumbuka baba yake.

Ni wakati mgumu sana alioupitia mpaka mama yake siku moja akamuuliza,

“Unaumwa?”

“‘Hapana mama…”

“‘Sasa kwanini unakonda namna hii?”

“‘Mama nina msongo wa mawazo …”

“‘Unawaza nini!, watoto wa siku hizi bwana..”

“Kila mda nakumbuka jicho alilonitazama baba siku anahukumiwa mahakamani na kila nikijaribu kusahau nashidwa…”

Baada ya kuongea hivo, Sikudhani aliekuwa amekaa pembeni mwa Salum, alikaa kimya kwa mda kisha akamjibu.

“Wewe unaongea nini?, Mudy mdogo wako kashasahau sasa wewe unangea nini?, chunga mdomo wako usije kuletea shida…” Mama Zuwena alitamka.

Zuwena aliziba mdomo wake nakubaki  kimya kisha akazama chumbani mwake.

“Huyu mtoto unapaswa kukaa naye karibu na siyo kumfokea laa sivyo atatuleta mabalaa…” Kwa sura ya mshutuko, alimwambia mkewe.

Mama Zuwena alitikisa kichwa kama ishara yakukubali.

*

Huko gerezani, toka amemalizana kuagana na familia yake, alipelekwa tena chumba maalumu cha siri ili kuweza kunyongwa .

Ali Mapito alilia sana lakini kilio chake hakikuweza kujibika .

“Makosa mnafanya wenyewe afu mnaanza kulialia” Askari mmoja aliongea huku akimsukuma kwenye kisogo chake.

Mapito alitamani kutoa sauti lakini isingesikika kulingana na kitambaa alichokuwa amefungwa.

Alipelekwa kisha mashine ikasetiwa na askari akasogea nyuma kidogo.

Zikiwa zinahesabika sekunde tu, mlango ulifunguliwa kwa haraka kisha askari akamvuta Mapito.

“Hee!..”askari mwenzie alishutuka.

“Tulitaka kufanya kosa kubwa sana!, walipewa kibari cha kunyongwa ni hao wanne afu huyu anatakiwa kusubiria kidogo mpaka miezi 2 ndipo tutakapofanya hivo..” alimwambia.

“Ohh ni kweli kabisa yaani leo tungefukuzwa kazi…” alimjibu.

“Broo!, kweli siku zako bado kidogo. Kama umepona leo…!.” Alikatisha maneno kisha wakamtoa na kumrudisha chumba chake  cha awali.

Chumba hicho mda wote kimejaa giza tupu huku mda wa usiku mbu wanazagaa kama nzi kwenye kinyesi cha mlevi.

“Ee Mungu wangu, nimekukosea nini mpaka nateseka hivi?, ni bora uniondoe kwenye dunia yako kuliko kuteseka namna hii…” alitamka peke yake

Sura yake ilibadilika na mvuto wake alokuwa nao ukapotea huku mwili wake ngozi yake ikijaa vipele .

Siku moja mida ya saa 12 za jioni, askari magereza mmoja alifungua chumba hicho kisha akamkuta Mapito akiwa amesinzia huku mwili ukionekana dhaifu sana.

“Heeyy..!” Alimshutua .

Mapito alizinduka na kumuona askari.

“Nimekuja hapa kukupa taarifa kuwa , siku zako zimebakia chache na miezi miwili ikiisha bila taarifa yoyote, unaenda kunyongwa,”

“Jamani Afande nisamehe maana sikutenda kosa lolote .”

“Ebu sikia nikwambie, hapa hatuna mamlaka yakubadili maamuzi ya mahakama, unachotakiwa ni kufanya mchakato wa rufaa kwa kuwajulisha ndugu zako ili wamuone wakili aweze kukusaidia..”

“Sasa ndugu zangu nitawaona wapi?, baada yakuagana na familia yangu, walienda kutoa taarifa kama nimenyongwa ndo maana sijawahi ona wakija tena kuniona…”

” Nitakusaidia kitu kimoja, kesho mida ya saa 2 za asubuhi, nitakuombea kwa mkuu wetu ili upate nafasi yakuandika barua uitume kwa ndugu zako..”

” Asante Mungu..Asante Mungu nashukuru ..” Mapito aliinama nakuanza kubusu buti za Askari.

” Unakufuru!, .mimi sio Mungu..” Askari alitamka kisha akaondoka.

Kesho yake mida ya saa 2 za asubuhi, Mapito aliitwa na kupelekwa chumba maalumu kisha akapewa karatasi na kalamu aandike barua kwenda kwa ndugu zake…

Alianza kuandika kwa hisia kali sana mpaka akawa anaichafua karatasi kwa machozi na kamasi laini.

” Jikaze we mwanaume! Unalialia tu!, karatasi ni moja tu !, ukiichafua utajua mwenyewe..” askari alitamka kwa sauti ya juu.

Baada ya mda, alimaliza kuandika barua iliyosomeka,

” KWAKO MAMA, MIMI ALI MAPITO NAPENDA KUWAJULISHA KUWA BADO NIPO HAI .NAOMBA MPOKEE SALAMU ZANGU NA MSALIMIE MTOTO WANGU MUDY KWA KUTONIONA. NIMEBAKIZA SIKU CHACHE KABLA YA KUNYOGWA LAKINI NIMEPEWA MDA WA MWISHO AMBAO NI KUKATA RUFAA . NAOMBA MNITAFUTIE WAKILI AWEZE KUNISAIDIA. KWAHERI JAPO AFYA YANGU SIO NZURI”

Askari alimrudisha kwenye chumba chake kisha akamfungia.

Baada yakufanya hivo, alipeleka barua hiyo mapokezi ili itumwe sehemu husika..

“Sasa barua gani hii? Haina anwani wala namba ya simu!, atajijua mwenyewe na nafasi huwa inatolewa mara moja tu tena ya upendeleo” askari wanapokeo aliongea….

JE BARUA HIYO ILITUMWA?

NA KAMA ILITUMWA ILIPOKELEWAJE?

PART: 07

ILIPOISHIA..

Mapito baada ya kuandika barua, alirudishwa ndani huku mchakato wa kupeleka barua ukifanyika…

SONGA NAYO…

Mnamo mida ya saa nne mchana huku akiwa ameketi kwa nje,

Mama Mapito alimuona mwanaume akiwa amevaa shati nyeusi na suruai pemoja na miwani.

Alimtizama huku akizidi kumkaribia ndipo alipojiuliza,

“‘Huyu ni nani?” Alijiuliza.

Mwanaume huyo alizidi kumsogelea na hatimaye akamfikia sehemu aliyokuwa amekaa.

“Shikamoo mama” alisalimiwa

“Marhaba..” aliitikia huku akiwa na mshangao kidogo.

“‘Samahani mama, nimeagizwa na mwenyekiti wa mtaa nikupatie ujumbe huu” alimwambia huku akiweka mkono mfukoni.

“‘Ujumbe upi huo?” Aliuliza.

Barua ilichomolewa taratibu kisha akapatiwa.

“‘Hee!, mwanagu siwezi hata kusoma maana macho yangu yanamatatizo.” Alitamka.

“Ohh ebu nipe nikusomee”

Alishika kibarua hicho kisha akataka kusoma lakini kabla hajaisoma, Rashid alitokea huku akiwa anapiga miruzi.

“Ohh iache naona mwanangu kaja…” .

Baada ya kupiga hatua chache, Rashid alifika sehemu hiyo kisha akapewa barua.

“Mwanangu ebu nisomee barua hii…”

Aliishika kisha akaweka macho mara mbili ndipo alipobaki ameganda kwa mshangao mkubwa.

“Hee! Ni kweli?!” Aliuliza kwa mshangao.

“Mie sijaisoma na nimepewa niwaletee kutoka kwa mwenyekiti…” alitamka.

“‘Nini mwanangu mbona unasoma peke yako?” Alimuuliza.

“Mama siamini !, siamini kabisa!”

“Si useme?” Mama aliongea.

“Mama eti Mapito yuko hai!”

“Hee!, mwanangu !”

“‘Ndiyo .”Alimsomea barua hiyo mwanzo mwisho ndipo Mama Mapito alipomwaga machozi kama mtoto mdogo.

“‘Sasa mama ngoja mda huu nikimbie mpaka gerezani na nikishatoka nitakuwa na uhakika kama yu hai au la”

Bila kuchelewa, alipanda boda na kuanza safari ya kwenda Segerea. Baada ya kufika, alikwenda moja kwa moja mpaka Mapokezi kisha akaulizia.

Walimhakikishia kuwa yu hai na mda wake ulobaki ni mdogo sana kabla ya kunyongwa.

Aliomba kuonana naye lakini haikuwezekana kwa wakati huo.

Aligeuza haraka na kurudi nyumbani kisha akatoa taarifa.

“Mama..mama!, bado yupo. Sasa hapa kazi iliyobaki na kumtafuta wakili Mapunda ili atusaidie kwa hili…”

“‘Una uhakika yu hai mwanangu?”

“Mama nimeuliza mwenyewe na wala sikudanganyi…”alitamka.

Mchako wa kumtafuta Wakili Mapunda, ulianza haraka sana huku Rashid akijaribu kila njia aweze kumpata.

Bahati nzuri aliweza kumpata na kumueleza yote ndipo alipomwambia,

“Kwanza mmechelewa sana . Hii rufaa ilikuwa wazi na nikiangalia mazingira ya kesi na hukumu yenyewe, hayaendani maana hakuna uthibitisho wa moja kwa moja..” Wakili Mapunda alitamka .

“‘Kwahiyo tunafanyaje?” Alimuuliza.

” Utachangia gharama za usafiri na chakula tu ila gharama nyingine niachie na nina uhakika nitashinda atatoka au kupunguziwa adhabu…”

“Siamini na sipati picha maana hata mke wake kashaolewa na kimwanaume …”

“‘Ebu tuyaache hayo kwanza. Nenda mahakamani ukaombe nakala ya hukumu afu kesho tuanze kazi rasmi…”alitamka.

Rashid aliagana naye kisha akaanza safari yakuelekea mahakamani Kisutu.

Baada ya kufika, alienda moja kwa moja mpaka kwa karani na kupewa control namba ili alipie kiasi cha sh 5000 kama gharama.

Alifanya hivo na kupata nakala hiyo ya hukumu.

Huko mtaani habari za chinichini zilianza kusambaa kuwa Mapito bado hajanyongwa ndipo walipojikuta na taharuki kubwa.

Miongoni mwa watu waliopata taarifa hizo, ni Sikudhani, mke wa Mapito.

“Mme wangu kuna taarifa hii umeipata?” Alimuuliza Salum huku Zuwena akiwa anasikilizia kwa mbali.

“‘Taarifa ipi hiyo?” Alimuuliza

“Yaani wameanza kuzusha eti Mapito bado yu hai na wanafanya mchakato wa kumtoa…”

“‘Hahaha…, achana nao. Tangu lini marehemu akawa hai?. Kashanyongwa tayari na kama ni kuoza basi kashaoza…” Salum alicheka .

“Afu kweli mme wangu. Kwanza ile kesi asingeweza kupona. Akwende zake” Sikudhani alitamka kisha wakakumbatiana.

” Afu huyo dogo Rashid ndo analeta habari hizo za uongo . Muache mda si mrefu atapotea bila kujijua na hawataona hata mfupa wake kama ataendelea kunifuatilia.. Salum alitamka.

” Yaani kiherehere kimemzidi na dawa yake ndo hiyo….”

Wakati wanaendelea na mazungumzo hayo, Zuwena alishutuka sana nakujikuta mapigo ya moyo wake yanaenda kasi.

“‘Kama ni kweli itakuwaje?!, ” Zuwena alishika tama na chozi la uchungu likamtoka.

***********

Mida ya jioni jua likiwa limeanza kuzama, Rashid alimpelekea nakala ya hukumu wakili Mapunda ili kuandaa sababu za rufaa  na baada ya kuipitia, alitikisa kichwa kisha akasema..

” Kazi imekwisha…”

” Kweli?!?” Rashi aliuliza kwa mshangao ulioambatana na furaha.

” Mwambe mama atulie …”

” Tutashukuru sana na ukifanikiwa nitakupa hata nusu ya mali zangu maana mke wake katuaibisha sana na li mme lake hilo…”

( waliagana )

JE WAKILI MAPUNDA ATAWEZA KUSHINDA RUFAA HIYO?

JE WAKIPATA UHAKIKA KUWA MAPITO YU HAI, SALUM NA FAMILIA YAKE MPYA WATAFANYA NINI?

PART: 08

ILIPOISHIA,

Rashid anaagana na Wakili Mapunda na kuelekea nyumbani..

SONGA NAYO…

Mnamo mida ya saa 2 za usiku mara baada ya kuagana na Rashid, Mapunda alishika kidafatari chake kidogo maarufu kama notebook  pamoja na pen yake yenye kutoa wino mweusi kisha akaketi kwenye kiti na kuanza kuichambua nakala hiyo ya hukukumu.

Aliisoma yote na kuirudia mara 3 huku akiwa anatikisa kichwa chake.

” Hii hukumu sio sawa kulingana na adhabu aliyopewa. Hapa kesho asubuhi na mapema naenda kuwasilisha rufaa yangu” aliongea peke yake.

Katika kupitia hukumu hiyo, wakili Mapunda aliibua maswali makuu 3 ambayo aliyatumia kama sababu ya kukata rufaa ambayo ni,

1. Mahakama imemhukumu mtuhumiwa bila kuwa na ushahidi wa mwilia au mabaki ya mwili kwa aliyedaiwa kuuawa.

2. Ushahidi uliotolewa na shahidi namba 1 ( Zuwena) hauna ukweli wa moja kwa moja kwani haoneshi wazi wakati mdogo wake anauwawa kwanini hakupiga kelele au kuacha alama ya damu

3. Je kama ameuwawa, sababu ya kuuawa ni ipi?.

Maswali hayo aliyaandika vizuri kwenye notebook yake na kuitunza.

Kesho yake asubuhi na mapema, Mapunda alivaa suti yake nyeusi pamoja na tai nyeusi iliyoambatana na shati nyeupe.

Akiwa anamalizia, mlango ulogongwa ndipo alipofungua,

” Ohh kumbe umeshafika” alimwambia Rashid.

” Ndiyo maana usiku mzima sijalala hata mama hajalala..” Rashid alitamka.

” Sawa namalizia kuvaa dakika 2 tunaenda.” Alimjibu.

Baada ya mda kama dakika 5 hivi, Mapunda aliwasha gari lake akiwa na Rashid ndani kuelekea Mahakama ya rufani kisutu.

Mnamo mida ya saa 2 na nusu za usubuhi, walifika kwenye viunga vya mahakama  ndipo waliposhuka na kuelekea chumba cha karani wa mahakama.

Wakili Mapunda aliwasilisha Rufaa yake kwa karani kisha akaipeleka moja kwa moja kwa mheshimiwa hakimu.

Aliipitia mara 3 hivi kisha akamuita na kumwambia,

” Rufaa yako imekubaliwa na kesi itaanza kusikilizwa mwanzo baada ya siku 3 kuanzia leo yani ijumaa. Faili la mwenendo wa kesi, litaletwa mahakamani hapa kwa kupitiwa upya..”

” Asante mheshimiwa hakimu” Mapunda alishukuru.

Wakati yupo ndani, Rashid yeye alikuwa ameshika tama kwenye ukumbi wa mahakama huku akiwa anatetemeka.

” Ewe mwenyezi Mungu, tunakuomba utusaidie tuvuke katika wakati huu mgumu maana wewe ndo mwenye haki ya kweli na mwenye kujua ukweli wa kila kitu” aliomba kimoyomoyo.

Akiwa anamalizia kuomba, Mapunda alitoka chumba maalumu cha mheshimiwa hakimu hakimu kisha akamkonyeza na kutoka naye nje.

Waliingia kwenye gari kisha Rashid akauliza ,

” Vipi umefanikiwa?, maana sipati usingizi kwa uchungu nilionao..”

” Usijali na wala usiwe na shaka yoyote. Haki itatendeka na tutashinda”

Alimjibu.

Wakiwa kwenye viunga hivyo, Rashid alitoa macho kwa mshangao mkubwa mpaka Mapunda akashutuka.

” Unashangaa nini?” Alimuuliza huku akiwa amemuangalia.

” Hee! Macho yangu yanachokiona ni kweli au!” alitumbua macho.

” Kwani umeona nini?”

” Huyo binti aliyesimama hapo mbona kama Zuwena mtoto wa kaka na anatafuta nini hapa mahakamani?”

” Mhh..ni yeye kweli au?, ebu shuka ukamuangalie kama ni yeye afu tujue anatafuta nini”

Rashid alishuka kwenye gari na kuanza kumsogelea binti hiyo.

Baada ya kumkaribia, alijiridhisha kuwa ni Zuwena ndipo alipomuita,

” Zuwena..Zuwena..”

Zuwena aligeuka kwani alikuwa hajamuona baba mdogo wake.

Ile anageuka, alikutana na sura ya Rashid ndipo aliposhutuka nakubaki amesimama.

” Njoo..” alimuita.

Zuwena alibaki amesimama kisha akaanza kutokwa na machozi na kuwaacha watu waliokuwa kwa nje wabaki na mshangao.

Kilio hicho, kilimfanya Rashid ajiulize masswali mengi ambayo hakuyapatia majibu.

” Unalia nini?, ebu njoo huku kwa nje..” Rashid alimuambia.

Zuwena akiwa ameshika bahasha mkononi, alikataa kutoka sehemu hiyo ndipo alipoamua kuzama ndani ya mahakama.

Kitendo hicho kilimuacha Rashid njia panda huku akiwa haelewi nini kinaendelea.

Alikimbia moja kwa moja mpaka kwa Mapunda huku akiwa anahema,

” Hee kulikoni tena!”

” Yaani haongei chochote na amekimbilia mahakamani huku akiwa na bahasha mkononi”

” Bahasha tena!”

” Ndiyo..”

” Ebu nenda taratibu ukachungulie ujifanye unaulizia utaratibu kwa karani”

Rashid, alipiga hatua kadhaa mpaka kwa karani ndipo Zuwena aliposhutuka mara baada ya kumuona Rashid.

” Subiria kwanza kwa nje nimalize kumhudumia huyu mtoto” Karani alimwambia Rashid huku akiwa na sura ya kustajabu.

Huko gerezani Segerea, Afya ya  Mapito inazidi kuzorota mara baada ya kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara na kuanza kupoteza matumaini ya kuishi tena na familia yake akiwa  hai.

JE ZUWENA AMEBEBA NINI HUMO?

JE YUPO PEKE YAKE AU ?

JE MAPUNDA ATASHINDA RUFAA? NA ITAKUWAJE?

PART: 09

ILIPOISHIA..

Zuwena aliingia mahakamani na kwenda moja kwa moja mpaka kwa karani huku akiwa ameshika bahasha mkononi, gerezani nako, hali ya Mapito ilizidi kuzorota sana kiafya..

SONGA NAYO…

Karani alianza kusoma barua hiyo iliyokuwa imeandikwa na Zuwena mpaka akajikuta machozi yanamlengalenga.

Alimuangalia usoni kisha akamuuliza,

“‘Uliyoandika humu ni kweli?”

“Ndiyo ni kwe…li..” alijibu huku akiwa anamwaga machozi.

“Mhhh.., ebu kwanza kaa hapo maana kesi yako ni nzito sana”

Zuwena aliketi kwenye kiti huku akiwa ameshika tama.

Baada ya mda kidogo, karani aliburuza barua hiyo kisha akatoa nakala 4 nakuzitunza kabatini kisha akamwambia,

“Kwakuwa kesi iliyokuwepo imekatiwa rufaa, basi barua hii itatumika kama kielelezo na kama kuna haja zaidi basi utaitwa utoe ushahidi mwingine wa maneno.” Alimwambian

“Asante lakini naomba sana utunze siri yangu ili mama na baba wasijue maana wanaweza kuniua..”

“Usihofu kwa hilo kwani mahakama inafanya kazi yake kwa umakini sana”

“Asante ,”

“‘Ayaa nenda salama..”

Zuwena alitoka nje na kuanza safari ya kurudi nyumbani.

Wakati amepiga hatua chache sana, Rashid alimwambia wakili Mapunda wamfuate ndipo alipojibiwa,

“Ebu muache  . Hatujui amepeleka nini mahakamani na kwa sheria zetu, kumbugudhi shahidi ni kosa kisheria. Sisi tutasimamia hoja zetu za rufaa..”

“Ohh sawa..”

Walitoka mahakamani hapo kisha kila mtu akaelekea makwao.

Baada ya kufika nyumbani, Zuwena alifungua mlango wa geti na kuingia ndani ndipo aliposhangaa kuona viatu kwa nje huku ndani watu wakisikika.

“‘Hee! , mama karudi?” Alijiuliza.

Ile anashangaashangaa, alimuona mama yake ( sikudhani) akiwa anatoka nje.

“‘Hee!, ulikuwa wapi wewe! tabia yako ya kuzurura siipendi na iwe mwanzo mwisho..”alimfokea

“Sahamani mama nilikuwa nimeenda kumuona rafiki yangu Irene .” Alijibu kwa wasiwasi.

“‘Usinichefue nenda ukapike chakula huko!”

Zuwena aliingia ndani na kumsalimia baba yake ( Salum) kisha akabadilisha nguo na kuanza mapishi.

Wakati Zuwena akiendelea na Mapishi, Sikudhani na mme wake Salum , waliketi sebuleni na kuanza kutizama Tv huku wakipanga mipango.

“‘Mme wangu, nikwambie kitu?”

“‘Niambie..”

“‘Hivi unanipenda kweli?”

“Hahaha mke wangu unachekesha kweli. Sasa nikupende mara ngapi?, mi nakupenda sana tena sana..”

“‘Mhh mimi nataka uninunulie gari maana sipendi kupanda daladala kama wake wa maskini..”

“Hilo tu, wala usijali kuna mchongo wa milioni kama 50  nausikilizia na mda wowote nitakununua mke wangu kipenzi”

Sikudhani alitabasamu kisha akambusu mmewe huku akiwa amemsogelea.

“Mke wangu, sasa ni vizuri twende chumbani maana hapa sio sehemu salama ukizingatia Zuwena ameshakuwa mkubwa ..”

“‘Sawa “

Walinyanyuka taratibu na kuzama chumbani.

Walipumzika kwani jua lilikuwa kali sana huku kila mtu akimuwekea mkono mwenzie mpaka wakapitiwa na usingizi.

Huko jikoni, Zuwena alijikuta mwenye mawazo makali sana hasa alipomkumbuka mdogo wake Zuhura pamoja na baba yake Mapito.

” Nateseka, moyo wangu hauna amani kwa maamuzi yangu nilofanya. Sikuwa na namna yoyote lakini naomba msamaha wako..” Zuwena alinyoosha mikono yake juu .

*****

Huko upande wa Mapito, afya yake ilizorota sana kiasi cha kuonekana mzee wa miaka 70 huku akiwa amepungua uzito kwa haraka sana.

Askari aliyekuwa anampatia chakula, alishutushwa na Mwenendo wa Afya yake ndipo alipoamua kumuuliza,

“‘Unaumwa”

“‘Ndiyo, tumbo linaniuma sana na mbu wameongezeka..”

“‘Hapo sina chakukusaidia maana chumba hiki  ni special kwa mateso na kwa takwimu nilizonazo, karibia nusu ya wafungwa wanaowekwa humu, hupoteza maisha. Sikutishi wala kukuogopesha bali jiandae kisaikolojia huku ukimuomba muumba wako maana yeye ndo mwenye hukumu ya kweli na ya mwisho”

Maneno hayo yalimfanya Mapito ainamishe kichwa chake kisha akamuuliza,

“‘Hujaona ndugu yangu yeyote kuja kuniangalia walau kwa mara ya mwisho ili nimpe wosia wangu maana ninavyojisikia sijui kama nitamaliza wiki hii..” alimwaga chozi la damu.

“Kwa kifungo  ulichonacho wewe, huruhusiwi kutoka nje tena wala ndugu yako kukuona . Barua uliyoandika tuliituma sasa sijui utekelezaji utakuwaje” alimjibu.

“Ohh..basi nakuomba unifungulie nikaone hata mwanga wa nje kwa sekunde hata 10. Kama unavyoniona sina nguvu zakukimbia na siwezi kukimbia .” Alitamka kwa huruma.

“‘Sio mimi bali ni sheria na taratibu. Inaniuma sana lakini nami sina uwezo wa kufanya hivo kwani tunaongozwa na sheria na kanuni za kazi. Isingekuwa hivo, ningekufungulia tena ukarudi nyumbani …” alimjibu.

“‘Ubarikiwe kwa moyo wako wa huruma. Japo sina matumani ya kupona lakini nakuombea uendelee na moyo kama huu kwa wengine . Alaah atakulipa…” Mapito kwa sauti ya chini  alimwambia askari huyo.

“‘Asante “

Askari alishukuru kisha akatoka na kufunga mlango

Usiku mida ya saa nane usiku, Mapito alianza kujihisi kama roho yake inatoka hivi ndipo alipozinduka huku mwili ukiwa mlegevu sana.

“Najua nimekukosea sana lakini kwa uchungu na maumivu niliyonayo, baba naomba unipokee…”

Alivua nguo yake na kuisokota kisha ….

JE ALIFANYA NINI?

JE BARUA YA ZUWENA INAHUSU NINI?

JE RUFAA WALIYOKATA ITAKUWAJE?

PART: 10

ILIPOISHIA,

Mapito alivua nguo yake na kuisokota kisha…

SONGA NAYO.

Baada ya kumaliza kuisokota, aliikunja vizuri kisha akafumba macho na kuitumbukiza shingoni.

Aliiruka kwa juu ili apate pa kuifungia ndipo alipogundua kuwa dirisha lilikuwa mbali sana.

” Hoo!..hoo!. ” alihema huku akiwa amechoka sana.

Alikaa chini na kujaribu kuivuta lakini haikuwezekana ndipo alipojigalagaza na kurusha miguu.

Alitoa kamba hiyo na kuikunjua kisha akaivaa kama hapo mwanzo.

Jaribio lake lakujinyonga, lilishindikana ndipo alipoanza kuwaza njia nyingine ya kujitoa uhai.

Wakatia anawaza njia ipi aitumie ili atoweke kwenye mateso hayo , mama yake pamoja na mdogo wake ( Rashid) waliendelea kupambana ili kuhakikisha walau wanamkomboa au apunguziwe adhabu.

Siku ya ijumaa kama ilivyokuwa imepangwa, Mapunda akingozana na Rashid kuelekea mahakamani kwa ajili ya Rufaa.

Walipofika mahakamani, kesi yao ilhàirishwa mpaka hapo jumatatu.

” Kesi imehairishwa mpaka tarehe 20 siku ya jumatatu.” Mheshimiwa hakimu alitoa tamko.

Rashid alionekana kuvunjika moyo huku akitamani isikilizwe hata siku moja.

Waliondoka na kurudi majumbani mwao ndipo mama Mapitoa alipomuuliza mwanaye,

” Mwanangu mmefikia wapi?”

” Mama !, daah sijui hakimu naye kala chochote?, maana ameihairisha mpaka hapo jumatatu na mda tulipewa kabla ya kunyongwa kwa Mapito umekaribia kuisha..”

” Jamani!, kwanini amefanya hivi, mwanangu Mapito nilikuzaa na ukaitwa jina la mapito, umepita sehemu isiyo salama nasi hatuna ujanja mwingine tofauti na kukuombea..” mama Mapitoa alitamka kisha akamwaga chozi.

” Mama usilie maana bado nafasi tunayo na hatujashindwa. Nitapambana mpaka tone la mwisho..” Rashid aliongea .

Mama mapito alishika tama na kuamua kwenda kujipumzisha ndani.

Wakati mchakato mzima unaendelea, Sikudhan na mme wake hawakujua chochote kile mpaka siku ya ijumaa mida ya jioni.

Wakiwa wameketi kwa nje, walimuoma mwanyeketi wa mtaa akiwa na hati ya wito ya kumtaka Sikudhani kuhudhuria mahakamani .

Aliisoma mara mbilimbili kisha akamuuliza mwenyekiti,

” Mahakani tena!, kufanya  nini” Sikudhan alimuuliza kwa mshangao.

” Hii ni hati ya wito lakini unatakiwa kufika maana ni wajibu kuitikia wito wa mahakama” alimueleza.

” Kwani nimekosa nini?, ebu niambie kama kuna shida yoyote..”

” Huu ni wito nami sina majibu sahihi kwani nimeletewa kama mwenyekiti..”

” Mhh..usije ukatuuza mwenyekiti ebu twambie ukweli..”

” Hahahah hamna shida wala usiogope…” alicheka kisha akaaga.

Baada ya kuondoka, Sikudhan alimuita mme wake kisha akakaa naye kitako.

” Hili unalionaje?” Alimuuliza

” Hapa naona kuna mtego na ikiwezekana tujaribu kuutegua..” Salum alimjibu

” Au wametungundua  nini?”

” Hapana sio kweli ila nahisi anaweza kuwa boya Rashid maana anakiherehere sana..”

” Kama ni huyo hata tusipo enda,  maana hana hata hela afu na mama yake ameshakuwa mzee ..”

” Haitaleta shida kweli..kutoenda..?” Alimuuliza.

” Mme wangu kama ni Shidi hana shida yoyote..”

” Aya mke wangu kipenzi” walikumbatiana.

Wakiwa wanaongea hayo, Zuwena alikuwa anasikiliza kwa mbali ndipo naye alipojikuta anatetemeka .

Ama kweli alosema siku hazigandi basi hakudanganya.

Hatimaye jumatatu iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu kubwa, iliwadia ndipo Salum na mkewe  Sikudhan walipoamka na kuulizana,

” Mke wangu niliongea na rafiki yangu kisha kaniambia kutotii wito wa mahakama  ni kosa kisheria hivo unatakiwa

Uende nami nitakusindikiza”

” Jamani  mme wangu si tumekubalina tusiende?”

” Twende usiogope mke wangu tutafika na kurudi”

” Ayaa mme wangu. “

Walijiandaa na kuanza kuelekea mahakamani…

Baada ya kufika kwenye viunga vya mahakama, Sikudhani akiwa na Salim, walimuona  Rashid akiwa pembeni mwao ndipo Sikudhani alipokohoa kozi na kutema karibu ya Rashid kisha akalikanyaga kohozi hilo.

Watu walimshangaa sana Sikudhan mpaka Rashid akajikuta anapandwa na hasira sana.

Alimsogelea na kutaka kumpiga ndipo Mapunda aliporuka na kumkamata Rashid.

” Usithubutu kumgusa wala kumnyooshea kidole. Huu ni mtego wamekutega ili ukamatwe na uwekwe ndani hapahapa”

” Sasa kwanini anatema kohozi mbele yangu?” Rashid alifoka.

” Ebu achana naye..”

Rashid aliamua kuwa mpole huku akiishia kimuangalia jicho kali.

Wakiwa wamesimama, kesi yao iliitwa kisha wakapanda ngazi kuelekea kwa mheshimiwa hakimu.

Baada ya kufika aliwambia,

” Baada ya hukumu kutolewa na mahakama, mtuhumiwa alikutwa na hatia na kuhukumiwa. Kulingana na sheria za mahakama, amekata rufaa hivo tunaanza, kuisikiliza mda huu” alitamka.

” Mheshimiwa hakimu, sasa rufaa ya nini kwa mtu ambaye tayari amenyongwa?” Sikudhani alitamka.

” Hee! Nakuomba ufuate utaratibu wa mahakama na uheshimu kiti hiki laa sivyo utaishia jela. Kama unataka kuongea chochote basi nyoosha mkono”

” Samahani mheshimiwa…” Sikudhani aliomba radhi.

” Ehee..endelea ulikuwa unasemaje..,

” Nimesema kuwa aliyehukumiwa tayari ameshanyongwa hivo ni kupoteza mda ..”

” Unauhakika na ushahidi?”Hakimu alimuuliza.

” Ndiyo…”

” Ebu saini hapa afu uithibitishie mahakama..”

 Sikudhani alitia saini kisha akasema,

”  Ni mda sasa umepita tangu amenyongwa. Nakumbuka nilienda pamoja na watoto wangu kumuaga kwa mara ya mwisho..”

” Unamaelezo ya ziada au  ni haya tu?” Alimuuliza.

” Ni hayo tu..”

” Ehee nyie wakata rufaa mnasemaje kuhusu hili!”

” Mheshimiwa hakimu, mteja wangu yuko hai na wala hajanyongwa kama anavyodai. Kwa uthibitisho, nina barua yake aliyoandika siku chache zilizopita ” Wakili Mapunda aliongea.

” Kwakuwa kumekuwa na sintofahamu, mahakama inawaomba barua ya uthibitisho wake kutoka Magereza akiwa hai au alishanyongwa na kesi imehairishwa mpaka hapo jumatano…” Hakimu alitamka…

JE HIYO JUMATANO ILIKUWAJE?

NA NINI KILIFUATA?

Share.
Leave A Reply

error: Content is protected !!